advert

http://

Thursday, 10 October 2013

WEMA SEPETU NA DIAMOND PLATNUMZ MAMBO MAZITO.PENZI LIKO PALEPALE.



Baada ya habari kuenea kuwa Diamond PLatnumz amerudiana na Wema walipokuwa Malaysia katika moja ya show zake na Platnumz kukanusha habari hiyo kupitia website yake, hatimaye BK imepata picha nyingi za Diamond na C.E.O wa Endless Fame Wema Sepetu wakiwa kwenye pozi tofauti tofauti za kimahaba nchini humo.

Baadhi ya picha hizo, moja inawaonesha Diamond na Wema wakiwa wamevaa Mapajama (nguo za kulalia) sehemu kama hotelini hivi na nyingine ikimuonesha Diamond akim-kiss Wema wakiwa kitaa. Lakini Diamond ni real boyfriend wa Penny…

Nimepata shida kidogo kuamini hii habari na picha coz nimeitoa kwenye blog ingine ikanibidi nichimbe kidogo ili nione kama ni kweli manake nilihisi hizo picha ni za zamani wakiwa na wema....nimetafuta picha ingine ya diamond ambayo alipiga juzi juzi wakati haya maneno yakiongelewa na kuziowanisha ..na nimegundua mtindo wa nywele ni ule ule kwa picha zote ona hii picha chini alafu fananisha na picha za juu....Au ndio wanacheza Movie??

Picha akiwa na Penny baada ya kutoka Malaysia....

Rapper Nay Wa Mitego amesema amekuwa akisumbuliwa mno na maafisa usalama pamoja na vyombo mbalimbali vya habari wanaomdhania kuwa anajihusisha na biashara ya madaya ya kulevya kitu ambacho amekuwa akikanusha kwamba sio kweli.


Nay amesema anasikitishwa kupokea taarifa zinazodai kuwa anajihusisha na biashara hiyo haramu, kitu ambacho hakifanyi kwakuwa anategemea shughuli zake za muziki zinazomlipa vizuri.

“Watu wamekuwa wakishangaa sifanyi show hata mwaka mzima lakini maisha yanaenda namiliki gari ndio maana wanaongea mengi huku media na maafisa usalama wananichunguza kila siku,” alisema Nay.

Pia msanii huyo wa Salam Zao, amesema yupo kwenye maongezi na kampuni ya simu ili imfanye kama balozi wake.


“Nasubiria mambo yangu yaende poa, nimeingia mkataba wa kuwa balozi wa mtandao wa simu hapa nchini bado muda wake kuuweka wazi kwasababu tupo kwenye makubaliano zaidi na pia ikifika muda nataka kuanika vyanzo vyangu vyote vya mapato, ” alisema

Ikiwa ni wiki chache toka kesi ya Agnes Gerald a.k.a Masogange ya kutuhumiwa kusafirisha dawa za kulevya kuisha kwa kulipa faini nchini Afrika Kusini na kuwa mtu huru, hatimaye juzi Jumanne amerejea nyumbani Tanzania.


Kupitia Instagram juzi Agnes alipost picha (hapo juu) akiwa uwanja wa ndege na kuandika “am cmng homeeeeeeeee”.

Mwishoni mwa mwezi uliopita (September) mrembo huyo aliachiwa huru pamoja na mdogo wake Melissa Edward ambaye mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg, Afrika Kusini ilimuachia huru baada ya kukosa ushahidi wa kumtia hatiani.

Kama tunakumbuka vizuri mwaka 2010 Puff Daddy alishawahi kusema kuwa analaumu maisha yake ya utotoni hakupata malezi ya Baba ndio maana mpaka sasa hana mpango wa kuwa na mke sababu anaogopa kuwa kama Baba yake,hivi karibuni kaongea mapya kuhusu ndoa.


Rapper Na mfanya biashara mkubwa Marekani Puff Daddy maarufu sasa kama  Pdd amesema hana mpango wa kufunga ndoa siku za karibuni kwani anaamini kuwa watu wengi hutumia muda mwingi kuboresha ndoa badala ya kuwa na maisha yenye furaha na mtu anaye mpenda.

Pdd anaendela kusema kuwa mpaka sasa hajapata sababu za kuwa na mke ila anapenda sana watoto wake na familia yake na Bado Yupo yupo.

Fahamu kuwa Puff Daddy kwa sasa ana mahusiano ya muda mrefu na msanii wa Rnb Cassie ambaye yupo chini ya lebel yake Ya Bad Boys Entertainment

 Klabu ya Sunderland ya Egland imemteua Kocha wa zamani wa Brighton, Gus Poyet kuwa kocha mpya wa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili.
Klabu hiyo ambayo inajulikana kama "The Black Cats " inashikilia mkia katika ligi kuu ya Premier na ilimuondosha kazini Paolo Di Canio mnamo mwezi wa September baada ya kushikilia nafasi hiyo kwa mechi 13 tu.
"nina hamu ya kuwathibitishia uwezo wangu mashabiki--ninataka wawe na imani kwa sababu tunahitaji kushikamana " Poyet, mwenye umri wa miaka 45, ameiambia wavuti wa klabu hiyo.
Ataungana na wasaidizi wake za zamani wa Brighton, Mauricio Taricco na Charlie Oatway.
"Nadhani msingi wa mafanikio yangu katika mechi za nyumbani Brighton ni uhusiano wangu na mashabiki, --na naweza kuona hali hiyo hiyo hapa ,"aliongeza Poyet, ambaye alipigwa kalamu na Brighton mnamo mwezi wa Juni.
"ni changamoto kubwa lakini inanipa motisha na nashukuru kwa kupata fursa hii ya kuongoza katika ligi kuu"
Poyet ambaye ni mchezaji wa zamani wa taifa wa timu ya Uruguay atakua meneja wa sita wa Sunderland katika kipindi cha miaka mitano.
Kocha msaidizi wa Sunderland Kevin Ball amekua akishikilia uongozi wa klabu hiyo tangu Di Canio afutwe kazi kutokana na malalamiko ya wachezaji.

 Mke wa rapper Wiz Khalifa, Amber Rose amekata mtindo mpya wa nywele na kuwapa mashabiki nafasi ya kutoa maoni yao kuhusu mtindo huu kwenye instagram yake. Mtindo huu ameuita Zig Zag. 


 

 Daniel amekuwa kinyozi wa Bale toka siku ya kwanza ameanza kuichezea Tottenham.Jamaa ni kinyozi anaye aminika sana na mastaa wa soka nchini Uingereza kwa ujuzi na ubunifu wake wa mitindo tofauti ya nywele. 


Pia anauwezo wa kusikiliza na kufanya anacho taka mteja wake bila tatizo.
Picha Zingine Zipo Hapa 
Daniel Akiwa na Mchezaji Wa Man Untd Rooney.
Daniel Akiwa na Mchezaji Wa Man Untd Rio Ferdinand.
Hapa Daniel alikuwa amemaliza kumnyoa Mario Balotelli
Ashley Young
Jermain Defoe

Rais wa Cameroon Paul Biya amemshawishi mshambuliajhi Samuel Eto'o kufikiria kwa mara nyingine juu ya maamuzi yake ya kustaafu soka la kimataifa.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Cameroon na klabu ya  Chelsea alikutana na wawakilishi wa Rais Biya jijini Yaounde wakijadili juu ya hatima ya baadaye ya mshambuliaji huyo.

Baada ya kukutana hatimaye Eto'o, amekubali kurejea kuitumikia tena Cameroon. 
Sasa anatarajiwa kusafiri kuelekea Ufaransa kujiunga na kikosi cha timu hiyo ambacho kinajiandaa kwa ajili ya mchezo wa hatua ya mwisho kusaka tiketi ya kufuzu kombe la dunia wakikabiliwa na mchezo dhidi ya Tunisia.

Eto'o mwenye umri wa miaka 32 hapo kabla aliwaambia wachezaji wenzake kuwa hana nia ya kuendelea kuitumikia Cameroon kauli ambayo aliitoa baada ya mchezo dhidi ya Libya ambao walishinda na kusonga mbele katika hatua ya mwisho ya mtono.
 
Licha ya taarifa za kujiondoa kikosini, bado kocha wa kikosi hicho Volker Finke ameendelea kumtaja mchezaji huyo katika kikosi chake kitakacho vaana na Tunisia kwani alikuwa bado hajawasilisha taarifa rasmi ya tangazo lake hilo.
Eto'o amekuwa hana mahusinao mazuri na mamlaka ya soka ya nchi yake tangu huko nyuma ambapo akiwa nahodha aliongoza mgomo wa kudai posho kiasi hata kuvuruga mchezo wa kirafiki dhidi ya Algeria mwaka 2011.
Tukio hilo lilipelekea kufungiwa kwa michezo 15 kabla ya adhabu hiyo kupunguzwa na kuwa miezi minane.
Hii si mara ya kwanza kwa Rais Biya kukatisha majaribio ya kustaafu kwa wachezaji, kwani aliwahi kufanya hivyo kwa Roger Milla ambaye alirejea dimbani katika fainali za kombe la dunia mwaka 1990 nchini Italia.

Baada ya miaka 12 ya kuwa Boy Friend Na Girl Friend na kupata mtoto moja wa kiume mwenye umri wa miaka mitano sasa, inasemekana rapper Fabolous amejipanga kwa ndoa.


Hii ni baada ya mpenzi wake wa muda mrefu Emily B kuonyesha pete yake ya uchumba aliyovalishwa na rapper huyo.

Msanii wa kike kutoka Tanzania mwenye uwezo mkubwa wa kufanya muziki  wowote 'Shaa' ametia wino kwenye mkataba wa miezi sita na Saidi Fella kupitia Mkubwa Na Wanawe.
Saidi Fella amesema leo  kuwa mkataba huu ni wa muda mfupi na watafanya kazi tofauti na Shaa sababu anauwezo mkubwa wa kuimba na kufundisha muziki.

Saidi Fella amesema wamefanya mazungumzo na Aliyekuwa manager wa Shaa 'Master J' na wamekubaliana kuwa atafanya kazi na mkubwa na wanawe kwa misingi yao na baraka zote wamepewa.

Bab Tale amekuwa akifanya kazi na Shaa kwa muda sasa na kuhamia kwa Said Fella kutaka msaidi zaidi Shaa kuteka soko la nyumbani zaidi. Shaa amekuwa moja ya  wasanii Kutoka Tanzania mwenye mashabiki wengi nje ya nchi yake.

Awali Shaa aliwahi kufanya kasimamiwa na  Ay Na Master J. I Hope hizi ngoma mbili kutoka kwa Shaa zitatisha sana hapa Tanzania, Moja amefanya na At na Nyingine Na Rapper Shetta.

Shaa amesema haya ni maamuzi mazuri na yataongeza sana mashabiki wa muziki wake Nyumbani.
Star wa Basketball Wives LA Malaysia Pargo amegundua njia nyingine nzuri ya kumbana mume au mke wako. Hii itasaidi zaidi wale wana ndoa wanaopenda kuvua pete wakati wana saliti ndoa zao.
Pete hii unayoiva kwenye kidole chako cha ndoa inabakiza neno MARRIED Kwenye kidole chako so ata ukitoa bado unaye mdanganya atajua tu kuwa upo kwenye ndoa.

Malaysia amesema wanaume husema wanapenda kuvua pete wakiwa Kwenye mazoezi 'Gym' na muda mwingine wana sahau kuzirudishia kidoleni.

Malaysia amesema tayari ametengeneza Pete moja kwa ajili ya mume wake na ndio hio kwenye picha.

Waombolezaji walikua wamejaa katika msiba wa mpiga misele (drifter or spinner) maarufu Bongani Makhubo (40) jijini Pretoria, Afrika Kusini.

Baada ya mazishi, wapiga misele wenzie wakaanza kupiga misele na magari yao kama kumtolea heshima marehemu, huku wahudhuriaji wakishangilia.

Ghafla binti huyu akavua chupi yake na kuipunga hewani huku akidansi katikati ya magari yanayozunguka kupiga misele


Baadhi ya waombolezaji walikerwa na kitendo hicho lakini cha ajabu wengi walimuacha aendelee na walikua wakishangilia

Wimbo huu hapa chini nloikuta leo youtube na tayari  imetazamwa na Watu zaidi ya elf 50 ni kituko kwa sababu Diamond hawezi kamwe kumshirikisha Tanzanite wakati wana Bonge La Bif.


Tanzanite ndo yule msanii alokopy wimbo wa Diamond uitwao Tatizo kwetu Mbagala na kuiita Uchawi naWanga.

Tangia hapo Diamond alimchukia mno huyo mtoto.Sasa huu wimbo eti wamefanya Pamoja.Inaitwa MAPENZI-DIAMOND FT TANZANITE.Tetesi ni kwamba Tanzanite aliipata juu kwa juu huu wimbo na kuamua kuingia studio na kuweka mashairi zake.Ni ngoma ambayo ilikuwa bado haijakamilika na Diamond hakutaka kuitoa kwa sasa.Tanzanite akamzidi ujanja!!

TAZAMA MWENYEWE HAPA CHINI UJIONEE VITUKO.



Mauaji ya kikatili yanayodaiwa kufanywa na Kikundi cha Chinjachinja dhidi ya vikongwe, yamezidi kuutikisa Mkoa wa Geita baada ya kikongwe mwingine, kuuawa kwa kukatwa kwa mapanga akiwa nyumbani kwake.


Marehemu huyo ametajwa kuwa ni, Maua Ikoti(60) mkazi wa Kasang'hwa, wilayani Geita .

Mauaji hayo yamekuja huku takwimu zikionyesha kuwa  vikongwe watatu, wameuawa na kikundi hicho katika kipindi cha wiki nne zilizopita.

Baadhi ya watu wanahusisha maujai hayo  na imani za kishirikina.

Tukio la mauaji hayo lilitokea saa 6 usiku wa kuamkia juzi  baada ya wauaji  kuvamia familia hiyo na kisha kuingia ndani ya chumba alimokuwa amekala kikongwe huyo.

Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kasang'hwa, Maganiko Ndiomali, alisema wauaji walimkata kwa mapanga kikongwe huyo kichwani,mikono na kwenye matiti.

Alisema pamoja na mayowe yaliyopigwa na watoto wa marehemu ili kuomba msaada, juhudi za wananchi kuwasaka wauaji hazikuzaa matunda.

Kuna madai kuwa kikundi kinachohusishwa na mauaji hayo kimekuwa kikodiwa na baadhi ya watu ili kulipiza kisasi baada ya kufiwa na ndugu zao wakiamini kwamba wamerogwa.

Kikundi hicho kinadaiwa kuhusika na mauaji ya kikatili dhidi ya Mondesta Nchambi (53) mkazi wa kitongoji cha Isabilo wilayani Chato kwa kumchinja mithili ya kuku.


Kamanda wa polisi mkoani Geita,Leonard Paulo alithibitisha kuwepo kwa matukio hayo lakini alisema hadi sasa hakuna mtu au watu waliokamatwa wakihusishwa na mauaji hayo.



Source-Mwananchi
MAKOMANDOO sita wa Jeshi la Marekani, wakiwamo wawili walioshiriki kumuua Kiongozi wa Al Qaeda, Osama bin Laden, wamefanikiwa kumuua kinara wa kundi la Al Shabaab anayedaiwa kupanga mashambulizi ya kigaidi katika jengo la biashara la Westgate mjini Nairobi nchini Kenya mwezi uliopita na kusababisha vifo vya watu 68 na wengine zaidi ya 175 kujeruhiwa.


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, aliyeko ziarani nchini Indonesia, aliwaambia waandishi wa habari jana, kuwa gaidi huyo aliuawa wakati wa mapambano kati yake na makomandoo hao. Hata hivyo, hakumtaja jina.

John Kerry alisema “Jumamosi iliyopita, makamandoo hao wa Marekani, walishambulia nyumba ya kiongozi huyo mjini Barawe, Somalia. Mashambulizi yaliyofanywa na wanajeshi wa kikosi maalumu cha Marekani nchini Libya na Somalia, yanaonyesha dhamira ya Serikali ya Marekani kuwasaka magaidi.”

Alisema kwamba, taarifa za kiintelijensia, zinaonyesha kinara huyo ambaye alikuwa mshirika mkuu wa Kundi la Al-Shabaab, alihusika moja kwa moja katika shambulio la kigaidi katika jumba la maduka la Westgate.

Kerry alisema kwamba, baada ya kumaliza kazi hiyo, wanajeshi hao waliondoka mjini Barawe na kurudi Marekani.


Ni katika operesheni hii ambapo pia makomandoo wa Marekani walimkamata kiongozi wa Kundi la Al-Qaeda, Anas al Libi katika mji mkuu wa Libya, Tripoli. Anas al-Liby, anahusishwa na matukio mengi makubwa yakiwamo ya kuwavizia watu wenye asili ya Marekani kuwakamata na kuwafanyia vitendo vya kinyama

HATIMAYE Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, ameweka wazi mshahara wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Zitto ameutaja mshahara huo wa Pinda anayejitambulisha kama ‘mtoto wa mkulima’ juzi mjini Mpanda na jana wilayani Sikonge wakati akihutubia mikutano ya hadhara katika ziara ya Kanda ya Magharibi kwa ajili ya ujenzi wa chama.

Alisema Pinda anapokea jumla ya sh milioni 26, ambazo ni kiasi kikubwa kulinganisha na uchumi wa nchi.

Akichanganua alisema Pinda anapokea sh mil. 11.2 kama mbunge, sh mil. 8 kwa nafasi ya waziri na kiasi kinachosalia kufikia sh mil. 26 kwa nafasi yake ya uwaziri mkuu.

Alisema sababu hiyo ya mishahara mikubwa isiyokatwa kodi ndiyo huwafanya viongozi wa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa wakali pale vyombo vya habari vinapotaka kuwafahamisha wananchi namna watumishi wao wanavyojilipa.

“Nimeanza na mshahara wa waziri mkuu pia siku zijazo nitataja na wa rais, kwa kuwa amesaini makubaliano na Serikali ya Marekani kuendesha nchi kwa uwazi, na moja ya uwazi ni kwa muajiri kujua kiasi anachomlipa mwajiriwa wake,” alisema Zitto.

Hatua ya Zitto imekuja baada ya kuwapo mvutano mkubwa kuhusiana na kile kinachodaiwa ‘usiri’ wa mishahara ya watumishi wa umma, wakati ni haki ya walipa kodi kujua kile wanachowalipa walioomba kuwaongoza.

Kodi ya laini za simu

Akizungumzia sakata la kodi katika laini za simu, Zitto alisema CCM ina ajenda ya kisiasa kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2015.

Alisema serikali baada ya kubaini watu wengi wanapeana taarifa kwa njia ya ujumbe mfupi, hususan katika masuala ya kisiasa, wakaona njia sahihi ya kudhibiti ni kuwatoza kodi ya laini ili kupunguza hatari ya mawasiliano hayo kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao.

“Sikuwepo bungeni wakati wabunge wa CCM wanapitisha kadhia hiyo ya kuwanyonya wananchi, wenzangu wakaniambai tukasema hapana, kwa maana tuliona hii leo kuna Watanzania wengi wasio na uwezo wa kuhudumia simu kwa kiasi cha sh 1,000 kwa mwezi,” alisema Zitto.

Akijibu maswali ya wananchi mjini Mpanda waliotaka kujua sababu ya kupunguza makali bungeni, Zitto alisema hakuna makali yaliyopungua bali ni mitazamo ya watu.

Alisema kwa kushirikiana na wabunge wenzake wa upinzani wamekuwa wakisimamia hoja zenye manufaa kwa wananachi huku wabunge wanaojipambanua kuwa majasiri kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwaunga mkono wazi wazi.

Akiwa  wilayani Sikonge, Zitto alisema Watanzania hawawezi kujivunia uhuru huku mama zao, watoto wao na wazee wao wakiwa hawana uhakika wa kupata huduma bora ya afya, elimu na maji safi.

Alisema kwa sasa Tanzania ni taifa moja lililogawanyika katika nchi mbili za wenye fedha na wasio na fedha.


Alisema nchi ya wenye fedha, fam

Wednesday, 9 October 2013

MAAJABU YA MTOTO ALIYEFUFUKA MENGI YAJITOKEZA BAADA YA KABURI KUFUFULIWA

.

Stori:Victor Bariety, Geita 
TUKIO la mtoto Shaaban Maulid, 16, aliyefariki dunia miaka mwili iliyopita kabla ya mwaka huu kuonekana (kufufuka), limeendelea kutikisa baada ya maajabu mengine kujiri.


Shaaban, alifariki dunia na kuzikwa Januari, 2011 lakini Septemba 30, mwaka huu, alionekana akiwa hai, ingawa alikuwa akizungumza kwa taabu.
Kwa vile kufufuka kwa Shaaban ni jambo lililoacha wazi midomo ya wengi hususan waliohudhuria mazishi yake miaka miwili iliyopita, ilibidi kaburi alilozikwa lifukuliwe ili ndani yake ijulikane kuna nini.
Tamko la kufukua kaburi la Shaaban ni azimio la kifamilia, hasa baada ya ndugu na majirani kupendekeza, kwani kufufuka kwake, kulivuruga vichwa vingi, wapo walioamini inawezekana, ila wengine wakipinga kwamba mtoto huyo aliyeibuka sasa ni mzimu tu.

MAUZAUZA KABURINI
Shaaban alizikwa kwenye eneo la nyumba ya baba yake, Maulid Shaaban, kwa hiyo haikuwa shida kulipata kaburi, kwani familia nzima na hata majirani wanalijua kwa sababu walishiriki kumzika.
Jumatano iliyopita, shughuli ya kufukua kaburi la Shaaban ilifanyika. Kazi hiyo ilianza saa 2 asubuhi chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi, kabla ya kukamilika saa 4.30 asubuhi.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa kipindi chote ambacho ufukuaji ulifanyika, mauzauza mengi yalitokea, hivyo kusababisha taharuki na hata watu wengine kutimua mbio.
Wakati shughuli ya ufukuaji ikiwa mbichi kabisa, alitokea mbwa kutoka kusikojulikana ambaye alifika na kuanza  kujigalagaza juu ya kaburi hilo, huku akibweka. 
Hali hiyo, ilitafsiriwa na wengi kwamba mbwa huyo alikuwa hataki kaburi hilo lifukuliwe, ingawa baadaye aliondoka taratibu akibweka na kutokomea kusikojulikana.
Saa 2.30 asubuhi wakati ufukuaji ukiendelea, mwanamke jirani anayeitwa Sharifa Hitler, alianguka na kupoteza fahamu, kabla ya kuzinduka dakika 20 baadaye, kufuatia jitihada za kumuwekea kipande cha sabuni mkononi.
Baada ya kuzinduka, Sharifa alisema kuwa alisikia kichwa kinakuwa kizito, akapatwa na kizunguzungu kisha akapoteza fahamu.
Saa 3.05 asubuhi, tukio lingine litokea, kwani kipindi kaburi linafukuliwa, ukuta wa nyumba ya baba yake Shaaban, nao ulianguka na kutoa sauti yenye mshindo mkubwa.
Sauti hiyo iliwatisha wengi, kwa hiyo watu walikimbia kwa kutawanyika, kila mmoja akishika uelekeo wake.
Kuanguka kwa ukuta huo, kulifanya kazi ya kufukua kaburi isitishwe kwa muda ili kutawanya kifusi cha ukuta wa nyumba, kuhakiki kama kuna mtu aliangukiwa na kufunikwa.
Hata hivyo, baadaye iliamriwa mambo yote mawili yafanyike kwa wakati mmoja, baadhi wahusike na utawanyaji wa kifusi na wengine waendelee kufukua kaburi ili kwenda na muda.

MAAJABU NDANI YA KABURI
Kule kwenye kifusi, ilionekana hakukuwa na tatizo lolote lakini kwenye kaburi baada ya ufukuaji kukamilika, mambo yaliyoonekana ni haya;
Mosi; kwa mila za Kiislam, ndani ya kaburi, kuna sehemu ndogo ambayo huchimbwa kulingana na kimo cha marehemu, kisha kulazwa ndani yake.
Sehemu hiyo huitwa mwanandani, kwa hiyo baada ya kufukua, badala ya kukuta mwili, wafukuaji walikutana na chungu kikubwa.
Pili; kile chungu kilikuwa kimefunikwa na mifuko aina ya viroba. Tafsiri ya wengi walioshuhudia tukio hilo ni kwamba sanda aliyozikwa nayo Shaaban miaka miwili iliyopita, ndiyo iliyogeuka kiroba.
Tatu; ndani ya chungu kulikuwa na mifupa ya kiumbe cha ajabu, kwani kwa muonekano haifanani na ya binadamu wala mnyama yeyote anayefahamika, kwani ilikuwa ni midogomidogo mno.
Nne; kulikuwa na madawa yenye umbo la kimimika, rangi nyeusi.
Dunia Mrisho ambaye alikuwa shuhuda wa tukio hilo na alikuwepo miaka miwili iliyopita wakati Shaaban akizikwa, alisema kuwa yaliyoonekana ndani ya kaburi hilo, yamewashangaza wengi.
“Huyu mtoto tulimzika kwa heshima zote za Kiislam na mwili wake ulikuwa kwenye sanda, hii mifuko ndani ya kaburi imetoka wapi? Tunashangaa pia kukuta chungu ndani ya kaburi na kina mifupa na yule mbwa aliyetokea na kutokomea ni wa nani? Hapa kuna kitu,” alisema Dunia ambaye ni mmoja wa wakazi wa eneo hilo.

KWANI SHAABAN ALIKUFAJE?
Januari Mosi, 2011, Shaaban akiwa na afya njema kabisa, aliondoka nyumbani kwao asubuhi kwenda kuchunga mbuzi kwenye malisho.
Tangu siku hiyo, Shaaban hakuonekana tena, ingawa jitihada za kumtafuta zilifanyika kwa nguvu sana kwa usimamizi wa jeshi la polisi.
Katika eneo la malisho, mbuzi alioondoka nao Shaaban walionekana wakiwa katika idadi kamili lakini mtoto huyo ndiye hakuonekana.
Siku nne baadaye, Shaaban alikutwa akiwa amefariki dunia na mwili wake ulikutwa ndani ya kisima katika Mtaa wa Mbugani, Geita.
Baada ya kujiridhisha kwamba amefariki dunia na wazazi wake kumtambua kwamba ni mtoto wao, alizikwa katika makaburi ya eneo la nyumbani kwao.

SHAABAN ALIFUFUKAJE?
Gazeti hili lilifanikiwa kuzungumza na mama mzazi wa mtoto huyo, Aziza Ramadhani, 45, ambaye alisimulia jinsi alivyoweza kumuona mtoto wake huyo akiwa hai.
“Ilikuwa Septemba 30, mwaka huu, nilikuwa naelekea sokoni kwenye shughuli zangu za kuuza mbogamboga. Ilikuwa saa 1.30 asubuhi, nikiwa Mtaa wa Nyankumbu, nilikutana na mwanangu Shaaban.
“Nilishtuka na sikuamini haraka. Nilimwita kwa jina lake, mwanangu Shaaban ni wewe? Akaniitikia kwa kutikisa kichwa. Hakuweza kutoa sauti vizuri, alikuwa anazungumza kwa taabu.
“Nilikwenda kumshika mkono kuhakikisha kuwa ni binadamu au mzimu huku nikiwa siamini kabisa kuwa ni yeye. Nilipoona kuwa ni yeye nilimpigia simu mume wangu, akaja tukamchunguza vizuri na kubaini kuwa kweli ni mtoto wetu Shaaban.
“Ni maajabu kabisa, sisi tuliamini amekufa na tukamzika miaka miwili iliyopita. Kweli hii dunia ni ya maajabu,” alisema Aziza ‘Mama Shaaban’.
Aliendelea kusema kuwa mtoto huyo alikuwa na alama ya kinundu kwenye paji la uso na mguuni ambalo ni kovu iliyosababishwa na kuchomwa na mwiba. 
Aliongeza kuwa vilevile Shaaban alikuwa na mwanya uliofanana na wa baba yake ambapo huyu alama zote hizo anazo.
Alisema kuwa walikagua alama hizo kipindi cha kuutambua mwili wake pale alipofariki dunia na kujiridhisha ndipo walipomzika.
“Baba yake alipokuja eneo la tukio, tulimpeleka hospitali kwa sababu hali yake haikuwa nzuri, mpaka sasa bado yupo hospitali akitibiwa,” alisema Aziza.

SHULENI KWAKE NAKO
Mtoto huyo aliyevuta hisia za watu wengi mjini Geita, amethibitishwa na walimu wake katika shule aliyokuwa anasoma kwamba ndiye aliyezikwa.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Mwatulole, Geita, Joseph Nungula, alisema kuwa amemwangalia Shaaban na kujiridhisha ni mwanafunzi wake yuleyule ambaye miaka miwili iliyopita zilitolewa taarifa za kifo chake na baadaye kuzikwa.
“Nimemtambua mtoto huyo kwa sura na alama, hasa ya usoni na alikuwa na mahudhurio mazuri shuleni. Pia maendeleo yake kitaaluma yalikuwa mazuri,” alisema mwalimu huyo huku akiungwa mkono na wanafunzi waliokuwa wanasoma na Shaaban.

BABA ANAZUNGUMZA
Maulid Shaaban ‘Baba Shaaban’, alisema kuwa ni kweli kabisa mtoto wao alitoweka na alipatikana akiwa ameshafariki dunia.
Aliongeza, mwili wa Shaaban ulikutwa ndani ya kisima cha maji, hivyo walitoa taarifa polisi kisha waliruhusiwa kuchukua mwili.
“Daktari alithibitisha alimkagua na kujiridhisha kwamba ameshakufa. Tukaamua kumzika kwenye kiwanja cha nyumbani kwangu, Kitongoji cha 14, Kambarage, hapa Geita.
“Shughuli zote za matanga tulifanya, baada ya hapo hatukuwa na wazo la Shaaban kurudi duniani. Leo hii kila kitu tunaona ni maajabu, Shaaban huyuhuyu ambaye tulimzika amerudi duniani,” alisema Maulid.

DAKTARI AELEZA
Shaaban amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Geita, akifanyiwa uchunguzi zaidi na matibabu zaidi kwa sababu bado hajaweza kuzungumza vizuri.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Geita, Dk. Adamu Sijaona anayemtibu mtoto huyo, alisema kuwa tayari wazazi wake wameshachukuliwa sampuli na kuhifadhiwa kwenye maabara na mifupa iliyokutwa kaburini imechukuliwa kwa uchunguzi wa DNA.
“Hali yake inaendelea vizuri hasa katika kutamka maneno ikilinganishwa na wakati anafikishwa hospitalini kwa mara ya kwanza kwa sababu alikuwa hawezi kutamka neno hata moja,” alisema Dk. Sijaona.

OFISI YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI
Mchunguzi kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Ziwa, Lukas Nduguru, aliliambia gazeti hili kuwa wamechukua vipimo vya wazazi na mtoto pamoja na baadhi ya mabaki ya mifupa iliyokuwa kwenye kaburi hilo kwa ajili ya vipimo vya vinasaba (DNA) ili kubaini mwili wa nani ulizikwa kwenye kaburi hilo.
“Ofisi ya mkemia mkuu wa serikali ilipata taarifa za huyo mtoto aliyezikwa mwaka 2011 kwamba ameonekana akiwa hai, kwa hiyo majibu ya vinasaba yatatoka ndani ya siku 14 au mwezi mmoja.
“Tuna changamoto za kukatika umeme mara kwa mara, kwa hiyo ndani ya kipindi hicho tutakuwa tumekamilisha,” alisema Dk. Ndunguru.

NENO LA KAMANDA WA POLISI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Leonard Paulo, mbali na kuthibitisha kufukuliwa kwa kaburi hilo kwa kibali maalumu cha mahakama, alisema mtu hawezi kufa kisha kufufuka kwa hiyo jeshi la polisi haliamini kama mtoto aliyezikwa ni yeye.
“Unajua hatuna imani na hili isipokuwa tunasubiri majibu ya uchunguzi wa watalaamu kutoka ofisi ya mkemia mkuu wa serikali,” alisema Paulo.

NI TUKIO LA PILI GEITA
Tukio kama hilo ni la pili kutokea katika Wilaya ya Geita katika kipindi kisichozidi miezi mitano ambapo Aprili 12, mwaka huu, mwanamke aliyetambulika kwa jina la Flora Onesmo, 45, aliyefariki dunia Februari 28, 2008 katika Hospitali ya Wilaya ya Geita kisha kuzikwa katika Kijiji cha Nakasenya, Kata ya Butundwe, alionekana akiwa hai.
Flora, alikutwa hai Aprili 12, mwaka huu, akiwa ameketi nje ya nyumba ya dada yake aitwaye Monica James, anayeishi Kijiji cha Kasamwa, Geita.

UWAZI LIPO KAZINI

Uwazi bado lina kazi ya kufanya kuhusiana na Shaaban na Flora, yapo maswali mengi hayajajibiwa, kwa hiyo lipo kazini likiibuka litakuwa na mengine mengi ambayo pengine yatakuwa mazito zaidi. MHARIRI


Source:Global publishers

Stori: Makongoro Oging’
AHADI ya Mchungaji Anthony Lusekelo au Mzee wa Upako katika msiba wa aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God  Tanzania (EAGT) Dk. Moses Kulola ya rambirambi ya shilingi milioni 15 imezua utata baada ya kiongozi huyo kutoitimiza.


Ahadi hiyo alitolewa na Mzee wa Upako siku ya kuuaga mwili wa kiongozi huyo Agosti 31, mwaka huu katika kiwanja cha Kanisa la EAGT, Temeke ambapo viongozi kadhaa wa makanisa akiwemo  Mchungaji Lusekelo walitoa ahadi zao za rambirambi.


Hata hivyo, utata unakuja kwani Mzee wa Upako mpaka Jumapili iliyopita fedha zake zilikuwa hazijafika kwa kamati husika inayoratibu rambirambi hizo.


Uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili umebaini kwamba wachungaji na maaskofu walioahidi wameshatimiza ahadi zao ndani ya siku nne baada ya kuuaga mwili lakini kwa upande wa Mzee wa Upako bado hajatimiza ahadi yake.


Mzee wa Upako ndiye mchungaji pekee aliyewashinda wenzake kwa kutangaza dau kubwa la rambirambi kiasi cha shilingi 15,000,000.


Askofu Kulola alifariki dunia  Agosti 29, mwaka huu ambapo sasa ni zaidi ya mwezi mmoja na siku kadhaa.


 Mweka Hazina wa Kanisa la EAGT kanda ya Dar es Salaam, Mchungaji Praygod Zawadi Mgonja ndiye aliteuliwa na uongozi wa kanisa hilo kuratibu, kupokea rambirambi na ndiye alikuwa akisimamia matumizi.


Gazeti hili liliwasiliana kwa njia ya simu ya kiganjani na Mchungaji Mgonja na kumuuliza kama ameshapokea mchango huo toka kwa mtumishi huyo wa Mungu ambapo alisema kwamba hajapokea na kudai kwamba huenda ameshapeleka mwenyewe kwa familia ya marehemu.


“Pamoja na kwamba ahadi hiyo kutonifikia huenda aliamua kupeleka kwa wana familia, jaribu kuwasiliana nao,”alisema Mchungaji Mgonja.


Mwandishi alimtafuta mtoto wa marehemu aitwaye Willy Kulola na alipoulizwa kama amepokea mchango wa rambirambi kutoka kwa Mzee wa Upako alisema familia haijapokea fedha hizo.
“Hatujapokea labda mumuulize Mchungaji Mgonja kwani ndiye aliteuliwa kuratibu mambo hayo,” alisema.
Mzee wa Upako alipoulizwa alikiri kuwa fedha hizo hajaziwasilisha kwa wahusika kwa madai kwamba hapendi kumpa Mchungaji Mgonja wala mtoto wa marehemu bali anataka kumkabidhi mke wa Askofu Kulola.
“Napenda taarifa hizi zimfikie 
mke wa Mzee Kulola ili anifuate na nitampa rambirambi hiyo hata kama ni kesho akija nitamuandikia cheki,” alisema.
Alipoulizwa endapo anaweza kutoa fedha hizo kwa mtoto wa marehemu, alisema hawezi kumpa labda kama atakuwa amemsindikiza mama yake.
Gazeti hili lilimtafuta tena Willy na kumweleza kuhusu majibu ya Mzee wa Upako, lakini kijana huyo wa marehemu alisema hataweza kumpeleka mama yake kwa mchungaji huyo kwa sababu bado anapokea wageni wanaokuja kuhani msiba.
“Itakuwa jambo la ajabu kwa mfiwa kuanza kuzunguka huku na kule kufuatilia rambirambi, hiyo siyo kawaida kwa mjane kukusanya rambirambi kwani kanisa liliweka utaratibu,” alisema Willy.
Katika kuaga mwili wa marehemu, Mchungaji wa kanisa la Assemblies of God Mikocheni B, Dk.Getrude Rwakatare alitangaza rambirambi zake kuwa angetoa shilingi milioni moja, akifuatiwa na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la Kawe, Mchungaji Josephat Gwajima aliyeahidi kutoa shilingi milioni 10. Wote wametimiza ahadi zao.
Baadaye alikabidhiwa kipasa sauti Mzee wa Upako ambaye alitangaza kwamba hawezi kuzidiwa na Mchungaji Gwajima, hivyo aliahidi kutoa shilingi milioni 15.

Hata hivyo, baadhi ya wachungaji na maaskofu waliamua kufanya siri ahadi zao.


Source:Global Publishers. 

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imetangaza kuanza kutumia huduma ya M-pesa katika kukusanyia marejesho ya mikopo kutoka kwa wanufaika hatua ikiwa ni katika mikakati ya bodi ya kuimarisha makusanyo ya urejeshaji wa mikopo hiyo.


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi Bw. Asangye Bangu amewaambia waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo mpya jijini Dar es salaam kwamba bodi inaendelea kujipanga kuhakikisha inaboresha njia za urejeshaji mikopo ili kuwpatia walengwa urahisi.

Amesema mojawapo ya kazi za Bodi ni kusimamia utoaji wa mikopo kwa wanafunzi waliodahiliwa kwenye vyuo vya elimu ya juu pamoja na urejeshwaji wa mikopo iliyotolewa na Serikali kwa waliokuwa wanafunzi wa elimu ya juu kuanzia mwaka 1994 mpaka sasa kwa nia ya kuufanya mfuko wa Elimu ya Juu kuwa endelevu.

"Tunayofuraha kubwa sana leo kutangaza kwamba sasa wanufaika wa mikopo ya Bodi wanauwezo wa kutumia mfumo wa M-pesa kufanya marejesho ya mikopo yao moja kwa moja kwa Bodi."Alisema Bangu

Bingu amesema bodi inaimani kuwa M-pesa itawapatia urahisi wanufaika kuweza kutimiza wajibu wao kisheria wa kurudisha mikopo waliopatiwa kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu.

Amesema wanufaika wa mikopo wanapaswa kuanza kurejesha mikopo yao mara baada ya miezi 12 kuanzia wanapohitimu masomo ya elimu ya juu au wanapositisha masomo kwa sababu yoyote ile, akiwa ameajiriwa ama hajaajiriwa.

Bingu amesema wanufaika walioajiriwa wanalipa mikopo yao kupitia kwa waajiri wao ambapo hukatwa marejesho ya mikopo kwenye mishahara yao ya kila mwezi na mwajiri huwasilisha makato hayo kwenye Bodi kupitia kwenye akaunti zake huku wale ambao sio waajiriwa hupeleka huwasilisha marejesho ya mikopo katika benki za bodi.

"Wanufaika wanaorejesha mikopo yao kwa pesa taslim wamekuwa wakipata changamoto mbalimbali wakati wa urejeshwaji wa mikopo yao kupitia kwenye akaunti za Benki ikiwa ni na benki hizo kutokuwa na matawi ya kutosha yaliyokaribu na warejeshaji wa mikopo pamoja na kutumia muda mwingi kwenye foleni."Alisema Bingu "M-pesa itapunguza changamoto hizo na hatimae kuwajengea mazingira mazuri ya urejeshwaji wa mikopo, Bodi inatangaza rasmi kuanza kutumika kwa utaratibu huu mpya wa urejeshaji kwa M-pesa kuanzia sasa."

Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Bw. Salum Mwalim amesema kuzimduliwa kwa huduma hiyo ni mwendelezo wa jinsi ambayo huduma ya M-pesa inavyorahisha miamala nchini kuzidi kuwa rahisi.

"M-pesa imekuwa suluhisho la changamoto nyingi zinazohusiana na malipo ama miamala mengine ya kijamii na kibiashara."Alisema Mwalim na kuongeza. "Ni wazi sasa hakuna atakaekuwa na usumbufu katika kulipia mkopo wake kwenye Bodi ni kiasi tu cha kupiga *150*00# na hapo anauwezo wa kufanya mrejesho wake wakati wowote mahali popote."

"Tunaishukuru Bodi kwa kuendelea kuiamini huduma yetu ya M-pesa walianza kwa kuitumia katika ukusanyaji wa ada za uombaji wa mikopo na sasa wanakwenda mbali zaidi kwa kuichagua kuitumia katika makusnayo ya marejesho ya mikopo kutoka kwa wanufaika."Aliongeza

Mwalim amesema kwa njia hiyo ni wazi sasa Bodi itashuhudia mabadiliko makubwa kwenye makusanyo ya marejesho kwa kuwa huduma hiyo imeenea nchi nzima na hasa kwa kuwa inauwezo pia wa kumuunganisha mteja na benki yake.

"Kwa mtandao mpana wa huduma hii mawakala na na mtengamano wake na mabenki na jinsi inavyotumika ni wazi mtarajie ufanisi kwa kuwa sasa mmewawezesah wanufaika wa mikopo kuwa na uwezo wa kufanya marejesho kwa njia rahisi zaidi Wakati wowote mahali popote kwa usalama na uhakika zaidi."AAliongeza


Ili mnufaika aweze kulipia kupitia M-pesa anapaswa kwanza kuhakikisha kuwa ana taairfa ya Mkpo(loan Statement),Kiwango cha Marejesho na Nambari ya Kumbukumbu amabvyo vinapatikana ofisi za Bodi hiyo ya mikopo. Taarifa hizo zitatumika Wakati w akulipia baada ya mteja kupiga *150*00# kutoka kwenye simu yake ya Vodacom na kuchagua nambari nne ambayo ni ya malipo na kuendelea na maelekezo kadri yanatakavyokuwa akiyapata kutoka kwenye simu yake ya kiganjani.
Habari tulizozipata zinasema kuwa gwiji la sanaa za vichekesho nchini, Amri Athumani 'King Majuto' ametangaza kugombea ubunge kwa 2015.


Muigizaji huyu mkongwe mzee Majuto ametangaza  kugombea ubunge jimbo la Tanga mjini.

Majuto  mwenye umri  zaidi ya miaka 60 ametangaza nia yake hiyo alipohojiwa na Clouds, na akadai atagombea kupitia CCM.

Bado tunamtafuta mzee majuto ili aweze kututhibitishia kama habari hizi ni kwa kweli au la na kama ni kweli ana mipango gani na jimbo hilo la Tanga mjini.


Je, kama ni kweli, unahisi ataweza? 

Vijana 11 wamekamatwa Mkoani Mtwara wakifanya mazoezi katika msitu wa Makolionga na CD zenye mafunzo ya kigaidi za Al Qaeda na Al Shabab pamoja na zana za hatari.


Polisi mkoani Mtwara imewakamata vijana kumi na moja wakiwa wanafanya mafunzo ya kijeshi kwa kutumia CD za Al Shabaab na Al Qaeda  katika mlima wa Makolionga...CD hizo zinaonyesha mbinu mbali mbali za kijeshi na mauaji .
 Baada ya bosi wa washika mitutu wa jiji la London Arsene Wenger kumuonya kiungo wake Jack Wilshere ambaye alikataa katakata juu ya mwenendo wake wa hovyo wa kuvuta sigara mbele ya hadhira, hatimaye kiungo huyo amekubali kosa na kuahidi kuwa haitatokea tena.
Wilshere amesema kuwa alifanya kosa baada ya kupigwa picha akivuta sigara nje ya ukumbi mmoja wa starehe huko London mida ya usiku.

Bosi wa Wenger aliweka hilo wazi Ijumaa iliyopita ambapo alikaririwa akisema hakubaliani hata kidogo na tabia hiyo na licha ya awali kiungo huyo wa kimataifa wa England kukanusha, sasa amekubali kufanya kuhukumiwa kwa kosa hilo.
Akiongea na mtandao wa klabu hiyo Wilshere amenukuliwa akisema 
"I made a mistake,"

"Players make mistakes. I'm not a smoker.

"Nimeongea na bosi na kunitaka kueleza kilichotokea na nimemueleza na hatimaye kutatua hilo na kunirejesha kikosini na nina matumaini na kumjibu kwa kufunga goli dhidi ya West Brom.

"Haitatokea tena, mimi si mvuta sigara hivyo nadhani hiyo itakuwa ni mara ya mwisho."

 Hizi picha tatu zipo kwenye baadhi ya miezi kwenye calendar hio.



STAA wa filamu za Kibongo, Wastara Juma 
Jumamosi iliyopita alikwea pipa kuelekea nchini 
Kenya ambako ana ziara ya siku nne kikazi na 
akiwa humo alipata fursa ya kupewa mguu wa 
bandia bure na wenyeji wake huku pia akiahidiwa kufanyiwa ‘
check-up’ ya mwili mzima.

Leo nimebahatika kukutana na huyu dogo aloimba wimbo ambao mpaka sasa ndo inaongoza kwa kusikilizwa na watu mtandaoni.Imesikilizwa na watu zaidi ya elf 51.Amefunika ngoma zote kali hapa Bongo.Wimbo huo amemchana kaka yake Diamond.Kaelezea maisha yake kabla hajatoka kimuziki.

Swali moja tu la msingi nlotaka kujua kutoka kwake ni Uhusiano wake na Diamond na amekiri kuwa Diamond ni kaka yake wa Damu,Baba moja Mama Tofauti na kadai Diamond kabla hajatoka kimuziki alikuwa anawajali ndugu zake ila kwa sasa hata baba yake mzazi hana muda naye.
Hivyo kadai yote aloimba kwenye huo wimbo ni ukweli mtupu.Ameomba watu kumkumbusha Diamond kukumbuka nyuma,Usuperstar ni maji ya Moto.Tazama PICHA ZAKE KATIKA POZ MBALIMBALI NA Chini kabisa ni wimbo huo ambao ishakuwa gumzo kwa kweli.



KAMA HUNA MBAVU USIDIRIKI KUSIKILIZA WIMBO HUU TAFADHALI.DOGO KAUA AJABU.NI BONGE MOJA LA NGOMA.