advert

http://

Sunday, 15 September 2013

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Padri Joseph Monesmo Magamba, wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui

.

 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Padri Joseph Monesmo Magamba, wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, alipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole,Mjini Unguja,baada ya kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana katika Mtaa wa Mlandege Mkoa wa Mjini Magharibi jana jioni, Padri alimwagiwa Tindikali alipokuwa akitoka kupata huduma ya Mtandao.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimsikiliza Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,akitoa maelezo jinsi alivyopata mkasa wa kutiwa  Tindikali jana na watu wasiojulikanwa,katika mtaa wa Mlandege Mjini Unguja, alipofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole,ambapo amelazwa na kuapatiwa matibabu.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwafariji jamaa  na ndugu wa Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,waliofika katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kumpa pole Padri huyo baada ya kumwagiwa Tindikali na Watu wasiojulikanwa jana jioni Mtaa wa
Mlandege Mjni. 
 Mmoja wa Ngugu wa Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,akimueleza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,hisia zake kwa Uchungu kutokana na kitendo hicho cha kumwagiwa Tindikali na watu wasiojulikanwa  kwamba zilichukuliwe hatua za kisheria na kukomeshwa Vitendo kama hivyo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifafanua jambo wakati akiwafariji jamaa na ndugu wa Padri Joseph Monesmo Magamba,wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui,waliofika kumuangalia Padri huyo aliyelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya kumwagiwa Tindikali na Watu wasijulikanwa jana jioni katika Mtaa wa Mlandege Mjini Unguja.

 
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira, amesema wapinzani wasitarajie tena kukaribishwa Ikulu, 
kutokana na msimamo wao wa kususia mjadala wa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2013, wakati wa kikao cha Bunge mjini Dodoma hivi karibuni, kwa majadiliano mengine. 
Waziri Wassira, alitoa kauli hiyo siku moja baada ya wasomi, wanasiasa na wanaharakati kutoa ushauri wa kumsihi Rais Jakaya Kikwete asisaini muswada huo ili kuwa sheria kamili, kwa vile hauna tija kwa Watanzania.

Akizungumza na MTANZANIA jana juu ya ushauri huo, Wassira alisema hoja na ushauri unaotolewa na makundi hayo hauna mantiki kwa sababu taratibu zote za sheria zilifuatwa, kuanzia mwanzo hadi kuupitisha muswada huo.

“Nianze kwa wanasiasa wa upinzani kususia na kutoka ndani ya Bunge kwa hoja ya kutowashirikisha wananchi wa Zanzibar, hili si kweli, kwa sababu Kamati ya Katiba na Sheria ilikwenda huko, sasa wasitake kulalamika na kutaka kukutana na Rais Kikwete.

“Hawa tumewalea siku nyingi na sasa wanafanya mazoea, ninachotaka kuwaeleza wasitarajie tena kuitwa Ikulu, nchi hii inaongozwa na misingi na kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria.

“Kwanza kitendo cha Kiongozi wa Upinzani, Freeman Mbowe kutotii kiti cha Spika wa Bunge ni dharau na alikiuka taratibu zinazoongoza Bunge, kwanza alisababisha kuwapo vurumai ambazo zimeshusha heshima ya Bunge.

“Upinzani wajue vurumai zao haziwezi kutengeneza Katiba wanayoitaka Watanzania, bali ni kufuata taratibu pale wanapoona kuna kasoro, hivyo kulalamika kwao bila kufuata taratibu hakutawasaidia kamwe.

“Kuna mazoea ya kwenda kwa wananchi kuwadanganya, sasa tunasubiri tumesikia wanaandaa tamko lao la upinzani, tutalisoma na kama wakienda kwa wananchi kueneza propaganda zao tutawafuata nyuma na kuwaeleza ukweli wananchi,” alisema.

Alisema Watanzania milioni 45, hawawezi kuaminishwa uongo wakati Serikali ipo na kuongeza kwamba nchi haiwezi kuendeshwa na vurugu wakati kuna vyombo vya dola vyenye mamlaka yake.

Kuhusu ushauri wa wasomi kutaka Rais Kikwete kukutana na wanaolalamika, alisema inategemea na utashi wake na jinsi atakavyoona inafaa.

Alisema imegundulika wasomi wa vyuo vikuu mbalimbali wamekuwa wakitumia mwavuli wa elimu yao kutoa maoni yao ambayo yanaonekana wazi ni ya itikadi ya vyama vya siasa.

“Hawa wanaojiita wasomi wote wana itikadi ya vyama vya siasa, sasa badala ya kutoa ushauri ambao utaonekana ni wa msomi, wanajikuta wanakuwa sehemu ya siasa tena.

“Sasa watu kama hao inapaswa kuwaangalia kwa makini sana, kwa sababu wanafanya kazi ya chama cha siasa kwa kutumia mwavuli wa usomi wake, hivyo hivyo kwa wanaharakati, badala ya kufanya kazi kama ilivyoelekezwa kwenye usajili wao, nao wanaingia kwenye siasa.

“Ninachowashauri, nchi hii haiendeshwi kwa ubabe, bali inasimamiwa na sheria, hivyo kila mmoja akifuata sheria hakuna ugomvi, pia haya madai ya kusema kuwa Katiba ijayo itakuwa ni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hayana msingi wowote,” alisema.

Juzi wasomi kutoka vyuo mbalimbali, kikiwamo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Tunguu kilichopo Zanzibar na vingine, walitoa ushauri wao wa kumtaka Rais Kikwete kufikiri zaidi na kuchukua tahadhari kabla ya kusaini muswada huo ili kuwa sheria kamili.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, Pindi Chana, alipoulizwa na MTANZANIA kuhusiana na malalamiko hayo, alisema: “Kamati yangu ilifanya kazi iliyotumwa na taratibu zote zilifuatwa.”


SOURCE:Mtanzania

MSANII aliyewahi kutamba kisha kuporomoka kwa kasi katika tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa sababu ya tabia zake chafu, Irene Uwoya, amefikishwa Kituo cha Polisi Msimbazi kwa wizi wa simu aina ya iPhone 5.

  
Kwa mujibu wa habari za kipolisi, mmiliki wa simu hiyo  ni mwanamme aliyejulikana kwa jina la Mohammed Marjey, mkazi wa Dar.
  
Uwoya ambaye siku hizi anajitutumua kwa kuanzisha kipindi kwenye runinga moja ya Bongo baada ya kushindwa kwenye filamu, alidakwa na askari wa Kituo cha Polisi Msimbazi, Dar baada ya kusakwa usiku na mchana kwa kutumia kumbukumbu ya jalada la kesi namba MS/RB/8522/13 WIZI KUTOKA MAUNGONI.

Simu aina ya iPhone 5 kama inayodaiwa kuibiwa na Uwoya.
Akizungumza na mwandishi wetu, Mohammed alisema simu hiyo aliinunua mwaka huu kwenye Duka la Grande Center jijini New York, Marekani alikokwenda kwa shughuli zake.Akasema Agosti 22, mwaka huu alirejea Bongo akiwa na simu hiyo ambayo ni toleo jipya la mwaka huu.
  
“Nilirejea hapa nchini nikiwa na simu hiyo. Tena unajua simu yenyewe ni ya kisasa, toleo la mwaka huu,” alisema Mohammed.Alisema Agosti 23, mwaka huu, akiwa kwenye gari katika Makutano ya Barabara ya Uhuru na Mtaa wa Nyamwezi, Kariakoo, Dar aliibiwa simu hiyo na mtu asiyemtambua.
  
“Nilikwenda Polisi Msimbazi kuandikisha maelezo na kupewa RB hiyo. Lakini nilitumia njia ya kitaalam kufuatilia, nikagundua simu yangu inatumiwa na mtu anayeitwa Peter, nikampigia simu kumwambia lakini hakuweka wazi aliipataje?
  
Mohammed alisema baada ya dakika kumi, alipigiwa simu na Uwoya na kumchimba mkwara kuhusu simu hiyo huku akisema ni yake yeye, jambo ambalo lilimshangaza jamaa huyo.
  
“Nilirudi Msimbazi na kuwaambia ndipo polisi wakaanza kazi ya kumsaka ili wamkamate.Amekamatwa akiwa na hiyo simu yangu,” alisema.


Inadaiwa kuwa polisi walimuuliza Uwoya alikoipata simu hiyo ambapo alisema alipewa na jamaa yake wa Afrika Kusini huku mlalamikaji huyo akitoa risiti ya kununulia.
  
Baada ya kumaliza kuhojiwa kituoni hapo, Uwoya alitolewa kinyemela kwa mlango wa nyuma ili waandishi  waliopiga kambi nje ya kituo hicho wasimfotoe.


Source:GPL 
.

No comments: