Mkuu wa wilaya ya Musoma Mjini, mheshimiwa Jackson Msome amesema wamemuandalia mapokezi mazuri kwa kuwa ushindi wake umeleta heshima kubwa katika mji huo.
“Kwanza ni mkazi wetu, ni mkazi wa mji wa Musoma. Sisi tukiwa kama wenzie na viongozi wake, kwanza tunayo fahari kwa ushindi wake. Lakini la pili tulimsapoti sana na tulimuomba sana Mungu amsaidie katika jitihada zake hizo. Ushindi wake huo unaleta heshima kwake, kwa wilaya yetu, kwa mkoa wetu, kwa kanda yetu na Tanzania kwa ujumla. Kwa hiyo tuna kila sababu ya kufurahi pamoja naye.” Mheshimiwa Msome aliiambia tovuti ya Times Fm.
Mheshimiwa Msome, ameelezea pia faida/changamoto waliyoipata vijana wa Musoma wenye vipaji kutokana na ushindi wa Emmanuel Msuya.
“Hii ni changamoto kwa vijana, kwamba vijana wapo na wana vipaji mbalimbali. Kinachotakiwa ni kutambua fursa zilizopo na hivyo kuzitumia kujitokeza kukuza vipaji vyao, na kwa kweli ni sehemu ya ajira kwa vijana wetu.”
Naye mratibu wa mapokezi hayo ambaye ni mdau wa muziki mjini musoma maarufu kwa jina la Kayombo, amesema kuwa mapokezi hayo yatakuwa ya kihistoria kwa mtu wa kawaida ambaye sio kiongozi wa nchi, na kwamba kutakuwa na misafara ya pikipiki na magari. Ameongeza kuwa kesho (December 15) washiriki waliombatana na Msuya watatumbuiza katika ukumbi wa Bwalo la Polisi.
Akiongea na Times Fm wakati akiwa uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam, Emmanuel Msuya amesema yuko na timu ya washiriki waliofika Top 5 ya shindano hilo pamoja na mama yake mzazi na wanaelekea Mwanza.
Amesema wanategemea kuingia Musoma majira ya saa kumi na moja jioni.
Emmanuel Msuya alitangazwa kuwa mshindi wa EBSS 2013, November 30 na kuwa mmiliki wa shilingi Million 50 zilizokuwa zinashindaniwa.
No comments:
Post a Comment