|
|
MAJAMBAZI wanne wakiongozwa na mwanamke juzi usiku walifunga barabara ya Ubungo Maziwa jijini Dar es Salaam na kupora Sh. 600,000 kwa mfanyabiashara wa duka la vyakula kisha kumua dereva la Shirika la Utangazaji (TBC) na kumjeruhi jirani kwa kumpiga risasi sehemu za makalio.
Dereva aliyeuawa ametajwa kwa jina la Ramadhani Giza, mkazi wa Gongolamboto na majeruhi alifahamika kwa jina la Mwarami Mshana mkazi wa Ubungo Maziwa.
Ebdelea kusoma habari hii hapa!!
http://www.djaroarungu.com/2013/11/huu-ndio-ukweli-kuhusu-kuuawa-kwa.html
|
|
Papa Francis |
Papa Francis akimbusu mtu anayesumbuliwa na ukoma kwenye ibada iliyofanyika asubuhi ya leo ndani ya St. Peter’s Square.
Hatuwezi fahamu maneno ya Mungu ambayo Baba Mtakatifu alimuombea mtu huyu, ila ni hii ni ishara ya kutukumbusha habari ya Mafunzo ya Mathayo....
Alipotoka mlimani, umati mkubwa wa watu walimfuata. 2 Na mtu mmoja mwenye ukoma akaja akapiga magoti mbele yake akasema, “Bwana, kama ukipenda, unaweza kunitakasa.” 3 Yesu akanyoosha mkono wake akamgusa, akamwambia, “Napenda. Takasika.” Wakati huo huo yule mtu akapona ukoma wake. 4 Na Yesu akamwambia, “Usiseme cho chote kwa mtu ye yote, lakini nenda ukajionyeshe kwa kuhani na utoe sadaka aliyoamuru Musa, iwe uthibitisho kwa watu kwamba umepona.” –Mathayo 8:1-4
|
Urafiki wa Wanawake: Usiku mmoja Mwanamke hakurudi nyumbani. Asubuhi ilipofika alimueleza mume wake kwamba alikuwa amelala kwa rafiki yake. Mume akaamua kuwapigia marafiki kumi wa karibu wa mke wake. Na majibu ni kwamba hakukuwa na hata mmoja aliyefahamu juu ya hilo.
Urafiki wa Wanaume: Usiku mmoja Mwanaume hakurudi nyumbani. Asubuhi ilipofika alimueleza mke wake kwamba alikwa amelala kwa rafiki yake. Mke akaamua kuwapigia simu marafiki kumi wa karibu wa mume wake, wanane kati ya hao kumi walisema kweli alilala kwao, na wawili waliobaki walisema kuwa bado wapo nae mpaka muda huo.
Wanaume hupenda kuungana mkono minongoni mwao. Unadhani ni kwanini...? Tafakari kwa makini utaelewa maana, ukielewa nieleze kwa faida ya wengine pia...
|
|
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Profesa Sifuni Mchome
Wakati Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne nchi nzima ukiendelea, imebainika kuwa madaraja na alama mpya za ufaulu kwa shule za sekondari zilizotangazwa na Serikali hivi karibuni ni tofauti na zile zilizopendekezwa na Kamati Maalumu
iliyoundwa kuchunguza suala hilo pamoja na zile zilizotolewa na makundi mbalimbali yaliyoshiriki kuandaa mfumo huo mpya.
Mbali na kwenda kinyume na maoni hayo, alama hizo zinaifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza duniani kuwa na viwango vya chini vya ufaulu.
Alama hizo zilizotangazwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome zinaonyesha kwamba: A=75-100, B+=60-74, B=50-59, C=40-49, D=30-39, E=20-29 na F=0-19, huku alama endelevu za upimaji wa mwanafunzi shuleni (Continuous Assessment-CA) ikiwa ni 40 na mtihani wa mwisho ukichangia alama 60.
Kabla ya Serikali kutangaza alama hizo mpya, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliunda Kamati Maalumu iliyopewa jukumu la kufanya uchunguzi na kuja na mapendekezo ya viwango vipya vya ufaulu na utaratibu wa CA.
Kamati hiyo ilifanya kazi hiyo na kukabidhi ripoti yake wizarani Septemba mwaka huu na mapendekezo yake kwenye upangaji wa alama hizo ilikuwa ni A= 80-100, B= 70-79, C= 50-59 D= 40- 49, E= 35- 39 na F= 0-34 huku wakitaka CA iwe alama 25.
Baada ya kuandaliwa kwa ripoti hiyo, Serikali ilitafuta maoni zaidi kutoka kwa wadau wengine kupitia makundi mbalimbali ambayo nayo yalitoa mapendekezo.
Kundi la kwanza lililotoa mapendekezo yake ni Jukwaa la Taasisi za Elimu za Serikali ambalo lilitaka ufaulu uanzie alama 40, kundi jingine ni Vyuo vya Watu Binafsi ambalo lilipendekeza ufaulu uanze alama 35 huku Wakuu wa Vyuo vya Serikali na Wakaguzi Wakuu wa Kanda wakitaka ufaulu uanzie alama 40 na CA iwe 30.
Ofisa mwandamizi kutoka Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), ambaye aliomba jina lake lisitajwe gazetini alisema kitaalamu CA hutakiwa kuwa chini ya alama ambayo inahesabika kuwa ndiyo ufaulu.
Alisema baada ya Serikali kupitisha mfumo ambao ufaulu unaanzia 20, ilitarajiwa CA kuwa chini ya 19 badala ya 40 iliyopitishwa na wizara.
Kwa mujibu wa kitabu kinachoonyesha viwango vya ufaulu duniani kila mwaka cha International Qualification, baada ya Tanzania kutangaza alama hizo mpya, sasa inakuwa nchi inayoongoza duniani kwa kuwa na alama za chini za ufaulu.
Nchi zinazofuatia kwa viwango vya chini baada ya Tanzania ni Kenya, Rwanda, Uganda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) ambazo hata hivyo, viwango vyake vipo juu kwa kiwango kikubwa vikilinganishwa na vile vya Tanzania.
Kenya, Rwanda na Uganda kwa mfano, zinatumia mfumo unaojulikana kwa jina la Flexible Grade Range (mfumo wa kubadilika badilika) ambao viwango vya alama zake vipo kwenye asilimia tofauti na Tanzania ambayo inatumia mfumo usiobadilika wa Fixed Grade Range.
Kenya kwa mfano, viwango vyake ni A=70-100, B=60-69, C=50-59, D=40, 49 F=0-39. Viwango vya Rwanda ni A=90-100, B=80-89, C+=70-79, C=50-69, na F=0-49 na vya Uganda ni A=80-100, B+=70-79, B=60-69, C=50-59, D=45-49 na F=0-44.
Kwa mujibu wa kitabu hicho, DRC na Burundi ambazo zinatumia mfumo usiobadilika kama Tanzania, bado viwango vyake vya ufaulu vipo juu. Viwango vya nchi hizo vinafanana navyo ni: A=90-100, B+=80-89, B=70-79, C+=60-69, C50-59 na F=0-49.
Kwa Afrika, Misri na Ethiopia ndizo zenye viwango vikubwa zaidi vya ufaulu. Misri viwango vyake ni: A=90-100, B=80-89, C=65-79, D=50-64 na F=0-49 wakati Ethiopia ni A=90-100, B=80-89, C=60-79, D=50-59 na F=0-49. Miongoni mwa nchi zenye viwango vikubwa vya ufaulu duniani ni China ambavyo alama zake ni A=100-80, B=79-70, C=69-60, D=0-59. Mwanafunzi anayepata alama chini ya 60 huhesabika kuwa amefeli.
Kwa mfumo mpya hakuna kufeli
Katika kujaribu matumizi ya alama hizo mpya za ufaulu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliiagiza Necta kupanga matokeo ya Kidato cha Nne mwaka 2012 na yale ya Kidato cha Sita mwaka 2013 kwa kutumia alama hizo.
Baada ya matokeo hayo kupangwa, ufaulu wa mtihani wa kidato cha nne ulionekana kupanda na kufikia asilimia 93.74 kutoka asilimia 43 ambayo ndiyo idadi ya wanafunzi waliofaulu mwaka jana baada ya matokeo ya awali ambayo ufaulu wake ulikuwa asilimia 35 kufutwa na kupangwa upya.
Wanafunzi ambao wangefeli, ambao kwa mfumo wa sasa wanaitwa ‘waliopata ufaulu usioridhisha’ ni 23,285 sawa na asilimia 6.26 kutoka wanafunzi 210,846 sawa na asilimia 57 waliopata sifuri kwenye matokeo ya awali.
Kwa upande wa mtihani wa Kidato cha Sita mwaka 2013, mfumo huo mpya uliotolewa unaonyesha kuwa wanafunzi ambao wangefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu ni asilimia 99.67 kutoka asilimia 80 za matokeo ya awali na Daraja la Nne wangekuwa asilimia 0.27 kutoka asilimia 10.18 na wale wa sifuri wangekuwa ni wanafunzi 26 tu sawa na asilimia 0.06 kutoka wanafunzi 2,604 waliopata sifuri kwenye matokeo ya awali.
Kuhusu alama za CA, ofisa huyo mwandamizi wa Necta alisema kwa kawaida walimu hutuma ufaulu wa alama hizo kuanzia 70 mpaka 100 hata kwenye somo ambalo wanafunzi hawakuwahi kusoma tangu walipoanza kidato cha kwanza.
“Kwa maana hiyo, kama mtoto ana CA ya 70, ukiigawanya kwa hiyo 40 ambayo wamesema ndiyo itakuwa wastani wake, mtoto huyo tayari atakuwa na 28, hapo tayari ameshafaulu kwa hiyo mwaka huu hata watoto wote wakiamua kuacha karatasi wazi bado watakuwa na matokeo mazuri,” alisema.
Profesa Mchome hakupatikana kuzungumzia suala hilo kwani simu yake ya mkononi iliita bila kupokewa na wakati mwingine kukatwa.Hata alipoandikiwa ujumbe mfupi (sms), bado hakujibu.
Msemaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ntambi Bunyanzu alisema kwa sasa wanasimamia tamko lililotolewa bungeni kuwa Serikali itawasilisha kauli yake juu ya ufafanuzi wa matumizi ya alama hizo.
Kuhusu kutozingatiwa kwa maoni ya kamati maalumu na wadau, alisema hawezi kutoa ufafanuzi wake kwa kuwa hajaona ripoti ya kamati hiyo.
Mwananchi.
|
Taarifa za kipa nyota, Juma Kaseja kutua Yanga zimewachanganya watu wengi.
Ingawa zimekuwa hazina uhakika, lakini Salehjembe imepata taarifa za uhakika kwamba mchana huu ndiyo amemalizana na Yanga.
Lakini bado watu wamekuwa wakihaha kutaka kujua kuhusiana na suala hilo.
Mmoja wa viongozi wa Yanga alisema; “Sitaki kulizungumzia kwa sasa, kama kuna walioandika sawa, lakini kumalizana kwetu na Juma ni leo (Alhamisi).
“Tulimpa mkataba, anao yeye, hivyo tutakutana na kumalizana leo na tumegawanya makundi mawili, moja litakuwa uwanjani katika mechi dhidi ya Oljoro na lingine katika ishu hiyo ya Kaseja.”
CHANZO NA SALEH JEMBE
|
Rapper mwenye mafanikio makubwa katika ulimwengu wa muziki Jay Z, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kumpa zawadi ya saa yenye thamani ya $ 34,000, mchezaji wa Baseball Robinson Cano katika siku yake ya kuzaliwa.
Utata huo ulikuja kwa kuwa mchezaji huyo ni mteja anaetumia bidhaa za Roc Nation hivyo kuzitangaza, kwa hiyo zawadi kama hiyo inaweza kuchukuliwa kama hongo ama njia ya kumshawishi mchezaji huyo aendelee kutumia bidhaa hizo.
Zawadi ya Jay Z ilivunja masharti yaliyowekwa na shirikisho la Baseball (MLBPA) ambayo yanakataza kampuni yoyote kumpa zawadi inayozidi $ 5000 mchezaji wa Baseball anaetumia bidhaa zake,na kwamba endapo itatokea kampuni inataka kumpa zawadi inayozidi kiwango hicho ni lazima iandike barua kwa shirikisho hilo.
Shirikisho hilo limeanza kumchunguza Jay Z kutokana na zawadi hiyo huku likiwa na ushahidi baada ya mchezaji huyo kuandika kwenye mtandao wa kijamii wa twitter akiishukuru Roc Nation kwa zawadi hiyo, kuweka picha na kuandika thamani yake.
“Thanks to the ROC NATION my birthday gift.” Alitweet mchezaji huyo, na kuongeza, “#2/100 made # Shawn Carter limited edition.”
|
KATIBU Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, amemtaka Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye, kujitambua na kufanya mambo yanayolingana na hadhi yake.
Pia amemtaka atumie muda wake kuwaeleza Watanzania sifa na uwezo wake, badala ya kupoteza muda kuzungumza na vyombo vya habari masuala yenye kumdhalilisha. Akizungumza na Rai jana Makamba alisema; “Nimesoma kwenye magazeti leo na kuona Sumaye akimsema mwenzake (Lowassa), binafsi sikupenda kabisa.
“Wale wanaosoma Biblia katika kitabu cha kwanza cha Timotheo, sura ya 3:1 imeandikwa: Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya Askofu, atamani kazi njema.
“Sasa na mimi nasema mtu akitaka kazi ya urais, basi atamani kazi njema. Hivyo wote wale wanaotamani urais wanatamani kazi njema. Sasa kuna sababu gani ya kusemana mbele ya vyombo vya habari?
“Watanzania wanataka uwaeleza sifa ulizonazo, lakini sidhani kama wanapenda au wanafurahia kuwaona viongozi wakubwa wakianza utamaduni wa kusemana kupitia vyombo vya habari.
“Pia mtu anayepaswa kujisifu ni yule anayetoka vitani, si yule anayekwenda, sasa Sumaye na Lowassa wameshakwenda vitani, kwa hiyo tunazijua kazi zao, uwezo na uhodari wao.
“Hawana sababu yoyote ile ya kulumbana, wasubiri muda ukifika wakachukue fomu, halafu sisi ndio tutaamua kutokana na tunavyowafahamu.
“Sumaye hana sifa ya kuzungumzia rushwa, tunakumbuka alikuwa Waziri Mkuu kwa miaka 10, na katika kipindi cha uongozi wake rushwa ilikuwapo, labda atuambie alifanya nini kukabiliana nayo?”
source-Rai.
|
Ni zaidi ya mwaka mmoja umepita toka kufariki kwa mwigizaji staa wa Tanzania Steven Kanumba, ambae aliacha kampuni ya kutengeneza filamu aliyokua akiimiliki pamoja na mali nyingine yakiwemo magari.
Baba mzazi wa Marehemu Mzee Kanumba anaeishi Shinyanga amesema ‘kwenye mirathi tumeshirikiana na Mama Kanumba ingawa Jaji kachanganya baada ya kuwekwa watoto ambao sio wangu… mimi na mama Kanumba ni sahihi ila watoto ambao sio wangu tumeandaa Mwanasheria kuwaondoa wasiohusika na tumbo langu vinginevyo na wa tumbo langu waingie kwenye mgao wa mirathi’
‘Watoto walioshirikishwa na sio wangu ni Seth Bosco ambae ni mtoto wa shemeji yangu mdogo wake mama Kanumba, Tina Mshumbuzi, Bella Kajumulo yani haya majina unayaona yako tofauti, hawa wawili nilikuta Mama Kanumba ameshazaa.. kwa hiyo hawawezi kuingia kwenye kurithi ndio maana nafatilia Mahakama itende haki na watoto wangu waingie mule vinginevyo aisee patachimbika’ – Baba Kanumba
Kwenye sentensi ya mwisho Baba Kanumba amesema ‘Kanumba hakua na mke wala mtoto hivyo hawezi kuingia mwingine pale, mirathi ni ya watu wawili mimi na Mama Kanumba tuliemleta duniani Kanumba, sijawasiliana bado na Mama Kanumba…. tutawasiliana Mahakamani’
Baba Kanumba ambae hakuweza kuhudhuria maziko Dar es salaam kutokana na kuumwa, anasema kwenye mazungumzo ya mwisho na Marehemu siku kadhaa kabla ya kufariki, alimwambia kuhusu pesa zaidi ya milioni 50 alizokua nazo benki pamoja na nyumba aliyokua ameianza ujenzi Dar es salaam.
|
Posted: 07 Nov 2013 04:49 AM PST
|
Kama unakumbuka kuna wakati wasanii wengi wanaofanya hip hop Tanzania walikataa kujumuishwa kwenye kundi la Bongo Fleva ambalo kwa kawaida lilichukuliwa kama jina lililowakilisha nyimbo za kizazi kipya za hapa bongo zilizoanza kusikika miaka ya 90, na hadi leo kuna wana hip hop ambao hawakubali kabisa kuhusishwa na jina hili ‘Bongo Fleva’.
Mweusi Joh Makini yeye hana tatizo kabisa na jina hilo na anaamini linaweza kutumika vizuri kuwakilisha muziki mzuri wa kizazi kipya wa Tanzania, lakini anachoona hakiendi sawa ni pale ambapo kila anaejaribu kuimba anaingia kwenye hili bus la Bongo Fleva.
Joh Makini alifunguka akiwa ndani ya ‘The Jump Off’ ya 100.5 Times fm, walipoweka mjadala huu mezani akiwa na Saleh Jabir aka Kuvichaka, Dj Ommy na mkali wa RnB Damian Soul.
“Sina tatizo kabisa na hili jina ‘Bongo Fleva’, ni kitu kizuri kwa sababu kama kikisimamiwa kinaweza kuwa ni identity ya muziki ambao unatoka Tanzania.
“Tatizo ni kwamba limekuwa kama treni au basi ambalo kila mtu anaweza kudandia, awe na talent asiwe na talent.” Amesema Mwamba wa Kaskazini.
Amesema kwa hali hii wana hip hop wanaona kama ni shida kukaa kwenye bus moja na watu ambao hawana vipaji.
“Mtu unaona, aaagh..I’m in the same bus with someone...huyu ambae anaibia tu, unaona bora niachie, but Bongo Fleva is a good thing.” That’s Joh Makini.
Joh Makini ameshirikishwa na Damian Soul kwenye ngoma yake mpya ‘Ni Mapenzi’ iliyotambulishwa Jumanne (November 5) kwenye The Jump Off.
SOURCE:Times fm.
|
MEPITA miezi minne tangu msanii mkongwe Bongo, Suzan Lewis ‘Natasha’ aingie kwenye ndoa, juzikati amefunguka kwamba amegundua ndoa ni tamu na anajiuliza kwa nini hakulijua hilo mapema.
Akistorisha , Natasha alisema baada ya kuingia kwenye ndoa amejikuta akifurahia maisha tofauti na yale aliyokuwa akiishi wakati wa ubachela.
“Nafurahia ndoa kwa sababu tuko wawili, nikisikitishwa na jambo napata faraja kutoka kwake. Nikitaka kwenda mbali naomba ruhusa kwa mume wangu, hilo pia linanipa furaha,” alisema Natasha.
|
STAA wa filamu za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameeleza chanzo cha wasanii Bongo kuigiza mapenzi kwenye filamu ni kwa sababu Tanzania hakuna uhuru wa kuigiza.
Akizungumza hivi karibuni jijini Dar, Ray alisema msanii anapoonesha kipaji chake kwa kuigiza kitu kwa ajili ya kuelimisha jamii anarudishwa nyuma kwani wakati mwingine inafikia hatua ya filamu husika kufungiwa.
“Hapa Tanzania hakuna uhuru wa kuigiza kama zilivyo nchi nyingine ndiyo maana kila siku tunaigiza mapenzi tu. Niliwahi kutoa filamu ya Second Wife (Mke wa Pili), Waislam hawakunielewa mpaka baadaye.
Juzikati nilitaka kutoa filamu ya Sista Maria, Wakatoliki wameipinga isitoke, sasa nini kimebaki, ni kuigiza filamu za mapenzi tu,” aliema Ray.
|
No comments:
Post a Comment