Brian Deacon ndio jina lake mwigizaji huyo ambaye ni mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia yao baba yake akiwa fundi makenika na mama yake akiwa ni nesi.
Ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika ambapo alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara Deacon,ndoa yake ya pili alioana na mwanamama Natalie Bloch mnamo mwaka 1998 mpaka sasa wapo kwenye ndoa hiyo.
Brian Deacon ndani ya filamu ya ''JESUS'' Aliigiza filamu ya Yesu ambayo pia ilimfanya aokoke mara baada ya kuitazama akiwa na miaka 30,baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260 wakijaribishwa kuigiza(screen test)kuona kwamba wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za majukwaani na uigizaji.
Brian Deacon miaka iliyofuatia baada ya kuigiza kama Yesu.
Amesema kabla ya kuchaguliwa mtihani wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala wake aliyemvunja moyo kwakumweleza hadhani kama yeye(Brian)atafaa kwenye kumwigiza Yesu,lakini anasema alifanikiwa,baada ya hapo akawa na wakati mgumu kutoka kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu kumweleza jinsi anavyotakiwa kuigiza,sauti yake na mambo mengine,ingawa yeye alisema nitatumia sauti yangu na maelezo kutoka kwa muongozaji.
Amesema wiki tatu kabla hawajaanza kurekodi filamu hiyo alisoma kitabu cha Luka mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa kutoka kitabu hicho ambapo Brian amesema kusoma kwake kulimpa nguvu sana na moyo wa kuigiza filamu hiyo na kuweza kumfahamu vyema Yesu kuwa ni mtu wa aina gani.
watu wakiangalia filamu ya Yesu ambayo bwana Brian Deacon ni mwigizaji mkuu.
Katika miezi saba waliyochukua kuigiza filamu hiyo Brian amesema,walikuwa wanaigiza kwa masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri mpaka mwisho wa siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake kwamba wamsaidie kwani amechoka sana hajui kwamba angeweza kuigiza kwa siku hiyo lakini anasema alikuwa anashangazwa na nguvu za ajabu alizokuwa akizipata na kuendelea kuigiza ingawa wakati huo nasema alikuwa mkristo jina wa kanisa katoliki,alikuwa anauwalakini kuhusu mafundisho na huduma ya Yesu kwa ujumla,siku moja wakati anaigiza alikuwa anawaombea watu mara mwanamke mmoja alishika mkono wake kumbe alikuwa na mapepo alimuombea na mapepo yalimtoka mwanamama huyo.
Siku nyingine waliokuwa wakiigiza kama wanafunzi wa Yesu wapatao 12 wakiwa ndani ya basi walikuwa wamepanga kugoma kutokana na malipo waliyokuwa wakipata cha ajabu Brian anasema director alikuja kumuomba yeye(Brian)azungumze nao warejee kazini akashangaa akamwambia mimi sio Yesu ni Brian Deacon,akaamua kuzungumza nao,baada ya masaa 36 walikubali kurudi kuendelea na kazi
Amesema mtihani mwingine ni siku alipokuwa hotelini Tel Aviv ghorofa ya 18 usiku mara kukawa na moto hotelini hapo baada ya mwingereza mmoja aliyekuwa akivuta sigara kusahau kuizima hivyo kusababisha moto,lakini anasema bahati nzuri hakuna aliyejeruhiwa ila walifanya kazi siku inayofuatia muda mrefu bila muongozaji kujali kwamba hawakulala vyema usiku.
|
watumishi wa Mungu wakiwa njiani kwenda kuonyesha filamu ya Yesu katika uinjilisti huko Kongo. |
Amesema siku hiyo mmoja wa waigizaji anayeitwa Tom Panella alianzisha mada kwa kusema moto uliokuwa umetokea ni hila za shetani,na kusababisha mjadala wa muda mrefu ni vipi shetani anahusishwa kwenye swala hilo lakini jibu likawa,shetani hataki filamu hiyo irekodiwe ndio maana analeta hila zake.haikuwa kazi rahisi kurekodi filamu hiyo na pia si ujuzi wa kufurahia,baada ya kumaliza kurekodi kwa takribani miezi 18 ilianza kuonyeshwa kwa baadhi ya watu na ndipo hata yeye kwa mara ya kwanza akaona ni kwa jinsi filamu hiyo ilivyonanguvu,ukweli na kugusa mioyo ya watu.
Baada ya filamu hiyo Briana anasema alirudi kuigiza majukwaani na kwenye runinga, ambapo kwa miaka zaidi ya 30 sasa tangu kutoka filamu ya Yesu tayari imetazamwa na watu zaidi ya bilioni tatu katika nchi 233(kwa takwimu za mwaka 2001),zaidi ya watu milioni 117 waliamua kubadilisha maisha yao na kumpokea Yesu,filamu hiyo ambayo ilitengenezwa chini ya Campus Crusade for crusade ambao kwasasa wanaitwa Life Ministry pia nchini Tanzania wapo chini ya mkurugenzi Dismas Shekhalage.ambapo tayari imetafsiriwa katika lugha zaidi 500 huku nyingine zaidi ya 200 zikiwa njiani kutafsiriwa.
Brian anawaambia watu kwamba yeye ni mwigizaji tu na sio Yesu kama watu wengine na kuwataka watu hao kujua hivyo ambapo anasema ameendelea kupata barua mbalimbali za kumpongeza na kumshukuru kwa kazi nzuri aliyofanya kwenye filamu hiyo,ambapo kwa upande wake anasema anayo nakala ya filamu hiyo kwenye maktaba yake nyumbani kwao Uingereza,ambapo kwa takribani miaka 20 filamu hiyo imekuwa ikitazamwa duniani kote na kubadilisha maisha ya watu.
kati ya filamu alizowahi kushiriki ni pamoja na A zed & Two Noughts ya mwaka 1985,The Feathered Serpent ya mwaka 1976-1978 na Tamthilia ya iitwayo Lillie iliyoigizwa mwaka 1978 akitumia jina la Frank Miles.
SOURSE: PAPARAZI BLOG
|
Nimevumilia aibu hii lakini nimeshindwa na hivyo nimeamua niwe muwazi ili niweze kusaidiwa.Sihitaji msaada wa kifedha, bali nahitaji ushauri tu.
Ndugu zangu mwenzenu juzi jumamosi nilipatwa na dhahama iliyo pelekea nione aibu kwenda kazini kuendelea na majukumu yangu baada ya kubakwa na mama mke wa mtu.
Ilikua jioni bosi aliponipigia simu nakuhitaji msaada wangu wa kumpeleka katika sehemu moja ya starehe .
MIMI ni dereva ninaye mwendesha. Nimefanya kazi kwa muda wa miezi sita sasa lakini hakuwahi kunionyesha dalili yoyote ya kimapenzi kwa kuwa anafahamu mimi ni mume wa mtu na yeye ni mke wa mtu.
Mume wake siyo mtu wa kushinda sana nyumbani.Ni mfanyabiashara na mara nyingi huwa nje ya nchi kibiashara. Nyumba yao ina geti kubwa na mlinzi mmoja.
Baada ya kumpeleka huko mapumzikoni, saa tano usiku alinipigia simu nikamchukue ili nimrudishe nyumbani. Nilimkuta akiwa amelewa sana, hivyo nikamkokota mpaka ndani ya gari tukaondoka.
Nyumbani tulikuta mwanae mdogo na house girl wamelala hivyo akaniomba nimpeleke chumbani kwake kwa madai kwamba alikuwa hawezi kutembea kwa sababu alizidisha pombe.
Nilimvuta mpaka chumbani kwake maana sikuwa na jinsi ya kukataa.Cha ajabu nilipomfikisha chumbani yule mama alipata nguvu akafunga mlango.
Alisimama pale mlangoni na kuanza kuvua nguo zake.Nilipojaribu kumvuta ili nitoke, yule mama alitishia kupiga kelele.Akanambia nitulie tulale, vinginevyo atapiga kelele kwamba nataka kumbaka.
Nikifikiria getini kuna mlinzi na nipo ndani ya chumba cha bosi wangu kiasi kwamba mlinzi akija ni lazima aamini kwamba nilikuwa nataka kumbaka..
Akili ya haraka haraka ilinituma nimkubalie tu, lakini nikakumbuka pia sina hata kipande cha kondom.
Jmani naomba niishe hapo maana nashindwa kuendelea kuelezea.Kwa kifupi ni kwamba nilifanya mapenzi na yule mama bila kinga yoyote.
Mlinzi alijua kila kitu tulichokifanya maana niliondoka asubuhi.Siwezi kuendelea na kazi tena maana mumewe akirudi ni lazima aambiwe kila kitu.. Kinachoniuma ni kwamba kazi nimeipoteza na huenda afya yangu nayo ikawa imeingia dosari.Tangu juzi sijafanya mapenzi na mke wangu.Nasubiri miezi mitatu ipite ili nikapime.
Lakini namwelezaje mke wangu kwa kipindi chote hicho ili anielewe.Na mimi kama mumewe naanzaje kumweleza kwamba nimebakwa? Ndoa yangu itakuwaje?
Naomba msaada wa ushauri toka kwenu na kwa wasomaji wenu.
Ni mimi Jose.
|
|
Mark X usafiri mpya kabisa wa msanii wa Bongo Fleva Ommy Dimpozi ukiwa hauna hata namba za usajili Jana umekatika maeneo ya Jaffarai Car Wash maeneo ya Mikocheni na kupigwa sopu sopu.
Chezea muziki wewe!!
|
Kampuni ya GS1 TANZANIA jana imeweza kumkabidhi PROF JAY msanii wa Hip Hop nchini na mkongwe katika mziki huu wa nyumbani BARCODE ili kuweza kutanua zaidi soko lake la biashara.
Prof Jay mbali na uwimbaji pia anamiliki studio yake mpya inayoitwa MWANALIZOMBE pamoja na saloon ya kiume ya kunyoa.
|
|
|
Japhet Lugobe Byeyanda mkazi wa Kahama Shinyanga leo amefika kwenye ofisi za Clouds Media na baiskeli yake baada ya kutumia siku 15 kusafiri na baskeli kutoka kanda ya ziwa.
Safari yake ilianzia huko anapoishi Shinyanga na kuelekea Mwanza,Bukoba,Tabora,Dodoma,Singida,Iringa,Morogoro,Pwani na Dar es salaam akiwa na baiskeli yake.
Bwana Japhet Lugobe ameongea na millardayo.com na kusema lengo lake la kusafiri na baiskeli kwenye mikoa kumi japo kuwa anasema alikuwa akipata hifadhi kwa watu tofauti njiani. “Lengo kubwa ni kufika Iringa kwenye maadhimisho ya Mwalimu Nyerere na siku ya kuuzima mwenge, ningeweza kwenda moja kwa moja hadi Iringa lakini nilikuwa napita na bendera yangu nimeifunga ikipepea kwenye mikoa yote kwa lengo la kuenzi amani aliyotuachia baba wa taifa.”
Source:Millardayo.com
|
|
|
WANASUBIRI NIFE BY AZMA.
''najua mnajua kuwa najua,ila hamuwezi nichukua kwenye tour,
mnawachukua wasiojua, mitego wanayotega naitegua,
siwezi nikajihusisha na makosa ya jinai ili napate riziki,
kipaji changu ni hiki,
bariki,kazi ya mikono yangu,
wabariki mariki na maadui zangu''
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI.
|
Rapper kike raia wa Australia Iggy Azelea ameamua kuwa expensive zaidi ya pesa na kuzitosa $1.5 Million, alizolipwa na tajiri wa kirusi ili watoke nae dinner.
Rapper huyo wa kike hivi karibuni amekuwa akielezea kuwa ana matatizo binafsi na alikuwa anatafuta mtu wa ku-date nae na kuamua kuanzisha shindano kwenye mtandao ili kumpata fan wake atakae kuwa na bahati ya kufanya mtoko na mrembo huyo.
Lakini pamoja na kuwepo shindano hilo, tweet ya tajiri mmoja wa Russia aliyeahidi mkwanja huo haikukidhi viwango ama haikuweza kumshawishi Iggy Azalea.
Bado haifahamiki sababu za yeye kumkatalia tajiri huyo ni kutokana na kubanwa na ratiba binafsi ama ameamua tu kuwa expensive zaidi ya mkwanja huo.
Iggy Azalea aliyetisha na mixtape yake ya kwanza ‘Ignorant Art’ ni moja kati ya wasanii watakaomsindikiza mama Blue Ivy, Beyonce kwenye tour yake ya ‘ The Mrs. Carter’.
|
MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zilizokutana jana baina ya watani wa jadi Simba na Yanga iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya mabao 3-3 imeingiza jumla ya Sh. Milioni 500.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Tanzania mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya mabao 3-3,Mashabiki 57,422 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo namba 63 kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000,sh.20,000 na sh. 30,000. Ni tiketi 131 tu ndizo hazikuuzwa ambazo ni 90 za VIP A, 40 za VIP B na moja ya VIP C. Tiketi zilizochapwa kwa ajili ya mechi hiyo ni 57,558 ambayo ndiyo idadi ya viti vilivyopo kwenye uwanja huo.
Kila klabu imepata mgawo wa sh. 123,025,564.32 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 76,382,084.75. Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 62,555,371.69, tiketi sh. 7,309,104, gharama za mechi sh. 37,533,223.01, Kamati ya Ligi sh. 37,533,223.01, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,766,611.51 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 14,596,253.39.
|
|
HATUA ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kutaja hadharani mshahara wa Rais na Waziri Mkuu, imechukua sura mpya baada ya Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) kulaani hatua hiyo na kuomba Spika Anne Makinda kuchukua hatua kwa vile ni ukiukaji wa sheria.
Chama hicho kimeeleza kusikitishwa na kitendo hicho kufanywa na Mbunge aliyehusika na upitishaji wa sheria hiyo huku wabunge wenyewe wakiwa wakali pale wananchi na wadau mbalimbali wanapohoji mapato yao.
Katibu Mkuu wa Tughe Taifa, Ally Kiwenge alisema Dar es Salaam jana kwamba pamoja na hatua hiyo kukiuka sheria ya kazi na uhusiano kazini inayosema mshahara ni siri ya mwajiri na mwajiriwa, pia kitendo hicho si ajenda ya wafanyakazi hivi sasa. Alisema ajenda ya wafanyakazi kwa sasa ni kuona wabunge wanapigana kufa kupona katika kuhakikisha kuwa mshahara wa mfanyakazi unaongezeka kukidhi mahitaji ya mwezi mzima na kuwaondolea mzigo wa mikopo inayowaandama. “Huu si wakati wa wafanyakazi kutaka kujua mishahara ya Rais au Waziri Mkuu, ajenda yetu kwa sasa ni kuona wabunge wanapigana ili kuboresha mishahara ya wafanyakazi ili ukidhi mahitaji muhimu tofauti na sasa,” alisema Kiwenge.
Alisema pamoja na hilo ni mkakati wa wafanyakazi sasa kuona wabunge wanatumia muda wao uliosalia kabla ya Bunge kuvunjwa kuhakikisha mambo makubwa mawili yanaingizwa katika Katiba mpya, moja ikiwa ni nafasi ya mfanyakazi kikatiba ikoje na pia kuona Katiba mpya inasema nini juu ya hatima ya maslahi ya wafanyakazi. “Tunataka Katiba mpya itamke wazi juu ya mishahara ya wafanyakazi ili iwe ni ile inayokidhi haja,” alisema.
Aeleza kuwa ni jambo la kusikitisha kuona wabunge wanaanza kutaja mishahara ya viongozi wa taifa hadharani kwa kudhani kuwa ndio njia sahihi ya kuwasaidia Watanzania bila kujua kuwa hatua hiyo itasababisha mgawanyiko wa matabaka na kuligawa Taifa, jambo ambalo ni la hatari.
“Sisi mishahara ya viongozi wote tunaifahamu na hata ya wabunge, lakini sheria inasemaje juu ya kutangaza mshahara wa mtu hadharani? Wafanyakazi wanaweza kuitaja lakini kwa vile wameandaliwa hawafanyi hivyo, wanazingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi. “Naamini kama wafanyakazi wangekuwa ni watu wa kukusanyana na wangekuwa hawana maadili wangeweza kusema mengi ambayo yangeshangaza jamii lakini hawafanyi mambo kwa kukurupuka au kuutafuta umaarufu usio na msingi,” alisema. Katibu Mkuu huyo wa Tughe alisema kwa kufuata mfano wa wafanyakazi, viongozi wakiwemo wabunge watoe kauli za kujenga nchi na si zenye kuashiria matabaka na ubaguzi, jambo linaloweza kusababisha migogoro mikubwa na kuliingiza taifa katika machafuko yasiyo na tija,” alisema.
Alisema wabunge wafahamu pia kwamba suala la mishahara litaendelea kubakia kuwa ni la mwajiri na mwajiriwa na ndio maana katika fomu au nyaraka nyingine zinazoelezea majukumu ya wabunge suala la mishahara na marupurupu yao haliwekwi wazi kwa vile ni siri kati yao na taasisi ya Bunge kisheria.
|
Baba mzazi wa Madee Ally Selengia ambae ana zaidi ya 50 sasa hivi lakini bado anaonekana kijana na hata mambo yake mengine ni ya ujana ujana, anayo mpaka a.k.a ya ‘Mwakitoki hoi’ ambayo Madee amekua akisikika akimrusha kwenye nyimbo zake.
Ni mzazi ambae kazi yake kwa zaidi ya miaka 20 ni kuendesha Taxi jijini Dar es salaam kama unavyomuona kwenye picha akiwa na Taxi anayoimiliki, ni biashara ambayo ndio imemuwezesha kuwasomesha kina Madee na kuilea familia kwa miaka yote.
Anasema kwa miaka kadhaa hata mpaka sasa hivi, nyumbani kwake analea baadhi ya Wasanii ambao ni marafiki zake Madee, kwa sababu wanafanya muziki na Madee imebidi akubali hali halisi ya maisha ya mwanae ambapo toka miaka hiyo amewalea watu kama kina MB Dogg yani kama watoto wake, chakula kinapikwa pamoja wanakula na kulala kama familia.
Baba Madee anasema yeye ndio alikua mtu wa kwanza kumkataza Madee kufanya muziki miaka hiyo kwa sababu hakuona faida yake ila kwa sasa ameiona na mpaka amemruhusu mdogo wake Madee wa mwisho kufanya muziki pia mwingine kuwa producer wa video.
Ni shabiki mkubwa wa Madee na anasikiliza sana nyimbo zake na hata kutokea kwenye video, faida mojawapo aliyoiona kutokana na muziki wa Madee, ni nyumba aliyowajengea kama Wazazi na nyumba nyingine Madee aliyoijenga kwa ajili ya kuishi yeye.
Moja kati ya Matukio asiyoyasahau Baba Madee ni pale ugomvi wa Madee na Ney wa Mitego ulivyopamba moto zaidi ya miaka kumi iliyopita, kuna kipindi Ney wa Mitego alikwenda nyumbani kwa kina Madee na kuweka kambi karibu na nyumba yao na kuanza kuimba nyimbo za kumtukana Madee.
Tukio jingine analolikumbuka kuhusu Madee ni siku ambayo kundi la Ney wa Mitego lilikwenda nyumbani kwao huku likimkimbiza Madee spidi kwamba ni mwizi, Madee alipokimbilia nyumbani ndani ilibidi mama yake atoke kusawazisha na ndio ikawa siku ya mama yake kubaki na alama ya kudumu usoni baada ya mmoja kati ya waliokuwemo kwenye kundi la Ney wa Mitego kurusha chupa iliyompiga usoni.
Uhusiano kati ya Madee na Ney wa Mitego uko vizuri sasa hivi na wamekua marafiki na hata wakati mwingine Ney akitaka kutoa single ni lazima ammtumie Ney ili asikilize kwanza mfano ni wimbo wa ‘Salamu zao’ ambao unapata airtime kubwa kwenye radio sasa hivi.
source:milardayo.
|
Kanye West kicked off his 'Yeezus' tour in Seattle, on Saturday October 19th and before his performance of his College Dropout hit song, Jesus Walks, a man dressed as Jesus walked on stage and Kanye jokingly asked "White Jesus, is that you?… Oh, shit!,". Later, Kanye and his female back-up dancers bowed to the Jesus look-alike as he stood on the mountain top. - See more at: http://www.africanewspost.com/2013/10/kanye-west-brings-jesus-lookalike-on.html#sthash.gcaOAcyy.dpuf
Kanye West kicked off his 'Yeezus' tour in Seattle, on Saturday October 19th and before his performance of his College Dropout hit song, Jesus Walks, a man dressed as Jesus walked on stage and Kanye jokingly asked "White Jesus, is that you?… Oh, shit!,". Later, Kanye and his female back-up dancers bowed to the Jesus look-alike as he stood on the mountain top. - See more at: http://www.africanewspost.com/2013/10/kanye-west-brings-jesus-lookalike-on.html#sthash.gcaOAcyy.dpuf
Kanye West kicked off his 'Yeezus' tour in Seattle, on Saturday October 19th and before his performance of his College Dropout hit song, Jesus Walks, a man dressed as Jesus walked on stage and Kanye jokingly asked "White Jesus, is that you?… Oh, shit!,". Later, Kanye and his female back-up dancers bowed to the Jesus look-alike as he stood on the mountain top. - See more at: http://www.africanewspost.com/2013/10/kanye-west-brings-jesus-lookalike-on.html#sthash.gcaOAcyy.dpuf
Kanye West alianza show yake vizuri kabisa ila ilipofika wakati wa kuimba wimbo wake kutika kwenye album ya College Dropout inayoitwa Jesus Walks alitokea mtu aliye vaa kama Yesu na Kanye West ambaye alikuwa na msaidizi wake wa kike kwenye kuimba wali inama na mbele ya Mtu Huyu na ndio wimbo ukaanza wa Jesus Walks.
TAZAMA VIDEO
|
Posted: 21 Oct 2013 01:58 AM PDT
Miongoni mwa mambo ambayo yamekuwa yakinipa woga na hofu ni kuoa mwanamke anayetumia sana mitandao ya kijamii zaidi ya moja mfano Twitter, Facebook, INSTAGRAM nk ,
Siku hizi wimbi kubwa limeibuka la wadada kutumia mitandao hii unaweza kwenda na mdada Date lakini asilimia 80 atakuwa anabofya bofya simu yake badili ya kuongea na wewe ...huwa naondoa 60% kuwa sitowezana naye maana ni bora mwanaume akawa anafahamu mambo mengi kuliko mwanamke atakudharua san maana kila mtakachozungumza lazima apeleke mtandaoni huku upo naye hapohapo na hivyo kuona huna jipya kwake, hii imenifanya mahusiano na m/ke kitu muhimu kuuliza ni kuwa anatumia mitandao gani ya kijamii ili namna ya kukabiliana naye au wadau mnasemaje watu hawa wanafaa kuwa wife material kweli!
|
|
|
Hichi ndicho alichoandika huyu star wa Bongo Fleva anayejulikana kwa Jina la Witnesz TZ katika ukurasa wake wa facebook juu ya Wanawake Wenzake. ''hivi ni asilimia ngapi ya wanawake wanatongoza wanaume humu fb? kiupande wangu ninapata mchefuko mkubwa wa moyo haswa pale wanapotolewa nje na bado wakazidi kung,ang,nia jamani ,hili ni jambo la aibu mno,
mwanamke akitongozwa ndo mahala pake mwanaume siku zote ni muwindaji kwa upande huu japo nasi huwa tunawakubali tuwapendao na wenye sera za msingi,sasa huu mfumo unatia aibu jamani utadhani hawajalelewa na wazazi wenye kujiheshimu mnatudhalilisha sana wenzenu wakati mwingine unapatwa na aibu hadi unatamani ufiche uke maana jinsi mtu anavyotolewa nishai na anapozidi kung,ang,ania unahisi amekuwakilisha na wewe! jamani acheni tabia mbaya wanawake wenzangu,ni hayo 2!''
|
Beyonce alivyokuwa kwenye ziara yake kwenye kisiwa cha New Zealand alipata nafasi ya kwenda kwenye moja ya majengo marefu kisiwani humo yanayo toa huduma ya kupoteza Uwoga wa Anga.
Beyonce alifungwa kamba sehemu muhimu kwenye mwili wake zitakazo weza kumshika wakata anashuka kwa kamba kwenye jengo hilo. Beyonce alivyokamilisha safari hii anasema kwa sasa hana hofu ya anga tena
|
Msanii wa Rnb Ciara anaye husishwa kimapenzi na msanii mwenzake Future ameonekana na muonekano tofauti hivi karibuni baada ya kubadilisha style yake ya mavazi na muonekano wake mbele za watu na kwenye show.
Hivi karibuni Ciara alikuwa Airport na alionekana akiwa na mbwa wake na kumbeba kama anaficha tumbo au kitu kwenye eneo la tumbo na pia kwenye show yake ya Paper Magazine alioneka kuvaa kivazi kilicho ficha tumbo lake kitu ambacho sio kawaida kwa msanii kama Ciara ambaye amekuwa akijivunia Umbo lake.
|
Standard Media wametoa taarifa nyingine ambayo inazidi kulipa shambulio la Westgate nguvu ya kuendelea kumiliki vichwa vya habari baada ya kuripoti kwamba Magaidi waliofanya hilo shambulio Nairobi mwezi September walitumia helikopta ambayo inamilikiwa na mwanasiasa maarufu wa zamani nchini Kenya ambae taarifa hii haijamtaja.
Imefahamika, sita kati ya magaidi walitumia helikopta hiyo kutoka kwenye kambi ya wakimbizi ya Dadaab mpaka Nairobi kwa kuhofia kushtukiwa mapema na kukamatwa iwapo wangetumia usafiri wa ardhini.
Wapelelezi wamesema wanaamini kwenye helikopta hiyo, magaidi hawa walibeba baadhi ya silaha za kivita ambazo zilitumika kwenye shambulio hili ambalo liligharimu maisha ya zaidi ya watu 60 akiwemo ndugu wa Rais Uhuru Kenyatta.
Magaidi hawa wanaaminika kuingia kwenye kambi ya Dadaab wakitokea Somalia miezi sita iliyopita ambapo walijifanya Wakimbizi huku wakiendelea kupanga shambulio la September 21 ambapo baadae walichukua hiyo helikopta ambayo tayari Pilot wake alikamatwa na kuhojiwa na kisha baadae kuachiwa.
Hata hivyo imegundulika pia ndani ya jumba la Westgate ambalo ndani yake lina maduka na migahawa mbalimbali, kwenye floor ya kwanza kulikua na raia wa Uturuki ambae alikodi chumba cha duka zaidi ya mwaka mmoja uliopita na kuanza kukitumia kwa biashara ya kuuza simu miezi sita iliyopita na pia chumba hichohicho kutumika na magaidi kama sehemu ya kuhifadhia silaha. Raia huyu wa Uturuki alisafiri kwenda nje ya Kenya siku moja kabla ya shambulio la Westgate na Polisi wanaendelea na msako ambao pia unalihusisha gari aina ya BMW ambalo lilimilikiwa na yeye na kutumika kubeba Magaidi hawa kwenye mizunguko mbalimbali ya Nairobi
Kuna UTAPELI mpya umeingia nchini Tanzania. Watu ambao wanajifanya wana makampuni na wanatafuta watu wa kazi namaanisha wanatangaza nafasi za kazi, nafasi hizo hutangazwa kupitia mitandao ya Internet ambayo huwa ina maeneo ya kutangaza nafasi za ajira, nitashindwa kuitaja mitandao hiyo kwa kuwa sio utaratibu ila wewe ambaye unajua kuwa kuna mitandao ambayo inatangaza ajira kupitia njia ya Internet ujue ndio hiyo ambayo tunaiongelea hapa.
Matukio yenyewe yanakuwaje? Watu hao hutangaza nafasi za kazi mbali mbali kupitia mitandao hiyo kwa kuandika wana makampuni na wanatafuta watu kwa nafasi mbambali kwenye makampuni yao feki, kwa kutambua watanzania wengi wana shida ya ajira hutangaza nafasi ambazo wanaamini wengi wataziomba na kuweka vigezo vya chini sana hasa eneo la Elimu na uzoefu kwa kuamini wengi wataomba, baada ya hapo, wewe mwenye shida ya ajira ukishatuma CV yako ambayo itakuwa pia inaonyesha mawasiliano yako, wao hutumia mwanya huo kukutumia ujumbe mfupi (SMS) na kujifanya wao ni wafanyakazi wa kampuni husika ambayo imetangaza nafasi hiyo na kujidai wanaweza kukusaidia kuipata kazi hiyo na kukutaka uwatumie hela ili wakufanyie mpango na kukutumia maswali ambayo utaulizwa kwenye INTERVIEW na majibu yake, hawa jamaa kwa kutambua shida ya Watanzania hawasemi wanataka kiasi kikubwa huwa wanataka kiasi cha Elfu kumi hadi Hamsini, wanafanya hivyo kwa kutambua wewe mtafuta ajira unaweza ukakipata kiasi hicho.
Matapeli hao hudiriki kukwambia na kiasi cha mshahara ambao utalipwa kwenye kazi hiyo ili kukutamanisha utume hiyo hela, simu hiyo ambayo imekutumia ujumbe huo ukiipigia huwa haipatikani na ikipatikana haipokelewi na wanakua wameziregister kwa majina ambayo wanakuaminisha ni yao kumbe ni majina ya uongo ya kutapelia watu.
Mpaka sasa wameshawaliza watu wengi sana kwa hiyo wewe mdau kuwa makini sana wakati unaomba ajira kupitia mitandao mbalimbali ya Internet, ukiona unaombwa hela baada ya kuomba ajira kupitia mitandao hiyo ujue ndio hao matapeli.
KUWA MAKINI EWE MTANZANIA
Source:Mubelwa Bandio.
|
|
Posted: 20 Oct 2013 03:25 PM PDT
Uchunguzi uliofanywa katika mikoa mbalimbali nchini umegundua kuwa mbali ya kusambaratisha ndoa nyingi, simu pia zimekuwa adui mkubwa kwa baadhi ya watumiaji badala ya kuwanufaisha kama inavyotakiwa.
Uzuri na ubaya wa simu
Wananchi walieleza uzuri na ubaya wa simu ambapo Peter Tesha mkazi wa Arusha aliitaja simu kuwa ndiyo chanzo cha kumfikisha alipo sasa akikosa fedha za matumizi yake ya kawaida licha ya awali kumiliki miradi mingi iliyokuwa ikimwingizia kipato.
Anaeleza kuwa baada ya kuoa mwaka 2009, alibahatika kupata watoto wawili na mkewe na maisha yao yakaendelea vizuri huku yeye akiendelea na biashara yake ya maduka matatu aliyokuwa akilimiki jijini Arusha na mawili ya Moshi.
Anasema kuwa katika maisha yake na mkewe hakuwahi kushika simu ya mkewe huyo mbali mkewe kuwa hodari wa kuchunguza simu yake.
Hata hivyo siku moja bila kupanga alichukua simu ya mkewe na kusoma ujumbe mfupi aliotumiwa, jambo analoapa kutolifanya tena maishani mwake kwani alikutana na ujumbe aliouelezea kuwa ulikuwa wa majibizano kati ya mkewe na mwanamume mwingine ambaye hata hivyo jina lililotumika lilikuwa la kijiji badala ya mtu.
“Siwezi kusahau, hata huu umaskini unaoniandama ni madhara ya simu. Ujumbe ule ulikuwa wa kulaumiana kati ya mke wangu na huyo mwanamume kuwa hawa watoto wangu ni wake, mke wangu akiuliza; Kwa nini umewatelekeza na kuniachia mzigo wa kulea mimi ambaye siyo watoto wangu?”anasema Tesha.
Anafafanua kuwa ujumbe huo ulifafanua: “Kama akiendelea kufanya hivyo ataiuzilia mbali nyumba aliyompa kwa ajili ya watoto, ambao mimi siku zote nilikuwa nikiamini ni baba yao.”
Anaeleza kuwa tangu alipofungua simu ya mkewe na kusoma ujumbe huo maisha yake yalibadilika kwani alikwenda kuwapima DNA watoto hao na kumbana mama yao ambapo ilibainika kuwa ni kweli watoto hao sio wake, jambo lililomchanganya na kumtia aibu kwenye familia na jamii hivyo akaamua kuwa mlevi.
Tesha anasema kuwa kuanzia hapo aliacha kusimamia biashara zake kutokana na kuchanganyikiwa na kukwepa aibu, huku akiishi kwa kujificha kwa zaidi ya mwaka na alipotulia na kujifikiria kwa nini amekuwa hivyo alikuwa tayari ameshachelewa, kwa kuwa baadhi ya maduka yalikuwa yamefungwa na aliowaacha hakuwa na cha kuwafanya akibaki na duka moja la Arusha ambalo pia lilikuwa limekufa kutokana na kuwa na bidhaa chache.
“Naishi kwa ushauri na ndiyo maana mara nyingi nimekuwa nakutumia ujumbe wa kutaka unishauri kwa kuwa siiamini tena akili yangu wala mwili wangu. Kama mwanamke ambaye nilikuwa naishi naye miaka yote aliweza kubeba mimba za mtu mwingine na nisijue, sina sababu ya kujiamini tena, nimekuwa masikini kwa sababu ya simu, sitamani simu ya mtu zaidi ya hii yangu, ambayo wakati mwingine huwa naamua kuifunga,”anamaliza Tesha.
Wakati Tesha akieleza hayo, upande mwingine Jennipher Lazaro wa Tanga anasema kuwa hawezi kuishi bila simu kwa kuwa humsaidia mambo mengi ikiwamo kujifunza zaidi kupitia mtandao, kumuunganisha na marafiki walio mbali naye.
Anafafanua kuwa akiambiwa achague kati ya simu na kuzungumza na mtu anayempenda kama mumewe atachagua simu kwa kuwa haimuuzi, lakini mumewe kuna siku huwa anamkera.
Naye Zaituni Mapunda (siyo jina halisi) wa Mbeya anasema kuwa simu kwake ni rafiki na adui, kwani imekuwa ikimpa mambo mengi mazuri huku pia ikimsababishia matatizo.
“Nikiachwa basi, cha kwanza kukilaumu ni simu kwani mara nyingi nakorofishana na mpenzi wangu, anakuta ujumbe niliotumiwa na wanaume wengine nasahau kuufuta,”anasema Mapunda.
Anafafanua kuwa mbali na hayo, bado anaithamini zaidi simu kwa kuwa ni kiunganishi kikubwa kati yake na watu wake wa karibu, huku akikiri kuwa mara nyingine hufanyia mambo yasiyo sahihi, ikiwemo kuwasiliana na wanaume wengi kwa wakati mmoja, ambao huwapanga kirahisi kwa kutumia simu.
“Nina uwezo wa kuwa na wanaume wengi kwa kutumia simu, lakini pia maisha yangu yanakuwa na unafuu kupitia simu,”anasema na kuongeza:
“Kama nitapewa adhabu kubwa basi ni kuambiwa nisiwe na simu au mpenzi wangu akishinda na simu yangu hawezi kuishi wala kunipenda tena maishani mwake, kwani atapigiwa simu na wenzake hadi atashangaa.”
Mudi Mkotopaje wa Dar es Salaam anasema kuwa ameshaacha wanawake wawili kutokana na kukuta maovu kwenye simu na kwamba aliyenaye kwa miaka miwili tangu waoane hataki awe na simu.
Anafafanua kuwa simu ni kishawishi kikubwa na kwamba wanawake wote aliwaacha huku bado anawapenda na wote walikuwa na kesi zinazofanana za kuwa na matumizi mabaya ya simu kwa kufanya uhusiano usio rasmi.
Anatoa ushauri kuwa hata kwa wazazi ili mabinti zao wasome kwa uhuru na kuelewa walichokusudia wasipewe simu.
Mwamvua Jumbe mama wa watoto wawili, anasema kuwa aliachana na mumewe kutokana na kumkuta na ujumbe wa mapenzi karibu kila siku.
“Wazazi wangu na wake walinikanya kuhusu kuchunguza simu yake nilishindwa kwa kuwa nilikuwa nampenda na nilikuwa naamini kuwa kuna kitu tofauti anafanya kunizunguka. Kila nilipojaribu kumchunguza nilimkuta na hatia. Kama ikitokea nikaolewa tena sintotaka kuwa karibu na simu ya mume wangu ili nisijue anachokifanya, kutokana na kupata shida ya kumlea mtoto peke yangu ,”anasema.
Mwanasaikolojia azungumza
Mtaalamu wa masuala ya saikojia wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) Modesta Kimonga alisema kuwa matumizi mabaya ya simu ni kifo kwa kuwa akili ya binadamu inabadilika kulingana na tukio lililotokea.
Alitoa mfano kuwa wakati msiba ukitokea mtu analia, akiona kitu siyo cha kawaida anaweza kufurahi au akatabasamu, akiongeza kuwa mtu ikiona kitu tofauti na inavyotarajiwa hubadilika na ndiyo sababu kuna watu wanajiua kwa vitu vidogo.
“Miongoni mwa vitu ambavyo tunatakiwa kuwa na tahadhari navyo ni simu kwani vinaweza kuleta athari kubwa kama havikutumiwa vizuri kwa matumizi yaliyokusudiwa tofauti na hapo zinaweza kuleta maafa,”anasema na kufafanua:
“Kwa mfano mume au mke anapekua simu ya mmojawao bila idhini ya mwenzake na kukuta kitu tofauti kinachoweza kumpa hasira, akapata matatizo ya kiafya au akaenda kumdhuru mkewe au mumewe kutokana na akili yake kuvurugika kutokana na alichokiona. Kila mmoja aelewe kuwa simu ya mkononi ni kwa ajili ya mwenye nayo.”
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
Mtaalamu wa takwimu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Hango Juma, alitaja idadi ya watumiaji wa simu nchini hadi Machi mwaka huu kuwa ni 27.6 milioni na kwamba mwenye haki ya kutumia simu ni mhusika wa simu hiyo.
“Si ruhusa kwa asiyekuwa mmiliki halali wa laini kuipeleleza kwa kwenda kwenye kampuni ya simu kujua amewasiliana na watu wangapi au kwa namna yoyote ile. Wafanyakazi kwenye kampuni za simu wanatakiwa kutunza siri za wateja kisheria na siyo kuzisambaza au kuzitoa kwa wahusika hata kama ni laini zao,”anasema Juma.
Tafiti yagundua
Wakati hali ikiwa hivyo Tanzania, nchi 11 za Ulaya zimefanyiwa utafiti na kubaini kuwa asilimia 94 ya watu wazima huona ni heri waishi bila ngono kuliko kuishi bila simu za mkononi, huku asilimia 65 ya watu waliofanyiwa mahojiano wakisema kuwa hawawezi kuishi bila simu na asilimia 53 walikiri kuwa wameathirika na simu zao.
Zaidi ya 2,570 watu wazima nchini Uingereza, wenye umri kati ya 18 na 30, walishiriki katika utafiti uliofanywa na Mobileinsurance.co.uk ambapo iligundulika kuwa asilimia tisa ya watu wazima wa Uingereza huona ni heri kuishi bila watoto wao kwa wiki kuliko kukaa bila simu za mkononi.
|
Old time rapper kutoka Tanzania D Knob amefungua mtandao unaojulikana kama www.mitaanimostwanted.co.tz utakao jihusisha na Usimamizi wa biashara tofauti na mambo ya burudani.
Mtandao huu utakuwa na kazi ya kuanda projects za biashara na mambo ya huduma tofauti mitaani. Kwa sasa mtandao huu unafanya kazi bega kwa bega na project ya Marco Chali Foundation kupitia Epic Open Mic.
|
Mwanamke mmoja wa nchini Marekani ametoa kali ya mwaka kwa kuamua kuandaa harusi na kujioa yeye mwenyewe kanisani.
Nadine Schweigert mwenye umri wa miaka 36 amekuwa gumzo kwenye vyombo vya habari nchini Marekani baada ya kuandaa harusi na kujioa yeye mwenyewe ambapo yeye ndiye alikuwa bi harusi na yeye pia ndiye aliyekuwa bwana harusi.
Nadine ambaye ni mkazi wa Fargo, North Dakota nchini Marekani alijioa mwenyewe kwenye sherehe iliyohudhuriwa na jumla ya watu 40.
Alikula viapo vya ndoa mbele ya umati huo wa watu ambapo mwisho wa viapo alipuliza busu angani badala ya hali iliyozoeleka ya bibi na bwana harusi kubusiana.
Harusi hiyo ilifuatiliwa na fungate la nguvu (honeymoon) kwenye hoteli moja mjini New Orleans.
Akiielezea ndoa yake hiyo kwenye kipindi cha televisheni moja nchini humo, Nadine alisema kuwa hivi sasa anajihisi ni mwenye furaha sana na ndoa yake imeweza kuyabadilisha maisha yake toka kwenye huzuni na kuwa mwenye furaha sana.
Nadine alisema kuwa aliamua kujioa mwenyewe baada ya ndoa yake na mumewe aliyezaa naye watoto wawili ilipovunjika na watoto wake kuamua kwenda kuishi na baba yao.
Nadine alisema kuwa alipita kipindi kigumu sana cha machungu ya kuvunjika kwa ndoa yake lakini baadae aliamua kukaa chini na kutafakari maisha yake badala ya kujiingiza kwenye ulevi ili kupoteza mawazo.
Nadine aliongeza kuwa ndipo alipogundua kuwa furaha ya kweli na mtu anayempenda sana ni yeye mwenyewe hivyo akaamua kujioa yeye mwenyewe na hivi sasa haitaji tena mwanaume kwenye maisha yake.
Nadine aliongeza kuwa katika maisha yake haya mapya amekuwa akijitoa out mara kwa mara na amekuwa akijinunulia zawadi yeye mwenyewe.
|
Bibi Li Xiufeng baada ya kuzinduka toka kuzimu
Bibi mmoja wa nchini China amewashtua ndugu na majirani zake baada ya kutangazwa kuwa amefariki dunia na kupelekea maandalizi ya mazishi yake kufanyika lakini alizinduka na kurudi duniani siku ya sita akitoka ndani ya jeneza.
Bibi Li Xiufeng mwenye umri wa miaka 95 aligunduliwa na majirani zake akiwa kitandani chumbani kwake akiwa hapumui na haonyeshi dalili yeyote ya kuwa hai.
Tukio hilo lilitokea wiki mbili baada ya bibi Li kuteleza na kuanguka njiani na kupelekea kupata majeraha kichwani kwake.
Baada ya majirani kumkuta chumbani kwake akiwa hapumui, walijaribu kumzindua lakini ilishindikana. Bi Li alikuwa hapumui na wala haonyeshi dalili yeyote ya uhai lakini mwili wake haukuwa wa baridi. Kwa fikira zao na majaribio machache waliyoyafanya, majirani walitangaza kuwa bibi Li amefariki dunia.
Mwili wa bi Li ambaye alikuwa akiishi peke yake akipewa kampani na majirani, uliwekwa kwenye jeneza ndani ya nyumba yake na kwa kufuata taratibu za tamaduni za China, jeneza halikufunikwa liliwachwa wazi juu ili kuwapa nafasi watu kuuaga mwili wa bi Li.
Siku ya sita, majirani walipoenda kuuangalia mwili wa bi Li kabla ya kuuzika rasmi siku iliyofuatia, walishangazwa kukuta mwili haupo ndani ya jeneza.
Msako mkali kijijini ulianza kuutafuta mwili wake na mazingira yanayoizunguka nyumba yake. Baada ya muda watu walishangazwa kumkuta bi Li akiwa jikoni anapika.
"Nililala kwa muda mrefu sana, baada ya kuamka nilihisi njaa kali ikanibidi niingie jikoni kupika kitu cha kula", alisema bi Li alipohojiwa na majirani zake.
Madaktari walisema kuwa kitaalamu bi Li alipatwa na "kifo cha bandia" 'artificial death', ambacho huelezewa kuwa mtu huwa hapumui lakini mwili wake huendelea kuwa wa moto.
"Utamaduni wa kuhifadhi mwili ndani ya nyumba kwa siku kadhaa ndio uliookoa maisha ya bi Li, kama si utamaduni huo bi Li angekuwa ameishazikwa kweli zamani", alisema mmoja wa Madaktari waliomfanyia uchunguzi bi Li baada ya tukio hilo.
|
MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Mjini, Aziz Abood ambaye ndiye mmiliki wa Kituo cha Abood Media alipokuwa akifanya kazi marehemu Nyaisangah akimpa mkono wa pole mke wa marehemu, Leah Nyaisangah nyumbani kwake Kihonda Mtaa wa Viwandani mkoani Morogoro.
Mke wa marehemu, Leah Nyaisangah akiwa na simanzi baada ya kuondokewa na mumewe.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa msibani kwa marehemu Julius Nyaisangah eneo la Kihonda Mtaa wa Viwandani mkoani Morogoro.
(PICHA ZOTE NA DUSTAN SHEKIDELE, GPL / MOROGORO)
|
MIMI ni msichana wa miaka 25 sasa ..Nashindwa hata nianzie wapi ila kifupi mimi sina bahati na wanaume at all..Nina sura na umbo zuri na amini hilo kwani kila napokwenda lazima nitongozwe ama nisumbuliwe na wavulana njiani mpaka nimezoea...
ila tatizo linakuja pale napomkubalia mwanaume na kuwa wapenzi ..wakishapata wanachohitaji hawakai kabisa...nimetembea na wavulana wengi tu kila anaenipata anakaa kidogo na kuanza visa na kuniacha ...Mie najua kupenda naamini....Marafiki zangu wanaolewa ila mimi hakuna hata aliye nivisha pete na uzuri wangu huu..hadi najilaumu labda umbo langu limekaa kistaree tu na sio wa kuolewa...kwa sasa nimekata tamaaa nawachukia wavulana kila atakaye nitongoza nahisi anataka kitu tu alafu akimbie...Nisaidieni kwa Ushauri...
|
Huyu jamaa aneye jiita Man Hit Aliweka Record Hii kutokana na Kudondoshewa Kitu Mfano wa Tufe Kichwani mwake.
Tamaza maajabu hapa Chini.
|
|
|
''MASAI NYOTAMBOFU'' na ''CHRISTIAN BELLA'' KATIKA POZZZ... |
BAADA ya (Rungu na mukuki) iliyofuatiwa na (Yero masai) ambayo kwa sasa VIDEO yake ipo mbioni kutoka, Sasa nawaahidi mafans wangu kwamba wakae mkao wakula kusubiria ngoma nyengine kali nafanya na ''CHRISTIAN BELLA'' katika Studio ya Producer ''C9 KANJENJE''
Producer C9 KANJENJE
|
HIVI NDIVYO NILIVYOPOKELEWA MJINI TABORA KABLA YA SHOW...!!! ''MASAI NYOTAMBOFU''
|
WATU WANGU WA TABORA MAMBO FIPIIIIIIIIIIIII?.... ''MASAI NYOTAMBOFU'' |
BAADHI YA MASHABIKI WA MASAI NYOTAMBOFU WAKIMPIGA PICHA KATIKA SIMU ZAO..
MASHABIKI WAKIONYESHA NYUSO ZA FURAHA BAADA YA KUMUONA MCHEKESHAJI ANATIKISA TASNIA YA VICHEKESHO HAPA NCHINI KATIKA SWAGA ZA KABILA LA WAMASAI.. ''MASAI NYOTAMBOFU''....!!!
|
MSANII ANAETIKISA BONGO KWA NGOMA YAKE YA KINYULINYULI ''SAMIR'' AKIWAPA LADHA KIDOGO MASHABIKI WAKE.. |
|
BOB JUNIOUR RAIS WA MASHAROBARO ALIVYOPOKELEWA MJINI TABORA...! |
|
|
MASELE CHA POMBE A.K.A AGHMADAAAAAAA....! |
MASELE CHA POMBE AKIWAPOMBESHA KILEVI MASHABIKI KWA MANENO
BOB JUNIOR AKIWARUDISHA KIMBIJI HADI TABORA MASHABIKI WAKE
SAMIR AWACHEZESHA KINYULINYULI WATOTO
MOJA YA DANCER WA BOB JUNIOR AKIFANYA MANJONJOO
THE CHOCOLATE; DANCERS WA BOB JUNIOR
NYOTA MBOFU ILING'AA TABORA...!
|
TUKIWAONYESHA MASHABIKI JISHI YA KUCHEZA STAIL YA (YERO MASAI..) |
HAPAKUTOSHAAAAAAAAA.
|
MCHEKESHAJI maarufu hapa nchini ''Masai Nyotambofu'' kutoka kundi la ''VITUKO SHOW'' Kundi linalotikisa tasnia ya Vichekesho Afrika mashariki, Msanii huyo ambaye pia ni mmiliki wa website ya www.masainyotambofu.com Akiongea na Babamzazi.com, Miongoni mwa mambo aliozungumzia ni kuhusu VIDEO ya wimbo wake mpya ( Yero Masai ) Aliowashirikisha wasanii nguli katika muziki wa kizazi kipya na dance, Rich mavoko na Kitokololo kalidjo rapa wa Fm Academia. Video hiyo ameifanya hivi majuzi Jijini Dar Es Salaam na kampuni ya Apex Videos Chini ya Director Pablo, Mazungumzo na mwandishi yalikuwa hivi,
Masai Nyotambofu: Kwanza naanza kwa kumshukuru M/mungu kwa kunisaidia hadi kukamilisha VIDEO yangu salama,
Mwandishi: Vipi kusu Changamoto zilizokukuta?
Masai Nyotambofu: Eem.. Chngamoto ni nyingi ila iliyovunja rekodi ni ile ya kuvunjika lence ya Camera wakati tukiwa katika harakati za Shuting ilitokana na kuanguka kwa Crayn ya Camera, Director akabadili Lence ili tuendelee, Mara Radio ikagoma kuimba! Tukabadili flash bado haikusaidia wakati huo muda ulikuwa unaenda na jua linatupa mkono matokeo yake mwanga ukapotea tukalazimika kuwasha taa, Bado hakikueleweka maana umeme nao ulizingua kaka mpaka nikasema kuna mkono wa mtu nini?, Yani full vikwazo, Ikatubidi tugairi kushut sikuhio, Siku inayofuatia tulifika location mapema kama kawaida Ndipo tulipomaliza kazi salama mpaka hivi sasa inamaliziwa Editing,
Mwandishi: Pole sana Nyotambofui, Unawaambia nini mashabiki wako wanaoisubiri Video yako ya ( Yero Masa )? Masai Nyotambofu: Wakae mkao wakula ( Yero Masai ) Video itakuwa On air siku chache zijazo.
|
Inasemekana kwamba Wema Sepetu ndio anaongoza kwenye List hii, kwa kweli she is beautiful.
Lulu Michael ndiye anachukuwa nafasi ya pili
Jaqi Cliff 'Lady Boss wa Bongo' anachukuwa nafasi ya tatu
4 Loveness Love
|
Mchezaji wa Yanga Mrisho Ngasa alikuwa amesema kuwa asipofunga goli ama kutoa pasi itakayo zaa goli zidi ya simba mechi ya leo basi angechoma moto nyumba zake tano
.....Lakini simesalimika baada ya kuwa mfungaji wa goli kati ya magoli matatu waliyo pata yanga .......Mechi hiyo simba na yanga walitoka droo ya 3-3
|
Wakati Shindano la kuimba linavyojumuisha waimbaji kutoka nchi za Afrika Mashariki na Sudan, likiendea ‘kunoga’, mmoja kati ya majaji hao Hermy B ameliezea dawati la majaji katika msimu huu wa sita,majaji ambao wamekuwa wakileta changamoto na kuvuta usikivu wa watazamaji kila wanapotaka kusema jambo kwa mshiriki aliyemaliza kufanya yake jukwaani.
“Kila Jaji ana nafasi yake katika lile shindano na kila jaji ana ufahamu wake wa muziki katika njia zake tofauti. Mimi ni producer wa muziki natumia masaa yangu mengi sana kushinda studio na wanamuziki na ku-develop talent. Juliana yeye ni mwana muziki kwa hiyo kazi yake kubwa ni stejini kwa hiyo na yeye anapitia process hii ya kushinda studio kuandika, kuji-brand, kwenda ku-perform. Ian yeye ni mwalimu wa muziki, kwa hiyo yeye anafuata adabu.” Amesema jaji Hermy B.
Jaji huyo ambae pia ni Producer na C.E.O wa BHitz Music Group, amefunguka pia mtazamo wake kuhusu comments zinazotolewa na jaji mwenzake Ian ambae amekuwa kivutio kikubwa pia katika shindano hilo kwa kuwa hatabiliki atasema nini kuhakikisha anachomaanisha kifike moja kwa moja bila kuchujwa.
“One thing ambacho watu wengi wanamchukulia tofauti Ian ni kwa sababu Ian anakwambia ukweli, kwamba umeimba vibaya, hatakwambia kama mimi navyokwambia labda ubadilishe sauti hapa na pale ili ku-improve, Ian atakwambia ni mbaya.
“Na mtu kukaa stejini for almost dakika 2 halafu unakuja kuambiwa ni mbaya, inauma. But Ian yuko Straight, hapindi, na in personal Ian sio mtu mbaya, actually Ian ni mchekeshaji mzuri.” Amefunguka Hermy B.
Shindano hilo linaendelea leo na litarushwa kupitia EATV.
|
Kiu ya kuimiliki simu mpya ya iPhone na kuendana na ulimwengu wa digital umewaponza wazazi waishio nchini China ambao wamejikuta mikononi mwa polisi baada ya kumuuza mtoto wao kwa pound za Uingereza 5,000.
Kwa mujibu wa ripoti za polisi wa Shanghai, wazazi hao waliotambulika kwa majina ya Mr. Teng na Miss Zhang, walichapisha tangazo kwenye gazeti wakiwa na nia ya kumuuza mtoto wao mwenye umri wa chini ya mwezi mmoja, na muda mfupi baada ya kumuuza mtoto huyo walienda kununua simu aina ya iphone, na kukaa kwenye mtandao (internet).
Wakiongea na gazeti la Jiefang Daily muda mfupi baada ya kukamatwa, wazazi hao walisema kuwa walikuwa na nia nzuri tu ya kumuuza mtoto wao kwa kuwa wao walikuwa hawawezi kumtunza vizuri kwa hiyo walitaka achukuliwe na familia bora yenye uwezo wa kumpa elimu bora.
Hata hivyo majirani zao walidai kuwa watu hao walianza kuwachanganya watu kuhusu hali ya ujauzito wa mwanamke huyo kwa kutaka watu waamini kuwa haukuwa ujauzito bali ni uvimbe tu usio na kitu (tumour).
Tukio kama hili la kuipata lilitokea mwaka jana nchini humo ambapo watu saba walifungwa jela katika jimbo la Hunan baada ya kujihusisha na ununuzi wa figo ya kijana mdogo ambae alitumia pesa hizo kununua iPhone na iPad.
|
MWANDISHI wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro ambaye hivi karibuni alikumbwa na madhila ya kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya na mzazi mwenzie, ameanza kufunguka kidogo kidogo na kueleza kwa kina jinsi tukio zima lilivyotokea.
Akizungumza kwa sauti ndogo na taratibu na gazeti hili kando ya kitanda alicholazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, mwanahabari huyo alieleza kushangazwa na ujasiri na nguvu za aina yake ambazo zilimwezesha kutambaa na kujiburuza hadi eneo la karibu ya barabara ili kuomba msaada wa kukimbizwa hospitali.
Ufoo ambaye alionyesha dhahiri kutofurahishwa na baadhi ya taarifa zinazozingira tukio lake, alisema tayari alikuwa amewahakikishia polisi waliofika kumjulia hali hospitalini hapo kwamba alikuwa akisubiri afya yake iimarike kabla hajaeleza kwa kina kila anachokijua kuhusiana na tukio hilo.
“Alifika hapa kunijulia hali na kuangalia maendeleo yangu afande Msangi na nikasema nitakuwa tayari kueleza kila ninachokijua baada ya afya yangu kuimarika. Nasikitika kuna watu wanasema mambo wakifikia hatua ya kutaka kuonekana wananifahamu vizuri kuliko hata ninavyojifahamu mwenyewe,” alisema akionyesha kutofurahishwa na baadhi ya taarifa zinazoripotiwa kuhusu sakata lake.
Ufoo ambaye alifikishwa hospitalini hapo Jumapili ya wiki iliyopita kutokana na kujeruhiwa kwa risasi na mwanaume aliyezaa naye mtoto mmoja alisema anamshukuru sana Mungu kwa uzima alionao sambamba na kuelezwa kupata faraja kubwa na kutiwa moyo na mwajiri wake, ndugu, jamaa na marafiki.
Mwanahabari huyo ambaye bado yuko chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa risasi mwilini mwake siku chache zilizopita, amelazwa katika chumba cha peke yake ambacho ingawa kina seti ya televisheni alisema alikuwa haruhusiwi kuiangalia kwa ushauri na maelekezo ya madaktari.
Huku akionekana wa chini ya uangalizi mwingine wa karibu na wa kudumu wa muuguzi ambaye muda wote wa mazungumzo haya alionekana kuwapo katika chumba hicho, Ufoo alisema alikuwa ana mapenzi makubwa kwa mzazi mwenzake huyo ambaye alipoteza maisha katika tukio hilo.
“Nilimpenda sana Antheri. Alikuwa kijana mtaratibu na mpole sana. Najua kile kilichotokea ni shetani tu na binafsi nilishasamehe alfajiri ile ile baada ya tukio lile,” alieleza Ufoo ambaye pia alimpoteza mama yake mzazi katika mkasa huo.
TUKIO ZIMA LILIVYOTOKEA
Ufoo ambaye mara kadhaa katika mazungumzo na gazeti hili alionekana kukunja uso akiashiria kupata maumivu, alionyesha eneo la chini ya bega katika mkono wake wa kulia lililofungwa na bandeji ambalo alisema ndipo alipopigwa risasi ya kwanza wakati akigeuka na kujaribu kuepuka mauti muda mfupi baada ya Antheri kumfyatulia risasi zilizomkuta mama yake mzazi.
Akijaribu kuvuta kumbukumbu ya tukio lilivyoanza, Ufoo alisema mzazi mwenzake huyo alifika nyumbani kwake akitokea Sudan alikokuwa akifanya kazi usiku huo huo wa tukio na akamtaka kwenda kwa mama yake (Ufoo) eneo la Kibamba, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Kabla ya kufika Kibamba na kwa sababu ambazo Ufoo hakuzieleza, alimkariri mzazi mwenzake huyo akisema alikuwa amefikia uamuzi wa kujiua yeye na mtoto wao.
“Hata sijui ni nini kilitokea. Wakati
|
|