advert

http://

Monday, 30 June 2014

Chui apanda boti na kumshambulia mvuvi akiwa na watoto wake.


Chui apanda boti na kumshambulia mvuvi akiwa na watoto wake
Imeripotiwa kuwa chui mwenye hasira na njaa aliingia majini na kupanda boti ya mvuvi aliyetajwa kwa jina la Shushil Manjhi huko Kolkata, India na kuondoka nae.

Taarifa zilizoripotiwa na vituo vya nchini India vinaeleza kuwa, mvuvi huyo alikuwa na watototo wake wawili (wa kike na wakiume) wakijaribu kutafuta kitoweo karibu na hifadhi ya taifa ya Sunderbans yenye wanyama wakali.
Mwanae wa kiume, Jyotish alieleza kwa njia ya simu kuwa chui huyo alirukia boti na kumkamata baba yake shingoni kwa upande wa nyuma na kuanza kumburuza akiondoka nae akielekea msituni.
“Alimrukia baba yangu kwa haraka mgogoni na kung’ata kwa nguvu kabla hajatokomea nae msituni.” Alieleza.
Mtoto huyo anaeleza kuwa baada ya chui huyo kumkamata baba yake, yeye na mdogo wake walijaribu kumpiga na fimbo na visu walivyokuwa navyo lakini hakuweza kumuachia.
Tukio hilo linatoa picha ya maisha duni ya wananchi masikini wa eneo hilo ambao licha ya kuwa na hatari kubwa ya kuuawa na wanyama wakali, hali ngumu ya maisha huwasukuma kuingia msituni kusaka kitoweo au chochote licha ya kwamba ni kinyume cha sheria kufanya uvuvi katika eneo la hifadhi ya wanyama.
Inaelezwa kuwa samaki wanaopatikana katika hifadhi hiyo hunuliwa kwa pesa nyingi katika miji ya jirani na vijiviji vya eneo hilo.

BOFYA HAPA UWACHEKI HAWA JAMAA KATIKA VIDEO, NI SHETTA FT DIAMOND, ILA NI FEKI SIO WENYEWE REAL https://www.youtube.com/watch?v=bRDoVEh9eh8


M 2 THE P AKIWA NA SWAHIBA WAKE NGWEAR KIPINDI HICHO
BOFYA HAPA KUINJOI SHOW YAKE  https://www.youtube.com/watch?v=WRtmRKzL5Zw&feature=em-subs_digest

Msichana aliyemuua mama yake kwa kumchoma visu mara 151 akwepa jela
 Taarifa kutoka Colorado, Marekani zinaeleza kuwa Msichana mwenye umri wa miaka 19, anaefahamika kwa jina la Isabella Yun-Mi Guzman ambaye alimchoma mama yake visu mara 151 ameachiwa huru.

 Mahakama imemuachia huru Isabella baada ya kubaini kuwa ni mgonjwa wa akili na kwamba wakati anatekeleza tukio hilo hakuwa katika hali ya kawaida kiakili hivyo kwa mujibu wa sheria hana hatia.
 Mahakama imeamuru msichana huyo kupelekwa katika hospitali ya wagonjwa wenye matatizo ya akili kwa ajili ya kupata matibabu badala ya kumpeleka jela.
 Kwa mujibu wa ripoti zilizofikishwa mahakamani hapo na polisi, Issabella alimchoma mama yake visu mara 151 (Mara 35 usoni, mara 51 shingoni, na mara 65 katika sehemu nyingine za mwili.
 Msichana huyo amepelekwa  Colorado Mental Health Institute.   



Millard Ayo (Mtangazaji machachari wa Clouds Fm) ameibuka kidedea kwa kunyakua tuzo mbili,
hivyo vikiwa ni vipengele vyote alivyoshindanishwa. Kilele cha Tuzo hizo kilikuwa ni Ijumaa hii
katika Serena Hotel, Dar es Salaam.

Kumbuka tu kwamba hivi majuzi nilikujuza kwamba Wema alikuwa mstari wa mbele kuwashawishi mashabiki kumpigia kura Millard Ayo, unaweza kujikumbusha hapa http://www.babamzazi.com/2014/06/millard-ayo-na-wema-sepetu-mhhh.html Je hatuwezi kusema Wema amechangia kwa kiasi kikubwa kushinda kwa Millard? Maana Wema ana fans wengi sana, na kama fans wake wote wamemuunga mkono kwa kutekeleza kile achowaomba nazani hilo halikuwa la kutowezekana. Picha kati ya waili hawa ikiendelea, basi ww.babamzazi.com itaendelea kuwajuza.

Tuzo alizonyakua Millard ni ya MTANGAZAJI WA REDIO
ANAYEPENDWA na KIPINDI CHA REDIO KINACHOPENDWA (Ambacho ni AMPLIFAYA)

Hongreara sana  Millard Ayo kwa kunyakua Tuzo mbili

Washindi wengine katika vipengele mbalimbali ni kama ifuatavyo:

1 na 2 = MILLARD AYO

3.MTANGAZAJI WA RUNINGA ANAYEPENDWA = Salim Kikeke – BBC Swahili

4. KIPINDI CHA RUNINGA KINACHOPENDWA= Mkasi – EATV

5. MWANAMICHEZO ANAYEPENDWA=Juma Kaseja – Yanga

6. MUONGOZAJI WA VIDEO ZA MUZIKI ZINAZOPENDWA =Nisher

7. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIUME=My Number – Diamond

8. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIKE= Yahaya – Lady Jaydee

09. MUIGIZAJI WA KIUME KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA= King Majuto

10. MUIGIZAJI WA KIKE KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA =Elizabeth ‘Lulu’ Michael

11. FILAMU INAYOPENDWA =Ndoa Yangu



     SOURCE:D'JARO ARUNGU

No comments: