advert

http://

Thursday, 6 June 2013

Karibu nyumbani Morogoro Ngwear,leo tunakupokea kwa nyimbo za maombolezo,Hayo ni maneno ya Afande Sele aliyoyasema kwa huzuni kubwa mwili wa marehemu ilipowasili.

Msanii wa muziki wa Hip Hop bongo anaeishi Morogoro na kufanya shughuli ya Muziki akiwakilisha Mkoa wa Morogoro Afande Sele The King amewakaribisha watu wanaofuatana na Mwili wa Marehemu Albert Mangwear kwa ajiri ya kumpumzisha katika makazi yake ya kudumu kesho.
“Karibu nyumbani morogoro Ngwear leo tunakupokea kwa nyimbo za maombolezo, may your Soul Rest in Peace”
Mwili wa Msanii Ngwear umeagwa Leo jijini Dar es salaam katika viwanja vya Leaders na kupewa heshima ya mwisho na watu wengi waliojitokeza katika viwanja hivyo,baada ya kutoa heshima ya Mwisho mwili ulianza kusafirishwa kutoka Dar es salaam na kuelekea Mjini Morogoro kwa ajiri ya mazishi yatakayofanyika siku ya Kesho alhamisi ya Tarehe 6 June.

No comments: