advert

http://

Saturday, 7 December 2013

Picha 19 za Nelson Mandela akiwa na watu mbalimbali maarufu duniani.



nelson-david-beckham--z
Nelson Mandela kutokana na historia yake ya harakati za kutokomeza ubaguzi wa rangi Afrika Kusini alivutia watu wengi sana hata wale maarufu wa dunia ambao walifanya juu chini kumtembelea Mzee Mandela ambapo hizi ni baadhi ya picha zenyewe.

-9b362eff4ab20164Evander Holyfield
50 cent50 Cent
0022190dec450bb3bc9929Michael Jackson
d57bec3fNaomi Campbell
img4217-gmannelson_full  Will Smithmandela diddyP. Diddy
mandela na iverpoolLiverpool F.C
mandela-clinton-1
Bill Clinton
mandela-with-celebs-featured-obamaMichelle Obama
mjMichael Jackson
morganMorgan Freeman
Nelson Mandela's Death- Celebrities-ReactMike Tyson
nelson_mandela_meets_bill_gatesBill Gates
pelePele
pg_nelson_mandela_whitney_houston_1994_MasterWhitney Huston
ronaldo--zCristiano Ronaldo
showbiz_nelson_mandela_celebs_gallery_2Beyonce
showbiz_nelson_mandela_celebs_gallery_10Michael Jackson

fifa 1June – July 2014 ndio fainali za kombe la dunia huko Brazil ambapo makundi yameshapangwa tayari, cheki mzigo wenyewe ulivyopangwa…

Group 1group 2group 3group 4group 5group 6group 7group 8


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa amepokewa kwa mabango katika mkutano wake wa hadhara 
wilayani Kakonko, Kigoma lakini akawaambia waliofanya hivyo kuwa chama chake hakitayumbishwa huku akiwataka wanaosimama na mabango kumtetea Zitto Kabwe kung’oka naye ndani ya chama. 
Dk Slaa yuko mkoani Kigoma ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 11 kutembelea Mikoa ya Shinyanga na Kigoma kukagua na kuimarisha uhai wa chama.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwenge Kakonko, Dk Slaa alisema Chadema ni chama imara na kinaendeshwa kwa misingi ya katiba na kanuni.
“Hakuna kiongozi aliye juu ya katiba, ninawaasa wote wanaobeba mabango kujiangalia kwa kuwa ninafahamu wanatumiwa.”

Kabla ya kupokewa kwa mabango hayo, Dk Slaa aliyewasili Kakonko saa 5:11 asubuhi akitokea Wilaya ya Kahama, Shinyanga alikwenda moja kwa moja katika Kata ya Mhange ambako alifanya mkutano wa hadhara.
Dk Slaa alikumbana na mabango hayo saa 8:45 mchana msafara wake ulipowasili Kakonko Mjini ukitokea Mhange.
Wakati Dk Slaa akiingia katika uwanja wa mkutano, ulio jirani na Ofisi za CCM Wilaya ya Kakonko, kuliibuka kundi la vijana wapatao watano wakiwa na mabango mkononi na kuanza kukimbia kuyafuata magari matatu ya msafara wa Dk Slaa huku wakionyesha mabango yao. Hatua hiyo iliwafanya polisi waliokuwapo eneo hilo la mkutano kuwazuia na kuanza kuwatimua lakini mara baada ya Dk Slaa kuteremka katika gari yake na kuingia uwanjani hapo, aliomba kipaza sauti na kuwataka askari hao kuacha kuwatimua wenye mabango. “Naomba msiwaondoe waacheni waje... waruhusuni kwenye mkutano na mabango yao. Waacheni waje hapa … msiwazuie, waacheni waonyeshe mabango yao na muwaruhusu tu wapite hapa mbele, msiwapige tafadhali,” alisema Dk Slaa.
Baada ya kauli hiyo, polisi waliwaruhusu vijana hao watano ambao walibakiwa na mabango manne, moja likiwa limechanika walipokuwa wanawazuia.
Mabango hayo yaliyokuwa na maandishi ya aina moja, yalikuwa na ujumbe uliosomeka: “Tanzania Kigoma Kakonko bila Zitto Haiwezekani”, ‘Mhe. Slaa, Mhe. Mbowe mnatakiwa kujiuzuru mara moja” na jingine lilisomeka; “Hatupo tayari kwa kusikiliza lolote bila ya Zitto”.
Mara baada ya kupanda jukwaani Dk Slaa aliwataka tena wenye mabango kusogea karibu na jukwaa kuu alipokuwa amesimama na kuanza kuwauliza maswali vijana hao iwapo wanajua Katiba ya Chadema na kama wana kadi za chama. “Naomba niwaulize, hivi nyie wenye mabango mnaijua Katiba ya Chadema?” Walimjibu: “Hapana.” Dk Slaa akawauliza tena: “Sasa mnadai nini kwa mabango yenu kama hamjui Katiba ya Chadema?”
Mmoja wa walioshika mabango hayo alijibu: “Mtetezi wetu Zitto.”
Kutokana na hali hiyo Dk Slaa aliwauliza, atakuwa amekosea akiwakabidhi kwa Polisi kuwa siyo wanachama wa Chadema lakini wanafanya vurugu katika mkutano halali?

Credit: Mwananchi.

Kama nilivyo elezea kwenye kichwa cha habari hapo juu,siku hizi watu wengi wamekuwa na mtindo wa kuajiri wasichana wa kazi (mahouse girl) ili kusaidia kazi za nyumbani.

Ndio hatukatai pengine mama mwenye nyumba anaweza kuwa anazidiwa na kazi,
Kama kufua nguo za mzee,watoto,kunyoosha, kuandaa chakula nk.
Lakini kuna wadada/wanawake wengine unakuta watu wako wawili yeye na mumewe,
eti nao wanaweka house girl sijui wa nini?eeh!!!
tena wengine sijui ni sifa eti anaajiri wawili kabisa kwa kazi zipi sasa?na wewe ufanye kazi gani?
Ya kupaka rangi kucha na kuchat kwenye mitandao? halafu bila aibu unasifia chakula alichoandaa house girl mbele ya mumeo.


Na unaangalia tu house girl anamnawisha mikono mumeo na kumkausha na taulo,wewe upo tu kwenye kiti kama umegundishwa na super glue vile.
huyo jamaa yako akila chakula kitamu cha house girl, si atataka ale na kile cha usiku aone utam wake?
hapo ndipo timing zinapoanzia na ukizingatia mahouse girl walivyo na heshima,
baba akifika na kamzigo anapokelewa kwa mikono miwili na anapigiwa goti,
wakati huo we upo upo tu kama koti la mvua linasubiri masika.
Sijui ndio kusema hamuelewi mko pale kwa ajiri gani?na house girl akiboronga kidogo tu macho na sauti ya ukali inakutoka kama nini,
Hujui kwamba unapofanya hivyo unamkomaza house girl,hapo kwako ni sawa na chuoni kwake anachukua mafunzo ya maisha.
Mumeo akisifiwa kazini nguo zake zinang'aa atamkumbuka house girl,
akisifiwa kwamba ananawili atamkumbuka house girl,
akisifiwa kwamba viatu vyake vinang'aa atamkumbuka house girl,
Ndio si house girl ndio anaye fanikisha yote hayo?wakati wewe uko bizy ku up load picha fb?
mwisho wa siku unatemwa kama big G iliyo chacha,
halafu watu wanabaki kushangaa mbona jamaa kamuacha mwanamke mzuri vile halafu kabeba house girl?
kumbe ni janga la kitaifa hajui A wala B kifupi hajitambui,
Badilikeni nyie kina Eva ma house girl watawapiga bao ohooo!!!!!! 

Leo ni siku ya kuzaliwa kwa miongoni mwa wasanii wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu hapa nchini Jacklyn Wolper.


Kupitia kwenye instagram Desemba 6 amepost picha ambayo ikionesha amenusurika kuumia baada ya kuondoa gari  lake kwa kasi na kupelekea kugonga tanki la maji na kusababishaa ajali.



Huu ndio ujumbe wake 'dah kuzaliwa cku moja na kufa ni cku moja nando maana kila cku nasisitiza upendo na chuki zisizokua na sababu.hvii leo ni bthday yangu lakn nilikua nauvaa ukuta wakat nasogeza gar ioshwe tayar kwa maandaliz .wakat nakanyaga brk kumbe nakanyaga mafuta maskn ya mungu nimebomoa matnk ya maji yote nimepasua mabomba yote nimegonga gar nyingne but yote nikumshukuru mungu kwakua sijaumia ila prsh ilishuka kidogo but now npo ok.asante mwenyezi mungu,mungu wa wote,kimbilio la wote na wewe ndo kimbilio langu.niombeeni maskn'Aliandika Wolper .

Jarida la Rolling Stone limataja album kubwa na bora za mwaka 2013 baada ya uchunguzi kufanyika kupitia mauzo bora, mapokezi ya album sokoni na mitaani, Ilivyozungumziwa na kutajwa zaidi kwenye mitandao na ubora wa muziki wake.

Album ya  Kanye West "Yeezus" imekuwa namba mbili kwenye orodha hio ya album hizo na Drake "Nothing Was The Same", Danny Brown "Old" zikifata kwenye top 20 ya Album bora za mwaka 2013.


Drake na cd yake ya Nothing Was The Same ipo namba 14 na Danny Brown 'Old' Ipo namba 17
 
Album ya Eminem The Marshall Mathers LP2 Imedondokea namba 24 huku album ya Chance The Rapper 'Acid Rap ikiwa namba 26.

Miley Cyrus na Bangerz amechukua namba 27 kwenye orodha bora ya album za mwaka 2013. 
Msanii wa Good Music na album yake ya My Name Is My Name 'Push T' imechukua namba 33 Huku J Cole na Born Sinner akiwa namba 41. Msanii M.I.A Amebana kwenye nafasi ya 47 na Matangi.

Ili kuonyesha uelewa na jinsi wanavyo thamini mchango wa wanawake kwenye maisha yao wanaume hawa wamekubali kuvaa viatu vya kike aina ya High Hill [Skuna] ilikuonyesha wako tayari kupitia

tabu na matatizo wanaopitia wanawake duniani na wanakubali sana mchango wao kwenye jamii. Wewe upo tayari kupiga picha na viatu hivi sasa? 
 


Video:  Filamu 6 zilizowahi kuigiza maisha ya Nelson Mandela
Watengezaji wa filamu wamekuwa wakivutiwa na maisha na historia ya Nelson Mandela katika kupambana na ubaguzi wa rangi kabla hajatoka jela mwaka 1990.
Na baada ya kuwa Rais wa Afrika Kusini historia yake ikawa ya kuvutia zaidi.
Alhamis, kiongozi huyo anayependwa duniani alifariki dunia na kuiacha dunia ikivutiwa na vitendo vyake vya kusamehe na umoja.
Kumuigiza Mandela si kazi rahisi kwa waigizaji. Hata hivyo hizi ni filamu 6 zilizoigiza maisha yake.
Idris Elba kwenye  Mandela: Long Walk to Freedom.

Idris Elba amepata sifa za mapema kwa kuigiza filamu ya Mandela: Long Walk to Freedom. Ili kufanya utafiti zaidi kwenye uhusika huo, Elba aliliambia shirika la Associated Press kuwa alikutana na mke wa pili wa Mandela, Winnie, aliyemuambia kuwa alihitaji kuona mwanaume mkakamavu kwenye screen

"Kila mmoja anajua Mandela alivyo na anavyoongea na mimi siko hivyo hata kidogo. Ilikuwa ni changamoto kubwa, lakini ilikuwa ni muda wa kukua na kujitahidi.”

Morgan Freeman kwenye Invictus

Morgan Freeman alitajwa kuwania tuzo za Oscar kwa kumuigiza Nelson Mandela kwenye filamu ya mwaka 2009, Invictus.  Alikuja kuiambia CNN kuwa kitu kigumu zaidi ilikuwa ni kuiangalia filamu hiyo ilipokamilika akiwa na Mandela mwenyewe.

"Nilikuwa nimekaa naye. Alionesha kidole kwenye screen na kusema 'Namjua jamaa huyo.' So, yeah, nadhani aliipenda."

Terrence Howard kwenye Winnie Mandela.

Terrence Howard alimuigiza Mandela akiwa na Jennifer Hudson kwenye filamu ya historia mke wa pili wa Mandela,  Winnie Mandela.

Bahati mbaya, Winnie Mandela na viongozi wengi wa Afrika Kusini hawakuifurahia filamu hiyo kwakuwa hawakuombwa ushauri..

Dennis Haysbert kwenye Goodbye Bafana

Sidney Poitier kwenye  Mandela and de Kler

Danny Glover kwenye Mandela.

Chukua Hiyo: Justin Bieber aliwaomba Blackberry awe balozi wao mwaka 2007 wakakataa, sasa hivi wanajutaKama mwenyekiti mtendaji wa record label aliyewakataa Beatles, kulikuwepo na mkuu wa masoko aliyekuwa akifanya kazi na RIM (sasa hivi BlackBerry) aliyeichezea siku aliyosikia jina "Justin Bieber".
Kwa mujibu wa jarida  Bloomberg BusinessWeek, Bieber aliifuata kampuni hiyo mwaka 2007 (kipindi ambacho hakuwa maarufu) na kuwaomba awe balozi wao (brand ambassador).
Aliyekuwa Meneja Mkuu wa maendeleo ya biashara wa RIM alisimulia:
“Kitu kimoja tulichokikosa kilikuwa kwamba Justin Bieber alitaka kuwa mwakilishi wa BlackBerry. Alisema:  Nipeni $200,000 na simu 20 na ntakuwa balozi wenu. Tuliwapelekea wazo watu wa masoko na kuwaambia:  Huyu ni mtoto wa Canada, alikulia hapa, watoto watapenda.  
Walitufukuza na kusema ‘huyu mtoto ni wa muda. Hawezi kufika popote. Na mimi kwenye mkutano niliwaambia ‘huyu mtoto atadumu zaidi ya RIM.” Kila mmoja alicheka.
Of course, mwaka 2013 RIM walibadili jina na kuwa BlackBerry. Bieber … bado anaitwa Bieber.
Kipindi hicho kampuni ilikuwa hata haifanyi matangazo kwakuwa umaarufu wake kwenye biashara uliwapa kiburi kuwa watu wangenunua tu simu. Mambo yalianza kuwa magumu kwa Blackberry baada ya simu iPhone na zinazotumia mfumo wa Android kushika kasi.
Mwaka huu pekee, kampuni ya Blackberry imepoteza dola bilioni 1 kwa miezi mitatu pekee.  Kwa miaka mitano iliyopita, thamani ya kampuni hiyo imeshuka kwa asilimia 85 hadi kufikia dola bilioni 4  kutoka dola bilioni 80 mwaka 2008.
Mwaka 2013, kampuni ya Fairfax ilitoa ofa ya kuinunua BlackBerry kwa dola bilioni 4.7. Mwezi  September, kampuni ilitangaza kuwaachisha kazi wafanyakazi 4,500.
Wakati huo huo, Justin Bieber ameendelea kupeta. Kwa sasa ana utajiri wa $130million,na amekamata nafasi ya 9 ya Forbes ya mastaa wenye ushawishi zaidi duniani.
Pole yao Blackberry.

Nelson Mandela atakumbukwa kwa Juhudi zake katika kuleta Ukombozi Barani Afrika na bado anabaki kama Alama ya Ushindi kwa Bara hilo huku Akiwaachia Simanzi kubwa Wakazi wa Nchi Hiyo ambao Mpaka sasa wanaonesha kutoamiani kilichotokea.



HISTORIA FUPI YA MANDELA.
Nelson Rolihlahla Mandela ni Rais wa kwanza Mwafrika wa Afrika Kusini ya kidemokrasia. Ni mtu aliyejijengea heshima kubwa duniani kutokana na jitihada zake kubwa zilizofanikisha uhuru wa nchi hiyo na nyinginezo katika Bara la Afrika.

Mzee Mandela anayefahamika pia kwa jina la Mzee Madiba amelazwa hospitalini mjini Pretoria, Afrika Kusini kwa zaidi ya mwezi sasa akiwa mahututi. Anasumbuliwa na ugonjwa wa mapafu.



Kutokana na umaarufu wa Rais huyo mstaafu wa Afrika Kusini mwenye umri wa miaka 95, JAMHURI tumeona vema kuchapisha historia fupi ya maisha yake kama ifuatavyo:


Nelson Mandela ni mwanasiasa mkongwe na mwanaharakati aliyepambana na sera za ubaguzi za makaburu wa Afrika Kusini na hatimaye kuwa Rais wa kwanza Mwafrika nchini humo. Ni mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel. Pia amepata kutunukiwa zaidi ya tuzo 250 katika miongo minne iliyopita.


Ni rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia nchini Afrika Kusini. Alikuwa mwanasheria na mwanachama wa Chama cha African National Congress (ANC) aliyepinga utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini.
Nelson Mandela alizaliwa Julai 18, 1918. Baba yake mzazi alifariki wakati Mandela akiwa na umri wa miaka tisa. Tangu kipindi hicho alilelewa na Jonintaba hadi alipoitoroka familia hiyo baada ya kutakiwa aoe mwanamke aliyepangiwa.


Mwaka 1943 Mandela alijiunga ANC. Aliiongoza Afrika ya Kusini dhidi ya ubaguzi wa rangi na kuibuka kiongozi shujaa duniani.

Alipoanza mapambano ya kupinga utawala wa ubaguzi wa rangi na kutafuta usawa kwa wote, ilitegemewa kuwa mke wake ndiye angekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.


Mandela alipata kuoa wake watatu katika historia ya maisha yake. Alimuoa mke wa mwisho siku alipokuwa akiadhimisha miaka 80 ya kuzaliwa kwake.


Madiba anatajwa kuwa katika kipindi chote cha historia yake amekuwa akiwaunga mkono watoto na upatikanaji wa elimu. Mfuko wa Nelson Mandela wa kusaidia watoto ni sehemu tu ya ushahidi wa mafanikio ya Mandela kuwasaidia watoto.


Mandela ni baba wa watoto sita. Watoto wanne aliwazaa na mke wake wa kwanza, Evelyn Mase na watoto wawili aliwazaa na mke wake wa pili, Winnie Madikizela.



Inaelezwa kuwa baadhi ya watoto wake hawakupata kwenda kumwona Madela alipokuwa gerezani.


Watoto wake wote wawili wa kike aliowazaa na mke wa kwanza walikuwa wakitumia jina la Makazawie.

Mtoto wake wa kwanza alifariki akiwa na umri wa miezi tisa na mtoto wa pili aliyejulikana kwa jina la Madiba Thembikile (Thembi) alifariki katika ajali ya gari mwaka 1969 akiwa na umri wa miaka 25. Mandela alikuwa gerezani na hakuruhusiwa kwenda kuhudhuria mazishi ya mwanay