Wapenzi wa muda mrefu Richard Laslett na Collin Gunther ambao wamedumu kwenye mahusiano kwa muda wa miaka 37 wamepata nafasi ya kuwa moja kati ya wapenzi wa jinsia moja 115 waliofungishwa ndoa kwa wakati mmoja mjini Toronto, Canada.
Ndoa hizo zimefungwa kwa pamoja na kuwakutanisha wapenzi wa jinsia moja kutoka maeneo mbalimbali duniani kusherekea nguvu ya mapenzi yao. Meya wa Toronto Norm Kelly amesema wanandoa hao wamekutana na kufurahia hatua hiyo muhimu ya kufunga pingu za maisha. Takribani nchi 15 duniani sasa zimeruhusu mapenzi ya jinsia moja .
|
Mamlaka nchini Australia imetoa tahadhari dhidi ya matumizi ya charger aina ya USB feki au zilizo chini ya viwango huku zikiwa zimechomekwa kwenye umeme baada ya mwanamke mmoja kufariki dunia wakati akitumia charger ya aina hiyo kucharge simu yake iliyokuwa imechomekwa kwenye kompyuta yake ndogo.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 28 alikutwa amevaa headphones masikioni akiwa na kompyuta yake mikononi huku akiwa na majeraha ya kuungua kifuani na masikioni nyumbani kwake huko Gosford, Kaskazini mwa Sydney.
Polisi nchini humo bado wanafanya uchunguzi kujua mazingira ya kifo hicho lakini kitengo cha biashara kilichofuatilia suala hilo kimetahadharisha kuwa charger za simu zilizo chini ya viwango ni moja ya sababu kubwa. Mwanamke huyo ambaye ripoti zinadai kuwa anatokea nchini Ufilipino na baadae kuwa raia wa Australia alivaa headphones zilizokuwa zimechomekwa kwenye kompyuta ndogo iliyokuwa imechomekwa kwenye socket ya umeme.
|
Ripoti zilizoandikwa na gazeti la The Daily Mirror zinaeleza kuwa lugha ya matusi kwenye nyimbo za Eminem ndio chanzo cha yeye kukataliwa kufanya show kwenye eneo la Hyde Park, Uingereza.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mmiliki wa Hyde Park, Linda Lennon ameeleza kuwa aliamua kutompa nafasi Eminem kuperform katika eneo hilo kwa kuhofia ujumbe wa nyimbo zke na lugha anayotumia ingewaudhi wateja wake. Ofisi ya Mayor wa jiji la London, Boris Johnson imeeleza kuwa haikuhusishwa kabisa katika uamuzi wa kumzuia Eminem kuperform katika Hyde Park. Walifafanua kuwa hawakufahamu Eminem ni nani na hawakuwa na uwezo wa kuingilia maamuzi ya Wamiliki wa eneo hilo. Eminen alitarajiwa kuperform katika Hyde Park June 3 kabla hajazuiwa.
|
Lupita Nyong’o anazidi kuwaongezea wakenya nafasi ya kutajwa kwenye tuzo za Oscar hata kama sio katika kupata tuzo tu baada ya kuongezwa kuwa kati ya watu 271 wanaounda Academy ya tuzo za Oscar mwaka huu.
Muigizaji huyo wa 12 Years A Slave, ambaye ni mshindi wa tuzo ya Oscar ya mwaka jana kama muigizaji bora wa kike msaidizi, anaungana na wasanii wengine waliong’ara mwaka jana katika tasnia ya filamu pamoja na mwanamuziki Pharrell Williams kama members wapya wa Academy hiyo. Wasanii wengine wenye umri mdogo watakaoungana na Lupita ni pamoja na Josh Hutcherson, Michael Fassbender, Ben Foster, Sally Hawakins, Julia Lousi-Dreyfus, Chris Rock na Jason Statham. Rais wa Oscar Academy, Cheryl Boone Isaac ameeleza kuwa Academy ya mwaka huu itawahusisha watu ambao wana vipaji zaidi na wabunifu katika masuala ya fulamu. “Mchango wao katika filamu umewaburudisha hadhira kote duniani, na tunajivunia kuwakaribisha kwenye Academy.” Aliseam Cheryl Boone.
|
Mashabiki wa soka nchini Uingereza wamegoma kuilaki timu yao wakati ilipowasili jijini Manchester, ikitokea nchini Brazil ambapo ilikuwa ikishiriki fainali za kombe la dunia za mwaka 2014.
Wakati kikosi cha Uingereza kikiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Manchester, palionekana kimya, kama mashabiki wa soka walikuwa hawajui kinachoendelea mara baada ya timu yao kushindwa kufurukuta kwenye michezo ya kundi la nne ambalo liliijumuisha timu ya Italia, Uruguay pamoja na Costa Rica. Hata hivyo wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza walionekana kutokuwa na furaha licha ya kurejea nyumbani salama, ambapo kila mmoja alionekana anashuka kutoka kwenye ndege akiwa na begi pamoja na mfuko mweupe ambao unahisiwa huenda ikiwa ni zawadi za familia zao. Kitendo cha mashabiki wa Uingereza kuilaki timu yao huko Manchester Airport, kimekuwa ni tofauti kubwa kilichoonekana katika nchi nyingine zilizoshindwa kuendelea katika fainali za kombe la dunia, ambapo imeonekana mashabiki wa nchi hizo kama Hispania wakijitokeza uwanja wa ndege na kuonyesha upendo dhidi ya wachezaji wao.
|
Alysia Montano, mwanariadha wa kike na mshiriki wa Olympic aliyewahi kushinda mara tano mashindano ya riadha ya Marekani ambaye hivi sasa anaujauzito wa miezi 8, bado anashiriki riadha na hali aliyonayo.
Alysia amewashangaza wengi baada ya kukimbia umbali wa mita 800 kwa dakika 2 na sekunde 32 huko California, jana (June 26), ikiwa amechelewa sekunde 35 tu ya uwezo wake wakati akiwa hana ujauzito. Mwaka 2010, mwanamke huyo akiwa katika hali nzuri alikimbia mita 800 kwa dakika 1 na sekunde 57. Mwanariadha huyo ameeleza kuwa yeye anajisikia vizuri kukimbia umbali huo akiwa na ujauzito na kwamba amekuwa akifanya hivyo katika kipindi chote cha ujauzito na ameruhusiwa na daktari. “I've been running throughout my pregnancy and I felt really, really good during the whole process.” Alisema baada ya kumaliza kukimbia.
|
Gwiji wa soka nchini Argentina Diego Armando Maradona ameushangaza ulimwengu wa soka baada ya kuonekana amevaa flana yenye maandishi yanayomuunga mkono mshambuliaji kutoka nchini Uruguy Luis Suarez ambaye ameanza kutumikia adhabu ya kufungiwa.
Maradona alionekana amevalia flana hiyo alipokuwa kwenye kipindi cha televishani usiku wa kuamkia hii leo huko nchini Brazil, ambapo maandishi hayo yalisomeka “Luisito, estamos con vos” yakimaanisha tupo pamoja na wewe. Hatua hiyo Maradona kuvaa flana yenye maandishi ya kumuunga mkono Luis Suares inadhihirisha ni vipi mchezaji huyo wa zamani wa Argentina hakubaliani na maamuzi ya FIFA. Mbali na kuhisiwa hivyo pia mashabiki wa soka duniani kote wameanza kubaini huenda watu wa Amerika ya kusini wakawa kitu kimoja katika harakati za kupingana na maamuzi ya FIFA ambayo yamenza kutafsiriwa kama kutaka kuwabeba baadhi ya wachezaji kwenye fainali za kombe la dunia zinazoendelea nchini Brazil. Hata hivyo hii si mara ya kwanza kwa Luis Suarez kuungwa mkono baada ya kuonyesha vitendo vya utovu wa nidhamu anapokuwa uwnajani, kwani kama itakumbukwa vyema mwaka 2011, wakati alipokabiliwa na sakata la kumtolewa maneno ya kibaguzi beki wa pembeni wa Man Utd Patrice Evra, wachezaji wenzake wa klabu ya Liverpool walivaa flana zilizokuwa na maandishi yalionyesha kuwa wapo pamoja na mshambuliaji huyo. Wachezaji wa Liverpool walivaa flana hizo kwa pamoja wakati wakijiandaa na mchezo wa ligi ya nchini humo dhidi ya Wigan katika msimu wa mwaka 2010-11.
|
Kenya imepiga marufuku uvutaji wa Shisha (Sheesha) kwa ladha 19 baada ya kugundua kuwa zinabeba madawa ya kulevya kama heroin, bangi na cocaine.
Amri hiyo imetangazwa jana na kuongezewa uthibisho na chombo kinachoshughulikia kampeni ya kupambana na matumizi ya dawa za kulevya, NACADA (National Campaign Against Drug Abuse) ambacho kilieleza kuwa kimefanyia majaribia ladha 100 za Sheesha wakiwa na ofisi ya wizara ya afya na wamegundua kuwa aina hizo 19 hubeba madawa ya kulevya. Kati ya ladha zilizopigwa marufu ni Al Fakher strawberry flavor, Al Fakher orange flavor, Al Fakher two apples with mint flavour, Al Fakher vanilla flavour, Al Fakher two appeals flavor, Al Fakher guava flavor, Al Fakher orange with mint flavor, Al Fakher orange flavor na
nyingine.
SOURCE:DJARO ARUNGU
|