advert

http://

Tuesday, 25 June 2013

MAGAZETI YA LEO!

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

IMG_2565
 Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Tamko la Mount Meru la kuwalinda waandishi wa habari 
wakiwa kazini Afrika Mashariki, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Bw. Francis
 Stolla akizungumza machache wakati wa uzinduzi huo ambapo alisisitiza umuhimu wa uhuru
 wa vyombo vya habari katika kujenga Demokrasia na Utawala Bora katika Ukanda wa Afrika Mashariki na kati.
 Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Misa-Tan Bw. Mohammed Tibanyendera (wa tatu kushoto),  Mjumbe wa MCT  Bw. Allan Lawa (kulia),  Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Abubakar Karsan
 ( wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa MISA-TAN Bw. Tumaini Mwailenge (kushoto). (Picha na Zainul Mzige wa Dewji Blog).
IMG_2504
Mtangazaji wa Radio Clouds Fm Regina Mwalekwa akisoma Tamko rasmi la Mount Meru lililoandaliwa siku ya maadhimisho ya Uhuru wa vyombo vya habari Duniani yaliyofanyika Mei 3-4 mwaka huu jijini Arusha yaliyohudhuriwa na washiriki mbalimbali toka vyombo vya habari, redio za jamii, jumuiya  mbalimbali za Kimataifa, Taasisi za mafunzo ya tasnia ya habari na mifuko ya Maendeleo ya Tasnia ya habari kutoka Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda.
IMG_2519
Mgeni rasmi Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Bw. Francis Stolla (wa pili kulia) akizundua rasmi Tamko la Mount Meru linalozunngumzia vipengele mbalimbali vitakavyowalinda waandishi wa habari Afrika Mashariki.
IMG_2533
Mgeni rasmi Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Bw. Francis Stolla akionyesha Tamko rasmi la Mount Meru la kutetea Uhuru wa Vyombo vya Habari kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.
IMG_2543
 Mgeni rasmi Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Bw. Francis Stolla akizindua rasmi CD ya wimbo ulioimbwa na Mjomba Band unaoitwa “Uhuru Wangu” uliopigwa kwa mara ya kwanza wakati maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika katika Hoteli ya Naura Springs jijini Arusha. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mwenyekiti wa Misa-Tan Bw. Mohammed Tibanyendera ( wa pili kushoto), Mjumbe wa MCT  Bw. Allan Lawa (kulia) na Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Abubakar Karsan (kushoto).
IMG_2550
Sasa umezinduliwa rasmi….Kaa tayari kuusikiliza katika radio mbalimbali na mitandao ya kijamii hapa nchini.
IMG_2490
Mjumbe wa MCT  Bw. Allan Lawa akizungumza umuhimu wa waandishi wa habari kujali maslahi mapana ya taaluma ya uandishi wa habari katika mchakato wa kuandika Katiba mpya kupitia mabaraza ya Katiba ya Wilaya.
Vile vile alisisitiza umuhimu wa waandishi wa habari kushiriki kikamilifu katika kujadili rasimu ya Katiba mpya iliyozinduliwa hivi karibuni na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal ili kuhakikisha Taifa linapata Katiba Mpya inayojali Uhuru wa vyombo vya Habari hapa nchini. 
IMG_2595
 Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Abubakar Karsan akifafanua jinsi  Mfuko wa Mwangosi utakavyokuwa ukisaidia waandishi wa habari wanaopata majanga wakiwa kazini vile vile utaenda sambamba na Tuzo ya Mwandishi ambaye atakuwa amepata matatizo, misukosuko katika kutafuta habari za uchunguzi na Tuzo hiyo itakuwa ikitolewa kila mwaka Septemba 6 siku aliyokufa Daudi Mwangosi na mshindi atajinyakulia Milioni 10 zitakazotolewa na waendeshaji wa mfuko huu UTPC.
IMG_2497
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania Jane Mihanji akiteta jambo na Usia Nkhoma Ledama wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) (Wa pili kushoto) na Bi. Rose Mwalimu kutoka UNESCO (wa pili kulia).
IMG_2585
Mdau kutoka Chama cha waandishi wa habari Wanawake Tanzania (TAMWA) akitoa maoni yake juu ya tamko la Mount Meru kwenye uzinduzi uliofanyika leo jijini Dar katika Hoteli ya Peacock.
IMG_2575
Baadhi ya waandishi wa habari waandamizi nchini kutoka kushoto ni Shermax Ngehemera Mhariri wa The African, Hamis Mzee wa MCT na Mhariri wa zamani wa Mwanaspoti ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osiah.
IMG_2495
Wadau mbalimbali kutoka kwenye vyombo vya habari waliohudhuria uzinduzi wa tamko la Mount Meru.
Kufuatia Mkutano wa Wadau wa Habari Afrika Mashariki waliadhimia yafuatayo;-
1.Serikali zote nchi za Afrika Mashariki zihakikishe kuwa Katiba za nchi zao zinakuwa na vipengele kwa ajili ya:
-Kuwa na tasnia ya habari ambayo ipo huru, salama na yenye kujitegemea ikijumuisha usalama wa wanahabari.
-Sheria nyingine zote ziheshimu Katiba  za nchi zikiendana na vyombo na mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu.
2. Wamiliki wa vyombo vya habari wafanye marekebisho ya miundo ambayo itazingatia yafuatayo;
- Uendeshaji bira- Ikiwa ni pamoja na masuala ya Ajira, Mishahara, Mikataba, Motisha na Marupurupu mengine ya kifedha.
- Viendeshwe kwa kufuata na kuheshimu miiko ya Kitaaluma.
-Kuhakikisha kuwa wanahabari wote  wanakuwa na Bima.
-Vyumba vya habari viongeze uwekezaji katika mitandao ya kijamii pamoja na utoajji elimu kwa wanahabari kuhusu mitandao binafsi yaani Blogs.
3. Baraza la Habari lishirikiane na taasisi na vyama vya kitaaluma vya wanahabari ili kudumisha na kulinda ueledi na umoja katika tasnia ya habari.
4. Wanahabari waanzishe vyama vya wafanyakazi ili kuwezesha na kuongeza mapatano na makubaliano ya hiari sehemu za kazi.
5. Wamiliki wa vyombo vya habari walinde na kutetea usalama wa wanahabari na vyombo vyao kupitia
-Wamiliki wa vyombo vya habari kuweka na kuzingatia taratibu za usalama sehemu za kazi
-Wamiliki wa vyombo vya habari wahakikishe wanwapatia waandishi wa habari vifaa vya usalama au vya kujikingia na hatari na wawezeshe mafunzo juu ya taratibu za usalama.
-Kujumuisha mitaala ya mafunzo ya usalama na ulinzi katika taasisi zote za mafunzo ya uandishi wa habari.
- Wanahabari wao binafsi wachukue vipaumbele na tahadhari katika usalama wao binafsi.
6. Jumuiya ya Afrika Mashariki lizitake nchi wanachama wake ambao walitia sahihi itifaki ya Udhibiti wa Tovuti wajiondoe katika Mkataba huo ikiwa ni njia moja wapo ya kudumisha utawala bora na uwajibikaji.
7. Serikali za Afrika Mashariki zifanya juhudi katika kuwezesha uanzishwaji wa mfumo wa kisheria wa kuruhusu uendeshaji bora wa mitandao ya kijamii na wakati huo huo wakilinda uhuru wa wadhibiti ili kuboresha na kuendeleza uhuru wa mitandao ya kijamii katika eneo la Afrika Mashariki.

WATOTO wawili walifariki na wengine saba wa familia moja kulazwa katika hospitali kuu ya wilaya ya Kilifi baada ya kula mhogo uliokuwa na sumu.
Kulingana na baba mzazi wa watoto hao Bw Donald Nzai mkewe alienda kliniki katika zahanati ya Vitengeni lakini alipokuwa anarudi akaomba mhogo kutoka kwa jirani.

“Alipofika nao nyumbani aliutayarisha na kuuchemsha ambapo tulikula sote tuliokuwa nyumbani lakini saa chache baadaye mtoto mmoja akaanza kutapika,” akasema.

Alisema alimwambia mkewe amchukue na kumpeleka katika zahanati aliyokuwa ametoka ambapo alitibiwa na kurejeshwa nyumbani wasijue sababu ni ule mhogo.

Bw Nzai alisema ilipofika saa mbili usiku wa juzi walipokuwa wametayarisha chakula cha usiku na wako karibu kula, watoto wote waliokuwa wamekula mhogo huo wakaanza kutapika vibaya.

Alisema walishirikiana kama familia na kuanza kutafuta njia za kuwapeleka hospitali ya Dida kwa uchunguzi wa kimatibabu.

“Wawili kati ya watoto wangu walikuwa hali mbaya sana ambao walifariki wakipokea matibabu katika hospitali ndogo ya Dida. Nalaumu maafisa wa matibabu kuchukua muda mrefu kuja kuwabeba watoto wangu kuwaleta Kilifi,” akasema.

Kupona
Alisema kama gari la kubeba wagonjwa wa dharura kutoka hospitali kuu ya wilaya ya Kilifi ingelikuja mapema, watoto wake wangelikuwa wamepona kwani walisumbuka kuanzia juzi mchana hadi mapema Ijumaa alfajiri mwendo wa saa kumi na moja.

Mamake watoto hao Bi Kanze Donald ambaye amelazwa katika hospitali kuu ya Kilifi pamoja na watoto wake wanne na wajukuu wawili alisema anajuta kuomba mhogo huo kwani kama angejua ni mhogo wa sumu asingethubutu kuuomba.

“Sitasahau maishani mwangu yote, nitaishi nikikumbuka. Niliuomba kwa nia njema lakini matokeo yake yamenipokonya wanangu wawili,” akasema huku akilia.

Naibu wa spika wa bunge la kaunti ya Kilifi na mjumbe mwakilishi wa eneo hilo Bw  Teddy Mwambire  alisema si mara ya kwanza watoto kufariki mkutokana na kula mihogo yenye sumu sehemu hiyo.

Alisema mwaka jana watoto watatu walifariki baada ya kula mhogo uliokuwa na sumu japo haukutoka kwa mkulima huyu wa juzi.

Bw Mwambire alisema ataongea na afisa tawala wa sehemu hiyo ili kutafuta njia ambayo itazuia watoto kufariki mara kwa mara hasa wakati wa njaa kama sasa kwa kula mhogo wa sumu.

Kiukweli nimejiuliza maswali mengi sana juu ya huyu msanii na 
sijapata jibu,imekuaje yeye pekee katika wasanii wote wale kwenye
huo msafara ndo azomewe na kurushiwa machupa na makopo ya
 
soda wakidai atoke hawamtaki.Naye kwa kuonyesha dharau alikomaa
mpaka akatimuliwa jukuani na Mabaunsa,kwamba toka bwana hutakiwi
kuimba hapa jukuani.

Hivi baada ya kushuka jukuani alijisikiaje?Na hii ni dalili ya nini kwake?
Mtu mwenyewe ndio kwanza ana nyimbo 3 lakini mmh!!
Aliwai pia kutimuliwa Kigoma All Stars kwa madai kuwa hana nidhamu.
Amewai pia kumsingizia msanii wa NAKO 2 NAKO eti kamuibia Vifaa 
vya gari yake.

Ommy huyu huyu juzi kati hapa alitoa maneno ya kashfa kwa marehemu 
Albert Mangwea kuwa kafa maskini na amechoka kuzika watu wenye 
majina makubwa ila maskini.

Wewe kama mdau wa muziki wa kizazi kipya hapa Tanzania sema chochote
juu ya huyu msanii kuzomewa na kurushiwa makopo na machupa na 
washabiki wake wakidai hawamtaki kabisa.





Mariam Migomba katika pozz ndani ya gari yake.
                                            Mwanamke urembo,na hasa ukijua kuzitumia



Mariam Migomba ni moja kati ya watangazji maarufu hapa Tanzania,anafanya vipindi vya TV na radio.
Tegea sikio j3 hadi ijumaa TBC fm saa 3 hadi 6 mchana.Hutochoka kumsikiliza kwa kweli.Ana sauti nzuri sana na pia ni mbunifu sana katika vipindi vyake.Kwa sura pia Mwenyezi Munngu kamjalia.
Amewai pia kuwa Mtangazaji bora wa Kike anayefanya vipindi vya Taarabu nchini Tanzania.
Wanajeshi wakitoa kichapo  huku mwingine akiwa ameninginizwa kama 

swala na wawindaji porini.



Taasisi ya Kupambana na Ukimwi Nchini (Tacaids) imesema tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa vitendo vya ngono kinyume na maumbile vinazidi kuongezeka.

Hayo yalisemwa jana na Dk. William Kafura, katika mkutano wa sita wa Chama cha Wabunge cha Kupambana na Ukimwi (Tapac).



Alisema hiyo inatokana na imani za kishirikina kwamba wakifanya vitendo hivyo watapata bahati kwa kupandishwa vyeo.

“Lazima tukubali tatizo lipo na tulitafutie suluhisho, utafiti upo umefanywa na Muhimbili, umefanywa na chuo kikuu cha Dar es Salaam, umefanywa na Tasisi ya Utafiti ya Ifakara,”alisema.

Alisema pia wafanyabiashara wanaamini kwa kufanya vitendo hivyo watajirika wakati wanawake wanaamini kuwa watazidi kupendwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TACAIDS, Dk. Fatuma Mrisho, alisema utafiti uliofanyika nchini unabainisha kuwa wanawake hawana uelewa wa kutosha juu ya kujikinga na maambukizi ya ukimwi.

Akizungumzia suala la kujikinga na ugonjwa wa Ukimwi Dk. Mrisho alisema kuwa wanaume wana uelewa mkubwa zaidi kuhusu ugonjwa huo kuliko wanawake.Hata hivyo, alisema kwa sasa ipo kazi kubwa ya kutoa elimu kwa wananchi na hivyo kuwataka wabunge na viongozi mbalimbali kutoa elimu juu ya kujikinga na gonjwa hatari la ukimwi.

Aidha Mrisho alisema kuwa kwa sasa Mkoa wa Njombe unaongoza kwa maambukizi ya Virusi vya ukimwi kwa asilimia 14.8 ambapo Unguja Kaskazini inamaambukizi madogo kwa asilimia 0.1.

Hata hivyo alisema kuwa kuna changamoto mbalimbali ambazo wanakumbana nazo ni pamoja na rasilimali za ukimwi kwa serikali, mashirika ya Dini na sekta binafsi kuwa pungufu kuliko mahitaji.

Alisema pamoja na kuwepo kwa changamoto lakini nia ni kufikia sifuri tatu ifikapo mwaka 2015. 
 NIPASHE


Maajabu  ya  uumbaji  yamemfanya  mama  mzazi  wa  Xiao Wei  ambaye  ni  mchina amwage  machozi  akiomba  msaada  wa  kunusuru  maisha  ya  mwanae   mwenye  umri  wa  miezi  7 aliyezaliwa  na  matako matatu...

Kalio  la  tatu  lipo  kama  mkia  mfupi, wenye  urefu  wa   sentimita  8  ( 8 cm ), katikati  ya  makalio  mengine  mawili.
Akiongea   kwa  uchungu, mama  mzazi  wa  mtoto  huyo  amedai  kuwa  kwa  muda  mrefu  amekuwa  akiwaomba  madaktari  wafanye  upasuaji  wa  tako  hilo  lakini  wao  wamekuwa  wakimjibu   kuwa  hiyo  si  kazi  nyepesi  kama  anavyodhani....
"Tukilikata  litaota  tena, hivyo  hatutakiwi  kukurupuka  na  badala  yake  tutakiwa  kupata  muda  wa  kupitia  vitu  vingi  ukiwemo  mrija  wa  uti  wa  mgongo  ambapo  kalio  hilo  limejiegesha"...Alisema  daktari  mmoja  akimjibu  mama  huyo
Suala la baadhi ya Watanzania kuhifadhi mabilioni ya fedha nchini Uswisi limechukua sura mpya, baada ya tume maalumu kuwahoji vigogo 200 wakiwamo wabunge, wanasiasa na wafanyabiashara.
Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa tume hiyo inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema tayari imeshafanya kazi hiyo kwa miezi miwili sasa.
Tume hiyo maalumu iliyoundwa na Serikali kwa Azimio la Bunge lililotolewa mwishoni mwa mwaka jana, inatarajiwa kukamilisha uchunguzi huo wakati wowote kuanzia sasa na kuwasilisha ripoti hiyo katika kikao kijacho cha Bunge. Jaji Werema alipoulizwa na Mwananchi Jumpili maendeleo ya uchunguzi huo, alisema kuwa kazi hiyo bado inaendelea.
“Uchunguzi huo unaendelea,” alisema Werema huku akisita kueleza kwa undani juu ya kazi hiyo kwa kile alichosema kuwa hana sababu ya kufanya hivyo kwa sasa.
“Subiri uchunguzi bado unafanywa,” alisema Werema na alipotakiwa kueleza utamalizika lini alisema: “Utamalizika tu.”
Mwanasheria huyo wa Serikali alikataa kutaja baadhi ya majina ya watu ambao tume yake imewahoji mpaka sasa.
Alisema anashangazwa na swali la namna hiyo, kwa maelezo kwamba ni jambo ambalo liko wazi kuwa ni kinyume na maadili kuwataja watuhumiwa wakati huu uchunguzi ukiwa bado unaendelea.
Uchunguzi huo unafanyika baada ya Benki ya Taifa ya Uswiss (SNB) kutoa taarifa mwezi Juni, 2012 kuhusu raia wa kigeni wanaomiliki akaunti za benki nchini humo.
Orodha hiyo iliorodhesha pia baadhi ya Watanzania wenye akaunti zinazofikia Dola196 milioni ambazo ni sawa na Sh323.4 bilioni.
Jarida la kimataifa la uchunguzi la The Indian Ocean Newsletter toleo la hivi karibuni, lilimnukuu Werema akisema uchunguzi huo kwa sasa unatia matumaini.
Werema anaripotiwa akikiri kuwa uchunguzi huo umefikia ‘hatua ya kutia matumaini’ na wanaendelea na kazi hiyo kwa uangalifu ili kuwa na uhakika wa taarifa wanazozitafuta.
Alisema kwamba taarifa ya awali inatarajiwa kutolewa hivi karibuni na tayari idadi kubwa ya wahusika wakiwamo wabunge wameshahojiwa.
Werema alisema wanaendelea na uchunguzi kuwabaini zaidi ya Watanzania 200, waliotajwa kuficha mabilioni ya fedha nje ya nchi.
Mbali na Werema, tume hiyo inaundwa na viongozi kadhaa wa taasisi nyeti kama vile Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hosea, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Rashid Othman na Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Benno Ndulu.
Tume hiyo inawahusisha pia Mkuu wa Sheria wa BoT, Mustapha Ismail na maofisa kutoka idara ya upelelezi na ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali.
Kwa mujibu wa jarida hilo la kimataifa, miongoni mwa watuhumiwa hao ni wanasiasa na majenerali wastaafu wanaotuhumiwa kutorosha zaidi ya Dola 133 milioni mwaka 2005, kupitia Mfuko wa Ulipaji Madeni ya Nje (EPA)
Baadhi ya watu wanaodaiwa kuhusika wamehojiwa kutokana na taaluma zao, familia zao, akaunti zao za benki zilizoko nchini na nje ya nchi pamoja na nchi walizotembelea mara kwa mara kwa miaka mitatu iliyopita.
Lengo la kuwahoji inaelezwa ni kutaka kujua iwapo walifuata njia zinazotakiwa katika kufungua akaunti hizo nje ya nchi na iwapo fedha zilizohifadhiwa huko zilipatikana kihalali.
Sakata la kashfa hiyo liliibuliwa Bungeni kwa hoja binafsi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe mwishoni mwa mwaka 2012.
Zitto alisema kwamba kiasi cha fedha kilichofichwa nchini Uswisi ni kikubwa zaidi ya hicho kilichotajwa.
Bunge liliipa Serikali kipindi cha mwaka mmoja ambacho kinaishia Oktoba mwaka huu, iwe imekamilisha uchunguzi na kuwasilisha ripoti hiyo bungeni.

Source mwananchi jumapili.