advert

http://

Sunday, 15 December 2013

MWANAMKE MMOJA AMWAGIWA MAJI YA MOTO NA MWANAMKE MWENZIE KISA WIVU WA KIMAPENZI.


Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili mzima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano na mume wa mtu. 


Muuguzi wa zamu Bi. Neema Bayo akimfunika majeruhi Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili mzima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano na mume wa mtu.  

Bi. Neema Teti aliyemwagiwa maji ya moto mwili mzima, kwa kudaiwa kuwa na uhusiano na mume wa mtu.

Na Gadiola Emanuel -Arusha

Mwanamke mmoja mkazi wa Mbuguni Arusha,Bi. Neema Teti amejeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa maji ya moto katika sehemu mbalimbali za mwili wake katika kisa kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi. Tukio hilo limetokea baada ya mtekelezaji wa kitendo hicho Mama Tatu Msuya ambaye ni jirani yake akidaiwa kumtuhumu majeruhi huyo kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mume wake.
Katika wodi ya wagonjwa majeruhi hosipitali ya Mkoa wa Arusha Mount Meru alikolazwa,Neema ameelezea tukio hilo kuwa limetokea juma lililopita baada ya kuitikia mwito wa jirani yake Tatu Msuya uliomtaka afike nyumbani kwake kwaajili ya kumsaidia uangalizi wa familia yake kutokana na kuhitajika msibani na ndipo alipomjeruhi vibaya kwa kumwagia maji ya moto.Neema Teti-Majeruhi
Muuguzi wa zamu katika hospitali ya Mount Meru,Neema Bayo amesema majeruhi huyo aliletwa hospitalini hapo akiwa katika hali mbaya lakini hali yake imezidi kuimarika baada ya kupatiwa matibabu na jopo la madaktari hospitalini hapo. Nae Muuguzi wa wodi ya majeruhi mount Meru Hospitali Bi.Neema Bayo amesema matukio kama hayo yakizidi kushamiri katika maeneo mbalimbali
nchini,bado inaelezwa kuwako kwa ugumu wa kutoa taarifa katika vyombo vya sheria kutokana na wahusika kuwaficha wahalifu mara wanapotoka hospitalini
Afisa wa dawati la jinsia mkoa wa Arusha Maria Maswa akizungumza wakati alipotembelea waathirika wa matukio ya unyanyasaji wa kijinsia katika hospitali ya mount Meru,amesema yanapotokea matukio hayo,walengwa wamekuwa wagumu kutoa ushirikiano kwa madai ya kumaliza swala hilo kinyumbani hatua inayochochea ukuaji wa matatizo hayo.Maria Maswa-Afisa Dawati la Jinsia Mkoa wa Arusha Bi. Maria Maswa alisema "Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limeeleza kuwa linaendelea na msako dhidi ya Mama Tatu Msuya anayedaiwa kutekeleza kitendo hicho; pia aliongeza kuwa jumla ya kesi 507 zimeripotiwa kati kipindi cha mwezi november 2012 mpaka sasa. 
Picha zote na Gadiola Emanuel wa Wazalendo 25 Blog.

Rihanna aandika historia nyingine kubwa kimuzikiRihanna amefanikiwa kuandika historia nyingine kimuziki kufuatia wimbo alioshirikishwa Eminem, Monster kuwa wimbo wake 13 kukamata nafasi ya kwanza kwenye chart za Billboard.
Akiwa na nyimbo 13 zilizokamata nafasi ya kwanza, amewazidi Madonna, Stevie Wonder na Whitney Houston na amefungana na hayati Michael Jackson.
Wanaoongoza kwa kuwa na nyimbo nyingi zilizoshika nafasi ya kwanza ni the Beatles walioingiza nyimbo 20 na kufuatiwa na Mariah Carey mwenye nyimbo 18.

Video: Mkalimani feki wa viziwi kwenye kumbukumbu ya Mandela ajitetea, asema aliona malaika wakiingia uwanjani akachanganyikiwaMkalimani anayeshutumiwa kwa kudanganya alama za viziwi wakati akitafsiri hotuba za viongozi mbalimbali wa dunia akiwemo Rais Barack Obama wa Marekani kwenye hafla ya kumbukumbu ya Nelson Mandela, Alhamis hii amesema alikuwa akiona malaika wakiingia kwenye uwanja huo wa mpira wa FNB na kwamba amekuwa akisumbuliwa na tatizo la akili.
Thamsanqa Jantjie amehojiwa na shirika la habari la The Associated Press aliloliambia kwamba mauzauza hayo yalianza alipokuwa akitafsiri na kwamba alijaribu kutopanic kwasababu polisi wenye silaha walikuwa karibu yake.
“Kilichotokea siku hiyo, niliona malaika wakiingia uwanjani. Nilianza kugundua kuwa tatizo lilikuwa hapa. Na tatizo, sijui shambulio la tatizo hili, litakujaje. Wakati mwingine huwa nakua katili sehemu hizo. Huwa naona vitu vinavyonifukuza,” alisema Jantjie.
“Nilikuwa kwenye wakati mgumu sana,” aliongeza. Na kumbuka watu hao, Rais na kila mtu, walikuwa na silaha, kulikuwa na polisi wenye silaha pembeni yangu. Ningeanza kupanick ningezusha tatizo. Nilitakiwa kukabiliana nalo ili nisiiabishe nchi yangu.”
Aliongeza kuwa aliwahi kulazwa hospitali ya wagonjwa wa akili kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Serikali ya Afrika Kusini imekiri kuwa kulifanyika makosa katika kumchukua Jantjie kwa kazi hiyo.
Naibu waziri wa Wanawake, Watoto na Walemavu, Hendrietta Bogopane-Zulu alisema maafisa wa serikali wamejaribu kufuatilia kampuni iliyompa kazi Thamsanqa Jantjie lakini wamiliki wa kampuni hiyo wameingia mitini.
Aliwaomba radhi watu wote wenye ulemavu wa kusikia na kusema kuwa uchunguzi unafanyika kubaini ni vipi Jantjie alikuwa amechukuliwa kufanya kazi hiyo.
Aliongeza kuwa kampuni hiyo ilitoa huduma chini ya kiwango na kwamba ujira waliomlipa mkalimani huyo kilikuwa kidogo mno. Mkalimani huyo alilipwa dola 85 tu.
AP waliomuonesha Jantjie video inayomuonesha akitafsiri kwenye hafla hiyo na kusema hakumbuki  chochote.
“I don't remember any of this at all.

Surprise: Beyonce aachia album mpya kwa kushtukizaWeekend hii, Beyonce ameachia album yake ya 5, iliyopewa jina lake mwenyewe na inapatikana itunes pekee yake.

Katika album hiyo, Beyonce amewashirikisha wakali akiwemo mumewe, Jay Z, Drake, Frank Ocean na mwanae Blue Ivy.
Hiyo ni album yake ya kwanza tangu mwaka 2011 alioachia albam yake ya nne, "4".
Beyonce ina jumla ya nyimbo 14. Cha kuvutia ni kuwa kila wimbo kwenye albam hiyo ina video yake ambayo nayo inapatikana iTunes.
Hizi ni nyimbo zilizopo kwenye "Beyonce":
1. Pretty Hurts
2. Haunted
3. Drunk In Love (feat. Jay Z)
4. Blow
5. No Angel
6. Partition
7. Jealous
8. Rocket
9. Mine (feat. Drake)
10. XO
11. Flawless (feat. Chimamanda Ngozi Adiche)
12. Superpower (feat. Frank Ocean)
13. Heaven
14. Blue (feat. Blue Ivy) 

Label ya Baby Madaha, Candy n Candy yakumbwa na mgogoro, polisi waingilia katiMigogoro kwenye label ya Kenya inayomsimamia Baby Madaha imeonesha kutengeneza makazi ya milele kila anaposainishwa msanii mpya. Ikumbukwe kuwa wasanii wa zamani wa label hiyo walianza kulalamika kuwa CEO wa label hiyo, Joe Kariuki alikuwa akimpendelea mno Baby Madaha na kuwaacha wao wakisaga miguu tu.
Na sasa baada ya kusainishwa msanii mpya wa Nigeria, Lil Gee na kuachia wimbo mpya na kisha kutaka afanyiwe video, vijana wa zamani wameanza kulalamika tena.
Mmoja wao ni Dazlah Kiduche, aka ‘Dazlah’ ambaye hiyo haijamuingia kichwani kwakuwa anashangaa iweje mgeni apate video wakati yeye aliyeanza kuachia wimbo wake “Bangereba” akiwa hana video bado. Wasanii hao walijikuta wakiingia kwenye ugomvi mkubwa uliofanya hadi polisi waitwe kwenye ofisi hizo kusuluhisha mambo.
Chanzo kilichoongoea na mtandao wa Niaje wa Kenya kimesema kuwa CEO Joe Kariuki bado hajaamua video ya nani ianze kutoka.

Rich Mavoko atolewa machozi na Mama Sharo anayedai kudhulumiwa haki za mwanaeMuimbaji wa Roho Yangu, Rich Mavoko amemtembelea mama mzazi wa marehemu Sharo Milionea huko wilayani Muheza Tanga.

Mavoko ameshare picha akiwa na mama mzazi wa msanii huyo aliyefariki November mwaka jana inayoonesha akiwa kwenye simanzi zito kutokana na alichokuwa akisimuliwa na mama huyo.
"Muda mwingine wasanii tunahitaji tukumbuke wenzetu walio tangulia tena kwa kuwa enzi ata kwa kuwatembelea ndugu zake coz kuna vitu vinauma sana ukielezewa hapa alikuwa ana nielezea sharo baada ya kufa haki zake nyingi hajui zipo zinaenda wapi na mambo mengi yanayo muhusu marehem sharo kiukweli ili niuma... pole sana mama angu binadamu ndivyo walivyo,” ameandika Mavoko.

Watu 41 akiwemo waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa wanusurika kifo baada ya ndege waliyopanda kupasuka matairi
Abiria 37 na wafanyakazi 4 wa ndege ya Precision Air wamenusurika kifo baada ya ndege waliyokuwa wamepanda kupasuka matairi wakati ikitua katika uwanja wa ndege wa Arusha leo majira ya mchana.

Waziri mkuu mstaafu ambaye ni mbunge wa Monduli, Edward Lowassa alikuwa miongoni mwa abiria wa ndege hiyo waliokuwa wakisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Arusha.  
Shirika la ndege la Precision Air limetoa tamko rasmi kwa umma, ambapo limeeleza kuwa watu wote waliokuwa kwenye ndege hiyo wako salama.

Ivo Mapunda kuichezea rasmi Klabu ya Simba

Baada ya uongozi wa Klabu ya Gor Mahia ya Kenya kuweka wazi mpango wa kumuongeza mkataba mlinda mlango wao shujaa wa kupangua michomo ya penalti, Ivo Mapunda, uongozi wa klabu ya Simba nao umesema umeshafanya mipango ya kumsainisha mkataba nyota huyo.

Uongozi wa mabingwa wa Ligi Ku ya Kenya -- Gor Mahia ulikaririwa juzi ukieleza kuwa utambakisha kipa Mapunda kwa gharama yoyote.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala, ambaye alikuwa nchini Kenya juzi, ameiambia NIPASHE kuwa Mapunda alitarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia 'Wanamsimbazi', na kwamba tayari ameshatanguliziwa shilingi million 15.

"Tayari tulishamkabidhi mke wake shilingi milioni 15 jijini Dar es Salaam jana (Jumatano) kabla ya kuja huku (Nairobi)," alisema Mtawala.

Katibu Mkuu huyo alisema wamelazimika kuja jijini hapa kumsajili baada ya kusikia kuwa klabu yake ya Gor Mahia ina mpango wa kumwongeza mkataba mpya.

Kipa huyo amejipatia umaarufu nchini hapa kwa ushujaa wake wa kupangua mikwaju ya penalti. Katika mchezo wa jana wa Kombe la Chalenji kutafuta mshindi wa tatu kati ya Zambia (Chipolopolo) na Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), Mapunda alidaka penalti mbili kati ya nane ambazo mabingwa hao wa zamani wa Afrika -- Chipolopolo walipiga.

Kutua kwa Mapunda Simba kutaisaidia timu hiyo iliyopo katika mgogoro mkali wa uongozi kwani kuanzia msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, hakuna timu itakayoruhusiwa kuwa na kipa wa kigeni ili kukidhi matakwa ya Azimio la Bagamoyo.
Source:Nipashe

No comments: