advert

http://

Monday, 30 June 2014

Chui apanda boti na kumshambulia mvuvi akiwa na watoto wake.


Chui apanda boti na kumshambulia mvuvi akiwa na watoto wake
Imeripotiwa kuwa chui mwenye hasira na njaa aliingia majini na kupanda boti ya mvuvi aliyetajwa kwa jina la Shushil Manjhi huko Kolkata, India na kuondoka nae.

Taarifa zilizoripotiwa na vituo vya nchini India vinaeleza kuwa, mvuvi huyo alikuwa na watototo wake wawili (wa kike na wakiume) wakijaribu kutafuta kitoweo karibu na hifadhi ya taifa ya Sunderbans yenye wanyama wakali.
Mwanae wa kiume, Jyotish alieleza kwa njia ya simu kuwa chui huyo alirukia boti na kumkamata baba yake shingoni kwa upande wa nyuma na kuanza kumburuza akiondoka nae akielekea msituni.
“Alimrukia baba yangu kwa haraka mgogoni na kung’ata kwa nguvu kabla hajatokomea nae msituni.” Alieleza.
Mtoto huyo anaeleza kuwa baada ya chui huyo kumkamata baba yake, yeye na mdogo wake walijaribu kumpiga na fimbo na visu walivyokuwa navyo lakini hakuweza kumuachia.
Tukio hilo linatoa picha ya maisha duni ya wananchi masikini wa eneo hilo ambao licha ya kuwa na hatari kubwa ya kuuawa na wanyama wakali, hali ngumu ya maisha huwasukuma kuingia msituni kusaka kitoweo au chochote licha ya kwamba ni kinyume cha sheria kufanya uvuvi katika eneo la hifadhi ya wanyama.
Inaelezwa kuwa samaki wanaopatikana katika hifadhi hiyo hunuliwa kwa pesa nyingi katika miji ya jirani na vijiviji vya eneo hilo.

BOFYA HAPA UWACHEKI HAWA JAMAA KATIKA VIDEO, NI SHETTA FT DIAMOND, ILA NI FEKI SIO WENYEWE REAL https://www.youtube.com/watch?v=bRDoVEh9eh8


M 2 THE P AKIWA NA SWAHIBA WAKE NGWEAR KIPINDI HICHO
BOFYA HAPA KUINJOI SHOW YAKE  https://www.youtube.com/watch?v=WRtmRKzL5Zw&feature=em-subs_digest

Msichana aliyemuua mama yake kwa kumchoma visu mara 151 akwepa jela
 Taarifa kutoka Colorado, Marekani zinaeleza kuwa Msichana mwenye umri wa miaka 19, anaefahamika kwa jina la Isabella Yun-Mi Guzman ambaye alimchoma mama yake visu mara 151 ameachiwa huru.

 Mahakama imemuachia huru Isabella baada ya kubaini kuwa ni mgonjwa wa akili na kwamba wakati anatekeleza tukio hilo hakuwa katika hali ya kawaida kiakili hivyo kwa mujibu wa sheria hana hatia.
 Mahakama imeamuru msichana huyo kupelekwa katika hospitali ya wagonjwa wenye matatizo ya akili kwa ajili ya kupata matibabu badala ya kumpeleka jela.
 Kwa mujibu wa ripoti zilizofikishwa mahakamani hapo na polisi, Issabella alimchoma mama yake visu mara 151 (Mara 35 usoni, mara 51 shingoni, na mara 65 katika sehemu nyingine za mwili.
 Msichana huyo amepelekwa  Colorado Mental Health Institute.   



Millard Ayo (Mtangazaji machachari wa Clouds Fm) ameibuka kidedea kwa kunyakua tuzo mbili,
hivyo vikiwa ni vipengele vyote alivyoshindanishwa. Kilele cha Tuzo hizo kilikuwa ni Ijumaa hii
katika Serena Hotel, Dar es Salaam.

Kumbuka tu kwamba hivi majuzi nilikujuza kwamba Wema alikuwa mstari wa mbele kuwashawishi mashabiki kumpigia kura Millard Ayo, unaweza kujikumbusha hapa http://www.babamzazi.com/2014/06/millard-ayo-na-wema-sepetu-mhhh.html Je hatuwezi kusema Wema amechangia kwa kiasi kikubwa kushinda kwa Millard? Maana Wema ana fans wengi sana, na kama fans wake wote wamemuunga mkono kwa kutekeleza kile achowaomba nazani hilo halikuwa la kutowezekana. Picha kati ya waili hawa ikiendelea, basi ww.babamzazi.com itaendelea kuwajuza.

Tuzo alizonyakua Millard ni ya MTANGAZAJI WA REDIO
ANAYEPENDWA na KIPINDI CHA REDIO KINACHOPENDWA (Ambacho ni AMPLIFAYA)

Hongreara sana  Millard Ayo kwa kunyakua Tuzo mbili

Washindi wengine katika vipengele mbalimbali ni kama ifuatavyo:

1 na 2 = MILLARD AYO

3.MTANGAZAJI WA RUNINGA ANAYEPENDWA = Salim Kikeke – BBC Swahili

4. KIPINDI CHA RUNINGA KINACHOPENDWA= Mkasi – EATV

5. MWANAMICHEZO ANAYEPENDWA=Juma Kaseja – Yanga

6. MUONGOZAJI WA VIDEO ZA MUZIKI ZINAZOPENDWA =Nisher

7. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIUME=My Number – Diamond

8. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIKE= Yahaya – Lady Jaydee

09. MUIGIZAJI WA KIUME KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA= King Majuto

10. MUIGIZAJI WA KIKE KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA =Elizabeth ‘Lulu’ Michael

11. FILAMU INAYOPENDWA =Ndoa Yangu



     SOURCE:D'JARO ARUNGU

Saturday, 28 June 2014

Canada wamefungisha ndoa 115 za jinsia moja kwa wakati mmoja.



wedding2
Wapenzi wa muda mrefu Richard Laslett na Collin Gunther ambao wamedumu kwenye mahusiano kwa muda wa miaka 37 wamepata nafasi ya kuwa moja kati ya wapenzi wa jinsia moja 115 waliofungishwa ndoa kwa wakati mmoja mjini Toronto, Canada.

weddind
Ndoa hizo zimefungwa kwa pamoja na kuwakutanisha wapenzi wa jinsia moja kutoka maeneo mbalimbali duniani kusherekea nguvu ya mapenzi yao.
Meya wa Toronto Norm Kelly amesema wanandoa hao wamekutana na kufurahia hatua hiyo muhimu ya kufunga pingu za maisha.
wedding3 
Takribani nchi 15 duniani sasa zimeruhusu mapenzi ya jinsia moja .
lesbian

ChargingCables22
Mamlaka nchini Australia imetoa tahadhari dhidi ya matumizi ya charger aina ya USB feki au zilizo chini ya viwango huku zikiwa zimechomekwa kwenye umeme baada ya mwanamke mmoja kufariki dunia wakati akitumia charger ya aina hiyo kucharge simu yake iliyokuwa imechomekwa kwenye kompyuta yake ndogo.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 28 alikutwa amevaa headphones masikioni akiwa na kompyuta yake mikononi huku akiwa na majeraha ya kuungua kifuani na masikioni nyumbani kwake huko Gosford, Kaskazini mwa Sydney.
ChargingCables
Polisi nchini humo bado wanafanya uchunguzi kujua mazingira ya kifo hicho lakini kitengo cha biashara kilichofuatilia suala hilo kimetahadharisha kuwa charger za simu zilizo chini ya viwango ni moja ya sababu kubwa.
Mwanamke huyo ambaye ripoti zinadai kuwa anatokea nchini Ufilipino na baadae kuwa raia wa Australia alivaa headphones zilizokuwa zimechomekwa kwenye kompyuta ndogo iliyokuwa imechomekwa kwenye socket ya umeme.
Eminem alizuiwa kuperform Uingereza kwa kuwa nyimbo zake zina matusi

 Ripoti zilizoandikwa na gazeti la The Daily Mirror zinaeleza kuwa lugha ya matusi kwenye nyimbo za Eminem ndio chanzo cha yeye kukataliwa kufanya show kwenye eneo la Hyde Park, Uingereza.

 Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mmiliki wa Hyde Park, Linda Lennon ameeleza kuwa aliamua kutompa nafasi Eminem kuperform katika eneo hilo kwa kuhofia ujumbe wa nyimbo zke na lugha anayotumia ingewaudhi wateja wake.
 Ofisi ya Mayor wa jiji la London, Boris Johnson imeeleza kuwa haikuhusishwa kabisa katika uamuzi wa kumzuia Eminem kuperform katika Hyde Park. Walifafanua kuwa hawakufahamu Eminem ni nani na hawakuwa na uwezo wa kuingilia maamuzi ya Wamiliki wa eneo hilo.
 Eminen alitarajiwa kuperform katika Hyde Park June 3 kabla hajazuiwa.
Lupita Nyong

 Lupita Nyong’o anazidi kuwaongezea wakenya nafasi ya kutajwa kwenye tuzo za Oscar hata kama sio katika kupata tuzo tu baada ya kuongezwa kuwa kati ya watu 271 wanaounda Academy ya tuzo za Oscar mwaka huu.
Muigizaji huyo wa 12 Years A Slave, ambaye ni mshindi wa tuzo ya Oscar ya mwaka jana kama muigizaji bora wa kike msaidizi, anaungana na wasanii wengine waliong’ara mwaka jana katika tasnia ya filamu pamoja na mwanamuziki Pharrell Williams kama members wapya wa Academy hiyo.
 Wasanii wengine wenye umri mdogo watakaoungana na Lupita ni pamoja na Josh Hutcherson, Michael Fassbender, Ben Foster, Sally Hawakins, Julia Lousi-Dreyfus, Chris Rock na Jason Statham.
 Rais wa Oscar Academy, Cheryl Boone Isaac ameeleza kuwa Academy ya mwaka huu itawahusisha watu ambao wana vipaji zaidi na wabunifu katika masuala ya fulamu.
 “Mchango wao katika filamu umewaburudisha hadhira kote duniani, na tunajivunia kuwakaribisha kwenye Academy.” Aliseam Cheryl Boone.

Uingereza warejea nyumbani kama yatima, mashabiki wagoma kujitokeza uwanja wa ndege
Mashabiki wa soka nchini Uingereza wamegoma kuilaki timu yao wakati ilipowasili jijini Manchester, ikitokea nchini Brazil ambapo ilikuwa ikishiriki fainali za kombe la dunia za mwaka 2014.

 Wakati kikosi cha Uingereza kikiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Manchester, palionekana kimya, kama mashabiki wa soka walikuwa hawajui kinachoendelea mara baada ya timu yao kushindwa kufurukuta kwenye michezo ya kundi la nne ambalo liliijumuisha timu ya Italia, Uruguay pamoja na Costa Rica.
 Hata hivyo wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza walionekana kutokuwa na furaha licha ya kurejea nyumbani salama, ambapo kila mmoja alionekana anashuka kutoka kwenye ndege akiwa na begi pamoja na mfuko mweupe ambao unahisiwa huenda ikiwa ni zawadi za familia zao.
 Kitendo cha mashabiki wa Uingereza kuilaki timu yao huko Manchester Airport, kimekuwa ni tofauti kubwa kilichoonekana katika nchi nyingine zilizoshindwa kuendelea katika fainali za kombe la dunia, ambapo imeonekana mashabiki wa nchi hizo kama Hispania wakijitokeza uwanja wa ndege na kuonyesha upendo dhidi ya wachezaji wao.

Mwanariadha mwenye ujauzito wa miezi nane akimbia mita 800 kwa dakika 2

 Alysia Montano, mwanariadha wa kike na mshiriki wa Olympic aliyewahi kushinda mara tano mashindano ya riadha ya Marekani ambaye hivi sasa anaujauzito wa miezi 8, bado anashiriki riadha na hali aliyonayo.

 Alysia amewashangaza wengi baada ya kukimbia umbali wa mita 800 kwa dakika 2 na sekunde 32 huko California, jana (June 26), ikiwa amechelewa sekunde 35 tu ya uwezo wake wakati akiwa hana ujauzito.
 Mwaka 2010, mwanamke huyo akiwa katika hali nzuri alikimbia mita 800 kwa dakika 1 na sekunde 57.
 Mwanariadha huyo ameeleza kuwa yeye anajisikia vizuri kukimbia umbali huo akiwa na ujauzito na kwamba amekuwa akifanya hivyo katika kipindi chote cha ujauzito na ameruhusiwa na daktari.
 “I've been running throughout my pregnancy and I felt really, really good during the whole process.” Alisema baada ya kumaliza kukimbia.
Diego Maradona awachokonoa FIFA, avaa nguo inayounga mkono utovu wa nidhamu

 Gwiji wa soka nchini Argentina Diego Armando Maradona ameushangaza ulimwengu wa soka baada ya kuonekana amevaa flana yenye maandishi yanayomuunga mkono mshambuliaji kutoka nchini Uruguy Luis Suarez ambaye ameanza kutumikia adhabu ya kufungiwa.
Maradona alionekana amevalia flana hiyo alipokuwa kwenye kipindi cha televishani usiku wa kuamkia hii leo huko nchini Brazil, ambapo maandishi hayo yalisomeka “Luisito, estamos con vos” yakimaanisha tupo pamoja na wewe.
 Hatua hiyo Maradona kuvaa flana yenye maandishi ya kumuunga mkono Luis Suares inadhihirisha ni vipi mchezaji huyo wa zamani wa Argentina hakubaliani na maamuzi ya FIFA.
 
 Mbali na kuhisiwa hivyo pia mashabiki wa soka duniani kote wameanza kubaini huenda watu wa Amerika ya kusini wakawa kitu kimoja katika harakati za kupingana na maamuzi ya FIFA ambayo yamenza kutafsiriwa kama kutaka kuwabeba baadhi ya wachezaji kwenye fainali za kombe la dunia zinazoendelea nchini Brazil.
 
 Hata hivyo hii si mara ya kwanza kwa Luis Suarez kuungwa mkono baada ya kuonyesha vitendo vya utovu wa nidhamu anapokuwa uwnajani, kwani kama itakumbukwa vyema mwaka 2011, wakati alipokabiliwa na sakata la kumtolewa maneno ya kibaguzi beki wa pembeni wa Man Utd Patrice Evra, wachezaji wenzake wa klabu ya Liverpool walivaa flana zilizokuwa na maandishi yalionyesha kuwa wapo pamoja na mshambuliaji huyo.
 Wachezaji wa Liverpool walivaa flana hizo kwa pamoja wakati wakijiandaa na mchezo wa ligi ya nchini humo dhidi ya Wigan katika msimu wa mwaka 2010-11.

Uvutaji Shisha wapigwa marufuku Kenya, hubeba dawa za kulevya
 Kenya imepiga marufuku uvutaji wa Shisha (Sheesha) kwa ladha 19 baada ya kugundua kuwa zinabeba madawa ya kulevya kama heroin, bangi na cocaine.

 Amri hiyo imetangazwa jana na kuongezewa uthibisho na chombo kinachoshughulikia kampeni ya kupambana na matumizi ya dawa za kulevya, NACADA (National Campaign Against Drug Abuse) ambacho kilieleza kuwa kimefanyia majaribia ladha 100 za Sheesha wakiwa na ofisi ya wizara ya afya na wamegundua kuwa aina hizo 19 hubeba madawa ya kulevya.
 Kati ya ladha zilizopigwa marufu ni Al Fakher strawberry flavor, Al Fakher orange flavor, Al Fakher two apples with mint flavour, Al Fakher vanilla flavour, Al Fakher two appeals flavor, Al Fakher guava flavor, Al Fakher orange with mint flavor, Al Fakher orange flavor na 

nyingine.



          SOURCE:DJARO ARUNGU

Friday, 27 June 2014

Yule mwanamke wa Sudan aliyehukumiwa kifo kwa kukana dini yake,ameachiwa huru

.
mwanamke
Kwa mujibu wa BBC, Mwanamke wa Sudan aliyehukumiwa kifo kwa kosa la kuikana imani ya dini yake na kuolewa na mwanaume anayempenda wa kikristu amechiwa kutoka gerezani.

Shirika la habari la Suna limeripoti kuwa, hukumu ya kifo iliyotolewa kwa mwanamke huyo Meriam Ibrahim ilibadilishwa na mahakama ya rufaa.

Mwanamke huyo aliolewa na mwanaume wa kikristu na alihukumiwa kifo kwa kutumia sheria za kiislamu baada ya kukataa kurejea kwenye dini yake.

Mume wake amesema kuwa anatarajia kumuona mke wake akirejea nyumbani.

Aliwekwa gerezani tangu February mwaka huu akiwa na mtoto wake mdogo wa kiume aliyejifungua akiwa ndani.
condomUnaambiwa kuna sheria mpya inatarajiwa kuwasilishwa katika bunge la Senet ambayo sheria hiyo itawaruhusu watoto kuanzia miaka 10 kupewa mipira ya kondomu na dawa za kupanga uzazi.

Sheria ya afya ya uzazi 2014 ambayo tayari ipo mbele ya Senet,inasema kuwa elimu kwa watoto kuhusu afya ya uzazi na ngono wapewe watoto pengine hata bila ya wazazi kutoa idhini.

Sheria hiyo imewasilishwa na Seneta mteule Bi.Judith Sijeny anayesema kwenye pendekezo la mswada huo kua watoto wanaovunja ungo wapawe nafasi yakutosha kupata habari kamilifu kuhusu elimu ya ngono na huduma za kisiri.

Ikiwa ni pamoja na habari za kutosha na orodha ya dawa za kupanga uzazi na habari kuhusu ujauzito na uzazi wa mpango,muwada huo unaashiria kwamba wanaovunja ungo ni walio kati ya umri wa miaka 10 na 17 ambao ni wanafunzi kati ya darasa la tano na kidato cha tatu.

miss iringa 2
IMG_0531Tano bora Redds Miss Iringa


 
Washindi wa Redds Miss Iringa katikati ni Martha John Redds Miss Iringa 2014, Kulia ni Foe Mkuchu mshindi wa 3 na Jilian Joel kushoto redds miss Iringa no. 2

IMG_3799Foe Mkuchu mshiriki wa Redds Miss Iringa akipita na vazi la ubunifu.

SAM_5663
SAM_5762
Meneja wa TBL mikoa ya Iringa, Ruvuma na Njombe Raymond Degera akimkabidhi redds miss iringa no 3 Foe Mkuchu zawadi yake.

SOURCE:DJARO ARUNGU