MCHUMBA wa ‘video queen’ maarufu Bongo, Agnes Jerald ‘Masogange ‘, Evance Komu amefungua kinywa chake na kusema; siku mchumba wake huyo atakapotia miguu nchini, wanafunga ndoa.
Masogange kwa sasa yupo nchini Afrika Kusini alikokuwa akikabiliwa na kesi ya madawa ya kulevya ambapo alifanikiwa kuwa huru baada ya kulipia faini ya randi 30,000 (shilingi 4,800,000) aliyoamriwa na Mahakama ya Kempton.
Akizungumza hivi karibuni mara baada ya Masogange kuachiwa, Evance alisema anamshukuru Mungu kwa kesi hiyo kumalizika na kinachofuata kwenye uchumba wao ni ndoa tu.
Evance aliweka bayana kuwa kinachomsukuma afanye uamuzi huo kwa sasa ni kutokana na jinsi alivyoguswa na changamoto kubwa alizopitia mchumba wake hivyo ameona kuna kila sababu ya kumuoa kabisa ili apate faraja ya milele.
“Mchumba wangu amepitia majaribu ya kutosha na mimi sioni muda wa kupoteza tena, akitua tu Bongo kinachofuata ni ndoa nina imani itakuwa ndiyo jambo kubwa la kumfariji na kumpa upendo wa hali ya juu,” alisema Evance pasipo kutaja siku ambayo mchumba wake atarejea.
Katika kesi hiyo iliyokuwa ikimkabili Masogange, alishikiliwa na mwenzake Melisa Edward ambaye naye aliachiwa huru kwa kukosekana na hatia.
|
Klabu moja ya Qatar inataka kumsajili Mrisho Ngassa kwa mkataba wa miaka miwili.
Mabingwa wa soka wa Tanzania Bara, Yanga wanaweza kumkosa mshambuliaji wao mahiri Mrisho Ngassa baada ya klabu moja ya Qatar kuonyesha nia ya kumsajili huku mchezaji huyo akikiri kwamba dau walilomuahidi linamshawishi.
Habari za uhakika ambazo Mwananchi ilizipata jana zilisema kuwa, tayari Ngassa amekwishafanya mazungumzo na klabu hiyo ambayo ipo tayari kuilipa Simba SC milioni 45 anazodaiwa na kuifidia Yanga kwa kumuuza mchezaji huyo.
Taarifa hizo zimesema kuwa klabu hiyo inataka kumtumia Ngassa baada ya usajili wa dirisha dogo.Ngassa alithibitisha hilo huku akikataa kutaja jina la timu hiyo kwa sababu za kisheria za usajili wa wachezaji na kuogopa adhabu ya Shirikisho la Soka Kimataifa (Fifa).
Mchezaji huyo alikiri kuwa timu hiyo ipo tayari kumpa mkataba wa miaka miwili na kuzilipa Simba SC na timu yake ya sasa, Yanga.
Alisema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya kuona suala lake la kuitumikia Yanga katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara linashika sura mpya kutokana na mvutano wa malipo.
Alifafanua kuwa klabu hiyo imemuahidi donge nono na kuamua kufuta msimamo wake wa zamani wa kutaka kucheza soka hapa nchini kutokana na maslahi anayopata.
“Maslahi yao mazuri na mazingira waliyoniahidi kimkataba, nimevutiwa nao kutokana na ukweli kuwa suala langu la kuichezea Yanga limekumbwa na vipingamizi vingi,” alisema Ngassa.
Alisema kuwa baadhi ya wadau wa Yanga na marafiki zake wana nia njema ya kutaka kumlipia fedha anazodaiwa na Simba, lakini uongozi wa Yanga bado haujatoa jibu la sakata hilo.
“Nimemaliza kifungo cha mechi sita, sasa suala lililobaki ni malipo, viongozi hawajatoa jibu mpaka sasa, ” alisema Ngassa.
Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Clement Sanga alikiri kuwa bado hawajailipa Simba fedha wanazomdai Ngassa kutokana na majadiliano waliyokuwa nayo.
Sanga alisema kuwa wana uhakika kuwa Ngassa ambaye anafanya mazoezi ya nguvu na Yanga, atacheza Jumamosi dhidi ya timu ngumu ya Ruvu Shooting.
Source:Mwananchi.
|
Anaitwa SaRaha na huu hapa Chini ni wimbo wake
unaitwa Mbele Kiza.Kaimba Vizuri kuliko hata wasanii wa Kibongo.Isikilize na kuidownload.
|
MSHAMBULIAJI Mrisho Ngassa wa Yanga, ameuambia uongozi wake yupo tayari ulilipe Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kitita cha Sh milioni 45 kutoka kwenye mshahara wake.
Ngassa amekubali kitita hicho cha fedha kitolewe kwa kuwa ana hamu ya kuanza kuitumikia Yanga baada ya kumaliza adhabu ya kutocheza mechi sita aliyopewa na TFF.
Imeelezwa Ngassa yupo tayari kukatwa katika mshahara wake na kuna taarifa katika Sh milioni 2 kila mwezi, atakatwa Sh 500,000.
Mshambuliaji huyo alisimamishwa mechi sita pamoja na kutakiwa kurudisha Sh milioni 30 alizolipwa na Simba pamoja na faini ya Sh milioni 15. TFF ilishikilia msimamo wake kwamba Ngassa hatacheza hadi atakapolipa fedha hizo za Simba.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zimeeleza kuwa, Ngassa amekubali kuhusiana na hilo na alifikia makubaliano hayo na mwenyekiti, Yusuf Manji walipofanya kikao walipokutana jijini Mbeya, hivi karibuni.
Alipoulizwa kuhusiana na hilo jana, Ngassa alisema: “Sawa, adhabu yangu ya kutocheza mechi sita za mashindano imemalizika, lakini siwezi kuongelea lolote, mimi ni mchezaji tu, kazi yangu ni ndani ya uwanja, hayo mengine ya kiutawala ni vyema yakatolewa ufafanuzi na viongozi,” alisema Ngassa.
Championi Jumatano lilimtafuta Manji ambaye alikiri kuzungumza na Ngassa kuhusiana na masuala kadhaa ya klabu yao likiwemo hilo. “Mimi ni mwenyekiti, hakuna ubaya kuzungumza na Ngassa. Tunazungumza kwa ajili ya klabu yetu, hivyo msubiri akicheza mtamuona,” alisema Manji.
Taarifa nyingine zilieleza kuwa, Yanga ilikuwa tayari kupeleka fedha hizo leo, lakini ilitaka TFF wakate Sh milioni 45 katika Sh milioni 70 inazowadai na walikuwa katika mazungumzo katika hilo. Kwa upande mwingine, Kocha Mkuu, Ernie Brandts, alisisitiza kwamba ana kila sababu ya kumpanga Ngassa kama atakuwa amerejea katika kikosi watakapoivaa Ruvu Shooting Jumamosi. “Tuko naye kikosini kila siku, tunafanya naye mazoezi na tunashirikiana. Kama amerejea na yuko katika afya nzuri, nitampanga maana ninamhitaji,” alisema Brandts. Wakati hilo la Ngassa linamalizika, taarifa nyingine za uhakika zimeeleza Manji alitarajia kukutana na kikosi kizima cha Yanga, jana usiku. Mwenyekiti huyo alipanga kukutana na wachezaji na benchi la ufundi katika hoteli ya Serena jijini Dar ili kula chakula cha usiku na baadaye kujadili masuala kadhaa kikiwemo kipigo cha Azam FC na nini cha kufanya baada ya hapo ili kusonga mbele na ikiwezekana kutetea -GPL
|
INGAWA duka la Westgate liko karibu dakika 15 tu kutoka nyumbani kwangu, nilikuwa nikienda kule kwa nadra kununua vitu. Mara kwa mara huwa kuna watu wengi katika duka hili katika siku za mwisho mwa wiki na hivyo niliona kama karaha. Jumamosi ilikuwa maalumu kwa sababu nilitaka kutumia muda wangu na mkwe yangu, Amina (si jina halisi) na baadhi ya marafiki zetu ambao watoto wao walikuwa wakishiriki katika shindano la upishi.
Tulikuwa juu ya ghorofa la mwisho saa 5.00 asubuhi. Shindano la upishi lilikuwa likiendelea.
Baada ya muda, Amina aliamua kuelekea chini kwa ajili ya kununua vitafunwa. Sikuwa na njaa sana hivyo niliamua kubaki hapo hapo. Nilitaka kuangalia watoto wakipika.
Karibu saa saba na robo, Amina alikuwa hajarejea nilipokuwa, lakini sikuwa na hofu na nilibakia hapo hadi niliposikia sauti ya milio ya bunduki.
Nilishikwa na kihoro na kumpigia simu mwanangu. Ni ofisa usalama na nilidhani pengine angeweza kusaidia.
“Kuna milio ya risasi hapa. Naweza kusikia milio ya risasi. Tafadhari fanya unaloweza,” nilimwambia.
Niliongea naye kwa muda mfupi kwa simu kwa sababu nilitaka kuzungumza na mkwe wangu. Katika simu aliniambia kuwa alikuwa amejificha katika benki iliyo kwenye kituo hicho cha biashara. Alisisitiza kwamba yu salama na alitaka niwe mwangalifu.
Mazungumzo yetu yalihitimishwa ghafla nilipoona watu wawili wakija juu. Walikuwa na bunduki na haikunichukua muda nikaona mabomu ya kutupwa kwa mkono yakining’inia katika mikanda yao.
Nyuso zao hazikufichwa na tuliziona wazi kana kwamba walikuwa hawajali iwapo tungeweza kuwatambua baadaye. Mara moja nilianza kuwa na wasiwasi huenda nisitoke hai.
Katika kitambo hicho, hofu yangu ilikuwa kubwa. Magaidi walipoanza kurusha risasi na magurunedi holela, umati ukaangua kilio kwa kihoro.
Watu walianza kukimbia kwa mshtuko huku mwelekeo wao ukiwa haueleweki. Nami nilikimbilia katika hema lililokuwa likitumika kama jiko la watoto na kujificha humo.
Awali nilidhani walikuwa wakifyatua risasi kwa bahati mbaya. Hata hivyo, punde nikaona kwamba wale watu waliokuwa wakikimbia huko na huko wakipiga kelele ni wale waliokuwa wamepigwa risasi. Huku kukiwa na makelele, niliwasikia magaidi wakiwaita Waislamu:
“Kama ninyi ni Waislamu, mnaweza kunyanyuka na kuondoka,” walisema.
Lakini haikuwa rahisi kama ilivyodhaniwa. Waislamu walitakiwa kuthibitisha imani yao. Walitakiwa kutaja jambo fulani kutoka aya za Korani kabla ya kuachiwa. Na hata baada ya hapo bado unaweza kupoteza maisha yako. Mwanamke mmoja ambaye alisema alikuwa Muislamu lakini hakuonekana kuwa Muislamu alipigwa risasi na kufa.
Sina uhakika kwa nini sikutumia dini yangu ili kujiokoa mapema. Pengine ilitokana na hofu. Pengine ilitokana na hali ya ukaidi.
Nikiwa nimejificha nyuma ya maboksi na meza katika hema, watu nisiowajua wakawa wa karibu nami kuliko marafiki. Magaidi lazima walijua tulipo; kulikuwa na maeneo mengi ambayo tungeweza kuyatumia kujificha.
Hata hivyo, tulitulizana wenyewe kwa wenyewe huku tukiwataka watoto wanyamaze kwa sababu sauti zingeweza kutufichua pale tulipo.
Lakini pamoja na juhudi zetu zote za kuwatuliza wanyamaze, bado baadhi ya watoto hawa hasa wale wadogo walilia.
Tuliomba. Tuliwasilisha maombi yetu kimyakimya kwa Muumba wetu, pengine tukiona hiyo ni siku yetu ya mwisho kuwa hapa duniani.
Tulikuwa tumejificha kwa dakika 20 wakati nilipomsikia mmoja wa magaidi akipokea simu kupitia simu yake ya mkononi. Hakuzungumza kwa sauti kubwa, lakini ilikuwa sauti tulivu ya Kiswahili iliyosikika vema masikioni.
Maneno halisi ilikuwa vigumu kuyakumbuka. Lakini alisema kuwa ameua watu wengi na wengine zaidi walijeruhiwa.
Dakika chache baadaye baada ya kupokea simu, magaidi walirusha risasi ovyo juu ya paa na kuondoka. Nikadhani kwamba milio hiyo ya mwisho ililenga kutuogopesha na kutuonya tusijaribu kuondoka mahali tulipo.
Tuliokolewa muda mfupi baadaye na wakati nikitembea kutoka katia jengo hilo tuliona miili ikiwa imezagaa sakafuni, nilijisikia nisiye na msaada kwamba sikuweza kufanya lolote kuzuia hali hii.
Nilikuwa huru lakini mkwe wangu alikuwa bado amenasa katika jengo. Nilipompigia simu alinihakikishia kuwa yu salama tena kwa sauti tulivu. Alinitaka nisiwe na wasiwasi, ombi ambalo halikuwezekana kwangu.
Amina aliokolewa saa 12 jioni. Saa kadhaa nikiwa nyumbani kwa mwanangu na kwa rafiki yangu kusubiri neno la matumaini kutoka kwake ilikuwa tete hakika.
Nilifarijika sana wakati alipompigia simu mwanangu akimtaka aende kumchukua kutoka Visa Oshwal.
Saa zaidi ya 24 baada ya ile iliyokuwa siku njema nikiwa na mkwe wangu iligeuka kuwa jinamizi, na bado ninatetemeka nikiikumbuka. Hata hivyo, nina furaha kuwa hai na ninashukuru Amina na mimi tulitoka Westgate bila majeraha.
*Hii ni simulizi ya mmoja wa watu waliookoka katika tukio la ugaidi la Westgate
|
MAMA wa aliyekuwa msanii maarufu Bongo, marehemu Hussein Mkiety ‘Sharo Millionea’, Zainab Mkiety amemkataa mtoto ambaye alipelekewa Tanga na mama yake anayetokea Geita akidai ni damu ya Sharo.
Mtu wa karibu na familia hiyo amesema kuwa baada ya msiba kupoa, mama wa mtoto huyo alifunga virago na mwanaye kwa ajili ya kwenda kutembelea kaburi la Sharo na kwenda kujitambulisha kwa bibi wa mtoto.
Chanzo hicho kilieleza kuwa mama mtoto huyo alipofika Muheza jijini Tanga, alipokelewa na watu wa bodaboda ambao walimsindikiza hadi nyumbani kwa mama Sharo.
“Alipofika alipokelewa lakini cha kushangaza mama Sharo alimkataa na kusema marehemu hakuwa na mtoto kwa sababu hakuwahi kumwambia,” alisema sosi huyo.
Ili kupata ukweli wa habari hiyo, paparazi wetu aliwasiliana na mama Sharo kwa simu ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli alikuja mwanamke akiwa amebeba mtoto ambaye alijitambulisha kwangu kuwa ametokea Geita.
“Alisema mtoto aliyekuwa amembeba ni wa Sharo lakini nilikataa nikamwambia kuwa mwanangu hakuwahi kuniambia kuwa ana mtoto na nilipowauliza marafiki zake walisema hawana taarifa hizo.
Nisingeweza kumpokea kwa sababu alishajitokeza mwingine na kudai kuwa ana mimba ya mwanangu, baada ya kumkataa mwanamke huyo aliondoka na mpaka leo sina mawasiliano naye.”
Sharo alifariki dunia kwa ajali ya gari Novemba 26, mwaka jana katika Kijiji cha Maguzoni-Songa, Wilaya ya Muheza jijini Tanga.
GPL
|
No comments:
Post a Comment