Watangazaji na wafanyakazi wa radio SAUT FM iliopo Mwanza wanayofuraha ya kuwakaribisha wadau na wapenzi wao katika maadhimisho ya kuzaliwa kwa radio hiyo inayotimiza miaka 15
tokea kuanzishwa kwake itakayo fanyika kesho Juma mosi kuanzia saa 1 usiku hadi majogoo katika viwanja vya Raila Odinga viliopo katika chuo kikukuu cha Mt. Augustino jijini Mwanza.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa maandalizi na Mkurugenzi wa idara ya Burudani radioni hapo Bw. Lucas Maziku kuwa kutakuwa na mambo mengi ikiwemo maonesho ya Mavazi, Dansi, Muziki kutoka kwa waimbaji mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya wa jijini Mwanza.
Ameongeza kuwa watu watapata pia kuwajua watangazaji na historia ya radio hiyo tokea ilipoanza mpaka hapa ilipo, vile vile amesema kuwa kiingilio ni bure kwa watu wote na ulinzi utakuwepo wa kutosha kwa yeyote atakaefika hapo kesho katika viwanja hivyo.
No comments:
Post a Comment