advert

http://

Tuesday, 10 December 2013

Hakuna mahali pa kukanyaga’ msibani kwa Mandela

.

Makazi ya Rais wa Kwanza mzalendo wa Afrika Kusini yaliyopo katika Mtaa wa Laa namba 12,
Houghton ambako ndiko alikokuwa hadi alipokutwa na mauti, ni kama hapaingiliki kutokana na wingi wa watu, magari na vyombo vya habari kutoka sehemu mbalimbali duniani ambavyo vimeweka kambi katika eneo hilo, usiku na mchana kufuatilia safari ya mwisho ya kiongozi huyo. 
Anga la mtaa huo na sehemu za jirani, limehanikizwa na sauti nyingi za nyimbo zikiongozwa na Wimbo wa Taifa wa Afrika Kusini ‘Nkosi Sikeleli Afrika’ (Mungu Ibariki Afrika), ukifuatiwa kwa zamu na nyimbo za kidini na zile za asili ambazo zinasifu ushujaa wa Mandela.
Katika lango la kuingia kwenye makazi hayo ya Mandela, kuna maombolezo ya aina yake kwani yameambatana na kitu ambacho kwa macho kinaonekana kama shamrashamra kwa nyimbo za sifa na kufurahia kile Waafrika Kusini wanachokiita kazi nzuri ya kutukuka ya Mandela aliyoifanya katika umri wa miaka 95 ya uhai wake.
Mwandishi wetui alitembelea makazi hayo ya Mandela jana na kushuhudia umati mkubwa wa watu wakifika nje ya nyumba yake kwa ajili ya kuomboleza; wakiweka mashada ya maua, mishumaa na kadi zenye ujumbe wa pole kwa familia yake. 
Miongoni mwa waliokuwapo katika eneo hilo ni Mtanzania, Christer Mwageni na watoto wake; Sabina na Faraja.
Mwageni alisema: “Kwa jinsi hali ilivyo, huwezi kukwepa kuwa mwombolezaji, mimi na wanangu tulikuja hapa kutembea tu kwa siku tatu hivi lakini tumejikuta tukishiriki msiba na hata kama tungekuwa hatutaki kushiriki, uhalisia unatulazimisha”.
“Kweli tuna mengi ya kujifunza, inaonekana msiba huu wa Mzee Mandela umewaunganisha zaidi Waafrika Kusini, maana wote bila kujali rangi wala kingine chochote, wanaonekana kuomboleza kwa dhati kutoka mioyoni kabisa.”
Katika eneo hilo la Houghton, ulinzi umeimarishwa na polisi wako kila kona na wamekuwa wakiwaelekeza waombolezaji na watu wengine njia sahihi za kufuata hadi kuyafikia makazi ya Mzee Mandela kutoka na barabara nyingi za kuingia katika eneo kufungwa na nyingine kugeuzwa maegesho ya magari ya waombolezaji.
Kwa ujumla, pilikapilika ni nyingi, lakini katika lango kuu la kuingia makazi ya Mandela, ulinzi ni mkubwa na hakuna anayeruhusiwa kulikaribia isipokuwa wanafamilia, vingozi wa Serikali na watu wengine wenye shughuli maalumu.

Soweto, Mandela Square
Hali kama hiyo ipo katika makazi yake ya zamani Mtaa wa Vilakazi Na: 8115, Orlando Magharibi, Soweto ambako kuna pilikapilika nyingi zinazoyahusisha makundi ya watu kutoka ndani na nje ya Afrika Kusini.
Mandela aliishi katika Mtaa wa Vilakazi kabla ya kukamatwa na kuwekwa kizuizini na alirejea katika nyumba hiyo miaka 27 baadaye alipoachiwa huru na kuishi humo kwa siku kumi na moja kabla ya kuhamia katika nyumba ya aliyekuwa mkewe, Winnie Mandela katika eneo hilohilo la Soweto.
Kama ilivyo Houngton, katika eneo hilo pia ulinzi umeimarishwa na baadhi ya njia zimefungwa kutokana na wingi wa watu na magari. Vyombo vya habari kutoka kila pembe ya dunia navyo vipo vikiendelea kufuatilia maombolezo hayo.
Katika nyumba ya Soweto ambayo sasa ni makumbusho ya Mzee Mandela, idadi kubwa ya watu wanafurika kujifunza historia ya kiongozi huyo na nje vipo vikundi vinavyoimba nyimbo za maombolezo na kumsifu Mandela kwa ushujaa wake.
Eneo la tatu ni Mandela Square lililopo katika Jiji la Sandton, Johannesburg ambako kuna sanamu kubwa ya kiongozi huyo yenye urefu wa mita sita kwenda juu, likimwonyesha katika hali ya kucheza muziki. Iliwekwa katika eneo hilo, Machi 31, 2004.
Katika eneo hilo, pia ulinzi umeimarishwa na askari wanalazimika kusimamia jinsi watu wanaovyoingia na kutoka. Watu wamekuwa wakisimama katika msitari mrefu kupata fursa ya kupiga picha katika sanamu hiyo yenye uzito wa tani mbili na nusu (kilo 2,500).
Pembezoni mwa sanamu hiyo, kama ilivyo Houghton na Malakazi, limetengwa eneo maalumu kwa ajili ya watu wanaoomboleza kuweka maua, nembo, nyaraka na mishumaa.
Maombolezo ya kifo cha Mandela yanaingia katika siku ya nne leo na yataendelea hadi Jumapili ijayo ya Desemba 15 wakati kiongozi huyo atakapozikwa kijijini kwake Qunu, Mthatha Mkoa wa Eastern Cape.


MADAM, Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ amesema anakumbuka vitu vitatu muhimu alivyokuwa akifanyiwa na marehemu baba yake, Abraham Sepetu.
 

Akizungumza na paparazi wetu, Wema alitaja matukio hayo ambayo ni kuona simu ya baba yake ikimpigia katika simu yake, jinsi alivyokuwa akimbembeleza na kubwa zaidi ni uwepo wake pia 
kwa jumla.
 
Wema (katikati) akiwa na mama yake pamoja na marehemu baba yake enzi za uhai wake.

“Maisha yangu yote nitakumbuka vitu vitatu ninavyovikosa baada ya kifo cha baba yangu, kwanza uwepo wake, kuona simu yake pindi anipigiapo, na alivyokuwa akinibembeleza. Nitamkumbuka sana baba yangu,” alisema Wema.

Huddah Monroe
Uhasama mkali unaozidi kuchemka kati ya rapa mbishi CMB Prezzo na 'msocialite’ Huddah Monroe wameamua kuanikana wazi na kuzitoa siri zao za ndani kwenye mtandao.


Tatizo nzima lilianza pale Huddah alipomkashifu Prezzo kwenye akaunti yake ya Instagram akimtaja kuwa mtu aliyeishiwa na anayependa kudekezwa sana.
Kama kawaida yake 'king wa maBling’ alijibu mpigo kwa kumwita Huddah kiruka njia asiyejielewa na ambaye yupo tayari kutumiwa na kila mtu.
Kipusa huyo naye hakuchoka kumjibu akisema kwamba kheri kuwa kiruka njia kuliko kuwa mtu wa kutegemea mamake hata katika umri mkubwa kama wake Prezzo
Majibizano yalizidi kuwa makali huku wawili hao wakitupiana cheche zaidi yenye soni kwenye akaunti zao mbalimbali za mtandaoni ikiwemo Twitter.

Letu ni jicho tu maana hatujui picha hii mbaya kati ya wawili hawa itaishia wapi, au labda ndio suala nzima la kusaka umaarufu.

nicki-minaj-birthdayFirst lady wa label ya YMCMB Nicki Minaj amesherekea birthday yake akitimiza miaka 31 na mafanikio ya kujivunia kwenye kazi yake ya muziki.

Party hiyo ikifanyika huko L.A na restaurant nzima ilibadilika rangi yake na kuwa ya pink maalum kwa ajili ya party ya Minaj ambayo ilihudhuliwa na Lil Twist,Safaree boyfriend wa Nicki Minaj na watu wengine.
Nicki aliletewa keki mbalimbali pamoja na stripper pole maalum kwa ajili ya party hiyo.
nicki-minaj-birthday2
nicki-minaj-birthday-3
nicki-minaj-birthday-4
nicki-minaj-birthday-5
nicki-minaj-birthday-6
nicki-minaj-birthday-7
nicki-minaj-birthday-8
nicki-minaj-birthday-9




Msanii maarufu wa Marekani Kelly Rowland, ametinga uwanja wa fisi Manzese Dar es salaam jana jioni baada ya kusikia sifa za maeneo hayo ya Uswahilini tangu akiwa USA. Msanii huyo ametua nchini kwa tiketi ya MTV kupitia taasisi yake inayojishughulisha na kampeni za kupambana na Ukwimwi (Staying AliveFoundation) ya nchini Marekani, Kelly akiwa balozi wake. Akiwa Uwanja wa Fisi, ambako kunasifika kwa ufuska wa kupindukia na rate kubwa ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa wasichana wadogo, Kelly alitembelea NGO ya EYG (Elizabeth Youth Group) inayojishughulisha na kutoa misaada ya elimu ya HIV/AIDS, uchangudoa, ulevi pamoja na uvutaji bangi kwa vijana nchini. 

jkuhuruRais Jakaya Mrisho Kikwete leo ameongoza maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanganyika uliopatikana Desemba 9, 1961.

Miaka 52 imetimia tangu Tanganyika (sasa Tanzania), kupata uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa Kiingereza, Desemba 9, mwaka 1961.
Maadhimisho haya yamefanyika uwanja wa uhuru hapa Dar es salaam,Rais Jakaya Kikwete amekagua gwaride la vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama ambavyo pia vimetoa heshima kwa kiongozi huyo kwa mwendo wa pole na haraka.kikosi cha anga pia kimetoa heshima zake na burudani mbalimbali ikiwamo ngoma na michezo ya halaiki. Sherehe hizi zimehudhuriwa na wageni mbalimbali waalikwa wa ndani na nje ya nchi, wakiwamo mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Katika maadhimisho haya kwa mwaka jana, yaliyohudhuriwa na viongozi 14 wa kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Rais Kikwete aliwataka Watanzania kujivunia na kuyaenzi mafanikio ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yaliyopatika tangu nchi ilipopata uhuru. 

Tundaman asema alimlazimisha Madee kuacha kurap ili apate shows nyingi kama yeye

Tundaman wa Tip Top connection amesema kuwa alichangia kwa kiasi kikubwa kumbadili mwana familia mwenzake wa Tip Top Connection Madee kuacha kurap na kuimba ili aongeze kipato zaidi.

Tundaman amefunguka katika kipindi cha Bongo Dot Home cha 100.5 Times Fm, alipokuwa akifanya mahojiano na Jabir Saleh aka Kuvichaka na Dj K_U.
Tunda amedai kuwa hakupenda kumuona Madee akiendelea kukaa wakati yeye anapiga shows nyingi mikoani, hivyo akamlazimisha kubadilika ili naye apate mashavu zaidi.
“Madee mimi nimemlazimisha asilimia mia, hebu acha kule njoo huku. Ndio maana umesikia Pombe yangu, umesikia Tema Mate Tuwachape. Nimembadilisha mimi kutokana na kuona mwanangu mimi naenda mkoani kila siku nabeba begi yeye mwanangu yuko nyumbani tu. Nikaona kwa nini abaki nyumbani wakati mimi Tip Top chama moja?” Amesema Tundaman.
Ameelezea kuwa baada ya kukubali ushauri wake na kubadilika siku hizi ana mfululizo wa shows.
“Sasa hivi kila wikendi ukimpigia simu Madee ujue haumkuti, yuko mkoa. Zamani ilikuwa kila siku yuko maskani pale.” Amefunguka Tundaman.
Kipindi cha Bongo Dot Home kinakuwa hewani kupitia 100.5 Times Fm kila Jumamosi, kuanzia saa kumi kamili jioni hadi saa moja kamili.
Unaweza kusikiliza Online kupitia tovuti hii, bofya sehemu iliyoandikwa ‘Listen’.
Credit:Times fm.

 Rais Kikwete awashauri wanaopanga kulipa kisasi wakipata madaraka, kuiga mfano wa Mandela

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amewashauri watu wanaopanga kulipa kisasi pindi watakapopata madaraka kuachana na mawazo hayo.

Rais Kikwete ametoa ushauri huo wakati akitoa hotuba yake kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanzania Bara, ambapo ameelezea mengi mazuri aliyoyafanya rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela na kuwataka viongozi wa Tanzania kuiga mfano wa maisha yake ikiwa ni pamoja na kusamehe na kusahau bila kulipa kisasi.
“Najua kuna wengine hapa wamepanga kulipa kisasi, wanasema nikipata watanikoma.” Amesema rais Kikwete na kuwataka waache yaliyopita yapite na kuendelea kuganga yajayo, “acheni kulipa kisasi.” Rais Kikwete amesisitiza.
Hotuba ya Rais Kikwete ilijikita zaidi katika maisha ya mzee Nelson Madiba Mandela, katika kuungana na Afrika Kusini kuomboleza kifo cha kiongozi huyo shupavu na kutoa mfano wa jinsi viongozi wa Afrika wanapaswa kuiga mfano wa uongozi.

Mimi ni Msichana wa Miaka 26 ..uwezi amini mpaka sasa sijawahi guswa na Mwanaume hata mmoja kwa maana hiyo nipo Bikira Kabisa...


Mimi ni Mwalimu wa Shule ya Msingi moja hapa Dar ..Wenzangu nikiwaambia hawaamini kabisa kuwa mpaka umri huu nipo Kigoli wengine wanasema eti nina matatizo..

NAPENDA KUSEMA HAYA

"With the influence of sex almost everywhere in the world of today I will still remain a virgin until my wedding night. It is the only respect I can reward my body. And this way I cannot worry about sexual transmitted diseases and unwanted pregnancies.

I believe that I am not abnormal as others may think. I am physically and mentally fit. I am just keeping myself clean."
Jesca. 


Amini Usiamini Wachina sasa Wameamua kuwekeza mpaka kwenye Ukahaba , Kama unataka kushuhudia hilo basi tembelea hotel za hapa dar zilizopo katika fukwe za bahari ya hindi ukajionee wadada wa kichana wana vyouza mapenzi kama karanga...Bei zao ni kuanzia 20,000 mpaka 60,000 .....Dahhhh 

Mkutano wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willbroad Slaa uliofanyika Uwanja wa Kiganamo, Kasulu Mjini leo umevunjika baada ya polisi kupiga mabomu ya machozi wakikabiliana na vijana waliorusha mawe kupinga mkutano usiendelee. Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, vijana hao wanadaiwa kuwa kati ya 10-15 ambao walirusha mawe baada ya wananchi kuwafukuza wakitaka kuwapiga wakipinga kitendo chao cha kupiga kelele ili mkutano usiendelee ndipo polisi walianza kulipua mabomu ya machozi na mkutano kuvunjika.

Credit:http://www.udakuspecially.com/2013/12/chae.html


Stori:  Issa Mnally na Richard Bukos
MREMBO wa haja ambaye jina halikupatikana amenusurika kubakwa na wanaume baada ya kuvaa kivazi kilichoacha wazi sehemu kubwa ya maungo yake nyeti.



Tukio hilo lilijiri sehemu yenye mkusanyiko mkubwa, Kariakoo jijini Dar ambapo mrembo huyo alikuwa kwenye ‘shopping’ kwa ajili ya sikukuu ijayo ya Krismasi.

Likiwa linarandaranda maeneo hayo, Ijumaa Wikienda lilinasa laivu tukio hilo ambapo mrembo huyo alivuliwa nguo hadharani na kuacha ‘vitu’ njenje vikishuhudiwa hata na watoto waliokuwa wakimzomea.

Wanaume hao waliokuwa wakiongezeka na kuanza kumshika sehemu nyeti, walisababisha dada huyo kuanza kutoka nduki ambapo alizama kwenye duka moja kisha akasitiriwa kwa khanga na mama mmoja msamaria mwema.

Alipotoka bado wanaume waliendelea kumzingira ambapo ilimlazimu kutoa shilingi elfu hamsini kisha kurukia kwenye ‘kenta’ iliyomuondoa eneo hilo na haikujulikana alikoelekea kwa sababu gari hilo lilichomoka mbio huku akiwa amekoma ubishi wa kutembea nusu utupu.

Mapenzi ni kitu kingine kabisa chali yangu usisikia mtu kajiua na Bastola ukadhani ni uchizi tu ..hiyo tunaita ni dhuluma ya penzi...Inauma sana jamani..

Unakuta upo mapenzini na Binti unampenda kupindukia na yeye unaona anakupenda unamfanyia kila kitu unamtoa katika hali fulani na kumpeleka katika daraja fulani kwa mfano unamsomesha mpaka anapata degree ukitegemea labda akimaliza mtaoana na kusaidiana maisha lakini pindi anapomaliza tu na kupata kazi nzuri anaanza kukuonyesha madharau na kuanza kutoka na watu wengine ,,wewe unakuwa Fala tu tena Boyaaa la kutupwa ....Ebu niambie hapo utachukua hatua gani? 




Huyo Ndio Shemeji yetu kwa Mbwana Samatta ..She is Cute No Doubt 



ANAVYOKUTAZAMA
Mwanasaikolojia Zick Rubin kutoka Chuo cha Havard nchini Marekani aliwahi kusema kwamba watu wanaopendana hutumia asilimia 75 kutazamana kuliko wasiopendana, ambao kiwango chao ni asilimia 30-50. 



Hii ina maana kwamba mwanaume anapotumia muda wake mwingi kumtazama msichana na kugeuka taratibu kuangalia vitu vingine kama mtu asiyependa kuacha kumwangalia, ujue anampenda.

MIPANGO 
Mwanaume anayekupenda atakushirikisha kwenye mipango yake hasa ya muda mrefu. Mfano akitaka kununua kiwanja, kujenga nyumba atakuambia na pengine kutaka mchango wako wa hali na mali katika kulifanikisha hilo. Ukiona mwanaume anakuficha mambo yake, tambua kuwa huyo ana walakini kwenye penzi la dhati na la muda mrefu.

ATAONESHA HUZUNI
Katika maisha ya mapenzi kuna wakati wa kuhuzunika. Mwanaume mwenye upendo wa dhati atashirikiana nawe wakati wa huzuni na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa unapata furaha. 





ATAKUAMINI
Dalili nyingine ya kupendwa na mwanaume ni kuaminiwa kwenye maisha kwa ujumla. Yaani mwanaume anayekupenda hatakuficha kitu, mfano pesa zake, atakupa uhuru kwenye simu yake na kukuamini katika usimamizi wa miradi yake.

ATAKUPA NAFASI
Ninapozungumzia nafasi nina maana atakukaribisha kwake bila hofu na kukupa nafasi ya kuingia na kutoka bila mipaka, atakupa nafasi ya kuweka vitu vyako kwenye kabati na kuruhusu nguo, picha na vitu vyako kuonekana wakati wote chumbani kwake.

UTAKUWA MWANAFAMILIA
Mwanaume aliyefikia chaguo la mwisho kwa mwanamke humshirikisha mpenzi wake kwenye masuala yake ya kifamilia, mfano atamwalika kwenye vikao vya harusi, kipaimara, atatoa nafasi ya kuambatana naye kuona wagonjwa, kusalimia ndugu na atakuwa huru kukutambulisha kwao.

ATAZUNGUMZA NAWE KUHUSU WATOTO
Kwa kuwa wanaume wengi hufikiria kuwa na familia, mwanaume anayekupenda atazungumza nawe mipango ya kupata watoto kwa kuwa atakuwa amekuchagua wewe kuwa mama wa wanaye na atapenda mazungumzo hayo.

ATAKUSAIDIA
Kwa kuwa kukwama ni sehemu ya maisha yetu, mwanaume anayekupenda atakuwa tayari kukusaidia unapokwama. Kila mara atahakikisha kuwa unakuwa na mafanikio na yeye atakuwa tayari kukupunguzia usumbufu wa maisha, kwa kukufuata kazini, kukusaidia baadhi ya mambo na hata ya nyumbani.

ATAJITOLEA
Ninaposema kujitolea ninamaanisha atakuwa tayari kufanya mambo yako na kuyaweka yake nyuma. Kwa mfano akiwa anapenda mpira na siku hiyo kuna mechi, lakini muda huo ukamwambia akufuate kwa mjomba wako atakuwa tayari kuacha furaha yake na kukujali wewe. Huyu ni mwanaume anayekupenda kwa dhati.

ATAAMBATANA NAWE
Wapenzi wengi wasiokuwa na mapenzi ya dhati huona aibu kuambatana na wapenzi wao kwenye mikusanyiko ya watu, lakini mwanaume anayekupenda atafurahia kutoka moyoni kuongozana nawe kwenye halaiki ya watu na kufurahia uwepo wako bila kuona aibu.


Kijana mmoja anayeaminika kuwa shabiki wa Manchester United Football Club amejiua jana usiku jijini Nairobi baada ya timu yake kufungwa 1-0 to Newcastle.


Polisi imesema kwamba John Jimmy Macharia, 23, alijirusha kutoka ghorofa ya 7 baada ya kujua timu yake imepoteza mchezo wa jana jioni. Kwa mujibu wa mkuu wa polisi jiji la Nairobi Benson Kibue, Macharia aliwaambia rafiki zake hawezi kuendelea kuangalia timu yake ikifungwa kila siku kabla ya kuruka ghorofani. “Mashahidi wote waliokuwepo wakati wa tukio bado wapo mikononi mwa polisi wanahojiwa,” alisema. Kibue aliwashauri vijana wa jiji la Nairobi kufahamu English Premier League ni mchezo tu kama ilivyo michezo mingine na hivyo waache kuchukua hatua za namna hii kisa michezo. Hii si mara ya kwanza kwa kwa kijana kupoteza maisha kwa ajili ya michezo inayochezwa  England,” alisema Ki

No comments: