WATUMIAJI wa simu wapatao milioni nane wapo hatarini kufungiwa simu zao ifikapo mwishoni mwa mwezi huu, Tanzania Daima limebaini.
Tayari Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeziandikia kampuni za simu waraka wa kuzitaka zianze kukata kodi mpya ya laini (simu card) mara moja kuanzia Julai 30, 2013.
Hatua hiyo inatokana na serikali kushindwa kufuta kodi hiyo ya sh 1,000 iliyopitishwa na Bunge kama alivyoagiza Rais Jakaya Kikwete baada ya kukutana na wadau wa sekta ya mawasiliano.
Kwa maana hiyo kila anayemiliki laini moja ya simu atakatwa sh 3,000; anayemiliki laini mbili sh 6,000 na anayemiliki laini tatu sh 12,000, lengo ni kuhakikisha serikali inakusanya sh bilioni 178 zitakazopelekwa kwenye bajeti kuu ya serikali.
Watumiaji wa simu sasa watalazimika kulipia kodi hiyo ya miezi mitatu ya Julai, Agosti na Septemba kwa wakati mmoja.
Bunge kupitia Kamati ya Bajeti inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM) lilitaka kuwapo kwa kodi hiyo ili kusaidia shughuli za bajeti ya Serikali Kuu.
Kupitishwa kwa kodi hiyo kuliibua malalamiko ya wanasiasa dhidi ya Chenge anayelazimisha kuwapo kwa kodi hiyo, huku akishindwa kuamini kwamba kuna Mtanzania anayekosa sh 1,000 kwa mwezi kwa ajili ya laini ya simu.
Malalamiko hayo yaliendelea hadi kwa wananchi na baadhi ya wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliotaka posho za wabunge zipunguzwe ili kuziba pengo hilo badala ya kuwabebesha wananchi mzigo.
Inadaiwa kwamba msimamo wa Chenge unaungwa mkono na Spika wa Bunge, Anne Makinda, jambo lililosababisha kutojadiliwa kwa hoja binafsi ya Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (CHADEMA) iliyohusu kodi hiyo katika mkutano wa Bunge lililopita kwa kisingizio cha kukosekana kwa muda wa kufanya hivyo.
Hata hivyo, takwimu zilizotolewa na kampuni za simu zinaonyesha kuwa miongoni mwa wamiliki wa laini za simu milioni 22; milioni nane wanatumia chini ya sh 1,000 kwa mwezi.
Baada ya malalamiko hayo, Rais Kikwete alikutana na wadau wa mawasiliano ambao ni wamiliki wa kampuni za simu Tanzania (MOAT), Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Waziri wa Fedha, William Mgimwa, kisha kuwaagiza waiondoe kodi hiyo.
“Rais alisema lengo kuu la mkutano huo liwe kupendekeza jinsi ya kuziba pengo la sh bilioni 178 zitakazopotea katika bajeti iwapo kodi hiyo itafutwa.
“Alisema hawezi kuifuta moja kwa moja kodi hiyo, bila kutafuta njia nyingine za kupata fedha kujazia pengo litakalotokeza huku tayari Bunge limezipangia matumizi,” alinukuliwa Makamba baada ya kikao hicho na rais.
Kwa upande wake, rais alikaririwa akiwaambia wadau hao wa mawasiliano kwamba: “Nakuombeni kaeni pamoja, wekeni bongo zenu pamoja, wekeni akili yenu pamoja tutafute namna gani tutajaza pengo hili la sh bilioni 178 endapo tutakubaliana kuwa kodi hii inawabebesha wananchi mzigo mzito, na kuwa pengine menejimenti ya kodi yenyewe ni ngumu.”
Licha ya agizo hilo la rais kutekelezwa kwa MOAT kutakiwa kuongeza kodi nyingine iitwayo ‘Excise duty’ kutoka asilimia 14 hadi 17 bila kujali kwamba katika Bunge la bajeti kodi hiyo iliongezwa kutoka asilimia 12 hadi asilimia 14, tozo hiyo ya laini za simu haijaondolewa.
Wachambuzi wa masuala ya siasa na mawasiliano walisema kutojadiliwa kwa mabadiliko ya kodi hiyo ya simu ni dalili kwamba Waziri wa Fedha amezidiwa nguvu na kiti cha spika kinachounga mkono hoja hiyo ya Chenge na kushindwa kutekeleza agizo la rais.
Wataalamu wa mawasiliano walilieleza gazeti hili kwamba kuongezeka kwa kodi hiyo kutaifanya Tanzania kuwa na kiwango cha juu cha kodi kuliko nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Ushauri wa wataalamu hao ulibainisha kwamba kuongezeka kwa kodi hiyo kunaleta nafuu kidogo kuliko ile ya laini za simu inayomuumiza zaidi mwananchi wa kawaida.
|
MAUAJI ya watu watatu wa familia moja yaliyotokea jijini Mwanza hivi karibuni yameibua maswali mengi lakini mwisho wa yote, imebainika kuwa kilichoiponza familia hiyo kukumbwa na mauti hayo ni hiki.
Mauaji hayo yalitokea saa 10 alfajiri ya Septemba 21, mwaka huu katika Kijiji cha Ihila, Kata ya Buhongwa, Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza ambapo inaaminika kuwa mgeni aliyekaribishwa kwenye familia hiyo ndiye aliyetekeleza mauaji hayo na alikaribishwa nyumbani hapo bila kujulikana tabia.
Debora Jonas Luhinga, mtoto wa marehemu ambaye alinusurika katika tukio hilo, alisema kuwa mgeni huyo aliyemfahamu kwa jina moja la Lameck alifika nyumbani hapo Septemba 18, mwaka huu lakini baada ya kutekeleza mauaji hayo alitokomea kusikojulikana. Debora mwenye umri wa miaka 12, alidai kuwa siku ya tukio, usiku akiwa amelala, mdogo wake aitwaye Eliudi aliyekuwa amelala naye aliamka na kuanza kulia sana. Alisema alichukua jukumu la kumbembeleza mdogo wake huyo lakini ilishindikana, ghafla Lameck aliingia chumbani humo na kumwomba mtoto huyo ili ampeleke chumbani kwa wazazi wake akabembelezwe. “Kilio cha mdogo wangu kilikuwa kikubwa, mara nikaona mlango unafunguliwa, Lameck akaingia, akasema kwa kuwa mtoto analia sana nimpe ampeleke kwa mama ili akambembeleze,” alisema Debora. Akaongeza kuwa alikubali kumpa Lameck mtoto huyo na kwa vile yeye alikuwa na usingizi mzito aliendelea kulala fofofo. Debora alisema alipoamka kulikuwa kumekucha, akashuka kitandani ili aende nje lakini akakuta mlango umefungwa kwa nje. “Nilipiga kelele baada ya kukuta mlango wa chumba changu umefungwa kwa nje, majirani walifika kunifungulia lakini nilipigwa na mshangao kukuta maiti ya baba ikiwa sakafuni sebuleni tena imetapakaa damu. “Nikiwa nimechanganyikiwa niliingia chumbani kwa wazazi wangu, nikashangaa kumuona mama yangu na mdogo wangu Eliudi wakiwa wameuawa kwa kunyongwa na miili yao imelazwa chini,” alisema Debora. Debora alisema anaamini Lameck ambaye mara nyingi alikuwa akimwona akizungumza na baba yake ndiye aliyetenda unyama huo. Alisema anaamini mtu huyo wakati anaingia chumbani kwake kumchukua mdogo wake alikuwa ameshawaua wazazi wake na aliamua kumtwaa mtoto huyo kwenda kumnyonga ili kilio chake kisiwafanye majirani wakafika nyumbani hapo kutaka kujua kulikoni na hivyo kugundulika alichokifanya kwa muda huo. Alikwenda mbele zaidi kwa kusema anaamini baba yake ndiye aliyeanza kuchinjwa kabla ya mama yake kunyongwa. Baadhi ya majirani waliozungumza na gazeti hili huku wakiomba majina yao kuhifadhiwa baada ya tukio hilo, walisema kwa nyakati tofauti kuwa huenda mauaji hayo ni ya kulipiza kisasi kwa mwanaume huyo ila mkewe na mtoto waliingizwa kwenye mkumbo tu.
Walisema haiwezekani watu wa familia moja wakauawa kikatili namna hiyo bila ya wauaji kuanika sababu. Waliongeza kwa kudai kuwa siku zote tatu alizoishi hapo, Lameck alikuwa akitafuta njia mwafaka ya kutekeleza ukatili huo. Walisema mauaji mengi ya aina hiyo yanayotokea katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mwanza huhusishwa na imani za kishirikina, migogoro ya ardhi au mirathi. Majirani hao waliongeza kuwa awali walikuwa wakimwona Lameck nyumbani kwa marehemu bila kujua uhusiano wao, wakaonya kuwa ni hatari sana kumkaribisha nyumbani mtu usiyemjua kwa undani kama ilivyokuwa kwa Lameck. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, ACP Ernest Mangu alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo huku akisema hakuna aliyekamatwa. Aliwataja marehemu kuwa ni Jonas Luhinga, mkewe Rusia Jonas na mtoto wao, Eliud Jonas.
Source:uwazi.
|
The lamentations of parents of this generation is simply that students have lost focus in every sphere of life. One major obvious screen to watch the decadence is the results they push out these days. What has taken over the minds of these young ones is simply the internet and the dirty displays they see on TV, and this has no doubt created such a picture as this. What is your take?
|
Wakati mapambano bado yanaendelea dhidi ya wanamgambo wachache wa al Shabaab waliobaki ndani ya Westgate Mall, maofisa wa Kenya wamesema angalau al Shabaab watatu wameuawa katika harakati za kuokoa mateka.
Taarifa zinasema mmoja wa magaidi hao ni mwanamke wa kizungu. Inaaminika kuwa mwanamke huyo aliyetajwa ni Samantha Lewthwaite, al-maarufu kama “White Widow” au “Mjane Mweupe” au “Mjane wa Kizungu” kwa Kiswahili. Samantha anaripotiwa kuwa ndiye kiongozi wa kundi hilo lililofanya mashambulizi.
Inasemekana kwamba kati ya magaidi waliouawa, mmoja wao ni mwanamke wa kizungu lakini bado haijajulikana kama ni Samantha.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail la Uingereza, mume wa Samantha alikua mpiga mabomu wa kujitoa mhanga (suicide bomber) anayeitwa Germaine Lindsay ambaye baada ya kusilimu alitumia jina la Abdullah Shaheed Jamal.
Abdullah Jamal alikua ni mmoja wa magaidi wenye asili ya Uingereza waliopiga mabomu ya kujitoa mhanga katika treni tatu na kuua watu 56 nchini uingereza Julai 7, 2005 ambao unajulikana duniani kama “Ugaidi wa 7/7″
Source:Udakuspecially.
|
No comments:
Post a Comment