advert

http://

Saturday, 8 June 2013

SSPRA KWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA WANAFUNZI YA CHUO KIKUU CHA MT.AUGUSTINO WAANDAA SHEREHE YA KUMUAGA PADRI DOKTA CHARLES KITIMA JANA KATIKA UWANJA WA RAILA ODINGA.

Aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Mt.Augustino Mwanza(SAUT) Mh.Padri Dokta Charles Kitima leo amewaaga wanafunzi na jumuiya yote ya mtakatifu augustino katika kiwanja cha raila odinga na kumkaribisha Makamu Mkuu Mpya Padri Pius Mgeni kuwa ndiye makamu mkuu wa chuo kwa sasa.

Akizungumza katika sherehe hiyo ya kumuaga padri charles kitima awewataka wasomi wote wa vyuo vikuu na viongozi wote kuiga mfumo wa hayati Mwalimu J.K Nyerere ambao aliutumia katika kuiongoza Tanganyika na kuwa mstari wa mbele katika kutetea rasimali za wazawa ambazo utoroshwa kwenda nje kwa njia za panya.

Aidha,Amewataka vijana kuendelea kusoma kazi mbalimbali ambazo Hayati Mwalimu JK Nyerere katika uhai wake aliwahi kuziandika kwa ajili ya watanzania,kama marejeo ya kuondokana na matatizo yanayoikabili la tanzania kwa sasa.

 Katika sherehe hiyo ya kumuaga iliendana sambamba na kikizinduua kitabu kipya kilichoandikwa na Boniphace Pesambili Mgeta ambaye ni mwanafunzi katika shahada ya mwasiliano ya umma(Bachelor of Arts in Mass Communications) katika chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino Mwanza.Pia amempongeza boniphace kwa kuandika hicho kitabu na kutaka aendeleze weledi katika kuandika kazi ambazo zinatetea haki za watanzania.

Padri charles kitima ametoa zawadi ya kwa wanafunzi wote wa chuo kikuu cha mtakatifu augustino kwa kuwanunulia nakala 300 ya vitabu vilivyoandikwa na Bw. Boniphace Mgeta

Kitabu hicho kimeandikwa kufuatia tafiti mbalimbali zilizofanywa na wanafunzi wailosoma katika chuo hicho katika kafuta suluhisho la matatizo mbalimbali ambayo yanawakabiri watanzania kwa sasa.

Zoezi hilo la uzinduzi wa kitabu lilisindikizwa na wakuu wa idara mbalimbali,Idara ya mawasiliano ya umma,Mkuu wa Idara ya sheria,na Mkuu wa idara ya Mahusiano ya jamii na matangazo.
Baadhi ya wanajumui ya  Mt.Augustino wa kimsikliliza Padri Dokta Kitima jana wakati wa kumwaga.

    
Padri Dokta Charles Kitima akitoa hotuba yake kwa wanafunzi na wanajumuiya ya SAUT.





Wa kwanza toka kulia ni Boniphace Mgeta ailiyeandika cha Ufiasadi wa Baadhi ya viongozi wetu wa Nchi




































                             























































   

Friday, 7 June 2013

MATUKIO YA MJADALA WA AMANI NA MAENDELEO ULIOFANYIKA KATIKA CHUO KIKUU CHA MT.AUGUSTINO KATIKA UKUMBI WA M13

Mhe.Steven Wasira akiwa na Padri Kitima na Nyambari Nyangwine,Denis Mpagaze na Bw..Kirangi katika meza kuu.
Mheshimwiwa steven wasira akisoma hotuba yake ya mbele ya wanafunzi wa  Saut,katika ukumbi wa m13 katika chuo kikuu cha mt.augustino Mwanza jana.

Pia katika hotuba yake aligusia suala la udini ambalo limekuwa likitaka kujitokeza hapa nchini kwa kuwataka wananchi wote kuwa wazalendo kwa nchi yao.

Nawe mbunge wa Bunda Mh.Nyambari Nyangwine amewataka wasomi wa vyuo vikuu kujikita zaidi katika suala la ujasiliamali na kuondoa dhana potofu iliyojengeka kwa wanazuoni wengi ya kutaka serikali iwaajiri.
Mhadhiri denis mpagaze wa kwanza kulia,akiwa na padri charles kitima


Padri charles kiitma akiongea kuhusu mjadala wa amani na maendeleo jana katika ukumbi wa m13
Padri Charles Kitima akichangia mjala wa amani na maendeleo

Mheshimiwa Mbunge wa Bunda wa pili toka kushoto meza kuu,Nyambari Nyangwine akimsikiliza Padri Kitima



Mhadhri Denis Mpagze akimsikiliza Dokta Charles Kitima jana 

Wanafunzi wa Baso mwaka wa pili wakisikiliza mjadala jana.

Wanafunzi, pamoja na waandishi wa habari wakiwa katika mjadala jana.





Kutoka kulia wa kwanza ni Aidan Mukandara Mwanafunzi wa BAPRM1ambaye alipata fursa ya kumuuliza mh.waziri swali jana katika mjadala wa amani na maendeleo.

wanafunzi wakisikiliza mada husika jana

wanafunzi wakisikiliza mada husika jana

wanafunzi wakisikiliza mada husika jana

wanafunzi wakisikiliza mada husika jana

wanafunzi wakisikiliza mada husika jana

wanafunzi wakisikiliza mada husika jana

wanafunzi wakisikiliza mada husika jana

wanafunzi wakisikiliza mada husika jana

wanafunzi wakisikiliza mada husika jana,pamoja na waandishi wa habari mbalimbali.










Wanafunzi wa saut wakifuatilia mjadala jana

Wanafunzi wa saut wakifuatilia mjadala jana

Wanafunzi wa saut wakifuatilia mjadala jana

wanafunzi wakisikiliza mada husika jana



Wanafunzi wa saut wakifuatilia mjadala jana
Mgeni Rasmi na viongozi wengine watitoka nje ya ukumbi wa m13 jana

Mhe.Steven Wasira akiongea na vyombo vya habari jana SAUT

Hapa ni  mgeni rasmi Alipo kuwa akiongea na wanafunzi wa SAUT

Mhe.Steven Wasira akiongea na vyombo vya habari jana SAUT



Mkuu wa idara ya mawasiliano ya umma,Bi Iman Duwe akiwa katika sura ya tabasmu na Amani Mbwaga mara tu baada ya mjadala kumalizika.

Thursday, 6 June 2013

Uvivu wamponza Mr Nice,atimuliwa Kenya.


Msanii kutoka Tanzania aliekuwa akifanya kazi chini ya Lebo ya Groundpa Records kutoka nchini Kenya Mr Nice ametoshwa na lebo hiyo kwa kuvunjiwa mkataba wa kazi,alikuwa amesaini chini ya Groundpa Records.
Kwa mujibu wa Groundpa Records wametoa sababu zilizowasukumua kumpiga chini Mr Nice kuwa ni msanii Mvivu,asie na ushirikiano wala kuaminika mbali na sababu hizo waliendelea kusema kuwa amekuwa akitumia vibaya pesa apatazo baada ya kufanya show,amekuwa bingwa wa kuwapa watu ofa za pombe
lakini sababu kubwa waliyoisema ni kwamba alikuwa amesaini mikataba miwili ni ule aliosaini kwa Lamar kutoka Tz na Sallam Sharaf CEO of Grandpa Records Refigah amesema kuwa Mr Nice amemkatisha sana tamaa na hamuitaji tena katika Lebo yao ya Groundpa tena maana habebeki.

Karibu nyumbani Morogoro Ngwear,leo tunakupokea kwa nyimbo za maombolezo,Hayo ni maneno ya Afande Sele aliyoyasema kwa huzuni kubwa mwili wa marehemu ilipowasili.

Msanii wa muziki wa Hip Hop bongo anaeishi Morogoro na kufanya shughuli ya Muziki akiwakilisha Mkoa wa Morogoro Afande Sele The King amewakaribisha watu wanaofuatana na Mwili wa Marehemu Albert Mangwear kwa ajiri ya kumpumzisha katika makazi yake ya kudumu kesho.
“Karibu nyumbani morogoro Ngwear leo tunakupokea kwa nyimbo za maombolezo, may your Soul Rest in Peace”
Mwili wa Msanii Ngwear umeagwa Leo jijini Dar es salaam katika viwanja vya Leaders na kupewa heshima ya mwisho na watu wengi waliojitokeza katika viwanja hivyo,baada ya kutoa heshima ya Mwisho mwili ulianza kusafirishwa kutoka Dar es salaam na kuelekea Mjini Morogoro kwa ajiri ya mazishi yatakayofanyika siku ya Kesho alhamisi ya Tarehe 6 June.

Sunday, 26 May 2013

Bayern Munich Mabingwa wapya wa Ulaya


Bayern Munich

Arjen Robben aliifungia klabju yake ya Bayern Munich goli dakika za mwisho mwisho za mechi yao ya fainali ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Borussia Dortmund, na kuisadia mabingwa hao wa ligi ya Bundesliga ya Ujerumani kutwaa ubingwa wa kombe la klabu bingwa barani Ulaya.
Ushindi huo kwa Bayern wa magoli mawili kwa moja sasa unafuta rekodi yao mbaya ya kupoteza kombe hilo mara mbili katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, ikiwemo, kushindwa kwao na Chelsea mwaka uliopita katika uwanja wao wa nyumbani wa Allianz Arena, kupitia mikwaju ya penalty.
hata hivyo Bayern sasa wameandikkisha historia nyingine ya kushinda kombe hilo kwa mara ya tano katika historia ya klabu hiyo.
Vilabu vya Real Madrid na Ac Millan ndivyo vimewahi kushinda kombe hili mara nyingine zaidi.
Real Madrid imeshinda mara tisa nayo Ac Millan imeshinda mara saba.
Kocha wa Bayern Jupp Heynkes ambaye anakamilisha kandarasi yake na Bayern sasa anaiga klabu hiyo kwa furaha baada ya kushinda kombe hilo kwa mara ya kwanza.
Pep Gaurdiola anatarajiwa kuchukua mahala pa Heynkes msimu ujao.

Saturday, 25 May 2013

Bingwa wa Uropa kufuzu kombe la Ulaya

Chelsea mabingwa wa Uropa
Washindi wa kombe la Uropa mwaka wa 2015 watafuzu moja kwa moja kwa michuano ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya msimu utakaofuata.
Hayo yamethibitishwa rasmi na shirikisho la mchezo wa soka barani Ulaya EUAFA.
Kwa mujubi wa UEFA, umauzi huo umechukuliwa ili kuimarisha viwango vya soka katika fainali hizo na pia kuifanya ligi hiyo ya Uropa ambayo ni ya pili kwa ukubwa kuvutia zaidi.
Uamuzi huo uliochukuliwa wakati wa mkutano mkuu wa EUFA, inajiri baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo kati cha shirikisho hilo na chama kinachoakilisha vilabu barani Ulaya..
Wakati huo huo mkutano huo, umeidhinisha kuwa fainali ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya mwaka wa 2015, itachezwa katika uwanja wa Olimpiki wa Berlin, huku fainali ya kombe la Uropa kuchezwa katika uwanja wa Kitaifa wa Warsaw.
Ligi ya Uropa haizalishi kiasi kikubwa cha fedha na pia haiangaziwi pakubwa na vyombo vya habari kwa michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.
Kwa mara kadhaa EUFA imejaribu mikakati kadhaa ya kuifanya shindano hilo kuvutia zaidi ikiwemo kubadili jina kutoka kwa kombe la UEFA mwaka wa 2009 na kuitwa kombe la Uropa.
Kwa sasa, timu zinazomaliza katika nafasi ya tatu katika makundi yao kwenye fainali za klabu bingwa hushushwa daraja na kushiriki katika kombe hilo la Uropa.
Fainali ya mwaka huu, ilivutia timu mbili ambazo zilifuzu kuambatana na sheria hiyo, na Chelsea ikiibuka na ushindi wa magoli mawili kwa moja dhidi ya Benfica katika fainali.Chanzo cha habari ni http://www.bbc.co.uk/swahili/michezo

Fainali ya kombe la klabu bingwa Ulaya


Wachezaji wa Bayern Munich wakichuana na Borussia Dortmund
Fainali ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya kwa mara ya kwanza, itahusisha timu mbili kutoka Ujerumani siku ya Jumamosi, ishara ya ufanisi wa ligi kuu ya Bundesliga ya kuwekeza katika kukuza vipaji hasa raia wa nchi hiyo.
Maandalizi yote yameshakamilika katika uwanja wa Wembley, na Kombe la Ligi ya mabingwa wa ulaya linameremeta, likisubiri nani atakayelinyakua kati ya vilabu viwili vya Ujerumani vitakavyokutana kwenye fainali.
Borussia Dortmund na Bayern Munich ziko tayari pia.
Mahasimu hao wa Ujerumani wamekuwa wakijiandaa kukutana ugenini Uingereza na mashabiki wamekuja kwa wingi.

Badala ya vilabu vya Uhispania na Uingereza ambayo vimekuwa vinahodhi soka ya Ulaya, sasa ni vilabu vya Ujerumani, licha kwamba nchini humo matajiri wakubwa hawaruhusiwi kumiliki vilabu.

Soka imeimarika Ujerumani?

Raia wengi wa Ujerumani wanasubiri fainali hiyo kwa hamu na ghamu na Chancellor Angela Markel atakuwepo katika Uwanja wa Wembley kutizama fainali hiyo.
Ikiwa huu ni mwanzo wa vilabu vya Ujerumani kutawala soka ya ulaya, haijalishi mashabiki wanashabikia klabu gani, tayari watakuwa washindi.
Takriban wachezaji wote wa timu ya taifa ya Ujerumani, watakuwa uwanjani wakati wachezaji wa Klabu ya Bayern Munich watakapotoana jasho na Borussia Dortmund, katika uwanja wa Wembley, wengi wa wachezaji hao wakiwa wametoka katika vyuo viwili vinavyomilikiwa na vilabu hivyo.
Hali hii kwa vilabu vingi vya uingereza ni kama ndoto. Na ila kufahamu jinsi vilabu hivi viliafikia ufanisi huu, tutaanza mwaka wa 2000.
Huo ni mwaka ambao Wajerumani walidhalalishwa katika mashindano ya bara Ulaya, wakati walipomaliza katika nafasi ya mwisho katika kundi lao hata bila kushinda mechi moja.
Wachezaji wengi wa timu ya Ujerumani waalikuwa wakonge na magazeti nchini Uholansi yaliandika kuwa ni fahari yao kuona viwango vya soka vikianguka na kuwa wakati wa Ujerumani kutawala mchezo huo umemalizika.
Wakati huo huo timu za taifa za wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 na 19 vile vile vilikuwa na matokeo mabaya, kwa sababu ya upungufu wa wachezaji wenye vipaji na ukosefu wa vilabu vya kutosha.
Kutokana na mazingira hayo yote, mchezo wa soka nchini Ujerumani ulionekana kuelekea kusambaratika zaidi, hatua iliyolazimisha shirikisho la mchezo wa soka nchini humo, vilabu na mashabiki kuanzisha mazungumzo ya pamoja, ya kutafuta mbinu ya kurekebisha hali hiyo.

Kilichofuata na mabadiliko ya kimsingi ikiwa ni pamoja ya kuwekeza zaidi katika vijana walionekana kuwa na vipaji na pia katika secta ya kuwahimiza vijana wengi kuanza kucheza mechi huo.
Mikakati hiyo ilianza kuzaa matunda na wachezaji wengi wasiozidi umri wa miaka 23, walianza kujumuishwa katika vikosi mbali mbali vya timu vilivyokuwa vikishiriki katika ligi kuu ya Bundesliga.
Mwaka wa 2006, timu ya taifa ya Ujerumani iliyojumuisha vijana wengi chipukizi ilimaliza katika nafasi ya tatu katika fainali za kombe la dunia na mwaka wa 2010 vile vile walimaliza katika nafasi hiyo.
Katika fainali hizo mbili za kombe la dunia, tuzo la mchezaji bora mchanga iliyakuliwa na wachezaji wa Ujerumani Lukas Podolski mwaka wa 2006 na Thomas Mueller mwaka wa 2010.

Tangu wakati huo vilabu vya Ujerumani na vimekuwa vikiandikisha matokeo mema, na mbali ya wachezaji wengi kusajiliwa na vilabu vinavyoshiriki katika ligi ya Bundesliga baadhi yao pia wamesajiliwa na vilabu vingine katika mataifa ya Ulaya.Chanzo cha habari http://www.bbc.co.uk/swahili/michezo

Rais Museveni afanya mabadiliko jeshini

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amefanya mabadiliko katika makamanda wake wakuu wa jeshi , huku kukiwa na taarifa za kutofautiana kwa majenerali wa jeshi kuhusu ikiwa mwanawe Museveni anaweza kumrithi babake kama rais.
Mkuu wa majeshi, Aronda Nyakairima aliyetajwa katika taarifa iliyofichuliwa kuwa mmoja wa wanaopinga mwanawe Museveni Muhoozi Kainerugaba kumrithi babake, amehamishwa hadi wadhifa wa kiraia kuwa waziri wa mambo ya ndani.
Taarifa za kutofautiana kwa majenerali jeshini ziliibuka mapema mwezi huu wakati magazeti ya Uganda yalipochapisha barua kutoka kwa Generali mkuu David Sejusa Tinyefuza, akidai kuwa Museveni anamtayarisha mwanawe kumrithi atakapoachia ngazi.
Barua hiyo pia inasema kuwa Museveni anapanga kuwaua wale wanaopinga njama yake.
Majenerali kadhaa wakuu walipinga barua ya Tinyefuza wakati kundi la wachache likimuunga mkono.
Mabadiliko katika jeshi yanakuja baada ya magazeti makuu ya upinzani yaliyotoa madai ya mgawanyiko jeshini , yakisalia kufungwa kwa siku ya tano huku polisi wakiendelea kufanya msako katika ofisi zao kuitafuta barua hiyo.
Taarifa ya serikali imesema mabadiliko hayo sio makubwa bali ni madogo katika kuhakikisha serikali inafanya vyema kazi yake.
Hata hivyo msemaji wa jeshi Paddy Ankunda alisema kuwa hayo ni mabadiliko ya kawaida jeshini.
Ankunda alisema kuwa hakuna mgogoro jeshini na kuongeza kuwa Museveni ana haki ya kufanya mabadiliko yoyote kama anavyoridhia.
Mkuu mpya wa majeshi ni Edward Katumba Wamala, ambaye amelimbikiziwa sifa tele kwa kuongoza jeshi la Uganda katika vita dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu (Al Shabaab) nchini Somalia.
Ofisi za magazeti ya Daily Monitor na Red Pepper zilifungwa na kuzuiwa kuchapisha magazeti yoyote na yameendelea kufungwa licha ya agizo la mahakama kutaka polisi kuondoka katika ofisi hizo.Chanzo http://www.bbc.co.uk/swahili/habari