.
Wafanyabiashara waliokuwa wakifanya biashara katikati ya jiji na kuondolewa kutokana na ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama, wamelalamika kuwa sasa wanakabiliwa na maisha magumu.


Obama anatarajia kuwasili nchini kesho katika ziara ya kikazi ya siku mbili huku akiambatana na ujumbe wa watu wapatao 700.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mwananchi Jumapili, wafanyabishara hao walisema kuondolewa huko kumewafanya kukosa kipato walichokuwa wakikipata hivyo kusababisha ugumu wa maisha.
Frank Mkama alilalamika: “Hapa Serikali isiseme kuwa wanafanya usafi wa jiji kwa kuwaondoa wafanyabiashara hii si kweli! Mbona hawakufanya zamani, hapa ni Obama ndiyo amesababisha sisi tukaondolewa.”
“Hivi sasa maisha yangu yamekuwa magumu. Kipato ambacho nilikuwa nakipata hapa na kula na familia yangu sasa sikipati.”
Naye, Elizabeth Makata alilalamika Serikali ilipaswa kuwaandaa wananchi kwa kuwaeleza ujio huo wa Obama watanufaika vipi na si kuwafanya waathirike kwa kuvunjiwa maeneo yao.
Alielezea wasiwasi kuwa huenda baada ya ziara hiyo wakashindwa kuendelea na biashara kwa kuwa watakuwa wamekula mitaji.
Kwa upande wake, Ramadhan Issa alisema ziara hiyo ya Rais Obama imeathri maisha yake kutokana na kuvunjiwa kibanda alichokuwa akifanyia biashara hivyo hajui hatima ya maisha yake.
Kadhalika Mwananchi Jumapili iliwashuhudia askari polisi wakionekana kuongezeka katikati ya jiji wakipita huko na kule kuhakikisha hali ya usalama inaimarika.
Pia hali ya usafi imeendelea kuimarika kutokana na ujio kutokana na juhudi zinazoendelea kufanywa kwa lengo la kusafisha mazingira.

Licha kwamba wafanyabiashara hao wameondolewa hivi karibuni baadhi yao wameanza kurejea kuendelea na shughuli zao kama kawaida.

Chanzo:mwananchi.
Hii ajali imetokea huko Anambra State Nigeria baada ya Mke wa mtu kukamatwa na mumewe live
akifanya mapenzi na bwana wake wa pembeni.

Watu wakaona isiwe tabu wakachukua sheria mkononi na kuwalazimisha waendelee kufanya 
mapenzi mbele ya umati wa watu.
Wakati yote hayo yanaendelea mwenye mke hakutaka kabisa kushuhudia badala yake
alienda nyumbani kumfungia mke wake virago.
Haya majanga yalitokea karibu kabisa na Chuo kikuu cha Anambra State.
Kazi kwenu mnaotoka na wake za watu mtakamatwa na kulazimishwa mfanye
sex hadharani kama sio kugandana.










Mwanafunzi mmoja amefumaniwa katika nyumba moja ya wageni (guest house) hapo jana, tarehe 29/6/2013 majira ya saa nane mchana katika eneo la Yombo Vituka jijini Dar es salaam.


Hata hivyo mfumaniwa mwenzake  ( mwanaume ) hajakamatwa kwani aliponyoka na kukimbia.

Wazazi wenye  uchungu na hasira wakiwa na binti yao mara baada ya fumanizi.
Wazazi wakimpiga binti yao kwa uchungu na hasira mara baada ya fumanizi.

(Picha zote na maelezo yameletwa na Dei Misana- Wavuti.com)


Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo yaNje na Ushirikiano wa Kimataifa, Edward Lowassa, amemtahadhalisha Rais Obama kujiepusha na kauli za kuunga mkono ushoga na ndoa za jinsia moja.


 Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, ameliambia NIPASHE Jumapili ofisini kwake jijini hapa jana kuwa ushoga na ndoa za jinsia moja vinaweza `kuiharibu’ ziara yake hapa nchini.

Mapema wiki hii, Rais Obama alikaririwa akizungumzia masuala hayo yanayotajwa kuwa ni moja ya haki za msingi za binadamu, alipokuwa Senegal, lakini akapingwa.
 

“Watanzania hawatalikubali na wataendelea kushikilia uhuru na heshima walizojengewa tangu awali, kwamba ushoga na ndoa za jinsia moja havikubaliki,” alisema.

Akiwa Senegal, Rais Obama alitaka serikali za Afrika kutoa haki kwa mashoga kama inavyotoa kwa raia wengine.
 

"Ninachotegemea, I pray and hope (ninasali na kutegemea) kwamba kuhusu mashoga na ndoa za jinsia moja, Rais Obama hatarudia kauli aliyoitoa kule Senegal,” alisema.

Aliongeza, "ninasema hivi kwa sababu Tanzania hatuamini katika ushoga, na endapo utawalazimisha Watanzania, watakukatalia na kushikilia uhuru na heshima waliyojengewa toka awali."

AHIMIZA MAPOKEZI MAZURI
Hata hivyo, Lowassa aliwataka Watanzania kuiheshimu na kuitumiavema fursa ya kutembelewa na Rais Obama, hivyo wajitokeze kumlaki kwa wingi.
 

"Tutambue mataifa makubwa yanakimbilia maslahi ya karne inayofuata, kwa mfano Rais wa China, Xi Jiping siku moja baada ya kuapishwa kwake alikuja hapa nchini, " alisema.
 

Hivyo, alitoa wito kwa Watanzania kuhakikisha maslahi na fursa za kiuchumi zinakuwa za kwanza kulindwa, kwa kuwa ziara hiyo itafungua milango zaidi kwa wawekezaji kuja nchini.
 

Pia, Lowassa alisema ziara ya Rais Obama ni kielelezo cha amani na usalama uliopo, na kwamba itasaidia kuwavutia watalii na wadau wa sekta nyingine za maendeleo kuitembelea Tanzania.

KITUO CHA KIJESHI
Kuhusu hofu na tetesi kuwa ziara hiyo imelenga taifa hilo kuja hapa nchini kufungua kituo cha kujiimarisha kiulinzi, Lowassa alisema Watanzania wanapaswa kufahamu kuwa tayari nchi hiyo ina kituo cha kijeshi nchini Kenya.


"Tuangalie maslahi yetu tuachane na mitazamo hasi, kama ni kituo cha kijeshi tayari kipo Kenya, tujiulize kwa nini marais wa Marekani Bill Clinton na George Bush walivyofanyaziara zao hapa nchini hawakwenda Kenya," alisema.

WALINZI WA NDANI KUWEKWA KANDO
Kuhusu ziara hiyo kutumia ulinzi wa kimataifa huku majeshi ya Tanzania yakiwekwa kando kwa ushiriki wa moja kwa moja, Lowassa alisema Rais wa Marekani ana kiwango cha juu cha ulinzi unaosimamiwa na nchiyake pekee.
 

"Ni sahihi walinzi wetu kukaa pembeni, huyu ni kama Rais wa dunia, lakini hata majeshi yetu yanafanya kazi ya ulinzi lakini sio kwamba yatakaa nyuma tu," alisema.
 

SUMAYE: TUMKARIBISHE
Naye, Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, alisema ziara ya Rais Obama haina ujumbe zaidi ya kuhimiza watu wajitokeze kumpokea.
 

Hata hivyo, Sumaye alikwepa kuzungumzia kwa undani hatua ya kuwafukuza wafanyabiashara kutoka kandoni mwa barabara, ili kupisha mapokezi ya Rais Obama.
 

“Ninachokielewa ni kuwa barabara ambazo wanapita viongozi kama Rais Obama zinatakiwa kuwa katikahali ya usalama na hivyo kutakiwa kuboreshwa,” alisema.

LIPUMBA: MAFANIKIO NI MADOGO KIUCHUMI
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba, alisema mafanikio ya ziaraya Rais Obama yapo katika kujitangaza kimataifa kuliko kiuchumi.
 

Profesa Lipumba ambaye ni mchumi aliyebobea, alisema changamoto iliyopo ni kwamba bado biashara kati ya nchi mbili hizo siyo kubwa kama ilivyo kwa nchi kama China na Tanzania.
 

Alitolea mfano, mwaka 2012 bidhaa za hapa nchini zilizouzwa Marekani zilikuwa na thamani ya Dola milioni 66 ikilinganishwa na zile zilizouzwa China ambapo zilikuwa ni zaidi ya Dola milioni 500.
 

Alisema bidhaa zilizoagizwa kutoka Marekani zilikuwa na thamani ya Dola milioni 230 huku za kutoka China zikiwa na thamani ya zaidi ya Dola milioni 1,100.

"Utakubaliana nami kuwa mahusiano yetu na China ni makubwa kuliko Marekani licha ya nchi hii kutoa fursa kwetu ambazo hatujazitumia ipasavyo," alisema
 

Profesa Lipumba alisema Marekani kupitia mpango wake wa kusaidia Maendeleo ya Afrika (AGOA), ulitoa fursa kwa bidhaa za Afrika kuuzwa nchini humo bila ushuru, lakini Tanzania haikuitumia.

Pia alisema utawala wa George Bush, uliisaidia Tanzania kupitia Mfuko wa Changamoto za Milenia (Millenium Challenge Compact (MCC) kupewa Dola milioni 700 kwa ajili ya kusaidia miundombinu na ujenzi wa nyaya za umeme kutoka bandarini hadi Zanzibar.

"Pana uwezekano wa mpango wa pili wa MCC, Tanzania ikapata msaada wa kuimarisha miundombinu ya umeme, lakini pia kampuni za Marekani kuja kuwekeza hapa kwetu," alisema.
 

Alisema uwekezaji wa kampuni hizoutategemeana na wafanyabiashara wa hapa nchini pamoja na serikali kutumia fursa mbalimbali za nchi hiyo.
 

Katika hatua nyingine, Profesa Lipumba alisema ili nchi iweze kujikwamua na umasikini itatokana na jinsi itakavyotumia sera na juhudina siyo kutegemea msaada kutoka nje.
 

HOTELI ZIMEJAA
Wingi wa wageni wakiwamo watakaofika kwa ajili ya ziara ya Rais Obama, umesababisha hoteli nyingi za jijini Dar es Salaam `kujaa’.
 

Uchunguzi wa NIPASHE Jumapili ulibaini kwamba kwa zaidi ya wiki sasa, hoteli nyingi hazikupokea wageni kutokana na kile kilichoelezwa kuwa, nyingine zililipiwa ingawa vyumba havikutumika kwa wakati.
 

POLISI: WASIO NA KAZI WASIJE MJINI
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga, amewataka wananchi ambao hawatakuwa na mambo muhimu ya kufanya katikati ya jiji, wasifike huko kupunguza msongamano wa watu na magari baada ya kuwasili kwa Rais Obama.
 

Alisema, baadhi ya barabara zitafungwa kwa muda kwa ajili ya viongozi kuzitumia, hivyo kusababisha msongamano.
 

Hekaheka zimetanda jijini Dar es Salaam, ikiwa ni zaidi ya saa 24 kabla ya kuwasili kwa Rais Barack Obama.
 

Rais Obama, atawasili nchini kesho akitokea Afrika Kusini, ambapo pamoja na mambo mengine, alizungumza katika mkutano wa ‘viongozi vijana wa Afrika’ na kujibu maswali kutoka nchi tofauti.
 

Mkutano huo ulifanyika jana jioni huko Soweto nchini Afrika Kusini, ambapo alipokewaa na kujibu maswali kutoka Kenya, Uganda, Nigeria na Afrika Kusini kwenyewe.
 

Jijini Dar es Salaam, shughuli kadhaazikiwamo za ulinzi na usalama, zinafanyika kwa kasi na umakini kuhakikisha ziara ya Rais Obama inafanyika pasipo bughudha. kujibu maswali kutoka Kenya, Uganda, Nigeria na Afrika Kusini kwenyewe.
 

Jijini Dar es Salaam, shughuli kadhaazikiwamo za ulinzi na usalama, zinafanyika kwa kasi na umakini kuhakikisha ziara ya Rais Obama inafanyika pasipo bughudha.
 

Hata hivyo, sehemu kubwa inayohusu masuala ya itifaki, ulinzi na usalama yanafanywa na taasisi za Marekani, kwa kuzishirikisha taasisi za ndani kwa kiwango kidogo.
 

“Hawa jamaa (Wamarekani) wanapoingia nchi yeyote wakiwa naRais wao, shughuli nyingi na uamuzi wanafanya wao, sisi wa ndani inakuwa kushirikishwa kwa kiasi kidogo,” kilieleza chanzo cha NIPASHE Jumapili kutoka moja ya taasisi zinahusika katika ziara hiyo.
 

Maeneo kadhaa ya jijini humo, yaliendelea kudhibitiwa kwa ulinzi mkali na doria za mara kwa mara, huku kandoni mwa baadhi ya barabara wakionekana askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ).
 

Mathalani, kandoni mwa barabara ya Morogoro, eneo la Ubungo, walionekana askari wa JWTZ maarufu kama MP.
 

Shughuli nyingine zimehusisha pia operesheni zinazofanywa na polisi kwa kusaidiana na mgambo wa jiji, kuhakikisha watu na bidhaa zilizopokandoni mwa barabara zitakazotumika kwa ziara ya Rais Obama, vinaondolewa.
 

Magari yaliyowabeba polisi wenye silaha za moto na mabomu ya machozi, yalionekana katika mitaa kadhaa jijini humu, wakihakikisha operesheni hiyo inafanyika pasipo kikwazo kutoka kwa wahusika.
 

Kila palipofanyika operesheni hiyo, baadhi ya askari walifanya doria zamu kwa zamu, kuhakikisha kuwa bidhaa na watu walioondolewa, hawarejei.
 

Hata hivyo, waathirika katika operesheni hiyo walieleza kutofurahia, huku wakihoji ni kwa nini serikali haikuwaandalia mazingira mbadala kabla ya utekelezaji wake. 
  
Walisema miongoni mwao, wamekopa mitaji kutoka kwenye taasisi za kifedha, hivyo kusimamisha biashara zao ili kupisha ujio wa Rais Obama, kutawaweka katika hali ngumu kiuchumi.
 

“Ikiwa ujio wa Rais Obama unatutesa wafanyabiashara kiasi hiki, ni vigumu kuhimili maisha yetu, kwa sababu hatujui hatma yetu baada ya yeye kuondoka,” alisema mfanyabiashara Zena Rashidi wa Kariakoo.
 

Hata hivyo, wamachinga walionekana jana katika kituo cha mabasi cha Mwenge walipofukuzwa, wakiwa wanaendelea na biashara zao.

Lakini walifanya hivyo kwa tahadhali ikiwamo kushika bidhaa chache mikononi, huku wakitumia 'janja' ya kupiga kelele za 'kumsifia' Rais Obama.
 

Walisikika miongoni mwao wakisema, 'praise to Obama' na wengine wakaitikia 'aaamen'. Walifanya hivyo zamu kwa zamu, lakini haikujulisha waliashiria nini.
 


BARABARA ZAPAMBWA
Aidha, barabara zote atakazopita Obama wakati wa ziara yake zimepambwa kwa bendera za Marekani na Tanzania; huku zikinakshiwa kwa picha yake ambayo imeandikwa 'President Barack Obama' karibu Tanzania.
 

Barabara hizo ni ile ya Nyerere kuanzia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Mwai Kibaki na Bagamoyo.

NIPASHE Jumapili imeshuhudia pichana bendera hizo zikiwa zimewekwa kwenye mabango yote yaliyo barabarani kuanzia Ikulu hadi kwenye barabara hizo huku usafi wa jiji ukionekana kuimarika zaidi.
 

Jana gazeti hili lilishuhudia karibu barabara zote, vijana wanaofanyakazi ya kuweka bendera na picha ya Obama wakifanyakazi hiyo.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Mahakama ya mwanzo Makete mjini wilayani Makete mkoani Njombe imemuhukumu katibu wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wilaya hiyo Bw Godfrey Mahenge (63) kwenda jela miezi 9 kwa kosa la kutotii amri halali ya jeshi la polisi Makete


Akitoa hukumu hiyo hakimu wa mahakama ya mwanzo Makete mjini Mh. John Mpitanjia amesema mtuhumiwa huyo alitumia lugha ya matusi kwa askari polisi na kuwaita kuwa ni wauaji na kudai kuwa wametumwa na chama cha mapinduzi (CCM)


Amesema baada ya mahakama yake kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashataka, mshtakiwa alitakiwa kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani lakini kutokana na kutenda kosa hilo kwa mara ya kwanza mahakama imeamua kumfunga miezi 9 gerezani ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo..



Mshtakiwa huyo hakuwa na lolote la kijitetea na hakimu kumpatia adhabu hiyo na kusema kuwa rufaa kwa mshtakiwa ipo wazi endapo anahisi ameonewa.


Chanzo:mpekuzi huru.
http://4.bp.blogspot.com/-QyjDD0XFVBk/UdBOAk5u4tI/AAAAAAAAYuE/4HWq8DhHJOw/s640/Mamaaa+yangu+weee...nisamehe+sitarudia.JPGKIBAKA Rajabu Hamisi Juma (15), Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Msasani, iliyoko Manispaa ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro, amenusurika kuuwawa na wananchi wenye Hasira kali baada ya kufamaniwa mchana wa leo akiiba katika Duka la mfanyabiashara Paulo Maile. 

Kibaka huyo ambaye ni mkazi wa Pasua, amekutwa na masahibu hayo baada ya
kuingia dukani hapo kwa kudhani kuwa mhudumu wa duka yuko mbali na ndipo
alipokutwa akiwa tayari ameshaiba Simu, aina ya Nokia huku akijaribu kuficha Laptop iliyokuwa dukani hapo.

Akizungumzia mkasa huo, kibaka Rajabu huyo aliamua kufanya hivyo kwa ajili ya kukosa ada ya kulipa shule kutokana na wazai wake kukataa kumlipia adaanayodaiwa shuleni hapo.
Tukio hilo lililowaacha mdomo wazi baadhi ya mashuhuda waliofika dukani
hapo , limetokea leo majira ya saa 6:10 mchana katika duka la Nguo
lililloko katika mtaa wa double Road, barabara kuu ya Moshi-Dar es
salaam linalomilikiwa na mfanyabiashara Paulo Maile mkazi wa Soweto.

Kuna ukweli kwamba, mwanaume ana namna tofauti ya kuyatazama na kuyakabili mambo, hasa anapokuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi. Kwa mfano, mwanamke anapokuwa maarufu, ni hatari sana kwake kujaribu kuutumia umaarufu wake katika kumshusha mumewe. Lakini, hata jaribio la kumwonesha mumewe kwamba, yeye ni zaidi yake ni kosa kubwa.


Ni kosa kubwa kwa sababu kwa asilimia ya kutosha wanaume wanawaogopa wanawake, ‘smart’ siyo hapa kwetu tu, bali hata Ulaya na Marekani. Kwenye tafiti fulani za hivi karibuni katika nchi za Ulaya na Marekani ilibainika kwamba, wale wanawake wenye kuonekana kuwa wanajua mambo mengi kuliko wanaume, wanaolewa kwa shida sana ukilinganisha na wale ambao, hawajui au wanajifanya kwamba, hawajui mambo.

Tafiti hizi zinaonesha kwamba, kwa kadiri mwanamke anayokuwa na uwezo zaidi wa kiakili, kulinganisha na wanaume wengi, ndivyo jinsi nafasi yake katika kuolewa inavyopungua kwa wastani wa asilimia 40.


Utafiti uliowahi kufanywa na chuo kikuu cha Michigan huko nchini Marekani, ulionesha kwamba, wanaume huamini kwamba, mwanamke ‘smart’ anakuwa kwenye nafasi nzuri ya kufanikiwa. Kwa wanaume, mafanikio ya mwanamke hasa kazini, yana maana ya mwanamke huyo kuwa katika nafasi ya kuzini sana. Unaona ilivyo eh..!

Ukweli ni kwamba, wanawake wengi kiasi cha kutosha walio ‘smart’ huathiriwa sana na mitazamo ya wanaume, pale inapotokea kwamba, mwanamke anaingia kwenye mafanikio ya kipato, yu mjanja zaidi au ana uwezo mkubwa kiakili kuliko mwanaume. Lakini cha ajabu ni kwamba, idadi ya wanawake wanaowazidi wanaume kimali na kiakili inazidi kuongezeka kila uchao. 

Haiyumkini hiyo ndio sababu kuna idadi kubwa ya wanawake wenye mafanikio ambao wamezalishwa na kutelekezwa na wanaume, huku ndoto zao za kuolewa na kujenga familia zikionekana kuwa ngumu kutimia.

Kwa bahati mbaya sana wanawake hawa hawafanikiwi kwenye matarajio yao ya kuolewa kwa sababu akilini mwa wanaume kuna kitu tofauti kinatembea humo. Kuna kitu chenye kuwaambia kwamba, mwanamke ‘smart’ hafai kabisa kuolewa……! 

“HII sasa ni kufuru!” Hivi ndivyo utakavyoweza kusema kwa Davies Mosha ambaye ni makamu mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga, ambaye nafasi yake kwa sasa klabuni hapo inashikiliwa na Clement Sanga.

Kwa tafsiri ya haraka, yawezekana Mosha anaweza kuwa ndiye kiongozi pekee wa soka nchini kumiliki gari la kifahari na lenye gharama kubwa aina ya Lamborghini kama ambalo linamilikiwa na mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney.
Gari analomiliki Mosha ambalo lina rangi ya njano, linaaminika kuwa miongoni mwa magari yenye thamani kubwa siyo tu Tanzania na Afrika, bali duniani kote, kwani hata siku Rooney alipolinunua wenzake wengi hawakutegemea, siyo kwa sababu hana fedha, ila kwa kuwa hakuwa mtu wa matumizi ya magari yenye thamani kubwa kama hilo.
Yafuatayo ni maelezo kuhusiana na gari hilo la kifahari kwa kuanzia kiwango cha mafuta na usumbufu anaoupata akiwa katika mizunguko yake.


Ameinunua kwa bei gani?
“Kutokana na ubora wa gari hili, nililazimika kutoa shilingi bilioni moja kwa ajili ya kulinunua, kama unavyojua ni fedha nyingi, nimenunua kwa mapenzi yangu.
“Hili gari kaniuzia mtoto wa Bakhresa (Yusuph), baada ya kufikia makubaliano kati yake na mimi, aliniuzia Julai 2011.
“Hili gari kasi yake ya mwisho ni 360, ni kasi kali na inatosha kwa matumizi yangu binafsi.

“Matumizi ya mafuta ni ya kawaida wala siyo ya kuogopesha sana, inategemea na umbali utakaotembea.
Usumbufu anaoupata“Usumbufu mkubwa ninaoupata kiukweli, nikiwa naendesha barabarani, madereva wengine wanalishangaa sana, hali inayosababisha kutokea ajali au msuguano mara kadhaa.“Hivi karibuni dereva mmoja aliigonga sehemu ya tairi la nyuma kushoto kutokana na kuishangaa, ilikuwa maeneo ya Masaki hapahapa Dar es Salaam.
“Matengenezo yake yaligharimu pauni 20,000 (zaidi ya shilingi milioni 50), hali iliyosababisha niwe makini nikiwa naendesha,” anasema Mosha.
SOURCE: GPL 

Nchini Thailand, Nyati  amezaaa mtoto anayefanana sana na mwanadamu. Hizi ni picha ya nyati zikionyesha uso  na wa binadamu hasa yake ambayo ni sawa . Hata hivyo, mikono yake na miguu inafanana  zaidi na  nyati. Lakini kwa ujumla nyati anafanana sana na ng’ombe. Lakini sio kwa binadamu.
Unbelievable+Human-like+Buffalo+Birth
Kwa bahati mbaya kiumbe huyu alikufa muda mfupi baada ya kuzaliwa. Hli jambo limeleta gumzo na mtafarukiu mkubwa katika kijiji hicho kuna imani kwamba tukio kama hilo linata baraka kwa watu wote wa sehemu tukio lilipotokea. kutokana na imani hii watu wengi wameonekana wakiomba na kusali ili wapate baraka. uso wa kiumbe  huyu huwezi kutofautisha ni binadamu au ni nyati alisikika mwanakijiji mmoja.


 Ramadhani Mahanga ambaye amenusurika kuuawa baada ya kukatwakatwa mapanga na kijana mwenzake anayefahamika kwa jina la Juma  Hamisi ambaye alidai anatembea na mkewe na hivyo kuchukua uamuzi wa kutaka kumuua  katika kijiji cha Isenga manispaa ya Tabora.


Baba wa kijana  Juma Hamisi ambaye anadaiwa kumkatakata  mapanga Ramadhani Mahanga akiwa amekwenda kumjulia hali katika Hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete ambako amelazwa kwa ajili ya matibabu.


WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, amesema usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda ni sera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya kusaidia kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana.


Akizungumza katika haraambee na uzinduzi wa mfuko wa waendesha pikipiki maarufu mkoani Arusha, Lowassa alisema sera hiyo ni ya kuwakomboa vijana.



Alisema kuwa kitendo cha wafanyabishara wa Arusha kujipanga kusaidia bodaboda ni mfano kwa wafanyabishara wengine nchini.



“CCM ni chama kinachotetea wanyonge, na nyinyi ni wanyonge mnaohitaji kunyanyuliwa kimaisha, kitendo hiki cha wafanyabisharaa wa Arusha ni cha kuunga mkono sera ya CCM,” alisema.



Lowassa alisema tatizo la ajira ni bomu linalosubiri kulipuka na kwamba wasipowasaidia vijana kuondokana na tatizo hilo amani itatoweka.



“Ndiyo maana CCM katika ilani yake ya uchaguzi imeliweka hilo na pia kulisisitiza katika vikao vyake vya juu vya Mkutano Mkuu pamoja na Halmashauri Kuu,” alisema.



  Wafanyabiashara maarufu jijini Arusha wakiongozwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Diwani wa Mererani, Mathias Manga, ndiyo waliyobuni wazo hilo la kuwaanzishia mfuko vijana wa bodaboda.

Katika harambee hiyo, sh milioni 84 zilipatikana huku Lowassa pamoja na marafiki zake wakichangia sh milioni 10 na pikipiki 10.

source:Masainyotambofu.

1. Kutokuwa na mawasiliano ya karibu na mwenzi wako.
2. Kutojali maumivu ya mwenzi wako.
3. Ubishi usiokuwa na maana.
4. Kupenda kujihesabia haki.
5. Kutokubali makosa.
6. Kutokuwa na roho ya msamaha.
7. Kutokuwa muwazi kwa mwenzi wako.
8. Usaliti wa mapenzi.
9. Kuigiza kupenda.
10. Kutomheshimu mwenzi wako.
11. Kuwa mjuaji kila kitu unajifanya unajua.
12. Kutokutambua uthamani wa mwenzi wako katika maisha yako.
13. Kuwa na jeuri.
14. Kutokuwa na kifua cha kuficha mambo ya nyumbani. [chumbani]
15. Kuto kujali watu wa nyumbani kwako [ndugu,watoto n.k]
16. Kujiamulia kufanya vitu bila ushauri wa pamoja.


17. Kutokuwa na faraja na mwenzi wako [kutokujua jinsi ya kumfariji mwenzi wako]
18. Kutomridhisha mwenzi wako kimapenzi.
19. Kuwa na amri kwa mwenzi wako hata kwa mambo yasiyokuwa na maana au malengo katika maisha yenu.
20. Ugomvi wa muda mrefu usiokuwa na suluhu.
21. Kuwa na ahadi za uongo.
22. Kumdhalilisha mwenzi wako mbele za watu.
23. Kupenda starehe kuliko kuujenga uhusiano wa kudumu [love]
24. Uchafu kutojipenda na kupenda mazingira yako.
25. Maudhi ya mara kwa mara.
26. Kutoonyesha hisia kali hisia kali za mapenzi kwa mwenzi wako.
27. Kutokuwa karibu na mpenzi wako mara anapokuwa katika msongo wa mawazo.
28. Kutokuwa mbunifu wa maisha mapenzi.
29. Kutokuwa na msimamo katika maamuzi yako [kutoendeshwa na watu]
30. Kutokuwa na muda na mwenzi wako.
31. Kutokuwa na shukrani.
32. Kutokujua gharama za upendo.
33. Kuwa na wivu wa kijinga.
34. Kuwa mbinafsi.
35. Kujifanya kuwa [busy] na kushindwa kumtunza na kumjali mwenzi wako
36. Kutokuwa na imani juu ya mwenzi wako.
37. Kutokubaliana na hali halisi ya maisha yenu.
38. Kutokukubali kujifunza.
39. Kutokutambua maana ya mapenzi na umuhimu wake.


Tabia hizo ndizo zinasababisha mahusiano ya watu wengi kuvunjika, hata
ndoa kuharibika maana huyu mtu unayemfanyia hivi ipo siku atachoka,
maana hana moyo wa jiwe bali ana moyo wa nyama. Kuvumilia nako
kunamwisho wake, hizo tabia ndizo zimechangia maumivu, vidonda vya
mapenzi, vifo vya watu wengi na kuwafanya watu wengine kuchukia kupenda
na kupendwa katika maisha yao



Edimoblaze


Rais wa Marekani, Barrack Obama (kulia) akiwa na mkewe Michelle, wakiwa katika vazi la kiasili la kizulu, walipotembelea nchini Afrika Kusini


Anatembea miguu juu mikono chini.

Nani kakwambia pesa hainyenyekewi.Tupigie magoti bila sisi wewe ni nothing.

Huyu akiwa demu wako na uko naye Ukumbini kachomoka ghafla
Kwenda kumkatikia msanii jukuani unaweza fanya nini?



Nilikuwa mkoa flan hv nilikutana na tamadun mmoja hv ambayo kiukwel ckuipenda kwa upande wangu ni pale nilikutata na binti mmoja kwenye huo mkoa.

akaniambia samahan kaka, nikamwambia bila ya samahan akaniuliza unaitwa nan , nikamjibu.

baada apo akaniambia kuna mtu anakuitwa nyumban pale alinioneshea kwa kidole nikamwambia nan akanijib ni mwanamama tu.

tukaenda nae yule mama akanikaribisha vizuri kwake tukaanza kusalimiana kaniuliza wapi natokea nikamjibu na nikamwambia kwa sasa nipo kwa grandmother wang hapa .

kidogo chakula kikaletwa na yule binti ambaye alînileta pale tukala c unajua tena kijijin nyama za kuku wa kienyeji nikafurahia .tulipo maliza yule mama akanza kuniambia mm cjaole kwa matatizo tu xa kibinadam kwa mm ni tasa cwez kuzaa.

hapo hapo nikamuuliza mama na hawa watoto ni wanani maana kulikuwa na watoto kama wa3 hv.

majibu y kawa hv hawa ni watoto wangu ,nikauliza tena mbna ww umesema kuwa hauwez kuzaa kanijib nikwamba mm ndo huwa naoa mabinti nalipa mahal wale watoto watakao patikana ni wakwangu mm ndo nafanya hyo , mungu wanguee sasa mama hauoni kwamba siku hiz kuna magonjwa meng ya zinaa je hao wake zako huwa unawashaur kuhus haya ,kajib ndio.

baada hapo nikamwambia mama mie naenda kaniambia subiri mwanangu nikuambie nilichôkuitia nika mwambia sawa niambie.

akanzg hv kijana wangu naomba unisaidie kîtu kimoja kauliza kitu gan mamaangu , akaniambia nimetokea kukupenda hyo chonde chonde nisaidie mke wangu mmoja naomba utembee nae mpaka apate ucjauzîto ukifanikisha hlo ntakupa Zawadi.

nikamwambia mama kweli hlo cwez kabisa akaendelea kunisih nikamwambia naomba nikafikirie kuhusu hil maana nilikuwa natafuta njia ya kuôndoka nikasema mm Abby cwez fanya upumbav kama huu.

kesho yake akaja yule binti akaniambia unaitwa nikamwambia nakuja .ilibid niondoke huô mkoa bila kupenda.



Nilichojifunza katika Safari Ya Obama Hapa Tanzania especially DSM.
1.Tanzania na Daresalaam Inaweza Kuwa safi kama Kilimanjaro,sema Tuu Ni Uvivu wa wasimamizi Husika.

2.Inawezekana Kupiga maendeleo Kwa Taifa la Tanzania Kwa Haraka kama energy iliyotengenezwa na viongozi na Kuipeperusha kwa wananchi kuwa na Joto kuwa Obama anakuja nao wote story zao zote Ni Obama anakuja,Basi spirit kama Hiyo Ikatengenezwa kwa Vijana Kuwa wajasiriamali na Kujaribu Kwa fursa mbalimbali nchi Tz itapiga Hatua.

3.Tanzania Kuna fursa Kubwa za Utalii,sasa Kama Hilo ni dili Basi wadau wote wa sekta ya Utalii wakae Pamoja na Kujadili na Kupanga way Forward sasa,Tuanze wekeza Hela za maana Kwa Vituo kama CNN,BBC,CCTV,CBC,etc Kuliko njia ya sasa Ya Kutumia Hela Kidogo kidogo kwa Kwenda club ndogo ndogo Ulaya na 
kutangaza Utalii,ALWAYS CHEAP IS EXPENSIVE.

4.Akili za Watanzania zinamchukulia Obama kama celebrity(Super star) na sio Fursa Ya Kujikwamua Kiuchumi,Inabidi Tubadilike Tuangalie sasa Nini Tufanye ili Tunufaike Kiuchumi.

5.Tunaweza Kuwa Wabaguzi wa kiuchumi,kama Yalivyo mataifa mengine Jirani na makubwa dunia Yana ubaguzi wa kutoa Tender kwa wageni na kujali wazawa.TUWE WABAGUZI WA KIUCHUMI SIO WABAGUZI WA RANGI AU KABILA AU DINI AU NINI!

Na wewe mdau umejifunza nini kuja kwa Obama.Mwenzetu Deo Kilewa katowa ya moyoni.
Wapenzi wameanguka na kufa baada ya dirisha walipokuwa wakifanyia mapenzi kufunguka ghafla nchini China.

Wawili hao wanasemekana kudondoka kutoka kwenye dirisha la jengo moja la makazi kwenye jiji la Wuhan nchini humo pale dirisha hilo walilokuwa wameegemea kufunguka.



Mashuhuda walivieleza vyombo vya habari vya China kwamba wapenzi hao walikumbatiana wakati wakianguka kwenye njia ya waenda kwa miguu nje.