DIWANI wa Kata ya Tai iliyopo Wilaya ya Rorya kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na Mwenyekiti wa Chama hicho wilayani hapo, Cristopher Masirori amenusurika kushambuliwa na Wananchi wenye hasira kali baada ya kukamatwa ugoni na mwanamke wa kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya hiyo.
Akizungumza na BLOG HII,mume wa Mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Thobias Rujora maarufu kwa jina la Ninja mkazi wa kijji cha Kiariko,alisema usiku wa saa 2 julai 23 alipigiwa simu na mtu asiyemfahamu akimuuliza kama ndiye anayeitwa Thobias na kumueleza mke wake yupo kwenye mazingira ya hatari na afike mara moja maeneo ya Obwere Shirati.
Alisema mtu aliyempa taarifa alisema mke wake ameingia katika nyumba ya kulala wageni na kiongozi mmoja wa Chama cha siasa na kuamua kuzifatilia habari hizo kwa kuwachukua baadhi ya jamaa zake hadi Obwere Shirati katika nyumba hiyo ya kulala wageni aliyetajiwa kuwa inaitwa Treepo A.
Rujora alisema baada ya kufika katika nyumba hiyo ya kulala wageni akiwa koridoni aliamua kupiga simu ya mke wake na kusikia ikiita na kuamua kutoka nje na kupiga simu kituo cha polisi Shirati kwa ajili ya kuomba msaada wa polisi ili watuhumiwa waweze kukamatwa.
"Baada ya kuona simu ya mke wangu ikiita chumbani niliamua kutoa taarifa polisi lakini watu niliowaacha pale nje walitaka kutumia nguvu ya kuvunja mlango na kuwazuia maana walikuwa na hasira na jambo baya lingetokea nami nlijipa ujasiri juu ya tukio hilo,"alisema Rujora.
"Niliwazuia na wakanielewa na baada ya muda mfupi askari polisi wapatao sita kutoka kituo cha polisi Shirati walifika na kuingia ndani na kugonga mlango zaidi ya mara sita ndipo ulipo funguliwa na Diwani huyo kukutwa ndani na mke wangu wakakamatwa.
Alipooulizwa kama katika siku za nyuma aliwahi kupata taarifa juu ya kuwepo kwa taarifa zozote za uhusiano kati ya kiongozi huyo na mke wake,Rujora alisema hajawahi kupata taarifa na kudai Diwani huyo amekuwa akilalamikiwa kwa vitendo vya kuwa na mazoea mabaya na wake za watu.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kituo cha polisi Wilaya ya kipolisi Shirati Musa Msenya alisema walizipata taarifa hizo kwa mtu anayedaiwa kuwa mume wa mwanamke aliyekamatwa na Diwani huyo na kuamua kwenda katika eneo la tukio..
"Ni kweli tukio hilo lilitokea Obwere Shirati nasi kuchukua uamuzi wa haraka kufika eneo la tukio baada ya kupata taarifa tayari watu walitaka kujichukulia sheria mikononi na tuligonga mlango baada ya muda kadhaa tulifunguliwa na wale wanaodaiwa kushikwa ugoni kuamua kuondoka nao.
"Tusingefika eneo lile mapema jambo baya lingeweza kutokea maana tuliwakuta wananchi wakiwa na hasira huku wakiwa wameshika silaha za jadi na kutoa maneno yaliyoathiri kutaka kumdhuru Mwenyekiti huyo wa Chadema Rorya,"alisema Msenye.
Wakizungumza na BLOG hii baadhi ya Wananchi walioshuhudia tukio hilo walisema Diwani huyo amekuwa na tabia ya kuwa na mahusiano na wake za watu na katika siku za hivi karibuni alifikishwa polisi na baadae ofisi za Ustawi wa Jamii akilalamikiwa na mkazi wa Rorya kuchukua mke wake ambaye aliacha watoto.
Source:http://shommibinda.blogspot.com/2013/07/diwani-wa-chadema-rorya-ashikwa-ugoni.html#main |
|
Katika historia ya muziki wa kizazi kipya hapa Tanzania haijawai tokea
msanii kukopeshwa kurekodi.
Hii ni mara ya kwanza na pia ni Neema kubwa
kwa wasanii wetu wenye Vipaji ila uwezo wa kurekodi inawashinda.
Producer wa siku nyingi ambaye habaatishi kazi zake STIVE WHITE,
amesema sasa anatoa msaada kwa wasanii chipukizi kwa kuwakoposha
kurekodi kwa Gharama ya shilingi elf 50 tu.
Msikilize hapa alipokuwa anaongea na D'JARO ARUNGU katika
kipindi cha swaga za kikwetu kinachoruka TBC fm j3 hadi ijumaa
saa 1usiku hadi2:30Usiku.
Kama wewe ni msanii na unataka kukutana na STIVE WHITE namba zake ni 0655424242 |
STAA wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekazia nia yake ya kutaka kurudi shule siku chache zijazo.
Lulu aliandika hayo juzikati alipokuwa akichati na mashabiki wake kupitia ukurasa wa facebook ambapo alikuwa akiulizwa maswali na kuyajibu live kupitia Runinga ya East Africa. Mmoja wa mashabiki wake alimuuliza Lulu kuhusu mipango yake ya kurudi shuleni ambapo alimjibu kuwa yupo katika mipango hiyo hivyo hivi karibuni atarudi darasani. “Am on process..soon mpenzi nitarudi darasani,” aliandika Lulu ambaye awali alidaiwa kukatisha masomo yake ya sekondari. |
Watanzania wenzetu wanavua samaki kwa kutumia sumu, wengine wanakaanga chips kwa mafuta ya transformer, kuku wanakuzwa kwa contraceptives (dawa za uzazi wa mpango), kitimoto nao wanapewa ARV's, samaki wanahifadhiwa kwa formalin (dawa ya kuhifadhia maiti) si hivyo tu, dawa feki kila kona?
Vyote hivi in a long run vitawaathiri watanzania wengi! Tunauana wenyewe kwa wenyewe kwa tamaa ya kutajirika haraka haraka! Mimi huu ujinga unanikera sana!! |
WANAFUNZI 12 wa Shule ya Sekondari ya Mlowa iliyopo Wilaya ya Iringa Vijijini wamenusurika kufa baada ya bweni walilokuwa wamelala kuungua kwa moto na kuteketeza vitu ambayo vilikuwemo ndani.
Tukio hilo linadaiwa lilitokea baada ya hitilafu ya umeme wa nishati ya jua (Sola) iliyosababishwa na wanafunzi ambao walikuwa wamelala katika bweni hilo kuunganisha nyaya kienyeji kwa ajili ya kusikiliza redio na kusababisha hasara ambayo inakadiriwa kufikia sh. milioni 1.8.
Akizungumzia jana ofisini kwake juu ya tukio hilo la kuungua kwa bweni na kunusurika kwa wanafunzi, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mlowa, Mwalimu Frank Mahai alisema wanafunzi wa l i o n u s u r i k a awa l i walikuwa wanaishi nje ya shule.
Alisema, mipango ya kuishi katika bweni hilo ilifanywa katika kikao cha wazazi na walimu kwa ajili ya wanafunzi ambao wanatoka mbali na shule ili wapate mahali pa kuishi katika muhula wa mitihani ya mwisho.
Mkuu huyo alisema kuwa, wanafunzi wengine wa shule hiyo wakati inaungua walikuwa wamekwenda kucheza mpira wa miguu kwa wavulana na wasichana katika Shule ya Sekondari ya Kalenga na kubakia wanafunzi 12 katika bweni ambapo saa 1:30 jioni moto ulianza kuunguza bweni hilo.
“Wanafunzi waliohusika na kuunguza ni baada ya kuunganisha nyaya kienyeji na kusababisha shoti hadi kuunguza bweni hilo,” alisema Mkuu huyo.
Alivitaja vitu vilivyoungua kuwa ni pamoja na nguo za wanafunzi, mabegi, madaftari, magodoro pamoja na paneli za sola ambazo zimeteketea moja kwa moja pamoja na dari ya chumba cha bweni ambapo jumla ya gharama zake zinafikia kiasi hicho cha fedha.
Hata hivyo Diwani wa Kata ya Mlowa, Charles Nyagawa (CCM) akizungumzia tukio hilo alisema kuwa amesikitishwa na kuungua kwa bweni hilo ambalo wazazi walishiriki kujenga na walitumia gharama kubwa.
Diwani huyo alisema, amesikitishwa na tabia za wanafunzi kuunguza bweni hilo kutokana na kujiingiza kwenye ufundi ambao hawaujui na wala hawana utaalamu nao.
Al i s ema k uwa , p i a anawashukuru wazazi na wananchi ambao walifika katika kijiji hicho na kuuzima moto na kuwa i n g awa h awa k uwe z a kufanikiwa anawashukuru kwa ushirikiano ambao w a l i u o n e s h a k a t i k a kuhakikisha moto huo unazimika na kuokoa baadhi ya mabweni mengine yasiendelee kuungua moto na kuteketea mali zingine zikiwemo za wanafunzi ambao walikwenda kwenye michezo na vitabu vya shule. Majira: |
Msichana Brave Cassidy Hooper (17) kutoka Charlotte, Kaskazini mwa Carolina Marekani aliyezaliwa bila pua wala macho anategemea kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kurekebisha uso wake.
Brave anategemewa kufanyiwa upasuaji huo (July 31) mwaka huu ambapo inategemewa sehemu ya mfupa utaondolewa katika ubavu wake kwaajili ya kutumika kutengeneza paji la uso wake, mfupa huo utasaidia kama kiunganishi cha pua mpya atakayowekewa. Msichana huyo ambaye yuko excited kwa ajili ya upasuaji huo mkubwa, tayari ameshafanyiwa upasuaji mara kadhaa kama sehemu ya maamdalizi ya upasuaji huo. Imechukua miaka sita kwa madaktari kufanya mchakato wa kutengeneza misingi ya kufika hatua ya kuwa katika nafasi ya kutengeneza pua mpya kwa Cassidy. Katika siku za nyuma, Cassidy alikuwa akitumia macho ya bandia, lakini kutokana na wazazi wake kushindwa kumudu gharama kubwa za $ 5,000 kila moja hakuendelea kuyatumia, kutokana na mahitaji ya kuyabadilisha kadri Hooper alivyokuwa anazidi kukua. Hooper amesema yuko excited kwaajili ya upasuaji huo mkubwa ambao anaamini kama utafanikiwa utamfanya aweze kupata pua na kunusa kama binadamu wengine. mpekuzi huru!! |
Mwanamke anaomba pesa toka kwa mumewe afanye biashara,anampa milioni tano. anachukua pesa hizo na kumpelekea OMAR, rafiki wa mumewe. Anamwomba awe naye ili apate ujauzito ili kunusuru ndoa yake.
EDA ni kipindi kisichopungua miezi mitatu ambacho anapaswa kukaa mwanamke bila kuolewa wala kushirikiana na mwanamume ama baada ya kutengana na mumewe au baada ya kufiwa na mume.Hii ni kwa mujibu wa dini ya kiislam.
EDA ni filam inayochambua changamoto za maisha ya ndoa katika familia nyingi.
Ndani ya filamu hii yumo Ussi Hajji kama YUSSUF. Marry Mwita kama YUSRA.Hidaya Njaidi na Abrahman Thomas kama wazazi wa Yusuf.Hashim Kambi na Khadija Ibrahim kama wazazi wa Yusra. Gerry wa Rymes kama OMAR rafiki wa YUSSUF, Sabrina Rupia kama KHAYRA mtumishi wa kampuni ya YUSSUF na rafiki wa yusra. Ahmed Olotu kama mwalimu wa dini. n.k
YUSSUF ni mtu mwenye uwezo mzuri kimaisha na wanaishi maisha ya furaha na uchamungu na mkewe YUSRA.YUSSUF yuko busy sana na masuala ya kazi, wanachelewa kupata mtoto jambo linalopelekea wazazi wa YUSSUF kumsakama mtoto wao wakitaka amwache mkewe wakidhani ndiye mwenye tatizo.
Huku wazazi wa YUSRA wakimsakama mtoto wao wakitaka atafute suluhisho mapema kabla tatizo hilo halijazua mtafaruku. YUSSUF na YUSRA wanakuwa katika hali ya mashaka ingawa wataalamu wa afya wamewathibitishia kuwa hakuna mwenye tatizo kati yao.
Jambo hili linawafanya wawashirikishe hata marafiki kwa nyakati tofauti. Hatimaye YUSRA anatafuta ushauri kwa KHAYRA ili kunusuru ndoa yake.
KHAYRA anamtumbukiza katika njia ngumu. YUSRA anaomba pesa toka kwa mumewe afanye biashara. YUSSUF anampa milioni tano.YUSRA anchukua pesa hizo na kumpelekea OMAR, rafiki wa mumewe. Anamwomba awe naye ili apate ujauzito kama alivyoshauriwa na KHAYRA, anusuru ndoa yake.
Lakini OMAR anamwogopa MUNGU na kuthamini utu wake. Anakataa na kumrudishia taarifa hizo YUSSUF akimwomba amkanye mkewe.
YUSSUF anakasirika na kumpa talaka moja mkewe. Wazazi wanachanganyikiwa . mama yake YUSRA anamlaumu mwanawe kwa kuchukua ushauri toka kwa rafiki asiye na ushauri mwema.
YUSRA anaingia katika EDA ya talaka…. Kwa mujibu wa sheria ya kiislam.
Siku 7 kabla ya EDA kwisha. Mama YUSRA anampigia simu YUSSUF kuwa mkewe yu mjamzito. YUSSUF anafurahi sana. Ananuwia kumrejea mkewe.
Akiwa njiani kwenda kumrejea mkewe anapata ajali......!!
JAMANI SITAKI NIKUMALIZIE UHONDO WA HII MOVIE EBU PATA NAKALA YAKO WIKI IJAYO
JUMATATU YA TAREHE 29,ITAKUWA MTAANI.NI BONGE LA FILAMU SIJAWAI KUONA!!
|
MWANAMKE mmoja Happiness Luhende mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa Lubaga katika manispaa ya Shinyanga, ameuawa kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kunyongwa na mume wake kwa kutumia kamba ya katani baada ya kumtuhumu kuwa anamsaliti kwa kufanya mapenzi na wanaumme wengine.
Tukio hilo limetokea juzi jioni majira ya saa 12 jioni katika kata ya Lubaga, ambapo watu walioshuhudia tukio hilo walisema Majija Clement mwenye umri wa miaka 22-23 ambaye ni mume wa marehemu aliona ujumbe mfupi kwenye simu ya mkewe uliokuwa unaashiria kuwa umetoka kwa mwanamme mwingine ukimtaka akutane naye eneo fulani, ndipo alipoamua kumpiga kisha kumnyonga kwa kutumia kamba ya katani. Akizungumzia tukio hilo mjomba wa marehemu, John Sumari, alisema mpwa wake aliolewa mwezi
Desemba mwaka jana na mpaka mauti yanamfika walikuwa hawajabahatika kupata mtoto.
“Marehemu ni mtoto wa dada yangu, wamekuwa wakigombana mara kwa mara, nimewahi kusuluhisha kesi mara mbili, kesi ya kwanza ilikuwa ni ya mwanamme kumtuhumu mke wake kuwa ana mwanamme mwingine baada ya kupigiwa simu. Kesi ya pili ilikuwa mwezi uliopita ambapo Majija Clement alimtuhumu mke wake kwamba anafanya mapenzi na balozi wa eneo hilo, lakini hayo yaliisha na leo ndiyo haya tena yametokea,” aliongeza. Walioshuhudia tukio hilo walisema mtuhumiwa ni mwenyeji wa wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza na alikuja Shinyanga kwa mama yake na kubahatika kumwona Happiness akaanza kuishi naye kama mke wake. Alisema mwanaume huyo anafanya shughuli za kuchoma tofali na kuendesha baiskeli maarufu 'daladala'. Mwenyekiti wa mtaa wa Lubaga, Shabani Mashishanga alisema mtuhumiwa alikuwa ni mhamiaji wa eneo hilo na ametoroka baada ya kufanya tukio hilo na jeshi la jadi (sungusungu) linamtafuta. Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Evarist Mangalla alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi huku akiwaomba kushirikiana na jeshi hilo kumtafuta mtuhumiwa ili sheria ichukue mkondo wake.
Na Kadama Malunde, Shinyanga
|
Royal Canadian Mounted Police (RCMP)
MWANAMKE mmoja aliyepotea kwa zaidi ya miaka 50 mjini Surrey, Columbia amepatikana akiwa hai na kikongwe huku akiwaacha na maswali waliompata kutokana na hali aliyokuwa nayo kwa sasa.
Mwana mama huyo, Lucy Johnson (77) alipotea akiwa na mumewe, Marvin Johnson tangu mwezi Mai, 1965 na taarifa kuripotiwa polisi wa mji huo kwa uchunguzi zaidi.
Hata hivyo baada ya juhudi za kumtafuta kushindikana kitengo maalumu cha polisi wa upelelezi kiliamua kumfungulia kesi mumewe juu ya tukio la kupotea kwa mkewe baada ya kuamini anahusika.
Hata hivyo uchunguzi ukiwa unaendelea Marvin alifariki dunia miaka ya 1990 akiwa bado hajahukumiwa juu ya kesi ya upotevu wa mkewe iliyokuwa ikimkabili.
Polisi wamekiri kuwa Lucy alipotea tangua miaka 1961 na taarifa zake kuwasilishwa.
Ikiwa ni zaidi ya miaka 50 sasa, Lucy ametambuliwa na mtoto wake wa kike, Linda Evans ambaye wakati mama yake anapotea binti huyu alikuwa na umri wa miaka kati ya saba na nane.
Linda Evans amefanikiwa kumpata mama yake mwezi Juni mwaka huu baada ya safari ndevu ya kumsaka kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa matangazo katika magazeti na majarida, hata hivyo amempata akiwa tayari ameolewa na mume mwingine na familia ya watoto wanne.
Evans alishangaa kupokea simu kutoka mjini Yukon kwa binti mmoja ambaye alijitambulisha kuwa mwanamke huyo anayetafutwa pia ni mama yake, hivyo kutaka kujua kama ni yeye au ni mtu mwingine anayefanana majina na yeye.
“…nina maswali mengi ya kutaka kumuuliza mama baada ya kumpata, nafikiri nitakuwa sehemu ya familia…nafikiri nikikutana naye nitamkumbatia na hapo maisha yangu yatakuwa ya mafanikio,” alisema binti huyo akihojiwa na gazeti moja mjini Columbia mara baada ya kupokea simu mama yake amepatikana.
Hata hivyo taarifa zaidi zinasema mama huyo baada ya kuhojiwa anasema hakumbuki kama aliwahi kuolewa na kuwa na familia, kama inavyojulikana.
|
|
MSICHANA wa kazi ‘hausigeli’ aitwaye Enjoy Cleofasi (19), hivi karibuni alipandisha mapepo na kumtwanga mwandishi wa habari aliyekuwa akimhoji kuhusiana na tukio la mauaji lililotokea mjini Dodoma
Tukio hilo la kukunjwa kwa mwandishi, lilitokea juzikati Kipunguni jijini Dar wakati Enjoy alipokuwa akisimulia jinsi alivyoutoa uhai wa mtoto wa jirani wakati alipokuwa akifanya kazi za ndani mkoani Dodoma.
Wakati Enjoy akisimulia mkasa huo, ghafla alibadilika na kuanza kuweweseka huku akionekana kama mgonjwa kisha kumkwida shati mwandishi (jina tunalo) ambaye naye alilazimika kukabana naye na kujitoa mikononi mwake. Timbwili zito likazuka kiasi cha kuwafanya baadhi ya watu waliokuwa eneo la tukio kukimbia kwa kuhofia mapepo ya msichana huyo. Msichana huyo akisimulia alivyoutoa uhai wa mtoto wa jirani mjini Dodoma, alisema matatizo yalianza baada ya kumuona mwanamke aliyemtokea katika mazingira ya kutatanisha akiwa shuleni mjini humo. “Mwanamke huyo alitokea kwenye maua na kuniita huku akiniambia ametokea kunipenda na kunitaka nimfuate, nilikataa ghafla nikawa sijielewi kisha nikapoteza fahamu,” alisema msichana huyo na kudai kwamba alikuja kuzinduka akiwa ofisini kwa walimu wake akiwa hakumbuki chochote. Baada ya tukio hilo, Enjoy alisema mwanamke huyo alimfuata tena usiku huku akiwa ananukia marashi, akiwa amevaa nguo nyeupe ilhali akiwa haonekani chini ya miguu yake na kujitambulisha kwa jina la Shakira. “Mwanamke huyo aliniambia kwamba yuko na wenzake, wametumwa kunichukua kwa sababu nina akili sana nikafanye kazi zao lakini nilikataa,” alisema Enjoy. Kutokana na mfululizo wa matukio hayo, Enjoy alisema alilazimika kubadili dini na kuwa Muislamu na kupewa jina la Jamila na Shehe aliyefika nyumbani kwako kumsomea dua. Jamila alisema baada ya kutibiwa na shehe huyo alipona na kuanza kwenda shule, safari hii akajiunga na shule ya bweni. Aliongeza kuwa, siku moja akiwa amelala usiku alishtuka na kukiona kitanda chote kikiwa kimelowa damu kiasi cha kutisha. Alisema alipiga kelele lakini haikusaidia kitu, walimu walipoiona hali hiyo walimrudisha nyumbani kwa ajili ya kupata matibabu. “Nilitibiwa na kurudi shule lakini nikiwa darasani nikawa naona giza, hivyo nikashindwa kuendelea na masomo. Nilirudi nyumbani kisha nikapata kazi ya ndani hapohapo Dodoma huku mauzauza yakiendelea,” alisema. Akiendelea kufanya kazi siku moja usiku alimuota tena yule mwanamke akiwa amemtokea na kumkabidhi kisu akimtaka akamuue mtoto mdogo wa jirani. “Nikiwa ndotoni niliota ninachukua kile kisu na kwenda kumchoma mtoto yule shingoni, cha ajabu wakati nikimchoma damu haikutoka baada ya hapo nikapewa kiapo nikitakiwa kuitunza siri hiyo la sivyo nitakiona cha moto,” alisema Enjoy. Akiendelea kusimulia msichana huyo alisema kuwa, asubuhi alipata taarifa kwamba yule mtoto wa jirani aliyemuota usiku amefariki dunia kwa kuchomwa na kisu. “Kilichonishtua zaidi ni pale majirani waliposema kwamba pamoja na mtoto huyo kuchomwa kisu, damu haikuonekana hata chembe ingawa jeraha lilionekana shingoni,” alisema Enjoy kwa majonzi. Enjoy alisema kuwa aliendelea kuitunza siri hiyo huku mauzauza yakiendelea na baada ya muda aliamua kuacha kazi na kuhamia Kipunguni Dar kwa dada aitwaye Regina Msafiri aliyeamua kumsaidia. chanzo:globalpublishers |
Binti mmoja (jina tunalo) kutoka Mtwara aliyeletwa Dar es salaam kuja kufanya kazi amejikuta kwenye mateso makali baada ya kutelekezwa bila nauli na kukutana na fataki aliomshawishi na kumuweka kinyumba na kusababisha majanga hayo makubwa.
Akiwa na umri wa miaka kumi na tano (15) tu, alitolewa kwao Mtwara na kuletwa hapa Dar na dada mmoja aliyemtaja kwa jina moja la Sophia kwa ajili ya usaidizi wa kazi za ndani.
Kwa maelezo yake ilitokea siku alimchapa mtoto wa bosi wake ndipo bosi alipokasirika na kufikia hatua ya kumtimua bila ya kumpa nauli ya kurudia kwao.
Alikutana na baba mwenye mke na watoto wa nne akamshawishi atampa maisha mazuri, akamweka kinyumba na kuanza kumtumia kimapenzi kinyume na maumbile. Kutokana na umri mdogo alionao,ilimsababishia kuharibika sehemu zake za siri na baba huyo na kumtelekeza baada ya kumtomlipia kodi sehemu aliyompangia chumba na majirani wa hapo ndio waliomsaidia. Hivi sasa binti huyo ameoza sehemu zake za siri anamiminika usaha tu na amehifadhiwa hospitali ya Amana anakopatiwa matibabu na misaada midogo kama chakula. Cha kusikitisha zaidi baada ya kupimwa kakutwa na Ujauzito wa miezi mitatu. na kapimwa virusi vya UKIMWI ambapo Vipimo vinatoka leo alhamisi kujua kama kaathirika au la.Baada ya leo nitakupa jibu nini kimeendelea kuhusu vipimo na jinsi ya kumpa msaada binti huyu. Source: mamuafrica |
Damu: Miguu ya Said Iddi ikivuja damu baada ya kukatwa.
ALI Omar, mkazi wa Kijiji cha Mabana, wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro anashikiliwa na polisi kwa kosa la kumkata miguu Said Iddi kwa kumtuhumu kumfumania na mkewe aliyejulikana kwa jina la mama Ali.
Mke wa mtu sumu: Said Iddi akiwa chini baada ya kukatwa miguu na Ali Omar.
MANENO YA SHUHUDA. Akizungumza na mwandishi wetu, shuhuda mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja alisema Said alifumaniwa ndani ya nyumba asubuhi akiwa na mke wa Ali baada ya kuwekewa mtego ambao ulimnasa vizuri. “Ali alipewa habari na kijana mmoja aitwaye God kwamba mkewe si mwaminifu katika ndoa, akamwongezea kuwa anatoka kimapenzi na Said. Ndipo Ali na mnyetishaji wake huyo walipopanga kumfumania jamaa,” alisema shuhuda.
Chini ya ulinzi: Mwenye mali, Ali Omar (kati) akiwa chini ya ulinzi baada ya kumkata Said.
MPANGO WA FUMANIZI. Habari zinapasha kuwa mara baada ya mnyetishaji kutoa taarifa za usaliti huo, Ali alimtafuta ‘baunsa’ ambaye jina lake halikuweza kujulikana mara moja na wakaweka mtego kwa kujificha karibu na nyumba hiyo ambayo Said angeingia ili kuivunja amri ya sita ya Mungu.
Umbea kazi: Kijana aitwaye God (kulia) aliyetoa taarifa kwa Ali naye akiwa chini ya ulinzi.
SAID ATINGA NYUMBANI KWA ALI. Habari zinasema mtoboa siri huyo alimwambia Said kuwa Ali amesafiri na ndipo jamaa akafunga safari kwenda kwa mama Ali kwa nia ya kujivinjari licha ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ukifikia katikati. Inasemekana Said akiwa ndani, Ali na baunsa wake waliibuka kwa kutaarifiwa na God na kumnasa jamaa huyo huku akidai ni mgoni wake. Alimuuliza maswali kadhaa, yakiwemo haya: “Umekuja kufanya nini ndani ya nyumba yangu? Kwa nini umekaa na mke wangu?” Habari zinasema Said alijibu hakuona ubaya kwa kuwa yeye ni mwangalizi wa mashamba ya mwanaume huyo hivyo anaweza kuingia ndani kwake wakati wowote.
Said Iddi akiwa amezungukwa na wananchi baada ya kukatwa miguu.
Jibu hilo lilidaiwa kumtibua Ali na ndipo yeye na baunsa wake walipomfunga kamba miguuni Said na kuanza kumkata kwa panga mguu mmoja kisha kuugeukia wa pili. Said alipiga mayowe yaliyowafanya wanakijiji kukimbilia eneo la tukio kwa lengo la kujua kulikoni ambapo walimkuta Said akiwa anavuja damu na sehemu ya nyuma ya miguu ikiwa nyanga’nyang’a.
Said akipelekwa kwenye difenda.
MWENYE MKE AKIMBIA, ANASWA.
Ali, God na baunsa walikimbia eneo hilo. Baadhi ya wanawake walitumia khanga zao kuifunga miguu ya Said kwa lengo la kujaribu kuzuia damu isiendelee kumwagika.
Said alikuwa akilia sana.
“Wanakijiji walichukizwa sana na ukatili uliofanywa na Ali, hivyo wakaanza kumsaka na kumkamata kichakani akiwa amejificha pamoja na God. Alipewa mkong’oto kwa lengo la kutaka kumuua, lakini viongozi wa kijiji walisihi asiuawe bali afikishwe kwenye kituo cha polisi,” alisema shuhuda.
MKE, MUME, MMBEYA WAFIKISHWA POLISI
Polisi wa Kituo cha Dumila waliitwa na kumchukua Said, Ali na God kwa kutumia gari aina ya Land Rover lenye namba za usajili T 750 AAJ. Mke wa Ali yeye alipelekwa polisi kwa pikipiki. Walipofika kituoni, Said alipewa fomu ya matibabu ya polisi (PF 3) na kupelekwa Hospitali ya Wilaya ya Kilosa kwa matibabu. “Pale hospitali Said alishonwa miguu yote lakini madaktari wakaamua ahamishiwe katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu zaidi,” alisema shuhuda huyo.
Bwana Said akiwa ndani ya difenda.
ANAWEZA ASITEMBEE TENA
Akaongeza: Daktari mmoja alisema haamini kama jamaa (Said) atatembea tena kwa sababu zana iliyotumika kumkata ilifika hadi kwenye mishipa ya nyuma ambayo ndiyo humfanya binadamu aweze kusimama na kutembea.
Said akishonwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa.
Afisa mmoja wa polisi kituoni hapo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini kwa kuwa si msemaji, alisema wanaendelea kumsaka baunsa aliyeshirikiana na Ali kumkata miguu Said.
...Said akizidi kupatiwa huduma.
|
Mto mwenye umri wa miaka 17 anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa na ngozi nne za chui zenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 22.8 Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe amesema kuwa mtoto huyo ni Mkazi wa Wilaya ya Handeni, alikamatwa kati ya Julai 21 na 23 mwaka huu wakati wa msako wa polisi uliofanywa kwa kushirikiana na Maafisa Wanyama Pori. Mtoto huyo alikamatwa akiwa Nyumbani kwao katika eneo la Zizini akiwa na ngozi hizo Nne za Chui zenye Thamani ya zaidi ya Millioni 22. “Operesheni hii ni kwa ajili ya kutafuta wahujumu wa nyara za serikali ... watambue kuwa itakuwa endelevu na tutawatia mbaroni wahusika wote," CHANZO: NIPASHE |
Huko Kamahuha, Maragua nchini Kenya kumetokea tukio ambalo liliwashangaza sana wakazi wa eneo hilo baada ya kukuta maiti ya Punda aliyedaiwa kubakwa mbaka kufa na watu wanne wenye njaa ya ngono.
Tukio hilo lilitokea usiku wa manane karibu na kanisa, amapo watu wa eneo hilo la Kamahuha walikimbia kwenye kituo cha polisi na kutoa taarifa juu ya kitendo hicho kilichofanywa na wanaume wanne walionekana usiku huo wakiwa
wamemning'iniza punda huyo juu ya mti na kuanza kumfanyia kitendo hicho cha ajabu.
Pia walikuta kondomu zilizotumika karibu na maiti ya Punda huyo huku akiwa amefungwa miguu yote ya nyuma.
Viongozi wa eneo hilo la Maragua wamelaani sana kwa kitendo hicho ambacho wamekiita ni cha Kishetani, pia wamedai wamekuwa wakiwaita wakazi wa eneo hilo na kuwasihi waachane na matendo hayo machafu ambayo mengi upelekewa na utumiaji wa pombe na madawa ya kulevya.
Masai Nyotambofu.
|
NAPENDA KUTOA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWA HAWA WAFUATAO 1.MAMA VERONIKA NDUNGURU 2.BABA LAURENT NSUHA WADOGO ZANGU 1.MONICA ROSES NSUHA 2.PHILIPO NERY NSUHA 3.DORAH NSUHA 4.BERTHA NSUHA 5.DOMMY NSUHA BILA KUWASHAU WATU WANGU WA KARIBU YAFUATAO: 1.DENIS MPAGAZE 2.ALLEN MOSHI 3.NESTRO NJAWIKE 4.ATHANAS SING'AMBI
Thursday, 25 July 2013
DIWANI WA CHADEMA AFUMANIWA NA MKE WA KADA WA CCM GUEST.
Subscribe to:
Posts (Atom)