Watu wasiojulikana wameushambulia ubalozi wa Korea Kusini kwenye mji mkuu wa Libya Tripoli ambapo walinzi wawili wa ubalozi huo waliuawa.
Wizara ya mashauri ya kigeni nchini Korea Kusini imesema kua watu hao walifyatua risasi wakilenga ubalozi huo wakiwa ndani ya gari.
Hakuna raia yeyote wa Korea Kusini aliyeripotiwa kujeruhiwa wakati wa shambulizi hilo.
CHANZO.BBCSWAHILI.