Mwalimu Gloria Tarimo ‘Ticha Gloria’ (29) aliyekuwa akifundisha katika Shule ya Mbezi High School ya jijini Dar, amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha
huku baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wakidai kifo chake ni cha kimiujiza. Ticha Gloria ambaye alikuwa akikaimu nafasi ya mwalimu mkuu wa shule hiyo, alifariki dunia Desemba 6, mwaka huu katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar huku wengi wakihisi kuna mkono wa mtu nyuma ya kifo hicho. Marehemu Glory A Tarimo enzi za uhai wake.
USHIRIKINA WAHUSISHWA Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa ndugu wa marehemu aliyeomba hifadhi ya jina lake kwa kuwa si msemaji wa familia alisema, kifo cha Ticha Gloria kinahusishwa na ushirikina kwa kuwa kabla ya mauti kumfika alikumbana na mambo mengi ya ajabu. “Ni kifo cha ajabu kwa kweli na kimemshangaza kila mmoja wetu. Nakumbuka ilikuwa Juni, mwaka huu ambapo alienda kazini na alipofika kwenye mlango wa ofisi yake alikuta nazi imevunjwa.
“Licha ya kushangazwa na uwepo wa nazi hiyo, aliiruka kisha akaingia ofisini kwake. Kuanzia hapo alianza kuumwa mguu, kuna wakati akawa anahisi unawaka moto. Tulimpeleka Hospitali ya Muhimbili, akapatiwa matibabu na akapata nafuu,” alisema ndugu huyo.
AKUTA NJIWA KWENYE KITI OFISINI Ndugu huyo alizidi kueleza kwa masikitiko kuwa, baada ya tukio hilo la kukuta nazi imevunjwa kwenye mlango wa ofisi yake, mambo hayakuishia hapo kwani hivi karibuni alipoingia ofisini kwake alikuta Njiwa kwenye kiti chake. “Alipiga kelele sana, walimu na wanafunzi wake wakaja kushuhudia huku kila mmoja akishangaa na kuogopa kumtoa njiwa yule kwenye kiti.
“Mwalimu mmoja aliyefahamikwa kwa jina la Fadhili ndiye aliyemuondoa njiwa yule. Bila kujua kuwa roho yake inasakwa, Gloria akakaa kwenye kile kiti na kuendelea na shughuli zake,” alisema ndugu huyo na kuongeza: “Haikuchukua muda mrefu akahisi kama anachomwa na kitu chenye ncha kali kwenye makalio yake huku kichwa kikimuuma sana. Walimu wenzake walimchukua na kumrudisha hospitalini.”
AANZA KUZIONA SIKU ZAKE MFULULIZO Ilielezwa kuwa, baada ya mwalimu Gloria kufikishwa hospitalini, hali ilizidi kuwa mbaya na akaanza kutokwa na damu ya hedhi mabongemabonge huku damu nyingine ikitokea puani.
Ndugu wa Marehemu.
“Hali ilikuwa hivyo, akawa anateseka sana huku wakati mwingine akilalamikia baadhi ya walimu wenzake kuwa ndiyo wanaotaka kumtoa roho. “Kuna siku alimuita daktari aliyekuwa akimhudumia na kumwambia anamshukuru kwa kujitahidi kuokoa uhai wake lakini anaamini hatapona kwani anajua kuna walimu wamedhamiria kumuua ili wakalie kiti cha ualimu mkuu, baada ya hapo alikata roho,” alisema ndugu huyo ambaye ndiye aliyekuwa akiwasiliana na marehemu mara kwa mara.
WALIMU WANASEMAJE? Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, baadhi ya walimu wa shule hiyo walisema wamesikitishwa sana na kifo cha Ticha Gloria, wakasema licha ya kwamba kila kifo kinapangwa na Mungu lakini hiki cha mwenzao kimeacha utata. “Kwa kweli kifo cha Gloria kimenifanya niamini kuwa Mungu yupo lakini pia ushirikina upo. Amekufa kifo cha kimiujiza sana, mambo yaliyomtokea kabla ya kufariki dunia yanaashiria kabisa kuna mkono wa mtu,” alisema mwalimu mmoja wa kike aliyeomba hifadhi ya jina lake. MSIKIE MWENYE SHULE Mkurugenzi wa shule hiyo aliyefahamika kwa jina la Said Mgude alielezea masikitiko yake juu ya kifo cha mwalimu Gloria kwa kuwa alikuwa mchapakazi sana ila akataka watu wasihusishe kifo hicho na mambo ya kishirikina.
“Kila mmoja lazima aumie kwa kifo cha Gloria, lakini nawasihi watu wamuamini Mungu na waachane na dhana za kishirikina. Shule yangu ni taasisi kubwa sana, minazi ipo mingi hivyo kama alikuta nazi imevujwa mlangoni inawezekana ilianguka tu na kupasuka. “Kuhusu Njiwa hapa Dar es Salaam siyo jambo la ajabu kwa sababu wapo wengi sana, mimi siwezi kukubaliana na mambo hayo ya kishirikina na hakuna kitu kama hicho,” alisema.
Mwili wa mwalimu Gloria uliagwa Desemba 10, mwaka huu katika Kanisa Katoliki Mbezi Mwisho jijini Dar na baadaye ulisafirishwa kwenda Moshi Rombo mkoani Kilimanjaro na kuzikwa siku iliyofuata ya Desemba 11. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-Amin.
Stori: Gladness Mallya, Nyemo Chilongani na Haruni Sanchawa.
|
Stori: Mayasa Mariwata na Chande Abdallah
JAMANI jamani! Dunia imefika pabaya zaidi, Mungu asaidie. Mwanamke mkazi wa Chalinze,
Mkoa wa Pwani, Moshi Rashid (43) amefanyiwa unyama uliopitiliza na watu wasiojulikana baada ya kumbaka na kumnyonga, inauma sana kwa kweli!
Mwanamke mkazi wa Chalinze, Mkoa wa Pwani, Moshi Rashid (43) amefanyiwa unyama uliopitiliza na watu wasiojulikana baada ya kumbaka na kumnyonga.
Tukio hilo la kutisha lilijiri usiku wa Desemba 7, mwaka huu…
Stori: Mayasa Mariwata na Chande Abdallah JAMANI jamani! Dunia imefika pabaya zaidi, Mungu asaidie. Mwanamke mkazi wa Chalinze, Mkoa wa Pwani, Moshi Rashid (43) amefanyiwa unyama uliopitiliza na watu wasiojulikana baada ya kumbaka na kumnyonga, inauma sana kwa kweli!
Mwanamke mkazi wa Chalinze, Mkoa wa Pwani, Moshi Rashid (43) amefanyiwa unyama uliopitiliza na watu wasiojulikana baada ya kumbaka na kumnyonga. Tukio hilo la kutisha lilijiri usiku wa Desemba 7, mwaka huu Chalinze Kwamwarabu ambapo mwanamke huyo alikwenda kujumuika na ndugu na majirani katika mkesha wa ngoma ya kuwatoa wari siku ya Jumapili.
Eneo la tukio Chalinze Kwamwarabu.
Mkasa huu unasimuliwa kwa majonzi mazito na mdogo wa marehemu ambaye alikuwa mshehereshaji wa shughuli hiyo ‘MC’, Siwema Rashid.
Alisema: “Mpaka sasa tunashindwa kuelewa kilichotokea maana siku ya tukio tulikuwa naye kwenye ngoma usiku. Alikuwa mchangamfu sana, aliifanya shughuli ipendeze.
“Ilipofika saa nane usiku baadhi ya watu walianza kulala, sasa sijui yeye ilikuwaje mpaka hali hiyo ikamfika maana hao watu walichomfanyia wametuachia historia kubwa sana.
“Walimbaka wakaona haitoshi wakamwingiza chupa ya soda sehemu ya siri ya mbele halafu wakamwingiza chupa ya bia sehemu ya siri ya nyuma.
“Ili kuzidi kutimiza unyama wao, waliondoka na kumwacha kama alivyozaliwa, inauma sana halafu matukio ya hivyo yamekithiri sana.” Aliongeza: “Marehemu ametuachia jukumu la malezi kwa watoto wake wawili, Sikudhani Juma (18) na Ally Juma (12).” Naye mtoto mkubwa wa marehemu, Sikudhani akisimulia kifo cha mama yake, alisema: “Nasikitika sikuweza kuuona mwili wa mama hata pale watu walipojazana na kumshangaa.
“Hata polisi na mganga mkuu wa mkoa walipofika kumchomoa zile chupa sikutaka kusogea kabisa, naamini Mungu atawaonesha jambo hao watu hapahapa duniani.” Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Yurichi Mtei akizungumzia ukatili huo alisema: “Taarifa za tukio hilo bado hazijafika kwangu kutokana na majukumu mengine ya kikazi, isipokuwa nalifanyia kazi kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa.” Tukio hilo lilifunguliwa jalada kwenye Kituo cha Polisi Chalinze kwa nambaCH/RB/3767/2013 MAUAJI. Mpaka kifo chake, mwanamke huyo alikuwa akiishi na mwanaume mmoja (jina halikupatikana mara moja lakini si aliyezaa naye watoto hao wawili). Alizikwa Jumapili iliyofuata, Chalinze. Mungu ailaze pema peponi roho yake. Amina.
source:GPL
|