advert

http://

Saturday, 29 June 2013

NAIBU MKURUGENZI WA CUF ATEKWA NA WANAUSALAMA HUKO MTWARA


Naibu Mkurugenzi wa Oganaizesheni Uchaguzi na Bunge wa Chama Cha Wananchi CUF - Shaweji Mketo ametekwa na wanausalama na wanajeshi waliopiga kambi Mtwara MJINI.

Mketo alienda Mtwara MJINI jana na Leo asubuhi alihudhuria mahakamani ambapo kesi ya Mwenyekiti wa vijana CUF taifa (JUVICUF) Katani Ahmed Katani iliahirishwa.

Baada ya ahirisho hilo, Mketo alikutana na wanachama wa CUF walioko Mtwara MJINI na kufanya nao kikao cha ndani. Katika kikao hicho alielezwa namna wananchi wanavyoteswa kikatili na askari jeshi. Moja ya jambo aliloelezwa ilikuwa ni juu ya mama mmoja aliyebakwa na askari na kisha mamlaka zote zimekataa kumsaidia kuujulisha umma unyama aliofanyiwa.

Mkurugenzi wetu Mketo alipojulishwa jambo hilo aliomba akutane na mama huyo. Baada ya kikao, Mketo na viongozi waandamizi wa wilaya akiwamo mhe. Kulaga ambaye ni katibu wetu wa wilaya walianza safari ya 
kuelekea Msimbati ambako mama huyo amejisitiri baada ya kubakwa na kunyimwa msaada na vyombo vilivyopaswa kumsaidia.

Mketo alifika Msimbati na kukutana na mama huyo na akachukua ushahidi mbalimbali. Wakati wanarudi Mtwara MJINI ndipo walipotekwa na Askari jeshi. Hivi sasa ukipiga simu za Mketo 0782 095 434 na ile ya Kulaga 0789 604968 zote zinapokelewa na askari jeshi na wanajibu kwa matusi ya nguoni na kebehi za Hali ya juu.

Tumefanya juhudi za kuwasiliana na viongozi mbalimbali wa ngazi za juu wa polisi na serikali bila mafanikio. Nimempata hewani RPC wa Mtwara ambaye anakiri kuwa hajawashikilia viongozi wetu. Nimemjulisha kama wako mikononi mwa wanajeshi na wanausalama anasema hana mamlaka yoyote juu yao. HII ina maana kuwa mkuu wa Jeshi la polisi wa mkoa Leo hana dhamana ya raia wanaokamatwa na kuteswa katija eneo lake la kazi. Kama Leo Mtwara iko chini ya Jeshi la wananchi na wanatesa watakavyo, Mbona rais hajatangaza Hali ya hatari Mtwara??

Kwa taarifa zenye ushahidi, hadi sasa askari jeshi hao wameshawakamata na kuwapeleka makambini zaidi ya wananchi 100 ambapo wote hao wameteswa kinyama kwa kuvuliwa nguo zote, kumwagiwa maji mwili mzima, kupakwa chumvi mwilini na kuanza kutandikwa viboko vya miti maalum na kisha wakimaliza kuteswa huachiwa na kurudishwa uraiani kuuguza vidonda vinavyotokana na vipigo. Hakuna utawala wa sheria Mtwara, ni ubabe, ukatili na dhuluma. Hakuna mahakama wala JAJI, kila anayedhaniwa kuwa anapaswa kukamatwa lazima atakamatwa na kamwe hapelekwi mahakamani, anateswa kikatili na kuachiwa.

Kwa namna askari waliowashikilia wanavyojibu kikatili, unaweza kupata picha Mketo, Kulaga, dereva Kashinde na yeyote mwingine walivyo chini ya mateso makali ya wanyama hawa.

Tunaposema kuwa nchi hii kuna siku kila mtu atachoka tusilaumiwe. Siku hiyo itakapofika hatutasita kuamuru raia wapambane na askari kila watakapowaona, tutakapofika hapo nchi itabakia vipandevipande. Haiwezekani Leo kusini mwa Tanzania kumegeuka sehemu ya mateso, ukatili na unyama.

Tunaendelea kupambana kwa nguvu kuhakikisha kuwa serikali inawajibika, jeshi linawajibika. Hatutakubali kuona uhuru na utu wa wananchi wa nchi hii unapotezwa kwa faida za watu wachache.

Vyombo vya HABARI hivi sasa haviripoti chochote kuhusu mateso ya wananchi Mtwara. Ripoti za mateso ni Arusha, DSM na Mwanza. Nani atasimamisha ukatili huu wa watu wasio na hatia kama siyo mimi na wewe?

Mawakili wetu pamoja na mimi binafsi tunaelekea Mtwara kesho, lazima haki itendeke na tutaitafuta haki kokote na kwa njia yoyote.

J. Mtatiro,
Naibu Katibu Mkuu,
Chama Cha Wananchi CUF,
Tanzania Bara.
+255717536759.

Friday, 28 June 2013

WASHIRIKI WA REDD’S MISS KANDA YA MASHARIKI 2013 WATEMBELEA MAENEO MBALIMBALI MJINI MOROGORO

 



Na John Nditi ,Morogoro.

WAREMBO wanaoshiriki kinyang’anyiro cha Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2013 , inayoundwa na mikoa ya Pwani, Lindi, Mtwara na Morogoro, Juni 27, mwaka huu, wamefanya ziara ya kutembelea Kituo cha Amani , banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na la TACAIDS mkoa wa Morogoro.

Kituo cha Amani kilichopo katika Kata ya Chamwino, Manispaa ya Morogoro ambacho kinamilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro ni cha kuwalea Watoto wenye Ulemavu wa viungo na mtindio wa ubongo.

Washiriki hao waliongozwa na Mratibu wa Shindano hilo, Alex Nikitas pamoja na mlezi ‘ matron’ wao Kudra Lupatu, ambaapo katika Kituo hicho walipokelewa na Mkurugenzi wake Padre Beatus Sewando na wasaidizi wake.

Walielezwa historia fupi na Mkurugenzi huyo , kuwa kituo kinawapokea watoto wenye ulemavu wa aina hiyo kutoka ndani na nje ya mkoa wa Morogoro , ambapo pia walitembezwa katika vyumba vya kulala na wao pia kupata fursa ya kuuliza mswali kabla hatua ya kutoa zawadi zao kwa uongozi wa Kituo hicho.

Washiriki hao pia walitembelea baadhi ya mabanda ya maonesho kwenye uwanja wa Jamhuri wa Mjini Morogoro yanakofanyika maadhimisho ya wiki ya Serikali za Mitaa Kitaifa.

Mabanda waliyotembelea ni la Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi ( TACAIDS) mkoa wa Morogoro na baadhi yao waliamua kupima damu zao.

Washiriki hao pia walitembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na kila mmoja alipima uzito pamoja na urefu kwa lengo la kubaini uwiano wa miili yao.

Kinyang’anyiro hicho cha shindano hilo kimepangwa kufanyika Juni 29, mwaka huu kwenye ukumbi wa Hoteli ya Nashera ya mjini hapa.

Warembo 14 wanawania taji hilo ambapo shindano hilo limedhaminiwa na Redd’s Original , Michuzi Blog, Dodoma Wine, CXC Africa, Nyumbani Park, Usambara Safari Lodge,Chilakale Resorts, Big Solution , Nashera Hotel na Mikocheni Resort Centre.

Mratibu wa Shindano hilo , Nikitas, aliwataja washiriki hao ni Muzne Abduly (19), Ummy Mohamed (21), Sabra Islam (19) na Diana Laizer (21) wote kutoka Mkoa wa Morogoro.

Wengine ni Ivony Stephen (22),Pulkeriah Ndovi na (21)Zulfa Semboja (19) kutoka mkoa wa Mtwara na kutoka mkoa wa Lindi ni Janeth Awet (19), Zainabu Shaaban (23 na Sophia Maganga (21).

Mkoa wa Pwani, washiriki wake katika kinyang’anyiro hicho ni, Elizabeth Perty (22),Suleiyah Abdi (22),Easther Albert (20) pamoja na Lilian Joseph (21).
Warembo wakabidhi msaada wa mafuta ya kula.
Baadhi ya washiriki wa Redd's Miss Kanda ya Mashariki ( kushoto) wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kituo cha Amani cha watoto wenye Ulamavu wa Viongo na Mtindio wa Ubongo, Padre Beatus Sewando.
Picha ya pamoja eneo la Kituo cha Amani

MASHUJAA BAND KUTAMBULISHA WANAMUZIKI WAPYA


BENDI ya Muziki wa dansi hapa nchini Mashujaa, inatarajia kuwatambulisha wapya sita katika hafla itakayofanyika kesho katika Ukumbi wa Zhonghua Garden Morocco Jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar leo, Meneja wa bendi hiyo Martine Sospter alisema, wapya hao kutoka Kongo wanne ni wanenguaji na wawili ni waimbaji ambao watasaidiana kazi ili kuimalisha bendi hiyo. 

Sospter alisema, mbali na utambulisho huo, watatumia siku hiyo kuwashukuru Watanzania kwa kuwateua hadi kuibuka bendi bora ya mwaka katika kinyang’anyiro cha Kill Music Award 2013 kilichofanyika hivi karibuni. 

“Sisi tunamshukuru mungu kwa kutufanya kuwepo imara mpaka sasa, na hatutawaangusha mashabiki wetu kwani tunaukubali sana mchango wao wa hali na mali na ndio maana tunawaomba wajitokeze kwa wingi Jumamosi ili wajionee mambo mapya ikiwemo kuwatambulisha wasanii wapya na wanenguaji,”alisema Sospter. Aliongeza kuwa siku hiyo Msanii wa kizazi kipya Dully Sykes atawasindikiza katika hafla hiyo. 

Nae Mratibu wa bendi hiyo, Kingdodoo Bouche aliwataja wapya hao kuwa ni, Gracia Mesu a.k.a John Boko, Bosawa Fany ‘Juma Kaseja’, Jolie Kindu ‘Mrisho Ngasa’ na Patricia Nzomba ‘Mbwana Samata’ huku waimbaji akiwa ni Jimmy Adoli na Eddy Mboyo. 

Aliongeza kuwa kwa kuwa bendi yao ni imara na ni ya utaifa ndo sababu ya wanenguaji hao kutumia majina ya wachezaji wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’.~ 


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Mahinda Rajapaksa wa Srilanka muda mfupi baada ya kuweasili nchini kwa ziara ya kikazi leo asubuhi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik.
Mtoto Faith Warioba anayesoma katika shule ya awali ya Montessori jijini Dar es Salaam akimlaki kwa maua Rais Mahinda Rajapaksa wa Srilanka muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ziara ya kikazi nchini huku Rais Dkt.Jakaya Kikwete akishuhudia.
Rais wa Srilanka Mhe.Mahinda Rajapaksa akisalimia na Msaidizi wa Rais Masuala ya Kidiplomasia,Balozi Liberata Mulamula wakati Rais Kikwete alipokuwa akiwatambulisha baadhi ya viongozi na wasaidizi wake kwa mgeni wake muda mfupi baada ya kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi leo asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais wa Srilanka Mhe.Mahinda Rajapaksa wakipokea heshima za urais muda mfupi baada ya mgeni huyo kuwasili katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Rais Wa Sri Lanka Me.Mahinda Rajapaksa akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo asubuhi kwa ziara ya kikazi nchini.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Mahinda Rajapaksa wa Sri Lanka wakiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za utamaduni vilivyokuwa vikitumbuiza katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati wa shamrashamra za kumpokea mgeni huyo wakati alipowasili leo asubuhi kwa ziara ya kikazi nchini.(picha na Freddy Maro~ 

MKUTANO WA JE NIFANYEJE WA VOA WAFANYIKA MJINI DODOMA


DSC03460Dr. Mary Mwanjelwa mbunge wa Mbeya (viti maalum) mgeni rasmi katika wa mkutano wa Je Nifanyeje ulioandaliwa na VOA kwa ushirikiano na USAID akifungua rasmi mkutano huo wa vijana katika ukumbi wa African Dreamer Dodoma Jumatano. DSC03455Katika meza kuu kutoka kushoto ni Mariam Salum Msahaba (Zanzbar), Josephine Johnson Genzabuke (Kigoma),Ritta Motto Kabati (Iringa), Faida Mohamed Bakari (Kusini Pemba) IMG_2784Washiriki wa "Town Hall meeting". IMG_2770Washiriki wakifuatilia mkutano. Washiriki wakiwa na mgeni rasmi.  IMG_2778Kutoka kushoto Mariam Salum Msahaba (Zanzbar),Faida Mohamed Bakari (Kusini Pemba),Dr. Mary Mwanjelwa Mbeya, Rose Mwakitwange,Ritta Motto Kabati (Iringa) na Rais wa wanafunzi wa CBE Dodoma. IMG_2796 
Mdau Sunday Shomary akisaini kwa washiriki wa semina.



MAKAMU WA RAIS,DKT. BILAL AFUNGA MAFUNZO YA UOFISA NA UKAGUZI WA JESHI LA POLISI,CHUO CHA TAALUMA YA POLISI KURASINI JIJINI DAR LEO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa na Wahitimu wa kozi ya Uofisa na Ukaguzi wa Jeshi la Polisi leo katika Chuo cha Taaluma ya Polisi, Kurasini, Jijini Dar Es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal akimvisha Cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Mhitimu wa Kozi ya Ukaguzi wa Polisi INSP. Leah Cheyeki kwa niaba ya Wahitimu wenzake kutokana na kufanya vizuri katika Mafunzo hayo. Sherehe za kuhitimisha Mafunzo hayo zimefanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi leo Kurasini, Jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wa kozi ya Uofisa na Ukaguzi wa Polisi wakipita mbele ya Mgeni Rasmi kwa mwendo wa haraka Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayupo pichani. Sherehe za kuhitimisha Mafunzo hayo zimefanyika leo katika Chuo cha Taaluma ya Polisi, Kurasini, Jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Judo kikionesha Onesho Maalum la namna ya kupambana na Mhalifu ambaye hataki kutii amri halali ya Polisi. Sherehe za kufunga Mafunzo ya Kozi ya Uofisa na Ukaguzi wa Polisi zimefanyika Chuo cha Taaluma ya Polisi, Kurasini, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Emmanuel John Nchimbi(wa pili kutoka kushoto mwenye suit nyeusi)akiwa na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambao wamehudhuria Sherehe hizo za ufungaji Mafunzo ya Kozi ya Uofisa na Ukaguzi wa Polisi(katikati) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja.
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria Sherehe za Ufungaji Mafunzo ya Kozi ya Uofisa na Ukaguzi wa Polisi katika Chuo cha Taaluma ya Polisi, Kurasini Jijini Dar es Salaam(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza

REDD'S MISS TEMEKE 2013 MAMBO YAANZA KUNOGA


Vimwana wa Redd's Miss Temeke 2013,wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa kutangaza kuanza kwa kambi yao pamoja na Mazoezi katika Ukumbu wa TCC,Chang'ombe jijini Dar.Shindano la Redd's Miss Temeke 2013,linatarajiwa kufanyika Julai 5,2013 kwenye Ukumbi wa TCC,Chang'ombe jijini Dar es Salaam.Jumla ya Warembo 15 watachuana

MBASPO YATOA ONYO AIRTEL RISING STARS,YAITANDIKA MBEYA SEKONDARI BAO 6-0



Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki, akikagua timu wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising Stars katika mkoa wa kisoka wa Temeke ambapo Faru Boys football ilichuana na timu ya Mapambano katika mechi ya ufunguzi.
Beki wa timu ya Faru Boys Nassoro Dibagula (kushoto) akitoa mpira katika eneo la hatari mbele ya Abdalah Juma wa Mapambano katika mechi ya ufunguzi wa michuanoa ya vijana wenye umri chini ya miaka17 ya Airtel Rising Star,. Mkoa wa Temeke, uliofanyika kwenye uwanja wa Twalipo jijini Dar es Salaam Juni 25, 2013. Faru Boys ilishinda 1-0.

Timu ya Mbaspo Academy ilifanya mauaji juzi Jumanne kwa kubamiza bila huruma timu ya Mbeya Sekondari 6-0 katika mashindano yanayoendelea ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa. Mechi hiyo ilichezwa kwenye kiwanja cha Magereza mkoani Mbeya.

Washindi walifungua kitabu chao cha magoli katika dakika ya sita kupitia kwa mshambuliaji wao mahili Jackson Mwaibale aliyefunga magoli manne peke yake. Mshambuliaji huyo kinda aliifungikia tena timu yake magoli matatu katika dakika za 16, 20 na 74. Wanafunzi wa shule ya sekondari Mbeya waliokuja kushangilia timu yao walijikuta kwenye hali ya kukata tamaa baada ya timu yao kuwanyong’onyesha na wapinzani wao Mbaspo.

Peter Noah, mshambuliaji mwingine hatari wa timu ya Mbaspo, aliifungia tena timu yake katika dakika ya 30. Alikua ni yeye tena katika dakika ya 68 alipoitimisha kalamu ya magoli baada ya kuwapita walinzi wa Mbeya Sekondari na kumuacha golikipa akiduwaa baada mpira kutinga wavuni.

Kwa upande mwingine timu ya Faru Boys football walipata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya wapinzania wao Mapambano katika mechi ya ufunguzi ya ARS, katika mkoa wa Temeke uliofanyika katika uwanja wa Twalipo jumanne jioni jijini Dar es Salaam.

Timu zote zilianza mchezo kwa kasi na babada ya kosa kosa za hapa na pale hatimaye Yohana Joseph ilifanikiwa kuitoa kimasomaso timu yake alipounganisha krosi kutoka upande wa kushoto ambayo iliingia moja kwa moja wavuni. Goli hili lilipokelewa kwa furaha na washabiki wa Faru.

Mchezo mwingine wa Another Airtel Rising Stars, mkoa wa Ilala, ilichezwa kwenye kiwanja cha soka cha shule ya sekondari ya Benjamin William Mkapa ambapo timu ya Amana Shooting ilishinda 2-0 dhidi ya Msimamo Youth Academy. Magoli hayo yalipatikana kupitia kwa Isiaka Mohamed dakika ya 22 na Ally Shaban dakika ya 68.

Mkoa wa Mwanza ulitarajia kuzindua mechi zake za ARS ngazi ya mkoa leo, Juni 26 wakati Morogoro na Mbeya walitarajiwa kuendeleza na mechi za mashindano hayo leo, Juni 26, 2013.

Wakati huo huo, mkoa wa kisoka wa Kinondoni umetangaza kombaini yao ya wachezaji 15 watakaowakilisha mkoa huo kwenye mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa yatakayofanyika wenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 2 hadi 7.

Wachezaji hao ni Hamza Mohamed, Hamza Abdallah, Twalib Athuman, Fred Bakari, Hazzad Jumanne, Salim James, Abubakary Mohamed, Willy Kalolo, Didas Proches, Mustafa Yusuf, Rashid Khalifan, James Msuva, Isiaka Lukana, Ally Amin na Shabani Idd.


UCHAGUZI WA VIONGOZI WA BFT KUFANIKA JULAI 7,2013


Uchaguzi wa viongozi wa BFT uliopangwa Kufanyika tarehe 7/7/2013 jijini Mwanza, utafanyika kwa tarehe hiyo kama ulivyopangwa.

Kikao cha kamati ya utendaji ya BFT kilichofanyika juzi katika ofisi za BFT kikiongozwa na Rais wa shirikisho Joan Minja kimesisitiza kuwa uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa na haujaairishwa kama baadhi ya kikundi cha watu wachache wanaojiita wadau wanavyoweka pingamizi na kupotosha kwa kuwashawishi wajumbe wa mkutanao mkuu hasa kutoka mikoani kutohudhuria mkutano huo wa uchaguzi,kwa manufaa yao binafsi na kinyume na katiba yetu.

Upotoshaji huo unafanywa na Akaroly Godfrey aliyekuwa kiongozi katika uongozi uliojiudhuru kutokana na kashfa za kusafirisha madawa ya kulevya     na kusababisha Tanzania kufutwa uanachama na chama cha ngumi cha dunia (AIBA) na kusababisha kutoshiriki mashindano,mikutano na shughuri     zote za kimataifa za chama cha ngumi cha Dunia AIBA. Naomba wadau na serikali kuwa makini na watu wanaoshawishi kwa lengo la masilahi yao binafsi na kusababisha michezo kudolola badala ya kusonga mbele.

Fomu za uchaguzi zilishaanza kutolewa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) toka tarehe 4//2013 na zitaendelea kutolewa hadi tarehe 4/7/2013 jijini Mwanza na tarehe hiyo ndio itakuwa siku ya mwisho ya kuchukua na kurudisha fomu, tarehe 5/7/2013 itatakuwa siku ya usaili na utafanyika jijini     mwanza, tarehe 6/7/2013 kupitia pingamizi na kuzitolea maamuzi na tarehe 7/7/2013 ndio siku ya uchaguzi.

Kimsingi taratibu zote za kuitisha uchaguzi kwa mujibu wa katiba yetu zimezingatiwa na zimekamilika.

Aidha BFT inatoa tamko kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu kufika katika uchaguzi uchaguzi, ili kupata viongozi halali kwa mujibu wa katiba, waendelee na shughuri za kuendeleza mchezo wa ndondi na kuaandaa timu ya taifa kushiriki katika mashindano ya Afrika nchini Mauritius Sept. 2013 BFT inatoa wito kwa watu wote wenye sifa, nia, moyo na uwezo wa kuongoza wajitokeze kuchukua fomu za kugombea uongozi kwani wakati ndio huu.

Makore Mashaga
Katibu ~ 

MACHUNGWA YAKIPIGWA SOP SOP....


Kamera yetu ilimnasa mdau huyu akipiga Sop sop Machungwa tayari kwa kuindia nayo mtaani.




MEMBERS OF MAJLIS A'SHURA OF THE SULTANATE OF OMAN VISIT TO TANZANIA


Yesterday a team of 6 MPs locally known as Member of the Majlis A'shura of the Sultanate of Oman touched down JNIA slightly after 13.00hrs graced by the presence of their speaker, H.E Sheikh Khalid Bin Bilal Bin Nasir Al Maawali. They were cordially received by the Deputy Speaker Hon. Yustino Ndugai and the Zanzibari Parliament Delegation. They will visit the Tanzanian Parliament in the cours of the week and later visit a handful of national parks then off to Zanzibar.
L_HE Sheikh Khalid Bin Bilal Bin Nasir Al Maawali, signing guest book at the VIP launge in JNIA.
L_HE Sheikh Khalid Bin Bilal Bin Nasir Al Maawali, Speaker and of Majlis A'shura of the Sultanate of Oman pamoja na R Yustino Ndugai, Deputy Speaker Tz.
Press conference.
Some members of parliament from Oman.




MKAZI WA MAJENGO MOSHI ANUSURIKA KATIKA AJALI


Na Dixon Busagaga wa globu ya jami Moshi.

Mkazi wa majengo mjini Moshi aliyefahamika kwa jina la Frank Ngowi jana usiku amaenusurika kifo baada ya kugongwa na gari aina ya Hiace (daladala) lenye namba za usajili T352 AFM ikifanya safari zake kati ya Kiboriloni na katikati ya mji wa Moshi .

Ajali hiyo imetokea jana majira ya saa 3 usiku eneo la majengo polisi jirani kabisa na zahanati ya Kishamba.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo walisema kuwa dereva wa daladala hiyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja alionekana amelewakupita kiasi.

Mashuhuda walidai dereva huyo baada ya kugundua amesababisha ajali alikimbia na kuelekea maeneo ya majengo sekondari ambapo waendesha bodaboda walimkimbiza na kufanikiwa kumkamata na kumrudisha mpaka kwenye eneo la ajali.

Askari polisi walifanikiwa kufika eneo la tukio na kumchukua dereva wa gari hilo pamoja na majeruhi kwa ajili ya hatua za awali.
Huu ndio usafiri aliokuwa akiutumia Bw Ngowi.
Baada ya dereva wa Hiece kufanikiwa kukimbia vijana walimkimbiza na kumshika na hapa walikuwa katika harakati za kumrudisha kwenye eneo la ajali.
Majeruhi wa ajali Frank Ngowi aliyegongwa na daladala wakati akiendesha baiskeli akionesha majeraha baada ya kupata ajali.
Hii ndio daladala iliyosababisha ajali na kufanikiwa kukimbia hata jitihada zilifanyika na kufanikiwa kukamatwa na kurudishwa katika eneo la ajali.
Jeshi la polisi lilifanikiwa kufika eneo la tuki

OCD MAKETE AWAASA WAHUDUMU WA NYUMBA ZA KULALA WAGENI KUWAANDIKISHA WATEJA WAO


Na Edwin Moshi, Njombe.

Jeshi la polisi wilayani Makete mkoani Njombe limewataka wamiliki wa nyumba za kulala wageni wilayani hapo kuhakikisha wanaandikisha taarifa za wageni wanaofika kulala kwenye nyumba hizo, kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kuwaweka salama pindi kunapotokea tatizo.

Hayo yamesemwa na mkuu wa polisi wilaya ya Makete SP Peter Kaiza wakati akizungumza katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo kuhusiana na tabia ya baadhi ya wahudumu wa nyumba za kulala wageni kudharau kuandikisha taarifa zinazowahusu wageni kwa kinachodhaniwa kuwa ni kuwaibia wamiliki kwani suala hilo ni hatari kwao na kwa jeshi la polisi pia.

“Akuja mgeni kulala kwenye nyumba unayofanyia kazi, wewe hujampa daftari akandika jina na taarifa zingine, usiku linatokea la kutokea mtu ananyooka(anakufa) sasa utajibu nini kwa bosi wakao na kuja kutoa taarifa polisi utaanza anza je” alisema Kaiza.

Katika hatua nyingine kaiza amezungumzia dhana iliyojengeka kwa wahudumu hao kuwa wateja wengi huandika taarifa za uongo hivyo kuona hakuna haja ya kuandika taarifa zao akisema si kweli kuwa kila taarifa itakuwa ya uongo na kusisitiza kuwa wawaandikishe kwa kuwa zitasaidia pindi likitokea tatizo.

Kwa upande wake afisa biashara wilaya ya Makete Bw. Adonia Mahenge(PICHANI) amesema ni vyema wahudumu wa afya wakatambua umuhimu wa kutunza taarifa hizo kwani ni suala la kisheria ambalo linatakiwa kufuatwa na kila mhudumu wa nyumba ya kulala wageni.

Amesema katika kusisitiza hilo watafanya ukaguzi muda wowote kuona kama hatua hizo zinafuatw na ambaye atakuwa amekiuka utaratibu atachukuliwa hatua kali za kisheria, waweke mabango yanayoonesha utaratibu na kanuni na masharti ya kulala kwenye nyumba ya wageni, kuboresha nyumba hizo ikiwemo usafi na ubora wa huduma.

Amesema maazimio hayo yanatakiwa kutumika ndani ya wilaya nzima ya Makete ikiwemo Makete mjini, Ikonda, Bulongwa, Matamba na maeneo mengine ambayo nyumba hizo zi ~