Kocha wa Everton David Moyes ambaye msimu ujao atakuwa kocha mkuu wa Manchester United, amesema hakupanga kuondoka Goodison Park ila ilikuwa vigumu kukataa ofa ya kuifundisha United.
Moyes mwenye umri wa miaka 50 ameyasema hayo wakati akizungumzia mchezo wa siku ya jumapili wa ligi kuu soka nchini England.
Kocha huyo raia wa Scotland amesema kuwa alipanga kuongeza muda wa kuifundisha Everton baada ya kukaa kwa miaka 11, lakini alipopewa mkataba wa miaka sita wa kuifundisha Manchester United alishindwa kukataa.Kauli hiyo ameitoa siku moja baada ya kutangaza rasmi ataicha Everton mwishoni mwa msimu huu na kujiunga Manchester United kama mrithi wa Sir Alex Ferguson ambaye alitangaza kustaafu kufundisha soka baada ya msimu huu kumalizika.
"Sikupanga kuondoka Everton, ila kiukweli ilipokuja ofa ya United, sikuweza kusema hapana" Alisema Moyes ambaye alianza kucheza soka kwenye klabu ya Celtic.
Aidha Moyes ambaye aligoma kujibu chochote kuhusu United, alisema anatambua changamoto atakazokutana nazo hapo jumapili wakati atakapokuwa akiongoza timu yake ya Everton katika mchezo wa ligi kuu England dhidi ya West Ham
Kocha wa Celti, Neil Lennon amepinga uvumi wa kuwa huenda akamrithi Moyes kwenye viunga vya Everton huku Michael Laudrup yeye akisema anataka kuendelea kuifundisha Swansea
CHANZO CHA HABARI.www.bbcswahili.co.uk
No comments:
Post a Comment