advert

http://

Saturday, 12 October 2013

DIWANI WA CHADEMA ATUHUMIWA WIZI WA MILIONI 10 ZA KITANZANIA MKOANI KILIMANJARO.




WATU tisa akiwemo Diwani wa Kata ya Old Moshi Magharibi, Elisaria Mosha (Chadema) wametiwa mbaroni wakituhumiwa kupokea fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia mradi wa umeme mkoani Kilimanjaro.


Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal, kufanya ziara mkoani Kilimanjaro na kuagiza watu waliofanya hivyo wakamatwe mara moja.

AKIZUNGUMZA na waandishi wa habari jana ofisini kwake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema diwani huyo anatuhumiwa kujipatia Sh milioni 9.6 kwa njia ya udanganyifu. 

Wengine wanaoshikiliwa ni Zakayo Kimathi (52) mkazi wa Mandaka, anayedaiwa kupokea Sh milioni 10.3, Oforo Kimambo (56) mkazi wa Mandaka anayedaiwa kupokea Sh milioni 29. 

Wengine wanaotuhumiwa kupokea malipo hayo kwa njia ya udanganyifu ni Daud Mallya (69) mkazi wa Chekereni aliyepokea Sh milioni 8.6, Richard Mlaki (69) mkazi wa Kiboroloni alipokea Sh milioni 18.6 na Focus Herman (88) mkazi wa Kilototoni aliyepokea Sh milioni 36. 

Boaz alisema kwa sasa watuhumiwa watatu hawajapatikana. Alieleza kuwa pamoja na watuhumiwa hao, polisi imemkamata Mwenyekiti wa Kijiji cha Mandaka Monono, Hassan Nduva (41) na Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Vendelini Shayo (58) kwa kuhusika kufanikisha malipo hayo. 

Dk Bilal alitoa agizo hilo mapema wiki hii wakati akizindua vituo vya kupozea na kusambaza umeme maeneo ya Kiyungi, YMCA na Makuyuni. 


Alipokea taarifa kwa Mkuu wa Mkoa kuwapo kwa wananchi ambao hawakulipwa fidia zao, kutokana na kuwapo watu waliotumia ujanja wa kupokea fedha hizo, Sh milioni 169.2. 

“Halmashauri ya Moshi Vijijini ndio ilikuwa wakala wa malipo hayo na ndio iliyofanya tathmini kwa kushirikiana na watendaji wa vijiji, ambapo wao walipeleka tathmini hiyo kwa Shirika la Umeme (Tanesco), ambalo lilitoa fedha hizo hivyo Tanesco hawahusiki,” alisema,” alisema Boaz. 

  Habari leo.

One week after the first episode of
the talent search show Tusker
Project Fame Season 6 went on air
from the academy in Nairobi, there
have been twists and turns in
events.

The Beat has reliably learnt that
organisers at the academy have
dropped Tanzanian judge, musician
Zahir Ali Zorro from the panel of
judges.

Details of the fallout are still sketchy
but word from Zahir Zorro’s camp
has it that it was an amicable
understanding between both
parties.

Speaking to The Beat , the veteran
musician said he had chosen to leave
the show in order to concentrate on
his personal musical engagements
back at home.

“After the show in Nairobi last week
it dawned on me that the responsibility was heavy and I
couldn’t handle both the academy
duties and my other engagements at
home satisfactorily,” he said.

Zahir Zorro’s appointment to the
judges’ panel was greeted with
cheers of hope as many thought he
would take the contest to a different
level after replacing producer
Hermes Bariki.

He was to work with Juliana
Kanyomozi who filled the Ugandan
spot and as agreed, controversial Ian
Mbugua filled the Kenyan spot.
But as the posts on the TPF website
announced that the vastly experienced musician had joined the
panel, discord was brewing.
Though there has not been any
official communication from
Endermol and East Africa Breweries,
sources privy to the academy cite his
laid back display at the inauguration
as the potential cause.

In his trademark bling-bling and
suit, Zorro barely said anything
during the blockbuster show that
ushered in 25 contestants. “He was a
bit uncomfortable with the
surroundings and looked not at ease
with the other judges who were
enjoying themselves throughout the
show,” said the source.

But in an interview with The Beat,
Zorro cited generation gap as the
reason for his mysterious exit from
the regional show. In hi own words:
“They will have to appoint a more
youthful person to take over from
me.”

This leaves some unanswered
questions whether it was the age
gap that left the singer in the cold.


Source:The Beat pull-out magazine,of The Citizen Newspaper,Tanzania

Binti wa Darasa la sita katika Shule ya Msingi Kilimani iliyopo Kipunguni, Dar mwenye umri wa miaka 12 (jina tunalihifadhi kwa sababu za kimaadili) amejikuta akishindwa kuendelea na masomo baada ya kupewa ujauzito na kijana wa mtaani aliyejulikana kwa jina moja la Roja.


Akizungumza kwa huzuni mama wa mtoto huyo, Aziza Mohammed alisema kuwa mwishoni mwa mwezi uliopita ndiyo aligundua kuwa binti yake huyo ni mjamzito na ilikuwa ni baada ya kukataa kwenda shule huku akitapika mara kwa mara.
Mama huyo alisema, baada ya kuona ilibainika kuwa ana mimba, wakanipa taarifalili hizo  aliamua kwenda kununua kifaa cha kupimia mimba lakini mwanaye huyo alikimbilia kwa mama yake mdogo, Temeke ambako waligundua kuwa ni mjamzito.
 “Alipofika kwa mama yake mdogo, nikawaomba wamlete kisha tukampeleka hospitali ambako tulithibitishiwa na daktari kuwa kweli ana ujauzito wa miezi mitano,” alisema mama huyo na kuongeza:
“Nilimbana aniambie mwenye mzigo huo ambapo alimtaja kijana aitwaye Roja. Akaniambia kijana huyo ambaye ni jirani yetu amekuwa akimbaka na kumtishia kumuua ikiwa atasema.
“Kwa maelezo hayo ilibidi tumtaarifu mjumbe wa mtaa wa Kipunguni B, Bakari Issa ambaye tulikwenda naye kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Stakishari na kufungua jalada la kesi lenye namba STK/RB/18639/2013 KUMPA
 MWANAFUNZI MIMBA
“Jamani naomba taasisi husika zinisaidie kwa sababu baada ya kutoa ripoti polisi nimekuwa nikuzungushwa tu...mtuhumiwa hakamatwi.”
 SIMULIZI YA KUSIKITISHA
Binti aliyepata dhahama hiyo alipata kuzungumza na Ijumaa ambapo alisimulia simulizi ya kusikitisha sana ikionesha jinsi mchezo mzima ulivyokuwa.
Alisema: “Wadogo zake Roja ndiyo walikuwa marafiki zangu...Roja alikuwa akiwatumia wao kuniita kila siku jioni na nilipoenda alikuwa akinifungia chumbani kwake na kunilazimisha kufanya naye mapenzi huku akinitishia kuwa nikisema ataniua.
“Pamoja na vitisho hivyo alikuwa akinipa shilingi elfu tatu hivyo nikawa naogopa kumwambia mama na nilipogundua nina mimba nilimtuma wifi yangu (dada wa Roja) akamwambie lakini akakataa na kusema mimba siyo ya ndugu yake, mimi sijawahi kufanya mapenzi na mwanaume mwingine zaidi yake,” alisema binti huyo.
 KUTOKA IJUMAA
Tukio hili linaumiza na kusikitisha. Ni wito wetu kwa taasisi husika kufuatilia sakata hili na kumsaidia binti huyu ambaye ndoto zake zimezimwa ghafla akiwa bado mdogo.

Aidha, ni vyema wazazi wakawa makini katika kufuatilia nyendo za watoto wao kabla mambo mabaya hayajawakuta
KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga, Ernest Brandts, amesema kuifunga Simba katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom itakayochezwa Oktoba 20 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ni kazi rahisi.


Brandts amewatoa hofu viongozi na mashabiki wa Yanga, huku akitamba kupata ushindi dhidi ya mahasimu wao Simba. 

Akizungumza na RAI jana, Brandts alisema Simba hawamtishi kwa kuwa ana kikosi bora ambacho kina kila sababu ya kushinda mechi hiyo.

Alisema amekuwa akiifuatilia Simba mara nyingi inapocheza mechi na hakuna ushindani ambao umekuwa ukionyeshwa na wachezaji wa timu hiyo, licha ya kupata ushindi katika mechi zake.

“Simba hawana kiwango kikubwa, wanabebwa na mabao ambayo kwa bahati wamekuwa wakifunga, kikosi changu mimi ni bora, wachezaji wangu wana nguvu za kutosha na uwezo zaidi kuhakikisha tunashinda,” alisema.


Yanga tayari imewasili Bukoba kwa ajili ya mechi yao dhidi ya Kagera Sugar itakayochezwa kesho kwenye Uwanja wa Kaitaba.


Source:Rai.

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa ameikumbuka timu yake ya zamani ya Azam FC baada ya kuonekana akiwa kwenye Uwanja wa Chamazi Complex nje ya jiji la Dar es Salaam.

Ngassa, ambaye awali aliuzwa na Yanga kwenda Azam FC kwa kitita cha pauni milioni 98, miaka mitatu iliyopita kabla ya kurudi msimu huu, juzi alitua kwenye Uwanja wa Chamazi na kushuhudia mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya wenyeji na Mgambo Shooting.


Ngassa aliyeondoka Azam FC kwa mgogoro huku timu hiyo ikimpeleka Simba, alikuwa kivutio na wengi walianza kuonyeshana alipokuwa amekaa jukwaani.


Baada ya kufika uwanjani hapo, moja kwa moja Ngassa alikwenda kukaa alipokuwa amekaa mshambuliaji wa Azam FC, Gaudence Mwaikimba waliyewahi kukipiga pamoja Jangwani.


Mara baada ya mechi hiyo, kiungo huyo aliyerudi kwa kasi katika Klabu ya Yanga, kwa kuifungia bao moja mpaka sasa, alisalimiana na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo na kuondoka zake.


Ngassa alipoulizwa sababu za kwenda uwanjani hapo alisema kwa ufupi: “Nimekuja kutembea tu.”

Tayari Ngassa yupo mjini Bukoba kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya wenyeji Kagera Sugar, kesho.
GPL


Mbali ya karipio hilo, Waziri Mkuu amewataka viongozi wengine wa Serikali, kuepuka mfumo usio shirikishi katika uamuzi wao kwa kuwa unasababisha migogoro ndani ya jamii na usumbufu kwa Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya mgomo wa wasafirishaji wa mizigo na abiria ulioanza Oktoba 5, mwaka huu, Pinda alisema Serikali imeamua kurejesha kwa muda wa mwezi mmoja asilimia tano ya uzito wa mizigo uliozidi kwenye mizani.


Alisema hatua zilizochukuliwa na Dk. Magufuli kufuta vifungu vilivyokuwa vikiruhusu asilimia tano zilifuata sheria, lakini tatizo lililojitokeza ni kutoshirikisha pande zinazohusika ili kushauriana na kupata uamuzi wa pamoja.

Alisema mbali ya kutoshirikisha pande hizo, uamuzi wa Dk. Magufuli ulikuwa wa ghafla kwa wasafirishaji kitendo ambacho kimewapa wakati mgumu wa utekelezaji, kwa sababu wafanyabiashara walikuwa wameingia mikataba na wateja wao.

“Chimbuko la mgogoro huu, ni tangazo la Dk. Magufuli alilotoa Oktoba mosi, mwaka huu la kuondoa ofa ya asilimia ya uzito uliozidi, baada ya uamuzi huo wadau wa usafirishaji wa malori na mabasi waliingia kwenye mgomo na kulalamikia hatua hiyo.

“Kutokana na mgogoro huu, nililazimika kukutana na Dk. Magufuli, baadhi ya mawaziri wa wizara zenye uhusiano na masuala haya, wanasheria na wataalamu wa masuala ya usafiri na uchumi.

“Kilichoongeza mgogoro ni tafsiri ya vifungu vya sheria na kwenye kanuni ya 7 (2) na 7(3) ambacho kinaeleza wasafirishaji wa magari yenye uzito uliozidi, lakini upo ndani ya asilimia tano ya uzito unaokubaliwa kisheria, wanatakiwa kupunguza mzigo, kupinga na iwapo watashindwa kutekeleza, watatakiwa kulipia mara nne ya tozo za kawaida.

“Sasa suala la asilimia tano, lilitokana na ombi la wadau wa usafirishaji kwa aliyekuwa waziri wa Ujenzi miaka ya nyuma na halikuwa sheria kamili, ndio maana limeondolewa baada ya kuonekana linatumiwa vibaya.


“Nakubaliana na Dk. Magufuli, wapo baadhi ya wasafirishaji ni wakorofi na hawataki kufuata sheria…ndio maana walifanya mazoea ingawa wapo wengine wazuri na hao nawapongeza sana kutii sheria.


Mtanzania.

MTAYARISHAJI mahiri wa muziki wa Kizazi kipya, anayemiliki studio za ya B Hits, Hermes Bariki ‘Hermy B’ ameteuliwa kuwa Jaji wa shindano la kusaka vipaji vya kuimba Afrika Mashariki la Tusker Project Fame.


Mkali huyo anayemiliki studio za B Hits, ataiwakilisha Tanzania na kwa kuungana na majaji wengine jijini Nairobi, nchini Kenya akichukua nafasi ya Zahir Zorro aliyekuwa Jaji katika shughuli ya kusimamia usaili wa shindano hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja wa bia ya Tusker, Sialouise Shayo, alisema katika kuelekea awamu ya kwanza ya shindano hilo msimu huu wa sita, wamejipanga kuhakikisha Watanzania wanahusishwa kikamilifu.

“Kama tunavyomkaribisha Jaji mpya Hermy B ambaye amekuwa katika kinyang’nyiro hiki cha Tusker Project Fame kwa muda mrefu, tunatumia fursa hii kuwatangazia Watanzania kuwa tumejifunza mengi kupitia kwa Zorro,” alisema.

Katika shindano hilo, Tanzania inawakilishwa na Angela Karashani, Elisha Simon, Mgeni Kalinga na Ussa Dubart.

Kwa upande wake, Hermy B aliishukuru Tusker kwa kumchagua kuwa Jaji katika shindano hilo kwa mara ya sita pamoja na Zahir Zorro.


Mshindi wa Tusker Project Fame atajinyakulia Sh 100, 000, 000 na mkataba wa kurekodi utakaogharimu Sh 200, 000, 000.