Manchester United imeendelea kuwa na msimu mbaya baada ya kupigwa bao 1-0 katika mechi iliyomalizika muda mfupi uliopita kwenye Uwanja wa Old Trafford wakati ilipokuwa ikipambana na Newcastle United katika mchezo wa Premier.
Kipingo hicho ambacho ni cha tano kimeifanya Man United iwe na msimu mbaya kuliko yote ndani ya kipindi cha miaka 20 iliyopita, ambapo Jumatano iliyopita, United ilifungwa bao 1-0 na Everton katika ligi hiyo. Bao la Newcastle lilifungwa na Yohan Cabaye katika dakika ya 61. |
Rapper Drake wa Young money amesema amehamasika kuisaidia shule ya hatari sana nchini marekani baada ya kuona taarifa ya shule na mazingira yake kwenye vyombo vya habari.
Drake ametangaza kujenga studio ya kurekodi muziki kwenye shule hio ya sekondari inayoitwa Strawberry Mansion iliyopo Philadelphia, Pennsylvania. Shule inawanafunzi 400 na imetajwa kama shule ya hatari sana Nchini Marekani kwa mujibu wa ABC News. "Nataka kuwajengea studio ya muziki sababu nawapenda, hii ni nafasi yenu ya kufanya kitu na maisha yenu, muwe na maisha mazuri baadae. Kama mtaitumia nafasi vizuri nitafurahi pia" Alisema Drake kwenye mahojiano. Kwenye interview ya wanafunzi hao, Walisikika wakisema , Hatuna mategemeo na hatuna cha kufanya shuleni na mitaani, Tutaishia pabaya kama kaka na dada zetu. |
Kiongozi mpinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Nelson Mandela atazikwa mnamo siku ya
Jumapili, December 15, nyumbani kwo Qunu, na ibada ya kumuombea itafanyika kwenye uwanja wa Johannesburg mnamo siku ya Jumanne, December 10, Rais Jacob Zuma ametangaza. Mwili wa Mandela utakuwa kwenye majengo ya Serikali ndani ya Pretoria kuanzia siku ya Jumatano, December 11, mpaka siku ya mazishi, na Jumapili hii ya December 8, itakuwa ni siku ya kitaifa ya kumuombea. |
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) Jerôme Valcke, amesema kama
ikitokea kwenye mechi wakati inaendelea na kukawa na joto kali, michezo kwenye baadhi ya mechi za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil inaweza kusimamishwa mara moja au zaidi ili kuwaruhusu wachezaji wapumzike kutokana na joto. "Kila mechi itakuwa na mratibu, daktari na refa wa mchezo. Watu hawa watatu watachukua hatua za msingi kuhakikisha mazingira yanayokubalika na watakuwa na amri ya kusimamisha mechi kwa ajili mapumziko", alisema Valcke, ambaye siku mbili zilizopita amekiri pia kwamba michuano hiyo ya Brazil 2014 itakuwa ni ya Kombe la Dunia lenye joto kali. |
Mcheza filamu za kibongo Wema Sepetu ametuma picha ya mpenzi wake wa zaman mwanamuziki Diamond Platnamu kwenye akaunti.yake ya instagram na kuandika,
“ i jus happen to love dis picture“ baada ya kuweka picha hiyo mashabiki wameanza kumsifia uku wakimponda mpenzi Penny ambae anaaminika ndio mpenzi wa Diamond kwa sasa Website hii imepitia akaunti ya Diamond na kukuta picha ile ile aliyoweka Wema ikiwa na maneno kuonesha kua usiku wa jana msanii huyu alikua kwenye sherehe ya kuzaliwa mrembo wa zamani wa Tanzania Jackline Ntuyabaliwe. |
|
Hivi majuzi aliripotiwa kambini na muendesha baiskeli (bodaboda) kwamba alimkodi akamwambia ampeleke Usagara maeneo akanywe bia mara bodaboda anashangaa anaelekezwa mitaa isio na dalili yeyote ya kuuzwa bia..! Ghafla wakafika kwenye nyumba flani wakamkuta dada na mpenzi wake wametulia nje kwao wanapunga upepo, Ndipo Msanii aliposhuka kwenye baiskeli nakuanza kumporomoshea matusi ya nguoni yule dada na mpenzi wake huku akijitapa kwamba yeye ana ukimwi na kashamuambukiza huyo mwanamke kwahiyo huyo mpenzi wake mpya ajiandae kufa kwa gonjwa hatari la ukimwi...!, Dada huyo ambaye alikuwa mpenzi wake kweli enzi hizo lakini kwasasa walishatengana aliamua kupiga simu kwa mmoja kati ya wasanii waVITUKO SHOW na kutoa malalamiko yake usiku huohuo Akakiri kutokurudia sualahilo Wasanii wenzake baada ya kufikishiwa taarifa hiyo na muendesha baikeli pamoja na simu iliyopigwa na dada huyo wamkalisha chini tena Kazi chini kama kawaida na kumuonya, Akakiri kutokurudia suala hilo. Amakweli siko la kufa halisikii dawa..! Cha ajabu jana kalewa tena na kuenda kumtukana dada huyo tena, Dada akaenda kuripoti polisi leo wamemtia mbaroni Kazi A.k.a Kijeba yupo kituo cha polisi makorora mkoani Tanga anasubiri kupanda mahakamani Jumatatu tarehe 9- December 2013 kusomewa mashtaka. Fatilia raarifa zaidi hapa katika website yako ya kijajnja masainyotambofu.com. Credit:Masainyotambofu.com |
Ilikuwa ni siku ya furaha sana usiku wa kuamkia leo kwenye sherehe ya kuzaliwa Miss Klynn aka MAMA MAPACHA pande fulani hivi jijini Dar es Salaam.
Party hii ilikuwa ni yaaina yake kwani ilikuwa ni kwa watu walioalikwa tu, kama unavyoona picha jinsi walivyokuwa safi na namuona Boss Mengi akiwa mwenye nyuso ya furaha baada yakutizama show kali ya Diamond. |
"Kila jambo lina muda na wakati wake.. usilazimishe kurudisha saa nyuma wakati ulishachelewa....kubali kushindwa na jipange upya ili upate kushinda siku nyingine..
thanx Wastara kwa kufanya kazi yangu pamoja na mimi kupitia kampuni yako ya Wajey film usivunjike moyo kwa mane no ya viblog uchwara na maneno ya binadamu wasiokua na akili timamu" Mr Bond.
|
Stori: Denis Mtima na Chande Abdalla
MTOTO Kulendya Rojason (3) ambaye siku za nyuma aliwahi kuripotiwa na vyombo vya habari kuwahi kulelewa na mbwa baada ya wazazi wake kumtelekeza yeye na ndugu zake, bado anazidi kuteseka kwa kukosa msaada wa chakula. Akizungumza kwa niaba ya mtoto huyo nyumbani kwao, Nyerere B, Mabatini Mwanza, dada wa mtoto huyo, Recho Rojason (18) alisema kuwa mdogo wake bado anateseka kwani hapati malezi ya kutosha kutokana na maisha yao kuwa magumu. Recho alisema kuwa, maisha yao yamekuwa magumu baada ya mama yake kuwatelekeza na kuolewa na mwanaume mwingine huku akimwacha baba yao ambaye ametopea kwenye ulevi na kushindwa kutoa msaada wowote. Recho ambaye ni hausigeli anayefanya kazi kwa ujira mdogo maeneo ya Mwanza Mjini, alisema wamekuwa wakipata fedha kidogo kutoka Halmashauri ya Jiji ambapo hazikidhi mahitaji yao na kuwaomba watu wajitokeze kuwasaidia. Aliomba msaada wa kupata fedha kwa ajili ya matibabu, masomo na malazi kwa kuwa yote hayo ni mahitaji yao yeye pamoja na wadogo zake watano akiwemo Kulendya. Akizungumzia sakata hilo jirani anayeishi na watoto hao, Chausiku Ibra alisema kuwa watoto wa familia hiyo wamegeuka machokoraa kutokana na huduma hafifu na kuongeza kuwa mtoto wa mwisho (Kulendya) ndiye yupo hatarini zaidi. “Huyu mtoto wa mwisho ndiye aliye hatarini zaidi kwa kuwa tangu alivyokuwa mtoto alikuwa akiletewa chakula na kutunzwa na mbwa. Mpaka anakuwa hivi ni jambo la kumshukuru Mungu kwa kweli. Watoto hawa wanahitaji msaada jamani,” alisema jirani huyo. Waandishi wetu walijionea, nyumba wanayoishi watoto hao ambayo imeonekana kuharibika kwa kiasi kikubwa sehemu za paa na kuta jambo ambalo ni hatari kwa watoto hao huku taarifa zikieleza kuwa, baba wa watoto hao, Rojason Ernest amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando akiuguza nyonga baada ya kuanguka akiwa anatokea kilabuni. Kama umeguswa na unataka kuwasaidia watoto hao, wasiliana nao kwa namba ya jirani yao, Chausiku: 0767445683. Imeandikwa na Global Publishers |
Mtangazaji wa kipindi cha Maskani cha 100.5 Times Fm, Gardner G. Habash aka Captain ameelezea jinsi anavyomkumbuka rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
Captain G. Habash ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa aliwahi kulitembelea gereza alilofungwa Mandela , Robben Island huko Afrika Kusini, na kushuhudia chumba alichokua akishikiliwa.
“Nimewahi kutembea South Africa na nikafika kwenye mji wa Cape Town, na kule niliwahi kutembelea sehemu moja ambayo ni gereza la Robben Island, alipowahi kufungwa na kushikiliwa Nelson Mandela kwa muda mrefu sana. Pale nilipata nafasi ya kuona kile chumba ambacho alikuwa akilala Mandela, na mazingira magumu ambayo alikuwa akiishi,” amesimulia Gardner.
“Tulipata hadithi pia ya jinsi ambavyo alikuwa akiteseka katika harakati za kufanya ukombozi wa kupigana vita dhidi ya ubaguzi wa rangi.” Gadner amesema pamoja na kushuhudia sehemu ya mazingira magumu na kusimuliwa mateso aliyoyapata Mzee Mandela, alishangaa kuona baada ya kutoka alikubali kusamehe na kusahau.
“Lakini kitu kikubwa ambacho nilistaajabu ni vile ambavyo alipitia Mandela, lakini baada ya kutoka akakubali kusamehe na kusahau kila kitu na kuunda taifa moja lenye manufaa kwa wa-South Africa wote, taifa ambalo aliliita Rainbow Nation kwa maana kwamba ni taifa la watu wa rangi zote. Taifa ambalo litakuwa ni kwa ajili ya wa-South Afrika pamoja na maslahi ya wa-South Africa,” ameongeza Gardner.
Amesema matendo ya Mandela yanamtofautisha na viongozi wengine wengi duniani, na kwamba anaamini kwamba yeye ndiye kiongozi bora zaidi kwa karne hii, mwenye hekima, busara pamoja na karama ya Mwenyezi Mungu.
“Naungana na South Africa, Afrika nzima pamoja na dunia kutoa heshima zangu kwa Mzee Nelson Mandela pamoja na familia yake.”
Source!Tovuti ya Times fm.
|
Justin Timberlake ni mmoja wa wamiliki wa mtandao wa Myspace baada ya kuwa sehemu ya timu iliyoununua kutoka kampuni ya News Corp kwa gharama ya dola milioni 35.
Timberlake anaumiliki mtandao huo pamoja na kampuni ya matangazo ya online Specific Media.
Msanii huyo ameweka pesa zake mwenyewe ndani ya mtandao huo japo hakuweka wazi ni kiasi gani.
Timberlake ana ofisi yake kwenye kampuni hiyo ya Myspace lakini haendi kazini kila siku kama watu wengine kutokana na kuwa na shughuli zingine za muziki na filamu.
News Corp iliinunua Myspace mwaka 2005 kwa dola milioni 580. Mwaka 2006 Google ilisaini deal la milioni 900 kuuza matangazo kwenye Myspace.
|
Baada ya kuwavunja mbavu watu kupitia nyimbo zao, John Walker na Ras Lion wameamua kuingia kwenye tasnia ya filamu na kufanya kipindi cha comedy walichokipa jina la ‘Kibombonya’.
John Walker amesema walikuwa kimya kimuziki kwa muda kwa kuwa walikuwa wanajipanga kufanya project yao mpya ya muziki na kushuti comedy yao ambayo imeshakamilika.
“Comedy yetu inaitwa Kibombonya, na wahusika wakuu ni mimi na Ras Lion kama kawaida. Lakini kuna vijana wengine kutokea Arusha wameshiriki. Hii ni comedy ambayo itakuwa ni kipindi endelevu cha TV.” Amesema John Walker.
Ameeleza kuwa wameamua kufanya Comedy seriously kwa kuwa wamekuwa wakishauriwa sana na watu kufanya comedy na wameamua kufuata ushauri hu, kwa kuwa watu wengine wamekuwa wakitumia nyimbo zao kufanyia comedy jukwaani kitu ambacho wao wangeweza kukikamilisha.
Kuhusu lini na kituo gani cha runinga comedy hiyo itakuwa inaoneshwa, Joh Walker amefunguka.
“Bado sasa hivi tuko kwenye maongezi na TV station kama tatu hivi, tutakayoelewana nayo tutaweka wazi sehemu gani itakayokuwa inarushwa.”
|
Afrika na dunia inatarajiwa kushuhudia kitu kipya katika maziko ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela (95) aliyefariki dunia juzi, baada ya kuugua kwa zaidi ya miezi sita.
Serikali ya Afrika Kusini imesema kiongozi huyo ambaye atazikwa Desemba 15, imeandaa mazishi ya kihistoria yanayosemekana yatazidi yale ya Papa John 11. Matukio ya shughuli mbalimbali zinazohusu mipango ya maziko ya kiongozi huyo maarufu yanatarajiwa kushuhudiwa sehemu mbalimbali duniani, tofauti na tukio jingine lililowahi kutokea barani Afrika mbali na kombe la dunia. Rais Jacob Zuma alisema jana kwamba “Mpendwa wetu Madiba atazikwa kwa heshima zote za Serikali. Nimeagiza bendera zote za Afrika Kusini zipepee nusu mlingoti na hiyo itaendelea hivyo hadi tutakapokamilisha mazishi yake. Mazishi ya Mandela yanalinganishwa na yale ya Papa John Paul II mwaka 2005, ambayo yalihudhuriwa na wafalme watano, malkia sita wa falme mbalimbali na marais wapatao 70 na mawaziri kadhaa, wakiwamo wafuasi wake zaidi ya milioni mbili. Yanakadiriwa pia kulingana na maziko ya Winston Churchil aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza mwaka 1965. Marais wote wa Marekani walio hai wanatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo iwapo afya zao zitawaruhusu kusafiri, pamoja na Prince Charles wa Uingereza na hata Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe. Pia watu maarufu wenye urafiki wa karibu na Mandela akiwamo msanii Oprah Winfrey wameshathibitisha kuhudhuria. |
Ni pale mwanaume anapoonyesha tamaa kubwa ya ngono na kulazimisha kukutana kimwili wakati mwanamke aliweka msimamo wa kutokutana
kimwili na mwanaume yeyote mpaka baada ya muda fulani tangu kufahamiana na kuwa wachumba au mpaka pale watakapofunga ndoa. Huu ni mtihani kwa wanawake wengi kwa sababu unawaweka katika wakati mgumu wa kuchagua kuvunja nadhiri waliojiwekea au kusimama imara kwenye msimamo waliyojiwekea kwa ajili yakulinda heshima zao. Swali kwa wanawake: Je unapokabiliwa na mtihani kama huu ni uamuzi gani unaona ni sahihi kwako….? |
Kutokana na makampuni karibu yote ya simu Tz kuwa na huduma hizi za mobile money, Je inapotokea mteja amefariki, makampuni yanawajibika vipi kuhusu kurudisha pesa za mteja wao kwa msimamizi wa mirathi au warithi?
swali hiili linazingatia kuwa wateja wanaoweza kutwa na mauti kwa vyovyote wanaweza kuwa na akiba kidogo kwenye ac zao za mitandao ya simu wanayotumia! Je kuna sheria yoyote ambayo imeweka bayana masuala haya? kwa wenzetu walio kwenye makampuni ya simu tafadhali mtusaidie kwa hili! naomba kuwasilisha kwa mjadala! |
Mabasi ya mwendo kasi 2014 kimara kivukoni. Picha kwa hisani ya Deo Mutta Mwanatanga Basi la kwanza la mradi wa mabasi yaendayo kasi limewasili nchini na kuanza kufanya majaribio katika barabara zilizokwisha kamilika huku mengine yakitarajiwa kuwasili mapema mwaka kesho. Mtendaji mkuu wakala wa mradi wa mabasi yaendayo haraka Bi Asteria lambo amesema basi hilo ni miongoni mwa mabasi madogo yatakayoingia nchini yenye uwezo wa kubeba zaidi ya abiria 40 na makubwa yatabeba abiria zaidi ya 150 na kuwataka wakazi wa jiji la Dar es Salamu kuendelea kuwa na subira na kuwahakikishia mradi huo sio ndoto na adha ya usafiri itapungua mapema mwaka kesho. Nao baadhi ya wakazi wa jiji walioshuhudia gari hilo wameelezea kufurahishwa na kuanza kuwa na imani na serikali yao ambapo wamesema kama mradi huo utakamilika kwa muda uliopangwa utakuwa faraja sana kutokana na adha kubwa ya usafiri wanayokumbana nayo huku wakitoa wito kwa mamlaka husika kupanga mikakati ya kupunguza nauli za mabasi hayo pindi yatakapoanza kufanya safari zao. |
NAPENDA KUTOA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWA HAWA WAFUATAO 1.MAMA VERONIKA NDUNGURU 2.BABA LAURENT NSUHA WADOGO ZANGU 1.MONICA ROSES NSUHA 2.PHILIPO NERY NSUHA 3.DORAH NSUHA 4.BERTHA NSUHA 5.DOMMY NSUHA BILA KUWASHAU WATU WANGU WA KARIBU YAFUATAO: 1.DENIS MPAGAZE 2.ALLEN MOSHI 3.NESTRO NJAWIKE 4.ATHANAS SING'AMBI
Sunday, 8 December 2013
MANCHESTER WANATAMANI SIR ALEX FUGERSON ARUDI TENA.ONA KILICHOWAKUTA TENA KWENYE UWANJA WAO WA NYUMBANI.AIBU.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment