advert

http://

Wednesday, 3 July 2013

JESHI LA MISRI LAMUONDOA MADARAKARI RAIS WA NCHI HIYO USIKU HUU



Waziri wa Ulinzi nchini Misri,Abdelfatah al-Sissi akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi uliopita kuhusiana na uamuzi Jeshi wa kumuondoa Madarakani Rais wa Nchi hiyo ya Misri,Mohamed Morsi baada ya kushindwa kumaliza mgogoro uliokuwa ukiendelea nchini humo.
Rais wa Misri,Mohamed Morsi ambaye ameondolewa madarakani usiku huu.
Huko mitaani ni shangwe kwa kwenda mbele baada ya kupokea taarifa ya kuwa Rais wa nchi hiyo hana mamlaka tena ya kuingoza.Sasa hivi nchi iko chini ya Uongozi wa Jaji Mkuu wa nchi hiyo.




MEYA WA MANISPAA YA ILALA ATEMBELEA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA - SABASABA LEO


IMG_8797
Mstahiki Meya Jerry Silaa akisalimiana Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal walipokutana kwenye Banda la Mfuko wa Fursa sawa kwa wote (EOTF) kwenye viwanja vya maonyesho ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar.
IMG_8830
Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Mama Anna Mkapa akiagana na Mstahiki Meya Jerry Silaa mara baada ya kutembelea Banda la (EOTF) linalotoa fursa kwa wajasiriamali nchini Tanzania kuonyesha bidhaa zao katika maonyesho hayo kila mwaka.
IMG_8735
Mkurugenzi Mtendaji wa Home Shopping Centre (HSC) Fahad Said Mohamed (kushoto) akimkaribisha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa kwenye Banda la HSC kwenye maonyesho ya 37 kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
IMG_8808
Mtsahiki Meya Jerry Silaa akipewa maelezo ya jinsi Mfuko wa Fursa sawa kwa wote unavyopambana na kutokomeza Ugonjwa wa Saratani ya Matiti kwa wakina mama nchini. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Mama Anna Mkapa.
IMG_8558
Mstahiki Meya Jerry Silaa akipata maelezo jinsi ya kutumia Kizimamoto Fanisi cha kurusha (Fire Extinguisher) ambacho ni rahisi kutumia na hakihitaji matengenezo na hudumu kwa miaka mitano pia Kifaa hicho ni rafiki wa mazingira na mvumbuzi bora kwa uokoaji wa dharura wakati alipotembelea Banda la GreenBat Fire Solutions katika maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea.
IMG_8542
Mstahiki Meya Jerry Silaa akisaini kitabu cha wageni katika banda la Arusha International Conference Centre (AICC) wanaoshughulika kutoa huduma za kumbi za Kimataifa za mikutano na Utalii jijini Arusha.
IMG_8531
Mstahiki Meya Jerry Silaa akingalia jinsi mtoto Range Jackson ( wa pili kushoto) mwenye ulemavu wa Ubongo akionyesha ramani ya Tanzania na Sehemu ya mipaka yake iliyotumika kumfundishia kujua kusoma na kuandika na ufundi stadi kupitia kituo cha VETA. Kulia ni Mkufunzi wa kuchomea (Welding Instructor) na Mwalimu wa watu wenye mahitaji maalum Bw. Kintu Kilanga na Wa tatu kulia ni Baba mzazi wa kijana huyo Bw.Jackson Range.(Picha na Zainul Mzige).




TBL YANOGESHA SIKU YA WAKULIMA WA SHAYIRI KARATU


 Mtafiti wa Mbegu,Geremiah Mrimi  (wa pili kushoto) akimuonesha Meneja wa Kiwanda cha Kimea cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Moshi, Vitus Mhusi mbegu aina ya Shayiri zilizokubaliwa na Wizara ya Kilimo, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wakulima wa Shayiri, wilayani Karatu, Arusha mwishoni mwa wiki. Wakulima wa zao hilo wana mkataba wa kuiuzia  Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), shayiri kwa ajili ya kutengenezea bia.

Mtaalamu wa Kilimo cha Shayiri, Joel Msechu (kulia) akitoa maelezo juu ya mbegu za Shayiri kwa Meneja wa Kiwanda cha Kimea cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Moshi, Vitus Mhusi (katikati) na Mhasibu wa Mashamba, Optaty Minja.Wakulima wa zao hilo wana mkataba wa kuiuzia TBL, shayiri kwa ajili ya kutengenezea bia.
 Mtaalamu wa Kilimo cha Shayiri, Joel Msechu (kulia) akitoa maelezo juu ya mbegu za Shayiri kwa Meneja wa Kiwanda cha Kimea cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Moshi, Vitus Mhusi (katikati) na Mhasibu wa Mashamba, Optaty Minja.Wakulima wa zao hilo wana mkataba wa kuiuzia TBL, shayiri kwa ajili ya kutengenezea bia.
 Anatoly Lohay,mkulima wa Rhotia kati Karatu.
Editha Temu,Afisa Ughani kiwanda cha TBL akielezea umuhimu wa zao hilo




TWANGA PEPETA NA BEN PAUL KUSINDIKIZA REDD'S MISS TEMEKE 2013


Mratibu wa shindano la Redd’s Miss Temeke Beny Kisaka akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar Es Salaam juu ya shindano la Redd’s kanda ya temeke linalotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa TCC Club Chang,ombe ijumaa ya juma hili.Kulia ni mkuu wa itifaki wa kamati ya Miss Tanzania,Albert Makoye.
Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania,Albert Makoye akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar Es Salaam juu ya shindano la Redd’s kanda ya temeke linalotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa TCC Club Chang,ombe ijumaa Julai 5,2013.Wengine Pichani ni Mratibu wa shindano la Redd’s Miss Temeke Beny Kisaka na Msanii Ben Paul pamoja na Warembo watakao shiriki kinyang'anyiro hicho.
Warembo wanaowania taji la Redd’s Miss Temeke wakiwa katika picha ya pamoja na waandaaji wa shindano hilo sambamba na wasanii watakaotumbuiza siku hiyo Ben Paul na Luiza Mbutu wa bendi ya Twanga pepeta ambapo shindano hilo litafanyika katika ukumbi wa TCC Club Chang,ombe ijumaa Julai 5,2013.




SERIKALI YAKABIDHIWA RASMI UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR LEO


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangaraka (kulia) akipokea Ufunguo wa mfano kutoka kwa Balazo wa China hapa nchini Balozi Lu Youging kuashiria kukabidhiwa rasmi kwa Uwanja wa Taifa.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara (Kulia) akishuhudia Balazo wa China hapa nchini Balozi Lu Youging akiweka sahihi katika hati ya makabidhiano ya Uwanja wa Taifa.Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga(Kushoto) akitia sahihi katika hati ya makabidhiano ya uwanja wa Taifa,kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi Habib Mkwizu.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara (Katikati) akishuhudia Balazo wa China hapa nchini Balozi Lu Youging akibadilishana hati ya makabidhiano ya Uwanja wa Taifa na Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga (Kulia).
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Utumishi Habib Mkwizu (Kushoto) akifafanua jambo kwa baadhi ya viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo mara baada ya sherehe ya makabidhiano ya Uwanja kukamalizika.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Assah Mwambene (Kulia) akizungumza akibadilishana mawazo na Katibu Mtendaji wa TFF Angetile Oseah walipokutana katika sherehe za makabidhiano ya Uwanja wa Taifa jana jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA FRANK SHIJA - MAELEZO.




MTU MMOJA AUWAWA NA JESHI LA POLISI JIJINI ARUSHA KWA KUDAIWA NI JAMAMBAZI


Mahmoud Ahmad Arusha

MTU mmoja anaedaiwa kuwa ni Jambazi afariki katika majibishano ya silaha na polisi katika tukio tofauti la kujibishana risasi na askari wa jeshi la polisi baada ya kumfyatulia askari risasi na kumkosa huko maeneo ya Sokon 1 jijini hapa jana majira ya jioni.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani hapa Kamishna msaidizi wa polisi Liberatus Sabas alisema kuwa mnamo majira ya saa11;15 huko mtaa wa Onjaftian jeshi hilo lilifanikiwa kumuuwa baada ya majibishano ya risasi na askari wa jeshi hilo jambazi sugu aliyefahamika kwa jina la Lembris Taiko au kwa majina mengine doctor mbushii,general mwarusha, mwenye umri wa miaka32-35 mkazi wa sokon 1 jijini hapa.

Kamanda alisema kuwa awali walipata taarifa kwa wasamaria wema kuwa kuna watu3 wanaosadikiwa majambazi na kufuatilia maeneo ya tukio na kuizingira nyumba walipojaribu kuingia ndani na kuwataka watu wote kujisalimisha ghafla risasi zilianza kutoka ndani kupitia ukutani na kumkosa askari hali iliyowalazimu askari kujibu mapigo na kufanikiwa kumuua jambazi huyo.

Sabas alisema kuwa uchunguzi uliofanya na askari wa jeshi hilo umebaini kuwa ni jambazi sugu huyo alikuwa akitafuta na jeshi hilo na akishiriki kwenye matukio ya ujambazi maeneo mbali mbali ikiwemo Arusha,Kilimanjaro na Dar es salaam na alikutwa akiwa na bastola mmoja,aina ya bereta iliyofutwa namba risasi moja chemba,ganda moja la risasi iliyofyatuliwa,risasi 3za bunduki aina ya shortgun,na funguo mbali mbali 26 na mordem ya kampuni ya Airtel.

“Jambazi huyu alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu na jeshi letu kwa kushiriki kwenye matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha za moto tukio ambalo lilitokea28\08\2012 huko maeneo ya olasiti jijini hapa ambapo walipora bastola yenye no.T0620-11J00491 aina ya tisas”alisema kamada sabas.

Katika tukio lingine jambazi huyo alijeruhiwa mguuni akafaniwa kutoroka lakini jeshi la polisi lilifanikiwa kumua jambazi aliefahamika kwa jina la peter Toshi katika majibizano hayo jambazi huyo alikutwa na bastola aina tisas inayoaminiwa kuwa ndio ilioporwa ikiwa imefutwa namba zake.

Kamanda sabas alisema kuwa kutoka eneo la tukio anabainisha kuwa mmiliki wa nyumba aliokuwa jambazi huyo anaefahamika kwa jina moja la Swalehe au baba Amiri ambaye hakuwepo wakati wa tukio hili jitihada za kumtafuta zinafanyika ili aweza kuhojiwa juu ya uhusiano wao na jambazi aliyeuwa na wapangaji wengine kwenye nyumba hiyo kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi.

Hata hivyo mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya mount meru kwa uchunguzi zaidi na juhudi za kuasaka majmbazi wengine badao zinaendelea kufanyika.




TAMASHA LA GRAND MALT TANZANIA OPEN FILM FESTIVAL LAENDELEA JIJINI MWANZA.


Baadhi ya Wakazi wa jiji la Mwanza wakitazama moja ya filamu iliyokuwa ikioneshwa jana usiku kwenye viwanja vya Nyamagana,ikiwa ni sehemu ya maonyesho ya Filamu ya wazi lililojulikana kwa jina la  ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’.Tamasha hilo lilizinduliwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Paul Mzindakaya na kusababisha shangwe tupu kwa wote waliokuwepo ndani ya uwanja huo.
 Katika uzinduzi wa tamasha hilo,kuna burudani mbalimbali zikitolewa ikiwemo na wakazi wa Mwanza wenye vipaji vya kucheza na kuimba,walipewa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kama ionekanavyo pichani,ambapo mwisho wa mashindano hayo kuna atakaeibuka na kitita cha shilingi laki mbili.
 Baadhi ya Wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza jana kushuhudia muenedelezo wa tamasha la filamu,lijulikanalo kama   ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ kwenye uwanja wa Nyamagana.




TWIGA BANCORP KUTUMIA MAWAKALA KUTOA HUDUMA ZAKE


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Twiga Bancorp Limited, Hussein Mbululo, akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na huduma mbalimbali za kibenki zinazopatikana katika katika Banda la Benki hiyo lililopo katika viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ambayo yanaendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere barabara ya Kilwa Dar es Salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Twiga Bancorp, Hussein Mbululo (kulia) akizungumza na Wafanyakazi wa Benki hiyo waliopo Viwanja vya Maonesho sabasaba, Ofisa Masoko, Adebert Archerd  na Katikati ni Ofisa Uendeshaji wa shughuli za Kibeki wa Twiga Bancorp, Upendo Tendewa

 Wakazi wa Dar es Salaam wakiingia katika Banda la Karume lililopo jirani nja Banda la Twiga Bancorp.


No comments: