''Mustapha waziri west'' Cameraman waVITUKO SHOW
 Masai Nyotambofu ambaye pia ni director wa website yawww.masainyotambofu.com akiwa kwenye pozz kabla hajaa nza shooting yani hapo alikuwa ametoka kuvalia gwanda lake la kimasai kwa ajili ya kuaza mashambulizi mbele ya Camera.
 Hapo Masai Nyotambofu anatibua hakawii kucharuka!
 Masai Nyotambofu akifanya yake katika kipengele chake kama kawaida yake..

 Kushoto ni msanii mkongwe Mwita maranya akiwa na Masai Nyotambofuwakiwajibika mbele ya Camera.
''Yosso Komando'' Camera man waVITUKO SHOW

 Muonekano wa Camera wakati wa kazi
Source:MasaiNyotambofu.


Kwa kawaida, mnapoanzisha uhusiano wa kimapenzi kila mmoja humueleza au kumuonesha mwenzake nini anapenda na kipi hakimfurahishi. Kwa kuwa mapenzi ni suala la hiyari, mwenzio anapokukabidhi moyo wake anategemea kuwa utayafanya yale yanayomfurahisha na kuepuka yale yanayomuudhi kwa kadiri uwezavyo. Wazungu wana msemo mmoja kwamba ‘penzi la kweli humsukuma mtu kumfurahisha mpenzi wake kwa kadiri ya uwezo wake na kamwe halitafuti visingizio’. 

Usitafute visingizio linapokuja suala la kumfurahisha mwenzio. Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo yanaweza kumgeuza mpenzi wako akawa adui yako.

UKISHINDWA KUMSIKILIZA
Mapenzi ni kusikilizana kwa kila jambo, hakuna nguzo muhimu kama kukubali kuupokea udhaifu wa mwenzako. Jenga mazoea ya kumsikiliza mpenzi wako kwa staha! Hata kama amekukwaza (lazima itatokea tu kwani yeye siyo malaika), tafuta namna nzuri ya kufikisha hisia zako kwake.
Kabla ya kumsikiliza usikimbilie kumhukumu, kumsimanga, kumvunja moyo au kutoa kashfa ambazo zitamfanya asononeke ndani ya moyo wake kwani vitu hivyo vikizidi, hupunguza hisia za upendo na chuki huanza kujengeka taratibu.
Epuka maudhi ya mara kwa mara, endapo mwenzako ameshakwambia kwamba jambo fulani halipendi, msikilize na muoneshe kwa vitendo kwamba umebadilika. Mpe muda wa kuzungumza mambo yanayomkera ndani ya moyo wake bila kumkatisha, hata kama anachokizungumza hukubaliani nacho.
Mapenzi ni hiyari, ni lazima wakati mwingine ukubali kuwa mjinga kwa lengo la kulinda uhusiano, usiendekeze malumbano na mabishano yasiyo na lazima kwani hapo ndiyo mbegu ya chuki humea haraka.
Kama amekuudhi na unadhani huwezi kuzungumza naye au kumsikiliza kwa wakati huo, kaa mbali naye mpaka hasira zitakapoisha kisha rudi na zungumza naye kwa lengo la kutaka suluhu.


Source:DrGulam Mhedu

Siku chache baada ya kuibuliwa kwa kashfa ya kupitishwa kiholela kwa dawa za kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Jeshi la Polisi limemwondoa Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege Kamishna Msaidizi (ACP), Deusdedit Kato pamoja na Mkuu wake wa Upelelezi, David Mwafwimbo.
Mbali ya maofisa hao, pia jeshi hilo limemwondoa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Linus Sinzumwa, naye ikiwa ni miezi michache baada ya kutokea kwa ghasia wakati baadhi ya wakazi wa huko walipokuwa wakipinga mpango wa Serikali wa ujenzi wa bomba la gesi kwenda Dar es Salaam.
Nafasi ya Kamanda Sinzumwa imechukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Zelothe Stephen kutoka Makao Makuu ya Polisi.
Taarifa iliyotolewa jana na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso ilisema Mkuu wa jeshi hilo, Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema amemteua, ACP Selemani Hamisi kuchukua nafasi ya Kato ambaye anahamishiwa makao makuu ya jeshi hilo. Kabla ya uteuzi huo, Kamanda Hamisi alikuwa Makao Makuu Idara ya Upelelezi.
IGP Mwema pia amemteua Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Hamad Hamad kuchukua nafasi ya Mwafwimbo aliyehamishiwa mkoani Lindi kuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Lindi (OCD).
Taarifa hiyo ya Polisi ilisema uhamisho huo ni wa kawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo yake. Hata hivyo, katika siku za karibuni, kumekuwa na malalamiko mengi kuwa vyombo vya usalama katika uwanja huo vimeshindwa kudhibiti biashara hiyo na matokeo yake Tanzania imechafuka katika medani ya kimataifa kutokana na idadi kubwa ya vijana wake kukamatwa sehemu mbalimbali duniani.
Matukio ya karibuni yanahusisha kukamatwa kwa wasanii Agnes Masongange na Melisa Edward waliokamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, Johannesburg, Afrika Kusini.
Kutokana na kashfa hiyo, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe aliamua kulivalia njuga suala hilo na kuchukua hatua kadhaa na pia alifichua jinsi wasichana hao walivyosaidiwa kupitisha dawa hizo na mtandao uliohusisha polisi, maofisa usalama wa taifa na baadhi ya wafanyakazi wa JNIA.
RPC Mtwara
Sinzumwa anaondoka Mtwara baada ya ghasia kubwa zilizozuka Mei mwaka huu wakati baadhi ya wakazi wa Mtwara walipokuwa wakipinga gesi kutoka Msimbati kusafirishwa kwa bomba hadi Dar es Salaam.
Katika ghasia hizo, ambazo Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), liliingilia kati, polisi walishutumiwa na wakazi wa huko kwa kutumia nguvu kubwa na kuwasababishia madhara.
Mwananchi.

Wanasayansi kutoka chuo kikuu cha tiba Washington, Marekani  wamegundua katika utafiti wao kuwa sumu iliyopo katika mwili wa nyuki iitwayo toxin melittin inaweza kuvivunjavunja na kuviharibu virusi vya Ukimwi pasipo kuacha madhara katika chembehai za mwili.
Habari hii imeelezwa katika taarifa ya tiba za dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi iliyotolewa mapema mwaka huu.
Watafiti hawa wanaeleza kuwa matokeo ya utafiti huu kufika katika hatua kubwa inayoleta matumaini ya kupamba na VVU  kwa kuweza kupata dawa ya kupaka ya majimaji ndani ya uke itakayotumika kupambana na maambukizi ya VVU.
Dk Joshua Hood anasema: “Matumaini yetu ni kwa maeneo ambayo hali ya maambukizi yapo juu na vigumu kuzuilika, dawa ya majimaji mazito inaweza kutumika kupaka ndani ya uke katika kuzuia maambukizi ya mwanzoni kabisa.”
Sumu ya nyuki, melittin, imeonyesha uwezo wa kupambana na VVU kwa kuvunja ganda linalomzunguka kirusi na virusi wengine kwa kulitoboa na kuacha matundu.
Mwandishi mwandamizi wa makala za biokemia,  Dk Samuel Wicline, Profesa wa Biochemia wa Taasisi ya Russel Hornsby anafafanua kuwa kuwa vijipande vidogo vilivyoshindiliwa vya sumu ya nyuki vimeonyesha kuwa na tabia ya kuweza kuua chembe hai zenye saratani.
Anaeleza mtaalamu huyo kuwa hii si mara ya kwanza katika ugunduzi wa tiba ya namna hii, kwani mwaka 2004 wanasayansi wa Croatia walitoa taarifa yao katika jarida la sayansi ya chakula na kilimo kuwa mazao ya nyuki, ikiwamo asali na sumu ya nyuki  vina uwezo wa kutumika kutibu na kuzuia saratani.
Chembehai za mwilini zenye afya huendelea kubaki salama pasipo kupata madhara wakati wa tiba kwani sumu hiyo ya nyuki imetengenezewa na kitu kama ngao ambayo ikikutana na seli za mwili hudunda na kwenda mbali bila kujishikiza.
Hii ni kwa sababu ya seli za mwili ni kubwa kimaumbille kuliko sumu ya melittin, wakati kwa  virusi vya Ukimwi ni vidogo kuliko melittin, hivyo ikikutana navyo ngao hiyo haiwezi kuzuia kirusi kidunde kwani ni kidogo, hivyo  kirusi hudakwa na melittin na kushikamana, hivyo kirusi huweza kuharibiwa.
Dk Hood anaeleza kuwa vijipande vilivyoshibishwa na sumu ya melittin huweza kushikamana na kirusi na kutoboa tundu katika ganda la kirusi na kuchana ganda lote, hivyo kirusi huweza kuvunjwa.
Wakati tiba kwa kutumia dawa za kufubaza makali ya VVU, yaani ARVs zinafanya kazi kwa kuzuia uwezo wa virusi kujidurufisha, kwa tiba ya melittin hushambulia sehemu muhimu ya kimaumbile ya  virusi ambayo ndiyo nguzo imara kwa virusi.
Mwananchi.


Daktari Bingwa wa Watoto katika Hospitali ya Muhimbili, Profesa Karim Manji (wa pili kushoto) akifurahia na wenzake baada ya kufanikiwa kwa operesheni ya kuwatenganisha watoto walioungana, kazi iliyofanywa na jopo la madaktari bingwa saba kwa saa 4. Picha na Michael Jamson.

Akizungumza muda mfupi baada ya kuruhusiwa kumwona mtoto wake, Hija alisema: “Ninamshukuru Mungu kwa yote na nazidi kumwomba amjalie mwanangu apone kabisa, nawashukuru na nitazidi kuwaombea madaktari wanaomtibu mwanangu.”
Alijifungulia nyumbani Agosti 18 maeneo ya Jang’ombe, Zanzibar watoto pacha walioungana mmoja akiwa amekamilika viungo vyote na mwingine akiwa na kiwiliwili.
Source:Mwananchi.


Augustine Jay Jay Okocha, Mwanasoka kutoka Nigera ambaye amejipatia umaarufu mkubwa duniani kutokana na uwezo wake wa kipekee wa kucheza soka kitaifa na kimataifa, aameamua kubadilisha fani baada ya kuwa katika soka kwa miaka mingi sasa.


Staa huyu wa mpira, amejiingiza katika tasnia ya filamu kama mtayarishaji, na sasa yupo katika mchongo wa kutayarisha filamu kuhusu nyota wa muziki wa reggae anayefahamika kwa jina Majek Fashek ambayo imeandikwa na Charles Novia iliyopo katika hatua za awali za utayarishaji wake.

Baadhi ya vipande vya filamu hii vitafanyika huko New York Marekani mwezi wa kumi, ambapo wahusika katika nafasi za filamu hii ni Francis Duru, Sam Dede, Stella Damascus pamoja na waigizaji wengine wakali kutoka Nollywood.

Vilio, simanzi na maombi ya kunena kwa lugha vilitawala jana katika Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Temeke Dar es Salaam wakati waumini na ndugu wa Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Dk Moses Kulola (83) walipopata taarifa za kifo cha kiongozi huyo.
Katibu Mkuu wa EAGT, Brown Mwakipesile alisema kuwa Askofu Kulola alifariki dunia jana saa tano asubuhi kwenye Hospitali ya Africa Medical Invesment (AMI), Dar es Salaam.

Mwakipesile alisema afya ya Askofu Kulola ilianza kubadilika Mei mwaka huu akiwa mkoani Mwanza ambako alipelekwa Hospitali ya Rufaa Bugando ambako alibainika kuwa na matatizo ya moyo.

 “Kanisa liliamua kuchukua jukumu la kumpeleka Hospitali ya Apollo, India kwa matibabu zaidi na baada ya kuona afya yake inatengemaa aliruhusiwa kurejea nchini, lakini Agosti 16, mwaka huu hali ilibadilika ndipo tukampeleka AMI alikofikwa na mauti,” alisema Mwakipesile.

Alisema kifo hicho kimeacha pengo kubwa ambalo haliwezi kuzibwa kwa sasa. Hata hivyo, wanafarijika kwa upande mwingine wakiamini kwamba Mungu amemchukua mtumishi wake kwa wakati alioukusudia.

Alisema mwili wa Askofu Kulola utasafirishwa kwenda Mwanza Jumamosi jioni kwa ndege baada ya kuagwa kanisani hapo. Atazikwa kwenye Uwanja wa Kanisa la EAGT Bugando.

Askofu Kulola ni mmoja wa viongozi wa dini waliokuwa na jina kubwa nchini na alifanya kazi za utumishi wa kanisa kwa miaka 53 kwa kuhubiri na kuwaombea wenye matatizo mbalimbali.

Mtoto wa kwanza wa askofu huyo, Goodluck Kulola alisema wamejifunza mambo mengi katika maisha ya baba yao, ikiwamo upendo na unyenyekevu ulioongozwa na uchaji Mungu.

“Baba alikuwa ni asiyependa kabisa migogoro ya kidini, kisiasa yaani ikitokea hali ya uvunjifu wa amani wa namna yoyote ile alikuwa anaumia sana. Alipenda watu kwa ujumla ametufundisha upendo.”

Askofu Kulola ameacha mke wake aitwaye Elizabeth, ambaye alibarikiwa kupata naye watoto 10 na wengine wawili wa kuasili. Hata hivyo, watoto watatu walishafariki dunia. Ameacha wajukuu 44 na vitukuu 10.

Askofu Kulola, ambaye alizaliwa 1928, alianza Shule ya Misheni ya Ligsha Sukuma mwaka 1939, baadaye alijiunga na Shule ya Bwiru kabla ya kusomea Usanifu Majengo huko Israel kisha kuanza kazi ya kumtumikia Mungu mwaka 1950.

Alifuzu Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Theolojia katika Chuo Kikuu cha California State Christian Marekani.

Aliwahi kutumika kwenye Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) mwaka 1966 mpaka 1991 alipoamua kuanzisha Kanisa la EAGT lenye matawi katika nchi za Zambia, Malawi, Burundi na Msumbiji.

Rais Jakaya Kikwete jana alituma salamu za rambirambi kutonana na kifo cha Askofu Kulola

Mtuhumiwa aliyempiga chupa mwigizaji Aunt Ezekiel Jumapili iliyopita nje ya Ukumbi wa Bilicanas ndiye aliyewahi kumchana viwembe mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ mwaka 2011.

Kumbukumbu  zinaonesha kuwa, mwaka 2011 Lulu alivamiwa na wadada wa mjini baada ya kunaswa katika pozi tata na mwanaume wa watu maeneo ya Kariakoo, jijini Dar. Alipoulizwa juu ya sakata hilo, Lulu alitiririka hivi:

“Naweza kumkumbuka mwanamke mmoja, namfahamu kwa jina la Yvonne, alinivamia na kuanza kunishambulia huku mkononi akiwa ameshika wembe...”

 Mwishoni mwa wiki iliyopita, Yvonne huyohuyo ndiye aliyedaiwa kumpiga chupa mkononi Aunt ambapo haikubainika mara moja sababu za kufanya tukio hilo.

Aunt alipelekwa katika Hospitali ya Dokta Mvungi, Kinondoni na kushonwa nyuzi sita huku mtuhumiwa akishikiliwa na polisi. 

Msanii mkongwe wa muziki wa dansi, Muhidin Gurumo akijaribu gari dogo alilokabidhiwa na mwanamuziki wa bongo fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond ‘ kutokana na kutambua mchango wake baada ya kustaafu kazi ya muziki.

Muhidin Gurumo akipokea funguo ya gari kutoka kwa Diamond
Gari alilozawadiwa mzee Gurumo.