advert

http://

Saturday, 26 October 2013

Ney Wa Mitego Aswekwa Sero Baada Kuvaa Sare Za Polisi.



 
Rapper Ney Wa Mitego ameniambia kuwa hii picha hapo juu tukio hilo limetokea Jana wakati wana shoot video ya wimbo wake Unaofanya vizuri kwa sasa kwenye radio stations ' Salam Zao'.


Ney Wa Mitego Amesema ' Nikweli nilitupwa sero jana baada ya raia wasio julikana kuleta fujo eneo la kazi yangu  kwasababu kulikuwa na waigizaji waliokuwa na sare za polisi. Watu hao sijuani nao na walijitambulisha kama askari na kutaka kujua kwanini natumia sare za polisi kwenye video yangu bila kibali. hicho ndio kitu kilichopelekea nikapelekwa polisi.

Mitego ameendela kusema kuwa baada ya kuka sero kwa dakika kama 15 mkuu wa kituo alikuja na kusikiliza tatizo hilo na ndio aliachiwa huru baada ya kutoa maelezo kuhusu tukio hilo na sare hizo kuonekana uraiani.

Ney aliwekwa sero Kwenye kituo cha polisi Urafiki kilichopo Manzese na wiki ijayo video hii itaonekana kwenye vituo vya televison Tanzania.

Source:sammisago.

Utafiti uliofanywa na mtandao wa kupambana na ulevi nchini Tanzania—TAANET umebaini kuwa idadi kubwa ya wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo nchini Tanzania wamekuwa wakijihusisha na ulevi.
 


Katibu uenezi wa mtandao huo Bw. Mathias Kimiro amesema hayo katika mahojiano na East Africa Radio jijini Dar es Salaam leo ambapo amewataka vijana kuacha kunywa pombe kutokana na kinywaji hicho kuwa na madhara makubwa kiafya.


Kwa mujibu wa Kimiro, upatikanaji wa pombe tena ikiwa kwenye vifungashio vinavyobebeka kiurahisi maarufu kama viroba imetajwa kuwa moja ya sababu zinazochangia vitendo vya ulevi kwa vijana hususani wanafunzi.

Siku za Hivi karibuni kumekuwa na tetesi zisizo rasmi kuwa mastaa wawili wa filamu Swahiliwood Yobnesh Yusuph(Batuli) na Irene Uwoya hawana maelewano
mazuri chanzo kikidaiwa ni Irene Uwoya kutaka kumpoteza Batuli kwenye tasnia ya filamu ili asifurukute. Habari hizo zinaenda mbali zaidi zikidai kuwa kuna kipindi Batuli alikuwa anaumwa maeneo ya kifuani lakini baadhi ya watu wakiwemo wasanii wenzake wakiamini Uwoya ndiye kamfanyia mambo ya kilozi(ushirikina). 

 Tetesi hizo tulizipuuza mwanzoni lakini zinaonekana kurudi tena kwa kasi hivyo tuliamua kuwatafuta mastaa hao wawili ili watoe ufafanuzi wao wenyewe na wa kwanza kuulizwa alikuwa Uwoya hata hivyo namba yake ilionekana kutokuwa hewani alipotafutwa juzi na jana alipotumiwa ujumbe namba yake ilionekana bado haipo hewani. Batuli nae alitumiwa ujumbe juzi kuhusu issue hiyo lakini hakujibu mpaka jana usiku ndiyo alijibu akisema alikuwa busy sana. Batuli alisema "sina ubaya na msanii yeyote na moyo wangu ni mweupe na nina mapenzi na wasanii wenzangu wote, nawapenda sana anayeniwinda kwa ubaya Mungu atanipa ulinzi wake, sipendi uadui na mtu namuachia Mungu atanilipia yote"

SOLO THANG a.k.a TRAVELLAH



Ni nadra sana kwa  staa  wa Tanzania kukubali kusema kiwango anachopata kwa mwezi kutokana na kazi yake ya umaarufu ila kwa Mzee Majuto hali imekuwa ni kinyume...


Akiongea  na  Millard Ayo, mzee Majuto amekubali kusema kila kitu kwenye kipato cha movie zake za vichekesho ambazo mpaka sasa ndio zinashika nafasi ya 1 kwa mauzo Tanzania.

Akiwa ni baba wa watoto tisa, mzee Majuto  amefunguka  kuwa   kwenye movie za kuigiza sasa hivi kama mtu akitaka kumshirikisha ni lazima amlipe milioni nane kutoka milioni 2 au tatu alizokuwa anazikusanya mwanzoni....

Bei  hiyo  ameibadili kuanzia mwezi September 2013  kwa sababu  kadri anavyocheza movie nyingi za kushirikishwa ndivyo anavyozidi kujipunguzia kipato chake  kwa mwezi kutoka kampuni ya STEPS iliyomwajiri’.

"Mpaka sasa nimecheza movie zaidi ya 600 toka nimeanza kuigiza  ( za kushirikishwa na zake mwenyewe) ...


"Nilianza kulipwa zaidi ya milioni moja kwenye movie toka mwaka 2007/2008 baada ya kuwa na kampuni ya Ally Riyami ambayo  ilikuwa inanilipa shilingi laki sita kwa kila movie ya Comedy kwa hiyo kwa mwezi nilikuwa napata mpaka  milioni 6 au saba kutokana na idadi ya movie nitakazoigiza’ – Mzee Majuto

"Kwa sasa hapa Steps nalipwa kuanzia milioni 17 mpaka 20 kwa mwezi, ni malipo mazuri sana ambayo napata kila mwezi na nimepangiwa kucheza movie 9 kwa mwaka lakini kule Ally Riyami kwa mwezi ndio nilikua nacheza hizo movie 10, yani unacheza movie mpaka unasikia kizunguzungu…. 

"Nilitakiwa kucheza movie 1 kila baada ya siku tatu ila kwa sasa kwenye mkataba wa Steps nacheza movie moja ya kampuni na moja ya nje ya kampuni, maisha mazuri’ 

Rapper Rick Ross ametoa maelezo kuhusu wimbo utakao changia mauzo ya album yake kuwa ni wimbo na rapper Jay z unaotoka mwezi ujao.

Rozay amesema December 17 album yake ya sita 'Mastermind' inatoka na baada ya cd kuingia mtaani atatoa wimbo uliopewa shavu kubwa na rapper Jay z . Fahamu kuwa Rozay ambaye ni mwanzilishi wa record lebel ya Maybach Music Group anategemea wimbo huo kubeba na kutangaza zaidi cd yake.

Hii sio mara ya kwanza Rozay anasikika kwenye wimbo moja na Jay z, Kwenye cd mpya ya Jay z 'Magna Carta Holy Grail'  Rick Ross ameshirikishwa kwenye wimbo moja unaoitwa  "FuckWithMeYouKnowIGotIt."  na kwenye cd ya Rick Ross  'God Forgives, I Don’t' Jay z alisikika kwenye '3 Kings' iliyomshirikisha producer  Dr Dre. Rozay hajasema wimbo na Jay z unaitwaje mpaka sasa.

 Beyonce atatoa Calendar ya mwaka 2014 itakayo kuwa na picha kibao kila mwezi, Hizi picha amezitoa za awali kwenye photo shoot ya Calendar hio.




LULU alikuwa kati ya wasanii waliofika kushiriki katika harambee ya kansa ya wanawake iliyoendeshwa na taasisi ya kuzuia kansa nchini ambapo baada ya zoezi hilo, waalikwa walijongea eneo la maakuli.


Huku akionekana mwenye ‘ubao’, Lulu alikwenda kwenye foleni na kuchukua pleti ya kwanza,akaifuta kisha akanyanyuka na kwenda kuchukua nyingine, nayo akaimaliza, baada ya muda akaenda kuchukua nyingine ambapo haikufahamika kama nayo aliifuta au alisaidiwa na mtu.


Akilizungumzia tukio hilo, Lulu alisema kuwa“Nakula sana na hii ni kawaida yangu, najua watasema lakini kwenye msosi huwa sikai nyuma.”