Simu chanzo cha maendeleo, ndoa kusambaratika.
Na Kalunde Jamal, Mwananchi.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti la Mwananchi katika mikoa mbalimbali nchini umegundua kuwa mbali ya kusambaratisha ndoa nyingi, simu pia zimekuwa adui mkubwa kwa baadhi ya watumiaji badala ya kuwanufaisha kama inavyotakiwa.
Uzuri na ubaya wa simu
Wananchi walieleza uzuri na ubaya wa simu ambapo Peter Tesha mkazi wa Arusha aliitaja simu kuwa ndiyo chanzo cha kumfikisha alipo sasa akikosa fedha za matumizi yake ya kawaida licha ya awali kumiliki miradi mingi iliyokuwa ikimwingizia kipato.
Wananchi walieleza uzuri na ubaya wa simu ambapo Peter Tesha mkazi wa Arusha aliitaja simu kuwa ndiyo chanzo cha kumfikisha alipo sasa akikosa fedha za matumizi yake ya kawaida licha ya awali kumiliki miradi mingi iliyokuwa ikimwingizia kipato.
Anasema kuwa katika maisha yake na mkewe hakuwahi kushika simu ya mkewe huyo mbali mkewe kuwa hodari wa kuchunguza simu yake.
Hata hivyo siku moja bila kupanga alichukua simu ya mkewe na kusoma ujumbe mfupi aliotumiwa, jambo analoapa kutolifanya tena maishani mwake kwani alikutana na ujumbe aliouelezea kuwa ulikuwa wa majibizano kati ya mkewe na mwanamume mwingine ambaye hata hivyo jina lililotumika lilikuwa la kijiji badala ya mtu.
“Siwezi kusahau, hata huu umaskini unaoniandama ni madhara ya simu. Ujumbe ule ulikuwa wa kulaumiana kati ya mke wangu na huyo mwanamume kuwa hawa watoto wangu ni wake, mke wangu akiuliza; Kwa nini umewatelekeza na kuniachia mzigo wa kulea mimi ambaye siyo watoto wangu?”anasema Tesha.
Anafafanua kuwa ujumbe huo ulifafanua: “Kama akiendelea kufanya hivyo ataiuzilia mbali nyumba aliyompa kwa ajili ya watoto, ambao mimi siku zote nilikuwa nikiamini ni baba yao.”
Anaeleza kuwa tangu alipofungua simu ya mkewe na kusoma ujumbe huo maisha yake yalibadilika kwani alikwenda kuwapima DNA watoto hao na kumbana mama yao ambapo ilibainika kuwa ni kweli watoto hao sio wake, jambo lililomchanganya na kumtia aibu kwenye familia na jamii hivyo akaamua kuwa mlevi.
Tesha anasema kuwa kuanzia hapo aliacha kusimamia biashara zake kutokana na kuchanganyikiwa na kukwepa aibu, huku akiishi kwa kujificha kwa zaidi ya mwaka na alipotulia na kujifikiria kwa nini amekuwa hivyo alikuwa tayari ameshachelewa, kwa kuwa baadhi ya maduka yalikuwa yamefungwa na aliowaacha hakuwa na cha kuwafanya akibaki na duka moja la Arusha ambalo pia lilikuwa limekufa kutokana na kuwa na bidhaa chache.
“Naishi kwa ushauri na ndiyo maana mara nyingi nimekuwa nakutumia ujumbe wa kutaka unishauri kwa kuwa siiamini tena akili yangu wala mwili wangu. Kama mwanamke ambaye nilikuwa naishi naye miaka yote aliweza kubeba mimba za mtu mwingine na nisijue, sina sababu ya kujiamini tena, nimekuwa masikini kwa sababu ya simu, sitamani simu ya mtu zaidi ya hii yangu, ambayo wakati mwingine huwa naamua kuifunga,”anamaliza Tesha.
Wakati Tesha akieleza hayo, upande mwingine Jennipher Lazaro wa Tanga anasema kuwa hawezi kuishi bila simu kwa kuwa humsaidia mambo mengi ikiwamo kujifunza zaidi kupitia mtandao, kumuunganisha na marafiki walio mbali naye.chanzo/www.babamzazi.com