advert

http://

Wednesday, 23 October 2013

PUMZIKA KWA AMANI MTANGAZAJI MAHIRI JULIUS NYAISANGAH.

Mke wa Marehemu



Julius Nyaisanga 1R.I.P kwa Mtangazaji legend ambae atakumbukwa na Watanzania wengi nikiwemo Mimi D'JARO ARUNGU, ni legend ambae upekee wa sauti yake pamoja na ubunifu wa vipindi alivyoviendesha  vilimpa heshima na jina lake kukua kila siku kutokana na kumbukumbu aliyokua anaicha kwa watu kila anaposikika.

Julius Nyaisanga ambae alifariki dunia October 20 2013 hospitalini Morogoro kutokana na maradhi ya Presha na kisukari, ameagwa Dar es salaam October 22 2013 na kusafirishwa kwenda kuzikwa kwao Mara.
Mpaka anafariki, Nyaisanga ambae amewahi kufanya kazi na vituo vikubwa kama TBC Zamani Radio Tanzania na ITV/Radio One alifariki akiwa na umri wa miaka 53 ambapo ofisi yake ya mwisho kuifanyia kazi ilikua Abood TV/Radio Morogoro.
Julius Nyaisanga
Julius Nyaisanga 6
Julius Nyaisanga 2
Julius Nyaisanga 3
Julius Nyaisanga 8
Julius Nyaisanga 5
Julius Nyaisanga 9
Julius Nyaisanga 10

Mke wa Marehemu
students1.Utafiti uliofanywa barani ulaya umegundua kuwa wanafunzi ambao ni mashabiki wa mchezo wa soka hufanya vibaya kwenye mitihani yao wakati timu zao zinapofanya vizuri yaani timu inaposhinda takwimu za matokeo ya mitihani huwa chini.

2.Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na The Happy Planet Index nchi inayoongoza kwa furaha duniani ni Costa Rica,marekani inashika nafasi ya 105 kwenye orodha ya nchi zenye furaha duniani.
San Jose Costa rica
San Jose Costa Rica
3.Kuna kitabu kimoja ambacho kinaitwa “what every man thinks about apart from sex” yaani “kitu ambacho wanaume wanafikiria tofauti na ngono”. kitabu hiki kimewahi kuweka rekodi ya mauzo ya juu , cha kushangaza kuhusu kitabu hiki ni kwamba kina kurasa 200 ambazo hazijaandikwa kitu chochote ndani yake.
KITABU4.Nchi ya marekani ni nchi ambayo inaongoza kwa kuwa na sheria za ajabu , mojawapo ya sheria hizo ni sheria iliyowekwa na serikali ya jimbo la North Carolina ambayo inasema kuwa ni hatia kuimba off key yaani ukiimba nje ya zile key za muziki basi umefanya hatia na unaweza kutozwa faini au kutumikia kifungo gerezani.

 Kama unafatilia habari za mastaa wa Marekani utafahamu kuwa hii issue alishawahi kufanya rapper Nicki Minaj wa Young Money.


Aliomba mashabiki watume picha wakiwa wamevalia mavazi kama yake na pozi zaki Nicki Minaj, Well Bongo Super Star Diamond amefanya yake kwenye instagram.
Picha zaidi ziko hapa.





NI ukweli usiopingika kuwa ndoa nyingi zimepoteza furaha kutokana na watoto kukosekana miongoni mwa wanandoa.


 Wanawake na wanaume wamejikuta wakiangukia katika mikono ya matapeli wanaojiita waganga na kufanyiwa mambo mengi ya

ajabu, ikiwa ni pamoja na kuf
anya mapenzi na mizuka au na watu ambao hawakuwatarajia ili tu waweze kupata watoto.

Hakuna ubaya wa kutafuta tiba ya ugonjwa endapo upo, lakini kutafuta tiba ya ugonjwa ambao haupo ni kuchosha mwili na matokeo yake huwa ni mabaya zaidi. Uchunguzi uliohusisha matatibu kutoka hospitali na vituo vingi vya afya unaonesha kuwa wagumba wengi wanaosaka tiba hospitalini wamebainika kutokuwa na matatizo ya kibaiolojia.

Ninaposema kibaiolojia nina maana kwamba wanandoa wengi
wagumba wamekutwa wakiwa na uhai katika viungo vyao vya uzazi.

Katika ulimwengu wa leo idadi ya watu wanaokosa watoto bila kuwa na sababu ya msingi inatajwa kuwa ni kubwa na kila siku wasichana na wavulana wanaingia katika chumba hiki cha huzuni isiyojulikana chanzo chake. Kukosa uzazi bila sababu ni tatizo ambalo limekuwa likizisumbua akili za wahitaji watoto wengi na mwisho kuwagotesha katika mawazo ya kurogwa na sababu kubwa ikiwa ni kutojulikana kwa chanzo cha wazi cha kutokuzaa kwao. 
Ukweli pekee ambao nimekusudia kuuzungumza leo kuhusiana na wasiokuwa na matatizo ya uzazi kutokuzaa ni ule ambao umeshawekewa misingi na watafiti walioandika taarifa yao katika jarida la Minerva Ginecologica la nchini Italia kwamba uchovu unaoletwa na mawazo ndiyo unaochangia kwa kiasi kikubwa watu wasipate watoto licha ya kwamba kibaiolojia hawana matatizo.

Tafiti za hivi karibuni zimebaini kuwa, wanawake wengi wenye viungo salama lakini hawazai, wana kiasi kikubwa cha homoni ya Cortisol inayoletwa na uchovu. Kwa mujibu wa utafiti huo aina hii ya homoni ndiyo inayosimamisha mchakato wa uzalishaji mayai kwa wanawake wakimbia riadha. Hivyo basi uwiano huu wa kasoro za ukuzaji mayai kati ya wakimbia riadha na wanawake wagumba unaweka usawa baina ya uchovu mkubwa wa mazoezi ya viungo na ule uchovu unaotokana na msongo wa mawazo ya ugumba. 
Uchovu wa kihisia huweza kumfanya mwanaume au mwanake asiweze kuzaa kabisa katika maisha yake. Hii ina maana kuwa watu wanaotingwa zaidi na mawazo ya kukosa fedha, migogoro katika ndoa zao na kujaribu mara kadhaa kupata watoto bila mafanikio wana uwezekano mkubwa wa kutokuzaa hata kama maumbile yao yataonekana kitabibu hayana kasoro. Imebainika kuwa watu wengi hujisogeza wenyewe katika nguvu ya kukosa mtoto kutokana na ukubwa wa kiu yao ya kupata mtoto, huku wakilazimisha kimawazo mchakato wa kubeba au kubebesha mimba kwa wakati ulipangwa na malengo yao.

Mkazo huu wa mawazo huwakumba hasa wanandoa na wapenzi ambao wanatamaa ya kupita kiasi ya kupata mtoto katika uhusiano wao.

Hawa hujiweka katika uzalishaji mkubwa wa homoni ya Cortisol ambayo huchipuka kwa kasi kutokana na msukumo wa kiu kubwa na ya haraka ya kukumbatia mwana. Kutokana na ukubwa wa tatizo hili la msongo wa mawazo, imebainika kuwa wagumba wengi wasiokuwa na kasoro katika viungo vya uzazi wanaweza kupona au kupata watoto bila hata kupewa tiba ya miti shamba au vidonge.

Tiba yake kubwa iliyobainishwa ni kupatiwa nasaha zitakazowaondolea mawazo tasa, wasiwasi na kutojiamini. Ukweli wa tiba hii ya ushauri imethibitishwa hivi karibuni na kituo kimoja nchini Marekani kinachojishughulisha na utafiti wa kuzalisha watoto, ambapo majibu yake yalichapishwa katika majarida na mitandao mbalimbali. 

Kwa mujibu wa taarifa ya kituo hicho asilimia 75 ya wanawake waliokosa watoto ambao walifika kituoni hapo na kupewa ushauri walifanikiwa kuzaa baada tu ya kuhudhuria kliniki na kupewa ushauri uliowatoa katika msongo wa mawazo. Nasaha ambazo zimekuwa zikitolewa na wataalamu hao si ngumu, bali ni zile zilizojaa maneno yenye kugeuza fikra hasi zenye kuondoa kiu kali ya kupata watoto kwa utashi na nyakati zilizopangwa na wahusika.

Pia wagumba hufundishwa namna ya kuepuka migogoro ya kimapenzi na kutoumizwa kupita kiasi na kejeli za watu kuhusiana na kutozaa kwao, huku wakijengewa imani kuwa kuzaa ni suala linalowezekana kwao, hivyo kuwafanya watupilie mbali hofu na mawazo kuwa wao ni wagumba. 

Lakini pamoja na nchi zilizoendelea kuwa na vituo vya kutolea nasaha kwa waathirika, bado wanasaikolojia wanakiri kwamba mtu mwenyewe anaweza kujiepusha na uchovu unaoletwa na mawazo kwa kurahisisha tatizo lake kutoka kutowezekana na kuwa linawezekana kutatuliwa. Akili ya mtu ndiyo inayopima na kuongoza utambubuzi wa ukubwa wa tatizo na si kwamba kuna matatizo makubwa na madogo kama watu wanavyofikiria.

Kwa maana hiyo ili mtu ambaye amejiwekea ukuta wa kutozaa kwa msongo wa mawazo yake kama nilivyosema aweze kuzaa lazima aondoe mawazo ya kwamba yeye ni mtu asiye zaa, kwani hakuna mtu wala vipimo vilivyompa majibu ya kwamba ni mgumba. Jambo jingine la kufanya ni kupuuza maneno ya kukatisha tamaa toka kwa watu wengine. Hii ina maana kuwa lawama zozote toka kwa mume/ mke au wanafamili zinazohukumu kosa la mtu kutokuza lazima zipuuzwe na zisipewe nafasi ya kutia simanzi moyoni.

Sambamba na hilo kuna suala la wanawake kuzingatia kalenda zao kwa kujichunguza na kubaini muda muafaka wa kukutana kimwili na mwanaume ili kupata matokeo mazuri ya utungishaji mimba.

Kwa mantiki hii kuna wanandoa wengi wameshindwa kupata mtoto kwa kutozingatia siku zenye uwezekano wa kupata mimba ambazi ni siku ya 11 hadi ya 16 tangu siku ya kumaliza hedhi.

Lakini kwa kuwa kuna suala la utumiaji wa dawa za uzazi wa mpango ni budi wahusiaka kusimamisha matumizi yake pindi mtoto anapohitajika ndani ya ndoa. Hata hivyo kuna umuhimu wa kutumia mitindo ya kuvuta kizazi nyakati za kufanya mapenzi, ili kuzipa msukumo wa haraka mbegu kunasa kwenye mfuko wa uzazi.

Sambamba na hilo wanaume wanatakiwa kuepuka ufanyaji holela wa mapezni ili kuzifanya mbegu zikomae na wakati wa tendo kuvuta hisia kali ili kuongeza msukumo wa manii kutoka kwenye uume kwenda kwenye uke. Na jambo la mwisho katika mchakato wa kupata mtoto ni lishe bora miongoni mwa wanandoa. 

Lazima miili iwe na nguvu za kutosha kusimamia uzalishaji wa mbegu bora. Inashauriwa wanaume waepukane na uvaaji wa nguo za ndani za kubana ambazo zinatajwa kuongeza joto kwenye kiwanda cha kuzalisha mbengu na hivyo kuzidhoofisha.
Posted: 22 Oct 2013 01:59 AM PDT
MacElvisMac Elvis alikuja Tanzania wiki mbili zilizopita kwa ajili ya consert Dar es salaam akiwa na wasanii wenzake kutoka Uganda ambao walirudi baada ya consert ila yeye akabaki ili kufanya kolabo na baadhi ya wasanii wa Tanzania.

Mtanzania Gee ambae ni rafiki yake, anasema ‘Alhamisi Elvis alikwenda kumtembelea rafiki yetu mmoja anaitwa Lulu (Sio mwigizaji) anaishi Mbezi Beach Africana ambapo Ijumaa jioni mida ya saa moja alijisikia kwenda kuogelea kwenye swimming pool, Lulu alimwambia asiogelee kwa sababu ilikua usiku umeshaingia lakini Elvis aliiamua kuogelea hivyohivyo’
‘Lulu alitoka nyumbani kidogo wakati huo Mac akienda kuogelea akiwa mwenyewe, ilikua ni kawaida kwake kuogelea mara nyingi huwa anapenda kuogelea hivyo hakikua kitu kigeni… Lulu aliporudi hakumuona Mac manake hakurudi hivyo akadhani mwimbaji huyu ameshaondoka, akawa anampigia simu rafiki anaeishi na Mac lakini haikupokelewa’ – Gee
‘Kesho yake mida ya saa nne mlinzi ndio akaona nguo pembeni na aliposogelea akaona mwili wa Mac ndani ya swimming pool chini ambapo baada ya kutolewa alionekana akiwa na jeraha kwenye paji la uso hivyo inaonekana alijigonga akitaka kujirusha, tumbo lake halikujaa maji kama ambavyo ilidhaniwa, tayari mipango ya kumsafirisha imekamilika na anapelekwa kwao Uganda leo October 22 2013′ – Gee

Ukimuuliza binti yeyote mwenye ndoto ya kuolewa,,akutajie sifa za mume ampendae,sifa ya "awe mpole" itakuwa ktk orodha ya mwanzo kabisa.



Ktk utafiti binafsi sifa hii imetajwa na wasichana 74 ikiwa ya kwanza,,wasichana 113 ikiwa ya 2.Lakini kwa wanawake walio ktk ndoa,,wanawake 20 walisema wanapenda mume mpole ikiwa sifa ya 1 na 42 waliobaki waliitaja ikiwa ya 2
Huo ni utafiti binafsi ambao ulitaka kujua tu UPOLE WA MWANAUME una nafasi gani kwa mwanamke

Lakini kwa nini wanawake au mabinti hupenda mwanaume mpole? Kwa nini mkorofi hatajwi kabisa? Je ni kweli ni watu wanaohitaji huruma kiasi hicho? Mtaalamu wa masuala wa mahusiano wa kimarekani Baruck Miller aliyetafiti mahusiano kwa miaka zaidi ya 20,,anasema "... Mwanamke anampenda mwanaume mpole ili AJITAWALE KTK MAHUSIANO..."
Siku zote,mwanamke anapenda awe huru kwenda apendapo au kupewa atakacho.Hivyo anapokuwa mbele ya mwanaume mpole hana wasi,,wala hana tabu ya kutimiziwa shida yake.Akikutana na mwanaume mpole sana kiasi cha kukaribia ujinga basi atamuendesha mume/mpenzi kama rimoti control.

Jambo wanalosahau wanawake ni kuwa,,upole wa wanaume wengi wanautafsiri kama ujinga,uzezeta au kuliona kundi hili la kuchuna wapendavyo.
Laiti wangekumbuka kuwa mwanaume mpole ni kama volcano tuli,,ikilipuka imelipuka basi sifa ya upole ingekuwa ya mwisho.

KUMEKUWA na maneno mengi juu ya uhusiano wa kimapenzi kati ya staa mwenye vyeo vingi Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kisha staa wa kikapu wa NBA ya Marekani, Mtanzania Hasheem Thabeet Manka.


Kwa mara ya kwanza mwanadada huyo amefunguka kupitia mahojiano maalum (exclusive interview) na gazeti bora la burudani Bongo, Ijumaa Wikienda na kufichua mazito nyuma ya pazia.

Jokate ni Miss Tanzania namba 2, 2006/07. Ana kofia nyingi kama mtangazaji wa Channel O, mwigizaji, mwanamitindo, MC, mwanamuziki na video queen wa nyimbo za Bongo Fleva.

DAKIKA 150
Katika mahojiano hayo ya dakika 150 (saa 2 na nusu) yaliyofanyika katika Makao Makuu ya Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita, pamoja na uhusiano wake na mastaa hao, Jokate anayependa kucheka na kuachia tabasamu pana, alifunguka mambo mengine mengi;

Ijumaa Wikienda: Jokate kuna taarifa kuwa uliwahi kuwa na uhusiano na Hasheem Thabeet. Je, ni kweli?
Jokate: Ni kweli. Nakumbuka ilikuwa baada ya Miss Tanzania 2006. Ilikuwa kitu kama 2007 au 2008.
Ijumaa Wikienda: Uhusiano wenu ulidumu kwa muda gani?
Jokate: Miaka miwili…mitatu (kicheko).

Ijumaa Wikienda: Ulikutana wapi na Hasheem na ilikuwaje?

Jokate: Tulikutana kwenye maonesho ya mavazi kwenye Ukumbi wa Water Front, Stesheni jijini Dar. Mwanzoni tulisalimiana lakini hakukuwa na chochote kwani nilikuwa nikikutana naye nacheka vile alivyo tall (mrefu). Naye alicheka tu.

PENZI LA HASHEEM
Ijumaa Wikienda: Ilikuwaje hadi mkaingia kwenye mapenzi?
Jokate: Baada ya kuwa washkaji tukiendelea kuchati, tulijikuta tumependana sana. Mimi nilijikuta nikimpenda sana Hasheem na bado nampenda sana lakini kuna mambomambo tu yalitokea kila mtu akawa kivyake.
Ijumaa Wikienda: Maisha yako ya kimapenzi na Hasheem yalikuwaje?

Jokate: Aisee usipime…nakumbuka tulikuwa tunanunua matunda tunakaa kwenye gari tunakula. Tunatoka wote sehemu mbalimbali japo hakupenda kujianika.
Ijumaa Wikienda: Una kumbukumbu yoyote mbaya kwa Hasheem?
Jokate: Wala…japokuwa kuwa watu walikuwa wananiona nimeharibika. Labda namfuata Hasheem kwa sababu ya fedha au vyovyote walivyosema lakini mimi nilimpenda sana.

Ijumaa Wikienda: Kabla ya Hasheem kulikuwa na mwanaume mwingine?
Jokate: Yaah…lakini sipendi kabisa kumzungumzia. Namchukulia Hasheem kama mwanaume wangu wa kwanza.

‘USICHANA’
Ijumaa Wikienda: Unaposema hivyo ina maana Hasheem ndiyo alikutoa ‘usichana’.
Jokate: Nisingependa kujibu hilo lakini hadi natoka kwenye Shindano la Miss Tanzania 2006, nilikuwa sijamjua mwanaume. Nafikiri nikisema hivyo inaeleweka.

KWA NINI ALIACHANA NA HASHEEM?
Ijumaa Wikienda: Umesema ulimpenda sana Hasheem. Je, kwa nini mliachana, kumwagana au kupeana likizo?
Jokate: Ilitokea tu halafu akatokea mwanaume aliyenikuta kwenye msongo wa mawazo akawa ananiliwaza nikaona yees…nijipoze moyo.

Ijumaa Wikienda: Kabla ya kuachana mliwahi kugombana?

Jokate: Kugombana ni sehemu ya mapenzi. Ni kuonesha kuwa mnapendana. Ilitokea hivyo kwangu kwa sababu Hasheem alikuwa na heshima tofauti na wanaume wengine. Nahisi hakuna kama yeye, alinionesha alikuwa ananijali kwa kiasi gani.


DIAMOND ALIMTIBULIA
Ijumaa Wikienda: Inasemekana mwanaume huyo ni Diamond.
Jokate: Yap…ni yeye lakini kulikuwa na vitu vingi akatumia nafasi au fursa kama wanavyosema siku hizi.

ANGEMTONGOZA MWAKA HUU ANGEKULA ZA USO
Ijumaa Wikienda: Ilikuwaje?
Jokate: Sijui…ilitokea tu. Nilikuwa kwenye hali fulani akatumia nafasi hiyo lakini angenitongoza mwaka huu nisingemkubali.
Ijumaa Wikienda: Jokate haukuwa mtu aliyetegemewa kugombea mwanaume na Wema Sepetu. Huoni kuwa uliharibu mtazamo wa watu juu yako?

Jokate: Kama nilivyosema sijui nini kilitokea.
Ijumaa Wikienda: Kwani ulikutana wapi na Diamond?
Jokate: Nakumbuka nilimwalika kwenye maonesho ya mavazi yangu. Watu wengi walikuwa wakisema kuwa nimemtoa uswahilini hadi ushuani. Sikupendezwa na watu walivyokuwa wanaponda.


Naye ni binadamu, anahitaji kila kitu anachohitaji binadamu mwingine. Ukweli ni kwamba yaliibuka maneno mengi mno. Baada ya hapo kweli alikuwa ananijali sana.


HAMKOSI MWANAMKE
Unajua jamaa anajua kuimbisha na ndiyo maana anawapata wanawake wengi. Mara ananiletea chakula, zawadi, nikitaka kwenda sehemu ananipeleka. Alikuwa anataka kwenda na mimi kila sehemu.


Ijumaa Wikienda: Vipi kuhusu kufumaniwa na Wema ukiwa na Diamond hotelini?

Jokate: Nakumbuka siku moja nilikutana na Diamond hotelini kuzungumzia kazi kabla sijaingia kwenye uhusiano naye, mara Wema akatokea, alipotuona akaondoka zake. Sasa sikujua nini kinaendelea. Huku na huku nikasikia eti Wema kanifumania jamani…hahahaa…


Ijumaa Wikienda: Ulidumu na Diamond kwa muda gani?
Jokate: Kama miezi miwili hivi...


Ijumaa Wikienda: Wakati unaingia kwenye mapenzi na Diamond hukujua kama yupo na Wema?


Jokate: (akiweka uso wa kazi) Nimesema sijui nini kilichotokea na nilikuja kujikuta najuta kuwa na Diamond japo naye ni binadamu.


Ijumaa Wikienda: Uhusiano wako na Wema ukoje?
Jokate: Simchukii Wema. Sina tatizo naye. Unajua lilipotokea lile tatizo la yeye kunikashifu niliona nikiendeleza malumbano haitakuwa busara.

Ijumaa Wikienda: Kwa nini uliachana na Diamond?
Jokate: Unajua Diamond ni mtu wa kujitangaza kuwa sasa nipo na huyu na mimi sipo hivyo so hata hapo sijui nini kilitokea lakini nitafanya naye kazi. Kuna wakati nilimwambia aniandikie wimbo ‘so’ tupo kikazi zaidi.
Ijumaa Wikienda: Unajuta kuwa na Diamond?
Jokate: Najuta. Ndicho kipindi ambacho kuliibuka mambo mengi sana.

SIRI YA DIAMOND KWA WANAWAKE
Ijumaa Wikienda: Diamond ni mwanaume wa aina gani?
Jokate: Mcheshi sana. Anajua kujali. Anajua kuzungumza na mwanamke kwa maneno matamu ndiyo maana akimtokea mwanamke hamkosi.

Ijumaa Wikienda: Diamond na Hasheem nani akikurudia unakubali?

Jokate: Hakuna lakini ukweli nilimpenda sana Hasheem.


ZAWAD

Katika dunia ya leo, watu hususan wafanyabiashara kuwa na wavuti (website) sio jambo la anasa wala la hiari. Kwa walio makini wavuti ni jambo la lazima.
Maendeleo ya Tehama yamefanya gharama za kutengeneza na kumiliki wavuti kushuka, huku watengenezaji wake wakiwa karibu na wateja.
Kila kona katika miji yetu wapo wataalamu wanaoweza kutengeneza wavuti, achilia mbali kampuni za Tehama kama vile Wordpress na Blogspot zinazowawezesha watumiaji wake kuwa na wavuti bila ya kulipia gharama yoyote.
Hata hivyo, kumiliki wavuti sio mwisho wa safari. Wamiliki wengi wana wavuti, lakini hazifanyi kazi kwa kuwa zimelala usingizi mnono. Kwa wenye biashara wavuti ni sehemu ya kujitangaza na pia njia mojawapo ya kuwasiliana na wateja.
Makala haya yanakusudia kuainisha makosa kadhaa yafanywayo na wamiliki wa wavuti na namna ya kuyaepuka kwa minajili ya kuupa mafanikio wavuti wako.
Kukosa mwelekeo.
Japo wavuti katika dunia ya sasa, ni sehemu ya biashara, wamiliki wengi hapa nchini hawajui nini kifuate baada ya kuwa na wavuti. Wengi huishia kwenye hatua ya kuwa na wavuti pekee.
Hivi umejiuliza kwa nini uliamua kuwa na wavuti? Haingii akilini kama jibu lako litakuwa ulifanya hivyo ili tu nawe uonekane.
Ili uweze kuona matunda ya wavuti, lazima ujue lengo na mwelekeo wako. Kwa wenye biashara, mwelekeo huo lazima uende sambamba na biashara husika. Kwa mtazamo wangu sioni tija ya kuwa na wavuti kama mtu hatojali maslahi hasa yale ya kibiashara.
Kutokutumia takwimu
Takwimu ni mojawapo ya vitu muhimu kwenye wavuti wowote. Hata hivyo, wengi hawajui umuhimu wake achilia mbali namna ya kuzitumia.
Swali muhimu, kama hujui idadi ya watembeleaji wa wavuti wako, wanafanya nini wakiwa huko au wanapendelea kurasa zipi za wavuti; utawezaje kupima uwezo wa wavuti uliouanzisha?
Kimsingi, takwimu hutoa picha halisi ya matumizi ya watembeleaji wa wavuti wako. Aidha takwimu zitakujulisha tabia za wateja wako, kurasa wanazopendelea, mahala walipo na hata muda wanaopenda kufungua wavuti wako.
Angalia mfano huu. Unamiliki wavuti kuhusu mgahawa uliopo Arusha, lakini kwa kutumia takwimu unabaini asilimia kubwa ya watembeleaji wanapatikana mkoani Dar es Salaam. Kwa mfanyabishara makini hii ni taarifa ya kuifanyia kazi kwa maendeleo ya mgahawa.
Ili kutatua tatizo hili, unashauriwa kutumia programu za takwimu, huku ukitafuta wataalamu wanaoweza kukutafsiria maana ya takwimu hizo kwenye lugha ya kibiashara zaidi.
Katika wavuti nyingi hivi leo,wahusika wameweka takwimu kuhusu watembeleaji pekee. Idadi pekee haitoshi kwani kuna mengi yanayopaswa kujulikana ili hatimaye yaweze kufungamanishwa na bishara na hata uwekezaji kwenye Tehama.
Kukosekana sehemu ya kutafuta taarifa
Kwa wavuti kubwa zilizo na vitu vingi au kufanyiwa mabadiliko ya mara kwa mara, sehemu ya kutafuta taarifa (search button) ni lazima.
Sehemu hii sio tu itasaidia kuokoa muda wa watembeleaji wa wavuti ambao hawana muda wa kuanza kujaribu kurasa moja hadi nyingine, lakini pia utasaidia kuongeza muingiliano kati ya wavuti na watembeleaji.
Cha muhimu hakikisha unakuwa na sehemu ya kutafuta taarifa kwenye wavuti wako. Pia hakikisha unaunganisa kitafuto hiki na mitambo ya takwimu, ili kukupa picha halisi ya vitu gani ambavyo watu wanavitafuta kwa kiasi kikubwa kwenye wavuti.
Zingatia mfano ufuatao; Una wavuti kuhusu saluni ya kinamama, ukiwa na sehemu ya kutafuta taarifa na kisha takwimu zikaonyesha watu wengi wanatafuta bidhaa X, taarifa hiyo itakuwezesha kuboresha mpango wa biashara yako.
Kurasa zisizoweza kutambazika
Kimsingi watu wengi wanapotafuta taarifa kwenye wavuti, hawasomi bali wanatambaza (scan) na huondoka mara wanapokosa taarifa husika. Hapa kuna kosa linalofanywa na wamiliki wa wavuti hasa Tanzania.
Wamiliki wengi wanashindwa kutoa picha ya website yao kwa jicho la kwanza. Wavuti na blogu nyingi za Tanzania zimejaa vitu vingi kiasi msomaji anashindwa aanzie wapi.
Ilivyo hutakiwi kuandika maneno milioni moja ili kumfanya mtu atumie wavuti wako. Watembeleaji hawana muda wa kuanza kudokoa kitu kimoja kimoja. Wengi wanadhani, kuwa na makala nyingi ndio kufanikiwa. Andaa taarifa inayojitosheleza katika njia nyepesi na rafiki zaidi.
Kukipa kisogo Kiswahili
Inasikitisha kuona wamiliki wengi wakitumia lugha ya Kiingereza kwenye wavuti zao ambazo kimsingi wateja wao wakubwa ni watumiaji wa lugha adhimu ya Kiswahili.
Inawezekana matumizi ya Kiingereza yakawa mujarabu zaidi ikiwa biashara husika ni ya kimataifa, lakini kama biashara ama taarifa inahusu zaidi Watanzania ambao wengi wanatumia Kiswahili, hakuna haja ya kutumia lugha ngeni.
Matumizi ya lugha ipi inafaa kwenye wavuti yategemee vitu kama vile lengo na mwelekeo wa wavuti na nani unawalenga. Ukijiuliza haya utakuwa na nafasi nzuri ya kuchagua lugha ya kutumia katika wavuti wako.
Wapo wanaotumia lugha zaidi ya moja kufikisha taarifa kwenye wavuti zao. Ni jambo la kupongeza na la kuigwa.
Mkata Nyoni ni mtaalamu wa Menejimenti ya Teknolojia ya Habari na Mshauri wa Biashara.Anapatikana kupitia barua pepe: mnyoni@dudumizi.com

Source:Mwananchi.

1Aliekua kocha wa club ya Manchester United Sir Alex Ferguson ambae hivi juzi jina lake lilizinduliwa rasmi kutumika kwenye moja ya barabara zilizokaribu na uwanja wa Old Traford, amekitambulisha kitabu chake kinaitwa ‘My Autobiography

Amezungumzia mambo kadhaa ndani ya hiki kitabu ikiwemo pia maisha yake ya soka kwa ujumla, vitu alivyokutana navyo.. wachezaji pamoja na matukio makubwa likiwemo la David Beckham kuondoka Manchester United mwaka 2003 ambapo namkariri akisema…
1. ‘Beckam alijiona yeye ni mkubwa kuliko Alex Ferguson, yani staa kuliko mimi’
2.  Alipoingia mapenzini na Victoria ndio kila kitu kilibadilika kuhusu yeye.
3. ‘Mimi ni mtu wa soka, wakati alipoiacha Real Madrid na kwenda LA Galaxy, kama angeniomba maoni ningemwambia exactly nilichokua nacho moyoni’
4. ‘Siku ulipotokea mkwaruzano kati yangu na yeye baada ya 2-0 dhidi ya Arsenal ndio ulikua wakati wa mwisho wa David Beckham Manchester United, majibu ya Beckham kwangu ndio yalinikasirisha sana’
5. ‘Nilikataa mara mbili ofa ya kuwa kocha wa England’

facebook 12Mtandao wa kijamii wa facebook una mpango wa kubadili sera yake ili kuwaruhusu watumiaji wake kuweza kuweka picha ambazo zina maudhui ya kutisha ambapo kama unakumbuka, May 2013 facebook ilipiga marufuku uonyeshwaji wa picha za matukio ya vurugu na mauaji pamoja na matukio yanayohusisha umwagaji wa damu na viungo vya mwili vilivyokatwa.

Sasa hivi huo uamuzi unageuzwa japo hata hivyo facebook itaruhusu watu wenye umri wa miaka 13 na kwenda mbele  kujiunga na kuweka picha za matukio kama haya lakini bado sera ya usalama ya facebook itaendelea kuzuia picha zinazoonekana kutukuza vitendo kama hivi.
facebook 133