Baada ya kuumia vibaya kichwani Manager wa Man Untd amesema Rooney hatocheza kwa wiki tatu sababu ya jeraha lake kichwani. Picha hii ilionekana kwenye ukurasa wa facebook wa Rooney akijaribu kutoa maelezo kuhusu tuhuma za kutotaka kuichezea timu ya taifa ya Uingereza. Rooney ameshonwa nyuzi 12 kwenye jeraha hilo na mpaka sasa imethibitishwa kuwa hatacheza kwenye mechi ya Uingereza na Moldova |
Golden Boy Promotions imethibitisha kuwa, Itamlipa mpigana masumbi Floyd Mayweather kiasi cha dola milioni 45.5 ili kupigana na Canelo Alvarez tarehe 14 mwezi Septemba huko Las Vegas Marekani. Ikiwa dili hii itakamilika, malipo haya yataingia kwenye rekodi ya kiasi cha juu kabisa cha pesa kuliopwa bondia, ambapo itavunja rekodi iliyowahi kuwekwa na bondia Evander Holyfield, ambaye aliwekewa dau la dola milioni 33 kurudiana na Mike Tyson mwaka 1997. Bondia huyu alijichukulia kitita cha dola milioni 32 alipopigana na Robert Guerrero mwezi May mwaka huu na pia kiasi hicho hicho kwa mpambano wake na Miguel Cotto mwezi May pia. Dola milioni 45, ni zaidi ya shilingi bilioni 72 za kitanzania kwa rate ya Dola 1=Tshs 1613.5 sammisago. |
Posted: 05 Sep 2013 11:38 AM PDT
|
MUZIKI UNALIPA,TENA SANA TU.HUYU MSANII AMENUNUA GARI YENYE THAMANI YA SH MILIONI 209 ZA KITANZANIA.
Muziki umeendelea kuwafaidisha wasanii na kuwasaidia kuishi katika ndoto zao ,na hii imethibitika kwa mara nyingine hasa baada ya msanii Davido kutoka Nigeria, kuamua kufunga macho na kununua gari mpya yenye thamani ya dola 130,000 ambayo ni zaidi ya shilingi milioni 209 za Tanzania. Gari hii mpya ya Davido ni Mercedes Benz G63AMG 2013 SUV, gari yenye hadhi na ya kifahari ambayo imevuta hisia za wengi mtandaoni kujadiliana juu ya uwezo wa kipesa wa msanii huyu na hatua ya kununua gari ya pesa nyingi namna hii. |
|
|
Producer Shedy ameamua kukata mzizi wa fitina kwa kuuanika ukweli wa mambo....
Haya ndo maeno ya shedy Claver. “Beat hii nilitengeneza mimi kwa idea zangu mwenyewe. Alikuja Dayna akaupenda ule mdundo na mimi sikumnyima , akafanya demo lakini hakulipia kitu. "Sasa ikapita zaidi ya miezi sita kila nikimuliza vipi anasema bado atakuja kufanya.Kuna siku Diamond akaja studio ,akataka kusikia midumdo niliyonayo. "Bila hiyana, nilimchezea midundo mbalimbali kama mteja, ila jamaa akavutiwa sana na ule mdundo ambao Dayna aliufanyia demo. "Baada ya Diamond kuupenda mdundo huo, niliamua kumpigia simu Dayna na kumuelezea kwamba Diamond kapenda kufanya kazi katika ile beat,Dayna akakubali kabisa, "Sasa nashangaa yeye kusema diamond kamuibia wakati alikubali yeye mwenyewe." |
Hatimaye teknolojia imefanikisha kuwakutanisha wazazi wa mshindi wa Big Brother Afrika ‘The Chase’ Dillish Mathews baada ya mwanaume mmoja aitwaye Abdi Galgayo Guyo kuja hadharani na kudai kuwa ni baba mzazi wa mshindi huyo wa The Chase.
Siku moja tu iliyopita, Pulse iliandika habari kuhusu mwanaume wa Kenya aitwaye Abdi Galgayo Guyo aliyetembelea ofisi za Standard Media ya Kenya na kudai kuwa yeye ndiye baba mzazi wa mshindi wa BBA Th Chase. Abdi ambaye kwa mujibu wa Standard ana asili ya Somalia alielezea jinsi alivyokutana na mama yake Dillish aitwaye Selma kati ya (April 1989) na (March 1990) alipoenda Namibia akiwa mmoja wa maaskari wa Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kilichopelekwa nchini humo kusimamia amani. Habari hizo zilipokelewa kwa hisia tofauti na watu mbalimbali ambao wengi wao walionekana kuamini kuwa Abdi anazusha ili apate pesa, na Dillish alivunja ukimya kwa kutweet akimshangaa mwanaume huyo na kusema baba yake ana asili ya Somalia hivyo anashangazwa Abdi ametokea wapi, “Why is this weird dude claiming to be my dad! My dad is Somali! Where did he fall from haaaaaaai” alitweet Dillish Ubalozi wa Kenya nchini Namibia ukishirikiana na Standard Group ya Kenya jana waliandaa mkutano wa kiteknolojia kupitia ‘Google Hangout’ ili kuwakutanisha mama yake Dillish Selma Pashukeni pamoja na Abdi Guyo ambao walizungumza huku wakionana kwa mara ya kwanza baada ya kupotezana kwa miaka 23. Upande wa Namibia Selma alikuwa na mjomba wa Dillish na mkewe ambao ndio walimlea Dillish, na upande wa Kenya Abdi alikuwa mwenyewe katika ofisi za Standard Group. Wakiwa wanaongea kwa furaha huku wakikumbushiana mambo yaliyotokea enzi za kukutana kwao, mama yake Dillish ambaye anaonekana bado mdogo na mrembo alithibitisha kuwa mwanaume huyo ‘Abdi’ ndiye baba mzazi wa Dillish . Katika hali ya utani mjomba wa Dillish alimwambia Abdi akitembelea Namibia aende na pesa nyingi kufidia gharama za malezi ya Dillish. Mwisho wa mazungumzo Abdi alikaribishwa kwenda Namibia kujiunga na familia hiyo katika sherehe ya siku ya kuzaliwa ambayo itakuwa September 16. Dillish pia alithibitisha kupita twitter kwa kuandika Tweet hiyo iliyofuatiwa na tweet nyingine “Lord, you have given me all I’ve been begging for!” Tazama video ya Mama na Baba wa Dillish walivyokutanishwa kwa teknolojia. |
Rais Jakaya Kikwete leo amefanya mazungumzo na Rais Paul
Kagame wa Rwanda katika mkutano wa saba wa kimataifa wa nchi za maziwa makuu, unaofanyika Kampala, Uganda. Haijafahamika mara moja walichozungumza, hizi ni picha za mkutano wao. Marais hao wamekutana wakati ambapo uhusiano kati ya nchi hizo mbili unaendelea kuzorota. |
|
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ameitisha mkutano wa dharura wa marais wa nchi za Maziwa Makuu (ICGLR), kujadili hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Rais Jakaya Kikwete ni miongoni mwa waalikwa kwenye mkutano huo ambao pia unatarajiwa kuhudhuriwa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame. Wakati hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ikidhoofika, katika siku za karibuni, uhusiano wa Tanzania na Rwanda umekuwa wa shaka hasa baada ya Rais Kikwete kuishauri Serikali ya Rwanda kukaa na wapinzani ili kumaliza mzozo uliolikumba eneo la Maziwa Makuu. Rais Kikwete alitoa ushauri huo wakati akiwa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU), zilizofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia. Mkutano wa leo utafanyika kwenye Ukumbi wa Commonwealth Resort, Munyonyo katikati ya Jiji la Kampala. Kwa mujibu wa taarifa Rais Museveni ameitisha mkutano huo hasa kuzungumzia hatua ya Umoja wa Mataifa kupambana na Kundi la Waasi wa M23. Mbali na viongozi hao wa Tanzania na Rwanda, viongozi wengine wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano huo wanatoka Angola, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Sudan, na Zambia. |
Jitihada za kurejesha heshima kwa viwanja vya ndege nchini zilizoanzishwa na waziri wa uchukuzu Dk. Harisson Mwakyembe zinaonekana kuzaa matunda baada ya mwanadada kutoka nchini Nigeria Anthonia Ojo (25) kukamatwa na kete 99 za madawa ya kulevya dar es salaam jana.
Mwanamke huyo amekamatwa akielekea Roma Italia kupitia Paris Ufaransa kwa ndege ya Ethiopian Airways na aliingia hapa nchini Agosti 30 akitokea Nigeria.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Viwanja vya Ndege, Renatus Chalya, Ojo ataendelea kubaki chini ya ulinzi wa polisi kwa uchunguzi zaidi, wakati madawa hayo yamepelekwa kwenye ofisi ya mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini aina ya dawa hizo na thamani yake...
|
NGULI wa muziki wa Dansi Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ ameanza kuugua tena ambapo tangu Sikukuu ya Iddi hadi sasa yupo hoi kitandani. Akizungumza kwa huzuni na mwandishi wetu, Banza alisema alipomaliza shoo ya Sikukuu ya Iddi na Bendi ya Extra Bongo, alianza kuugua, akaenda Hospitali ya Yemen iliyopo Sinza, Dar ikagundulika ana malaria kali ambapo alipewa dozi ya siku saba. “Nilipewa dawa za malaria nikameza nikaambiwa baada ya siku saba nitajisikia vizuri lakini mpaka sasa sioni mabadiliko yoyote, bado mwili unaniuma sana, nashinda kitandani kila siku hivyo muziki basi kwa sasa,” alisema Banza na kuongeza: “Najua mashabiki wangu watanimisi lakini kwa sasa muziki nimepumzika, naomba mashabiki waniombee.” |
Ndugu wa mfanyabiashara Erasto Msuya (43)aliyeuawa kwa kupigwa risasi Agosti 7, mwaka huu, wameangua kilio na kuzimia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi, Kilimanjaro baada ya mahakama kuhairisha usikilizaji wa kesi hiyo.
Ndugu hao ni dada wa marehemu, Antuja Msuya na Bahati Msuya ambao katika tukio hilo, wote walipoteza fahamu.
Hali hiyo ilijitokeza baada ya mahakama kuahirisha kesi hiyo kufuatia maelezo ya upande wa mashtaka kuwa upelelezi haujakamilika na hivyo kuzua simazi na majonzi miongoni mwa watu waliohudhuria usikilizaji wa kesi.
Wakili wa Serikali Stella
Majaliwa, aliomba mahakama kuridhia hoja ya kuahirisha shauri hilo ili kutoa nafasi ya kukamilisha shughuli za upelelezi.Watuhumiwa walifikishwa mahakamani saa 5: 10, wakiwa ndani ya karandika la polisi. Washtakiwa hao ni Sharifu Mohammed (31), mkazi wa Kimandolu mkoani Arusha, na Musa Mangu (38), mkazi wa Shangarai kwa Mrefu jijini Arusha.
Wanatuhumiwa kumuua Msuya kwa kukusudia, kinyume cha kifungu cha sheria namba 196 cha kanuni ya sura 16 ya mwaka 2012. Hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Theotimus Swai, aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 18 mwaka huu.
Mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo Shaiba Mpunga, hakuwepo mahakamani kwa kile kilichoelezwa kuwa ana matatizo ya kiafya.
Mshtakiwa wa kwanza na wa tatu katika kesi hiyo wanatetewa na Wakili Hudson Ndusyepo.
PICHA ZA MATUKIO:
Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya bilionea wa madini Erasto
Msuya,Sharifu Mohamed na Musa Mangu wakiwa mahakamani.
Ndugu wa marehemu Erasto Msuya wakiwa mahakamani.
Ndugu wa marehemu Erasto Msuya wakiwa mahakamani.
Wakazi wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha walifurika mahakamani
kusikiliza kesi hiyo.
Mtuhumiwa Sharifu Mohamed akiteta jambo na wakili wake
Mhe. Hudson Ndusyepo mara baada ya kuhairishwa kwa kesi hiyo .
Dada wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Antuja
Msuya baada ya kupoteza fahamu mara baada ya kuahirishwa
kwa kesi.
Dada wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Antuja
Msuya baada ya kupoteza fahamu mara baada ya kuahirishwa kwa kesi.
Dada wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Antuja Msuya akiangua kilio na baadae kupoteza fahamu mara baada ya
kuahirishwa kwa kesi.
Mdogo wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Bahati Msuya akiwa anasaidiwa kupelekwa kwenye gari mara baada ya kuahirishwa kwa kesi
hiyo.
Mdogo wa marehemu Msuya aliyefahamika kwa jina la Bahati Msuya akiwa anasaidiwa kupelekwa kwenye gari mara baada ya kuahirishwa kwa kesi
hiyo.
Mama mzazi wa marehemu Erasto akisindikizwa na wanandugu kwenda kwenye gari la familia.
Umati mkubwa wa wananchi ulifurika mahakamani hapo.
Soma hapa Chini ili kujua alikufaje huyu Bilionea.Inauma kwa kweli.
Pia soma hapa chini ili kuona alivyozikwa.Mazishi
yaligarimu zaidi ya milioni 100.
Jeneza lake lilikuwa linafunguliwa na rimoti.
|
NAPENDA KUTOA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWA HAWA WAFUATAO 1.MAMA VERONIKA NDUNGURU 2.BABA LAURENT NSUHA WADOGO ZANGU 1.MONICA ROSES NSUHA 2.PHILIPO NERY NSUHA 3.DORAH NSUHA 4.BERTHA NSUHA 5.DOMMY NSUHA BILA KUWASHAU WATU WANGU WA KARIBU YAFUATAO: 1.DENIS MPAGAZE 2.ALLEN MOSHI 3.NESTRO NJAWIKE 4.ATHANAS SING'AMBI
Friday, 6 September 2013
Wayne Rooney aumia Vibaya kichwani,Atapotea Uwanjani Kwa Wiki Tatu.Ameshonwa nyuzi 12
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment