advert

http://

Friday 20 September 2013

BAADA YA KUTWAA UBINGWA WA DUNIA FRANCIS CHEKA AAMUA KURUDI SHULE.KIDATO CHA KWANZA

.

Bingwa wa dunia wa WBF Francis Cheka ambaye hivi karibuni alipewa zawadi ya  kiwanja na Rais Jakaya Kikwete baada ya ushindi wake dhidi ya bondia wa Marekani, ameamua kurudi shule.

Cheka anasema hakupata nafasi ya kwenda shule kutokana na matatizo ya kifamilia na kuishia darasa la saba. “Mimi sikusoma niliishia darasa la saba, lakini nimeamua kurejea darasani baada ya kupewa udhamini na shule ya St Joseph”.

“Nahitaji kuwa Cheka mpya kielimu ili nifike mbali, miaka kumi ijayo hadi namaliza elimu yangu nitakuwa na miaka 41. Hapo nitaamua niendelee na ngumi au nifanye biashara zangu nyingine “.


Habari kamili ipo kwenye gazeti la Mwananchi la Sept 17.

Jeshi la  polisi  mkoani Iringa  linamshikilia mwalimu wa  shule ya msingi Makungu wilaya ya  Mufindi Bw Edwin Ambukile kwa  tuhuma  za  kuwasaidia majibu wanafunzi wa  darasa la  saba katika mtihani  wa Taifa  wa kuhitimu elimu ya msingi.


Kamanda  wa polisi mkoa  wa Iringa Bw Ramadhan Mungi (pichani) amesema  kuwa tukio  hilo limetokea  Septemba 15 mwaka  huu.

Alisema kuwa mwalimu  huyo ambae ni mwalimu wa masomo ya Sayansi katika  shule  hiyo pia alikuwa ni mwalimu wa masomo ya ziada ( katika  shule  hiyo na  sababu ya  kuwasaidia  wanafunzi majibu ni kutaka  kupata umaarufu kwa wanafunzi  watano aliokuwa akiwafundisha masomo ya  ziada aliopata  kuwaahidi kuwa watafaulu mtihani  huo. 

Alisema  kuwa  mwalimu  huyo tarehe 11 septemba  alipokea mitihani kutoka kwa msimamizi  na baada ya hapo akafungua bahasha   ya masomo ya  Sayansi na kuanza  kufanya mwenyewe  na majibu kuyatuma kwa Sms kwa  mke  wake . 

Hata  hivyo  siku ya mtihani mmoja kati ya wanafunzi  waliopata majibu hayo alipoingia katika  chumba  cha mtihani alionekana akitetemeka  kupita  kiasi na  hivyo msimamizi wa mitihani alipompekua alimkuta na majibu hayo na kueleza jinsi alivyosaidiwa na mwalimu  huyo .
  
Kamanda  wa  polisi alisema  siku ya mtihani  mwalimu Ambukile  alipangiwa kusimamia  shule  ya msingi Igomaa na  sasa amekamatwa na atafikishwa mahakamani  wakati  wowote kuanzia sasa.


Shule ya Sekondari Ilboru, imefungwa na serikali kufuatia tishio la kuchomwa moto. Hii inatokana na mgogoro wa wanafunzi na waalimu. Wanafunzi 4 wanahojiwa, 800 wamerudishwa nyumbani.


source:Udakuspecially.

Katika hali isiyo ya kawaida mamba mkubwa mwenye futi 8 amezua tafrani baada ya kuingia chini ya kitanda cha Mkurugenzi wa hoteli moja ya kitalii iitwayo Humani iliyopo pembezoni mwa mto Turgwe huko nchini Zimbabwe na kukaa zaidi ya masaa 8.
Mr Whittall, ambaye ni mkurugenzi wa hoteli hiyo alisema kuwa mamba huyo aliingia kwa siri chumbani kwake na kukaa chini ya kitanda chake usiku na kugundulika asubuhi ya siku iliyofuata.
Alisema kuwa mamba huyo alitoka nyuma ya pori lililopo karibu na hoteli hiyo ambapo hata yeye alipoamka hakumuona na alining’iniza miguu yake huku mamba huyo akiwa chini ya kitanda ambapo alitoka kwenda kupata kifungua kinywa kwenye mgahawa wa hoteli hiyo.
Inaelezwa kuwa mamba huyo aligundulika na mfanyakazi aliyekuwa akifanya usafi katika chumba hicho na kupiga mayowe yaliyomshtua Mr Whittall ambapo alitoka mbia kwenda kushuhudia kulikoni na kumkuta mamba huyo akiwa chini ya kitanda chake kumbe alilala naye kwenye chumba hicho usiku mzima.
Mamba ni wataalam wa kujificha na ndiyo maana hunusirika kuuwawa na wanyama wengine hususani binadamu hata wakiwa nje ya maji,alisema Mr Whittall.
Na huweza kutulia sehemu moja kwa muda mrefu bila kugundulika na myama yoyote hivyo kumtambua inakuwa ni vigumu hiyo ni kutokana na maumbile yao yalivyo na hukimbilia ndani ya vichaka au kuingia kwenye nyumba kama hotelini hapo kufuata joto hasa katika kipindi cha mvua na baridi kali na alipenda kukaa chini ya kitanda hicho kwasababu kulikuwa na joto.
Mkurugenzi huyo alilazimika kuwaita wafanyakazi wengine ambao walisaidiana kumuondoa mamba huyo kutoka kwenye chini ya kitanda na kumtupa kwenye bwawa la hoteli hiyo.


Polisi wawili wa Musoma, Mkoa wa Mara na Kibaha, Pwani wanashikiliwa kwa tuhuma za kukutwa wakisafirisha risasi 3,000 kutoka Musoma kwenda Dar es Salaam.
Wanaoshikiliwa kwa tuhuma hizo ni aliyekuwa mtunza chumba cha silaha Kikosi cha FFU Musoma na mwenzake mwenye cheo cha Koplo Wilaya ya Kibaha, Pwani. Inadaiwa walikamatwa Juni 2, mwaka huu saa 11:00 alfajiri.
Watuhumiwa wanashikiliwa Kituo cha Polisi Musoma na wamefunguliwa jalada MUS/RB/2465/013 wizi wa risasi 1,056, wanasubiri taratibu zingine za polisi.
Habari zinadai shehena hiyo ilisafirishwa kwa kutumia pikipiki hadi Kituo cha Mabasi, lakini polisi tayari walikuwa wameweka mtego baada ya kupata taarifa kuhusu wizi huo.
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali ikiwamo wahusika wa basi na nyumba moja ya kulala wageni iliyopo jirani na stendi, baadhi ya askari waliovaa kiraia walionekana maeneo hayo mapema.
Kwa mujibu wa habari za uhakika kutoka ndani ya polisi, Koplo huyo alikutwa na shehena hiyo karibu na kituo cha mabasi ya Kampuni ya Mohammed Trans, akijiandaa kuelekea Dar es Salaam ambako inasemekana wana wateja wao.
Inadaiwa koplo huyo aliomba ruhusa ya ugonjwa kazini kwake na kuitumia kusafiri hadi Musoma kuchukua mzigo huo, inadaiwa biashara yao hiyo ni ya muda mrefu na wana mtandao na watu wanaojihusisha na uhalifu.
Mtandao huo unadaiwa kuwagusa baadhi ya polisi Mkoa wa Tarime na Rorya, ambao huwauzia watu wanaojihusisha na uhalifu wa kutumia silaha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Absalom Mwakyoma alipotafutwa kwa simu zake za mkononi licha ya kuitwa, hazikupokewa.
Hata hivyo, aliomba atumiwe ujumbe, licha ya kupelekewa huo ujumbe, hakujibu ingawa taarifa zinadai ameanza likizo ya kustaafu hivi karibuni.
Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mara, Jafari Mohammed alipoulizwa kuhusu tukio hilo, alikanusha kufahamu suala hilo huku akigeuka kuwa mkali kwa mwandishi.
“Hilo mimi silijui, nani kakwambia wewe… askari kukutwa na risasi mfukoni ni jambo la kawaida huenda ni uzembe tunamshughulikia kwa uzembe,” alisema.

Mwananchi.

STAA wa sinema na Bongo Fleva, Baby Madaha amenaswa live akiingia na kula bata hotelini akiwa na mwanaume aliyetajwa kwa jina la Joe Kariuki. 


Tukio hilo lililopigwa chabo na shushushu wetu lilijiri wikiendi iliyopita, majira ya usiku mnene katika Hoteli ya De France iliyopo Sinza, Dar ambapo Madaha alionekana akiwa amejiachia vya kutosha kwa mwanaume huyo

Ili kupata mzani wa habari hiyo, gazeti hili lilizungumza na Madaha ambaye alikiri kuwa na mwanaume huyo hotelini hapo huku akidai ni meneja wake.

“Joe (Kariuki) ni meneja wangu wa Kampuni ya Candy n’ Candy Records ya Nairobi, Kenya ndiye anayesimamia kazi zangu na tayari nimeachia ngoma moja inayo-hit ya Summer Holiday,” alijitetea Madaha.


Source:GPL.