Kwenye mahojiano yake ya kwanza mara baada ya kuachiwa toka gerezani kwa kuhusishwa na kifo cha nguli wa muziki wa pop duniani Michael Jackson, Dokta Conrad Murray alielezea kwenye mahojiano aliyofanya na The Mail kwamba, Michael hakuwa baba wa hata mtoto wake mmoja, aliathiriwa na madawa kiasi cha kufikia hatua ya kuhitajika kuwa anavaa condom sababu mkojo ulikuwa unatoka wenyewe kwenye uume wake.
“Unataka kufahamu ni kwa kiasi gani mimi na Michael kwa vile tulikuwa karibu? Nilikuwa nikishukilia uume wake kila usiku. Nilikuwa namvalisha condom sababu mkojo wake ulikuwa ukitoka wenyewe. Michael alikuwa hajua namna ya kuvaa condom, hivyo ilinibidi niwe namvallisha. Kilikuwa ni kitu cha kipekee sana ila aliniamini mimi. Sikumuuwa Michael Jackson, aliathiriwa na madawa, Michael Jackson kwa bahati mbaya alimuuwa Michael Jackson, naamini aliamka na kuamua kufanya aliyozoea kufanya, akajidunga sindano haraka ambayo ilisababisha kumpeleka kwenye hali iliyomfika.’’
Alikuwa kwenye majanga mwishoni mwa maisha yake, akiwa na msongo wa kimawazo na kupaniki … Mwishoni, Michael alikuwa mtu aliyekata tamaa. Nilijaribu kumlinda ila mwisho wa siku niliangushwa naye.
Jackson alikuwa ameingia kwenye matatizo ya kuathirika kiakili na kimwili kutokana na ziara yake ya London.’’ Alisema Dokta Conrad Murray.
|
|
Hii itakuwa ni kwa mara kwanza kwa mwimbaji wa Tanzania na pengine Afrika kuwa followed na Rais Barack Obama wa Marekani kwenye twitter ambae ana zaidi ya followers milioni 40 lakini yeye anafollow watu laki sita. Vanessa Mdee ameingia kwenye list ya watu laki sita ambao Rais Barrack Obama ana wa-follow sasa hivi ambapo baada ya Rais huyu kufollow, kwa furaha Vanessa alishare kwenye instagram screenshot ya ukurasa wake wa twitter ukionyesha Barack Obama ameanza kum-follow. Kama ilivyo twitter, hii inamaanisha ana Vanessa ana uwezo wa kumuandikia msg binafsi kwenye inbox Rais Obama.
|
Zifuatazo ni kauli za Ismail Aden Rage ambazo nimemnukuu akiongea na Waandishi kutokana na stori zilizochukua headlines kwa siku kadhaa kuhusu Kamati kumsimamisha kama Mwenyekiti wa Simba. 1. ‘Kwanza napenda kuipongeza kamati ya utendaji ya TFF kwa kuafiki mimi Ismail Aden Rage ndio Mwenyekiti halali wa Club hii ya Simba na nimepata barua yao jana ileile, katika katiba ya Simba kuna kitu wengi hawajui maana ya Kamati ya utendaji wanadhani ni wale watu saba… hapana!!! kamati ya Utendaji ni Mwenyekiti, Makamu wa Mwenyekiti… hamna kaimu hapo, kuna Wajumbe 7 waliochaguliwa katika mkutano halali… , Wajumbe saba wa kuchaguliwa mmoja wapo akiwa ni Mwanamke na wengine wawili wa kuteuliwa na Mwenyekiti, leo nitateua mwingine mmoja.. nimetoa mmoja’ 2. ‘Kwa bahati mbaya Club ya Simba haina Makamu Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti alishajiuzulu ila ina Kaimu Mwenyekiti tu ila huku kwenye katiba hatajwi, kwenye katiba ya Simba Makamu Mwenyekiti ana kazi mbili, moja kwa kuelekezwa na Mwenyekiti na pili Makamu Mwenyekiti anafanya kazi wakati Mwenyekiti hayupo’ – Aden Rage 3. ‘Joseph Itangire ni Kaimu Mwenyekiti tu niliemteua lakini hajapata uhalali wa kikatiba kwa hiyo katiba hii inaendelea kusema, mwenye mamlaka ya kuitisha kamati ya Utendaji mara nne kwa mwaka ni Mwenyekiti, nimekua muungwana tumefanya mara 12 mwaka huu.. kama Mwenyekiti hayupo, katiba inasema anakaimu hana mamlaka ya kuitisha kikao chochote kwa mujibu wa katiba kwa hiyo kikao kile kilichofanyika hakina tofauti na kikao cha harusi’ 4. ‘Maamuzi yangu kama Mwenyekiti wa Simba sasa, kwa kuwa mkutano ule ulikua ni batili… jana niliandika barua kwa TFF kwamba viongozi hawa wamevunja katiba za TFF, Simba, CAF na FIFA… ukitaka kulalamika ni lazima uwe na ushahidi wa aina mbili unaokubalika ambao ni document na video casette iliyo na sura za watu na maneno yao waliyosema, wana document ambayo kwenye barua ya Malinzi amekiri anayo na imesainiwa na Makamu Mwenyekiti wa Simba Joseph Itangire’ 5. ‘Nimesikitika sana na maagizo ya TFF ya kunitaka niitishe mkutano na Wanachama wa Simba ndani ya siku 14, sijui wameitoa wapi kwenye katiba ya TFF na Simba, wamekwenda mbali na kuninyang’anya madaraka… wamenipa alafu wameninyang’anya alafu wamenipa na Ajenda ya mkutano, sasa wamenirudishia madaraka ya nini? mimi kama Mwenyekiti wa Simba… siitishi mkutano, nalindwa na katiba kwa hilo’ 6. ‘Unaponipa amri unaninyang’anya madaraka yangu, katiba inasema kama naona itafaa nitaitisha… tuheshimu katiba, nilitegemea taarifa ya kwanza ya TFF mpya ingelaani mapinduzi ya kipuuzi yanayotokea’ 7. Heshima yangu mimi ni Mbunge taifa linaelewa hivyo, nimekuta ofisi hii hakuna umeme miaka 18 pamoja na pazia za magunia, nimekuta uhuni mtupu.. wachezaji wameuzwa, Henry Joseph, Matole na wengine uliza wanachama wa Simba ilipata shilingi ngapi? leo imani inawatoka kusikia nimeuza Wachezaji wawili tu Congo DRC milioni 320 na nikaweka wazi hadharani sio kuwaambia Mke wangu na watoto wangu.. 8. Leo nimetumiwa msg kutishia kuuwawa na tayari nimesharipoti Polisi, leo hii msg nimepata mtu kaniambia ‘Nisipotoka Simba ataniua’ alivyokua mpumbavu hajui hizi simu zinasajiliwa, nimecheki jina lake mpaka mtaa anaokaa pengine sasa yuko Lupango… why??? mpira ni burudani!! kuna mtu alikua Simba sasa yuko TFF anataka kuleta vurumai ndani ya TFF na Simba, kwa nini? kwa nini ununue watu? waandishi wa habari hebu tuache kuchochea, wewe Mwandishi ni nani ununuliwe? kuna Mwanamke Mwaandishi mmoja kalipwa milioni 2 ili anichafue, sijali.. ‘ 9 Nimefanya Demokrasia sana na ndio inanitokea puani, nimeteua kamati… ziko kamati nyingi sana lakini sijaona Mwandishi hata mmoja anakwenda kuuliza kamati ya ufundi, Usajili ila kila mmoja ananishambulia mimi, leo sitaki maswali ya Waandishi wa habari, sasa mna hiari… kuandika au kuacha wala hamnipi tabu nyie, kuchafuliwa nimezoea’ 10. Ukitaka kuwa kiongozi teka Ikulu kwanza, hapa ndio ikulu.
|
Zaidi ya watoto 60 wanadaiwa kutekwa na kufichwa katika handaki lililopo kwenye msitu wa Mabwepande, Wilaya ya Kinondoni ,Dar es Salaam, ambalo ndani yake kuna jengo kubwa lenye vyumba.
Utekaji huo unadaiwa kufanywa na raia wa kigeni (Wazungu), wakishirikiana na Watanzania ambapo watoto hao hufungiwa katika vyumba hivyo, kuteswa, kulawitiwa na kubakwa.
Mtoto Emmanuel Robert (11) anayesoma darasa la tano Shule ya Msingi Maendeleo iliyopo Tabata, Segerea, Dar es Salaam na mdogo wake Godianus Robert (8), anayesoma darasa la tatu shuleni hapo, ndio waliofichua ukatili huo mwishoni mwa wiki.
Watoto hao walitekwa na Wazungu w awiliasubuhiyaSeptemba2mwaka huu, wak ati wakiendas huleni n akufan ikiwa kutoroka katikaj engohiloSeptemba 23 mwaka huu.
Wakiwa wamechoka na afya zao kuzorota katika Kituo kidogo cha Polisi, Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani, watoto hao walisema ndani ya jengo hilo kuna watoto wengi wa kike na kiume.
Walisem a w atoto hao wanafanyishwa kazi na kuteswa kwa kutandikwa fimbo, kuchomwa moto na kupigwa shoti ya umeme hasa wanapowaulizia wazazi wao ambapo baadhi yao hubakwa na kulawitiwa.
"Jumba hili limejengwa ndani ya handaki, tulikuwa tukifanyishwa kazi ngumu na nzito, usiku tunajaza maji katika mapipa mengi na kubebeshwa ndoo kupanda na kushuka kilima.
"Tunapigwa fimbo, wasichana wanafungiwa kwenye vyumba, wanabakwa na kulawitiwa kwa zamu na Wazungu, tunachomwa moto (alionesha mguu wake uliochomwa) na kupigwa shoti ya umeme tunapowaulizia wazazi wetu," alisema Emmanuel kwa uchungu akitokwa na machozi.
Aliongeza kuwa, asubuhi ya Novemba 23 mwaka huu, katika jengo hilo kulitokea kutokuelewana kati ya Wazungu na Waswahili ambapo mswahili mmoja aliwatisha wazungu kwa kuwaambia polisi wanakuja hivyo walikimbia na kuacha mlango wazi.
"Hali hiyo iliniwezesha mimi, mdogo wangu na watoto wengine wachache waliokuwa na nguvu kufanikiwa kutoroka, nilimshika mkono mdogo wangu ambaye alionekana kuchoka nikamvuta.
"Watoto wengine wachache waliokuwa na nguvu nao wakatoka, wengi hawakuweza kutoka kutokana na kukosa nguvu, wanaumwa, wana vidonda vikubwa mwilini kutokana na kuchomwa moto na kupigwa shoti ya umeme, wasichana hawakuweza kabisa kutoka kwa kuwa wamefungiwa ndani ya vyumba," alisema Emmanuel
Aliongeza kuwa , alijikokota taratibu na mdogo wake mbali ya maumivu makali waliyonayo akatokea Mswahili mmoja ambaye alikuwa na gari lenye vioo vyeusi akawaambia wapande ili awatoroshe.
"Tulipanda gari hilo akatushusha darajani mpakani mwa Manispaa ya Kinondoni na Wilaya ya Kibaha, jirani na mzani eneo ambalo sisi hatukuwa tukilifahamu...dereva huyo alituambia gari limeishiwa mafuta hivyo alitutaka tumsubiri aende kuyanunua.
"Tulitembea kidogo tukiwa hatujui tunakokwenda... tulikaa kando ya barabara kutokana na uchovu pamoja na njaa kali kwani katika jengo hilo mbali na kazi nzito tulizokuwa tukizifanya na mateso mengi, mlo ulikuwa mmoja tu kwa siku.
"Tulikula saa 10 jioni, wali na maharage...tukiwa kando ya barabara, nilisikia sauti ya baba yangu wa kufikia, dereva wa magari makubwa yanayobeba kokoto ikiniita.
"Nilidhani naota kumbe ilikuwa kweli, alikuja akatukumbatia akalia kwa uchungu kwa namna tulivyokuwa tumechoka na afya kuzorota, akatupeleka polisi ambapo tulipatiwa maji tukaoga na kupewa chakula kizuri na kitamu, tukala na kupata nguvu za kuzungumza vizuri," alisema Emmanuel.
Akizungumza na Majira, Emmanuel alisema baada ya kutekwa yeye na mdogo wake, walifungwa na vitambaa vyeusi usoni hadi walipofikishwa ndani ya jumba hilo la mateso.
Aliiomba Serikali kufanya jitihada za hali na mali ili kuwaokoa watoto wengine waliopo katika jengo hilo.
Mama mzazi wa watoto hao, Martha Godianus (29), ambaye anafanya shughuli za mama lishe, njia panda y a Ba r a k u d a , Ta b a t a Manispaa ya Ilala, alisema amehangaika zaidi ya miezi mitatu kuwatafuta watoto hao bila mafanikio.
"Nimepoteza fedha nyingi kwa kuwatafuta na kutapeliwa mara kadhaa katika kuhangaika," alisema Godianus huku akitokwa na machozi ya furaha katika Kituo kidogo cha Polisi Maili Moja.
Alisema zaidi ya watoto saba walipotea katika mtaa wao, wawili wakapatikana baada ya wiki mbili, wengine wakiwemo wanaye wakawa hawajapatikana na kuomba Serikali ilichukulie kwa uzito suala hilo ili kubaini kundi linalowateka watoto na kuwatesa.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuanza kulifanyia kazi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Dar es Salaam.
Alisema makachero wa polisi wamewahoji watoto hao ili kupata maelekezo ya kufika katika andaki hilo na kuwataka watu wote wenye taarifa za eneo hilo watoe ushirikiano. Credit-Gazeti la Majira.
|
|
''Nicki Minaj''
|
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe amesema ataendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa chama hicho licha ya wiki iliyopita kuvuliwa wadhifa huo na kamati kuu kwa madai amepanga njama ya kukipindua chama.
Akiongea na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana, Zitto alisema atakuwa mtu wa mwisho kutoka ndani ya chama hicho. “Nitakuwa wa mwisho kutoka kwenye chama hiki kwa hiari yangu,” alisema.
“Mimi sitoki. Wanaotaka nitoke, wanitoe wao.”
|
Hii ndio Orodha Ya Washindi Wa Tuzo Za American Music Awards 2013 ambazo msanii Justin Timberlake ameongoza kwa kuchukua tuzo 3. Washindi wako hapa.
Favorite Male Pop Rock Artist - Justin Timberlake Favorite Female Artist, Soul/R&B - Rihanna Favorite Album, Country - Red, by Taylor Swift Favorite Album, Rap/Hip-Hop - The Heist, by Macklemore & Ryan Lewis Favorite Artist, Alternative Rock - Imagine Dragons Favorite Artist, Latin - Marc Anthony Favorite Album, Pop or Rock - Take Me Home, by One Direction New Artist of the Year - Ariana Grande Favorite Male Artist, Soul/R&B - Justin Timberlake Favorite Female Artist, Country - Taylor Swift Single of the Year - “Cruise,” by Florida Georgia Line, featuring Nelly Favorite Album, Soul/R&B - The 20/20 Experience, by Justin Timberlake Favorite Artist, Electronic Dance Music (EDM) - Avicii Favorite Male Artist, Country - Luke Bryan Favorite Band, Duo or Group, Pop or Rock - One Direction Artist of the Year - Taylor Swift
Credit:Sammisago
|
Shindano la kuimba lenye lengo la kusaka vipaji la Epique Bongo Star Search 2013 limeingia katika hatua ya mwisho ambapo wasanii watano wamechaguliwa kuingia fainali na mmoja kati yao atakabidhiwa shilingi za kitanzania million 50 Jumamosi hii (November 30).
Jana (November 24), Mandela Nicholas aliyaaga mashindano hayo akiwa amepata faida ya kufanya wimbo wake wa pekee na moja kati ya producers wanaofanya vizuri kwa sasa Tanzania.
Kuondolewa kwa Mandela kumefanya mshiriki namba 21, Emmanuel Msuya kuwa mwanaume pekee aliyeingia katika fainali huku akichuana na wasichana wanne.
Amina Chibaba, Maina Thadei, Melisa John na Elizabeth Mwakijambile ndio wasichana walioingia fainali. Je, nani atazifanya nyayo za Walter Chilambo? Majibu yatapatikana Jumamosi hii katika fainali itakazofanyika jijini Dar es Salaam.
|
PICHA za aliyekuwa mke wa marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ Wastara Juma akiwa na mwigizaji Bondi bin Salim ‘Bond’ zimezua utata ambao unakazia ukweli wa taarifa ya kuwa wawili hao ni wapenzi.
Kikizungumza na Ijumaa Wikienda chanzo chetu kilicho makini, kilisema kinawashangaa sana Wastara na mwenzi wake huyo kuukana upenzi wao kila kukicha wakati picha zinajieleza.
“Wastara amekuwa akimkana Bond kuwa si mpenzi wake ila ni kaka yake sasa hebu tazama picha zao mpya, hata mtoto mdogo humdanganyi kitu,” kilisema chanzo hicho huku wawili hao wakiendelea kukanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi.
Credit:G.P.L
|
No comments:
Post a Comment