Thamsanqa Jantjie amehojiwa na shirika la habari la The Associated Press aliloliambia kwamba mauzauza hayo yalianza alipokuwa akitafsiri na kwamba alijaribu kutopanic kwasababu polisi wenye silaha walikuwa karibu yake.
“Kilichotokea siku hiyo, niliona malaika wakiingia uwanjani. Nilianza kugundua kuwa tatizo lilikuwa hapa. Na tatizo, sijui shambulio la tatizo hili, litakujaje. Wakati mwingine huwa nakua katili sehemu hizo. Huwa naona vitu vinavyonifukuza,” alisema Jantjie.
“Nilikuwa kwenye wakati mgumu sana,” aliongeza. Na kumbuka watu hao, Rais na kila mtu, walikuwa na silaha, kulikuwa na polisi wenye silaha pembeni yangu. Ningeanza kupanick ningezusha tatizo. Nilitakiwa kukabiliana nalo ili nisiiabishe nchi yangu.”
Aliongeza kuwa aliwahi kulazwa hospitali ya wagonjwa wa akili kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Serikali ya Afrika Kusini imekiri kuwa kulifanyika makosa katika kumchukua Jantjie kwa kazi hiyo.
Naibu waziri wa Wanawake, Watoto na Walemavu, Hendrietta Bogopane-Zulu alisema maafisa wa serikali wamejaribu kufuatilia kampuni iliyompa kazi Thamsanqa Jantjie lakini wamiliki wa kampuni hiyo wameingia mitini.
Aliwaomba radhi watu wote wenye ulemavu wa kusikia na kusema kuwa uchunguzi unafanyika kubaini ni vipi Jantjie alikuwa amechukuliwa kufanya kazi hiyo.
Aliongeza kuwa kampuni hiyo ilitoa huduma chini ya kiwango na kwamba ujira waliomlipa mkalimani huyo kilikuwa kidogo mno. Mkalimani huyo alilipwa dola 85 tu.
AP waliomuonesha Jantjie video inayomuonesha akitafsiri kwenye hafla hiyo na kusema hakumbuki chochote.
“I don't remember any of this at all.