NAPENDA KUTOA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWA HAWA WAFUATAO 1.MAMA VERONIKA NDUNGURU 2.BABA LAURENT NSUHA WADOGO ZANGU 1.MONICA ROSES NSUHA 2.PHILIPO NERY NSUHA 3.DORAH NSUHA 4.BERTHA NSUHA 5.DOMMY NSUHA BILA KUWASHAU WATU WANGU WA KARIBU YAFUATAO: 1.DENIS MPAGAZE 2.ALLEN MOSHI 3.NESTRO NJAWIKE 4.ATHANAS SING'AMBI
Monday, 14 October 2013
Sunday, 13 October 2013
MAGAZETI MAWILI YAFUNGIWA , NI MWANANCHI NA MTANZANIA
Serikali imeyafungia kutochapishwa Magazeti ya MWANANCHI na MTANZANIA kuanzia 27 Septemba,2013 kutokana na mwenendo wa magazeti hayo kuandika habari na makala za uchochezi na uhasama kwa nia ya kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola hivyo kuhatarisha amani na mshikamano ulipo nchini.
Gazeti la MWANANCHI limefungiwa kutochapishwa kwa siku kumi na nne(14) kuanzia 27 Septemba,2013.Adhabu hii imetangazwa kwa Tangazo la Serikali(Government Notice )Namba 333 la tarehe 27 septemba,2013.
Gazeti la MWANANCHI limepewa adhabu hiyo kutokana na hivi karibuni kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na uvunjifu wa amani,mfano tarehe 17 Julai,2013 katika toleo Namba 4774 ilichapisha habari isemayo “MISHAHARA MIPYA SERIKALINI 2013” kwa kuchapisha waraka uliozuiliwa kwa matumizi ya vyombo vya habari waraka huo ulikuwa wa Siri haukupaswa kuchapishwa Magazetini.
Aidha, katika toleo la Jumamosi,tarehe 17 Agosti,2013 lilichapisha habari yenye kichwa kisemacho “WAISLAM WASALI CHINI YA ULINZI MKALI” habari hiyo ilikolezwa na picha ya mbwa mkali mwenye hasira.Habari na picha hiyo ilitoa tafsiri ya kuwa Jeshi la Polisi lilipeleka Mbwa katika maeneo ya ibada ya waumini wa dini ya kiislam.Jambo ambalo halikuwa la ukweli.
Jeshi la Polisi katika doria siku hiyo halikupeleka mbwa katika maeneo ya Misikiti.Serikali na jeshi la Polisi linaheshimu na kuzingatia maadili ya dini ya Kiislamu na kwa hiyo Jeshi lake haliwezi kupitisha au kuingiza mbwa katika maeneo ya ibada.
Hivyo basi,kwa gazeti hili kuchapisha habari iliyokolezwa na picha ya mbwa ni uchochezi wa kulichonganisha Jeshi la Polisi na waumini wa dini ya kiislam mbwa ni najisi hapaswi kuingia katika maeneo ya ibada.
Gazeti la MTANZANIA limefungiwa kutochapishwa kwa siku tisini(90) kuanzia tarehe 27 Septemba,2013 kwa kuchapisha habari zenye uchochezi.Gazeti hili limeonywa mara nyingi lirekebishe mtindo wake wa uandishi wa kichochezi na lizingatie maadili na Sheria na Kanuni za fani ya Habari.
Pamoja na kuonywa gazeti hili halikuonyesha kuzingatia maelekezo ya Msajili wa Magazeti, mfano ;katika toleo na 7262 la 20 Machi,2013 liliandika habari yenye kichwa kisemacho “URAIS WA DAMU”,tarehe 12 Juni,2013,toleo Namba 7344 lilichapisha makala isemayo “MAPINDUZI HAYAEPUKIKI”.
Aidha, siku ya Jumatano,tarehe 18 Septemba,2013 katika toleo Namba 73414 ukurasa wa mbele lilichapisha Kichwa cha habari kisemacho “SERIKALI YANUKA DAMU” taarifa hiyo ilikolezwa na picha zilizo unganishwa kwa ustadi mkubwa kwa kutumia kompyuta kutapakaza rangi nyekundu mithili ya damu nyingi kumwagika .Katika habari hiyo gazeti hilo limedai bila uthibitisho kuwa Jeshi la Polisi linahusika na wahanga waliomizwa na watu wasiojulikana kwa kumwagiwa tindikali na waliyovamiwa na kujeruhiwa vibaya.
Vile vile gazeti hilo limeishtumu serikali kuwa goigoi katika kushughulikia matukio yenye sura ya kigaidi.
Kwa ujumla wake habari hiyo ni ya kichochezi ina lengo la kuwafanya wananchi wavichukie vyombo vya ulinzi na usalama wavione kuwa haviwasaidii.
Kutokana na makosa yalitajwa hapo juu serikali imelifungia gazeti la Mtanzania kutochapishwa kwa muda wa siku tisini(90) kwa Tangazo la Serikali Namba 332(Government Notice No.332) la tarehe 27 septemba,2013,.
Serikali inawataka wamiliki,wahariri na wanahabari kwa ujumla kuwa makini,kuzingatia weledi,miiko na madili yataaluma uandishi wa habari.
Serikali inawataka wamiliki na hasa wahariri kuhakisha kuwa habari wanazoziandika na vipindi wanavyoviandaa vinazingatia taaluma,kuweka mbele maslahi ya taifa letu kwa kuwa na uzalendo wa hali ya juu.
Serikali inavionya vyombo vya habari vinavyoutumia uhuru wa habari bila wajibu kuwa haitasita kuvichukulia hatua kali ikiwemo ya kuvifungia .Serikali haitakubali kuona vyombo vya habari kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani nchini.
Imetolewa na
MKURUGENZI IDARA YA HABARI
WIZARA YA HABARI,VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
Saturday, 12 October 2013
DIWANI WA CHADEMA ATUHUMIWA WIZI WA MILIONI 10 ZA KITANZANIA MKOANI KILIMANJARO.
![]() WATU tisa akiwemo Diwani wa Kata ya Old Moshi Magharibi, Elisaria Mosha (Chadema) wametiwa mbaroni wakituhumiwa kupokea fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia mradi wa umeme mkoani Kilimanjaro. Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal, kufanya ziara mkoani Kilimanjaro na kuagiza watu waliofanya hivyo wakamatwe mara moja. AKIZUNGUMZA na waandishi wa habari jana ofisini kwake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema diwani huyo anatuhumiwa kujipatia Sh milioni 9.6 kwa njia ya udanganyifu. Wengine wanaoshikiliwa ni Zakayo Kimathi (52) mkazi wa Mandaka, anayedaiwa kupokea Sh milioni 10.3, Oforo Kimambo (56) mkazi wa Mandaka anayedaiwa kupokea Sh milioni 29. Wengine wanaotuhumiwa kupokea malipo hayo kwa njia ya udanganyifu ni Daud Mallya (69) mkazi wa Chekereni aliyepokea Sh milioni 8.6, Richard Mlaki (69) mkazi wa Kiboroloni alipokea Sh milioni 18.6 na Focus Herman (88) mkazi wa Kilototoni aliyepokea Sh milioni 36. Boaz alisema kwa sasa watuhumiwa watatu hawajapatikana. Alieleza kuwa pamoja na watuhumiwa hao, polisi imemkamata Mwenyekiti wa Kijiji cha Mandaka Monono, Hassan Nduva (41) na Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Vendelini Shayo (58) kwa kuhusika kufanikisha malipo hayo. Dk Bilal alitoa agizo hilo mapema wiki hii wakati akizindua vituo vya kupozea na kusambaza umeme maeneo ya Kiyungi, YMCA na Makuyuni. Alipokea taarifa kwa Mkuu wa Mkoa kuwapo kwa wananchi ambao hawakulipwa fidia zao, kutokana na kuwapo watu waliotumia ujanja wa kupokea fedha hizo, Sh milioni 169.2. “Halmashauri ya Moshi Vijijini ndio ilikuwa wakala wa malipo hayo na ndio iliyofanya tathmini kwa kushirikiana na watendaji wa vijiji, ambapo wao walipeleka tathmini hiyo kwa Shirika la Umeme (Tanesco), ambalo lilitoa fedha hizo hivyo Tanesco hawahusiki,” alisema,” alisema Boaz. Habari leo. |
|
One week after the first episode of
the talent search show Tusker
Project Fame Season 6 went on air
from the academy in Nairobi, there
have been twists and turns in
The Beat has reliably learnt that
organisers at the academy have
dropped Tanzanian judge, musician
Zahir Ali Zorro from the panel of
judges.
Details of the fallout are still sketchy
but word from Zahir Zorro’s camp
has it that it was an amicable
understanding between both
parties.
Speaking to The Beat , the veteran
musician said he had chosen to leave
the show in order to concentrate on
his personal musical engagements
back at home.
“After the show in Nairobi last week
it dawned on me that the responsibility was heavy and I
couldn’t handle both the academy
duties and my other engagements at
home satisfactorily,” he said.
Zahir Zorro’s appointment to the
judges’ panel was greeted with
cheers of hope as many thought he
would take the contest to a different
level after replacing producer
Hermes Bariki.
He was to work with Juliana
Kanyomozi who filled the Ugandan
spot and as agreed, controversial Ian
Mbugua filled the Kenyan spot.
But as the posts on the TPF website
announced that the vastly experienced musician had joined the
panel, discord was brewing.
Though there has not been any
official communication from
Endermol and East Africa Breweries,
sources privy to the academy cite his
laid back display at the inauguration
as the potential cause.
In his trademark bling-bling and
suit, Zorro barely said anything
during the blockbuster show that
ushered in 25 contestants. “He was a
bit uncomfortable with the
surroundings and looked not at ease
with the other judges who were
enjoying themselves throughout the
show,” said the source.
But in an interview with The Beat,
Zorro cited generation gap as the
reason for his mysterious exit from
the regional show. In hi own words:
“They will have to appoint a more
youthful person to take over from
me.”
This leaves some unanswered
questions whether it was the age
gap that left the singer in the cold.
Source:The Beat pull-out magazine,of The Citizen Newspaper,Tanzania
|
|
Binti wa Darasa la sita katika Shule ya Msingi Kilimani iliyopo Kipunguni, Dar mwenye umri wa miaka 12 (jina tunalihifadhi kwa sababu za kimaadili) amejikuta akishindwa kuendelea na masomo baada ya kupewa ujauzito na kijana wa mtaani aliyejulikana kwa jina moja la Roja.
Akizungumza kwa huzuni mama wa mtoto huyo, Aziza Mohammed alisema kuwa mwishoni mwa mwezi uliopita ndiyo aligundua kuwa binti yake huyo ni mjamzito na ilikuwa ni baada ya kukataa kwenda shule huku akitapika mara kwa mara. Mama huyo alisema, baada ya kuona ilibainika kuwa ana mimba, wakanipa taarifalili hizo aliamua kwenda kununua kifaa cha kupimia mimba lakini mwanaye huyo alikimbilia kwa mama yake mdogo, Temeke ambako waligundua kuwa ni mjamzito. “Alipofika kwa mama yake mdogo, nikawaomba wamlete kisha tukampeleka hospitali ambako tulithibitishiwa na daktari kuwa kweli ana ujauzito wa miezi mitano,” alisema mama huyo na kuongeza: “Nilimbana aniambie mwenye mzigo huo ambapo alimtaja kijana aitwaye Roja. Akaniambia kijana huyo ambaye ni jirani yetu amekuwa akimbaka na kumtishia kumuua ikiwa atasema. “Kwa maelezo hayo ilibidi tumtaarifu mjumbe wa mtaa wa Kipunguni B, Bakari Issa ambaye tulikwenda naye kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Stakishari na kufungua jalada la kesi lenye namba STK/RB/18639/2013 KUMPA MWANAFUNZI MIMBA “Jamani naomba taasisi husika zinisaidie kwa sababu baada ya kutoa ripoti polisi nimekuwa nikuzungushwa tu...mtuhumiwa hakamatwi.” SIMULIZI YA KUSIKITISHA Binti aliyepata dhahama hiyo alipata kuzungumza na Ijumaa ambapo alisimulia simulizi ya kusikitisha sana ikionesha jinsi mchezo mzima ulivyokuwa. Alisema: “Wadogo zake Roja ndiyo walikuwa marafiki zangu...Roja alikuwa akiwatumia wao kuniita kila siku jioni na nilipoenda alikuwa akinifungia chumbani kwake na kunilazimisha kufanya naye mapenzi huku akinitishia kuwa nikisema ataniua. “Pamoja na vitisho hivyo alikuwa akinipa shilingi elfu tatu hivyo nikawa naogopa kumwambia mama na nilipogundua nina mimba nilimtuma wifi yangu (dada wa Roja) akamwambie lakini akakataa na kusema mimba siyo ya ndugu yake, mimi sijawahi kufanya mapenzi na mwanaume mwingine zaidi yake,” alisema binti huyo. KUTOKA IJUMAA Tukio hili linaumiza na kusikitisha. Ni wito wetu kwa taasisi husika kufuatilia sakata hili na kumsaidia binti huyu ambaye ndoto zake zimezimwa ghafla akiwa bado mdogo. Aidha, ni vyema wazazi wakawa makini katika kufuatilia nyendo za watoto wao kabla mambo mabaya hayajawakuta |
|
|
|
KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga, Ernest Brandts, amesema kuifunga Simba katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom itakayochezwa Oktoba 20 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ni kazi rahisi.
Brandts amewatoa hofu viongozi na mashabiki wa Yanga, huku akitamba kupata ushindi dhidi ya mahasimu wao Simba. Akizungumza na RAI jana, Brandts alisema Simba hawamtishi kwa kuwa ana kikosi bora ambacho kina kila sababu ya kushinda mechi hiyo. Alisema amekuwa akiifuatilia Simba mara nyingi inapocheza mechi na hakuna ushindani ambao umekuwa ukionyeshwa na wachezaji wa timu hiyo, licha ya kupata ushindi katika mechi zake. “Simba hawana kiwango kikubwa, wanabebwa na mabao ambayo kwa bahati wamekuwa wakifunga, kikosi changu mimi ni bora, wachezaji wangu wana nguvu za kutosha na uwezo zaidi kuhakikisha tunashinda,” alisema. Yanga tayari imewasili Bukoba kwa ajili ya mechi yao dhidi ya Kagera Sugar itakayochezwa kesho kwenye Uwanja wa Kaitaba. Source:Rai. |
|
KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa ameikumbuka timu yake ya zamani ya Azam FC baada ya kuonekana akiwa kwenye Uwanja wa Chamazi Complex nje ya jiji la Dar es Salaam.
Ngassa, ambaye awali aliuzwa na Yanga kwenda Azam FC kwa kitita cha pauni milioni 98, miaka mitatu iliyopita kabla ya kurudi msimu huu, juzi alitua kwenye Uwanja wa Chamazi na kushuhudia mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya wenyeji na Mgambo Shooting. Ngassa aliyeondoka Azam FC kwa mgogoro huku timu hiyo ikimpeleka Simba, alikuwa kivutio na wengi walianza kuonyeshana alipokuwa amekaa jukwaani. Baada ya kufika uwanjani hapo, moja kwa moja Ngassa alikwenda kukaa alipokuwa amekaa mshambuliaji wa Azam FC, Gaudence Mwaikimba waliyewahi kukipiga pamoja Jangwani. Mara baada ya mechi hiyo, kiungo huyo aliyerudi kwa kasi katika Klabu ya Yanga, kwa kuifungia bao moja mpaka sasa, alisalimiana na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo na kuondoka zake. Ngassa alipoulizwa sababu za kwenda uwanjani hapo alisema kwa ufupi: “Nimekuja kutembea tu.” Tayari Ngassa yupo mjini Bukoba kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya wenyeji Kagera Sugar, kesho. GPL |
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amemuonya Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli kwa mara nyingine tena kuacha tabia ya kufanya uamuzi wa jambo lolote bila kushirikisha pande zinazohusika.Mbali ya karipio hilo, Waziri Mkuu amewataka viongozi wengine wa Serikali, kuepuka mfumo usio shirikishi katika uamuzi wao kwa kuwa unasababisha migogoro ndani ya jamii na usumbufu kwa Serikali. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya mgomo wa wasafirishaji wa mizigo na abiria ulioanza Oktoba 5, mwaka huu, Pinda alisema Serikali imeamua kurejesha kwa muda wa mwezi mmoja asilimia tano ya uzito wa mizigo uliozidi kwenye mizani. Alisema hatua zilizochukuliwa na Dk. Magufuli kufuta vifungu vilivyokuwa vikiruhusu asilimia tano zilifuata sheria, lakini tatizo lililojitokeza ni kutoshirikisha pande zinazohusika ili kushauriana na kupata uamuzi wa pamoja. Alisema mbali ya kutoshirikisha pande hizo, uamuzi wa Dk. Magufuli ulikuwa wa ghafla kwa wasafirishaji kitendo ambacho kimewapa wakati mgumu wa utekelezaji, kwa sababu wafanyabiashara walikuwa wameingia mikataba na wateja wao. “Chimbuko la mgogoro huu, ni tangazo la Dk. Magufuli alilotoa Oktoba mosi, mwaka huu la kuondoa ofa ya asilimia ya uzito uliozidi, baada ya uamuzi huo wadau wa usafirishaji wa malori na mabasi waliingia kwenye mgomo na kulalamikia hatua hiyo. “Kutokana na mgogoro huu, nililazimika kukutana na Dk. Magufuli, baadhi ya mawaziri wa wizara zenye uhusiano na masuala haya, wanasheria na wataalamu wa masuala ya usafiri na uchumi. “Kilichoongeza mgogoro ni tafsiri ya vifungu vya sheria na kwenye kanuni ya 7 (2) na 7(3) ambacho kinaeleza wasafirishaji wa magari yenye uzito uliozidi, lakini upo ndani ya asilimia tano ya uzito unaokubaliwa kisheria, wanatakiwa kupunguza mzigo, kupinga na iwapo watashindwa kutekeleza, watatakiwa kulipia mara nne ya tozo za kawaida. “Sasa suala la asilimia tano, lilitokana na ombi la wadau wa usafirishaji kwa aliyekuwa waziri wa Ujenzi miaka ya nyuma na halikuwa sheria kamili, ndio maana limeondolewa baada ya kuonekana linatumiwa vibaya. “Nakubaliana na Dk. Magufuli, wapo baadhi ya wasafirishaji ni wakorofi na hawataki kufuata sheria…ndio maana walifanya mazoea ingawa wapo wengine wazuri na hao nawapongeza sana kutii sheria.
Mtanzania.
|
|
MTAYARISHAJI mahiri wa muziki wa Kizazi kipya, anayemiliki studio za ya B Hits, Hermes Bariki ‘Hermy B’ ameteuliwa kuwa Jaji wa shindano la kusaka vipaji vya kuimba Afrika Mashariki la Tusker Project Fame.
Mkali huyo anayemiliki studio za B Hits, ataiwakilisha Tanzania na kwa kuungana na majaji wengine jijini Nairobi, nchini Kenya akichukua nafasi ya Zahir Zorro aliyekuwa Jaji katika shughuli ya kusimamia usaili wa shindano hilo. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja wa bia ya Tusker, Sialouise Shayo, alisema katika kuelekea awamu ya kwanza ya shindano hilo msimu huu wa sita, wamejipanga kuhakikisha Watanzania wanahusishwa kikamilifu. “Kama tunavyomkaribisha Jaji mpya Hermy B ambaye amekuwa katika kinyang’nyiro hiki cha Tusker Project Fame kwa muda mrefu, tunatumia fursa hii kuwatangazia Watanzania kuwa tumejifunza mengi kupitia kwa Zorro,” alisema. Katika shindano hilo, Tanzania inawakilishwa na Angela Karashani, Elisha Simon, Mgeni Kalinga na Ussa Dubart. Kwa upande wake, Hermy B aliishukuru Tusker kwa kumchagua kuwa Jaji katika shindano hilo kwa mara ya sita pamoja na Zahir Zorro. Mshindi wa Tusker Project Fame atajinyakulia Sh 100, 000, 000 na mkataba wa kurekodi utakaogharimu Sh 200, 000, 000. |
Subscribe to:
Posts (Atom)







.jpg)
.jpg)

















