advert

http://

Tuesday, 26 November 2013

DR WA MAREHEMU MICHAEL JACKSON AELEZA SIRI NZITO KUHUSU MAREHEMU.



Kwenye mahojiano yake ya kwanza mara baada ya kuachiwa toka gerezani kwa kuhusishwa na kifo cha nguli wa muziki wa pop duniani Michael Jackson, 
Dokta Conrad Murray alielezea kwenye mahojiano aliyofanya na The Mail kwamba, Michael hakuwa baba wa hata mtoto wake mmoja, aliathiriwa na madawa kiasi cha kufikia hatua ya kuhitajika kuwa anavaa condom sababu mkojo ulikuwa unatoka wenyewe kwenye uume wake.

“Unataka kufahamu ni kwa kiasi gani mimi na Michael kwa vile tulikuwa karibu? Nilikuwa nikishukilia uume wake kila usiku. Nilikuwa namvalisha condom sababu mkojo wake ulikuwa ukitoka wenyewe. Michael alikuwa hajua namna ya kuvaa condom, hivyo ilinibidi niwe namvallisha. Kilikuwa ni kitu cha kipekee sana ila aliniamini mimi. Sikumuuwa Michael Jackson, aliathiriwa na madawa, Michael Jackson kwa bahati mbaya alimuuwa Michael Jackson, naamini aliamka na kuamua kufanya aliyozoea kufanya, akajidunga sindano haraka ambayo ilisababisha kumpeleka kwenye hali iliyomfika.’’ 

Alikuwa kwenye majanga mwishoni mwa maisha yake, akiwa na msongo wa kimawazo na kupaniki … Mwishoni, Michael alikuwa mtu aliyekata tamaa. Nilijaribu kumlinda ila mwisho wa siku niliangushwa naye.

Jackson alikuwa ameingia kwenye matatizo ya kuathirika kiakili na kimwili kutokana na ziara yake ya London.’’ Alisema Dokta Conrad Murray. 
Video Mpya:Snura-Nimevurugwa

Hii itakuwa ni kwa mara kwanza kwa mwimbaji wa Tanzania na pengine Afrika kuwa followed na Rais 
Barack Obama wa Marekani kwenye twitter ambae ana zaidi ya followers milioni 40 lakini yeye anafollow watu laki sita.
Vanessa Mdee ameingia kwenye list ya watu laki sita ambao Rais Barrack Obama ana wa-follow sasa hivi ambapo baada ya Rais huyu kufollow, kwa furaha Vanessa alishare kwenye instagram screenshot ya ukurasa wake wa twitter ukionyesha Barack Obama ameanza kum-follow.
Kama ilivyo twitter, hii inamaanisha ana Vanessa ana uwezo wa kumuandikia msg binafsi kwenye inbox Rais Obama.
Zifuatazo ni kauli za Ismail Aden Rage ambazo nimemnukuu akiongea na Waandishi kutokana na 
stori zilizochukua headlines kwa siku kadhaa kuhusu Kamati kumsimamisha kama Mwenyekiti wa Simba.
1. ‘Kwanza napenda kuipongeza kamati ya utendaji ya TFF kwa kuafiki mimi Ismail Aden Rage ndio Mwenyekiti halali wa Club hii ya Simba na nimepata barua yao jana ileile, katika katiba ya Simba kuna kitu wengi hawajui maana ya Kamati ya utendaji wanadhani ni wale watu saba… hapana!!! kamati ya Utendaji ni Mwenyekiti, Makamu wa Mwenyekiti… hamna kaimu hapo, kuna Wajumbe 7 waliochaguliwa katika mkutano halali… , Wajumbe saba wa kuchaguliwa mmoja wapo akiwa ni Mwanamke na wengine wawili wa kuteuliwa na Mwenyekiti, leo nitateua mwingine mmoja.. nimetoa mmoja’
2. ‘Kwa bahati mbaya Club ya Simba haina Makamu Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti alishajiuzulu ila ina Kaimu Mwenyekiti tu ila huku kwenye katiba hatajwi, kwenye katiba ya Simba Makamu Mwenyekiti ana kazi mbili, moja kwa kuelekezwa na Mwenyekiti na pili Makamu Mwenyekiti anafanya kazi wakati Mwenyekiti hayupo’ – Aden Rage
3. ‘Joseph Itangire ni Kaimu Mwenyekiti tu niliemteua lakini hajapata uhalali wa kikatiba kwa hiyo katiba hii inaendelea kusema, mwenye mamlaka ya kuitisha kamati ya Utendaji mara nne kwa mwaka ni Mwenyekiti, nimekua muungwana tumefanya mara 12 mwaka huu.. kama Mwenyekiti hayupo, katiba inasema anakaimu hana mamlaka ya kuitisha kikao chochote kwa mujibu wa katiba kwa hiyo kikao kile kilichofanyika hakina tofauti na kikao cha harusi’
4. ‘Maamuzi yangu kama Mwenyekiti wa Simba sasa, kwa kuwa mkutano ule ulikua ni batili… jana niliandika barua kwa TFF kwamba viongozi hawa wamevunja katiba za TFF, Simba, CAF na FIFA… ukitaka kulalamika ni lazima uwe na ushahidi wa aina mbili unaokubalika ambao ni document na video casette iliyo na sura za watu na maneno yao waliyosema, wana document ambayo kwenye barua ya Malinzi amekiri anayo na imesainiwa na Makamu Mwenyekiti wa Simba Joseph Itangire’
5. ‘Nimesikitika sana na maagizo ya TFF ya kunitaka niitishe mkutano na Wanachama wa Simba ndani ya siku 14, sijui wameitoa wapi kwenye katiba ya TFF na Simba, wamekwenda mbali na kuninyang’anya madaraka… wamenipa alafu wameninyang’anya alafu wamenipa na Ajenda ya mkutano, sasa wamenirudishia madaraka ya nini? mimi kama Mwenyekiti wa Simba… siitishi mkutano, nalindwa na katiba kwa hilo’
6. ‘Unaponipa amri unaninyang’anya madaraka yangu, katiba inasema kama naona itafaa nitaitisha… tuheshimu katiba, nilitegemea taarifa ya kwanza ya TFF mpya ingelaani mapinduzi ya kipuuzi yanayotokea’
7. Heshima yangu mimi ni Mbunge taifa linaelewa hivyo, nimekuta ofisi hii hakuna umeme miaka 18 pamoja na pazia za magunia, nimekuta uhuni mtupu.. wachezaji wameuzwa, Henry Joseph, Matole na wengine uliza wanachama wa Simba ilipata shilingi ngapi? leo imani inawatoka kusikia nimeuza Wachezaji wawili tu Congo DRC milioni 320 na nikaweka wazi hadharani sio kuwaambia Mke wangu na watoto wangu..
8. Leo nimetumiwa msg kutishia kuuwawa na tayari nimesharipoti Polisi, leo hii msg nimepata mtu kaniambia ‘Nisipotoka Simba ataniua’ alivyokua mpumbavu hajui hizi simu zinasajiliwa, nimecheki jina lake mpaka mtaa anaokaa pengine sasa yuko Lupango… why??? mpira ni burudani!! kuna mtu alikua Simba sasa yuko TFF anataka kuleta vurumai ndani ya TFF na Simba, kwa nini? kwa nini ununue watu? waandishi wa habari hebu tuache kuchochea, wewe Mwandishi ni nani ununuliwe? kuna Mwanamke Mwaandishi mmoja kalipwa milioni 2 ili anichafue, sijali.. ‘
9 Nimefanya Demokrasia sana na ndio inanitokea puani, nimeteua kamati… ziko kamati nyingi sana lakini sijaona Mwandishi hata mmoja anakwenda kuuliza kamati ya ufundi, Usajili ila kila mmoja ananishambulia mimi, leo sitaki maswali ya Waandishi wa habari, sasa mna hiari… kuandika au kuacha wala hamnipi tabu nyie, kuchafuliwa nimezoea’
10. Ukitaka kuwa kiongozi teka Ikulu kwanza, hapa ndio ikulu. 


Zaidi ya watoto 60 wanadaiwa kutekwa na kufichwa katika handaki lililopo kwenye msitu wa Mabwepande, Wilaya ya Kinondoni ,Dar es Salaam, ambalo ndani yake kuna jengo kubwa lenye vyumba.


Utekaji huo unadaiwa kufanywa na raia wa kigeni (Wazungu), wakishirikiana na Watanzania ambapo watoto hao hufungiwa katika vyumba hivyo, kuteswa, kulawitiwa na kubakwa.

Mtoto Emmanuel Robert (11) anayesoma darasa la tano Shule ya Msingi Maendeleo iliyopo Tabata, Segerea, Dar es Salaam na mdogo wake Godianus Robert (8), anayesoma darasa la tatu shuleni hapo, ndio waliofichua ukatili huo mwishoni mwa wiki.

Watoto hao walitekwa na Wazungu w awiliasubuhiyaSeptemba2mwaka huu, wak ati wakiendas huleni n akufan ikiwa kutoroka katikaj engohiloSeptemba 23 mwaka huu.

Wakiwa wamechoka na afya zao kuzorota katika Kituo kidogo cha Polisi, Kibaha Maili Moja, mkoani Pwani, watoto hao walisema ndani ya jengo hilo kuna watoto wengi wa kike na kiume.

Walisem a w atoto hao wanafanyishwa kazi na kuteswa kwa kutandikwa fimbo, kuchomwa moto na kupigwa shoti ya umeme hasa wanapowaulizia wazazi wao ambapo baadhi yao hubakwa na kulawitiwa.

"Jumba hili limejengwa ndani ya handaki, tulikuwa tukifanyishwa kazi ngumu na nzito, usiku tunajaza maji katika mapipa mengi na kubebeshwa ndoo kupanda na kushuka kilima.

"Tunapigwa fimbo, wasichana wanafungiwa kwenye vyumba, wanabakwa na kulawitiwa kwa zamu na Wazungu, tunachomwa moto (alionesha mguu wake uliochomwa) na kupigwa shoti ya umeme tunapowaulizia wazazi wetu," alisema Emmanuel kwa uchungu akitokwa na machozi.

Aliongeza kuwa, asubuhi ya Novemba 23 mwaka huu, katika jengo hilo kulitokea kutokuelewana kati ya Wazungu na Waswahili ambapo mswahili mmoja aliwatisha wazungu kwa kuwaambia polisi wanakuja hivyo walikimbia na kuacha mlango wazi.

"Hali hiyo iliniwezesha mimi, mdogo wangu na watoto wengine wachache waliokuwa na nguvu kufanikiwa kutoroka, nilimshika mkono mdogo wangu ambaye alionekana kuchoka nikamvuta.

"Watoto wengine wachache waliokuwa na nguvu nao wakatoka, wengi hawakuweza kutoka kutokana na kukosa nguvu, wanaumwa, wana vidonda vikubwa mwilini kutokana na kuchomwa moto na kupigwa shoti ya umeme, wasichana hawakuweza kabisa kutoka kwa kuwa wamefungiwa ndani ya vyumba," alisema Emmanuel

Aliongeza kuwa , alijikokota taratibu na mdogo wake mbali ya maumivu makali waliyonayo akatokea Mswahili mmoja ambaye alikuwa na gari lenye vioo vyeusi akawaambia wapande ili awatoroshe.

"Tulipanda gari hilo akatushusha darajani mpakani mwa Manispaa ya Kinondoni na Wilaya ya Kibaha, jirani na mzani eneo ambalo sisi hatukuwa tukilifahamu...dereva huyo alituambia gari limeishiwa mafuta hivyo alitutaka tumsubiri aende kuyanunua.

"Tulitembea kidogo tukiwa hatujui tunakokwenda... tulikaa kando ya barabara kutokana na uchovu pamoja na njaa kali kwani katika jengo hilo mbali na kazi nzito tulizokuwa tukizifanya na mateso mengi, mlo ulikuwa mmoja tu kwa siku.

"Tulikula saa 10 jioni, wali na maharage...tukiwa kando ya barabara, nilisikia sauti ya baba yangu wa kufikia, dereva wa magari makubwa yanayobeba kokoto ikiniita.

"Nilidhani naota kumbe ilikuwa kweli, alikuja akatukumbatia akalia kwa uchungu kwa namna tulivyokuwa tumechoka na afya kuzorota, akatupeleka polisi ambapo tulipatiwa maji tukaoga na kupewa chakula kizuri na kitamu, tukala na kupata nguvu za kuzungumza vizuri," alisema Emmanuel.

Akizungumza na Majira, Emmanuel alisema baada ya kutekwa yeye na mdogo wake, walifungwa na vitambaa vyeusi usoni hadi walipofikishwa ndani ya jumba hilo la mateso.

Aliiomba Serikali kufanya jitihada za hali na mali ili kuwaokoa watoto wengine waliopo katika jengo hilo.

Mama mzazi wa watoto hao, Martha Godianus (29), ambaye anafanya shughuli za mama lishe, njia panda y a Ba r a k u d a , Ta b a t a Manispaa ya Ilala, alisema amehangaika zaidi ya miezi mitatu kuwatafuta watoto hao bila mafanikio.

"Nimepoteza fedha nyingi kwa kuwatafuta na kutapeliwa mara kadhaa katika kuhangaika," alisema Godianus huku akitokwa na machozi ya furaha katika Kituo kidogo cha Polisi Maili Moja.

Alisema zaidi ya watoto saba walipotea katika mtaa wao, wawili wakapatikana baada ya wiki mbili, wengine wakiwemo wanaye wakawa hawajapatikana na kuomba Serikali ilichukulie kwa uzito suala hilo ili kubaini kundi linalowateka watoto na kuwatesa.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuanza kulifanyia kazi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Dar es Salaam.

Alisema makachero wa polisi wamewahoji watoto hao ili kupata maelekezo ya kufika katika andaki hilo na kuwataka watu wote wenye taarifa za eneo hilo watoe ushirikiano.

Credit-Gazeti la Majira.




 ''Nicki Minaj'' 

Zitto: Nitakuwa wa mwisho kutoka CHADEMA kwa hiari yangu (Video)

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe amesema ataendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa chama hicho licha ya wiki iliyopita kuvuliwa wadhifa huo na kamati kuu kwa madai amepanga njama ya kukipindua chama.

Akiongea na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana, Zitto alisema atakuwa mtu wa mwisho kutoka ndani ya chama hicho. “Nitakuwa wa mwisho kutoka kwenye chama hiki kwa hiari yangu,” alisema.
“Mimi sitoki. Wanaotaka nitoke, wanitoe wao.”

 Hii ndio Orodha Ya Washindi Wa Tuzo Za American Music Awards 2013 ambazo msanii 
Justin Timberlake ameongoza kwa kuchukua tuzo 3. Washindi wako hapa.



Favorite Male Pop Rock Artist - Justin Timberlake
Favorite Female Artist, Soul/R&B - Rihanna
Favorite Album, Country - Red, by Taylor Swift
Favorite Album, Rap/Hip-Hop - The Heist, by Macklemore & Ryan Lewis
Favorite Artist, Alternative Rock - Imagine Dragons
Favorite Artist, Latin - Marc Anthony
Favorite Album, Pop or Rock - Take Me Home, by One Direction
New Artist of the Year - Ariana Grande
Favorite Male Artist, Soul/R&B - Justin Timberlake
Favorite Female Artist, Country - Taylor Swift
Single of the Year - “Cruise,” by Florida Georgia Line, featuring Nelly
Favorite Album, Soul/R&B - The 20/20 Experience, by Justin Timberlake
Favorite Artist, Electronic Dance Music (EDM) - Avicii
Favorite Male Artist, Country - Luke Bryan
Favorite Band, Duo or Group, Pop or Rock - One Direction
Artist of the Year - Taylor Swift


Credit:Sammisago

EBSS: Emmanuel Msuya ndiye mwanaume pekee aliyeingia fainali, mshindi kukabidhiwa million 50 Jumamosi hiiShindano la kuimba lenye lengo la kusaka vipaji la Epique Bongo Star Search 2013 limeingia katika hatua ya mwisho ambapo wasanii watano wamechaguliwa kuingia fainali na mmoja kati yao atakabidhiwa shilingi za kitanzania million 50 Jumamosi hii (November 30).
Jana (November 24), Mandela Nicholas aliyaaga mashindano hayo akiwa amepata faida ya kufanya wimbo wake wa pekee na moja kati ya producers wanaofanya vizuri kwa sasa Tanzania.
Kuondolewa kwa Mandela kumefanya mshiriki namba 21, Emmanuel Msuya kuwa mwanaume pekee aliyeingia katika fainali huku akichuana na wasichana wanne.
Amina Chibaba, Maina Thadei, Melisa John na Elizabeth Mwakijambile ndio wasichana walioingia fainali. Je, nani atazifanya nyayo za Walter Chilambo? Majibu yatapatikana Jumamosi hii katika fainali itakazofanyika jijini Dar es Salaam.

PICHA za aliyekuwa mke wa marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ Wastara Juma akiwa na mwigizaji
Bondi bin Salim ‘Bond’ zimezua utata ambao unakazia ukweli wa taarifa ya kuwa wawili hao ni wapenzi.

Kikizungumza na Ijumaa Wikienda chanzo chetu kilicho makini, kilisema kinawashangaa sana Wastara na mwenzi wake huyo kuukana upenzi wao kila kukicha wakati picha zinajieleza.
“Wastara amekuwa akimkana Bond kuwa si mpenzi wake ila ni kaka yake sasa hebu tazama picha zao mpya, hata mtoto mdogo humdanganyi kitu,” kilisema chanzo hicho huku wawili hao wakiendelea kukanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi.

Credit:G.P.L

Friday, 22 November 2013

Ismail Aden Rage amerudi bongo, kuna sentensi yake juu ya kuvuliwa Uwenyekiti wa Simba



DSC_0023Mwenyekiti wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage amewasili Dar es salaam Tanzania leo akitokea Sudan ambapo alipokelewa na baadhi ya Wanachama wa Simba kwenye Uwanja wa ndege wa mwalimu JK.Nyerere.

Waandishi wengi walikua na maswali mengi kuhusu yeye kusimamishwa kuwa Mwenyekiti wa Simba lakini akayapangua kwa kusema kesho mchana ndio atazungumza na Waandishi kuhusu kila kitu ila sentensi moja iliyonyakwa na millardayo.com ni ‘taarifa za kusimamishwa Uwenyekiti sijazipata ndio kwanza nakusikia wewe, ninachojua mimi bado ni Mwenyekiti wa Club ya Simba’
‘Nimefurahi kwa mapokezi mazuri ambayo yameonyesha imani ya Wanachama kwangu mimi, mimi kama Mwenyekiti nitatoa tamko langu rasmi kesho mchana makao makuu ya Club ya Simba, sasa hivi siwezi manake rafiki yangu mpenzi Zitto kabwe ameondolewa kwenye Unaibu katibu mkuu na mimi sijafurahia kwa hiyo siko kwenye mood ya kuongea’ – Aden Rage
Alipoulizwa kama ana taarifa za kocha mpya Simba na pia kikao hicho atakifanyiaje Makao Makuu wakati ameondolewa kwenye Uwenyekiti, Rage kasema swala la kocha atalizungumza kesho ila hilo la kufanyia mkutano na Waandishi wa habari makao makuu ya Simba, waandishi wasiwe na wasiwasi kwani yeye ndio Mwenyekiti.
rageKuhusu kikao kilichofanyika na kumuondoa kwenye nafasi ya Uwenyekiti, Ismail Aden Rage amesema kikao kilichofanyika sio halali manake ukisoma katiba ya Simba, FIFA na CUF katika aya zote hakuna aya inayosema kamati ya utendaji ina mamlaka ya kumsimamisha Rais au Mwenyekiti.
DSC_0005            Baadhi ya Wanachama wa Simba wakicheza wakati wa mapokezi.


Credit:Millardayo.


3Ni Gabriel Munissi ambae alijiua kwa risasi Ilala Dar es salaam November 19 2013 baada ya kuua
watu wengine wawili kwa risasi asubuhi kati ya saa moja na saa mbili, amezikwa kwao Nkoshashi Wilaya ya Hai Kilimanjaro leo November 22 2013.
Gabriel ambae amefariki akiwa na umri wa miaka 31, anadaiwa kufanya mauaji ya watu wawili aliowasubiria nje ya geiti wakitoka nyumbani kwao (waliouwawa) huku chanzo kikitajwa kwamba ni kisa cha kimapenzi.
Kama alijua kitakachotokea, alichokiandika cha mwisho kwenye page yake ya facebook kiko chini kabisa mwa hii post.
8
7Baba na mama wa Marehemu.
6
5Mkuu wa Bandari ya Bukoba Ernest Nyambo, Athuman Tippo na Waziri Kabago wakiwa na brothers wengine waliojumuika kumzika Gabriel.
4Nyambo akizungumza na baba mzazi wa Marehemu.
2
1
Hii ni status ya mwisho ya Gabriel kwenye facebook
Hii ni status ya mwisho ya Gabriel kwenye facebook.
Credit:millardayo




Ni ajabu kuona wanadamu wanakuwa wabaguzi kwa kiasi hiki kwa sababu  ya maumbile.
Mambo mengi yamesemwa kuhusu tatizo la mtindio wa ubongo, hali ambayo imekuwa ikisababisha jamii mbalimbali kuwanyapaa na hata kuwabagua watoto wenye tatizo hilo.
Kitaalamu, mtindio wa ubongo unaelezwa kuwa ni hali inayompata mwanadamu kwa ubongo wake kushindwa kufanya kazi katika utaratibu wa kawaida. Kimsingi, ni uwezo wa ubongo kutokukua vizuri na kushindwa kufanya kazi yake katika mazingira yake ya kawaida.
Wataalamu wa afya kutoka sehemu mbalimbali duniani ikiwamo Tanzania wanabainisha kuwa mtu mwenye uwezo mdogo wa kufikiri, si kwamba ana matatizo ya akili ama mtindio wa ubongo.
Mtindio wa ubongo unaweza kusababishwa na hali mbalimbali ikiwamo ubongo kuathirika wakati wa kuzaliwa, na hata maisha ya utoto.
Kumbe, yapo mambo matatu yanayosababisha matatizo kwenye ubongo wa mtoto ambaye hajazaliwa mfano ugonjwa wa down syndrome hujitokeza baada ya matatizo katika vinasaba kutokea ambayo baadhi ya matumizi ya dawa husababisha mabadiliko katika vinasaba kama vile dawa za kunywa, ulevi kupindukia (fetal alcohol syndrome) na kuwa na mwili wenye afya dhaifu (fragile X).
Viasili, wakati mwingine huwa ni matokeo ya mtindio wa ubongo. Hiyo hutokana na asili ya kifamilia kuwa inapotokea mmoja wa wanafamilia wana asili na hali hiyo, basi wengine miongoni mwao watapata.
Mbali na hayo, pia matumizi ya dawa kali anazotumia mama wakati wa ujauzito, matumizi ya dawa za kulevya, pombe, hali ya hewa, au hata ajali husababisha kufikwa na hali hiyo.
Utafiti uliowahi kufanywa katika sehemu mbalimbali, unaonyesha kuwa pombe ina athari kubwa na mbaya hasa kwa kina mama wajawazito na matatizo wanayopata yanafahamika kitaalamu Fetal Alcoholic Syndrome (FAS).
Watoto wengi wanaozaliwa na tatizo hili wanakuwa na nyuso ambazo siyo za kawaida (facial deformities). Kwa mfano, watoto hawa wanaweza kuwa na pua bapa na macho yaliyoingia ndani au kupata matatizo ya kusikia na kutokuwa na uwezo wa kusoma.
Ukweli ni kwamba ni vigumu kwa wazazi kuwatambua watoto wao wenye tatizo hili na mara nyingi ni kwa watoto kabla ya kutimiza miaka kati ya mitatu na minne.
Hata hivyo, dalili zifuatazo zinaashiria kuwa mtoto ana tatizo hili. Kwanza, haonyeshi dalili yoyote ya kulia au anaweza kulia kwa kiasi kidogo, huchelewa kutembea na hata kuongea, haonyeshi kuvutiwa na mazingira yanayomzunguka, kwa maana kwamba hata kama kuna vitu vya kuchezea hawezi kujishughulisha navyo.
Endelea kusoma habari hii hapa.http://www.mwananchi.co.tz/Mtindio-wa-ubongo--Sababu-ya-watoto-wengi-kubaguliwa/-/1596774/2084498/-/12w9cvez/-/index.html

Majanga yazidi kumuandama DMX, rafiki yake amuibia gari alilompa akamuuzie Mambo yanazidi kuwa magumu kwa member wa zamani wa Ruff Ryders DMX ambaye yuko katika hali mbaya kifedha na hata kisaikolojia.

Hata muonekano wake unaonesha yuko katika kipindi kigumu (pichani).
Kwa mujibu wa TMZ rapper huyo ameripoti polisi akidai kuibiwa gari na rafiki yake aliyempa gari hilo mwezi uliopita ili akamsaidie kuuza angalau apate chochote.
DMX na girlfriend wake Desiree Lindstrom walimpa gari na copy ya kadi ya gari hilo rafiki yao waliyemfahamu kwa jina moja la ‘Lonny’ ili akawasaidie kuuza lakini rapper huyo amedai kuwa tangu walipompa gari hilo amepotea na simu yake haipatikani.
Kwa bahati mbaya DMX anafahamu jina moja tu la rafiki yake huyo, kiasi kwamba ameshindwa kuandika jina lake la pili katika maelezo yake katika kituo cha polisi.
Polisi wameanza msako wa gari hilo, lakini kitu kikubwa wanachopeleleza sasa ni jina la pili la ‘Lonny’ aliyepotea na gari hilo kwa kuwa Lonny ni jina linalotumiwa na watu wengi.
Dark Man X’s aka DMX sasa hivi amefilisika kiasi ambacho anapewa msaada wa kutafutiwa shows ili aweze kurudisha hali yake ya kifedha.
Hata hivyo producer mkali Swizz Beatz ametangaza kumsaidia DMX kwa hali na mali katika kuhakikisha anamrudisha kwenye game kama zamani.

Ni muda mrefu sasa kumekuwa na mtafaruku mzito ndani ya Chadema ambao umekuwa ukikitafuna
sana chama hicho, na pia kuna utabiri mzito sana ulitolewa na Waziri Wassira kwamba Chadema ipo katika siku zake za mwisho.

Ninasema hivi kufa kwa Chadema kama dalili zinavyoonyesha sasa hivi sio the best Interest ya chama chetu CCM.

Tunahitaji kuwasaidia sana waendelee kuwepo kwa sababu they have proven time and time kwamba ni paper tiger tu, wazuri kwenye makaratasi lakini hawana nguvu yoyote kisiasa.

Kupitishwa kwa musawada wa Katiba mpya juzi bungeni ni mfano mzito sana ulio hai wa jinsi wasivyo na nguvu kabisa za kisasa za opposed na makelele yao ya kila siku na lile gazeti lao lenye makao makuu yake kwenye Club ya Disco ya Mwenyekiti wao.


Ninawaomba sana CCM tunahitaji kuwa makini sana na matatizo ya chama hicho sasa hivi, tutumie nafasi hii kuwasaidia wasisambaratike maana Chadema ikisambaratika tutaanza kufukuzana na adui tusiyemjua,ni bora kushindana na huyu huyu adui tunayemjua, anayelia posho za wabunge ni kubwa na huku anazipokea, anayelia lia kwamba magari ya wabunge ni ya gharama sana na huku anayapokea hayo hayo. Anayelia lia safari za Rais huku wabunge wake wanasafiri kila siku nje kwa visingizo vya kamati za bunge.

AGAIN KWA WANA-CCM WOTE NI KWAMBA TUNAWAHITAJI SANA CHADEMA HII INAYOONGOZWA NA AKILI NDOGO, MAANA OTHERWISE TUTAKUTANA NA WAPINZANI WENYE AKILI KUBWA WATATUSUMBUA, TUWASAIDIE WASISMBATRATIKE!! ha! ha! ha!

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!!


source:http://www.udakuspecially.com/2013/11/wasi.html


Arfi ambaye pia ni mbunge wa Mpanda mjini (CHADEMA) amefikia uamuzi huo leo baada ya 
Kamati Kuu ya CHADEMA kuwavua uongozi Zitto Kabwe na Dr. Kitila Mkumbo.
Nafasi ya Zitto amepewa mchungaji Peter Msigwa

Hapa Chini ni Barua aliyoandika ya kujiuzulu.

Subject: KUJIUZULU MAKAMU MWENYEKITI (BARA)

Salaam,
Napenda kuwasilisha kwako taarifa ya kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara kuanzia Leo Ijumaa 22 Novemba 2013 kwa kuchoshwa na Unafiki unaoendelea ndani ya Chama. Napenda ifahamike pia kwangu maslahi ya Wapiga kura, Wakaazi na wananchi wa Mpanda Mjini na Wilaya ya Mpanda ni muhimu katika kuwatumikia, hivyo basi sipo tayari kuchaguliwa marafiki. 

Kwa kipindi kirefu zimekuwepo shutma dhidi yangu na kutiliwa mashaka mahusiano yangu na Mhe Pinda Waziri Mkuu pamoja na kulijadili katika vikao kadha Mpanda na Dar es Salaam bado yapo mashaka kwa nini alipita bila kupingwa hayo yalikua maamuzi ya Wanampanda kwenu imekua ni tatizo lakin hamsemi kwa nini Majimbo mengine 16 nchini yalipita bila kupingwa mlikua wapi na nani alaaumiwe huu ni Unafiki wa kupindukia.

Aidha mmechukizwa sana kwa nini nilihoji kauli ya Muasisi wa Chama Mhe Mtei kutuchagulia viongozi naomba ifahamike wazi kwamba huu ni mtazamo wangu na utabakia hivyo siku zote kwa chama cha demokrasia kutoruhusu uongozi wa kiimla kwa kukidhi matakwa ya Waasisi ambao huvigeuza vyama kuwa Mali binafsi

Kwa kusema ukweli na kusimamia ukweli daima itabakia kuwa lengo langu katika maisha yangu siku zote hata kama itanigharimu maisha yangu

Nawasilisha.


Said A Arfi (mb)
Nakala Vyombo vya Habari


source:jamii forum.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimemvua nyadhifa zote Naibu Katibu mkuu wake Zitto Kabwe ambae ni mbunge wa Kigoma Kaskazini.

Mwanasheria mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu kwenye makao makuu ya chama hicho, amesema Zitto na wenzake watatu wamebainika kukihujumu chama  kwa kuanzisha kitu kinaitwa Mkakati 2013 kinacholenga kukisambaratisha chama hicho ili kuwaondoa madarakani Mwenyekiti na Katibu mkuu wake.
Nyadhifa alizovuliwa ni Unaibu katibu mkuu pamoja na Naibu kiongozi wa upinzani bungeni ambapo yeye, Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba na mwingine mmoja Makao makuu wamepewa siku kumi na nne wajieleze kimaandishi kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi za kinidhamu ikiwemo kuvuliwa Uanachama.


Source:http://www.udakuspecially.com/2013/11/LISSU.html

http://theclicktz.blogspot.com/
Folorunsho Alakija wa huko Nigeria ni mwanamke mwenye utajiri mkubwa wa kiasi cha dola Billioni 3.3. 


kama ulizani Oprah ndie mwanamke mweusi tajiri pekeyake utakuwa umekosea dada huyu ni mmiliki na muanzilisha wa kampuni kubwa ya mafuta iitwayo Famfa Oil.

Alianza kufanya kazi kwenye Bank ya International Merchant Bank of Nigeria, na baadae kwenda England kusomea mambo ya Fashion. Aliporudi Nigeria alianzisha kampuni ya Supreme Stitches ambayo ilizalisha nguo, ulipofika mwaka 1993 ndipo alipo anzisha kampuni ya mafuta.



Credit:The ClickTZ

1Majambazi kumi wanaodaiwa kumuua Dr. Segondo Mvungi wamefikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu na kusomewa shitaka la kumuua Dr. Mvungi.

Kesi imesomwa na Hakimu Mkazi Sundi Fimbo ambapo Watuhumiwa hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na Mahakama kutokua na uwezo wa kusikiliza kesi ya mauaji hivyo wanarudishwa Segerea mpaka tarehe tano December kwa ajili ya kesi kutajwa.
2Hapa chini kuna majina yao, umri, wanakoishi pamoja na taarifa zao nyingine.
3
4
5

Credit:Millardayo.


Audio:B

Jana B’Hitz Music Group iliweka wazi uamuzi wa kuwaondoa kwenye label hiyo wasanii watatu ambao ni Vanessa Mdee, Mabeste na Gosby.

Japokuwa Vanessa na Mabeste walitangaza wiki hii kujitoa kwenye label hiyo, huku Gosby akiwa bado hajasema chochote, timu ya BHits imesema kuwa wasanii hao waliondolewa kwenye label hiyo miezi miwili iliyopita japokuwa hawaamua kutangaza.
Mabeste aliiambia Times fm kuwa ameamua kujiondoa katika label hiyo kwa kuwa muziki wake ulikuwa haumlipi na kwamba maisha aliyokuwa anaishi ndiyo yaliyopelekea yeye kudhaniwa kuwa anafanya show za nje, na kwamba amechoka kuwa mzigo kwao.
Tovuti ya Times fm ilimtafuta Amani Joachim ambaye ni mwana sheria na Chief Operations Officer wa B’Hits Music Group ili kufahamu kuhusu sababu alizozitoa Mabeste kwa upande wa B’Hits, na mikataba ikoje na kama watachukua hatua zozote za kisheria.
“Hiyo statement ambayo Mabeste ameamua kuisema kwangu mimi naona haiko sawa kabisa. Sisi ni ndugu na tulikuwa tunaishi hivyo, tatizo la mtu mmoja ni tatizo la mtu mwingine yaani tunakuwa pamoja kabisa. Na kuna vitu vingi ambavyo Mabeste anajua kwamba tunavifumbia macho. Hata hiyo mikataba, sisi na Mabeste kuna kipindi tume-deal hata bila mikataba na mambo yakawa safi tu kwa sababu kuna ile heshima na kuaminiana.” Amesema Amani.
Ameyaelezea pia madai ya Mabeste kuwa mabadiliko yake katika maisha ndiyo yaliyosababisha B’Hits kuhisi kwamba anapiga shows za nje.
“Mabeste inabidi aangalie statements zake, na muda ambao anaamua kutoa hizo kauli kwa sababu kati yetu sisi tuna siri nyingi sana (Mabeste na Upande wa B’Hits). Tusifike sehemu kwamba tukaanza kufaidisha kila mtu, hicho ndicho kitu ambacho ningependa kukiweka sawa. Hizo shows na vitu vingine ambavyo labda alikuwa anavifanya akiwa nje tunavifahamu vingi tu, lakini kutokana na ule u-brother na nini tunavichunia tu.” Ameeleza kiongozi huyo wa B Hits.
Hata hivyo Amani amekubaliana na kuwepo kwa ubovu wa soko la muziki ambapo amesema hata shows zikiwepo bado malipo yanayotolewa yako chini kiasi kwamba Kampuni haliwezi kuendeshwa kwa kutegemea kugawana kipato hicho na msanii.
Aliongelea pia madai ya Mabeste kuwa B’Hits haikuwa inamfanya atengeneze pesa kupitia muziki wake.
“Well, hopefully kule anakoenda atapata. Tunaelewa Mabeste ana majukumu, maisha yake tunajua kwamba yamebadilika kwa namna flani. Personally nafahamu, sijui akina Harmy na Pancho. That’s why I’m ready to stay quiet kwenye vitu kama hivyo, nilikuwa tayari kukaa kimya…sina haja ya kufunguka ni vitu vingapi ambavyo Mabeste ameshafanyiwa katika hali ya u-brother, I will not say them kwa sababu kipindi mimi navifanya nilivifanya katika good will na nilitaka iishie hivyo, Amani will never say them.”
Jana C.E.O B Hits Hermy B aliuambia mtandao wa Bongo5 kuwa Vanessa, Gosby na Mabeste hawana shukurani kwa kile ambacho B Hits imewafanyia na kutoa mfano kuwa alitoa shilingi million nane mfukoni kulipia video ya Closer ya Vanessa  na kiasi kingine kulipia kazi alizofanya nje ya studio za B Hits, fedha ambazo hazijawahi kurudi.
Nae Amani Joachim alitoa ushauri kwa Vanessa, Mabeste na Gosby kwa ujumla kuwa wawe na amani na waendelee kufanya mambo yao na kuacha kutengeneza vita kati yao na B’Hits kupitia media kwa kuwa hata yeye ameamua kuyafumbia macho mengi.  
Lakini vipi kuhusu hasara ambayo B’Hits itaipata kutokana na kuondoka kwa wasanii hao kwa kuwa walichukuliwa wakiwa hawana majina na wakati huu wanaondoka wakati wameanza kuwa productive.
Mwana sheria na Chief Operations Officer wa B’Hits anaeleza.
“They were real productive na naweza kukwambia kweli hawa watu wako very talented, na B’Hits haijawahi kum-house mtu ambaye ni mbovu, na ndo maana watu wanashangaa kwa nini mna nyumba kubwa ya media halafu mna watu watatu tu, sisi kuna kipindi tulikuwa na msanii mmoja tu Mabeste for like 4 years, ni kwa sababu tunaangalia talent.
“Na kusema kwamba sasa hivi tutakuwa hatujarudi nyuma utakuwa ni uongo, kuondoka kwao ndio tutarudi nyuma steps kadhaa, lakini pia kutokana kwamba plans tulizopanga kufanya wakati tukiwa nao zilikuwa hazijafika kuiva, we are ready to do that with someone else, Mungu hajagawa kipaji kwa watu wawili au watatu.”
Amesema anaamini baada ya Gosby, Vanessa, na Mabeste watakuja watu wengine ambao wana vipaji pia.
Kauli ambayo inaungana na ile ya Hermy B kuwa B’Hits itatangaza wasanii wapya wa label hiyo mwanzoni mwa mwaka ujao.
Tovuti ya Times fm ilitaka kufahamu kutoka kwa mwana sheria huyo kuhusu mkataba kati ya B’Hitz na wasanii hao na damages/athari za kuvunja mkataba huo zikoje na iwapo watawadai wasanii hao.
Amesema mikataba ilikuwa tight lakini kwa mazingira ya Tanzania na hali halisi ya kipato cha wasanii wa Tanzania hiyo mikataba inakuwa kama useless kwa kuwa kiasi kinachotakiwa kulipwa na msanii huyo ni kikubwa kuliko hali halisi ya maisha ya msanii husika.
“Ukimchukua bwana mti ukampeleka mahakamani, mahakama inaangalia damage ambayo imeingia katika kampuni, na mwisho wa siku inachukua maamuzi ambapo itakwambia bwana mti kama amepatikana na kosa amlipe bwana jose million 150 Kwa mfano, haimfungi. Problem ni kwamba bwana mti hana hata shilling 200 mfukoni mwake, we unadhani utamfanyaje bwana mti?” Alieleza kwa mfano.
“Kwa sababu mahakama ikishakupa judgement inakuacha ukatafute hiyo hela, haimfungi mtu. Kesi za madai sio kesi za jinai..sasa hapo imagine hapo ni wasanii wangapi leo unawafanyia kazi ya million 40 Million 50, ambayo ukiingia katika intellectual property court (mahakama ya maswala ya copy right), na copy right ni very expensive, tunaongelea six figures, eight figures. Sasa angalia ni wasanii wangapi hapa Tanzania wanaweza kukulipa eight figures.?” Amesema.
Kutokana na hali hiyo amesisitiza kuwa kuna haja ya kuwalipa wasanii pesa nyingi katika kazi zao huko wanakoenda kufanya ili wanapopata matatizo waweze kulipa, na kwamba bila hivyo mikataba ya label na wasanii Tanzania itakuwa useless.
Hii inamaanisha kuwa hakuna hatua zozote za kisheria ambazo B’hits itachukua kudai fidia kutoka kwa wasanii hao.
Hata hivyo uongozi wa B’Hits umesema utaachia nyimbo nyingine za wasanii hao zilizoko studio na kwamba zitachezwa redioni, lakini wasanii hao hawatakuwa na haki ya kuzitumia kwa kuwa ni mali halali ya kampuni hiyo.
Msikilize hapa Amani Joachim:

Credit:Times fm.



Vanessa Mdee, Gosby na Mabeste hawapo tena B’Hits Music Group. Kwa mujibu wa B’Hits Mabeste aliondolewa tangu miezi minne iliyopita japo 
hawakutangaza rasmi na Mabeste alipewa muda wa kujitetea kutokana na kwenda kinyume na mkataba wake ikiwa ni pamoja na kufanya show bila kutoa taarifa kwa uongozi.


Mabeste ambaye leo ametangaza kutokuwa chini ya label hiyo kupitia Facebook, amesema pamoja na label hiyo na kutengeneza hits nyingi, muziki wake haukuwa ukimpa kipato anachostahili na kusema kuwa tatizo lake na B’Hits ni katika kuufanya muziki wake uingize fedha zaidi pamoja na kuufanyia promotion.

Amesema nyimbo zote alizowahi kutoa amekuwa akiachiwa yeye zaidi kuzifanyia promotion na kuzifikisha mahali kitu ambacho anaamini ilikuwa ni kazi ya label yake.

“Sitaki kuonekana mzigo kwao. Haiwezekani kila siku wao wawe wanarekodi halafu wao hawaoni faida. Baada ya kutoona faida, wanarekodi nyimbo nyingine tena wananipa inaenda,” amesema Mabeste.

Aliongeza kuwa anaumia kuona producer wake Pancho ambaye alimkutanisha na B’Hits miaka mitano iliyopita hapati faida ya muziki wake. Hata hivyo amekanusha madai ya kufanya show bila kutoa taarifa kwa uongozi na kudai kuwa katika dunia ya sasa si rahisi kufanya show kwa siri bila kujulikana.

“Sasa mabadiliko ambayo yanatokea ndani ya haya maisha, wanahisi maybe mimi ninapata show siwaambii. Hivi hii Tanzania sasa hivi social networks ilivyotawala, kuna mahali unaweza kupiga show mtu asijue? Na nani atakuita show yake na aachie kuifanyia promotion kwa social network,” amehoji Mabeste.

Mabeste amesema kutokana na maisha kubadilika na kwakuwa sasa amekuwa baba, kiasi alichokuwa anakipata akiwa B’Hits ni kidogo kuweza kukidhi mahitaji yake ya kila siku na hivyo kumfanya aishi na stress wakati ana uwezo mkubwa.

Hata hivyo CEO wa B’Hits Music Group, Hermy B amesema anashangaa kumsikia Mabeste akilalamika hivyo wakati wao walimtoa mbali ambako alikuwa akiishi maisha ya chini na kuingia gharama nyingi za kumtunza ikiwa ni pamoja na kumlipia kodi ya nyumba, kumnunulia nguo pamoja na kumpa fedha ya kujikimu pale alipokuwa akihitaji.

Hermy B amesema kama akiamua kujumlisha gharama alizotumia kwa Mabeste zinafika si chini ya shilingi milioni 30 na haoni kama Mabeste ana uwezo wa kuzirejesha.

Ameongeza kuwa wote Mabeste, Gosby na Vanessa hawana shukrani kwa kile B’Hits imewafanyia.

Ametoa mfano kuwa video ya Closer ya Vanessa Mdee aligharamikia fedha zake kutoka mfukoni ambazo ni takriban shilingi milioni 8 ambazo hazijawahi kurudi hadi sasa na pia alilipia kwa hela yake hata kazi alizofanya kwenye studio nje ya B’Hits.

Naye Amani Joachim, ambaye ni mwanasheria na mmoja wa viongozi wa B’Hits, alisema Vanessa Mdee na Gosby waliondolewa B’Hits kutokana na kuingia mkataba wa kufanya show ya Fiesta Dar bila kuutaarifu uongozi. Amesema wawili hao walifikia hatua ya kwenda kufanya fujo B’Hits wakidai nyimbo zao kwaajili ya kutumbuiza kwenye show hiyo hali iliyokiuka masharti ya mkataba wao.

Ameongeza kuwa ukimya wao umewafanya watu wengi waamini kuwa wasanii hao walijiondoa wenyewe wakati uongozi ndio ulifanya uamuzi wa kwanza wa kuwaondoa.

Pamoja na hivyo, Hermy B amesema B’Hits itaziachia nyimbo zote za wasanii hao zichezwe redioni kwakuwa kuzifungia kutakuwa na hasara kwao kutokana na kutumia nguvu na akili nyingi kuziandaa.

Hata hivyo amesema, wasanii hao hawatakuwa na haki ya kuzitumia popote kwakuwa ni mali halali ya kampuni. Hermy B amesema, uongozi wa B’Hits hauna ugomvi na wasanii hao na mwanzoni mwa mwaka ujao wanatarajia kutangaza wasanii wapya watakaokuwa chini ya label hiyo.

Imebainika kwamba sababu ya shambulizi la risasi lililotokea Ilala Bungoni, Dar es Salaam Jumanne iliyopita na kusababisha vifo vya watu watatu, ni wivu wa mapenzi uliopindukia.


Akizungumza nyumbani kwao Ilala Bungoni jana, mmoja wa majeruhi ambaye ndiye aliyekuwa kiini cha shambulizi hilo, Christine Newa alisema si kweli kwamba sababu ya mchumba wake, Gabriel Munisi kuwashambulia na kuwajeruhi kwa risasi yeye na mama yake mzazi, Ellen Eliezer na kumuua mdogo wake wa kike, Alpha Newa ni kutokana na kusaliti uchumba wao.

Awali, ilidaiwa kwamba sababu ya shambulizi hilo ni Christine kumkataa Munisi, (ambaye pia alijiua baada ya kufanya mauaji hayo) na kuchumbiwa na rubani wa ndege, marehemu Francis Shumila ambaye pia alifariki katika tukio hilo... “Kwanza Shumila hakuwa mchumba wangu kama ilivyoelezwa. Alikuwa shemeji yangu, mume wa dada yangu Caroline Newa. Pia hakuwa rubani wa ndege, bali nahodha wa meli.”

Alisema amekuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Munisi katika kipindi kisichofikia mwaka mmoja lakini sehemu kubwa ya maisha yao ikitawaliwa na misuguano iliyowafikisha polisi mara kadhaa.

Alisema katika kipindi cha uhusiano wao marehemu Munisi alikuwa akimpiga, akimkataza kufanya kazi, kusoma na alikuwa na wivu uliopindukia.

Christine kuona hivyo, aliamua kufanya mipango ya kwenda kusoma katika Visiwa vya Cyprus kimyakimya pasi na kumuaga, jambo ambalo alisema lilimkera mchumba wake huyo na kuweka kisasi.

“Nikiwa huko, Munisi alitafuta mawasiliano hadi akayapata na tukawasiliana na siku niliporejea alikuja kunipokea uwanja wa ndege lakini cha ajabu, alinikataza kwenda nyumbani na badala yake akanipeleka moja kwa moja hadi Mwanza eneo la Kitangiri,” alisema na kuongeza: “Tukiwa njiani kuelekea Mwanza, katika maeneo ya Singida, alisimamisha gari akaniambia nishuke, akatoa bastola na kuniuliza kwa nini niliondoka bila ya kumuaga. Je, nataka kumuacha?”

Alisema alimwomba msamaha na kuendelea na safari yao. Anasimulia kwamba baada ya kufika Mwanza, alimpora simu zake zote na kumfungia ndani kwa zaidi ya wiki mbili hadi alipopanda kwenye dirisha na kuomba msaada kwa majirani na kuwapa namba za simu za ndugu zake ili wamsaidie kuwapa taarifa.

Ndugu zake walianza mchakato wa kuwasiliana na polisi hatua iliyofanikisha msichana huyo kurudishwa Dar es Salaam... “Hata hivyo niliondoka na khanga na fulana tu. Vitu vyote niliviacha huko.”