|
Wanasayansi wa maabara ya Bristol Robotics Uingereza wamegundua njia ya kutumia mkojo kama chanzo cha kuzalisha umeme wa kuchaji betri za simu, na kudai kuwa wa kwanza kutengeneza “the world’s first microbial fuel cells (MFC) powered mobile phone”.
Watafiti hao walielezea juu ya ugunduzi wao kupitia jarida la ‘Physical Chemistry Chemical Physics’.
Dr Ioannis Ieropoulos amesema, huo ndio ugunduzi wa kwanza wa kuzalisha nguvu ya umeme kwa kutumia mkojo, na katika majaribio ya utafiti huo wamefanikiwa kuchaji simu ya Samsung.
Wanasayansi hao wanaamini kuwa teknolojia yao inaweza kutumika katika mabafu huko mbeleni kwaajili ya kuwashia mashine za kunyolea au kupasha moto maji ya kuoga na kuwasha taa.
|
KUFUATIA Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, staa wa Filamu za Kibongo, Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ au maarufu kama Madam amebadilika na kuondoa vitu vyote visivyo vya asili mwilini mwake.
Wema alitupia picha yake kwenye mtandao wa kijamii akionekana amekata nywele zote huku akiwa ameondoa kope za bandia na kutoa kucha alizobandika kuashiria kuuheshimu mwezi huu huku akibaki na kila kitu cha asili yake.
“Mwezi Mtukufu ni wa kuheshimiwa na kuweka kila kitu pembeni, nafurahi kuwa hivi kwa maana hata kama nikifunga swala zangu zitapokelewa vizuri,” alisema Wema.
|
Mwaka 2013 utakuwa na surprise nyingi sana... So far tumeshapata surprise kibao ikiwemo ile ya jana ya promoter na Mkurugenzi wa Watanashati Entertainment, Ostaz Juma na Musoma kuingia kwenye hip hop na kurekodi wimbo mmoja aliomshirikisha Young Killa.
Surprise zinaendelea na sasa inakuja bombshell nyingine. Kwa mujibu wa mtangazaji wa Take One ya Clouds TV, Zamaradi Mketema, muigizaji wa filamu nchini maarufu kama Mzee Magali ametupa karata yake kwenye muziki.
“Mzee magali augeukia mziki wa bongo fleva now.. sikiliza movie Leo siku ya KESHO on CLOUDS FM Radio ili usikie wimbo wake mpya kabisa wa kwanza ambao ameufanya SAA NNE na Dk 45 asubuhi,” ameandika Zamaradi kwenye Instagram.
|