Ukiliona shamba hilo la Mbela licha ya kuwa na mahindi, pia lina maharage, magimbi na ndizi yaliyostawi na kupendeza.Huwezi kuamini kuwa shamba hilo linalimwa na Mbela, ambaye ni mlemavu kwa kutumia miguu yake.Ulemavu huo umemkuta na kulazimika kulima kwa miguu, baada ya kukatwa mikono yake alipokuwa akidai kurejeshewa mahari kutoka kwa wakwe zake.Mbela anasema kuwa pamoja na ulemavu alioupata ukubwani, hawezi kutembea mitaani kuombaomba wakati bado mwili wake una viungo vingine anavyoweza kuvitumia kujipatia mahitaji yake ya kila siku.
Kilichosabisha kukatwa mikono.
Mbela alizaliwa miaka 53 iliyopita akiwa na mikono miwili na mwenye afya tele, lakini misukosuko ya maisha imemfanya leo abaki hana mikono yake miwili, huku akiishi peke yake.Anaeleza kuwa kabla ya kuwa mlemavu, aliwahi kuajiriwa na Jeshi la Polisi, akifanyia kazi Kituo cha Polisi Makuyuni mkoani Arusha miaka ya nyuma, lakini alicha kazi hiyo baada ya kuugua kwa muda mrefu.Baada ya hali hiyo, aliona bora arudi nyumbani kwao Kijiji cha Malumba wilayani Tunduru ili kuendelea kupata matibabu.Mbela anasema kuwa alipofika kijijini kwao, aliendelea kupata matibabu na baadaye akapona.Akizungumza kwa kusaidiwa na rafiki yake wa karibu ambaye amejitambulisha kwa jina la Zacharia Dikala, maarufu kama Babu Masai, Mbela anasema kuwa alikutana na matatizo ya kukatwa mikono miaka minne iliyopita.Mbela ambaye pia ni baba wa watoto Mwanabibi Salim (28), Siku Salim (19) na Said Salim (24) anaeleza kuwa akiwa na mkewe na familia yake, siku moja alikwenda nyumbani kwa wakwe zake waliokuwa wakiishi katika kijiji hicho cha Malumba na kuchukua mbuzi wake aliotoa mahari miaka ya nyuma wakati akimchumbia mkewe ambaye ndiye aliyemzalia watoto hao.Anasema kuwa wakati huo alikuwa na nguvu na alitumia mabavu kufanya fujo, hadi akafanikiwa kufika zizini na kupora mbuzi, bila kujua kama maisha yake yange badilika na kuishia pabaya.
|
Hawa ni baadhi ya omba omba jijini Dar es Salaam wakihamishwa maeneo yao
ya kazi ya kuomba.Kama unavyoona kwa picha hawako tayari kuhama kwa sababu hawana kazi ya kufanya zaidi ya kuomba wa wapita njia.Hivyo wanajua kabisa kitendo cha kuwaondoa katikati ya jiji ni kuwaua na njaa.Ok wavumilie Obama akimaliza ziara yake huenda serikali itawaruhusu tena kuendelea kuomba katikati ya jiji.
|
Siri Imefichuka.Tazama Picha ya Wema Sepetu Alivyofumaniwa Akiwa Anatomaswa Live na huyu jamaa ambaye inasemakana ndio Mpenzi Wake Siku Hizi.Huyu ni Raheem Mtangazaji wa Times fm
ambaye pia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar-Es Salaam.Mhhhhhhhhhhh!! Kazi kwako Wema yetu macho. Source:http://lukemusicfactory.blogspot.com/2013/05/inasemekana-kuwa-raheem-ndiyo-chaguo.html |
Tanzania Breweries Limited (TBL) chini ya kinywaji chake cha Kilimanjaro, inaendelea na ziara ya tamasha kubwa la muziki la ‘Kili Music Tour 2013’ ambapo wikiendi hii ya Jumamosi ya tarehe 29 mwezi Juni, litafanyika Mjini Tanga kwenye kiwanja cha Mkwakwani likijumuisha wasanii wakali wanane ambao ni Ally Kiba, Snura Mushi, Professor J, Mwana FA, Recho, Mzee Yusuph, Roma na Kala Jeremiah.
Ziara ya Kili Music Tour ilianzia Dodoma wiki iliyopita na kuacha kumbukumbu isiyofutika kwa wakazi wa Dodoma na viunga vyake, ambao walipata burudani kutoka kwa wasanii nyota kama vile Ben Pol, Roma, Ally Kiba, Linex, Professa Jay, Ommy Dimpoz, Lady Jay Dee pamoja na Mkali Kala Jeremiah.
Kili Tour kwa mwaka huu inakujia ikiwa na kauli mbiu ya “Kikwetu kwetu” kwani burudani itayokuwa ikitolewa ni kutoka kwa wasanii wa nyumbani, wakikupa ladha za ala za muziki wa nyumbani na katika viwanja vya nyumbani. Kama kawaida, mambo yataanza saa 10 jioni, jumamosi hii pale Mkwakwani na unakabidhi shilingi elfu mbili na mia tano mlangoni, ambapo utapata bia moja bureee, unaingia unapata burudani kutoka kwa wasanii bora kabisa Tanzania, Kili Music Tour 2013, Kikwetu Kwetu zaidi. |
Posted: 27 Jun 2013 04:46 PM PDT
UJIO wa Rais wa Marekani, Barack Obama ni kufuru tupu, kiasi cha fedha ambacho kinachotumika kugharamia ziara yake peke yake kinazidi mara mbili ya kile kilichoteketea pale mtangulizi wake, George W. Bush, alipotembelea nchini mwaka 2008.
Rais wa Marekani, Barack Obama.
Obama, rais wa kwanza mwenye asili ya Bara la Afrika kutawala Marekani, atawasili nchini Julai Mosi, mwaka huu na kufanya ziara ya siku mbili.
Inaaminika kuwa Bush alipokuja nchini, msafara wake uliigharimu Marekani kiasi cha dola milioni 50 (shilingi bilioni 80) lakini Obama na timu yake watatumia mara mbili ya hapo, yaani dola milioni 100 (shilingi bilioni 160). Hesabu hiyo, ilimtisha hata Mbunge wa Singida Mjini (CCM), Mohamed Dewji ‘Mo’ ambaye aliandika kwa mshangao katika akaunti yake ya Twitter, Jumamosi iliyopita: “Ujio wa Obama Tanzania utaigharimu Marekani dola milioni 100.” UKUBWA WA MSAFARA Kwa mujibu wa ziara mbalimbali ambazo Obama alishazifanya tangu alipoingia madarakani Januari 2009, msafara wake huwa na watu zaidi ya 800. Obama ambaye ni Rais wa 44 wa Marekani, akiwa na mkewe, Michelle, huongozana na watu 500 ambao ni watumishi wa kawaida wa Ikulu ya Marekani, White House. Katika wahudumu hao 500, wapo madaktari sita pamoja na wauguzi wengine zaidi ya 30, wapishi na kadhalika. Msafara wa Obama, haukamiliki bila walinzi karibu 300 ambao jukumu lao huwa ni kumlinda rais huyo kwa ukaribu zaidi. Kutokana na hesabu hiyo ni wazi kuwa Tanzania itakuwa na msukosuko wa aina yake pale Obama atakapowasili Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Hata hivyo, kwa vile ndege ya Rais wa Marekani, Air Force One, haina uwezo wa kubeba idadi hiyo ya watu, wengi wao watawasili kwa mafungu wiki hii ili kufanya maandalizi ya ujio wake.
Ulinzi wa Obama.
MASHUSHUSHU KILA KONA
Kuelekea siku ya ujio wa Obama, Jiji la Dar es Salaam, limeshawekwa chini ya ulinzi, mashushushu kutoka Marekani wametanda kila kona kuhakikisha rais huyo hapatwi na zahama yoyote akiwa nchini. Maofisa wa CIA (Central Intelligence Agency) ambao kiuhalisia ndiyo Idara ya Usalama wa Taifa la Marekani, wanadaiwa kuwepo nchini tangu Januari, mwaka huu, lengo likiwa ni kuratibu na kuhakiki usalama wa nchi. Vilevile inadaiwa, makomandoo wapatao 400 kutoka Taasisi ya Upelelezi ya Marekani, FBI (Federal Bureau of Investigation), waliwasili nchini kwa mafungu kuanzia mwishoni mwa mwaka jana, jukumu lao likiwa ni kuweka mambo sawa. Madai hayo yanajengwa na hoja kwamba hata pale FBI walipojitolea kutoa mchoro wa mtu aliyedaiwa kumpiga risasi na kumuua Padri Evarist Mushi, Machi mwaka huu, ilikuwa ni kwa haraka sana. “Wale FBI walikuwa hapahapa Tanzania ndiyo maana walijitolea kutoa mchoro wa Padri Mushi kwa haraka sana, ingekuwa wapo Marekani wasigejitolea haraka vile. “Sema sasa ilikuwa siri kubwa. Taarifa za ujio wa Obama kuja zipo tangu mwaka jana ila zilifanywa siri kwa sababu za kiusalama,” alisema ofisa mmoja wa Ikulu ya Tanzania kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini.
ANAKUJA NA MAGARI 21
Kwa mujibu wa taarifa za ziara za Rais Obama, kiongozi huyo husafiri na jumla ya magari 21. Obama husafiri na gari lake binafsi kama Rais wa Marekani aina Limousine Cadillac, ambalo halilipuki wala kuharibika hata likipigwa na bomu. Gari hilo likilipuliwa na bomu, matairi peke yake ndiyo huungua lakini hubaki na rimu ambazo hutembea kwa umbali wa kilometa 500 bila wasiwasi. Limousine Cadillac ambalo ni toleo maalum la mwaka 2009 kwa ajili ya Obama pekee, huambatana na magari mengine 20. Kutokana na tafsiri hiyo, Obama akiwa nchini, atakuwa na msafara wake uliokamilika na unaojitegemea kwa asilimia 100. MAGARI 21 YATAKUJA VIPI? Habari zinasema kuwa Limousine Cadillac ndilo litakalokuja na Air Force One, Julai Mosi, mwaka huu, mengine 20 yatawasili kabla ya ujio wa Obama. Inaelezwa kuwa sababu ya magari hayo 20 kutokea Marekani ni kwamba utaratibu wa White House unaeleza kuwa msafara wa Rais wa Marekani ndani ya nchi unapaswa kufanana na wowote ule anapokuwa nje ya nchi. Habari zinaeleza kuwa magari hayo 20, yatawasili na manowari kubwa ya Marekani ambayo inategemea kuwasili nchini wakati wowote kupitia Bahari ya Hindi. Inaelezwa kuwa kazi nyingine ya manowari hiyo ni kudumisha usalama baharini, kuhakikisha watu wenye lengo la kufanya uvamizi hawafanikiwi kwa njia ya majini katika kipindi hiki cha siku chache kabla ya ujio wa Obama na hata pale akiwepo. HOTELI ZA NYOTA TANO ZAJAA Uchunguzi wa Risasi Mchanganyiko umebaini kuwa ujio wa Obama umekuwa na neema kwa hoteli zenye hadhi ya nyota tano ambazo karibu zote zimekodiwa jumla. Hoteli hizo zimechukuliwa na Marekani kwa ajili ya watu watakaombatana na Obama ikiwemo wahudumu pamoja na walinzi mbalimbali. Inaelezwa, baadhi ya hoteli kuna wateja walihamishwa wiki mbili kabla ili kupisha wageni kutoka Marekani ambao wamekuwa wakiwasili nchini kwa mafungu. WENYE MAGARI MAPYA WAULA Uchunguzi zaidi umebaini kuwa wamiliki wa magari mapya yenye nafasi, hususan Toyota Noah, kwao ni neema ya aina yake. Risasi Mchanganyiko limebaini kuwa wenye magari hayo hutakiwa kuripoti Ubalozi wa Marekani nchini kisha vyombo vyao hupimwa kuona uzima wake. Habari zinasema, kila mwenye gari ambalo litafuzu vipimo, atalipwa shilingi 200,000 kwa siku katika kipindi chote litakapotumika katika ziara hiyo ya Obama. BUSH NAYE ANAKUJA Katika hatua nyingine, Bush ambaye ni Rais wa 43 wa Marekani, atawasili nchini hivi karibuni. Hii ina maana kuwa kipindi ambacho Obama atakuwepo nchini, Bush naye atakuwepo ndani ya Tanzania. Bush yeye anakuja kwa ajili ya kuhutubia mkutano wa wake za marais mbalimbali duniani ambapo imeelezwa kuwa mke wa Obama, Michelle, naye atahudhuria. KARIBU OBAMA Ujio wa Obama ni fahari ya Tanzania kwamba nchi yetu ni salama na inavutia ndiyo maana hata kiongozi huyo wa taifa kubwa kabisa duniani, ameweza kushawishika kuja. Karibu sana Tanzania Rais Obama. MHARIRI. http://g5click.com/profiles/blogs/ujio-wa-obama-kufuru |
Na:Mbeya yetu
|
|
Posted: 27 Jun 2013 01:53 PM PDT
Huenda wengi hawamkumbuki Mwisho Mwampamba.Huyu ni Mshiriki wa kwanza Big Brother Afrika na alifanya vizuri katika mashindano hayo na kuibuka mshindi wa pili. Baada ya hapo akarudi Tanzania na kuachana na aliyekuwa mchumba wake na kuwa na Mwanamziki Ray C kimapenzi kwa muda mrefu sana. Baadaye aliachana na Ray C na kupigika sana kimaisha.Hata hivyo akawa kimya kwa muda sana kumbe alikimbilia Namibia na familia yake na sasa amerudi Bongo na kufungua Duka la vifaa vya watoto.Mambo yake poa sana. |
Posted: 27 Jun 2013 01:38 PM PDT
KLABU ya Simba ya Jijini Dar es Salaam,jana ilitangaza rasmi kumtema Nahodha wake ambaye pia ni Nahodha wa timu ya Taifa na Simba, Juma
Awali Kaseja, alikuwa akikaririwa na Vyombo vya habari kuwa hajajua
hatima yake na Klabu ya Simba na kuhusishwa ukimya wake na kuhamia Timu ya Azam, ambao awali walionyesha nia ya kumhitaji.
Lakini alipohojiwa Kaseja, alisema kuwa bado alikuwa akihitaji
kupumzika ili kujua kuwa atasain tena simba ama la, na kwa upande
wa Azam, walipohojiwa kuhusiana na hilo, nao waliruka Kimanga
kuonyesha nia ya kumhitaji Kipa huyo namba moja wa Simba.
|
Posted: 27 Jun 2013 10:57 AM PDT
|
Wanafanya mazoezi TTC Chang'ombe jijini Dar es salaam na Mashindano ni July 5 mwaka huu hapo hapo TTC Chang;ombe Jijini Dar es salaam. |
|
|
|
WIMBI la vitendo vya Watanzania kukimbilia nje ya nchi kutokana na sababu mbalimbali, zikiwamo kutafuta maisha, kujificha na kushiriki biashara za magendo, limechukua sura mpya, baada ya raia zaidi ya 35 kukamatwa nchini Pakistan.
Raia hao, ambao wametajwa kwa majina, wameonekana wengi wamezaliwa Dar es Salaam, Zanzibar na Tanga, huku umri wao wa kuzaliwa ukiwa kati ya 1957 hadi 1983, wamewekwa katika magereza mawili ya Lahore na Rawalpindi, nchini Pakistan. Taarifa iliyotolewa juzi na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara ya Uhamiaji kwa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam, ilisema Watanzania hao wanashikiliwa kutokana na kujihusisha na makosa mbalimbali. Kaimu Msemaji wa Idara ya Uhamiaji, Tatu Buruhani, aliiambia MTANZANIA jana kuwa Watanzania hao wanashikiliwa kutokana na makosa mbalimbali, yakiwamo ya kukutwa na dawa za kulevya, wizi wa mali za umma, kuishi Pakistan bila kibali na kutokuwa na hati za kusafiria. “Katika taarifa yetu ya awali hatukutoa sababu, lakini kutokana na kuhojiwa na waandishi wengi tumelazimika kutoa sababu ambapo tuliwataka wazazi, ndugu na jamaa wajitokeze hapa kwetu ili watoe ushirikiano kwa lengo la kufanikisha kuwarejesha nchini. “Raia hawa walianza kwenda nchini Pakistan kuanzia miaka ya 1989 na hujulikana ni raia wa Tanzania, baada ya kufanya makosa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. “Kwa hawa raia walio katika magereza hayo, walihukumiwa kuanzia miaka ya 2003 hadi mwaka jana, wengine wamemaliza vifungo vyao hivyo hawawezi kuachiwa mpaka wakabidhiwe kwenye nchi husika. “Hawa wanaotakiwa kurudishwa nchini, ni wale waliomaliza kutumikia vifungo vyao, kuna wengi walihukumiwa kulipa faini, lakini kutokana na kutokuwa na ndugu, walitumikia kifungo. “Tumechunguza umri wao na miaka waliyokaa huko, tumegundua walikwenda wakiwa na umri wa vijana kati ya 25 hadi 30 na biashara yao ilikuwa ni dawa za kulevya, pengine tayari wametengeneza familia isiyo halali nchini humo,” alisema. Alisema idara yake imeshindwa kuweka mawasiliano ya moja kwa moja na ndugu wa raia wanaoshikiliwa, kwa sababu ya kukwepa usumbufu. Watanzania wanaoshikiliwa Pakistan ni Usma Mdoe, mzaliwa wa Tanga, Hemed Himji (Dar es Salaam), Mbwana Eka (Zanzibar), Furahisha Seif (Dar es Salaam), Omar Twaha (Mwanza), Alamgiri Akbar (Dar es Salaam), Abubakar Khamis (Tanga), Mohamed Abdul (Tanga), Mohamed Mohamed (Tanga) na Ali Kipuya (Dar). Wengine ni Ashraf Zakhy (Tanga), Mwinyi Mwinyigoha (Pwani), Athuman Singano (Tanga), Abubakar Ally (Zanzibar), Said Mohamed (Dar es Salaam), Omar Suleiman (Pwani), Abdullah Rayngul (Lindi), Jamal Jaffar (Dar es Salaam), Frank Kimweri (Dar es Salaam), Rajab Simbaulaya (Dar es Salaam), Hafdh Sharif (Tanga), Juma Chonanga (Dar). Pia wamo, Mohamed Juma (Zanzibar), Hassan Mohamed (Dar es Salaam), Bonane Dilunga (Dar es Salaam), Rajab Msalagala (Tanga), Mansoor Kaswamba (Dar es Salaam), Ally Said (Tanga), Mohamed Bashiri (Dar es Salaam), Uruka Malipula (Morogoro), Seif Seif (Zanzibar), Shaaban Mussa (Dar es Salaam), Said Madelelia na Rashid Sambatora (Dar es Salaam). Alisema Watanzania wamekuwa na tabia kukimbilia nje ya nchi kwa ajili ya kutafuta maisha, bila kufuata taratibu zinazotakiwa. Alisema wengi wao, wamekuwa na tabia ya kukimbilia nchi za Afrika Kusini, Pakistan, Botswana na nchi nyingine ambazo ni jirani. |
BINTI aitwaye Nuru Omari anayedaiwa kufariki dunia mwaka 2010 ameibuliwa hivi karibuni wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani na mganga akiwa hai kwenye banda kuukuu.
Kwa mujibu wa baba wa binti huyo, Omari Salum, mwaka 2010 ndugu wa mkewe aitwaye Nyasenene aliyekuwa akiishi Charambe Mbagala, jijini Dar alifika nyumbani kwake na kuwaomba wampe mtoto wao kwa ajili ya kwenda kufanya kazi za ndani ‘hausigeli’.
Baada ya binti huyo kufanya kazi kwa muda mfupi aliugua malaria, baba mtu akapewa taarifa na kufika Dar kwa ajili ya kumuona mwanaye aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar.
Mzee huyo amesema alikwenda Muhimbili na kufanikiwa kuzungumza machache na mwanaye huyo ambapo alikuwa akilalamikia maumivu ya tumbo.
Mzee huyo alisema ilibidi aondoke licha ya mwanaye kumtaka alale lakini kwa vile yeye ni mwanaume isingewezekana kulala hospitalini hapo.
“Kesho yake nilipewa taarifa kuwa mwanangu amefariki dunia usiku. Tulianza taratibu za mazishi na kumzika kwenye Makaburi ya Kichangani, Mbagala, Dar kutokana na kukosa fedha za kuusafirisha mwili hadi Mkuranga,” alisema mzazi huyo
Mganga wa kienyeji aliyejulikana kwa jina la Said Ali Ngaora ‘Dr. Lamba’ anayeishi Mbagala Rangi Tatu, Dar alifika katika kijiji hicho cha Kalole mwaka huu na kuwaambia wananchi kuwa kijijini hapo pana mtu anaonekana alikufa na kuzikwa lakini bado yupo hai na amewekwa sehemu na kutaja gharama za kumtoa ni shilingi milioni tatu.
Akielezea tukio zima Dr. Lamba alisema wananchi walimruhusu akaanza kazi kwa kushirikiana na wataalamu wenzake.
Dr. Lamba na timu yake walifanikiwa kumuibua msichana huyo anayekadiriwa kuwa na miaka 12-15 kwenye mji ambao hakuna mtu anayeishi akiwa ndani ya banda la kuku huku kukiwa na chungu chenye damu, asali na udongo ambavyo vilikuwa ndivyo vyakula vyake akiwa na muonekano wa kutisha kwa kuwa na nywele ndefu na chafu na kucha zikiwa ndefu mithili ya jini.
Baada ya kumtoa alipelekwa katika uwanja wa mpira kijijini hapo na kuogeshwa pamoja na kukatwa kucha kisha akapelekwa katika nyumba aliyofikia mganga huyo, hata hivyo hakuweza kuongea vizuri.
Kwa mujibu wa mashuhuda ulimi wa Nuru ulikuwa mzito na mpaka sasa anazungumza kwa vitendo kama bubu huku chakula ambacho ameanza kula vikiwa ni ugali na kuku, uji na juisi ya embe.
Mbali na shilingi milioni tatu za kutoa, mganga huyo anataka milioni 15 kutokana na dawa anazompa kwa ajili ya matibabu ili arudi katika hali ya kibinadamu .
Hata hivyo, baadhi ya ndugu wanaopinga kuwa Nuru siyo mtoto wao lakini baba mzazi anasema ni mwanaye kutokana na alama zilizopo mgongoni mwake na anafanana sana na mdogo wake.
Makamu Mwenyekiti wa kijiji hicho, Ali Hassan Ndeko alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mpaka sasa wanakijiji wanaendelea kumiminika kwa ajili ya kumuona mtoto huyo akiwa chini ya uangalizi maalumu wa mganga huyo huku wakijitolea vyakula.
GPL: |
|
Posted: 27 Jun 2013 02:28 AM PDT
|
Posted: 27 Jun 2013 01:33 AM PDT
Nilimtambulisha kwa ndugu zangu kama ndiye ndugu yao atakayeongezeka na yeye alinitambulisha kwa baadhi ya ndugu zake. Miaka ilivyozidi kwenda niliona mabadiliko kwa mwenzangu kitabia kwani kuna wakati alikuwa akinidanganya kwamba amesafiri kumbe yupo na hajaondoka. Kumbe mwenzangu alishaanzisha uhusiano na wazee wa mujini wenye pesa zao hivyo akawa ananipotezea kwani kwa wakati huo ndo nilikuwa namalizia mwaka wangu wa mwisho chuoni. Hali ilizidi kuwa mbaya zaidi kwani ilifika kipindi akanambia ile mipango tuisitishe. nilipomuuliza kwa nini, hakuwa na jibu la wazi. Ilinichanganya sana lakini nilipata faraja kutoka kwa rafiki zangu na ndugu nikatulia. Baada ya miezi kama sita kupita niliamua kwenda kupima na nikagundulika kwamba niko na maambukizi ya VVU, nilichanganyikiwa sana na niliona kama hakuna haja ya kuishi tena. Sikumwambia mtu mwingine zaidi ya doctor mmoja na mimi mwenyewe kuugulia maumivu yangu peke yangu ila kuna wakati ndugu na jamaa walikuwa wakiniona nimebadilika ila nawaambia hakuna shida yoyote na nipo kawaida. Nilijitahidi kutokukaa peke yangu kwani mawazo ndo yangenizidia. Mpaka sasa hivi nipo vizuri na nna afya njema ila napata wakati mgumu sana kwani wasichana wengi wanaonesha dalili za kutaka kuwa na uhusiano na mimi lakini nawaonea huruma sana kwani inaniuma sana nikifikiria kumwambukiza mtu mwingine. Wengi wao nimekuwa nikiwakwepa mpaka wengine wananitangazia kwamba jogoo wangu hawiki, huwa inaniuma sana kwani sitaki wajue na sipendi kuwafanya wawe kama mimi. Nisiwasumbue sana, naomba nihitimishe kwa kusema; hili tatizo ni gumu sana hasa unapokuwa wewe ndiwe 100%. Tupigeni vita unyanyapaa ili watu wasiwe na mawazo ya kwambaTUFE WENGI. Pia unayemnyanyapaa hujui aliupata vipi kwani si kila mwenyeVVU alikuwa kuruka njia. Kuna wengine wameupata kutoka kwa watu wanaowaamini sana! Na wengine miaka ya leo wamezaliwa nao hivyo sio kosa lao kwa hapo walipo. Source:Talk Bongo Blog |
Huyu ndie Bwana Elly Okech Kisi anayeishi na HIV kwa zaidi ya miaka 20.
Ugonjwa wa Ukimwi bado linaendelea kuwa janga la Taifa huku wataalam kote duniani wakiendelea kuumiza vichwa bila mafanikio.
Bwana Elly Okech Kisi mkazi wa Gongo la Mboto Ukonga,anasema tatizo hilo ilimkuta toka mwaka 1993 mpaka sasa anaishi na Virusi vya Ukimwi.
Anasema aliyempa ukimwi ni mke wake ambaye alifariki mwaka 1998,Na kabla hajafa alimwambia ukweli na kumwomba msamaha.Nilifanya naye mahojiano ili kutaka kujua amewezaje kuishi kwa muda mrefu hivyo na HIV,jamii inamchukuliaje,marafiki na ndugu zake,Hata yeye mwenyewe anajionaje kuwa na HIV.Maswali yote hayo na mengine mengi aliyasema hapa.SIKILIZA.
Hapa akiwa kwake kwa ndani ya nyumba yake ambayo hajaimalizia. Nyumba yake kwa juu,kapiga bati upande moja tu Nyumba ya OKECH inavyoonekana kwa Nyuma Hichi ndicho chumba anachoishi Bwana Okech Akiwa anatembea pembeni mwa nyumba yake Hapa ni ndani ya nyumba.Kiukweli kama unavyoona anahitaji msaada Hapa nipo naye katika picha Aliniambia anataka apunguze mawazo jabo na bia mbili.Nikamuuliza kama ni tatizo yeye kunywa akasema si mbaya na amekuwa akinywa mara kwa mara. Kiukweli hayo ndio maisha ya Bwana Okech.Pamoja na kwamba anaishi na Virusi vya Ukimwi zaidi ya miaka 20 lakini maisha yake ni duni sana.Anaitaji msaada wa hali na mali. Mwenye kuguswa na mkasa huu anapatikana kwa namba za simu 0784335000 na 0713015405 |
NAPENDA KUTOA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWA HAWA WAFUATAO 1.MAMA VERONIKA NDUNGURU 2.BABA LAURENT NSUHA WADOGO ZANGU 1.MONICA ROSES NSUHA 2.PHILIPO NERY NSUHA 3.DORAH NSUHA 4.BERTHA NSUHA 5.DOMMY NSUHA BILA KUWASHAU WATU WANGU WA KARIBU YAFUATAO: 1.DENIS MPAGAZE 2.ALLEN MOSHI 3.NESTRO NJAWIKE 4.ATHANAS SING'AMBI
Friday, 28 June 2013
Nani alikwambia ukiachana na mke wako unadai mahari.Ona yaliyomkuta huyu Askari Polisi.Akatwa mikono yote miwili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment