Mwenyekiti wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage amewasili Dar es salaam Tanzania leo akitokea Sudan ambapo alipokelewa na baadhi ya Wanachama wa Simba kwenye Uwanja wa ndege wa mwalimu JK.Nyerere.
Waandishi wengi walikua na maswali mengi kuhusu yeye kusimamishwa kuwa Mwenyekiti wa Simba lakini akayapangua kwa kusema kesho mchana ndio atazungumza na Waandishi kuhusu kila kitu ila sentensi moja iliyonyakwa na millardayo.com ni ‘taarifa za kusimamishwa Uwenyekiti sijazipata ndio kwanza nakusikia wewe, ninachojua mimi bado ni Mwenyekiti wa Club ya Simba’
‘Nimefurahi kwa mapokezi mazuri ambayo yameonyesha imani ya Wanachama kwangu mimi, mimi kama Mwenyekiti nitatoa tamko langu rasmi kesho mchana makao makuu ya Club ya Simba, sasa hivi siwezi manake rafiki yangu mpenzi Zitto kabwe ameondolewa kwenye Unaibu katibu mkuu na mimi sijafurahia kwa hiyo siko kwenye mood ya kuongea’ – Aden Rage
Alipoulizwa kama ana taarifa za kocha mpya Simba na pia kikao hicho atakifanyiaje Makao Makuu wakati ameondolewa kwenye Uwenyekiti, Rage kasema swala la kocha atalizungumza kesho ila hilo la kufanyia mkutano na Waandishi wa habari makao makuu ya Simba, waandishi wasiwe na wasiwasi kwani yeye ndio Mwenyekiti.
Kuhusu kikao kilichofanyika na kumuondoa kwenye nafasi ya Uwenyekiti, Ismail Aden Rage amesema kikao kilichofanyika sio halali manake ukisoma katiba ya Simba, FIFA na CUF katika aya zote hakuna aya inayosema kamati ya utendaji ina mamlaka ya kumsimamisha Rais au Mwenyekiti.
Credit:Millardayo. |
watu wengine wawili kwa risasi asubuhi kati ya saa moja na saa mbili, amezikwa kwao Nkoshashi Wilaya ya Hai Kilimanjaro leo November 22 2013.
Gabriel ambae amefariki akiwa na umri wa miaka 31, anadaiwa kufanya mauaji ya watu wawili aliowasubiria nje ya geiti wakitoka nyumbani kwao (waliouwawa) huku chanzo kikitajwa kwamba ni kisa cha kimapenzi.
Kama alijua kitakachotokea, alichokiandika cha mwisho kwenye page yake ya facebook kiko chini kabisa mwa hii post.
|
Ni ajabu kuona wanadamu wanakuwa wabaguzi kwa kiasi hiki kwa sababu ya maumbile.
Mambo mengi yamesemwa kuhusu tatizo la mtindio wa ubongo, hali ambayo imekuwa ikisababisha jamii mbalimbali kuwanyapaa na hata kuwabagua watoto wenye tatizo hilo.
Kitaalamu, mtindio wa ubongo unaelezwa kuwa ni hali inayompata mwanadamu kwa ubongo wake kushindwa kufanya kazi katika utaratibu wa kawaida. Kimsingi, ni uwezo wa ubongo kutokukua vizuri na kushindwa kufanya kazi yake katika mazingira yake ya kawaida.
Wataalamu wa afya kutoka sehemu mbalimbali duniani ikiwamo Tanzania wanabainisha kuwa mtu mwenye uwezo mdogo wa kufikiri, si kwamba ana matatizo ya akili ama mtindio wa ubongo.
Mtindio wa ubongo unaweza kusababishwa na hali mbalimbali ikiwamo ubongo kuathirika wakati wa kuzaliwa, na hata maisha ya utoto.
Kumbe, yapo mambo matatu yanayosababisha matatizo kwenye ubongo wa mtoto ambaye hajazaliwa mfano ugonjwa wa down syndrome hujitokeza baada ya matatizo katika vinasaba kutokea ambayo baadhi ya matumizi ya dawa husababisha mabadiliko katika vinasaba kama vile dawa za kunywa, ulevi kupindukia (fetal alcohol syndrome) na kuwa na mwili wenye afya dhaifu (fragile X).
Viasili, wakati mwingine huwa ni matokeo ya mtindio wa ubongo. Hiyo hutokana na asili ya kifamilia kuwa inapotokea mmoja wa wanafamilia wana asili na hali hiyo, basi wengine miongoni mwao watapata.
Mbali na hayo, pia matumizi ya dawa kali anazotumia mama wakati wa ujauzito, matumizi ya dawa za kulevya, pombe, hali ya hewa, au hata ajali husababisha kufikwa na hali hiyo.
Utafiti uliowahi kufanywa katika sehemu mbalimbali, unaonyesha kuwa pombe ina athari kubwa na mbaya hasa kwa kina mama wajawazito na matatizo wanayopata yanafahamika kitaalamu Fetal Alcoholic Syndrome (FAS).
Watoto wengi wanaozaliwa na tatizo hili wanakuwa na nyuso ambazo siyo za kawaida (facial deformities). Kwa mfano, watoto hawa wanaweza kuwa na pua bapa na macho yaliyoingia ndani au kupata matatizo ya kusikia na kutokuwa na uwezo wa kusoma.
Ukweli ni kwamba ni vigumu kwa wazazi kuwatambua watoto wao wenye tatizo hili na mara nyingi ni kwa watoto kabla ya kutimiza miaka kati ya mitatu na minne.
Hata hivyo, dalili zifuatazo zinaashiria kuwa mtoto ana tatizo hili. Kwanza, haonyeshi dalili yoyote ya kulia au anaweza kulia kwa kiasi kidogo, huchelewa kutembea na hata kuongea, haonyeshi kuvutiwa na mazingira yanayomzunguka, kwa maana kwamba hata kama kuna vitu vya kuchezea hawezi kujishughulisha navyo.
Endelea kusoma habari hii hapa.http://www.mwananchi.co.tz/Mtindio-wa-ubongo--Sababu-ya-watoto-wengi-kubaguliwa/-/1596774/2084498/-/12w9cvez/-/index.html
|
Mambo yanazidi kuwa magumu kwa member wa zamani wa Ruff Ryders DMX ambaye yuko katika hali mbaya kifedha na hata kisaikolojia.
Hata muonekano wake unaonesha yuko katika kipindi kigumu (pichani).
Kwa mujibu wa TMZ rapper huyo ameripoti polisi akidai kuibiwa gari na rafiki yake aliyempa gari hilo mwezi uliopita ili akamsaidie kuuza angalau apate chochote.
DMX na girlfriend wake Desiree Lindstrom walimpa gari na copy ya kadi ya gari hilo rafiki yao waliyemfahamu kwa jina moja la ‘Lonny’ ili akawasaidie kuuza lakini rapper huyo amedai kuwa tangu walipompa gari hilo amepotea na simu yake haipatikani.
Kwa bahati mbaya DMX anafahamu jina moja tu la rafiki yake huyo, kiasi kwamba ameshindwa kuandika jina lake la pili katika maelezo yake katika kituo cha polisi.
Polisi wameanza msako wa gari hilo, lakini kitu kikubwa wanachopeleleza sasa ni jina la pili la ‘Lonny’ aliyepotea na gari hilo kwa kuwa Lonny ni jina linalotumiwa na watu wengi.
Dark Man X’s aka DMX sasa hivi amefilisika kiasi ambacho anapewa msaada wa kutafutiwa shows ili aweze kurudisha hali yake ya kifedha.
Hata hivyo producer mkali Swizz Beatz ametangaza kumsaidia DMX kwa hali na mali katika kuhakikisha anamrudisha kwenye game kama zamani.
|
Ni muda mrefu sasa kumekuwa na mtafaruku mzito ndani ya Chadema ambao umekuwa ukikitafuna
sana chama hicho, na pia kuna utabiri mzito sana ulitolewa na Waziri Wassira kwamba Chadema ipo katika siku zake za mwisho. Ninasema hivi kufa kwa Chadema kama dalili zinavyoonyesha sasa hivi sio the best Interest ya chama chetu CCM. Tunahitaji kuwasaidia sana waendelee kuwepo kwa sababu they have proven time and time kwamba ni paper tiger tu, wazuri kwenye makaratasi lakini hawana nguvu yoyote kisiasa. Kupitishwa kwa musawada wa Katiba mpya juzi bungeni ni mfano mzito sana ulio hai wa jinsi wasivyo na nguvu kabisa za kisasa za opposed na makelele yao ya kila siku na lile gazeti lao lenye makao makuu yake kwenye Club ya Disco ya Mwenyekiti wao. Ninawaomba sana CCM tunahitaji kuwa makini sana na matatizo ya chama hicho sasa hivi, tutumie nafasi hii kuwasaidia wasisambaratike maana Chadema ikisambaratika tutaanza kufukuzana na adui tusiyemjua,ni bora kushindana na huyu huyu adui tunayemjua, anayelia posho za wabunge ni kubwa na huku anazipokea, anayelia lia kwamba magari ya wabunge ni ya gharama sana na huku anayapokea hayo hayo. Anayelia lia safari za Rais huku wabunge wake wanasafiri kila siku nje kwa visingizo vya kamati za bunge. AGAIN KWA WANA-CCM WOTE NI KWAMBA TUNAWAHITAJI SANA CHADEMA HII INAYOONGOZWA NA AKILI NDOGO, MAANA OTHERWISE TUTAKUTANA NA WAPINZANI WENYE AKILI KUBWA WATATUSUMBUA, TUWASAIDIE WASISMBATRATIKE!! ha! ha! ha! KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!! source:http://www.udakuspecially.com/2013/11/wasi.html |
Arfi ambaye pia ni mbunge wa Mpanda mjini (CHADEMA) amefikia uamuzi huo leo baada ya Kamati Kuu ya CHADEMA kuwavua uongozi Zitto Kabwe na Dr. Kitila Mkumbo. Nafasi ya Zitto amepewa mchungaji Peter Msigwa Hapa Chini ni Barua aliyoandika ya kujiuzulu. Subject: KUJIUZULU MAKAMU MWENYEKITI (BARA) Salaam, Napenda kuwasilisha kwako taarifa ya kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara kuanzia Leo Ijumaa 22 Novemba 2013 kwa kuchoshwa na Unafiki unaoendelea ndani ya Chama. Napenda ifahamike pia kwangu maslahi ya Wapiga kura, Wakaazi na wananchi wa Mpanda Mjini na Wilaya ya Mpanda ni muhimu katika kuwatumikia, hivyo basi sipo tayari kuchaguliwa marafiki. Kwa kipindi kirefu zimekuwepo shutma dhidi yangu na kutiliwa mashaka mahusiano yangu na Mhe Pinda Waziri Mkuu pamoja na kulijadili katika vikao kadha Mpanda na Dar es Salaam bado yapo mashaka kwa nini alipita bila kupingwa hayo yalikua maamuzi ya Wanampanda kwenu imekua ni tatizo lakin hamsemi kwa nini Majimbo mengine 16 nchini yalipita bila kupingwa mlikua wapi na nani alaaumiwe huu ni Unafiki wa kupindukia. Aidha mmechukizwa sana kwa nini nilihoji kauli ya Muasisi wa Chama Mhe Mtei kutuchagulia viongozi naomba ifahamike wazi kwamba huu ni mtazamo wangu na utabakia hivyo siku zote kwa chama cha demokrasia kutoruhusu uongozi wa kiimla kwa kukidhi matakwa ya Waasisi ambao huvigeuza vyama kuwa Mali binafsi Kwa kusema ukweli na kusimamia ukweli daima itabakia kuwa lengo langu katika maisha yangu siku zote hata kama itanigharimu maisha yangu Nawasilisha. Said A Arfi (mb) Nakala Vyombo vya Habari source:jamii forum. |
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimemvua nyadhifa zote Naibu Katibu mkuu wake Zitto Kabwe ambae ni mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Mwanasheria mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu kwenye makao makuu ya chama hicho, amesema Zitto na wenzake watatu wamebainika kukihujumu chama kwa kuanzisha kitu kinaitwa Mkakati 2013 kinacholenga kukisambaratisha chama hicho ili kuwaondoa madarakani Mwenyekiti na Katibu mkuu wake. Nyadhifa alizovuliwa ni Unaibu katibu mkuu pamoja na Naibu kiongozi wa upinzani bungeni ambapo yeye, Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba na mwingine mmoja Makao makuu wamepewa siku kumi na nne wajieleze kimaandishi kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi za kinidhamu ikiwemo kuvuliwa Uanachama. Source:http://www.udakuspecially.com/2013/11/LISSU.html |
Folorunsho Alakija wa huko Nigeria ni mwanamke mwenye utajiri mkubwa wa kiasi cha dola Billioni 3.3.
kama ulizani Oprah ndie mwanamke mweusi tajiri pekeyake utakuwa umekosea dada huyu ni mmiliki na muanzilisha wa kampuni kubwa ya mafuta iitwayo Famfa Oil. Alianza kufanya kazi kwenye Bank ya International Merchant Bank of Nigeria, na baadae kwenda England kusomea mambo ya Fashion. Aliporudi Nigeria alianzisha kampuni ya Supreme Stitches ambayo ilizalisha nguo, ulipofika mwaka 1993 ndipo alipo anzisha kampuni ya mafuta. Credit:The ClickTZ |
Majambazi kumi wanaodaiwa kumuua Dr. Segondo Mvungi wamefikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu na kusomewa shitaka la kumuua Dr. Mvungi.
Kesi imesomwa na Hakimu Mkazi Sundi Fimbo ambapo Watuhumiwa hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na Mahakama kutokua na uwezo wa kusikiliza kesi ya mauaji hivyo wanarudishwa Segerea mpaka tarehe tano December kwa ajili ya kesi kutajwa.
Credit:Millardayo. |
Jana B’Hitz Music Group iliweka wazi uamuzi wa kuwaondoa kwenye label hiyo wasanii watatu ambao ni Vanessa Mdee, Mabeste na Gosby.
Japokuwa Vanessa na Mabeste walitangaza wiki hii kujitoa kwenye label hiyo, huku Gosby akiwa bado hajasema chochote, timu ya BHits imesema kuwa wasanii hao waliondolewa kwenye label hiyo miezi miwili iliyopita japokuwa hawaamua kutangaza.
Mabeste aliiambia Times fm kuwa ameamua kujiondoa katika label hiyo kwa kuwa muziki wake ulikuwa haumlipi na kwamba maisha aliyokuwa anaishi ndiyo yaliyopelekea yeye kudhaniwa kuwa anafanya show za nje, na kwamba amechoka kuwa mzigo kwao.
Tovuti ya Times fm ilimtafuta Amani Joachim ambaye ni mwana sheria na Chief Operations Officer wa B’Hits Music Group ili kufahamu kuhusu sababu alizozitoa Mabeste kwa upande wa B’Hits, na mikataba ikoje na kama watachukua hatua zozote za kisheria.
“Hiyo statement ambayo Mabeste ameamua kuisema kwangu mimi naona haiko sawa kabisa. Sisi ni ndugu na tulikuwa tunaishi hivyo, tatizo la mtu mmoja ni tatizo la mtu mwingine yaani tunakuwa pamoja kabisa. Na kuna vitu vingi ambavyo Mabeste anajua kwamba tunavifumbia macho. Hata hiyo mikataba, sisi na Mabeste kuna kipindi tume-deal hata bila mikataba na mambo yakawa safi tu kwa sababu kuna ile heshima na kuaminiana.” Amesema Amani.
Ameyaelezea pia madai ya Mabeste kuwa mabadiliko yake katika maisha ndiyo yaliyosababisha B’Hits kuhisi kwamba anapiga shows za nje.
“Mabeste inabidi aangalie statements zake, na muda ambao anaamua kutoa hizo kauli kwa sababu kati yetu sisi tuna siri nyingi sana (Mabeste na Upande wa B’Hits). Tusifike sehemu kwamba tukaanza kufaidisha kila mtu, hicho ndicho kitu ambacho ningependa kukiweka sawa. Hizo shows na vitu vingine ambavyo labda alikuwa anavifanya akiwa nje tunavifahamu vingi tu, lakini kutokana na ule u-brother na nini tunavichunia tu.” Ameeleza kiongozi huyo wa B Hits.
Hata hivyo Amani amekubaliana na kuwepo kwa ubovu wa soko la muziki ambapo amesema hata shows zikiwepo bado malipo yanayotolewa yako chini kiasi kwamba Kampuni haliwezi kuendeshwa kwa kutegemea kugawana kipato hicho na msanii.
Aliongelea pia madai ya Mabeste kuwa B’Hits haikuwa inamfanya atengeneze pesa kupitia muziki wake.
“Well, hopefully kule anakoenda atapata. Tunaelewa Mabeste ana majukumu, maisha yake tunajua kwamba yamebadilika kwa namna flani. Personally nafahamu, sijui akina Harmy na Pancho. That’s why I’m ready to stay quiet kwenye vitu kama hivyo, nilikuwa tayari kukaa kimya…sina haja ya kufunguka ni vitu vingapi ambavyo Mabeste ameshafanyiwa katika hali ya u-brother, I will not say them kwa sababu kipindi mimi navifanya nilivifanya katika good will na nilitaka iishie hivyo, Amani will never say them.”
Jana C.E.O B Hits Hermy B aliuambia mtandao wa Bongo5 kuwa Vanessa, Gosby na Mabeste hawana shukurani kwa kile ambacho B Hits imewafanyia na kutoa mfano kuwa alitoa shilingi million nane mfukoni kulipia video ya Closer ya Vanessa na kiasi kingine kulipia kazi alizofanya nje ya studio za B Hits, fedha ambazo hazijawahi kurudi.
Nae Amani Joachim alitoa ushauri kwa Vanessa, Mabeste na Gosby kwa ujumla kuwa wawe na amani na waendelee kufanya mambo yao na kuacha kutengeneza vita kati yao na B’Hits kupitia media kwa kuwa hata yeye ameamua kuyafumbia macho mengi.
Lakini vipi kuhusu hasara ambayo B’Hits itaipata kutokana na kuondoka kwa wasanii hao kwa kuwa walichukuliwa wakiwa hawana majina na wakati huu wanaondoka wakati wameanza kuwa productive.
Mwana sheria na Chief Operations Officer wa B’Hits anaeleza.
“They were real productive na naweza kukwambia kweli hawa watu wako very talented, na B’Hits haijawahi kum-house mtu ambaye ni mbovu, na ndo maana watu wanashangaa kwa nini mna nyumba kubwa ya media halafu mna watu watatu tu, sisi kuna kipindi tulikuwa na msanii mmoja tu Mabeste for like 4 years, ni kwa sababu tunaangalia talent.
“Na kusema kwamba sasa hivi tutakuwa hatujarudi nyuma utakuwa ni uongo, kuondoka kwao ndio tutarudi nyuma steps kadhaa, lakini pia kutokana kwamba plans tulizopanga kufanya wakati tukiwa nao zilikuwa hazijafika kuiva, we are ready to do that with someone else, Mungu hajagawa kipaji kwa watu wawili au watatu.”
Amesema anaamini baada ya Gosby, Vanessa, na Mabeste watakuja watu wengine ambao wana vipaji pia.
Kauli ambayo inaungana na ile ya Hermy B kuwa B’Hits itatangaza wasanii wapya wa label hiyo mwanzoni mwa mwaka ujao.
Tovuti ya Times fm ilitaka kufahamu kutoka kwa mwana sheria huyo kuhusu mkataba kati ya B’Hitz na wasanii hao na damages/athari za kuvunja mkataba huo zikoje na iwapo watawadai wasanii hao.
Amesema mikataba ilikuwa tight lakini kwa mazingira ya Tanzania na hali halisi ya kipato cha wasanii wa Tanzania hiyo mikataba inakuwa kama useless kwa kuwa kiasi kinachotakiwa kulipwa na msanii huyo ni kikubwa kuliko hali halisi ya maisha ya msanii husika.
“Ukimchukua bwana mti ukampeleka mahakamani, mahakama inaangalia damage ambayo imeingia katika kampuni, na mwisho wa siku inachukua maamuzi ambapo itakwambia bwana mti kama amepatikana na kosa amlipe bwana jose million 150 Kwa mfano, haimfungi. Problem ni kwamba bwana mti hana hata shilling 200 mfukoni mwake, we unadhani utamfanyaje bwana mti?” Alieleza kwa mfano.
“Kwa sababu mahakama ikishakupa judgement inakuacha ukatafute hiyo hela, haimfungi mtu. Kesi za madai sio kesi za jinai..sasa hapo imagine hapo ni wasanii wangapi leo unawafanyia kazi ya million 40 Million 50, ambayo ukiingia katika intellectual property court (mahakama ya maswala ya copy right), na copy right ni very expensive, tunaongelea six figures, eight figures. Sasa angalia ni wasanii wangapi hapa Tanzania wanaweza kukulipa eight figures.?” Amesema.
Kutokana na hali hiyo amesisitiza kuwa kuna haja ya kuwalipa wasanii pesa nyingi katika kazi zao huko wanakoenda kufanya ili wanapopata matatizo waweze kulipa, na kwamba bila hivyo mikataba ya label na wasanii Tanzania itakuwa useless.
Hii inamaanisha kuwa hakuna hatua zozote za kisheria ambazo B’hits itachukua kudai fidia kutoka kwa wasanii hao.
Hata hivyo uongozi wa B’Hits umesema utaachia nyimbo nyingine za wasanii hao zilizoko studio na kwamba zitachezwa redioni, lakini wasanii hao hawatakuwa na haki ya kuzitumia kwa kuwa ni mali halali ya kampuni hiyo.
Msikilize hapa Amani Joachim:
Credit:Times fm.
|
Vanessa Mdee, Gosby na Mabeste hawapo tena B’Hits Music Group. Kwa mujibu wa B’Hits Mabeste aliondolewa tangu miezi minne iliyopita japo
hawakutangaza rasmi na Mabeste alipewa muda wa kujitetea kutokana na kwenda kinyume na mkataba wake ikiwa ni pamoja na kufanya show bila kutoa taarifa kwa uongozi. Mabeste ambaye leo ametangaza kutokuwa chini ya label hiyo kupitia Facebook, amesema pamoja na label hiyo na kutengeneza hits nyingi, muziki wake haukuwa ukimpa kipato anachostahili na kusema kuwa tatizo lake na B’Hits ni katika kuufanya muziki wake uingize fedha zaidi pamoja na kuufanyia promotion. Amesema nyimbo zote alizowahi kutoa amekuwa akiachiwa yeye zaidi kuzifanyia promotion na kuzifikisha mahali kitu ambacho anaamini ilikuwa ni kazi ya label yake. “Sitaki kuonekana mzigo kwao. Haiwezekani kila siku wao wawe wanarekodi halafu wao hawaoni faida. Baada ya kutoona faida, wanarekodi nyimbo nyingine tena wananipa inaenda,” amesema Mabeste. Aliongeza kuwa anaumia kuona producer wake Pancho ambaye alimkutanisha na B’Hits miaka mitano iliyopita hapati faida ya muziki wake. Hata hivyo amekanusha madai ya kufanya show bila kutoa taarifa kwa uongozi na kudai kuwa katika dunia ya sasa si rahisi kufanya show kwa siri bila kujulikana. “Sasa mabadiliko ambayo yanatokea ndani ya haya maisha, wanahisi maybe mimi ninapata show siwaambii. Hivi hii Tanzania sasa hivi social networks ilivyotawala, kuna mahali unaweza kupiga show mtu asijue? Na nani atakuita show yake na aachie kuifanyia promotion kwa social network,” amehoji Mabeste. Mabeste amesema kutokana na maisha kubadilika na kwakuwa sasa amekuwa baba, kiasi alichokuwa anakipata akiwa B’Hits ni kidogo kuweza kukidhi mahitaji yake ya kila siku na hivyo kumfanya aishi na stress wakati ana uwezo mkubwa. Hata hivyo CEO wa B’Hits Music Group, Hermy B amesema anashangaa kumsikia Mabeste akilalamika hivyo wakati wao walimtoa mbali ambako alikuwa akiishi maisha ya chini na kuingia gharama nyingi za kumtunza ikiwa ni pamoja na kumlipia kodi ya nyumba, kumnunulia nguo pamoja na kumpa fedha ya kujikimu pale alipokuwa akihitaji. Hermy B amesema kama akiamua kujumlisha gharama alizotumia kwa Mabeste zinafika si chini ya shilingi milioni 30 na haoni kama Mabeste ana uwezo wa kuzirejesha. Ameongeza kuwa wote Mabeste, Gosby na Vanessa hawana shukrani kwa kile B’Hits imewafanyia. Ametoa mfano kuwa video ya Closer ya Vanessa Mdee aligharamikia fedha zake kutoka mfukoni ambazo ni takriban shilingi milioni 8 ambazo hazijawahi kurudi hadi sasa na pia alilipia kwa hela yake hata kazi alizofanya kwenye studio nje ya B’Hits. Naye Amani Joachim, ambaye ni mwanasheria na mmoja wa viongozi wa B’Hits, alisema Vanessa Mdee na Gosby waliondolewa B’Hits kutokana na kuingia mkataba wa kufanya show ya Fiesta Dar bila kuutaarifu uongozi. Amesema wawili hao walifikia hatua ya kwenda kufanya fujo B’Hits wakidai nyimbo zao kwaajili ya kutumbuiza kwenye show hiyo hali iliyokiuka masharti ya mkataba wao. Ameongeza kuwa ukimya wao umewafanya watu wengi waamini kuwa wasanii hao walijiondoa wenyewe wakati uongozi ndio ulifanya uamuzi wa kwanza wa kuwaondoa. Pamoja na hivyo, Hermy B amesema B’Hits itaziachia nyimbo zote za wasanii hao zichezwe redioni kwakuwa kuzifungia kutakuwa na hasara kwao kutokana na kutumia nguvu na akili nyingi kuziandaa. Hata hivyo amesema, wasanii hao hawatakuwa na haki ya kuzitumia popote kwakuwa ni mali halali ya kampuni. Hermy B amesema, uongozi wa B’Hits hauna ugomvi na wasanii hao na mwanzoni mwa mwaka ujao wanatarajia kutangaza wasanii wapya watakaokuwa chini ya label hiyo. |
Imebainika kwamba sababu ya shambulizi la risasi lililotokea Ilala Bungoni, Dar es Salaam Jumanne iliyopita na kusababisha vifo vya watu watatu, ni wivu wa mapenzi uliopindukia.
Akizungumza nyumbani kwao Ilala Bungoni jana, mmoja wa majeruhi ambaye ndiye aliyekuwa kiini cha shambulizi hilo, Christine Newa alisema si kweli kwamba sababu ya mchumba wake, Gabriel Munisi kuwashambulia na kuwajeruhi kwa risasi yeye na mama yake mzazi, Ellen Eliezer na kumuua mdogo wake wa kike, Alpha Newa ni kutokana na kusaliti uchumba wao. Awali, ilidaiwa kwamba sababu ya shambulizi hilo ni Christine kumkataa Munisi, (ambaye pia alijiua baada ya kufanya mauaji hayo) na kuchumbiwa na rubani wa ndege, marehemu Francis Shumila ambaye pia alifariki katika tukio hilo... “Kwanza Shumila hakuwa mchumba wangu kama ilivyoelezwa. Alikuwa shemeji yangu, mume wa dada yangu Caroline Newa. Pia hakuwa rubani wa ndege, bali nahodha wa meli.” Alisema amekuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Munisi katika kipindi kisichofikia mwaka mmoja lakini sehemu kubwa ya maisha yao ikitawaliwa na misuguano iliyowafikisha polisi mara kadhaa. Alisema katika kipindi cha uhusiano wao marehemu Munisi alikuwa akimpiga, akimkataza kufanya kazi, kusoma na alikuwa na wivu uliopindukia. Christine kuona hivyo, aliamua kufanya mipango ya kwenda kusoma katika Visiwa vya Cyprus kimyakimya pasi na kumuaga, jambo ambalo alisema lilimkera mchumba wake huyo na kuweka kisasi. “Nikiwa huko, Munisi alitafuta mawasiliano hadi akayapata na tukawasiliana na siku niliporejea alikuja kunipokea uwanja wa ndege lakini cha ajabu, alinikataza kwenda nyumbani na badala yake akanipeleka moja kwa moja hadi Mwanza eneo la Kitangiri,” alisema na kuongeza: “Tukiwa njiani kuelekea Mwanza, katika maeneo ya Singida, alisimamisha gari akaniambia nishuke, akatoa bastola na kuniuliza kwa nini niliondoka bila ya kumuaga. Je, nataka kumuacha?” Alisema alimwomba msamaha na kuendelea na safari yao. Anasimulia kwamba baada ya kufika Mwanza, alimpora simu zake zote na kumfungia ndani kwa zaidi ya wiki mbili hadi alipopanda kwenye dirisha na kuomba msaada kwa majirani na kuwapa namba za simu za ndugu zake ili wamsaidie kuwapa taarifa. Ndugu zake walianza mchakato wa kuwasiliana na polisi hatua iliyofanikisha msichana huyo kurudishwa Dar es Salaam... “Hata hivyo niliondoka na khanga na fulana tu. Vitu vyote niliviacha huko.” |
NAPENDA KUTOA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWA HAWA WAFUATAO 1.MAMA VERONIKA NDUNGURU 2.BABA LAURENT NSUHA WADOGO ZANGU 1.MONICA ROSES NSUHA 2.PHILIPO NERY NSUHA 3.DORAH NSUHA 4.BERTHA NSUHA 5.DOMMY NSUHA BILA KUWASHAU WATU WANGU WA KARIBU YAFUATAO: 1.DENIS MPAGAZE 2.ALLEN MOSHI 3.NESTRO NJAWIKE 4.ATHANAS SING'AMBI
Friday, 22 November 2013
Ismail Aden Rage amerudi bongo, kuna sentensi yake juu ya kuvuliwa Uwenyekiti wa Simba
Subscribe to:
Posts (Atom)