advert

http://

Monday 18 November 2013

DIAMOND SI MWENZETU TENA ONA ALICHOPOST AKIWA NCHINI NIGERIA!!



Diamond anaweza kuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania kufanya video na director mkubwa wa Nigeria Clarence Peter
ambaye ameshafanya video nyingi za wasanii wakubwa nchini Nigeria na Africa kwa ujumla.
 

Diamond ame-post picha moja ya behind the scene wakiwa wanatengeneza hiyo video na aliandika hii caption , “Naamini ipo siku nasi Tanzania tutasimama vyema katika ramani hii ya muziki worldwide na kuipa sifa na heshima zaidi East Africa yetu. Eeeh Mwenyezi Mungu ibariki Tanzani, ibariki East Africa na Africa yetu kwa ujumla. #LastNight #Onset #NumberOneRemix#DiamondFtDavido #ClarencePeterBehindTheCamera.


akuna kusanda,hakuna kumbwanda,mbele kwa mbele makamanda,vua gamba vaa gwanda kisha kaza mkanda, wanashuka sisi tunapandaaa,,,,Leo tunaanza kuandika historia mpya ktk mkoa wetu wa morogoro na tz kwa ujumla kwa sababu nikiwa kama msanii wa muda mrefu na mfalme pekee wa mzk wa kizazi kipya ninaetunga nyimbo zangu kwa kuzingatia ujumbe muhimu ktk jamii kwa mambo ya kisiasa,kiuchumi,elimu,amani na upendo nk,Sasa leo nimeamua kwa ridhaa yangu iliyosukumwa na uzalendo na mapenz makubwa kwa taifa langu kuchukua kadi ya kujiunga rasmi uanachama wa CHADEMA,tukio hilo kubwa litafanyika leo jioni ktk mkutano wa hadhara utakaofanyika kata yetu ya mafiga/misufini na utahudhuriwa na viongoz mbalimbali wa chama kutoka makao makuu ya chama Dsm pamoja na mbunge wa nyamagana mh Ezekiel Wenje,kwa wakaz wa Moro wazalendo nyote mnakaribishwa saaana, ahsanteni wana’ndugu, siasa si uadui, tupingane/tusipigane, Pendo moja!,,,,”
Baada ya mahusiano yao kuongelewa sana Kwenye 
Mitandao hatimaye Peter Okoye wa P-Square Amefunga ndoa na mchumba wake wa muda Mrefu anayejulikana  kwa jina la Lola....Congrats Bro.....


Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amefyatuka na kuwananga mahasimu wake wanaowania urais wa 2015 kwa kuandaa bajeti ya zaidi ya Sh. bilioni 10 ili waingie madarakani kwa njia ya rushwa.


Amedai kuwa watu hao wamekula yamini ya nchi kuongozwa na mtu tajiri kupitia njia ya mkato.

Aidha, akasema kuna hatari wakati taifa likielekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani, na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, kuzuka kwa kundi la matajiri, ambao wengi wao ni wakwepa kodi mashuhuri, watoroshaji wa madini ya nchi na watoroshaji wa nyara na maliasili za nchi.

Akizungumza jana katika mahafali ya 17 ya Shule ya Sekondari ndogo ya Agape inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini, Sitta alisema walafi hao wa madaraka ni pamoja na baadhi ya viongozi waliojitajirisha kupitia fursa za serikali kwa njia ya rushwa, mikataba mibovu, wauza madawa ya kulevya na mawakala wa maovu.

Alisema kutokana na mwelekeo huo potofu, amewataka wananchi wamruhusu kutumia hadhara hiyo kuzungumzia hatari kubwa inayoikabili nchi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

“Katika mazingira haya inasikitisha kwamba viongozi wengi hususani wenye uroho wa madaraka na mali wamejigeuza kuwa wachekeshaji wa mfalme kwa kumuunga mkono, kujipendekeza na kumsifia kiongozi wanayejua maovu yake kwa mategemeo ya kupewa fedha na vyeo. Watu hao katika miaka miwili wamejipambanua kwa njia ya harambee mbalimbali zinazotangazwa kwa mbwembwe na kelele katika baadhi ya makanisa, misikiti na makundi mengine ya jamii,” alisisitiza.

Alisema kuwa hadi sasa, watu hao wamechangia fedha zinazokadiriwa kufikia Shilingi bilioni saba huku wakiwa wameshaandaa bajeti ya bilioni 10 kwa ajili ya rushwa ya uchaguzi ambayo hawataki iitwe rushwa kwa sababu macho yao yamepofuka.

Alisema kuwa Watanzania hawahitaji shahada ya siasa kubaini watu hao wakifanikiwa katika malengo yao. Alisema uongozi utakaotokana na genge hilo hautaweza kuleta neema kwa Tanzania kwa kuwa ngazi zote za uongozi katika himaya ya aina hiyo, zitajazwa na watu wanaofanana katika maadili potofu.

“Masikini na wanyonge watabanwa mbavu zaidi, matabaka ya wenye utajiri na masikini yatapanuka kiwango ambacho hakitavumilika. Lakini pia ukusanyaji wa kodi na mapato mengine ya serikali utadorora na kudidimiza huduma zote za jamii na kipato cha kila Mtanzania… hatimaye misingi yetu ya umoja na usawa itabomoka na kulitumbukiza taifa katika machafuko,” alisema.

Kuhusu hatma ya taifa kabla na baada ya uchaguzi mkuu, Sitta alisema Watanzania wasipokuwa na mtazamo wa kizalendo na wakasimama kwa dhati ya mioyo yao kupambana na kulikataa jambo hilo, watawaachia watoto wao urithi ambao utatafuna vizazi hata vizazi.

“Dhambi kubwa katika taifa lolote ni pale mbele ya maovu, watu wema wanaamua kukaa kimya. Mimi na wewe tukiamua hali hii ikome sasa, inawezekana na cha msingi ni kurudi nyuma na kujipanga upya kupambana na hali hii kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho,” alisema.

Kuhusu suala la maamuzi magumu, Sitta alisema tatizo jingine linalodhihirisha mgawanyiko wa kitabaka ni kiburi cha baadhi ya viongozi ambao wanatamba kwamba hawawajibiki kwa vyombo vya sheria kama wafanyavyo watu wa kawaida.

Sitta ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo yaliyoambatana na harambee ya kuchangia ujenzi wa chepo ya Seminari hiyo, alichangia Sh. 5,750,000.

Awali akisoma risala ya wahitimu wa seminari hiyo, Shaine Mapunda, alisema inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo ukosefu wa zahanati ya shule ambayo husababisha wanafunzi kukosa masomo kwa ajili ya kufuata matibabu hospitali ya Marangu.

“Tunaomba kuongezewa vitabu vya michepuo ya sanaa ili kuongeza ufaulu na ubora kwa wanafunzi wa michepuo ya sanaa, uboreshaji wa viwanja vya michezo ufanyike kwa awamu ili kuzidi kukuza na kuinua vipaji vya michezo mbalimbali,” alisema Shaine.

Mkuu wa Shule hiyo, Sista Elistaha Mlay, alisema shule hiyo yenye mikondo ya kidato cha tano na cha sita yenye jumla ya wanafunzi 548, inakabiliwa na tatizo la uhaba wa maji na umeme hali inayosababisha kero kwa wanafunzi kujisomea. Jumla ya wanafunzi 108 wa kidato cha nne wamehitimu.


============

Source: Nipashe.

Wakati Serikali ikisisitiza kuwa huduma ya kumwongezea mgonjwa damu hospitalini ni bure, imebainika kwamba baadhi ya watu mitaani wakiwamo wabeba mizigo sokoni wanauza damu zao kwa watu wanaohitaji.
Mbali ya watu kuuza damu zao, majimaji hayo mekundu muhimu mwilini yamegeuka bidhaa adimu baada ya baadhi ya wauguzi na madaktari nao kugeuza huduma hiyo kuwa kitegauchumi chao.
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ni kosa kwa mtumishi yeyote wa afya nchini kumuuzia mgonjwa damu na wala hakuna biashara ya kuuza damu kwa kuwa hutolewa bure na watu wanachangia kwa hiari.
Uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili katika hospitali mbalimbali nchini, umebaini hospitali nyingi hazina damu za kutosha na hivyo kusababisha baadhi ya wagonjwa kuwalipa watu mitaani, ili kuwatolea damu au kuinunua kwa wauguzi na madakari.
Hata hivyo, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid alisema kuwa wahudumu wa afya wanaoendesha vitendo hivyo ni watu wanaojaribu kuizidi maarifa Serikali na kwamba wananchi wamepewa taarifa za kutosha kuwa damu haiuzwi.
“Kuna watu wanajaribu kutuzidi maarifa, hiyo ni tabia inayopaswa kupigwa vita. Mtu yeyote atakayetakiwa kununua damu, atoe taarifa kwa mganga mkuu au kituo chochote cha polisi,” alisema.
Mkoani Dodoma
Wabeba mizigo wa soko la Majengo Mjini Dodoma, wamekuwa mkombozi kwa wagonjwa wanaofika katika hospitali ya mkoa huo baada ya kugeuza miili yao kuwa sehemu ya kuvuna damu na kuiuza kwa ndugu wa wagonjwa hao.
Gharama za kuuza damu hiyo ni kati ya Sh10,000 hadi Sh30,000 kwa chupa moja, kutegemea na uwezo wa ndugu wa mgonjwa huyo, lakini baadhi wamekuwa wakitoa zaidi kama sehemu ya shukurani.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na kuthibitishwa na baadhi ya wabeba mizigo hao, imebainika kuwa kitendo cha kutoa damu kwa wabeba mizigo ni cha kawaida na kwamba utaratibu huo ulianza muda mrefu.
Enock Ayub ambaye ni mmoja wa watu ambao wamechangia damu zaidi ya mara tatu kwa nyakati tofauti, alilimbia gazeti hili kuwa biashara ya kutoa damu anaipenda na kwamba inampa matumaini ya kuishi kwa kuamini kuwa bado ni mzima.
“Mimi nimechangia damu zaidi ya mara tatu, lakini tukifika kule tunabadilisha majina maana madaktari wanataka mtu ukae muda za miezi sita bila ya kutoa, sisi tunataka fedha ‘mkwanja’, hatuna jinsi,” alisema Ayubu na kuongeza:
source:http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Hatari--Watu-wauza-damu-zao-mitaani/-/1597296/2076318/-/uqttc3/-/index.html

Majiji yote matano nchini pamoja na Zanzibar na mikoa mingine kadhaa yatakuwa na giza kwa siku kumi kuanzia leo, hivyo kusababisha adha kwa wakazi wake. 
Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Badra Masoud, amethibitisha kuwepo kwa adha hiyo, akielezea kuwa hali hiyo inatokana na kuzimwa kwa mitambo ya Kampuni ya Pan African iliyopo Songosongo.
“Mitambo hiyo itazimwa kwa sababu ya matengenezo ya lazima, hakuna jinsi ya kuzuia hali hiyo Tanesco tunasikitika sana kwa kuwa kutakuwa na upungufu mkubwa wa umeme kwenye gridi ya taifa,” alisema Masoud.
Alifafanua mitambo hiyo inaendeshwa na gesi ambayo imepungua katika kisiwa hicho cha Songosongo Wilaya ya Kilwa, Lindi. 
“Upungufu huo umesababishwa na matengenezo ya kiufundi yanayofanywa kwenye visima vya gesi, lengo ni kuboresha upatikanaji wa gesi ya kutosha kwenye visima hivyo,” alisema.

 Marekani imetoa ripoti inayozungumzia usafirishaji wa binadamu ya mwaka 2013, huku ikiitaja Tanzania kuwa kinara wa kunyanyasa wasichana, kuwatumikisha katika ngono na usafirishaji wa binadamu.
Ripoti hiyo iliyotolewa na idara ya nchi hiyo inayohusika na diplomasia (US Department of State, Diplomacy in Action), pia inaitaja Tanzania kuwa ni kitovu cha njia ya kusafirisha wanawake, watoto na wanaume ambao hutumikishwa kwenye kazi za mashambani na biashara ya ngono.
Ripoti hiyo iliyozinduliwa Julai  mwaka huu   na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Seneta John Kerry inaweka bayana kwamba biashara ya usafirishaji wa binadamu hufanywa na baadhi ya ndugu na marafiki ambao hutoa ahadi kwa wahusika kwamba wanakwenda kuwasomesha au kuwatafutia ajira nzuri mijini.
“Unyonyaji wa wasichana wadogo na utumikishaji majumbani ndilo tatizo linaloongoza, ingawa kesi za watoto kusafirishwa kwa ajili ya biashara ya ngono katika mpaka wa Tanzania na Kenya zinaongezeka. Pia, wasichana wananyonywa kwenye maeneo ya utalii,” inasema sehemu ya ripoti hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watoto kutoka Burundi na Kenya, watu wazima kutoka Bangladesh, Nepal, Yemen na India wanatumikishwa kufanya kazi kwenye sekta za kilimo, madini na majumbani nchini Tanzania.
“Baadhi ya raia kutoka nchi  jirani huingia Tanzania kwa hiari yao, lakini hulazimishwa kufanya kazi majumbani kabla ya kupelekwa kutumikishwa kwenye biashara ya ngono Afrika Kusini, Ulaya na Mashariki ya Kati,” inaeleza.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki alimtaka mwandishi kumtumia ripoti hiyo kwa njia ya baruapepe ili aweze kuisoma na kuitolea maelezo.
Alipotafutwa siku ya pili, alisema kuwa ameipokea na kuikabidhi ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP) ili ifanyiwe kazi na baadaye kutoa majibu.
“Ripoti niliipata nikaikabidhi ofisi ya DPP kwa kuwa wao ndio wanaoweza kuitolea maelezo baada ya kuisoma. Maoni yangu lazima yawe ya kitaalamu siwezi kusema bila kupata taarifa kutoka kwao,” alisema.
Credit:Mwananchi.

Inavyoonekana Rihanna ni ‘team drake’ na Drake ni ‘team Riri’ na hilo tu linatosha kuwafanya wawe 
zaidi ya marafiki, kwasababu inavyoonekana ‘urafiki’ wa wawili hao unazidi kuimarika kadri siku zinavyozidi kwenda.

Ikiwa ni siku chache toka Drake aonekane katika tour ya Rihanna huko Dallas, alamisi wiki hii Rihanna naye amerudisha fadhila kwa kuhudhuria show ya Drake huko Houston, Marekani.

Baada ya show hiyo wawili hao ambao walikana kuwa na uhusiano wa kimapenzi japo zipo dalili nyingi zinazoashiria kuna kitu kikubwa kinaendelea kati yao, walielekea katika club moja ya strippers ambako kwa mujibu wa TMZ walimwaga mvua ya pesa $12,000 kwa ujumla kwa kinadada wanaocheza nusu uchi (strippers), na chanzo kimoja kiliiambia TMZ kuwa baadae Drake na Rihanna waliondoka pamoja mishale ya saa 11 alfajiri.


Credit:Bongo5.
Leo hii mwanadada wema sepetu ameonekana akipost kitu kwa mara ya kwanza kwenye mitandao ya kijamii baada ya muda mrefu toka msiba wa baba yake ulipotokea hivi karibuni.

Katika post hiyo Wema amewataka “Teamwema” wapunguze jazba juu yanayotokea juu yake na kuwasihi kuwa wapunguze kutumia lugha ya matusi kwenye mitandao hiyo maana wanamuumiza ‘madame’
Ujumbe wake unasomeka kama ifuatavyo….
"...my darlings... im still grieving... i know you guys miss me... nd i miss you more... im jus still nat okay... but im right here... nipo pamoja na nyinyi... muda tu kidogo... dats all im asking for... nawapenda... saana kupita maelezo... im gone be baq... very soon... i promise... its jus dat sipo sawa. .. but inshallah... ntakuwa sawa... inshallah... its hard... i hope mnanielewa... i repeat nawapenda mno... mno... more dan u think... u kip me goin... u make me who iam... sema tu msifanye vile basi... msitukane... me mwenzenu bado im nat okay... alafu mnaniongezea matatizo... mi spendi... all in all i still love you guys... basi msinikere... sawa... sometimes its best to jus keep quiet... okay.... much love... P.S: Iam a father's daughter.

Huwa nawakumbuka naamini kabisa kitambo si kirefu watakua huru.. wakati nafanya album yangu ya kwanza (mkuki moyoni) zaidi ya miaka kumi 
iliyopita kuna ile track MAYOWE REMIX imepigwa live band ingawa MAJANI alipiga kick, lakini BASE & SOLO GUITAR alicharaza MZEE NGUZA (babu seya) mwenyewe, ukisikiliza vyema ile kazi utasikia kila chombo kwa wakati wake hiyo imechangiwa na ustadi wa Mzee Nguza zaidi, mtoto wake ambae ni PAPII KOCHA alifanya chorus ilikua vibe sana nakumbuka siku ile pale BONGO RECORDS. wakati huu ambao nakaribia kutimiza miako kumi ya KING OF RHYMES i wish mungekuepo tufanye kitu, MFUNGWA, MFUNGWA NI NANI? IMAM, RAISI. ASKOFU, MWALIMU, HAKIMU, JAJI, MASIKIN, TAJIRI, MCHUNGAJI anaweza kuwa mfungwa... .. MUNGU ni muweza wa yote na hashindwi na chochote naamini kabisa tutakua pamoja uraiani .. nawapenda, nawaombea na maelfu ya Watanzania wako pamoja nanyi

Huu ni waraka wangu kwako wewe mdada ninaekupaga lifti asubuhi. Nimevumilia sana mpaka nimechoka aisee maana imekua ni kero sana.


Toka tuanze biashara ya kupeana lift imekua tatizo sana mpaka najuta kukufahamu. Sina uhakika sana kama wewe ni member humu Jf,
But hata kama sio member, najua hukosi kufanya kazi na Member wa humu ambae sina shaka atakufikishia ujumbe.

1) Kwanza kabisa mimi ni mume wa mtu. Biashara ya wewe mke wa mtu kunipigiaga simu asubuhi asubuhi na kuniamsha siitaki. Mimi ninaamka kwa ratiba zangu, simu unazinipigiaga kuniamsha hua zinanipa wakati mgumu sana kujitetea kwa my wife wangu.

2) Sipendi kabisa tabia ya mimi kukusubiri wewe getini kwako. Mimi sio dereva wako, hujaniajiri wala kwa lifti ninayokupa sifaidiki chochote zaidi ya kua tu wewe ni jirani yangu, nakuonea huruma ukigombea daladala asubuhi. Wewe unatakiwa uwe umeshajiandaa asubuhi na nikukute getini. Cha ajabu siku hizi nikishafika getini mpaka nikupigie simu ndio utoke. Jana umeniuzi sana eti ulishajiandaa ila ukawa unasubiri nikupigie simu.


3) Kunichagulia nyimbo za kusikiliza kwenye gari sipendi. Mimi ni mpenzi mkubwa wa Bongo Flava, hizo R&B zako kama unazipenda sana basi ka-dowload ukasikilize nyumbani kwako/kwenu.

4) Inaendana na namba (3) pale juu. Hua napenda sana kusikiliza Magazeti redioni asubuhi. Sipendi kabisa tabia ya wewe kujifanya ndio controller wa radio ya gari langu. Kupitia Magazeti radioni ndio najua mambo mbalimbali yahusuyo Siasa, Mchezo n.k. kabla sijafungua JF.

5) Mimi sio mpenzi sana wa AC kwenye gari, napendelea kitu Natural Air. Sijui kwanini hujalifahamu hili. Eti ukiingia tu unaanza kupandisha Vioo na kuwasha AC, huangalii kama kio changu pia kimepanda ama vipi. Wewe unatakiwa unifuatishe mimi na sio kujifanyia mambo utakavyo.

6) Kuna mafuta mengine unapaka yananikera kwelikweli harufu yake. Nafikiri hata huko kazini kwenu wanaipata fresh.

7) Unaongea mno aisee, yaani kama umemeza kanda. Yaani njia nzima unaongea wewe tu. Binadamu tumepewa mdomo mmoja na masikioo mawili ili tuongee kidogo lakini tusikilize sana, lakini kwa wewe mdada sio hivyo aisee. Unahdithia mastory ya kazini kwenu ambayo hayanihusu, mi ya nini?? 

8) Ukiwa na mimi ujue ni straight to Mjini. Mambo ya kuniambia eti tupitie sijui Steers au Jamaa fast Food kuchukua vitafunwa mi siiizimkii aisee. Pengine wewe umezoea kuchelewa kazini, basi tusicheleweshane. Sometimes nakua na viporo kibao kazini nahitaji kuwahi kuvimalizia, we unaanza kuzusha safari zako za asubuhi asubuhi, why we mwanamke??

9) Hivi gari umejifunzia wapi?? Sijawahi kukuona ukiendesha na wala hujawahi kunionyesha hata leseni yako, leo unaniambia siku moja moja niwe nakuachia uwe unaendesha wewe, ili iweje?? Unataka kujifunzia gari kwangu? 

10) Mimi ndio dereva, najua wapi ni-over take na wapi nipite wapi. Cha ajabu hata speed unanipangia wapi nikimbize na wapi niendeshe slow, wewe umeomba lifti tu, kaa subiri ufikishwe kazini kwako, biashara ya njiani naijua mimi. Mimi nimeanza kuendesha gari toka unasoma shule ya msingi so sipendi ujifanye mwalimu wangu wakati naeendesha.

11) Gari yangu sio saluni kwenu. Eti unaweka miguu juu, mara sijui unakata kucha, halafu hizo kucha zinaporukia wala hujishughulishi kuzitafuta. Matokeo yake tunataka kuvunjiana ndoa. Halafu ukifungua kioo cha kujiangalia cha "kizuia jua" uwe unakirudishia baada ya kukitumia. Pia sipendi ukae kwa kulaza siti kwa nyuma. We asubuhi asubuhi umeamka bado una energy za kutosha halafu unakaa kwa kulaza siti, hizo kazi zitafanyika kweli??

12) Tena sipendi uwe unaongea kwa kunipiga piga begani au mkononi, hua naumia na pia naweza kupoteza control ya sterling. 

Haya ni baadhi tu ya ambayo unayafanyaga wewe abiria wangu naekupaga lifti ambayo yananikera sana asubuhi. Nashindwa tu kujua nianzie wapi kukuambia ukweli navyokereka.

Chanzo:Jamii Forums
Meneja wa Bendi ya Akudo Impact, Ramadhan Pesambili, Novemba 14, mwaka huu ameliambia Risasi Jumamosi kwamba wamepata taarifa za kushikiliwa kwa Kanal Top nchini China kwa tuhuma hizo.


“Taarifa hizo tumezisikia, tunazifuatialia kwa umakini mkubwa na kuweza kujua kama ni kweli ama la, maana zinachanganya sana,” alisema Pesambili.

Aidha,  meneja huyo ameonesha kusikitishwa na habari hizo na kudai kwamba zinaichafua bendi yao kutokana na watu mbalimbali kumpigia simu kumuulizia juu ya taarifa hizo na wengine  kumfafanulia zaidi jinsi Kanal Top alivyonaswa.

“Kama meneja wa Akudo nasikitishwa na taarifa hizo, kwa kuwa Kanal Top hatuko naye zaidi ya miezi minne sasa, mwanzo aliaga anakwenda Kongo kuoa na  aliporudi aliomba ruhusa ya kwenda Dubai kufanya shoo ya wimbo wake wa Mama Vanesa nasi tukamruhusu kwa moyo wote.

“Wiki tatu zilizopita tulisikia habari za uvumi huo na tulipofuatilia tukagundua si kweli,” alisema meneja huyo.
Pesambili alisema kuwa hata Mzee  Kapuya (Juma, mmiliki wa Akudo) alisikia uvumi huo na akasema kama kweli Kanal Top anajihusisha na biashara hiyo basi asirudi kwenye bendi yake na ikiwezekana akamatwe kabla hajachafua hali ya hewa.
“Lakini  kabla hatujachukua hatua zozote ndiyo juzi tukasikia tena kuwa amekamatwa nchini China.

“Viongozi wa Akudo tumesikitishwa sana na taarifa hizo ingawa bado tunaendelea kuzifuatilia ili tuweze kujua zaidi, maana tunasikia amekamatwa akiwa na wanamuziki wa FM Academia, wengine wanasema alikuwa na mkewe,” alisema Pesambili huku akikiri simu ya China ya Kanal Top haipatikani.

Chanzo: Global Publishers


YANGA na Azam kama zinamtaka straika wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi ni fedha yao tu, lakini kuna sharti lazima walifanye.


Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) limetoa masharti na muongozo wa klabu zinazomtamani mchezaji huyo aliyesitisha mkataba na Etoile du Sahel ya Tunisia.

Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba aliiambia Mwanaspoti kuwa: “Hakuna kinachoizuia klabu kutaka kumsajili Okwi, cha muhimu wanatakiwa kuongea na Etoile du Sahel ya Tunisia, wakimalizana nao basi watamchukua, hivyo ni ruksa cha muhimu ni kufuata sheria na haki.”

Okwi ameidhinishwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kuichezea SC Villa ya Uganda kwa muda wa miezi sita huku sakata lake la Etoile likifanyiwa ufumbuzi.

Mchezaji huyo anaidai Etoile malimbikizo ya mishahara pamoja na dau lake la usajili huku Simba iliyomuuza kwa Waarabu hao nayo ikidai dau lake Sh 480 milioni.

Suala hilo lipo Fifa na Kawemba amewahakikishia Simba kwamba wasiwe na wasiwasi watapata haki yao.


credit:Mwanaspoti.

KAMA utahitajika kuwataja wasanii kumi wanaofanya vizuri katika muziki wa Injili Bongo na hata Afrika Mashariki, haitakuwa rahisi kuyaacha
majina ya Rose Mhando, Bahati Bukuku, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Christina Shusho, Siana Ulomi, Martha Mwaipaja, Jeni Miso na Jennifer Mgendi.

Ni kwasababu hao ni waimbaji ambao katika kila duka linalouza kazi za muziki huo, ni vugumu kupita saa mbili kabla mmoja wao hajauza kazi yake.

Katika wakati ambao wanamuziki wa Bongo Flava na dansi wanalilia kupata soko la kazi zao, waimbaji wa Injili wanaendelea kula kuku kwa mrija kwani kazi zao sokoni zinanunuliwa kama njugu.

Kwa baadhi ya nchi, nyimbo zao hupigwa hata katika kumbi za starehe kwa kuamini ni nyimbo za kujirusha kutokana na mvuto wake.

Rose Mhando

Huyu ndiye kiboko yao, wanamuziki wa Bongo Flava wanamfahamu kwa jinsi anavyowapiga bao katika uuzaji wa kazi zake, si tu katika CD na video, Rose Mhando pia ni kinara wa mauzo katika miito ya simu.

Diamond ambaye anasifika kwa kuuza miito ya simu, akikutana na Rose Mhando anakaa chini kwani mapema mwaka huu alimwacha mbali kwa kuingiza Sh29 milioni ndani ya miezi mitatu huku Diamond akiingiza Sh21 milioni.

Albamu zake za ‘Mteule Uwe Macho’, ‘Kitimutimu’, ‘Jipange Sawasawa’ na ‘Utamu wa Yesu’ bado zinaendelea kufanya vizuri pamoja na kuwa wasanii wengine wanaingiza albamu mpya kila kukicha.

Bahati Bukuku

Huyu anatajwa kushikilia nafasi ya pili ya mauzo ya CD na video katika maduka mbalimbali ya kazi za sanaa Bongo. Pamoja na kutotoa kazi mpya mara kwa mara, albamu yake moja ilimfanya kuwa mwimbaji namba mbili katika mauzo na matamasha nchini.

Tamasha lolote la Injili haliwezi kukamilika bila kupigwa nyimbo kama ‘Waraka wa Amani’, ‘Nimesamehewa Dhambi’, ‘Nyakati za Mwisho’ na ‘Mapito’.

Mwanamuziki huyu kwa sasa anatamba na albamu mpya aliyoizindua mwezi uliopita iitwayo ‘Dunia Haina Huruma’.


Upendo Kilahiro

Inavyoonekana muziki wa Injili unamlipa sana kwani ameweza kuanzisha Chuo cha Ushonaji kiitwacho, New Day Africa Foundation, ambacho wanafunzi wake hawalipi hata shilingi moja kwa muda wanaochukua ujuzi chuoni hapo.

Kilahiro anayetamba na nyimbo za ‘Unajibu Maombi’ na ‘Usinipite’, ni msanii namba tatu kwa mauzo ya nyimbo za Injili Bongo.

Upendo Nkone

‘Niacheni Niimbe’, ‘Nimebaki na Yesu’, ‘Uniongoze Yesu’ na ‘Nakaza Mwendo’, ni baadhi ya nyimbo zinazofanya kazi zake ziendelee kununuliwa kwa wingi. Kila anapoachia wimbo mpya, huendelea kuzifanya zile za zamani ziwe nzuri zaidi.

Mbali na kuuza kazi zake, pia ni mwanamuziki anayeongoza kwa kufanya matamasha ndani na nje ya Bongo. Mara kwa mara hufanya ziara nchini Kenya ambako anakubalika na kuheshimika.

Christina Shusho

Huyu anazo sababu zaidi ya mia moja za kuwa mwanamuziki anayeuza sana katika muziki wa Injili. Kwanza sura yake inapokaa kwenye ‘kava’ inampa mteja hamu ya kutoa pesa yake kununua CD, pili unapopata bahati ya kuisikia sauti yake kwa mara ya kwanza, hakika utataka kuisikia tena na tena na tatu tungo zake zinazogusa maisha ya kawaida na kiroho zimekuwa kivutio kikubwa.

Flora Mbasha, Jeni Misso, Jennifer Mgendi, Martha Mwaipaja na Siana Olomi nao wanaingia kwenye kundi hilo, lakini wanapishana kidogo kutokana na sababu mbalimbali zilizotolewa na wafanyabiashara wa kazi hizi.

Waimbaji Jeni Misso, Martha Mwaipaja na Siana Olomi ni kama wanachipukia kwenye soko kuu la kazi hizi, lakini wamekuwa wakichuana na wakongwe akina Flora Mbasha na Jennifer Mgendi ambao wamekuwa katika muziki huu kwa muda mrefu.

Wafanyabiashara wa kazi hizi wanasema, Jennifer Mgendi na Flora Mbasha, waliwahi kuwa vinara wa mauzo lakini walipoanza kujichanganya na biashara nyingine iliwapunguzia mashabiki ambao walianza kununua kazi za waimbaji wengine.

Flora Mbasha kujihusisha na kampeni mbalimbali zikiwamo za  vyama vya siasa na Jennifer Mgendi kujiingiza katika uigizaji wa filamu, zinatajwa kuwa ni sababu zilizowarudisha nyuma.

Yote kwa yote hii ndiyo ‘krimu’ ya wasanii wanaoongoza sokoni kwa muziki huo, tamasha lolote la muziki wa Injili Bongo au Afrika Mashariki, haliwezi kukamilika bila uwepo wa waimbaji hawa.


credit:Udakuspecially.
Stori: Chande Abdallah
MWIGIZAJI Koletha Raymond ‘Koletha’ amefunguka kuwa hapendi umaarufu kwa kupiga picha za utupu kama wasichana wengi walio katika tasnia ya filamu wafanyavyo.



Koletha aliyasema hayo ikiwa ni siku chache tu baada ya mitandao kadhaa kusambaza picha ya utupu inayoonesha sehemu ya kiuno, ikidaiwa kuwa ni ya msanii huyo ambapo paparazi wetu alipomhoji kuhusiana na picha hiyo, alitiririka:

Hiyo picha siyo yangu. Mimi siwezi hata siku moja kusaka usupastaa kwa kupiga picha za uchi, kwanza sipendi na sitaki kufanya hivyo sababu ninajiheshimu tofauti na wenzangu wanaoendekeza mambo hayo wakati hawana kazi hata moja sokoni,” alisema Koletha.

http://www.globalpublishers.info.