advert

http://

Monday, 1 July 2013

HUYU NDIYE REDDS MISS LAKE ZONE 2013
























Karibu, karibu
Karibu rafiki mkuu
Karibu rafiki wa amani
Karibu rafiki mkuu wa Islael
Karibu Muungwana
Karibu Rais Barack Obama
Mimi Rafiki wa Israel na USA.
Diamond The Platnum akikisanukisha ndani ya show ya kubwa iliyopata mashabiki ambao idadi yao haijawahi kutokea ya Tigo Nkabaa uwanja wa CCM Kirumba Mwanza na kupata shangwe za kutosha. 

We wachaaaaa....!!

The Platnum mwenyewe.

Shangwe za hapa ilikuwa balaaa.. toka kwa mashabiki kwenda kwa supa staa huyu.

Chekshia magoli ya basketball yalipogeuka kuwa majukwaa.

Ney wa Mitego alipata shangwe za kutikisa...

Ngosha ze Swagz' Fid Q

On the one & two.

Roma akisalimia watu wake ambapo dimba la CCM Kirumba lilitapika kwa kuwa na mashabiki mizunguko yote...

Siwasikiiiii.

Seksheni ya Chomaz na Dada Dory.

Jirambeeeee.

Rich Mavoko... akilimeneji stage.


Recho toka THT.

Full house full nyomiiii....watu zaidi ya elfu 40.

Recho dance.

Stiko jukwaani...

Jinsi hali ilivyokuwa ikisonga mbele nao mashabiki kusogea zaidi kulifikia jukwaa askari walitumia mbwa kusogeza mashabiki wakati huo milango ikafungwa hakuna ruhusa kuingia watu tena. 

Hata show iliposimama mashabiki waliendelea kuwapo ndani ya uwanja wakidhani ni mkwara tu show ingeendelea kumbe ndiyo bye bye ya Nkabaaaa...

Afande Kotecha akiwaamuru mashabiki kuondoka sasa uwanjani kwani hali ya usalama siyo nzuri na mashabiki wameshindwa kutulia.

"Sasa tumetuliaaaa...." Ni kama kauli za mashabiki walioshuka toka majukwaani na kuketi nyasini wakilizonga jukwaa ili wapate kuendelea na burudani.

Afande Kotecha akimwamuru Diamond kushuka ili pasitokee maafa.

Njia iliwekwa sawa.....kisha mnyamwezi  the Platnum akapanda kwenye gari maalum na kusepa...

Hata kutoka kiwanjani napo kulikuwa inshu...

Kazi kweli kweli dimbani CCM Kirumba Mwanza Tanzania, hakika hii ni historia nyingine mpya imewekwa jijini hapa.
By G. Sengo.

 Timu ya Maji Maji songea leo inaingia katika kinyang'anyilo cha uchaguzi wa viongozi huyo hapo ni Humphery Millanzi mgombea nafasi ya mwekiti katika timu ya Maji Maji akimwaga sela zake jana katika mdahalo uliofanyika  jioni majira ya saa kumi katika Radio Jogoo kwa kushirikiana na Demashonews.blogspot.com, Moja ya ahadi zake ni kuhakikisha timu ya Maji Maji inapanda daraja , kuhakikisha timu inakuwa na wanachama hai na wakudumu kwa kuandaa mikutanao na kunadi sela za timu pia kuisaidia timu inakuwa na vyanzo vya pesa ili timu kuondokana na omba omba vile vile timu kuwa kampuni. Ameendelea kusema kwa kipindi hiki akiwa kiongozi wa mpito ameweza kuisaidia timu hadi kushika nafasi ya pili wakati timu haina vyanzo vya mapato hivyo sasa atakuwa na tiba mbadala katika kuiwezesha timu hiyo endapo atachaguliwa.
Toka kushoto ni Shekhan Mzaina akiwa na Hilda Kapinga mgombea nafasi ya ujumbe pia ni mmiliki wa timu ya Luwiko football Academy ya watoto chini ya miaka kumi na saba ana aihidi kuifikisha timu ya Maji Maji mbali sana akiwa kama mpenzi wa mpira wa miguu , huku akitolea mfano wakati timu hiyo ilipoenda kucheza Mbeya na kufungwa bao 6 kutokana na wachezaji  kutokuwa na uwezo wa kifedha na kuwa na mazingira mabovu
 Toka kulia kwako ni Salum Masamaki, Said Mangwe wagombea nafasi ya wajumbe na Mohamedi Issa mgombea nafasi ya Mwenyekiti.
 Toka kushoto ni Mohamed Mtika mgombea nafasi ya ujumbe akiwa na Hamphery Millanzi mgombea nafasi ya mwenyekiti wakitafakali kwa kina juu ya sela za wenzao walizokuwa wakitoa katika mdahalo uliokuwa ukiendelea katika Studio za jogoo FM kwa kushirikiana na demashonews.blogspot.com
 Toka kushoto ni Mohamed Mtika mgombea nafasi ya wajumbe , Hamphery Millanzi mgombea nafasi ya mwenyekiti, John Kabisana mgombea nafasi ya wajumbe na Mohamed Issa mgombea nafasi ya mwenyekiti

Toka kushoto ni mtangazi wa Radio Jogoo kipindi cha michezo Hosam Ulaya , Shekhan Mzaina na Hilda Kapinga mgombea nafasi ya wajumbe
 Wagombea uongozi katika Timu ya Maji Maji wakiandika maswali yaliyokuwa yakiuliuzwa kwa njia ya simu na wasikilizaji kupitia Radio Jogoo
 Baada ya kutoka katika mdahalo
 Picha ya pamoja toka kulia walio simama ni Hamphery Millanzi mgombea nafasi ya mwenyekiti,Said Mangwe wagombea nafasi ya wajumbe,Mohamed Issa mgombea nafasi ya mwenyekiti, Mchele, Tamimu Adamu  mtangazaji wa Radio Jogoo,Mohamed Mtika mgombea nafasi ya wajumbe,Salum Masamaki, John Kabisana mgombea nafasi ya wajumbe na kuoka kulia kwa walio chuchumaa ni Hilda Kapinga mgombe nafasi ya wajumbe, Shekhan Mzaina  na Hosam Ulaya
Humphery Millanzi mgombea nafasi ya mwekiti akiteta jambo na Hilda Kapiga mgombea nafasi ya wajumbe.
Leo (jumapili ya tarehe 30/06/2013) ndiyo siku ambayo itakwenda kuandika historia mpya katika timu ya Maji Maji kwa kufanyika uchaguzi kuanzia saa  saa nne asubuhi na jana ilikuwa ni kujinadi kila mgombea kutoa sera zake ambapo mambo yote ni leo.