![]() Baada ya kuumia vibaya kichwani Manager wa Man Untd amesema Rooney hatocheza kwa wiki tatu sababu ya jeraha lake kichwani. Picha hii ilionekana kwenye ukurasa wa facebook wa Rooney akijaribu kutoa maelezo kuhusu tuhuma za kutotaka kuichezea timu ya taifa ya Uingereza. Rooney ameshonwa nyuzi 12 kwenye jeraha hilo na mpaka sasa imethibitishwa kuwa hatacheza kwenye mechi ya Uingereza na Moldova |
![]() Golden Boy Promotions imethibitisha kuwa, Itamlipa mpigana masumbi Floyd Mayweather kiasi cha dola milioni 45.5 ili kupigana na Canelo Alvarez tarehe 14 mwezi Septemba huko Las Vegas Marekani. Ikiwa dili hii itakamilika, malipo haya yataingia kwenye rekodi ya kiasi cha juu kabisa cha pesa kuliopwa bondia, ambapo itavunja rekodi iliyowahi kuwekwa na bondia Evander Holyfield, ambaye aliwekewa dau la dola milioni 33 kurudiana na Mike Tyson mwaka 1997. Bondia huyu alijichukulia kitita cha dola milioni 32 alipopigana na Robert Guerrero mwezi May mwaka huu na pia kiasi hicho hicho kwa mpambano wake na Miguel Cotto mwezi May pia. Dola milioni 45, ni zaidi ya shilingi bilioni 72 za kitanzania kwa rate ya Dola 1=Tshs 1613.5 sammisago. |
|
Posted: 05 Sep 2013 11:38 AM PDT
|
MUZIKI UNALIPA,TENA SANA TU.HUYU MSANII AMENUNUA GARI YENYE THAMANI YA SH MILIONI 209 ZA KITANZANIA.
![]() Muziki umeendelea kuwafaidisha wasanii na kuwasaidia kuishi katika ndoto zao ,na hii imethibitika kwa mara nyingine hasa baada ya msanii Davido kutoka Nigeria, kuamua kufunga macho na kununua gari mpya yenye thamani ya dola 130,000 ambayo ni zaidi ya shilingi milioni 209 za Tanzania. Gari hii mpya ya Davido ni Mercedes Benz G63AMG 2013 SUV, gari yenye hadhi na ya kifahari ambayo imevuta hisia za wengi mtandaoni kujadiliana juu ya uwezo wa kipesa wa msanii huyu na hatua ya kununua gari ya pesa nyingi namna hii. ![]() |
|
|
![]() |
|
Producer Shedy ameamua kukata mzizi wa fitina kwa kuuanika ukweli wa mambo....
Haya ndo maeno ya shedy Claver. “Beat hii nilitengeneza mimi kwa idea zangu mwenyewe. Alikuja Dayna akaupenda ule mdundo na mimi sikumnyima , akafanya demo lakini hakulipia kitu. "Sasa ikapita zaidi ya miezi sita kila nikimuliza vipi anasema bado atakuja kufanya.Kuna siku Diamond akaja studio ,akataka kusikia midumdo niliyonayo. "Bila hiyana, nilimchezea midundo mbalimbali kama mteja, ila jamaa akavutiwa sana na ule mdundo ambao Dayna aliufanyia demo. "Baada ya Diamond kuupenda mdundo huo, niliamua kumpigia simu Dayna na kumuelezea kwamba Diamond kapenda kufanya kazi katika ile beat,Dayna akakubali kabisa, "Sasa nashangaa yeye kusema diamond kamuibia wakati alikubali yeye mwenyewe." |
|
Hatimaye teknolojia imefanikisha kuwakutanisha wazazi wa mshindi wa Big Brother Afrika ‘The Chase’ Dillish Mathews baada ya mwanaume mmoja aitwaye Abdi Galgayo Guyo kuja hadharani na kudai kuwa ni baba mzazi wa mshindi huyo wa The Chase.
Siku moja tu iliyopita, Pulse iliandika habari kuhusu mwanaume wa Kenya aitwaye Abdi Galgayo Guyo aliyetembelea ofisi za Standard Media ya Kenya na kudai kuwa yeye ndiye baba mzazi wa mshindi wa BBA Th Chase. Abdi ambaye kwa mujibu wa Standard ana asili ya Somalia alielezea jinsi alivyokutana na mama yake Dillish aitwaye Selma kati ya (April 1989) na (March 1990) alipoenda Namibia akiwa mmoja wa maaskari wa Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kilichopelekwa nchini humo kusimamia amani. Habari hizo zilipokelewa kwa hisia tofauti na watu mbalimbali ambao wengi wao walionekana kuamini kuwa Abdi anazusha ili apate pesa, na Dillish alivunja ukimya kwa kutweet akimshangaa mwanaume huyo na kusema baba yake ana asili ya Somalia hivyo anashangazwa Abdi ametokea wapi, “Why is this weird dude claiming to be my dad! My dad is Somali! Where did he fall from haaaaaaai” alitweet Dillish Ubalozi wa Kenya nchini Namibia ukishirikiana na Standard Group ya Kenya jana waliandaa mkutano wa kiteknolojia kupitia ‘Google Hangout’ ili kuwakutanisha mama yake Dillish Selma Pashukeni pamoja na Abdi Guyo ambao walizungumza huku wakionana kwa mara ya kwanza baada ya kupotezana kwa miaka 23. Upande wa Namibia Selma alikuwa na mjomba wa Dillish na mkewe ambao ndio walimlea Dillish, na upande wa Kenya Abdi alikuwa mwenyewe katika ofisi za Standard Group. Wakiwa wanaongea kwa furaha huku wakikumbushiana mambo yaliyotokea enzi za kukutana kwao, mama yake Dillish ambaye anaonekana bado mdogo na mrembo alithibitisha kuwa mwanaume huyo ‘Abdi’ ndiye baba mzazi wa Dillish . Katika hali ya utani mjomba wa Dillish alimwambia Abdi akitembelea Namibia aende na pesa nyingi kufidia gharama za malezi ya Dillish. Mwisho wa mazungumzo Abdi alikaribishwa kwenda Namibia kujiunga na familia hiyo katika sherehe ya siku ya kuzaliwa ambayo itakuwa September 16. Dillish pia alithibitisha kupita twitter kwa kuandika Tweet hiyo iliyofuatiwa na tweet nyingine “Lord, you have given me all I’ve been begging for!” Tazama video ya Mama na Baba wa Dillish walivyokutanishwa kwa teknolojia. |
|
Rais Jakaya Kikwete leo amefanya mazungumzo na Rais Paul
Kagame wa Rwanda katika mkutano wa saba wa kimataifa wa nchi za maziwa makuu, unaofanyika Kampala, Uganda. Haijafahamika mara moja walichozungumza, hizi ni picha za mkutano wao. Marais hao wamekutana wakati ambapo uhusiano kati ya nchi hizo mbili unaendelea kuzorota. |
|
|
|
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ameitisha mkutano wa dharura wa marais wa nchi za Maziwa Makuu (ICGLR), kujadili hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Rais Jakaya Kikwete ni miongoni mwa waalikwa kwenye mkutano huo ambao pia unatarajiwa kuhudhuriwa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame. Wakati hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ikidhoofika, katika siku za karibuni, uhusiano wa Tanzania na Rwanda umekuwa wa shaka hasa baada ya Rais Kikwete kuishauri Serikali ya Rwanda kukaa na wapinzani ili kumaliza mzozo uliolikumba eneo la Maziwa Makuu. Rais Kikwete alitoa ushauri huo wakati akiwa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU), zilizofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia. Mkutano wa leo utafanyika kwenye Ukumbi wa Commonwealth Resort, Munyonyo katikati ya Jiji la Kampala. Kwa mujibu wa taarifa Rais Museveni ameitisha mkutano huo hasa kuzungumzia hatua ya Umoja wa Mataifa kupambana na Kundi la Waasi wa M23. Mbali na viongozi hao wa Tanzania na Rwanda, viongozi wengine wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano huo wanatoka Angola, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Sudan, na Zambia. |
|
Jitihada za kurejesha heshima kwa viwanja vya ndege nchini zilizoanzishwa na waziri wa uchukuzu Dk. Harisson Mwakyembe zinaonekana kuzaa matunda baada ya mwanadada kutoka nchini Nigeria Anthonia Ojo (25) kukamatwa na kete 99 za madawa ya kulevya dar es salaam jana.
Mwanamke huyo amekamatwa akielekea Roma Italia kupitia Paris Ufaransa kwa ndege ya Ethiopian Airways na aliingia hapa nchini Agosti 30 akitokea Nigeria.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Viwanja vya Ndege, Renatus Chalya, Ojo ataendelea kubaki chini ya ulinzi wa polisi kwa uchunguzi zaidi, wakati madawa hayo yamepelekwa kwenye ofisi ya mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini aina ya dawa hizo na thamani yake...
|
|
NGULI wa muziki wa Dansi Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ ameanza kuugua tena ambapo tangu Sikukuu ya Iddi hadi sasa yupo hoi kitandani. Akizungumza kwa huzuni na mwandishi wetu, Banza alisema alipomaliza shoo ya Sikukuu ya Iddi na Bendi ya Extra Bongo, alianza kuugua, akaenda Hospitali ya Yemen iliyopo Sinza, Dar ikagundulika ana malaria kali ambapo alipewa dozi ya siku saba. “Nilipewa dawa za malaria nikameza nikaambiwa baada ya siku saba nitajisikia vizuri lakini mpaka sasa sioni mabadiliko yoyote, bado mwili unaniuma sana, nashinda kitandani kila siku hivyo muziki basi kwa sasa,” alisema Banza na kuongeza: “Najua mashabiki wangu watanimisi lakini kwa sasa muziki nimepumzika, naomba mashabiki waniombee.” |
|
Ndugu wa mfanyabiashara Erasto Msuya (43)aliyeuawa kwa kupigwa risasi Agosti 7, mwaka huu, wameangua kilio na kuzimia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi, Kilimanjaro baada ya mahakama kuhairisha usikilizaji wa kesi hiyo.
Ndugu hao ni dada wa marehemu, Antuja Msuya na Bahati Msuya ambao katika tukio hilo, wote walipoteza fahamu.
Hali hiyo ilijitokeza baada ya mahakama kuahirisha kesi hiyo kufuatia maelezo ya upande wa mashtaka kuwa upelelezi haujakamilika na hivyo kuzua simazi na majonzi miongoni mwa watu waliohudhuria usikilizaji wa kesi.
Wakili wa Serikali Stella
Majaliwa, aliomba mahakama kuridhia hoja ya kuahirisha shauri hilo ili kutoa nafasi ya kukamilisha shughuli za upelelezi.Watuhumiwa walifikishwa mahakamani saa 5: 10, wakiwa ndani ya karandika la polisi. Washtakiwa hao ni Sharifu Mohammed (31), mkazi wa Kimandolu mkoani Arusha, na Musa Mangu (38), mkazi wa Shangarai kwa Mrefu jijini Arusha.
Wanatuhumiwa kumuua Msuya kwa kukusudia, kinyume cha kifungu cha sheria namba 196 cha kanuni ya sura 16 ya mwaka 2012. Hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Theotimus Swai, aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 18 mwaka huu.
Mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo Shaiba Mpunga, hakuwepo mahakamani kwa kile kilichoelezwa kuwa ana matatizo ya kiafya.
Mshtakiwa wa kwanza na wa tatu katika kesi hiyo wanatetewa na Wakili Hudson Ndusyepo.
PICHA ZA MATUKIO:
Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya bilionea wa madini Erasto
Msuya,Sharifu Mohamed na Musa Mangu wakiwa mahakamani.
Ndugu wa marehemu Erasto Msuya wakiwa mahakamani.
Ndugu wa marehemu Erasto Msuya wakiwa mahakamani.
Wakazi wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha walifurika mahakamani
kusikiliza kesi hiyo.
Mtuhumiwa Sharifu Mohamed akiteta jambo na wakili wake
Mhe. Hudson Ndusyepo mara baada ya kuhairishwa kwa kesi hiyo .
Dada wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Antuja
Msuya baada ya kupoteza fahamu mara baada ya kuahirishwa
kwa kesi.
Dada wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Antuja
Msuya baada ya kupoteza fahamu mara baada ya kuahirishwa kwa kesi.
Dada wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Antuja Msuya akiangua kilio na baadae kupoteza fahamu mara baada ya
kuahirishwa kwa kesi.
Mdogo wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Bahati Msuya akiwa anasaidiwa kupelekwa kwenye gari mara baada ya kuahirishwa kwa kesi
hiyo.
Mdogo wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Bahati Msuya akiwa anasaidiwa kupelekwa kwenye gari mara baada ya kuahirishwa kwa kesi
hiyo.
Mama mzazi wa marehemu Erasto akisindikizwa na wanandugu kwenda kwenye gari la familia.
Umati mkubwa wa wananchi ulifurika mahakamani hapo.
Soma hapa Chini ili kujua alikufaje huyu Bilionea.Inauma kwa kweli.
Pia soma hapa chini ili kuona alivyozikwa.Mazishi
yaligarimu zaidi ya milioni 100.
Jeneza lake lilikuwa linafunguliwa na rimoti.
|
NAPENDA KUTOA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWA HAWA WAFUATAO 1.MAMA VERONIKA NDUNGURU 2.BABA LAURENT NSUHA WADOGO ZANGU 1.MONICA ROSES NSUHA 2.PHILIPO NERY NSUHA 3.DORAH NSUHA 4.BERTHA NSUHA 5.DOMMY NSUHA BILA KUWASHAU WATU WANGU WA KARIBU YAFUATAO: 1.DENIS MPAGAZE 2.ALLEN MOSHI 3.NESTRO NJAWIKE 4.ATHANAS SING'AMBI
Friday, 6 September 2013
Wayne Rooney aumia Vibaya kichwani,Atapotea Uwanjani Kwa Wiki Tatu.Ameshonwa nyuzi 12
Sunday, 1 September 2013
HAYA KWELI MAJANGA''MWANAMKE KICHECHE AMEZA SIMU ILI BOYFRIEND WAKE ASISOME MESEJI''
Mwanamke wa miaka 19 kutoka Brazil anayeitwa Adriana Andrade alikuwa so desperate kumficha boyfriend wake asisome meseji iliyokuwa kwenye simu yake kiasi kwamba alipomwambia anaomba asome alikimbia.
Na alipofika mbali alifanya 'the unthinkable' akaimeza simu yake. Anatakiwa afanyiwe oparesheni ili simu hiyo itolewe. Chanzo:Spanish website Yipeta.com |
|
Inasemekana Mwanamke anapofikia umri wa miaka 25 huanza kujiuliza kuhusu kuolewa, lakini pia huanza kujiuliza kuhusu watoto. Kama hajaolewa, hana mchumba au anahisi kutokupata mtu anayeamini atamfaa, huanza kuhofia.
Anapofikia umri huo huanza kujiuliza pia kuhusu watoto. Hofu za maisha ya upweke ya baadaye humjaa na kumfanya kuanza kubabaika. Ni katika kubabaika huko, ndipo ambapo huweza kufanya mambo ambayo watu wengine hujiuliza ni kitu gani kimemsibu. Kwa kuhofia kuchelewa kuolewa au kutoolewa kabisa, anaweza kumkubali mtu ambaye vinginevyo asingekubali kuwa naye kama mume. Kwa hofu ya kuingia kwenye umri mkubwa akiwa hana mume, humbeba yeyote. Katika mazingira kama haya ndipo ambapo unakutana na wale ambao huolewa kwa madai ya kuondoa mkosi. Anachotaka ni kuolewa na mwanaume yeyote, ili mradi ionekane kwamba, maishani mwake naye alishawahi kuolewa. Girls mfunguke ni kweli haya. Udakuspecially. |
|
PapaaDolaa & Chedu2R na ngoma "Michano" ikiwa ni Nafasi waliojishindia katika Msimu wa kwanza katika shindano la PUNCH KWA MTAA, inayoendeshwa na DJ Mwaka ndani ya MJ FM Radio.
Hawa ni wawili kati ya washindi wanane jumla katika Round ya kwanza zawadi kuu ikiwa ni Kurekodi nyimbo katika Studio ya Noizmekah. Kwa mawasiliano zaidi check na Papaa Dolaa kupitia +255 753 470 004. Sikiliza wimbo hapa chini na download. |
|
|
Sun, Sep 1, 2013 at 5:20 AM
|
| ||||||||
|
| ||||||||
|
Msanii wa muziki wa bongo fleva Dayna Nyange mwenye maskani yake mjini Morogoro,ambaye pia ni msanii pekee wa kike anafanya vizuri kutoka Morogoro
alisema “Kukweli ni nimekwazika sana pia imeniuma,kwani sikutarajia msanii kama Diamond anaweza KUIBA nyimbo yangu na kwenda kuifanya yeye.Unajua nilikuwa nataka nimshirikishe kwenye nyimbo yangu ambayo nimefanya kwa Shedy Clever pale Tabata,hivyo nikarekodi demo,nikamtafuta na kumpatia ili aweze kusikia na kujua jinsi gani ataweza kuimba.
Baada ya muda ya nikamtafuta tena vipi ili tufanye kabisa ile nyimbo,ndipo akaanza kusema yupo bize nisubiri lakini.Lakini nashangaa sasa hivi nakisikia tena ile nyimbo ameeimba yeye tena alafu kibaya zaidi ametumia beat ile ile pia na mashairi yale yale.
Kiukweli alichokifanya sio kitu kizuri,kwani watu wote tunatafuta maisha sasa yeye ameangalia zaidi maslahi yake.Na usiku wa jana ndio ametoka kuitambulisha rasmi video ya wimbo huo.
Nilikuwa namheshimu sana ila kwa hili nashindwa kusema kitu maana imenigusa sana,nyimbo yangu ilikuwa inaitwa my number one. Mpaka sasa bado sijajua nifanye kitu gani nipo katika kufikiri cha kufanya.
| ||||||||
![]() | ||||||||
|
| ||||||||
|
Mwanaume mmoja nchini Kenya amejikuta akiambulia aibu ya mwaka baada ya uume wake kubadilishwa kuwa uke....
Mwanaume huyo anadaiwa kufanyiwa mchezo huo baada ya kufumaniwa akizini na mke wa mtu katika kitanda cha mumewe... Taarifa zinadai kwamba, mume huyo alipomfumania mkewe hakufanya vurugu yoyote na badala yake alitoweka na kwenda kwa mganga wa jadi ambaye aliuchukua uke wa mkewe na kuupachika katika uume wa mzinzi huyo. Bofya hapa kutazama picha. http://3.bp.blogspot.com/-g-7TNzdVzYQ/UiIR3mbSdUI/AAAAAAAAlJU/4Bgn3Ey9oII/s1600/AIBU1.png | ||||||||
|
Nay wa Mitego kuachia kibao chake kinachotamba kama Salamu zao....ndani ya nyimbo hiyo ametoa kama kufikisha ujumbe kwa watu kadhaa, lakini kuna mstari alikuwa akimuongelea Chief Judge wa EBBS & Benchmark Production Manager Madam Rita Poulsen. Kuna tetesi zilizuka kuwa Madam Rita alikuwa yupo mbioni kumfungulia mashitaka Nay wa Mitego,lakini nataka kukuambia na kukujuza kiundani kabisa kuwa amna lolote kati ya hayo ukweli ni Nay wa Mitego na Madam Rita wapo sawa kabisa na upendo umeshamiri kati yao.
| ||||||||
|
Msichana mmoja ambaye jina lake halikujulika amejikukuta katika wakati mgumu baada ya kuzomewa na kuchapwa viboko na kundi la
watu katika eneo la soko la nmc jiji arusha kwa madai ya kuvaa nguo fupi hali iliyowalazimu wasamaria wema kuingilia kati na kutumia nguvu kubwa ili kumwokoa na kumsitili kwa kumfunika na nguo zingine. Watu walio shuhudia tukio hilo wamedai kuchukizwa na aina ya nguo alizizovaa msichana huyo ambazo haziendani na maadili ya Kitanzania, ndiyo maana waliamua kumwadabisha ili kukomesha tabia hiyo. Kwa upande wao wanawake walio msitili msichana huyo kwa kumpa nguo za heshima na kumhifadhi katika Gareji ya jirani kabla ya kumkimbiza kwa gari aina ya Toyota Hiace wamesema hawaridhishwi na tabia hiyo inayowazalilisha wanawake na kuwataka wasichana kuavaa nguo za kujisitili ili kujenga heshima katika jamii. | ||||||||
|
MBIO za Mwenge wa Uhuru nusura ziahirishe shughuli za Bunge baada ya baadhi ya wabunge kutaka zifutwe na hoja hiyo ijadiliwe bungeni.
Hata hivyo, suala hilo liligeuka shubiri kwa Waziri wa Nchi, Ofisa ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika, kuzomewa na kurushiwa maneno ya kejeli alipojaribu kuzitetea mbio hizo. Chanzo cha mzozo huo kilitokana na maswali ya mbunge wa Musoma Mjini, Vicent Nyerere (CHADEMA), aliyeihoji serikali kama kuna uwezekano wa kutoukimbiza Mwenge katika maeneo ya watu wasiouhitaji. Nyerere alisema watu wa wilaya ya Musoma, mkoani Mara, hawautaki Mwenge huo kwa sababu unachochea uhasama, chuki na upotevu wa rasilimali. “Wakati wa mbio za Mwenge Musoma Mjini walilazimisha kuchukua magari ya halmashauri likiwemo la wagonjwa... huduma za afya zilisimama na hivyo kuleta chuki badala ya mwanga,” alidai. Nyerere pia alitaka kujua nini faida za mbio hizo, bajeti yake ni kiasi gani kwa mwaka na matumizi yake kama yanafanyiwa ukaguzi. Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Amos Makalla alisema serikali haina taarifa kama Musoma yalitokea mambo hayo wakati wa mbio hizo. Alisema kuwa Mwenge hautaachwa kukimbizwa katika maeneo fulani bali utaendelea nchi nzima na wanaotaka kuchangia waendelee kufanya hivyo bila kusita. Makalla alisema mbio hizo zilianzishwa kwa falsafa ya kuhamasisha ukombozi wa taifa la Tanganyika na bara zima la Afrika kama alivyosema Baba wa Taifa, Hayati Julius Nyerere. “Mbio za Mwenge wa Uhuru zimeendelea kuwahamasisha wananchi nchini kubuni, kuchangia na kutekeleza miradi ya maendeleo. “Mwaka 2012/2013 jumla ya miradi 273 yenye thamani ya sh bilioni 15.8 ilizinduliwa na mingine kuwekewa jiwe la msingi nchini kote,” alisema. Aliongeza kuwa kupitia mbio hizo, wananchi walichangisha sh bilioni 11.5 kwa hiari kwa ajili ya kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya zao. Makalla alisema serikali imetenga sh milioni 450 kwa mwaka wa fedha 2013/2014 kwa ajili ya shughuli za Mwenge wa Uhuru. Majibu hayo yaliwanyanyua wabunge wote wa upinzani lakini Naibu Spika Job Ndugai alimpa nafasi mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari (CHADEMA) aliyehoji Mwenge huo unamulika wapi. Alidai kuwa licha ya kuendelea kukimbizwa kila mwaka rushwa, dawa za kulevya, ongezeko la maambukizo ya ukimwi, ubadhirifu vimeendela kuongezeka. Baada ya majibu ya Makalla kutotosheleza, Ndugai alimpa nafasi mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy (CCM), aliyesema mbio hizo hazina faida kwa wananchi na zinatumia fedha nyingi. Alisema kila zinapopita mbio hizo, shughuli za kiserikali, kijamii husimama kwa muda usiopungua siku tatu. “Jamani tuwe wakweli Mwenge huu hauna faida, kila unapopita watendaji wote wa serikali au halmashauri hukimbia ofisi zao, sasa wananchi wanahangaika,” alisema. Baada ya mbunge huyo kutoa kauli ile, Naibu Spika alisema “Nimekupa nafasi ya kuuliza swali nikidhani utampatia ahueni kumbe ndiyo umeharibu kabisa.” Akijibu maswali hayo, Makalla alikiri kusimama kwa shughuli hizo unapokuwepo Mwenge lakini faida zake ni kubwa kuliko hasara. Ufafanuzi wa Makalla ulifuatiwa na majibu ya nyongeza kutoka kwa Mkuchika akisema Mwenge huo uliwashwa na kuwekwa Mlima Kilimanjaro ili uwasaidie wananchi wa Tanganyika kupata nuru palipokuwa na giza, kuheshimiwa na kukombolewa. Alisema anamshangaa Nyerere (Vicent) kuukataa Mwenge wakati babu yake ndiye aliyeuanzisha kwa lengo la kuwakomboa Watanzania; kwamba baadhi ya wabunge hawana uelewa juu ya umuhimu wa mbizo hizo ndiyo maana wanataka ufutwe. Ufafanuzi huo uliwafanya wabunge waanze kumzomea huku wengine wakisikika kuwa ‘ukimwi’ kila unapokesha. Mkuchika alijibu mapigo akisema: “Watu wanazomea wakati mimi natoa elimu; najua hiyo ndio tabia yao kuzomea, hivyo hawanipi shida.” Mzozo huo ulizidi kuwa mkubwa kwani baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu walijitokeza wabunge watatu kuomba muongozo huku mbunge mmoja akitoa hoja ya kuahirishwa kwa shughuli za Bunge. Moses Machali mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR), alisimama na kutoa hoja kwa Naibu Spika kwa kuomba kuahirishwa kwa shughuli za Bunge ili kuruhusu kujadiliwa kwa jambo hilo la Mbio za Mwenge. Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF), alisema suala la Mwenge muktadha wake mzima sio mbaya lakini kumekuwa na malalamiko na manung’uniko muda mrefu. Alitaka ifanywe tathmini ya kina kujua faida na hasara zake ili kwenye upungufu kufanyiwe maboresho. Mbunge wa Simanjiro Ole Sendeka aliomba muongozo akidai Mwenge huo ambao ni alama na tunu ya taifa kuleta tumaini pale ambapo hapana matumaini kwa wale wanaojua historia. Alisema kwa kuwa kuna uelewa mdogo kwa Watanzania juu ya jambo hilo huku wengine wakijipenyeza na kuingia ni bora ofisi ya Bunge ikatoa elimu. Naibu Spika alitoa nafasi kwa Mkuchika kutoa maelezo kwa yale ambayo yamemgusa na kuongeza kuwa kuhusiana na miongozo mingine ataitolea taarifa baadaye. Mkuchika alisema hakuwa na nia mbaya na badala yake alikuwa ananukuu kauli ya Mwalimu Nyerere aliyoisema kabla Tanganyika na Zanzibar hazijaungana. Tanzania daima. | ||||||||
|
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amenaswa na msanii mwenzake, Esterlina Sanga ‘Linah’ wakiwa kwenye mapozi ya kimahaba ambayo yametafsiriwa vibaya.
Katika tukio hilo lililojiri juzikati kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ndani ya Tamasha la Serengeti Fiesta, Diamond alishuhudiwa akiwa amempakata Linah ndani ya basi huku mikono ya jamaa huyo ikishika maeneo nyeti. Mara baada ya kutimba uwanjani hapo wakitokea hotelini tayari kwa kufanya shoo, Diamond na Linah walibaki kwenye basi wakiwa wamepakatana na hata msichana huyo alipomaliza shoo yake kali mishale ya saa 3: 00 usiku, alirejea mikononi mwa Diamond ambaye alimpachika mapajani.
Kwa mujibu wa mashuhuda, kama kweli mchumba wa Diamond, Penniel Mungwilwa ‘Penny’ anakubali mambo kama hayo, basi atakuwa na roho ngumu au moyo wa chuma.
Siyo mara ya kwanza Diamond na Linah kuripotiwa wakiwa wamepozi kimahaba kwani mwaka jana walifanya hivyo wakiwa jijini Mbeya hivyo kutafsiriwa kuwa inaonekana ni katabia kao kabaya wanakaendekeza. |
Subscribe to:
Posts (Atom)









.jpg)









































