Msanii kutoka Tanzania aliekuwa akifanya kazi chini ya Lebo ya Groundpa Records kutoka nchini Kenya Mr Nice ametoshwa na lebo hiyo kwa kuvunjiwa mkataba wa kazi,alikuwa amesaini chini ya Groundpa Records.
Kwa mujibu wa Groundpa Records wametoa sababu zilizowasukumua kumpiga chini Mr Nice kuwa ni msanii Mvivu,asie na ushirikiano wala kuaminika mbali na sababu hizo waliendelea kusema kuwa amekuwa akitumia vibaya pesa apatazo baada ya kufanya show,amekuwa bingwa wa kuwapa watu ofa za pombe
lakini sababu kubwa waliyoisema ni kwamba alikuwa amesaini mikataba miwili ni ule aliosaini kwa Lamar kutoka Tz na Sallam Sharaf CEO of Grandpa Records Refigah amesema kuwa Mr Nice amemkatisha sana tamaa na hamuitaji tena katika Lebo yao ya Groundpa tena maana habebeki.