advert

http://

Tuesday, 24 September 2013

MZEE MAJUTO ADAI ANA WAKE FEKI WENGI SANA HAPA TOWN.



Majuto anasema kuwa ana watoto tisa ingawa hakuwa tayari kuwazungumzia mama wa watoto hao zaidi ya kumwongelea mkewe wa sasa, Aisha Mbwana kwa kuwa wake zake aliozaa nao baadhi ya watoto kwa bahati mbaya walishafariki dunia.

Alisema kuwa yanapokuja masuala ya familia huwa anapenda azungumze mkewe na kwa ridhaa yake. Kwa mujibu wa Majuto anapenda aitwe mke halali kwa kuwa wake feki anao wengi kupitia michezo ya kuigiza na wengine wenye fikira potofu hutumia picha hizo kutengeneza habari za uongo.


Aisha anaizungumziaje familia yake
Kama kawaida ya wanawake wa Tanga ana lafudhi ya huko ambayo huvutia kuzungumza nao, anaanza kwa kunieleza kuwa alianza kuitwa mke halali wa nguli huyo wa sanaa za maigizo mwaka 1997, walipofunga ndoa .
Anasema kuwa alikutana na nguli huyo maeneo ya Buguruni, Dar es Salaam, ambako alikuwa akiishi na dada yake aliyekuwa kaolewa na rafiki yake mzee Majuto, ‘Mwanachia’ (kwa sasa ni marehemu), ambaye walikuwa wakiigiza pamoja.
Anasema hakuwa na hili wala lile hadi alipoamua kuondoka na kurudi kwao maeneo ya Vingunguti, ambako ndiko walikokuwa wanaishi wazazi wake na kupewa taarifa kuwa posa imepelekwa kwa ajili yake.
“Nilipoambiwa kuhusu hiyo posa sikufikiria kama atakuwa ni mzee Majuto kwa kuwa alikuwa ni kama shemeji yangu kutokana na kuwa karibu na shemeji yangu,” anasema Aisha ambaye ni mama wa watoto watatu.
Anaendelea kueleza kuwa siku ambayo wanafamilia walikutana na kumuuliza kama anamfahamu mchumba na kutajiwa jina kuwa ni Amri Athumani, aliuliza mara mbili kwa kuwa alikuwa hamfahamu huyo mtu hadi alipoambiwa kuwa ni King Majuto.
“Kwa mila za Wabondei mchumba wa kwanza anakubaliana na wazazi, halafu binti anapewa taarifa na kwa kuwa wazazi ni wakubwa inabidi binti akubali, na ndivyo ilivyokuwa kwangu nikakubali na kuolewa na Majuto,” anasema mama huyo.
Anaingia kwenye uigizaji kufuata nyayo za mumewe
Aisha anafafanuwa kuwa kabla ya kuolewa na Majuto hakuwa mwigizaji lakini baada ya kuolewa, mumewe huyo alimwingiza kwenye uigizaji na filamu ya kwanza kuigiza na mumewe huyo ni ‘Fukara hatabiriki’.
Mkewe huyo anasema kipindi hicho Majuto alikuwa anafanya kazi bila kuwa na kikundi zaidi ya wanafamilia, hivyo na yeye alikuwa mmoja wao akicheza kama mama na Majuto kama baba.

"Hey Guys Pliz Kwa Heshima Zote na taadhima naomba msiwe mna comment about Huddah Or Prezzo in My Page. That Chapter is closed muda mrefu sana and matter of fact Dont need Drama. My Life seems to be Naturally .


I never have plans for where it’s going to take me. Huwa nafuta na kujisikia vibaya nikiona mbaendelea comment about Prezzo. well The truth ni Kuwa My heart Belonged to another man and The Tattoo of his name katika Mkono wangu itakuwa removed yes …. working on that. I Respect him and he is such a good Person but pliz enough with his name on My Page….hope mmenielewa. love you all" Says Loveness Diva
Mwanamke raia wa Uingereza, Samantha Lewthwaite aka The White Widow, *anahisiwa* kuongoza kundi la magaidi wa Al-Shabaab walioivamia mall maarufu ya Westgate ya jijini Nairobi nchini Kenya jana na kuwaua watu zaidi ya 68 na kujeruhi wengine zaidi ya 175.



Tayari mashirika makubwa ya habari duniani yakiwemo, CNN, The Sun na IBTimes yameandika habari kuhusu uwezekano wa mwanamke huyo kuwa kiongozi wa magaidi hao walioshambulia Westgate.

Nayo akaunti ya Twitter ya American Jihad Watch ‏@watcherone, imepost picha ya gaidi wa kike iliyedai ilipigwa na camera za ndani ya mall huyo na kudai kuwa ‘huenda’ akawa ni The White Widow. “Female jihadi caught on mall camera at Westgate Centre Shopping mall earlier yesterday may be infamous ‘White Widow’, imesomeka tweet hiyo.
Picha ya gaidi akiwa ndani mall hiyo

Kwa mujibu wa baadhi ya watu waliokolewa kwenye mall hiyo, miongoni mwa magaidi hao alikuwepo mwanamke wa kizungu.


Kwa mujibu wa CNN, magaidi watatu ni wa Marekani, mmoja wa Kenya, Uingereza, Finland na wawili wa Somalia. Bado wamo ndani ya mall hiyo.

Hata hivyo Kwa mujibu wa mtandao wa Telegraph, jana usiku ofisa wa shirika la kupambana na ugaidi Kenya alikanusha taarifa kuwa Samantha Lewthwaite anaweza kuhusika na shambulio la jana.

Samantha Lewthwaite aka The White Widow ni nani?

Ni mwanamke anayetafutwa kwa udi na uvumba kwa kuhusika kwake kwenye matukio mbalimbali ya kigaidi nchini Uingereza na Afrika Mashariki. Yeye ndiye aliyepanga shambulio la kigaidi jijini London la mwaka 2005 lililosababisha vifo vya watu 52 ambapo mume wake Jermaine Lindsay alijitoa muhanga.


Akitokea Aylesbury, Buckinghamshire, nchini Uingereza, The White Widow kwa sasa ni kiongozi wa juu wa mashambulio ya Al Shabaab nchini Kenya na Somalia. Mwanamke huyo anadaiwa kuwa mfadhili mkuu wa shughuli za kundi hilo la kigaidi.

No comments: