advert

http://

Wednesday, 2 October 2013

DAWA YA FUNGUS YA MIGUU YAONEKANA KUWA NA UWEZO WA KUTIBU UKIMWI.


A drug commonly prescribed to treat nail fungus appears to come with a not-so-tiny side effect: killing HIV in cell cultures.

In a study performed at Rutgers New Jersey Medical School, not only does the drug Ciclopirox rid infectious HIV from cell cultures, but the virus also doesn't bounce back when the drug is withheld.
The same group of researchers had previously shown that Ciclopirox -- approved by the FDA and Europe's EMA as safe for human use to treat foot fungus -- inhibits the expression of HIV genes in culture. Now they have found that it also blocks the essential function of the mitochondria, which results in the reactivation of the cell's suicide pathway, all while sparing the healthy cells.
The researchers said that one aspect of HIV that makes it particularly persistent, even in the face of strong antiviral treatments, is its ability to disable a cell's altruistic suicide pathway -- which is typically activated when a cell is damaged or infected. In other words, infected cells that would normally commit suicide to spare healthy cells no longer pull any altruistic kamikaze missions. Ciclopirox tricks these cells back into their old ways with a double negative, disabling the disabling of the suicide pathway.
"The key thing these drugs do is, unlike anti-retrovirals in the current clinical arsenal, and there are lots of them and they have controlled this disease pretty successfully, these drugs kill the HIV-infected cell," says Michael Matthews, lead researcher and chair of the school's department of biochemistry and molecular biology. "That's what's so new and so promising about it."
It's obviously still going to take clinical trials on humans to study the safety and efficacy of Ciclopirox as a potential topical HIV treatment, but the fact that it's already deemed safe for one type of human use could make the regulatory process faster than usual.
Unfortunately, says Dr. Robert Gallo, a professor of medicine at the University of Maryland best known for co-discovering HIV in 1984, even if the topical antifungal treatment successfully kills HIV-infected cells in clinical trials, it would need to be a systemic treatment, not a topical one, to actually treat (instead of simply prevent) HIV.
"On the positive side, I know Mike Matthews, and he's a superb scientist, probably the lead guy on this," says Gallo, who did not participate in this research. "And that is exciting that it kills cells. That would be very exciting if you could give it systemically and it kills only HIV-infected cells. But topical treatment would be for prevention, not as a therapy. The only way you could use it as a therapy is systemically, and it would be unlikely this could be used systemically."
Posted: 01 Oct 2013 03:41 PM PDT
Matukio yote mawili yametokea jijini Dar es Salaam na kuacha vilio kwa ndugu na jamaa wakiwa hawaamini kilichowakumba wapendwa wao. 

WALIOTENDWA
Wanawake waliojulikana kwa majina ya Mwanahamisi na mwenzake Waisiko Robert Mtundi ndiyo waliodaiwa kuuawa na waume zao, kisa kikubwa kikidaiwa ni hofu ya wanaume hao kusalitiwa katika mapenzi.
WANAODAIWA KUTENDA
Juma Shaban, mkazi wa Manzese Kwamfuga Mbwa na Samuel Gesire Mlimi, mwenye makazi yake Msongola, maeneo yote hayo yapo Dar ndiyo wanaodaiwa kutekeleza ukatili huo wenye kutoa machozi mpaka basi.
MWANAHAMISI ALIVYOUAWA
Ilikuwa saa tatu usiku, Septemba 21, mwaka huu, kila familia ya eneo la Kwamfuga Mbwa ilikuwa ndani kwa chakula cha usiku au maandalizi ya kulala, ndipo waliposikia zogo kutoka ndani ya chumba cha kwa wanandoa hao.
ZOGO NA MANENO
Kwa mujibu wa majirani hao waliozungumza na gazeti hili baada ya tukio, zogo hilo liliambatana na maneno ya shutuma kutoka kwa Juma kwamba mkewe huyo si mwaminifu ndani ya uhusiano wao.
Majirani walisema shutuma za Juma ziliambatana na kelele za Mwanahamisi kuomba msaada akisema ‘nauawa jamani! Nauawa mwenzenu!’
Wakasema baada ya kama saa moja ya mzozo ulipita ukimya, ndipo kila jirani alitoka nje na kuulizana nini kinaendelea ndani ya chumba cha Mwanahamisi na mumewe!
“Baada ya dakika kumi, tulimwona Juma akitoka chumbani kwake huku akiwa anabofyabofya simu yake ya mkononi na kutokomea kusikojulikana,” alisema jirani mmoja huku macho yakiwa yamevimba kwa sababu ya kumlilia Mwanahamisi ambaye wakati huo alikuwa chini ameshakata roho.
Akaendelea: “Baada ya Juma kuondoka tulipatwa na wasiwasi, tukaenda kumwangalia Mwanahamisi chumbani na kumkuta hajitambui, amelala kifudifudi, ana majeraha sehemu mbalimbali za mwili huku akiwa ametapakaa damu. Alikuwa akipumua kwa mbali.
“Alikuwa hawezi kuongea vizuri, mimi nilimsikia akisema hana uhai tena, tumwombee mtoto wake. Ndani ya chumba tuliona viroba vya pombe kali na kisu kikiwa kimelowa damu, nahisi ndicho alichotumia Juma kufanyia ukatili wake.
“Tuliamua kumwahisha hospitali Mwanahamisi lakini kutokana na hali yake tuliona ni vizuri kuwasiliana na polisi ambao walifika baada ya muda.
“Lakini siku yake Mwanahamisi ilitimia kwani wakati polisi wakijiandaa kumchukua kumkimbiza hospitali aliaga dunia.”
KUMBE NI MWEZI MMOJA BAADA YA KUHAMIA
Wengine waliozungumza na gazeti hili siku ya tukio huku wakitoa machozi, walisema Juma ambaye alitoroka baada ya ukatili huo, alihamia kwenye nyumba hiyo mwezi mmoja nyuma lakini walipata umaarufu mtaani hapo kutokana na tabia yao ya kupigana mara kwa mara.
MJUMBE WA MTAA NAYE ANENA
Akizungumza na gazeti hili katika eneo la tukio, Mjumbe wa Nyumba Kumi, Techla Tesha aliwalaumu majirani na wapangaji wa nyumba hiyo kwa kushindwa kumpelekea taarifa mapema huku wakijua mtuhumiwa alikuwa na tabia ya kumpiga mkewe mara kwa mara.
WAISIKO ALIVYOUAWA
Awali ya yote, inadaiwa Waisiko ni mke mkubwa, mke mdogo jina lake halikupatikana mara moja.
Siku ya tukio, saa tatu usiku inadaiwa Samuel alikwenda nyumbani kwa Waisiko ambapo si mbali sana na nyumbani kwa mke mdogo na kuangusha timbwili zito.
“Samuel aliingia ndani na kuanza kumpiga mkewe mkubwa huku akionya majirani kuwa asiwepo mtu wa kwenda kuamua ugomvi wao.
“Sisi kama majirani tuliogopa kwa sababu Samuel alikuwa akitishia kuwa atakayeingia atamchoma kisu.
“Licha ya vitisho hivyo, tulisimama nje ya chumba chao huku vitisho vikiongezeka lakini namna ya kutoa msaada tulishindwa. Hatukujua chanzo cha ugomvi wao.
“Kauli za mwanamke kila wakati ziliashiria alichokuwa akitendwa kwa wakati huo, mfano kuna wakati tulimsikia akisema anavunjwa mgongo, akasema anang’olewa kucha. Pia kuna muda alilalamikia kuvunjwa mkono. Jamani, marehemu aliteswa sana kabla ya kufariki dunia,” alisema shuhuda mmoja.

NI MATESO YA USIKU KUCHA!!
Shuhuda huyo aliongeza: “Mateso ya mwanamke huyo huenda yalikuwa ya usiku kucha kwani nakumbuka mpaka alfajiri ndipo tukasikia sauti ya mwisho ya Waisiko akisema Samuel umeshaniua,  nimalizie kabisa basi. Baada ya hapo hatukusikia tena sauti wala vurugu.

SERIKALI YA MTAA YAZUNGUMZA
Makamu Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Msongola, Juma Chacha alipohojiwa kuhusiana na mauaji hayo, alisema ana taarifa lakini mtuhumiwa alikimbia baada ya kutenda unyama huo na anatafutwa na polisi.

UWAZI LABAINI KISA
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa chanzo cha ugomvi huo ni wivu wa mapenzi kwani ilidaiwa kuwa Samuel alikuwa akimhisi mkewe huyo kutoka nje ya ndoa. 
Chanzo chetu kilisema siku ya tukio, Samuel aliwachukua baadhi ya marafiki zake na kwenda nao baa ambako aliwaambia kuwa anahisi mkewe huyo ana jambo kwani akimuuliza kitu anamjibu jeuri.
Mtoa habari wetu alisema Samuel akiwaambia marafiki hao kwamba siku hiyo akirudi nyumbani, mwanamke huyo atamtambua.

POLISI WALIVYOIKUTA MAITI
Polisi walipofika na kuichunguza maiti waliikuta imevunjwa mkono wa kushoto na kung’olewa kucha za miguu huku uti wa mgongo nao ukiwa umevunjika.
Habari zinasema mara baada ya mtuhumiwa kufanya mauaji hayo, alikwenda kwa mkewe mdogo na kumtaka akamuone mke mwenzie, alipokwenda yeye nyuma akatoroka.
Polisi Mkoa wa Ilala tayari wamemfungulia jalada mtuhumiwa huyo lenye namba STK/RB/10058/2013 MAUAJI.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, ACP Marietha Minangi amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo.


SOURCE:UWAZI.


HATIMAYE siri ya kutekwa, kupigwa na kuumizwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Steven Ulimboka,  imefichuka baada ya raia wa Kenya, Joshua Muhindi, kuiambia mahakama kuwa polisi walimlazimisha kusema uongo juu ya kuhusika na tukio hilo.


Alidai polisi walimpa vitisho vingi ambavyo vilimfanya aseme ili kunusuru maisha yake. Muhindi, alitoa siri hiyo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mjini Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi, Aloyce Katemana baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka kumsomea maelezo ya awali.

Mshtakiwa anadaiwa alifika katika Kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo Kawe mbele ya Mchungaji Joseph Kiliba kuungama kwa kushirikiana na watu wengine, waliomtesa Dk. Ulimboka katika msitu wa Pande.

Kweka alidai alichukuliwa na kwenda kuhojiwa Oysterbay Polisi, alikubali kufanya kitendo hicho, akapelekwa kwa mlinzi wa amani Mahakama ya Mwanzo, akakataa ndipo alipofunguliwa shtaka la kutoa taarifa ya uongo.

Muhindi alikiri maelezo yote ni sahihi na Kweka aliomba apewe adhabu inayostahili kisheria kwa kuangalia mazingira ya kesi hiyo ilivyojengeka katika jamii na dhima iliyojificha katika jambo hilo. Hakimu Katemana, alimtaka Muhindi kujitetea ili mahakama iweze kumpunguzia adhabu, mshtakiwa alitumia nafasi hiyo kutoa siri ya sakata zima hadi alipofikishwa mahakamani kwa mashtaka hayo.

“Nilitokea Kenya kuingia Tanzania kwa ajili ya kufanya biashara ya nguo, nikiwa Arusha Juni 27, 2012 nilitekwa, nilihamaki na niliweza kufanya chochote alichokuwa akitaka nifanye aliyeniteka.

“Aliyeniteka alikuwa na silaha, aliniambia kila atakachoniambia nikaseme kwa atakayeniambia nikamwambie, kwa vitisho vyake nilipelekwa hadi Tanga mahali nisipopajua wala sijawahi kufika.

“Kaniambia mimi ni Mkristo, ananituma kwa Mkristo mwenzangu, alinipa taarifa ambazo zimesomwa hapa mahakamani na Wakili wa Serikali, nilienda kanisani kutokana na vitisho, yule alikuwa mtu wao ningesema vinginevyo angewaambia ikabidi nimpe taarifa mchungaji kama nilivyoambiwa niseme.

“Nilipokubali kosa kwa kuogopa vile vitisho walinitoa pale kanisani na kunipeleka Polisi Oystebay, Polisi waliniambia ukiendelea kusema vile tulivyokwambia tutakurudisha kwenu na kukubadilishia maisha yako.

“Mimi ni Mkristo, ile kubadilishiwa maisha isingenifanya niseme uongo bali nilisema uongo kwa kuhofia vitisho, Polisi wakubwa walikuja kuniambia tuambie vile vile watu walivyokwambia kusema, walinirekodi nikaona haina haja ya kubishana na Serikali,” alidai.

Alidai baada ya kurekodiwa alipelekwa kwa mlinzi wa amani akaeleza vile vile, lakini alishangaa kuona anafikishwa mahakamani kwa mashtaka ya kujaribu kumteka Dk. Ulimboka.

“Siilaumu Serikali, Polisi, Mungu wala Wakili wa Serikali kwa kukaa gerezani zaidi ya mwaka, najilaumu mwenyewe kwa sababu hata ningekufa kwa kutokubaliana nao mimi si bora kuliko watu wengi katika nchi hii.

“Suala hili lilileta shida katika Serikali ya Tanzania, naiomba mahakama iniamini kwamba taarifa hizi nilizitoa kwa hiari yangu kwa sababu nilikubaliana nao kwa kuhofia kutendewa vitendo vya kuhatarisha maisha yangu.

“Nimekosa mbele ya Mungu na mahakama, naomba kwa ubinadamu na upendo nifikiriwe adhabu kwa sababu nina miaka 23, sijajipanga kimaisha na mkiwa kama wazazi mfikirie kwani hamjui kitakachokuja watokea watoto wenu, katika adhabu mzingatie hayo,” alimaliza kuomba.

Akisoma hukumu hiyo, hakimu Katemana alisema kazingatia maelezo ya pande zote mbili, mshtakiwa alikaa gerezani zaidi ya mwaka, adhabu ya makosa yanayomkabili kisheria ni miezi sita jela au faini ya Sh 1,000.

“Mahakama imezingatia hoja za pande zote mbili, mshtakiwa amekiri kosa hivyo mahakama inamuhukumu kwenda jela miezi sita au kulipa faini ya Sh 1,000,” alisema Hakimu Katemana.

Muhindi aliyefikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Julai 2012, alikuwa hana fedha ya kulipa faini hiyo hivyo mwandishi wa Redio Times FM, Chipangule Nandule, alitoa Sh 1,000 kwa ajili ya kumnusuru kwenda jela miezi sita

Wema kunyongwa China’ ndio kichwa cha habari iliyomtoa machozi Miss Tanzania (2006) Wema Abraham Sepetu leo iliyoandikwa na gazeti liitwalo ‘Filamu’ katika ukurasa wake wa mbele.


Wema ambaye ni CEO wa kampuni ya Endless Fame leo alianza kwa kupost picha ya gazeti hilo na kuandika “Hahahahha.. haya niombeeni watanzania…. aisee… magazeti ni noumerrr… mambo ya kunyongwa tena na wakati sufuria zina shake zenyewe… dah… this made my day”

Na masaa mawili baadaye hiki ndicho Wema alikiandika kupitia Intagram kuhusiana na kilichoandikwa na gazeti hilo.

Dah, Siwezi sema niko happy, im not at all, na sikuwahi kufikiria kwamba magazeti yetu ipo siku yatakuwa na gut ya kuandika uongo wa namna hii. Just because nakaaga kimya ndo muone kwamba mnaweza nionea all da time, roho inaniuma sana, naumia kwasababu nimechoka kuchafuliwa jina bila sababu.

Nimesema nitoke zangu kimya kimya kuja huku kujihangaikia zangu kuhusu kazi zangu ila nimeonekana nimekuja kuuza unga na nitanyongwa soon. Wen are you guys gon leave me in peace..sidhani kama nishawahi kumkosea mtu yeyote kati yenu. Maskini ya Mungu naishi maisha yangu mwenyewe sina habari na mtu. Sijawahi hata kufikiria kufanya those stuff. Nimeumia sana. Da last time I cried was wen nilipoambiwa nina pepo la ngono…leo ninalia ten aim jus so so hurt… God help me please.

Wema siku za karibuni amekuwa aki post picha mbalimbali zinazoashiria yuko nje ya nchi.

Tunasikitika kuwaarifu kuwa kutokana na sababu zisizozuilika, tutashindwa kuendelea kuwaletea habari mpya kupitia tovuti yetu (www.mwananchi.co.tz) na mitandao ya kijamii ya Mwananchi kwa wakati wote ambapo uzalishaji wa gazeti la Mwananchi utakuwa umesitishwa.


Tunasikitika kwa usumbufu wowote utakaosababishwa na hali hii na tunatumaini mtaendelea kuwa nasi wakati wa kipindi  
 hiki kigumu cha mpito. Tunatarajia kurejea rasmi hewani na habari moto moto wiki ijayo, Ijumaa, tarehe 11 October.

Tunawakaribisha muendelee kusoma habari zetu za zamani (archives) kwenye tovuti ya Mwananchi na kurasa zetu za Facebook na Twitter ili mzidi kuhabarika.

Pia tunawakaribisha mtembelee tovuti zetu za www.thecitizen.co.tz na www.mwanaspoti.co.tz ambazo zitaendelea kufanya kazi kwa ufanisi, zikiwaletea habari za uhakika na kuaminika kipindi hiki ambapo Mwananchi imefungiwa.

Ahsanteni,

Wahariri.

Mbunge wa viti maalum kupitia kundi la vijana toka chama cha mapinduzi akiwakilisha mkoa wa Mara wilaya ya Bunda alikuwa akifanyiwa mahojiano katika kipindi cha ''hot mix'' kinachorushwa kupitia kituo cha television cha EATV - Chanel 5!


Akaulizwa swali kuwa nje ya siasa anapenda kufanya shughuli gani?mojawapo ya shughuli aliyoitaja kwamba huifanya ni pamoja na kusoma vitabu na kusikiliza hotuba za wanaharakati kama Martin Luther King Jr., Mwalimu Nyerere na Mandela! 


Katika kukoleza maelezo yake akasema anapenda sana kusoma kitabu kinachoitwa ''How to be a Good Political Leader''. Mtangazaji akamuuliza jina la Author wa hicho kitabu lakini mheshimiwa mbunge akashindwa kumtaja kwakuwa alikuwa hamkumbuki pamoja na kuomba apewe muda ili amkumbuke!!

MY TAKE:
Kwa mtazamo wangu si rahisi mtu kusahau jina la author wa kitabu unachokipenda kukisoma mara kwa mara! Pengine Mh.Esther alikuwa anatafuta mileage kwamba ni msomaji mzuri wa vitabu lakini kachemka kwa kutomjua author wa kitabu akipendacho!


source-JF.



leo tarehe 2 October ni siku ya kuzaliwa kwa Diamond Platnum na katika siku hii maalum amepewa zawadi ya Wimbo na Dogo aitwaye Dogo S.Kide anayedai Diamond ni nduguye wa Damu na amemtenga wala hakumbuki alipotoka.

Wimbo huu kiukweli inamwelezea Diamond Kabla hajatoka Kimuziki.Dogo kaua balaa.Kama hujapata bahati ya kuisikiliza basi isikilize hapa Chini na kuidownload.Ni Bonge 1 la Ngoma.Happy birthday Diamond Platnum.

 Rihanna's New Look iliyoteka headlines kwenye blogs na website tofauti Duniani. Hapa alikuwa akifanya shooting ya video yake mpya ya Pour It Up.

 




 Alicia Keys amefanya kazi kubwa ya kurudisha 
umbo lake baada ya kujifungua. 
Hii Ndio Moja ya show zake za kwanza alizo 
fanya baada ya kurudisha Shapu yake. 








Msanii MAC 2 B amezikwa  leo katika makaburi ya YOMBO MAKANGALAWE  wasanii waliojitokeza kumzika ni wachache sana tofauti na misiba mingine ya wasanii inavyokuwa, ''hii kitu yakuchagua watu wakuwazika sio nzuri kabisa alisikika mdau mmoja akisema'' wasanii wana ubakuzi na hawana ushirikiano.ukiangalia hapa kuna wasanii wachache sana waliojitokeza kumzika mac 2 b. Na hawa ndio wasanii niliowaona leo na watu maalufu katika msiba wa mac 2 b. CRAYZE BUFA,PROD LAMAR,MABAGA FRESH,MOX,KIMALIO,HK,RICH ONE na DAZ BABA .

wasanii wengine mko wapi jaman sio vizuri kabisa.

Mwigizaji Irene Uwoya ambae alipata tuzo ya Steps kama mwigizaji bora kike 2012/2013 amethibitisha kuacha kuigiza movie kwa sasa ili kufanya kazi ambayo ameianza hivi karibuni.


Namkariri akisema: “Nimeamua kuacha mambo ya movie na kuwaachia wengine, haya maamuzi nimeyafanya kama miezi sita iliyopita… Mara ya mwisho kuigiza ni zaidi ya miezi sita iliyopita pia.”

Irene ambae ni mama wa mtoto mmoja kwa sasa anafanya show ya TV ya kusaidia Watanzania wanaoishi kwenye nyumba ambazo ni mbovu au hazina mahitaji muhimu yanayotakiwa kwenye nyumba.

Ni show ambayo haitahusika kujenga nyumba bali kuzirekebisha kwa gharama za mamilioni kwa kutegemea ubovu wa nyumba yenyewe, ambapo Irene amethibitisha hakuna kiwango cha mwisho cha pesa kama bajeti ya kutengeneza nyumba moja bali lengo ni kukarabati nyumba ikamilike.

Movie alizocheza mpaka sasa zinafika 40 lakini za kwake ni nne tu na amekiri kwamba kuacha kwake kuigiza hakuta mshushia kipato chake cha siku zote ambapo kwa movie moja ya kwake mwenyewe alikua anaiuza mpaka kwa milioni 35.

Show yake ya TV imeshaanza kuonekana Tanzania pamoja na kupata wadhamini ambao watamuwezesha kwenye kazi hii kubwa ya kupokea maombi ya Watanzania mbalimbali ambao wanahitaji nyumba zao zirekebishwe bure, kupitia kipindi hicho cha TV.


Mama  mmoja  nchini  Kenya  amejifungua  mtoto  wa  ajabu  ambaye  anafanana  na  viumbe  wawili  wa  dunia  hii.


Sehemu  ya  juu ya  mtoto  huyo  inafana  na  chura  huku  sehemu  ya  chini  ikifanana  na  binadamu  wa  kawaida....

Mtoto  huyo  ambaye  alizaliwa  wikiendi iliyopita  anaonekana  kutokuwa  na  shingo  huku  macho  yake  yakiwa  kama  ya  chura.

Ripoti  ya  kitaalamu  toka  hospitali  ya  Gaurishnkar  ambako  mtoto  huyo  alizaliwa  imeeleza  kuwa  mama  huyo  aliingiliwa  na  mbegu  za  uzazi  wa  chura wakati  akioga  katika  bwawa  la  maji..

"Tulifanya  mazungungumzo  na  huyu  mama  na  akatueleza  kuwa  alikuwa  na  mazoea  ya  kuoga  katika  bwawa.Tunaamini  kwamba  mbegu  za  chura  zitakuwa  zilimwingia  wakati  akiwa  katika  siku  hatari"..Alisema  dakatari  mmoja.


Godzilla akiwa katika studio za R NAME

    R Name na Suma Ryder katika pozz.
   Producer R NAME

Anaitwa Tonya na timu yake ni Mashujaa ya Vingunguti.Amekuwa Bingwa wa Pool Table Mwaka huu.

Mashindano hayo yalifanyika huko Morogoro ambapo Timu yake imeambulia nafasi ya 4 huku Top Land ya Kinondoni ikiibuka Clab Bingwa Mwaka huu.Nafasi ya pili Mpo Afrika na ya Tatu ni Timu kutoka Mkoa wa Manyara.