advert

http://

Saturday, 1 March 2014

Aunt Ezekiel aeleza kilichomsukuma kufanya Bongo Flava


Aunt Ezekiel aeleza kilichomsukuma kufanya Bongo Flava, auelezea wimbo wake
Msanii wa filamu za Kiswahili, Aunt Ezekiel ambaye anatarajia kuachia wimbo wake mpya wa Bongo Flava alioupa jina la ‘Mguu kwa Mguu’
aliomshirikisha Linex Mjeda, ameeleza sababu kubwa iliyomfanya aingie kwenye game la Bongo Flava.
“Unajua game la Tanzania linabadilika badilika kwa hiyo nimeona ngoja pia nijihusishe katika uimbaji ili niendelee kuteka mashabiki, mimi zamani nilikuwa napenda sana Bongo Flava na sio kwamba nilikuwa naimba hapana, nilikuwa kama nikiona wasanii wakianza kuimba basi moyoni nafurahi sana. Siku moja wakanipa ushauri na hapo ndipo nikaingia studio na kutengeneza wimbo wa ‘Mguu kwa Mguu.” Aunt Ezekiel ameiambia tovuti ya Times Fm.
Ameeleza kuwa alitegemea kuachia wimbo huo mwaka jana ila ratiba zake hazikwenda vizuri hivyo aliamua kuiachia rasmi mwaka huu.
Mguu kwa Mguu ni wimbo uliotayarishwa na Mr. T Touch ndani ya Seductive Records .
 Samuel Eto

Mshambuliaji wa Chelese, Samuel Eto’o amechukizwa na kauli iliyotolewa na kocha wake Jose Mounrinho, kauli iliyoonekana kukeje umri wa mshambuliaji huyo kuwa sehemu ya kikwazo cha timu yake kupata ushindi dhidi ya Galatasaray.

Kipande cha video kinachoonesha maongezi ya Mourinho kilirushwa na Canal Plus, ambapo ilikuwa ni sehemu ya maongezi faragha kati yake na mfanyabiashara mmoja.
“Tatizo la Chelsea ni kwamba nakosa mfungaji. Eto’o ana miaka 32, labda 35, nani anajua?” alisema Mounrinho.
Hata hivyo Samuel Eto’o ambaye ana umri wa miaka 32, alijibu pia kwa kejeli kwa kutumia takwimu ile ile aliyoitoa Mourinho, na kudai kuwa kama aliweza kufunga magoli matatu dhidi ya Manchester akiwa na miaka 37 basi anaweza kufunga magoli mengi zaidi hata akiwa na miaka 50.
Baada ya maelezo ya Mourinho kuoneshwa kwenye television, kocha huyo aliomba radhi na kueleza kuwa bado uhusiano wake na Eto’o haukuathiriwa na tukio hilo.
Naye Caude Le Roy aliyewahi kufanya kazi na timu ya taifa ya Cameroon alieleza kuwa aliongea na Eto’o kwa njia ya simu na kwamba alionesha kukasirishwa na kauli ya Mourinho.
Makala: Mkasa wa Ostaz Juma na PNC, somo kwa Ostaz na wengine kuhusu nguvu ya mitandao ya kijamii

Moja kati ya matukio makubwa yaliyoteka ‘attention’ ya watu wengi ni picha na video zilizowekwa kwenye ukurasa wa Facebook na boss wa Mtanashati Entertainment, Ostaz Juma zikimuonesha mwimbaji toka Mwanza PNC akiwa amepiga magoti na kuonesha ishara ya mikono kama anaomba mbele ya boss huyo aliyetulia kwenye kochi akiwa amekunja 4.

Picha na video hizo ziliwekwa na Ostaz Juma mwenyewe kwenye ukurasa wake wa Facebook na kuandika, ““hahaha jamani mziki ni kazi pnc arudi kuomba msamaha ili aendelee kufanya kazi mtanashati.”
Haikuchukua muda, watu mbalimbali ambao ni wadau wa muziki wa kizazi kipya walipaza sauti wakilaani kitendo hicho kupitia mitandao ya kijamii wakiwemo wasanii mbalimbali ambao hawakusita kumchana Ostaz kwa kile kilichoonekana kuwa ni kumdhalilisha mwimbaji huyo.
Lakini wapo mashabiki ambao waliporomosha matusi kufuatia tukio hilo na habari hiyo kusambaa kwa nguvu kwenye mitandao ya kijamii, hali iliyompelekea Ostaz kudai kuwa siye aliyeziweka picha hizo. Lakini kilichowashitua wengi baadae, ni pale ilipoonekana post nyingine kwenye ukurasa wake akiwaponda watangazaji wa Tanzania na wasanii kuwa wanasumbuliwa na njaa.
“Naona watu mmeguswa sana na mimi kuanika picha ya PNC katika mitandao et, tatizo wasanii wa Tanzania mnanjaa sana kuanzia watangazaji Radio na wasanii njaa ndizo zinazo wasumbua...”
Lakini baadae aliongea na Moko Biashara aka One B wa Times Fm kueleza kuwa ukurasa wake metekwa na wezi wa akaunti za watu mtandaoni (hackers) na kwamba hiyo sio post yake.
“Daah, nshachanganyikiwa rafiki yangu watu wamehack akaunti yangu wanaandika matusi wanatukana watu..hadi hapa mimi nimeshachanganyikiwa hadi hata kuongea siwezi bro.” Alisema Ostaz.
Nadhubutu kusema kwa msisitizo kuwa picha hizo ziliwekwa na Ostaz Juma kwa jinsi nilivyozifanyia utafiti na kuzingatia kauli yake aloyoniambia kwa mara ya kwanza, “Ndio PNC kunipigia magoti na kuniomba radhi, lakini sasa mimi nikaamua kuwaonesha watanzania kwamba PNC amerudi kweli kuniomba msamaha. Je, kama kweli PNC alikuwa analalamika ‘Ostaz anafanya kazi zake hanijali hanisaidii…”
Hata hivyo sina uhakika…huenda kweli hakuandika kauli ya kuwaponda watangazaji na wasanii…nasema huenda kwa kuwa muda mchache baada ya kudai kuwa akaunti yake ilikuwa imetekwa na hackers na kubadili ‘password’, aliingia tena na kuifuta post hiyo na kuandika nyingine ya kuomba radhi na kueleza kuwa ilikuwa imetekwa kwa kipindi kile. Kwa upande wangu ‘no comment’ kwenye hilo.
Anyways, kwa maelezo yote hapo juu bila shaka umepata picha nzima ya tukio hilo japo kwa ufupi.
Sasa niende moja kwa moja kwenye mada na lengo langu, mkasa huu unapaswa kuwa zaidi ya somo la kawada kwa Ostaz Juma na wengine hasa watu maarufu ambao huichukulia mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter, Instagram n.k kama sehemu fulani tu ya kuandika unachotaka kama jinsi ulivyopewa uhuru ‘What’s on your mind’. Kumbe unatakiwa kufikiria sana kabla hujaandika na sio kuandika tu kile kilichoko kichwani kwako, kama unajali.
Ntatumia fikra ambazo nadhani alikuwa nazo Ostaz Juma kabla hajayaona matokeo ya alichokifanyana, matokeo yaliyomchanganya.
Huenda Ostaz Juma alikuwa bado anafikiria kuwa Radio, Television na magazeti pekee ndio vyombo vya habari vikubwa kuliko ‘social media’, wazo ambalo ni la kizamani kwa dunia ya sasa hivi.
Huenda Ostaz alikuwa hafahamu kuwa hivi sasa kwa kiasi kikubwa Traditional Media kama Radio, Television na magazeti zimeungana na ‘New Media’ ambazo ni mitandao ya kijamii, tovuti pamoja na blogs na habari husambaa kwa nguvu kupitia vyombo hivyo huku vikibadilishana.  
Habari nyingi zina-break kwenye mitandao bila kujali muda na huzua mijadala mikubwa kama hiyo.
Huenda alikuwa hafahamu kama, unachoandika Facebook kikishachukuliwa na watu wakaanza kushare hata ukifuta bado kitaendelea na kufika mbali zaidi na hata watu kuhamishia kwenye magroup ambayo huwa na maelfu ya watu au hata kuhamishiwa ‘watsapp’ na huenda wakati unajitetea watu hao wasisikie ama wakakupuuzia.
Huenda yeye aliona ana marafiki 2,258 akaona sio watu wengi na kwamba isingekuwa issue serious kiivo kama ambavyo angesema kwenye radio na vituo vya television.  
Huenda alikuwa hafahamu kama picha inaongea lugha zote duniani (universal language) hata bila kufuatilia nani kaandika nini. Hata mchina atakuwa ameielewa picha hiyo kwa lugha yake!
Ngoja nimfungue macho kama kweli alikuwa anafikra hizo.
Hadi kufikia mwishoni mwaka jana, takwimu zilionesha kuwa watu zaidi ya billioni 1.2 duniani kote wanatumia Facebook na kwamba hao ni active members, na kwa wastani kila mtumiaji ana marafiki zaidi ya 130 ambao anaweza ku-share nao habari na ikasambaa duniani kote kwa muda mfupi.
Takwimu hizo zinaonesha kuwa takribani asilimia 60 ya watu wazima wanaingia kwenye mitandao mbalimbali ambapo hata kama hawajajiunga na mitandao ya kijamii wanatembelea tovuti mbalimbali ambazo zinachukua habari kwenye mitandao ya kijamii.
Habari kama hizo zinazotokea Facebook huendelea kusambaa pia kwenye mitandao mingine ya kijamii kama Instagram, na hata Twitter ambayo inachukua 18% ya watumiaji wote wa mitandao, ambao wengi wao ni ‘active users’ na ndio kundi kubwa la watu wenye ushawishi (influential) kama watu maarufu. Twitter ina watumiaji zaidi ya milioni 640.
Kwa upande wa Instagram, kwa mfano Diamond akiishare picha hiyo wataiona watu zaidi ya 90,000 ambao wanaweza pia kushare, na huenda watu wakaiamini moja kwa moja habari hiyo kuwa kuwa msanii wanaempenda kalaani kitendo hicho.
Kwa takwimu hizo, ni vyema kufahamu kuwa kupitia mitandao ya kijamii hususani watu ambao wanafanya biashara inayotokana na kuuza kazi zilizobebwa na ‘image’ yao kama vile kazi za muziki, wanaweza kutengeneza biashara kubwa kwa kuwa wateja wengi wanaoweza kufanya maamuzi wako kule.
Uamuzi wa kuandika kitu kwenye mitandao ya kijamii kwa watu wenye biashara kama hiyo nikitolea mfano wa Ostaz Juma lazima uwe unamnyima uhuru wa kuandika kila anachofikiria tu, bali kuwaza mara mbili ama tatu matokeo ya kuweka mtandaoni kile anachofikiria.
Mtu kama Ostaz ambaye anawasaidia wasanii wa Tanzania, anatakiwa kufahamu kuwa msaada wake kwa wanamuziki hao kwao ni biashara ambayo inahitaji zaidi ya pesa kwa kuwa wanauza vitu viwili ambavyo ni muziki na ‘image’. Uropokaji wa mambo unaweza kuvunja image ambayo kuijenga itamgharimu msanii huyo zaidi ya pesa alizopewa kurekodi wimbo, kushuti video, kupigishwa pamba na hata pesa ya promotion.
Kwa mtu maarufu anayetegemea kuuza kutokana na sapoti ya watu, anatakiwa kufahamu kuwa ukurasa wake wa Facebook sio kijiwe cha washikaji zake ambacho anaweza kusema chochote kilicho kichwani kwake bila kujali na wakakipotezea baadae.
Ingawa Radio, Television na magazeti inawafikia watu wengi zaidi duniani na ina nguvu, ni vyema kwa mtu kama Ostaz na wengine wenye nafasi katika jamii kuelewa kuwa kila chombo cha habari kina nguvu kubwa na sio vyema kukilinganisha na chombo kingine ama kukipuuza.
Yale yalitokea sebuleni kwake (Ostaz Juma) yalipaswa kuwa faragha kwao wote wawili na sio kuyaweka kwenye mitandao ya kijamii.
Mwisho, ni vyema kwa mtu yeyote kutumia kanuni ya mitandao ya kijamii kuwa usiandike kitu chochote kwenye mtandao wa kijamii ukiwa na hasira ama ukiwa ‘too emotional’. Jitahidi kuvumilia kukaa nacho moyoni kwa muda na baada ya kutafakari unaweza kushare na watu.
Imeandikwa na Josefly Muhozi.
Mwanadada Wema Sepetu ambaye pia aliwahi kuwa Miss Tanzania 2006 ambaye kwa sasa anaendesha kampuni yake binafsi iitwayo Endless Fame inayojishughulisha zaidi na utengenezaji wa Filamu mbalimbali.


Kupitia kipindi cha Leo tena February 28 Wema Sepetu amekubali kutaja sifa za mwanaume anayempenda kuwa na mvuto kwake,swali lililoulizwa na Watangazaji wa kipindi hicho ni kuhusu mwanaume wa sifa gani anayedhani anaweza kuolewa nae ambapo Wema alijibu “Kuolewa sio shida je huyo mwanaume nampenda,maana naweza kuja kuchumbiwa lakini nisimpende”


“Mimi nampenda Mwanaume mweusi,wanaume weupe sio kwamba sijawahi kuwa nao lakini nakuwa sina mzuka nao”.
Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Diamond amekiri kwa kusema’Kweli niko na Nasib - Diamond na nadhani muda huu kutakua na utulivu ndani yake,ule utoto tuliokua tunafanya nadhani ulikua utoto na imekua Power Couple toka mwaka 2010 kwa hiyo tuna ni miaka 4 sasa,kwa sasa tumeamua kuwa serious’.

Habari kwa Hisani ya Millard Ayo

Wema Sepetu pia kaandamana na Ant Ezekiel kwenye interview ya kipindi hicho kinachorushwa na Clouds Fm.
SKENDO nzito ya Bongo Muvi imeibuliwa na baadhi ya wabunge waliopo mjini Dodoma kufuatia kuwalipua wasanii wake kuwa, ni ombaomba balaa, Risasi Jumamosi lina mkanda mzima.


Kwa mujibu wa wabunge hao ambao walitaka majina yao yasitiriwe kwa sasa, baadhi ya wasanii hao ambao wengi ni mastaa wamekuwa wakiwazukia na kuwapiga mizinga jambo linalowashangaza hasa wakizingatia kuwa, wapiga mizinga hao wana majina makubwa na huonekana wakitembelea magari ya kifahari.

“Hivi nyie mapaparazi, mnashindwa kabisa kukomesha hii tabia ya mastaa wa Bongo Muvi? Hawa jamaa ni ombaomba sana.

“Wamekuwa wakitupiga mizinga sana. Tunawashangaa maana wengine wana majina makubwa, wanatembelea magari ya kifahari lakini bado wanaomba pesa ndogo,” alisema mbunge mmoja ambaye anatoka kwenye moja ya majimbo ya Mkoa wa Dar es Salaam.

KINACHOWASHANGAZA WABUNGE
Kwa mujibu wa wabunge hao, linalowashangaza zaidi ni kwamba wasanii hao ambao  ni wake kwa waume, wamekuwa wakipiga mizinga ya pesa ndogo badala ya kuomba pesa za kufanyia mambo makubwa yenye mikakati mizito.

“Mtu anakuja, anasema anasumbuliwa na kodi ya nyumba au anasema hajala. Hivi kweli mastaa wakubwa kama akina…(anataja jina) ni wa kuomba vijisenti kama vya kodi ya nyumba jamani?” alihoji mbunge mwingine kati ya watano waliokuwa wakizungumza na gazeti hili.

Waheshimiwa hao waliendelea kuwaanika mastaa hao kwa kudai kwamba, walichogundua ni kuwa inapotokea wakapewa hitaji lao la fedha, huishia kukaa baa hadi usiku wa manane na asubuhi wakiamka wako vilevile kama hawakupewa.

MWAKIFWAMBA ABANWA NA RISASI
Ili kuweka sawa madai hayo mazito na yenye aibu kubwa kwa tasnia hiyo maarufu nchini, Risasi Jumamosi lilimtafuta Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania ‘TAFF’, Simon Mwakifwamba ambaye alikiri kuwepo kwa malalamiko hayo ya wasanii wake kuwa ombaomba!

HUYU HAPA MWAKIFWAMBA
“Ni kweli kabisa. Mimi mwenyewe nimewahi kusikia malalamiko hayo, lakini unajua tena ni mambo binafsi, mtu anapiga mizinga kwa mambo binafsi si rahisi kumwingilia,” alisema rais huyo.
Aliendelea kusema kuwa, katika vikao mbalimbali vya kisanii, amewahi kuweka wazi msimamo wa taasisi kwamba kila msanii aishi maisha yenye heshima huku akiwa mbali na mazingira yenye kusababisha aibu katika jamii.

KUMBE HATA JK ALIWAHI KUMLALAMIKIA
Katika kuonesha hasira zake juu ya tuhuma hizo zenye dharau katika gemu la filamu, Mwakifwamba alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, katika moja ya mazungumzo yake na Rais wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Kikwete ‘JK’ aliwahi kumlalamikia kwamba, wapo mastaa ambao kazi yao ni kupiga mizinga isiyo na tija.

“Rais mwenyewe aliwahi kuniambia kuna wasanii wakiwasiliana na yeye wanamwambia mambo ya pesa za kula.

“Kuna msanii aliwahi kumtumia meseji JK akimwambia, ‘mjukuu wako leo hali mbaya’,” alisema Mwakifwamba.
Akaendelea: “Sasa we’ unakutana na rais badala ya kumweleza mikakati mikubwa na nini cha kusaidiwa kuifanya tasnia iweze kuendelea, unapiga mizinga hujala, ni aibu sana.”

WALISHAMPIGA ‘MIZINGA’ HADI ‘MTOTO WA MKULIMA’
Mwakifwamba hakukubali kufumba midomo yake bila kupasua yote ambapo alizidi kudai kuwa, hawashangai sana wasanii wake hao kwani waliwahi kumpiga mizinga hadi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda ‘Mtoto wa Mkulima’. 
“Niliwahi kukutana na Waziri Mkuu Pinda, nikamwomba mambo ya kuisaidia tasnia ya filamu Tanzania, akasema afadhali mimi nimeongea vitu vya maana, kuna wenzangu alikutana nao ‘wakambomu’ fedha za matumizi binafsi, nilishangaa sana,” alisema Mwakifwamba. 

RISASI LAWASAKA MASTAA, WAPATIKANA HAWA:
Jacqueline Wolper, ni staa wa filamu za Kibongo. Filamu yake ya kwanza ni Ama Zao Ama Zangu. Yeye alipoulizwa kuhusu madai hayo, alisema:
“Ni kweli, sikatai kwamba hiyo tabia ipo tena sana tu. Lakini wanaoongoza ni mastaa wa kiume, hao ndiyo wanaotutia aibu ya kuonekana sisi ni o
mbaomba.”

STEVE NYERERE
Yeye ndiye Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity. Alisema anavyojua kuna kuonana kirafiki na waheshimiwa na kuonana kiajenda.
“Tabia ya kuomba fedha kwa waheshimiwa ipo. Lakini linapokuja suala la tasnia yetu kupeleka hoja kwao, tunaanza hoja baada ya hapo kuna waheshimiwa wengi wana urafiki na wasanii, tunaitana pembeni na kupiga kirungu.
“Siwezi kukaa na waheshimiwa kama Rostam Aziz, William Ngeleja, Mheshimiwa Abood na Nimrod Mkono halafu nikawaacha hivihivi, kisa eti mimi ni Mwenyekiti wa Bongo Muvi,” alisema Steve akionesha kumshangaa mwandishi aliyempigia simu kutaka usawa wa mizani ya habari hiyo. 
ODAMA YEYE
Jennifer Kyaka ‘Odama’ yeye alipata umaarufu mkubwa kupitia Tamthiliya ya Odama iliyokuwa ikirushwa na Televisheni ya Taifa (wakati huo TVT). Alipopigiwa simu iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa licha ya kurudiwa mara kadhaa.
AUNT EZEKIEL
Risasi pia lilimtafuta  nyota mwingine aliye mahiri kwenye sinema za Bongo, Aunt Ezekiel ambaye filamu iliyompaisha sana inaitwa Miss Tanzania. Yeye simu yake ya mkononi ilionesha kutokuwa hata na laini kwa wakati huo.

RAY AFUNGUKA
Staa mkongwe katika gemu tangu enzi za Kaole Sanaa Group, Vincent Kigosi ‘Ray’ aliposakwa na kuulizwa kuhusu madai hayo ya wasanii kuwa ombaomba alisema:
“Wasanii wengi wanawaza maisha ya hapa na si baadaye. Badala ya mtu kuweka shida zake kwenye mfuko wa karatasi, anaweka kwenye rambo ambao unapiga kelele.
“Mwisho wa siku anaomba shilingi milioni tatu akagombolee gari au asaidiwe kodi ya nyumba, anasahau kuwa kapata nafasi ya kuonana na mheshimiwa azungumzie tasnia tunavyonyonywa hadi kuuza hati miliki,” alisem Ray.
Credits:Global Publishers.
Tovuti ya Times Fm imefanya mahojiano ‘exclusively’ na Robina Nicholaus, msichana aliyeshika nafasi ya kwanza/ aliyeongoza kitaifa (Tanzania One) kwenye matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2013.


Robina, mwenyeji wa wilaya ya Bunda mkoa wa Mara ambaye alikuwa anasoma katika shule ya wasichana ya Marian, akiwa na ndoto ya kuwa daktari wa watoto amejibu maswali kumi muhimu na majibu yake yanaweza kuchukuliwa kama mfano wa kuigwa kwa wanafunzi walioko shuleni ambao wanakumbwa na changamoto kadhaa, na wazazi wanaowapeleka watoto wao shule.
Ulifanya nini ghafla ulipopata taarifa kuwa umekuwa wa kwanza Tanzania nzima, na je, ulitegemea?
 Nilipopata matokeo kwamba nimekuwa wa kwanza, kwanza nilifurahi sana na kilichobaki zaidi ilikuwa ni kumshukuru Mungu kwa sababu yeye ndiye kayawezesha yote. Nilihisi kama kupaa vile…nilifurahi sana halafu my mom alikuwa pale… alikuwa analia akaniinfluence na mimi machozi yatoke, I was very happy yaani. Sikutegemea kuwa wa kwanza lakini nilikua na uhakika wa kufanya vizuri kwa sababu niliplan kufanya vizuri.
Kama msichana ulifanya nini kuzivuka changamoto za kimasomo na kufanikisha kwa kiasi kikubwa? 
Safari ya taaluma ni ndefu ndio, kwenye safari ya masomo kuna changamoto za hapa na pale, ambapo mara nyingi wasichana waga tunafanya maamuzi ambayo sio sahihi. Lakini kwangu mimi nimeweka interest yangu sana kwa wazazi. Kwa hiyo nilikuwa open kwa wazazi na kuwaomba ushauri wa hapa na pale nifanye nini. Na katika vyote nilivyokuwa nafanya ni kufanya kile kitu ambacho hakiwezi kusubiria kwanza ambacho ni masomo. Kwa hiyo naweka juhudi pale ili ukishafanya kila mtu ajue kwamba umefanya.


Ilikuwa mbaya sana kwenye kusoma hasa form three ambapo nilianza kushuka and all that. Kwa hiyo wazazi pamoja na walimu pia walikaa na kuweza kunisaidia na mimi mwenyewe nilikuwa tayari kusikia ushauri wao na kuweza kusoma kwa bidii zaidi ili niweze kupata ile nafasi yangu niliyokuwa naipata toka nianze.

Nini kilichofanya ushuke kimasomo wakati huo?

 Kilichofanya nishuke ni ile kupoteza malengo na juhudi zangu, na pia kuona kwamba vitu vinaanza kuwa vigumu halafu kuweka hiyo kwenye akili kwamba hicho ni kigumu siwezi kukifanya. Lakini nilipoamua kuweka juhudi na kuona kwamba ni vitu vya kawaida kwamba navyozidi kukua na vitu vinazidi kuwa vigumu na natakiwa nitafute njia ya kuvi-overcome, ndo hivyo nikaweza kufanikiwa.

Ratiba yako ya siku ulipokuwa shule kwa ujumla wake ilikuwa vipi na muda gani ulikuwa unajisomea?

Asubuhi nilikuwa naamka mapema kabla ya time table ya shule haijaanza kwa sababu tunatakiwa tuamke mapema kwenda misa kwenye saa kumi na moja hivi. Kwa hiyo naamkaga kwenye saa tisa najiandaa naenda darasani kwa sababu siwezi kusoma usiku kwa sababu usiku nakuwa nimechoka, kwa hiyo my extra time inakuwa asubuhi ambako I’m still fresh. 
Nasoma then ikifika muda wa misa naenda kusali. Nikitoka kusali kuna kazi ndogo ndogo za kufanya kujiandaa na time table ya school and all that. And my free time ile mchana nikitoka darasani kuanzia saa nane, nakuwa nimepanga nini natakiwa nifanye, ni somo gani natakiwa kulisoma at that time ambapo ni saa nane mpaka saa kumi na nusu. Ambapo ni muda wa concentration, kama kuna kitu ambacho sijaelewa naenda kuwafuata waalimu kwa sababu wanakuwa wapo at that time. And kuna some free time kama ile break time, ni kuanzia saa nne na dakika 40 mpaka saa tano na robo, pale hauwezi kusema unatake breakfast all the time, unatake breakfast for a short time halafu nyingine inabaki unaweza kufanya maswali matano ya physics. Yaani every little time ambayo unaweza kuipata, you don’t let it go to waste tu, una-utilize.
Marafiki ulionao wanaweza kusaidia kukupandisha au kukushusha. Wewe ulikuwa na marafiki wa aina gani? 
Marafiki wangu nimewachagua kwa category..yeah (anacheka), ikifika muda wa kusoma nakuwa na mtu ambaye najua atanisaidia, kwa hiyo nilikuwa na rafiki yangu anaitwa Sarafina amekuwa wa nne. Alikuwa ananiinfluence sana kusoma, huyo ni wakati wa kusoma, kwenye academics namfata yeye.

Ikifika wakati wa social siwezi kumfata sarafina kwa sababu she is not that social, yeye yuko kama mimi we are not that social, kwa hiyo ninaye social friend. Pia ikifika muda wa kuspend, I have an economical friend. Ambaye I’m sure nikikaa nae nikiwa naspend siwezi kwenda beyond my budget. Kwamba siwezi kufulia. Kwamba we are all in the same status, same friends, yeah.
Ni kitu gani kilikuwa kinakuboa sana shuleni na kukunyima furaha muda mwingine?
Kitu ambacho kilikuwa kinaniboa sana, ikifika wakati ambapo kwa mfano watu wachache kwenye darasa wamefanya kosa halafu sasa mnakuwa included as a whole class halafu mnapata adhabu. Hiyo adhabu directly itaharibu time table yangu ya kusoma. Kwa hiyo badala ya kusoma nafikiria ningekuwa nasoma physics, I’m either slashing an area..yaani hiyo ilikuwa inaniboa sana yaani.
Ulishawahi kuitwa ‘Msongo’ au majina kama hayo? Ulikuwa unaichukuliaje na je, ilikutenga na marafiki zako? 
Yeah, msongo…kauzu. Yeah mimi naipenda hivyo kwa sababu nafanya nachotakiwa kufanya ambacho ni kusoma. Hiyo haikunitenganisha na marafiki zangu. 

Vuta taswira, je, ingetokea ukapata division Zero na kuwa wa mwisho Tanzania nzima ungefanyaje? Na unawashauri nini waliofeli kwa kiasi hicho?
Kama ningepata zero, kwanza ningefikiria…na ningekuwa very disappointed kweli, lakini pia ningefikiria kuhusu kujipa second chance, ningeenda kusoma tena. 
Kwa waliofeli ningependa kuwashauri wasikate tamaa hata kidogo and wajipe second chance. Kwa wengine pia ambao wana vipaji vyao wanaweza kuviendeleza. But pia kwa kuwa elimu ni muhimu..ku-reseat pia ingekuwa ana option.
Robina Nicholaus ni msichana wa aina gani?

Robina ni mtu mkimya lakini mcheshi pia. Nisingependa nikae na mtu halafu nikawa kimya just because ni mkimya... I will try kuchekesha, and of course I’m funny anyway.
Mtoto Anastazia Jumanne (12) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi katika wilaya na mkoa wa Geita amefanyiwa ukatili wa kutisha baada kufungwa mpira kwenye pikipiki na baba yake mzazi na kisha kuanza kumburuza mtaani.


Tukio hilo la kusikitisha limetokea jana majira ya sa tatu asubuhi katika moja ya mitaa ya mjini humo ambapo inadaiwa kuwa binti huyo anayesoma darasa la nne katika shule hiyo alikataa kwenda shule kitendo ambacho kilimkasirisha baba yake aitwaye Jumanne Nkoyogi ambaye pia ni mfanyabiashara wa samaki mjini Geita.

 mashuhuda wa tukio hilo baada ya kuona asubuhi hiyo mtoto huyo akiburuzwa huku amefungwa kwenye pikipiki walianza kupiga makelele na kukusanyana kwa lengo la kumkamata baba huyo aliyekuwa anafanya unyama huo.

  Baada ya kumkamata na kumtia kumtia mikononi mwao walimpeleka kwenye ofisi ya sungusungu iliyopo Ihayabuyaga kata ya Kalangalala na kufungiwa humo kwa usalama wake.
Akizungumzia tukio hilo katibu wa sungusungu kata ya Kalangalala aliyempokea mtuhumiwa huyo Abel Richard amesema tukio hilo liliwafanya wananchi kujaa jazba dhidi ya mzazi huyo na kutaka kumpiga.

Amesema mzazi huyo kwa sasa anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani Geita baada ya katibu huyo kuwasiliana na uongozi wa jeshi hilo na kuwatuma askari kwake kumchukua haraka kwa usalama wake.

Afisa upelelezi wa mkoa wa Geita Simon Pasua amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi hadi sasa kwa upelelezi zaidi