NAPENDA KUTOA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWA HAWA WAFUATAO 1.MAMA VERONIKA NDUNGURU 2.BABA LAURENT NSUHA WADOGO ZANGU 1.MONICA ROSES NSUHA 2.PHILIPO NERY NSUHA 3.DORAH NSUHA 4.BERTHA NSUHA 5.DOMMY NSUHA BILA KUWASHAU WATU WANGU WA KARIBU YAFUATAO: 1.DENIS MPAGAZE 2.ALLEN MOSHI 3.NESTRO NJAWIKE 4.ATHANAS SING'AMBI
Kwa jina unaweza muita Leilani Franco ana urahia wa nchi mbili (Uingereza / Philippines) alisafiri katika nafasi backbend umbali wa 20m katika muda wa 10.05 dk katika tamasha la Royal Hall mjini London Uingereza, tarehe 11 Machi 2013. Backbend binadamu ambaye ana uwezo wa kutembealea mikono na miguu kwa umbali mrefu. Pia kama inavyothaniwa kwa kawaida Mtu anaweza tumia mikono kwa kulia chakula na kufanya shughuli nyingine, lakini kwa mwanamke huyu imekuwa ni tofauti kabisa, Mwamake huyu ana uwezo wa kutumia miguu yake katika shughuli zake binafsi kama Kula na kadhalika..... Hatimaye, Leilani pia anashikilia rekodi ya Dunia kutokana na uwezo wake katika kuuzungusha Mwili wake. TAZAMA MAAJABU YA HUYU MREMBO KATIKA VIDEO!! |
Anafafanua kuwa siku zote mpenzi wako hawezi kuacha kukuhonga kwakuwa kwenye mapenzi kusaidiana ni lazima,kwahiyo haoni ajabu yoyote mtu kuhongwa. "Kusema ukweli mimi mwenyewe boy friend wangu kanisaidia sana na bado anaendelea kunisaidia,mimi sijali mtu aseme lolote analotaka lakini kama nahongwa for benefit sina tatizo na hilo"alisema Linah. Ameongeza kuwa tatizo watu wamekuwa wana maneno maneno sana na kufuatilia ya watu badala ya kufanya mambo yao lakini ili mradi mambo yake yanakwenda safi hajali lolote anatazama maisha yake zaidi. |
Mwanalizombe Studios Ni Recording Lebel Inayomilikiwa na Rapper Profesa Jay, Studio ipo msasani na Ameamua kuipa Jina la Mwanalizomba kwasababu Jay Ni mtu wa Ruvuma na Mwanalizombe maana yake ni Mwana Ruvuma na kufanya hivyo ameonyesha mapenzi ya mkoa wake wa Ruvuma. Producer kwenye studio hii ni Duke Touchez.
Profesa ameshindwa kusema amewekeza kiasi gani cha fedha kwenye studio hio ila fahamu kuwa vifaa vilinunuliwa kwa wakati tofauti na ni vifaa vya hali ya juu sana. |
Rapper Prezzo wa Kenya aliyehusishwa hivi karibuni na msako wa polici baada ya kusemekana alirushiana risasi na askari, Prezzo amejitokeza na kuweka mambo wazi kuhusu issue hizo na nini hasa kilitokea siku hio na kuhakikisha jina lake linasafishwa. Prezzo ni moja ya rappers wenye aka ya Bad Boy so sio issue mpya kusikia story kama hizi. Sasa Bwana Jackson Makini aka Prezzo ana habari mpya kwa shabiki wake kuhusu muziki wake. Kaa tayari kwa ngoma mpya kutoka kwa Prezzo Itaitwa " 7 Am" na itatoka siku yoyote mwezi huu. Star huyu kwa sasa bado anatamba na wimbo wake wa ‘Celebration Of Life’aliyomshirikisha Chess . |
Rita Paulsen aka Madam Rita wa Bongo Star Search na Walter Chilambo tayari wameshazijibu Salamu za Nay wa Mitego na jana ilikuwa zamu ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe .
Kwake mbunge huyo, Nay ni msanii wa pili wa Hip Hop anayemkubali zaidi Tanzania baada ya Roma na kwamba anakiheshimu kile alichokisema kwenye wimbo huo kwakuwa ni kazi ya sanaa. Tazama tweets hizi. CarolNdosi @CarolNdosi I wonder if @zittokabwe ever listens to hip hop..local or international..
“@CarolNdosi: I wonder if @zittokabwe ever listens to hip hop..local or international..” I do. Roma is my favourite followed by Ney
@zittokabwe @CarolNdosi surprising, after everything Nay Wamitego said in his new truck Salam zao ft Neiba Hon: Zitto still ranks him his n2
@SadiqAbdallah @CarolNdosi Ney amefanya sanaa. Nachukua maneno yake kama changamoto. Ni kazi ya Sanaa ninayoithamini sana.
|
|
Pichani juu ni taswira mbalimbali za muonekano mpya wa Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ ambaye kwa sasa yupo uraiani baada ya kufutiwa mashitaka yaliyokuwa yakimkabili ya kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya crystal methamphetamine yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8, Julai 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
|
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), jana alitikisa Jiji la Arusha baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kumfutia kesi ya uchochezi iliyokuwa ikimkabili.
Lema alidaiwa kutoa kauli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo alienda kwenye Chuo cha Uhasibu Arusha kama anaenda kwenye sherehe za kuaga mtoto wa kike “send off”. Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi, Devota Msofe baada ya wakili wa serikali, Eliananyi Njiro, kutumia kifungu cha 20 kifungu kidogo cha 1 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kuliondoa shauri hilo ambalo lilikuwa lianze kusikilizwa kwa siku mbili mfululizo. Upande wa serikali ulipanga kuleta mashahidi tisa. Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliofurika mahakamani hapo kusikiliza mwenendo wa kesi hiyo waliupokea uamuzi huo kwa shangwe kubwa. Akizungumza nje ya mahakama mara baada ya uamuzi huo, Lema alisema kuwa alikuwa anajua shauri hilo ni la kutengenezwa ndiyo maana mashahidi wengi walikuwa ni polisi. “Ni kama nimeshinda kesi, na Mungu ameendelea kutupigania, na tutaendelea kupambana kutafuta haki bila hofu maana miili yetu na nafsi zetu zimeishapoteza maumivu kwa sababu ya mateso yaliyojaa uongo na hila. “Tutaendelea na kelele zetu za kupigania haki bila kurudi nyuma huku uvumilivu ukiwa nguzo yetu kubwa,” alisema Lema. Hata hivyo, alikiri kutamka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mulongo alienda Chuo cha Uhasibu kama anaeenda kwenye “send-off” kwani yeye ndiye alimpigia simu akimtaka afike kusikiliza kero za wanachuo, lakini hakulipa uzito unaostahili suala hilo hasa ikizingatiwa kuwa pale kuna mwanachuo alikuwa amepoteza maisha. Lema alisema kuwa wanaweza kuwa wamemfutia kesi hiyo ili kesho wamfungulie nyingine jambo alilodai kuwa yuko tayari kwani anaelewa kuwa lengo ni kutaka kumuogopesha ili aache kuwatetea wananchi kitu alichodai kuwa hawatafanikiwa kwani tayari ana ganzi mwilini mwake, hivyo haogopi kufa, kesi wala kufungwa. Kwa upande wake wakili wa Lema, Method Kimomogoro alisema kuwa ni vema kama serikali ingeamua kutumia busara ya kuona hakuna kesi toka awali, hivyo wasingefungua kabisa shauri hilo lililopoteza muda wa mahakama na mteja wake, kwani hata maelezo ya kesi yalionyesha dhahiri hakukuwa na kosa la uchochezi. Alisema kuwa sheria inaruhusu kumfurahia, kumkejeli au kumzomea mtu, ndiyo maana hata bungeni wanaonekana waheshimiwa wakizomeana na kurushiana vijembe, na akadai hata kauli iliyodaiwa kutolewa na Lema dhidi ya mkuu wa mkoa ilikuwa kijembe tu. Kimomogoro alilitaka Jeshi la Polisi kutenda kazi zao kwa mujibu wa sheria, huku akiwataka warudi kwenye hoja ya msingi na wawaeleze wananchi endapo wameshawakamata waliohusika na mauaji ya mwanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha. Awali, ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mnamo Aprili 24, mwaka huu, mshtakiwa Lema akiwa eneo la Freedom Square ndani ya Chuo cha Uhasibu, alitoa maneno ya uchochezi yaliyosababisha uvunjifu wa amani. Maneno hayo yanayodaiwa kutamkwa ni kinyume na kifungu cha 390 sura ya 35 cha sheria ya kanuni ya adhabu, marejeo ya mwaka 2002 . “RC anakuja (Chuo cha Uhasibu) kama anaenda kwenye send-off, hajui chuo kilipo wala mauaji ya mwanafunzi wa chuo hicho... (RC) Ameshindwa hata kuwapa (wanafunzi) pole kwa kufiwa na amesema hawezi kuongea na wanafunzi wasio na nidhamu.” Yalinukuliwa baadhi ya maneno yaliyodaiwa kuwa yalitamkwa na Lema. Kauli hizo zinadaiwa zilipandisha hasira za wanafunzi ambao walianza kumrushia mawe na chupa Mkuu wa Mkoa, Mulongo alipokuwa akiwahutubia kuhusiana na tukio la kifo cha mwanafunzi, Henry Koga kilichotokea Aprili 23, mwaka huu. |
Kwa miaka mingi Coca cola imekuwa ni bidhaa namba moja yenye ubora wa kimataifa lakini mwaka huu Bidhaa Apple ikiwemo simu za Iphone imechukua namba moja kwa kuwa ni bidhaa boraDuniani.
Namba mbili imechukuliwa na Google kwa bidhaa zake mbali mbali...Namba tatu ndio imechukua Coca Cola
From New York Times
Apple is the new most valuable brand in the world, according to a closely followed annual report. The report, to be released next Monday, is from Interbrand, a corporate identity and brand consulting company owned by the Omnicom Group that has been compiling what it calls the Best Global Brands report since 2000. The previous No. 1 brand, Coca-Cola, fell to No. 3.
Not only has Apple replaced Coca-Cola as first among the 100 most valuable brands based on criteria that include financial performance, this is the first time that the soft drink known for slogans like “It’s the real thing” has not been No. 1.
|