Wanajeshi wa DRC
Afisa mmoja wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ametiwa nguvuni baada ya kuchafua maiti za wapiganaji wa waasi nchini humo.


Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa DRC, Lambert Mende, ameiambia BBC kwamba Luteni Solomo Bangala alizuiliwa jana Alhamisi na maafisa wa kijeshi baada ya mapigano kuzuka kati ya jeshi na waasi wa M23 katika eneo la mashariki karibu na mji wa Goma.

Kukamatwa kwa afisa huyo kunajiri muda mfupi tu baada ya katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon kuzungumzia madai ya kuwepo dhuluma na mateso dhidi ya wafungwa kutoka makundi ya waasi pamoja na wale waliouwawa zinazotekelezwa na wanajeshi wa Kikongomani.

Kikosi cha kulinda amani cha umoja wa mataifa kinatathmini upya hatua yake ya kuunga mkono vikosi vya serikali ya DRC kufuatia shutuma hizo.

Mapigano kati ya jeshi la DRC na waasi wa M23 yalianza siku ya Jumapili karibu na mji wa Goma.

Mwandishi wa BBC Maud Jullien aliyepo katika mji wa Goma anasema uwanja wa mapigano ulikuwa takriban kilomita 7 katika vilima kutoka mji huo.

Hapajakuwa na mapigano yoyote katika kipindi cha siku mbili zilizopita na jeshi limesema limefanikiwa kuwafukuza waasi yapata kilomita 6, anasema mwandishi wetu.

Mwezi Novemba, wanamgambo wa M23 waliuteka kwa kipindi kifupi mji wa Goma, kisha wakaondoka baada ya kutimizia msururu wa ahadi ikiwemo kuanzisha mazungumzo na serikali.

Waasi wa M23, ambao kwa wingi wanatoka kabila la Watutsi walijiondoa katika jeshi la serikali mwezi Aprili mwaka 2012, na kuanzisha mapigano yaliyowaacha takrikaban watu 800,000 bila makao katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa madini.

Mazungumzo ya amani yaliyofanyika nchini Uganda mwaka huu ili kushughulikia malalamishi ya waasi hao yamekwama.

BBCSwahili.

Mtoto Dora Juma (12) akiwa na majeraha mwilini.
Kisa kiporo cha ugali alichowapa bata
Mtoto Dora Juma,12, mwanafunzi wa Shule ya Msingi Wazo Hill, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam imedaiwa ameunguzwa kwa maji ya moto na binamu yake aliyetajwa kwa jina la Saum Masud.


Dora ambaye ni yatima alikutwa na dhahama hiyo hivi karibuni eneo la Wazo Dar alikokuwa akiishi na binamu yake huyo kama mlezi wake baada ya kufiwa na baba yake.

Akisimulia tukio hilo Dora alidai kuwa siku ya tukio aliamka asubuhi kufanya usafi wa uwanja nyumbani na akaingia katika banda la bata kwa ajili ya kulisafisha.

“Baada ya kumaliza usafi niliingia ndani na kukuta kiporo cha ugali nikakata kipande nikawapa bata bandani, wakati huo dada (Saum) alikuwa amelala, alipoamka na kukuta kiporo cha ugali kimekatwa aliniuliza nikamueleza nimewapa bata, hakuamini.

“Akaniambia twende bandani kuangalia kama nasema kweli, tulifika tukakuta bata wameula hali iliyomfanya  dada  kutoamini, alinifunga mikono na miguu na kuniunguza kwa maji ya moto sehemu mbalimbali mwilini,” alidai Dora.

Alisema baada ya kufanyiwa unyama huo hakupewa huduma yoyote na kusababisha vidonda kuoza na aliokolewa na ndugu yao mmoja aliyekwenda kuwatembelea na kutaka kumnyoa nywele.

“Aliniambia nivue fulana ili nywele zisinidondokee, nilipovua alishangaa kuona nina vidonda mwilini, nilipomueleza mkasa mzima aliwapigia simu ndugu wengine hali iliyofanya dada Saumu kukimbia na kwenda kusikojulikana,” alidai.

Dora alisema alichukuliwa na msamaria mwema aitwaye Kauthari Issack ambaye alisema kuwa kweli alimchukua binti huyo baada ya kuguswa na unyama aliofanyiwa.

“Baada ya kumchukua nilikwenda polisi kupata PF3 ili akatibiwe na anaendelea kutibiwa, askari wakafungua jalada namba  KW/RB/6034/2013 na wakaanza kumsaka mtuhumiwa lakini wakafanikiwa  kumkamata mumewe aitwaye Hamisi Kayanda ili aisaidie polisi,” alisema Kauthari.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni ACP Camillius Wambura amethibitisha mtoto huyo kufanyiwa kitendo hicho na kusakwa mtuhumiwa. 
“Niwaonye wananchi kwamba ukatili kama huu hauwezi kuvumiliwa, watu wajiepushenao maana watachukuliwa hatua za kisheria,” alionya Kamanda Wambura.
...Alivyounguzwa mgongoni.
Dora akiwa na msamaria mwema aitwaye Kauthari…
Mtoto Dora Juma (12) akiwa na majeraha mwilini.
...Alivyounguzwa mgongoni.
Dora akiwa na msamaria mwema aitwaye Kauthari Issack.


Source:Haruni Sanchawa.
GPL.

Mrembo aliyeuawa enzi za uhai wake.
UHUSIANO wa kimapenzi, ulioanzishwa kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, umesababisha kifo cha mrembo nchini Nigeria.


Habari za mtandaoni zinadai kuwa mrembo huyo (jina halikutajwa) pamoja na boyfriend wake (jina pia halijatajwa), walikuwa kwenye uhusiano wa muda mrefu.

Imedaiwa kuwa wakati wawili hao wakiwa kwenye utekelezaji wa hatua za mwanzo za kufunga ndoa, mrembo huyo alimtaarifu boyfriend wake kuwa amepata mpenzi mwingine kwa njia ya Facebook.

Chanzo cha habari kiliiambia tovuti moja ya nchi hiyo kwamba mrembo huyo alianzisha urafiki wa Facebook na kijana mmoja raia wa Marekani (jina halijatajwa) kabla ya kibao kubadilika na kuwa wapenzi.

Chanzo kiliendelea kupasha habari kwamba mrembo huyo na mpenzi wake wa Facebook, walidumisha uhusiano wao kwa njia ya mawasiliano ya simu kwa muda mrefu kabla ya kukata shauri la kuonana ana kwa ana.

“Yule kijana raia wa Marekani alitembelea Nigeria, akafikia hoteli moja kubwa. Yule mrembo akaenda kukutana naye na kutumia muda mrefu chumbani.

“Ni kama baada ya kukutana ndiyo mapenzi yaliongezeka zaidi, kwani alipoondoka hotelini, yule mrembo alirudi kwa boyfriend wake aliyepanga kufunga naye ndoa na kumueleza kwamba mapenzi yamekwisha.

“Baada ya kuambiwa hivyo, kijana aliyekuwa na mategemeo ya kufunga ndoa na mrembo huyo, alimpeleleza mpenzi wake na kubaini mahali ambako kijana kutoka Marekani alifikia.

“Siku iliyofuata alivamia kwenye ile hoteli, akamkuta mpenzi wake na yule kijana wa Facebook, hapo ugomvi mkubwa ulizuka. 

Ugomvi haukuishia hapo kwa sababu kijana wa Nigeria aliahidi ni lazima aue mtu.

“Siku moja baada ya ugomvi hotelini, kijana wa Nigeria alimteka mpenzi wake na kumuua kwa kumkatakata na silaha inayodhaniwa kuwa ni panga,” alisema mtoa habari huyo.

Kwa mujibu wa mtandao huo mpaka pale habari hiyo inachapishwa, mtuhumiwa wa mauaji alikuwa hajakamatwa.


• Hasira za mara kwa mara katika mambo madogo,
• kupendelea sana kuangalia picha za uchi,
• Kusahausahau,
• Kupendelea story za mapenzi,

• Kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi (Mke),
• Kupenda kurukiarukia mambo ya watu wengine (tabia ya kufuatilia mambo yasiyokuhusu),
• Kuumwa na kichwa,
• Kukakamaa mgongo (wanaume),
• Kuingiliwa kirahisi na jini mahaba,
• Kupoteza umakini ktk kazi (efficiency),
• Siku ukikutana kimwili na mwenye virusi bila kinga utaambukizwa kirahisi mno,
• Waweza ku-develop tabia mpya ambayo hukuwahi kuwa nayo ili iwe mbadala kama ulevi n.k.

Pia kumbuka kufanya mapenzi mara kwa mara ina 
madhara yake.
Bofya hapa kujua hayo Madhara!!http://www.babamzazi.com/2013/07/madhara-ya-kufanya-mapenzi-mara-kwa-mara.html


UBAGUZI baina ya vyama vya upinzani uliopata nguvu bungeni wakati wa kuanzisha Kambi Rasmi ya Upinzani chini ya Chadema,umeanza kutafuna chama hicho chenye ushawishi mkubwa kuliko vyama vingine vya upinzani Tanzania Bara.

Uundwaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, ulitokana na msimamo wa Chadema yenye wabunge wengi bungeni, kukataa kushirikisha vyama vingine vya upinzani, ikiwamo CUF ambayo ilikuwa na idadi ya wabunge wanaotosheleza kuunda Kambi ya Upinzani, lakini imezidiwa kiidadi na Chadema.

Chadema pia ilikataa kushirikiana na NCCR- Mageuzi, TLP, UDP na kuamua kuunda kambi ya wabunge wa Chadema pekee, ambapo kwa busara kwa kuwa CUF pia ingeweza kuunda Kambi ya Upinzani, kambi hiyo ya Chadema ikapewa jina la Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni.

Athari za ubaguzi huo zilijitokeza Arusha hivi karibuni, ambapo chama hicho kilionekana kutaka kuongoza halmashauri ya jiji hilo, lakini kikashindwa baada ya kukosa kura mbili tu za TLP, na jana imejidhihirisha wakati wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.



Katika siasa za Arusha, baada ya Chadema kutetea viti vyake vinne vya udiwani katika uchaguzi mdogo na uliokuwa muhimu kwa siasa za Chadema, ilifikisha viti 15 kwenye Baraza la Madiwani la Arusha, huku CCM ikibakiwa na viti 12 na TLP viti sita.


Pia Chadema mbali na kuwa na viti hivyo 15, inayo nafasi ya kuongeza kiti zaidi, kwani kuna nafasi moja ya viti maalumu iliyokuwa ikishikiliwa na Rehema Mohamed, aliyetimuliwa mwaka 2011.



Hata hivyo, pamoja na Chadema kuongoza kwa kuwa na viti vingi vya udiwani Arusha, haikuwa na uwezo wa kumweka Meya, kwa kuwa idadi ya madiwani wake ni 16 na kingehitaji zaidi ya kura 17 katika baraza, ili kupata nafasi ya kuongoza halmashauri hiyo.



Hivyo Chadema ilihitaji kushirikiana na TLP, ili kupata zaidi ya nusu ya kura inayohitajika kikanuni kumuweka Meya madarakani.



Uvinza Baada ya Chadema kusema haina uroho wa madaraka katika umeya wa jiji la Arusha, chama hicho kimejikuta katika mazingira kama ya Arusha,  mkoani Kigoma.

Mkoa wa Kigoma, katika halmashauri mpya ya Uvinza, Chadema ikishindwa kuishawishi NCCR-Mageuzi kuwaunga mkono, itakuwa katika mazingira ya kukosa nafasi ya kuongoza halmashauri hiyo mpya.


Katika halmashauri hiyo, CCM ina madiwani wanane, Chadema madiwani saba na NCCR-Mageuzi inayo madiwani watano na Mbunge mmoja, ambaye anaingia katika Baraza la Madiwani na anaruhusiwa kupiga kura na hivyo chama hicho kuwa madiwani sita.



Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema) alinukuliwa akiwataka madiwani wa Chadema na NCCR- Mageuzi, kuunganisha nguvu ili CCM iunde Kambi ya Upinzani katika halmashauri hiyo.



“Chadema na NCCR-Mageuzi tuna madiwani 13 katika Halmashauri ya Wilaya Uvinza…CCM ina madiwani wanane tu, hivyo tuna kura nyingi upinzani. Chadema ina madiwani saba, NCCR-Mageuzi watano na Mbunge mmoja,” alinukuliwa Zitto akishawishi huku akisema wakishindwa kuungana, CCM itapita katikati.

 
Umoja wavunjika Tofauti na matazamio ya Zitto, kwamba vyama hivyo vingeweka mgombea mmoja dhidi ya mgombea wa CCM, Hamisi Mkwafi, NCCRMageuzi pamoja na kuwa na madiwani sita tu, ilisimamisha mgombea wake, Fidelis Kumbo, na Chadema ikaamua kuweka mgombea wake, Cassiano Mabondo.



Katika mazingira yaliyoonesha kuwa vyama hivyo vya upinzani, ikiwemo Chadema vilikuwa na uroho wa nafasi ya Mwenyekiti, havikusimamisha mgombea katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti, ambayo CCM ilijikuta ikiwa haina mpinzani baada ya kumsimamisha Diwani wa Kalya, Lucas Kanoni.


Awamu ya kwanza ya uchaguzi huo uliokuwa ukisimamiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, Nicolous Kombe na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, ulishindwa kupata mshindi baada ya kila chama kupata kura saba.


Matokeo hayo yaliamsha mjadala wa muda mrefu na mwishowe walikubaliana uchaguzi huo urudiwe, ambapo matokeo yake yalionesha kuwa wajumbe walipigia kura wagombea wa vyama vyao kwani mgombea wa CCM, aliongoza kwa kupata kura nane na kufuatiwa na mgombea wa Chadema aliyepata kura saba na wa NCCR -Mageuzi aliambulia kura sita.

 
Utata Baada ya matokeo ya uchaguzi wa raundi ya pili, mjadala uliibuka tena kuhusu matakwa ya kikanuni, kwamba mshindi anapaswa kupata zaidi ya nusu ya kura za wajumbe waliopiga kura, ambazo ni 11, jambo ambalo hakuna mgombea hata mmoja aliyefikisha.


Msimamizi wa Uchaguzi, Kombe alilazimika kusitisha mjadala huo kwa muda, ili wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wapate ufafanuzi wa kisheria, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).



Baada ya zaidi ya saa moja ya kusubiri, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kigoma, Miriam Mbaga, alisema majibu waliyopata yanaeleza kuwa aliyeshinda kwa kura nyingi, mgombea wa CCM Mkwafi, anapaswa kutangazwa mshindi.


Majibu hayo ya Mkurugenzi yalizua tafrani ambapo baadhi ya madiwani walimtaka Mkurugenzi huyo kufuta kauli hiyo, kwa madai kwamba si kauli rasmi.



Mkurugenzi huyo alilazimika kufuta kauli hiyo, na baadaye Msimamizi wa Uchaguzi, Kombe aliahirisha uchaguzi huo hadi utakapoitishwa upya. 


Baada ya kuahirishwa kwa uchaguzi wa Mwenyekiti, wajumbe walikataa kupiga kura kumchagua Makamu Mwenyekiti, ambayo ilikuwa na mgombea mmoja, Kanoni (CCM).

Source:mpekuzihuru.


Alisema hayo alipozungumza kwenye mkutano wa hadhara mjini Songea juzi, katika ziara yake ya wiki moja mkoani Ruvuma, baada ya kuutembelea mkoa mpya wa Njombe.



“Ni kama vile tozo iliyoongezwa kwenye mafuta ya petroli, ambayo imetupa fedha nyingi kwenye Mfuko wa Barabara, za kuunganisha miji na mikoa na nyingi zimejengwa na zinaendelea kujengwa.



“Nani asiyetaka vijiji vipate umeme kama miji, ili usaidie kuondoa giza, uendeshe viwanda vidogo vidogo na usaidie kukuza uchumi? Wanaopinga tozo hii, hawatutakii mema,”alisema Pinda.


Bunge la bajeti lililomalizika mwezi uliopita, lilipitisha tozo ya Sh 1,000 kwa matumizi ya simu za mikononi, ili fedha zitakazopatikana zisaidie katika mpango mkubwa wa kueneza umeme vijijini unaoendeshwa na Wakala wa Umeme Vijijini, (REA). Kwa mkoa wa Ruvuma peke yake, vijiji vipatavyo 150 vitapatiwa umeme chini ya mpango huo.


Katika mikoa yote nchini kuna idadi inayotofautiana ya vijiji vingi vitakavyonufaika katika mpango huo. Umeme umo katika sekta ya nishati ambayo ni moja ya sekta sita zilizoteuliwa kutekelezwa chini ya mpango wa kuhakikisha matokeo makubwa yanapatikana sasa, wenye upeo wa miaka mitatu, kuanzia mwaka huu wa fedha wa 2013/14. Sekta nyingine ni Kilimo, Uchukuzi, Maji, Elimu na Mapato.


Kabla ya mkutano wa hadhara, Waziri Mkuu alizindua Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Songea, kinachodahili zaidi ya wanafunzi 500 na kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa mfundi stadi mbalimbali.



Awali Waziri Mkuu Pinda alisema bei ya mahindi kutoka kwa mkulima katika mkoa wa Ruvuma, itakuwa ni Sh 500 kwa kilo badala ya Sh 450, ili wakulima wahamasike kuuza mahindi kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA).


Mkoa wa Ruvuma ni moja ya mikoa inayozalisha mahindi, chakula kikuu nchini kwa wingi na NFRA inatarajia kununua tani 50,000 kutoka katika mkoa huo.


NRFA imepangiwa kununua zaidi ya tani 200,000 nchini kote kwa ajili ya hifadhi ya chakula, kiwango kikubwa kuliko mwaka uliopita.


Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Pinda pia aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa soko la kimataifa katika kijiji cha Mkenda kwenye mpaka na Msumbiji, ikiwa ni moja ya masoko 48 yatakayojengwa mipakani kurahisisha biashara na kukabiliana na magendo. Leo Waziri Mkuu ataondoka Songea kurejea Dar es Salaam baada ya kumaliza ziara yake mkoani humo.

Mpekuzi huru.

Ikiwa ni takribani mwezi mmoja tu tangu bomu lilipolipuka kwenye mkutano wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mkoani Arusha, jana tukio kama hilo lilitokea jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, ambao aliutishia kwa lengo la kuwaelezea wananchi mrejesho wa yaliyojiri bungeni hivi karibuni na kuhamasisha wananchi kushiriki kutoa maoni kwenye rasimu ya Katiba mpya.
Tofauti na Arusha, jana bomu hilo lililipuka likiwa kwenye gari la Polisi waliokuwa kwenye mkutano huo katika viwanja vya Sahara, katika Kata ya Mabibo jijini Dar es Salaam na kuibua taharuki kubwa kwa wananchi na wafuasi wa Chadema waliokuwa wamehudhuria mkutano huo.


Polisi wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba bomu hilo lililipuka kwa bahati mbaya na kwamba ni la jeshi hilo.

Akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jana, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Kinondoni, Yusuf Mrefu, alisema mlipuko huo ulitokea kwa bahati mbaya na kwamba haikuwa nia ya polisi kutumia nguvu au kuzuia mkutano wa Chadema.

 "Ni bomu la mkononi. Polisi walikuwa na mazungumzo na viongozi wa Chadema na siyo kwamba kulikuwa na vurugu au matumizi ya nguvu, ni tukio la bahati mbaya," alisema.

Mrefu alisema pia kwamba Polisi haikuwa imepanga kupiga mabomu kwenye mkutano huo wala kuuzuia.

"Siwezi kueleza limetengenezwa wapi, ni aina gani au kazi yake; kwa sababu mimi mwenyewe nimepewa taarifa kwa simu, sikuwa eneo la tukio, nilikuwa kwenye msafara wa Makamu wa Rais," alisema.

Aidha, Kaimu Kamanda huyo bila kufafanua alisema: "Halina madhara." Hata hivyo, alipoulizwa kazi ya bomu hilo ikiwa halina madhara, alijibu kwamba asingeweza kueleza zaidi kwa kuwa hakuwa na taarifa za kina kwa kuwa hakuwa eneo la tukio.

Hata alipoulizwa jina la kitaalamu la bomu hilo alisema hana taarifa za kina.

Wakati Polisi wakieleza hayo, mashuhuda pamoja na taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zilidai kwamba mtu mmoja alijeruhiwa kwenye tukio hilo.

Taarifa zinaeleza kwamba mlipuko huo ulitokea baada ya Mnyika kwenda kwenye gari ya Polisi kwa nia ya kuwasalimia na ndipo kishindo kilichoashiria mlipuko wa bomu kilisikika.

Kufuatia tukio hilo, mkutano huo ulipigwa marufuku na kuhamishiwa eneo la Ubungo Mataa ambako ulifanyika.

 Diwani wa Ubungo (Chadema), Boniface Jacob, akifungua mkutano huo alisema waliamua kuchukua vibali viwili vya mkutano huo kwa tahadhari cha Mabibo na cha Ubungo.

Akizungumzia kuhusu tukio hilo wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Ubungo jana, Mnyika alidai kuwa waliomba kibali cha kufanya mkutano huo siku tano kabla kwa kuwaandikia polisi barua, lakini hawakuwajibu hadi jana asubuhi wakiwataka kusitisha kwa sababu kulikuwa na ziara ya Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, kukagua shughuli za usafi jijini Dar es Salaam.

Mnyika alisema aliwajibu polisi kuwa hawezi kupokea taarifa za kusitisha mkutano wake huyo kwa simu bali aliwataka wampe kwa maandishi.

Alisema baadaye polisi waliandika barua ya kumuagiza asitishe mkutano wake huo kupisha ziara ya Makamu wa Rais.

Alisema hata hivyo, alipoangalia ratiba ya ziara ya Makamu wa Rais, aligundua kuwa haikugusa jimboni mwake na kuwaomba tena polisi wamruhusu kufanya mkutano huo.

Alisema alimtafuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova na kujibiwa yuko nje ya nchi, hivyo aliwaomba wasaidizi wake wampe kibali lakini hawamkujibu na kumuomba asubiri wajadiliane kwanza.

Mnyika alisema kutokana na muda kuyoyoma, alimtafuta Mkuu wa Jesh la Polisi nchini, Inspekta Jenerali Said Mwema, kumuomba amsaidie, lakini aligonga mwamba baada ya kumjibu kuwa hawezi kutengua maamuzi yaliyotolewa na kiongozi wake wa chini na kumtaka aandike barua nyingine ya kuomba kibali cha kufanya mkutano.

"Wakati naendelea kuwasiliana na viongozi wa polisi kuomba wanipe kibali, nilikuwa tayari kwenye viwanja vya Sahara na ndipo zikaja defender (magari ya polisi) tatu za polisi," alisema na kuongeza kuwa:

"Ziliposimama niliwafuata na kwenda kuwaambia kuwa vipi tena mbona mmekuja wakati nimeomba kibali cha kufanya mkutano, ndipo lilipolipuka bomu hilo ndani ya gari ambalo nami nilikuwa nimesimama karibu nalo."

Alisema baada ya kulipuka bomu hilo, watu walikuwa wamekusanyika katika viwanja hivyo walikumbwa na taharuki na kukimbia ovyo kunusuru ya maisha yao. Kwa mujibu wa Mnyika, wakati watu hao wakikimbia ovyo, alikwenda lilikoangukia bomu hilo kumuwahi majeruhi, Thomas Jarome.

Alisema polisi nao walikwenda kumuwahi majeruhi huyo na kumbeba 'mzobemzobe' wakati wakitaka kumuingiza kwenda gari lao, Mnyika na viongozi wengine wa Chadema waliwazuia na kumpeleka hospitalini ambako alipatiwa matibabu na kuruhusiwa kuondoka.

Alisema wakati majeruhi huyo akiendelea kupatiwa matibabu, viongozi wa chama hicho walikusanyika na kujadili sehemu nyingine ya kwenda kufanyia mkutano wao na kubaini kuwa Diwani wao wa Ubungo alikuwa na kibali cha kufanya mkutano eneo la Abiani Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Aliwatangazia wananchi wafuasi na wapenzi wa Chadema wakiwaomba wahamie Abiani.

Katibu wa Mbunge wa Ubungo, Gastone Garubindi, alidai bomu hilo lilipigwa na polisi kwa lengo la kuwatisha wananchi wasihudhurie mkutano huo.

Akizungumza na NIPASHE majeruhi Jerome, alidai kuwa polisi walikusudia kulipua bomu hilo kwani lilikuwa mikononi mwao na askari waliopata mafunzo ya kutosha kuhusu milipuko.

Alisema baada ya kujeruhiwa, viongozi wa Chadema walimpeleka katika kituo Mabibo ambako alipewa PF3 na kwenda zahanati Tandale na kutibiwa.

Jerome alisema baada ya kutibiwa aliruhusiwa kurejea nyumbani na kutakiwa kurudi leo kwa uchunguzi zaidi na kuchomwa sindano ya pepopunda (tetanus).

Tukio la jana limekuja huku uchunguzi wa mlipuko wa bomu uliotokea Juni 15, mwaka huu katika viwanja vya Soweto, Kata ya Kaloleni mkoani Arusha kwenye mkutano wa kufunga kampeni za udiwani wa Chadema, ukiwa bado unaendelea. Katika tukio hilo, watu watatu walipoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya. Bomu hilo linaelezwa kuwa lilipuka kwenye mkusanyiko wa watu mita chache kutoka jukwa kuu, wakati mkutano huo ulipokuwa umekwisha na shughuli ya kukusanya michango ikiendelea.

Viongozi wa juu wa Chadema, Freeman Mbowe na Godbless Lema walikuwapo kwenye eneo hilo.

Hadi sasa hakuna mtu ambaye amekamatwa kuhusiana na mlipuko huo pamoja na kwamba Serikali imetangaza donge nono la Sh. milioni 100 kwa mtu atakayefanikisha kukamatwa kwa mhusika au wahusika wa tukio hilo.

Zaidi ya watu 70 walijeruhiwa baada ya tukio hilo kufuatia polisi kufyatua risasi za moto kwa nia ya kukabiliana na wananchi waliokuwa wanawashambulia.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alikaririwa akieleza kwamba bomu lililolipuka Arusha lilitengenezwa China.

Aidha, Septemba, 2012 aliyekuwa Mwakilishi wa Kituo cha Chanel Ten mkoani Iringa, Daudi Mwangosi, aliuawa kwa kupigwa bomu la machozi na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) eneo la Nyololo Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Alipigwa bomu hilo baada ya kupokea kipigo kutoka kwa baadhi ya askari wa FFU waliokuwa wakiizuia Chadema kuendesha harakati zake za kufungua tawi la chama hicho katika eneo hilo.

Mwangosi ambaye pia alikuwa  Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC), aliuawa mbele ya wananchi, askari wa FFU na aliyekuwa  Kamanda wa jeshi hilo mkoani humo, Michael Kamuhanda.

Askari huyo anayedaiwa kumuua Mwangosi, Pacificus Cleophase Simon (23), alikamatwa na kufikishwa mahakamani akikabiliwa na tuhuma za mauaji hayo na kesi hiyo bado inaendelea kutajwa. 

source:nipashe.
Posted: 22 Jul 2013 05:02 AM PDT

Binadamu wote ni sawa lakini kiukweli tunatofautiana vingi....
Like ·  · Share · about an hour ago · 

Baraka kijana mrefu Tanzania

Inasemekana ni kijana mrefu kuliko wote Tanzania. Kijana huyu (katikati pichani) ambaye anadhaniwa ni mrefu kuliko vijana wote Tanzania anaishi maeneo ya Gongolamboto, Banana jijini Dar es salaam.

 Kijana huyu huwa haonekani sana mitaani, lakini aliingia mjini siku hiyo na kuleta kizaa zaa kikubwa pale alipoibuka mitaa ya Aggrey, Kariakoo. Alikuwa kivutio kwa kila aliyemuona, alifunga mtaa watu wakimshangaa na kumgombania kupiga nae picha. Kila aliyetaka kupiga nae picha alitoa Shilingi elfu moja Tsh. 1000. 

Picha hiyo amepigwa ndani ya Kinyozi (Salon) aliyoingia kupunguza nywele zake na umati wa watu walikuwa nje ya kinyozi huyo kumsubiri atoke. Mpaka sasa hajajulikana jina lake kamili na anafanya nini. 
Hapa Hasheem Thabit alipokutana na Baraka

Kwa kile kinachoelezwa kupisha zoezi la upulizwaji wa madawa ya kuua wadudu na mazalia yake katika wodi za wagonjwa za Kibasila na Mwaisela, hospitali ya Mhimbili ililazimika kuwalaza nje wagonjwa ili kupisha zoezi hilo. 

Hali hii iliwashtua wengi kutokana na ukweli kwamba, kulaza wagonjwa nje ni hatari kwa afya zao! Lakini jambo hili linaweza kuonekna ni la kupuuzwa, huu ni ukweli kwamba bado sekta ya afya ina mahitaji makubwa sana ili kukidhi mahitaji ya Watanzania.

Udaku specially.

Waswahili wanasema Ukstaajabu ya Musa utaona ya FIlauni!ni kwelii ndugu zangu!yametokea na muda huu ninaoandika ndivyo ilivyo!!
Hali ilikuwa ivi mdada cheupe dawa toka kanda ya juu,alinogewa na penzi la baba mwenye familia yake huko pande za MBAGALA KIASI CHA KUMFANYA Baba huyo kuisahauu kabisa familia yake ya mke na watoto wawili nae kwa kujiona mjanjaa sana akamdhibiti na maisha yakaendelea,huku nyuma mama wa watu akiwa ameachwa na watoto wawili na mimba juu siku ilipofika ya kujifungua hakupata msaada wowote ule na hata alipokuwa anapiga simu kuitaji msaada toka kwa mzazi mwenziwe alijibiwa kwamba hana pesa na ajitahidi tu mwenyewe aende hospitali,

majirani mwenye utu na mioyo yahuruma wakajichanga na kumkimbiza hospitalini mama yule!lakini riziki haikuwa upande wake Mungu akampenda zaidi akiwa na mtoto tumboni kwa maana kwamba alicheleweshwa! Baba akapwa taarifa,kwa aibu akaenda nyumbani kwa jili ya mazishi lakini ndugu majirani walimwacha azike mwenyewe!!!
Baada ya mkasa huo akarudi kule alikokuwa amempangisha Cheupe dawa wake ili kuendelea na maisha,maisha yakaenda akamzalia wana wawili na baada ya muda Baba sasa yupo kwa penzi Zito na jimama lenye pesa zake.kahama kwake na mazimaa yupo kwa huyo jimama na jimama alivyo na jeuri ya pesa anampa kila kitu Baba huyo asiye na soni wala haya na kinachomfanya huyo dada aliye ni ile hali ya jimama hilo kumwita msamba na kwamba kama yeye mwanzo alimwiba basi atulie sasa ni zamu yake na hata inapotokea BABA huyo yupo kwake humpigia simu cheupe dawa na kusema nipo na mumeo sasa we ulie tuuu!....Cheupe dawa hana kazi alikuwa akimtegemea kila kitu BABA maana kwa mujibu wake mama huyo keshampachika jina baba huyo kwamba ni BONGE LA BWANA!
uNAAMBIWA HALI NI tata cheupe dawa aanatelekezwa na wanawe wawili na mmoja aliyekutwa naye jumla watatu na yule Bonge la bwana keshatangaza kumuowowa BONGE LA MAMA ..huku nyuma cheupe dawa anatembea na kisu popte aaatakapowakuta ama zake ama zao!!!jamani chondechonde mwenye no ya Gea HABIBU atoe ili anusuru uhai hii jamani si uongoooooooooooo!! ni true story hata anavyotusimulia mwenyewe ni kama vile kasahau yeye alivyomtenda mwenzake!''
Je wanawake hii mnaionaje?toeni maoni ushauri gani apate ili asije ozea jela mana kinachomuuma zaidi ni huyo BONGE
LA BWANA KUHEHUKA NA PENZI LA HUYO MAMA NA KUMWELEZEA KILA KITU KINACHOFANYIKA PINDI WANAPOKUWA CHUMBANI..SASA KISASI CHA HUYU dada kipo kwa huyoooo BONGE LA MAMA!
SOURCE.....ALIYEPORWA MUME!


Ukatili wa kutisha umewakuta watoto wawili wa familia tofauti wakidaiwa kubakwa na wazazi wao huku mmoja akifanyiwa unyama huo na baba yake mzazi na mwingine baba yake mdogo. 


Habari zilizopatikana kutoka kwa ndugu, wazazi na majirani wa watoto hao zilisema kuwa wote walifanyiwa ukatili huo siku moja kwa nyakati na mazingira tofauti wilayani Temeke, Dar hivi karibuni.

Watoto hao ambao wote walifikishwa siku moja katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke kwa matibabu, walieleza jinsi walivyotendewa unyama huo wa kusikitisha ambao mzazi au mlezi hapaswi kumtendea mwanaye. 

Wakwanza ni Anifa (8) ambaye alieleza kuwa alibakwa na baba yake mdogo aliyemtaja kwa jina moja la Amani.
Wapili ni Prisca ambaye alimweleza mwanahabari wetu kuwa alibakwa na baba yake mzazi aliyemtaja kwa jina moja la Charles.


Wakizungumza na mwandishi wetu kwa nyakati tofauti wakiwa wodini hospitalini hapo wakiuguzwa majeraha, watoto hao waliokuwa sambamba na mama zao, walieleza kwa kina kile walichofanyiwa na wazazi wao.

Anifa alisema mara nyingi baba yake mdogo alikuwa akimpa pipi na akimuonesha muvi za picha za utupu na kumshawishi wafanye uchafu huo. 


“Kuna wakati alikuwa akiniambia atanipa pesa lakini pia alinitisha kwa kisu au panga ili nimpe, nikawa nakataa lakini siku hiyo usiku alinibaka huku amenishikia kisu,” alisema mtoto Anifa kwa huzuni.

Kwa upande wake, Prisca alisema baba yake alimwambia atampa pesa ili wafanye mapenzi na wakati anamwingilia alikuwa ameshika noti ambayo hata hivyo alishindwa kusema ilikuwa na thamani gani.

Moja kati ya mambo yaliyoibua maswali ni kama kweli wabakaji wa watoto hao ni baba zao? 


Ili kupata majibu  mwandishi wetu alizungumza na watoto hao kwa kina juu ya ukweli kama wahusika wanawafahamu vizuri ambapo katika mahojiano hayo yaliyorekodiwa, kila mmoja alikiri kuwa wanawajua fika wazazi wao hao.

Bila kupepesa macho wala kuogopa, mtoto Anifa alikiri kuwa mbakaji wake ni baba yake mdogo ambaye mara nyingi alikuwa akimtishia ili afanye naye mapenzi bila mafanikio hadi siku aliyopata nafasi usiku.

Kilichowashangaza wengi ni umri mdogo wa watoto hao kwani mtoto Anifa ana miaka nane huku mwenzake akiwa na umri wa miaka mitano.
 

“Mwanangu ana miaka mitano tu, sasa najiuliza huyu baba yake alikuwa anatafuta nini kwake, kwa kweli imeniuma sana na nimechanganyikiwa kwa kitendo alichofanyiwa na baba yake,” alisema mama wa Prisca huku mama wa Anifa akithibitisha umri wa mtoto wake kuwa ni miaka minane akiwa ni denti wa darasa la tatu katika shule ya msingi (jina kapuni).

Mama mzazi wa Prisca aliyejitambulisha kwa jina moja la Maria, alisema alishitushwa na taarifa za mumewe kumbaka mtoto wao.
 

“Nimeshaachana na mume wangu na sasa ameoa mwanamke mwingine, kwa kweli niliumia sana baada ya kupata habari za mwanangu kubakwa na baba yake.
 

“Nilikwenda Polisi Chang’ombe (Dar) nikamfungulia jalada la kesi namba CHA/RB/6028/2013-UBAKAJI ambapo mtuhumiwa alikamatwa na sasa yupo mahabusu katika Gereza la Keko akisubiri kesi yake kusikilizwa,” alisema mzazi huyo.
 

Kwa upande wa Anifa, shangazi yake aitwaye Wamoja alisema kuwa mtuhumiwa wa ubakaji wa Anifa alikamatwa mara alipokwenda hospitalini hapo kwa ajili ya kumjulia hali mgonjwa.
 

“Alijifanya hajui chochote akaja hospitali kwa kuwa Anifa alishamtaja kule polisi, ndipo akakamatwa na kufikishwa polisi Chang’ombe akisubiri kufikishwa mahakamani,” alisema Wamoja.

Baadhi ya mashuhuda wa matukio hayo, walishangazwa na madai ya watoto hao kubakwa na wazazi wao ambapo walisema kuwa siyo bure, lazima kuna kitu nyuma ya pazia.


GPL