advert

http://

Sunday 6 October 2013

HAWA KWELI WANASTAILI KUWA MABINGWA DUNIANI.WAMEWEKA REKODI DUNIA NZIMA.




Jionee Mwenyewe hapa Chini Picha na Video za Watu wa Ajabu Duniani.


MWANAMKE MWENYE ULIMI MKUBWA DUNIANI


MWANAMKE MWENYE KUCHA NDEFU ZAIDI DUNIANI


MWANAMKE MWENYE UWEZO WA KUJIKUNJA ZAIDI DUNIANI


TAZAMA VIDEO HII UJICHEKEE MWENYEWE.



 Mama wa staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila kwa mara ya kwanza amemfungukia marehemu Steven Kanumba aliyefariki dunia Aprili 7, 2012. Mahojiano hayo yamefanywa hivi karibuni na gazeti la Risasi linalotolewa na kampuni ya GPL
Katika mahojiano rasmi na Risasi jijini Dar, Mama Lulu aliweka wazi kila kitu kuhusu madai mbalimbali ya yeye na mama Kanumba,Lulu na marehemu Kanumba.

Mambo yaliyoelekezwa ayajibu mwanamama huyo ni pamoja na madai kwamba alishapokea barua ya posa ya Kanumba kutaka kumuoa Lulu, yeye na mama Kanumba kugombana hivi karibuni na Lulu kumjali zaidi mama Kanumba kuliko yeye.


Awali, mwanamke huyo alisema miongoni mwa watu waliofiwa na Kanumba yeye yupo mstari wa mbele kwani uchungu alioupata siku ya tukio mpaka leo haujamtoka.


Mahojiano kamili yalikuwa kama ifuatavyo:
Risasi: Mama kuna madai kadhaa ambayo ni vyema uyajibu.
Mama Lulu: (Kwa ukali kidogo) maswali gani? Mimi sitaki waandishi, nilishasema! Kama ni kuhusu Lulu muulizeni mwenyewe.
Ilibidi waandishi watumie kazi ya ziada ili mama huyo aweze kuzungumza.
Risasi: Ni mambo ya kawaida tu mama, wewe ndiyo unafaa kujibu, tafadhali tusikilize.
Mama Lulu: Haya, ulizeni.

ALIUJUA UHUSIANO WA KANUMBA NA LULU?
Risasi: Kuna madai kwamba uliujua uhusiano wa kimapenzi kati ya Lulu na Kanumba,  lakini mama Kanumba alikuwa hajui kinachoendelea, ni kweli?


Mama Lulu: Kwanza katika maisha yangu hakuna siku niliyowahi kupata mshtuko kama niliposikia Kanumba amefariki dunia na mwanangu Lulu kahusishwa na kifo kile, nilishtuka sana.


“Ilikuwa mara yangu ya kwanza kujua kumbe Kanumba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanangu Lulu, lakini kabla ya hapo sikuwa najua lolote.


ALIMKABIDHI LULU KWA KANUMBA?
“Ninachoweza kukiweka wazi ni kwamba, nilikutana na Kanumba nikamkabidhi mwanangu kwa moyo mweupe amlee kisanii kwa sababu nilijua anaweza, kumbe na wao wakaanzisha uhusiano huo kwa siri.


KWA NINI ALIMKABIDHI LULU KWA KANUMBA?
 “Mimi na Kanumba tulikuwa tumezoeana sana. Alinipa heshima zote kama mama yake na alikuwa kijana mwenye aibu kwangu kutokana na heshima, haikuwa rahisi kuangaliana machoni na ndiyo maana niliamua kumpa Lulu amkuze kisanii.


ALIPOKEA BARUA YA POSA YA KANUMBA?
“Si kweli, sijawahi kuona wala kupokea barua ya posa ya Kanumba kumchumbia Lulu.


KAMA KANUMBA ANGETAKA KUMUOA LULU?
“Lakini nataka kusema kwamba kama Kanumba angekuwa hai na angetaka kumuoa Lulu ningefurahi sana kwani naamini mpaka sasa wangekuwa wamepata mtoto mzuri na sisi wazazi tukaitwa bibi.”


MADAI YA KUGOMBANA NA MAMA KANUMBA?
Risasi: Kuna madai kwamba wewe na mama Kanumba kwa sasa ni paka na panya, na sababu kubwa ni Lulu kumjali zaidi mwanamke huyo kuliko wewe, ni kweli habari hizi?


Mama Lulu: Mimi na mama Kanumba hatuwezi kugombana hata siku moja. Kwanza Lulu nimempa jukumu kwamba kwa sababu wote ni mama zake, akinunua nyama kilo tano kwa ajili yangu na kwa mama Kanumba apeleke tano.


“Akinunua vocha ya elfu tano kwangu na mama Kanumba amtumie kama hiyohiyo. Kwa hiyo hakuna ugomvi.”


Risasi: Je, Lulu akimzidishia mama Kanumba wewe hutajisikia vibaya?


Mama Lulu: Siwezi kujisikia vibaya ingawa mimi kwa sababu naishi naye ni lazima nitapata zaidi, lakini akimsaidia naona ni sawa tu.

ALIKUWA AKIMUOGOPA MAMA KANUMBA?
Mwandishi: Ilikuwaje ukakutana na mama Kanumba kwa mara ya kwanza?
Mama Lulu: Lulu ndiye aliyekuwa akinishawishi kila mara niende nikaonane na mama Kanumba ingawa wakati mwanangu yuko jela kiukweli nilikuwa namuogopa sana.


“Unajua yule aliyepotea (Kanumba) ni mtoto kama wangu, lakini alipotoka tulikwenda nyumbani kwake na tunamshukuru alitupokea vizuri. Awali kabla ya kifo cha Kanumba sikuwahi kufahamiana naye.


Risasi: Ukiambiwa uongee na Watanzania utataka kuwaambia nini?


Mama Lulu: Cha kuwaambia ni kwamba, mimi na mama Kanumba si marafiki bali ni mtu na dada yake.
 

Nawaomba wawaombee mama Kanumba na Lulu mwenyewe ili waendelee kupatana na kufanya kazi za sanaa pamoja kama walivyoanza.

Risasi: Tunashukuru sana mama.
Mama Lulu: Karibuni sana, mimi huwa naogopa sana magazeti, sipendi sana kuongea na waandishi wa habari.


KUMBUKUMBU YA LULU
Katika mahojiano na kipindi cha Take One kinachorushwa na Clouds TV, Lulu alisema:''Katika maisha yangu sitakaa nimsahau Kanumba kwa sababu alikuwa ni zaidi ya mpenzi. Kamwe sitamsahau''



source:GPL.


Mwanasheria mmoja wa Illinois ambaye alipatikana na hatia ya kufanya ngono na mwanaume mmoja kwa malipo ya Dola za Marekani 100 anamshitaki aliyekuwa wakili wake wa utetezi na mawakili wengine wawili kwa madai ya kusambaza picha zake za utupu.


Reema Bajaj, mwenye miaka 27, anasema wakili wake wa zamani Timothy Johnson, mwendesha mashitaka wa zamani Calvin Campbell, na mwanasheria aliyeorodheshwa kwenye hati ya mashitaka kama 'John Doe' walitoa hadharani picha zake za siri sambamba na taarifa kumhusu yeye.

Sasa wateja, wazee wa mahakama, na majaji wote wameshayaona makabrasha hayo ya kuaibisha, Bajaj anasema. Ana 'hasira mno, huzuni, aibu, na fedheha,' kwa mujibu wa hati yake ya mashitaka, ambayo ilisambazwa katika mtandao na gazeti la Illinois la the Daily Chronicle.


Johnson na Campbell, ambao sasa wana changamoto yao pamoja, hawakujibu simu mara moja walipotakiwa kutoa maoni yao kuhusu hati hiyo ya mashitaka.



Bajaj alipatikana na hatia ya ukahaba wakati wa majira ya joto. Alipigwa faini ya Dola za Marekani 2,500 na kutakiwa kufanya kazi za kujitolea kwa jamii masaa 50.

Polisi walimkamata Bajaj mnamo Juni 2011, wakisema wamegundua baruapepe kati yake na mwanaume ambaye alimlipa kwa ajili ya kufanya naye ngono kama sehemu ya uchunguzi kwenye kesi isiyohusiana, imeripotiwa. Alitiwa hatiani kwa makosa matatu ya ukahaba, lakini mawili yalitupiliwa mbali.

Polisi walisema hakukuwa na uhusiano wowote kati ya ukahaba wake na wateja wa kampuni yake ya uwakili. Katika hati yake ya mashitaka aliyowasilisha Jumatatu, Bajaj alisema anahofia picha hizo na maelezo kwamba zilidaiwa kusambazwa baada ya kukamatwa kwake zinaweza kuathiri biashara ya kampuni yake.

Alikuwa na changamoto yake binafsi, kwa mujibu wa ripoti mbalimbali za habari. Tovuti ya kampuni yake ya uwakili kwa sasa haifanyi kazi.

Kabla ya kushitakiwa kwa ukahaba, Bajaj alijitolea muda wake katika Ofisi ya Utetezi wa Jamii Boone County, iliripoti Rockford Register baada ya kukamatwa kwake.


Pengine huwa unajiuliza kwamba kwanini mzungu akivaa bikini na kutembea ufukweni mwa bahari hakuna anae shituka wala kupiga kelele, lakini binti wa ki afrika akivaa bikini na kutembea ufukweni au kupiga picha utasikia maneno mengi ya kumsifia, au kumsema kwamba yuko uchi. 


Ajabu ni kwamba wale wale wanaompigia kelele binti wa kiafrika ndio wasioshituka wamuonapo binti wa kizungu. Je, unajua kinachosababisha utata huu?


Tatizo sio utamaduni, mila au mazoea. Ukweli ni kwamba wanaume wengi wa kiafrika huvutika zaidi wanapomuona binti wa kibantu kuliko mzungu. 


Hali hii inasababishwa na mazoea ya wanaume wengi wa ki afrika kuwa na mahusiano (sex) na wasichana wa kwao (wabantu) na hivyo kuufanya ubongo kuvutika zaidi na rangi au maumbile ya aina fulani. 

Ndio maana mwanaume anaejenga uhusiano na msichana mwembamba, si ajabu akatafuta msichana mwingine mwenye umbile linalofanana na hilo endapo kama ataachana na huyo aliyenae. 

Ukweli huu unaungwa mkono na wanasayansi walioendesha uchunguzi maalum kutaka kujua vikolombwezo vinavyo mvutia mwanamume.
Mamia ya wanaume waliofanyiwa uchunguzi wa picha za ubongo walionesha kupata msisimko zaidi  katika hypothalamus (sehemu ya ubongo inayoshughulika na mahusiano/sex) kila walipo oneshwa picha za mwanamke wa asili yake hasa kama muhusika hajapata kuwa na uhusiano na mpenzi wa rangi au asili nyingine.

 Hata hivyo tofauti ilijitokeza kwa wanaume waliooa wanawake wa asili/rangi tofauti. Hata hivyo wanasayansi hao walikubali pia kwamba sura na umbile la mwanamke lilisaidia kuongeza msisimko kwa namna tofauti....


Linah, staa wa muziki Bongo ambaye hivi karibuni kumekuwa na maneno mengi ambayo yamezungumziwa juu yake kuhusiana na swala zima la mahusiano ya kimapenzi, huku akihusishwa na skendo za kukubali kuhongwa na pia kuendeleza mahusiano na msanii mwenzake Amini ambaye alikwishatangaza kuachana naye, ameamua kutolea ufafanuzi swala hili ili kuwaweka mashabiki wake sawa.


Linah amekanusha vikali swala zima la yeye kuhongwa, vilevile kuhusiana na mahusiano ya kwake ya kimapenzi amesema kuwa kwa sasa ana mpenzi wake ambaye hayuko tayari kumuweka wazi katika vyombo vya habari, na katika hali hii hawezi kusema kitu chochote ambacho kitamuumiza yeye ama mahusiano yake.

Lina amesema kuwa yeye na Amini walikiss katika jukwaa ili kuleta  uhalisia na burudani tu na haimaanishi kwa namna yoyote kama wana uhusiano na yeye kama msichana hawezi kujivunjia heshima yake kwa kuhongwa.
Posted: 05 Oct 2013 11:25 AM PDT

Shilole amefichua kuwa, role model wake katika muziki kwa sasa ni nyota Lady Gaga ambaye kitu kikubwa alichojifunza kutoka kwake ni kujiachia pindi anapokuwa jukwaani, na kuwaridhisha wale ambao wametoa pesa zao ili kushuhudia burudani kutoka kwake.


Shilole pia amewataka mashabiki wake kukaa tayari na kolabo ambayo aliwaahidi kuwa atafanya na mwanamuziki Jennifer Lopez ambayo anatarajia kuikamilisha mwisho wa mwaka huu atakapokwenda tena ziarani Marekani.


Mazoezi yana umuhimu mkubwa kwa maisha yako endapo utaweza kuyafanya kwa jinsi ipasavyo. Kujua muda wa kula na kitu cha kula kunaweza kukusaidia kupata matokeo tofauti katika ufanyaji wako wa mazoezi.

Wanasayansi wanasema kuwa ulaji na mazoezi ni vitu vinavyoenda bega kwa bega. Ni vizuri kuelewa chakula unachokula kinaathiri vipi mazoezi yako.

Baada ya kugundua hilo wataalamu hao waliona si vibaya ikiwa watakuja na mwongozo utakaowasaidia wafanyaji mazoezi kupata matokeo mazuri kwenye programu zao.

Unachotakiwa kuelewa  ni kwamba muda wako wa kufanya mazoezi 
unaendana na kiasi cha chakula na maji ulichopata.  Hii inawahusu hasa wale wanaotaka kupunguza uzito kwa kutumia mazoezi.

Watu walio katika kundi hili, wamekuwa wakiharibu maana nzima ya mazoezi kwani badala ya kula chakula kinachoweza kuwaongezea nishati katika ufanyaji wa mazoezi, wengi wao huamini kuwa kwa kuacha kula wanaweza kufanikiwa zaidi.

Mara nyingi kitendo cha kaacha kula na kuendelea na mazoezi huchangia kwa kiasi kikubwa kumfanya mtu husika akose nguvu na badala yake kudhoofika na hatimaye hushindwa kufanya mazoezi.

Mambo muhimu ya kuzingatia unapotaka kufanya mazoezi:

1.   -Pata kifungua kinywa sahihi kiafya
Ikiwa unafanya mazoezi asubuhi, unashauriwa kuamka mapema na kupata kifungua kinywa saa mbili kabla ya kuanza mazoezi. Kwani kwa wakati huo nishati yote uliyopata kwenye chakula cha usiku,      itakuwa imetumika usiku hivyo hadi kufikia muda huo, utakuwa una kiwango kidogo sana cha nishati na sukari katika damu pia itakuwa chini.

Ikiwa hutakula kabla ya kufanya mazoezi utajisikia mchovu. Ikiwa utaamua kula kabla ya mazoezi unashauriwa kula chakula chepesi kama vile juisi au hata matunda pamoja na maji ya kutosha. Unashauriwa kula chakula kitakachosaidia kukuongezea sukari katika damu.
Ikiwa wewe si mlaji wa asubuhi sana, jaribu kunywa hata juisi tu kabla ya kufanya mazoezi. Pia ikiwa utaweza kupata kikombe cha kahawa itakuwa ni sawa tu.

2.   -Zingatia kiasi cha chakula
Epuka kula chakula kizito kabla ya kuanza mazoezi kwani kwa kufanya hivyo unaweza kujiweka kwenye hatari ya kuongezeka zaidi badala ya kupungua au kuimarisha mwili wako.
Pia, kula kiasi kidogo cha chakula. Ikiwa utakula chakula kingi unaweza kusikia uvivu kufanya mazoezi na hivyo kuishia kupumzika badala ya kuchangamka kufanya mazoezi.


3.   -Vitafunwa vyenye virutubisho kiafya ni bora zaidi.
Unaposema kula kitafunwa haimaanishi kuwa kila kitafunwa ni sahihi, hapa unapaswa uwepo wa virutubisho muhimu katika kitafunwa husika. Wataalamu wa afya wanashauri ulaji wa matunda zaidi katika hili.
Matunda yanaweza kumweka mfanyaji mazoezi bila kumchosha hata kama atakuwa amekula kiasi kikubwa tofauti na vyakula vingine.

Ikiwa utaweza kupata mlo unaoendana na mazoezi yako, ni wazi kuwa  mazoezi yako yatakuwa yenye tija, kwani utaweza kuona tofauti.




Zitto-KabweBy ZItto Kabwe:
Napenda kuujulisha umma kwamba jana Ijumaa tarehe 4 Oktoba, 2013 nimewasilisha kwa Katibu wa Bunge muswada binafsi Bungeni kufuta Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976.
Changamoto iliyopo ni Sheria mbadala ya vyombo vya habari baada ya Sheria ya sasa kufutwa. Hata hivyo wadau wa habari kama Baraza la Habari Tanzania wameshafanyia kazi suala hili kwa muda mrefu sana na wana mawazo kuhusu sheria mbadala. 

Nimejulishwa kuwa muswada wa sheria mpya ya habari tayari upo. Kwa hiyo katika mchakato wa kujadili muswada binafsi wa kufuta sheria ya magazeti ya mwaka 1976 mabadiliko yanaweza kufanywa ili kutunga sheria mpya.

Hatua ya kwanza ni kuifuta sheria hii kandamizi ambayo kiukweli tumechukua muda mrefu sana na baada ya madhara makubwa kufikia hatua ya muswada wa kuifuta.

Nimeamua kutumia njia za kawaida za kuwasilisha muswada na kuepuka njia ya dharura ili kujenga mazingira ya wadau wa habari kushiriki vya kutosha katika mabadiliko yanayotakiwa. 

Njia ya dharura ni ya haraka lakini huziba fursa za kupata maoni ya wadau ambao kimsingi ndio wenye sheria yenyewe haswa. Hivyo nimepeleka muswada jana ili uchapwe kwenye gazeti la Serikali (GN) kwa mujibu wa kanuni za Bunge, kisha usomwe kwa mara ya kwanza, uende kwa wadau kwa mjadala na marekebisho na kisha kusomwa kwa mara ya pili na kupitishwa na Bunge.

Ikumbukwe kuwa juhudi za kufuta sheria hii ni juhudi za wadau wa tasnia ya habari na ni juhudi walizofanya kwa muda mrefu sana. Mimi kama Mbunge ninawasilisha tu kwa sababu taratibu zetu za kuandika sheria zinataka ama Serikali, Kamati ya Bunge au Mbunge kuwasilisha muswada.

Kwa muda mrefu tumewaangusha wana habari kwa kutosukuma vya kutosha mabadiliko waliyokuwa wanayapigania. Hata hivyo, kuna msemo wa kihindi ‘asubuhi huanza pale unapoamka’. Sasa tuchukue hatua za kufuta sheria hii kandamizi.
Zitto Kabwe,Mb
Kigoma Kaskazini

Ilikuwa siku ya kawaida kama siku zingine msichana wa miaka 18 aliyejulikana kwa jina Chekwube Mbaka alitumwa sokoni kununua mahitaji ya chakula cha jioni katika mtaa mmoja huko Naigeria....lakini njiani alikutana na vijana wanane ambao walimbaka wote mpaka kupoteza maisha yake.


Polisi wamewashikilia vijana wawili kwa kutuhumiwa kuhusika na tukio hilo ....inasemekana vijana hao ni watengeneza majeneza wa eneo hilo.

 Jana ilikuwa ni zamu ya tamasha la fiesta Mjini Tanga.....Kama kawaida yake mwanadada Shilole hakosi vituko ....Safiri hii aliwapa nafasi mashabiki wawili kucheza nae jukwaani huku yeye akiimba .




Source:Udaku Specially Blog

Rihanna amejikuta kikaangoni tena wiki hii baada ya mashabiki wake kumshambulia kutokana na video yake mpya ya wimbo ‘Pour It Up’ wakisema ni chafu na ina matusi mno.


Mamia walitumia mitandao ya kijamii kumponda mrembo huyo kwamba ‘hana hata haya’ kutoa video chafu kama hiyo. 

ITAZAME HAPA CHINI!!

Mtu mmoja aliejulikana kwa jina la Burhan Islam(fundi wa gari) amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria aina ya Fuso kugonga lori lingine nae kubanwa na bodi na kuokolewa baada ya
jitihada zilizofanywa na baadhi ya Abiria waliokuwa wakisafiri katika barabara kuu ya Dar es salamu kwenda Mtwara na Lindi.
Gari hilo lenye namba za usajiri T 56ANQ lililokuwa likiendeshwa na Kunja Mshamu limepata ajali hiyo leo katika kijiji cha Mkwajuni wilayani Lindi baada ya kutaka kulipita gari lenye namba za usajili T 402 AJG Scania lililokuwa likiendeshwa na Amos Chadenyile na kushuhudiwa jitihada zilizokuwa zinafanywa kuokoa maisha ya kijana huo.Majeruhi huyo baada ya kuokolewa katika ajali hiyo alikimbizwa katika kituo cha afya kitomanga kwa huduma ya kwanza kabla ya kupelekwa katika hospital ya Mkoa wa Lindi kwa Uchunguzi zaidi
Katika ajali hiyo iliyousisha malori hayo hakuna majeruhi mwingine
aliepata jeraha huku gari hiyo ya Fuso likiwa limeharibika sana





IPO HIVI!!

WAKATI ulilalamika kuwa umelala njaa kwa siku mbili.
WAPO wenzako wanalalamika kuwa hawajapata mtoto mwaka wa tisa sasa.

WAKATI unaombaomba mtaani ilimradi upate pesa ya kujikimu kwa siku moja tu.
WAPO wengine wamelala vitandani wakimwomba Mungu muujiza tu aweze kumponya baba yao ambaye ni kila kitu katika familia.

WAKATI unalalamika kuwa mafua yanakusumbua na unachukia kuzaliwa,
WAPO wengine hiyo pua ya kuwa na mafua hawana. Iling’oka katika ajali ya treni. Na bado wanaishi.

WAKATI unamshangaa mkurugenzi mwenye suti kushindwa kumsaidia ombaomba mtaani.
YEYE anaumia kichwa kila mtu anamtazama yeye katika ukoo wake, kila mtu anamwomba yeye…..

WAKATI unalilia hadi kukufuru kisa una mgonjwa hospitali.
WAPO wenzetu walipoteza ukoo mzima katika vita vya wenyewe kwa wenyewe!!

WAKATI ukiona aibu kurudia nguo uliyoivaa jana.
WAPO wenzetu wanatamani walau kupata magunia wajivike miili yao.

WAKATI unapanga mipango ya kuwadanganya wasichana wanne na wote uwe nao katika mapenzi
KUNA wengine mamia kwa maelefu walifanikiwa na sasa ni wagonjwa vitandani wanatamani muda ungerudi nyuma wawe waaminifu.

WAKATI unatafuta mwanaume tajiri nd’o akuone.
NA YEYE anatafuta wasichana masikini awachezee kisha awaache.

WAKATI unamwita mtoto wako wa kumzaa ‘mbwa’ ama fisi.
WAPO wanaolala na midoli kitandani wakitamani kupata mtoto walau mmoja tu!!!

WAKATI unayasoma maandishi haya.
WENZAKO ndo wanakwapuliwa uhai dakika hii…..

**WEWE ni nani hadi uwe hai mpaka dakika hii!!!
JIGEUZE kuwa ombaomba, mwombe Mungu kila wakati na ukumbuke kumshukuru kwa zawadi ya uhai akupatiayo kila kukicha!!!

Ukiguswa na habari hii Ruksa kushare!!

Photo: Eti jamani unahisi hiki anachokitenda huyu mama ni sahihi?

9
Ndege iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu ambaye alikuwa gavana wa Nigeria, imepata ajali na baadhi ya abiria kufariki na wengine kukimbizwa hospitali.


Baadhi ya abiria hao walikuwa wanasindikiza mwili huo kwa ajili ya maziko lakini safari iliingia hitirafu.Ajali hiyo ilitokea baada ya injini kufeli ndege ikiwa hewani muda mfupi baada ya kupaa kwenye airport moja huko Nigeria. Ndege ilikuwa na watu 20 na watu watano ndiyo wamejeruhiwa na kukimbizwa hospitali 
1

HAKIKA ni mateso, tena makubwa. Mtoto Selemani Rajabu mwenye umri wa miaka 17, mkazi wa Ukonga kwa Guta, jijini Dar yuko katika mateso makali baada ya mguu wake mmoja kuvimba mithili ya tairi la gari kiasi kwamba hawezi kufanya jambo lolote zaidi ya kujiburuza tu.


 kijana huyo amesema kwamba anakumbuka amezaliwa akiwa na ulemavu kidogo chini ya nyayo za miguu yake ambazo zilikuwa nene kiasi cha kumfanya ashindwe kutembea na badala yake akawa ni mtu wa kutambaa tu.


Alisema wakati huo alikuwa akiishi na wazazi wake wote wawili, lakini baadaye wazazi hao walitengana na kumfanya aishi na mama yake huko Pugu Kajiungeni. Kutokana na uwezo duni wa mama yake, alimpeleka hospitali mara moja tu, licha ya mguu wake kuendelea kuvimba kila siku.


“Nakumbuka mama yangu aliwahi kunipeleka hospitali mara moja tu nilipokuwa mdogo, lakini sikumbuki kama aliwahi kunipeleka tena,” alisema Selemani akiwa na sura ya kukata tamaa.


Alisema tangu wakati huo, mguu wake uliendelea kuvimba siku hadi siku mpaka akashindwa hata kutambaa kama mwanzo na sasa akalazimika kujiburuza licha ya uzito mkubwa wa mguu wake kutokana na kuongezeka kwa uvimbe.


Kutokana na hali hiyo kuzidi kuwa mbaya, alisema mwaka jana mama yake alimpeleka Hospitali ya CCBRT ambako baada ya madaktari kumuangalia walisema mguu wake hauna maji ambayo wangeweza kuyanyonya ili kuyatumia kupata vipimo na kujua tatizo linalomsumbua.


Hata hivyo, kwa bahati mbaya, mama yake mzazi alifariki na kumlazimu baba yake kwenda kumchukua na kumpeleka kwa bibi yake huko Manzese.


Hali ya bibi haikuwa nzuri kiafya, hivyo baba alinichukua tena na kuishi naye kwake nikiwa na mama wa kambo,” alisema Selemani. 


Mtoto huyo analalamika kuwa anatamani hata mguu wake huo ukatwe kutokana na adha anayoipata kwani anakosa raha kama watoto wengine wanaotoka nje wenyewe tofauti na yeye anayetolewa kwa kuburuzwa na watu zaidi ya wawili.


“Siku zote  kunapokucha najiona kama sina thamani, natamani hata mguu huu ukatwe, siwezi kufanya kitu chochote, natamani kuwa kama watoto wenzangu,” alisema.


Licha ya adha hiyo, Selemani alisema kingine kinachomuumiza ni kufanya haja zote  sehemu alipokaa na hivyo kutoa wito kwa wasamaria, akiwemo Rais Jakaya Kikwete kumsaidia ili aweze kupata matibabu.


Kwa wenye nia ya kumsaidia mtoto Selamani, kwa matibabu au chakula, wanaombwa kuwasiliana na chumba cha habari kwa simu namba 0713 612 533. 

Harufu ya rushwa! Safu ya ulinzi katika maduka ya biashara ya Mlimani City, Dar kwenye geti la kuingilia na lile la kutokea, inadaiwa kutawaliwa na rushwa ambapo walinzi wamenaswa ‘laivu’ wakipokea ‘mlungula’.


Kwa mujibu wa walalamikaji, walinzi hao wanadaiwa kujiwekea utaratibu usiyo rasmi chini ya kampuni ya ulinzi wa eneo hilo iliyotajwa kwa jina la Omega Nitro Risk Solutions ya jijini Dar ambapo ‘vijana’ wake wanatuhumiwa kutoza watu faini ya shilingi elfu kumi kwa gari ambalo mhusika wake amepoteza kadi ya kuingia na kutoka. 


Madai hayo yalikwenda mbele zaidi ikielezwa kuwa kumekuwa hakuna utaratibu mahususi kwenye ishu hiyo kwani baadhi ya walinzi kila mmoja hujiamulia kuchukua fedha bila mhusika kupewa risiti ya malipo.


“Kuna tatizo kwenye safu ya ulinzi, huwa tunatozwa faini shilingi elfu kumi ukipoteza kadi,” alisema mmoja wa walalamikaji hao.


Baada ya malalamiko kutua kwenye kitengo chetu cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM), kazi ilianza ambapo kikosi kazi kilifanya doria kwa siku kadhaa na kufanikiwa kunasa laivu hatua kwa hatua, tukio la walinzi hao wakilamba ‘kitu kidogo’.


Tukio hilo lilijiri hivi karibuni katika geti la Mlimani City la upande wa Barabara ya Sam Nujoma ambapo walinzi hao walizuia gari la jamaa aliyekuwa amepoteza kadi na kuchukua rushwa.


Katika hali ya kushangaza au njaa, tofauti na kiasi cha shilingi elfu kumi kilichotajwa awali, walinzi hao walikubali kumpunguzia jamaa huyo hadi elfu tano bila kujua kwamba walikuwa wakirekodiwa hatua kwa hatua.


Baada ya kujikusanyia ushahidi wa kutosha, OFM ilizungumza na bosi wao ambaye ni Senior Inspector wa Omega Nitro Risk Solutions, Leo John Masuka juu ya vitendo hivyo ambapo mbali na kuonesha kushangazwa na habari hizo, pia alianika kila kitu jinsi wanavyofanya kazi.

“Nashangaa kama kuna tatizo kama hilo kwani  tumesitisha kuwatoza faini wanaopoteza kadi, nitafanya uchunguzi ili kuwabaini watu hao ambao wanaharibu sura ya kampuni.


Katika hali hiyo kwa kipindi hiki cha tishio la ugaidi ni rahisi kwa magaidi kutoa rushwa kisha kuingia na kufanya utekaji kama walivyofanya nchini Kenya kwenye maduka ya Westgate.


GPL.

Ajali mbaya  nyingine  imetokea  jana usiku katika mlima Kitonga wilaya ya Kilolo mkoani Iringa katika barabara  kuu ya Dar es Salaam -Iringa . 

Katika  ajali  hiyo  watu  wawili wamekufa papo hapo huku wa wawili  wakijeruhiwa  vibaya baada ya malori mawili kugongana  uso kwa uso . 
Ajali  hiyo imetokea  mida ya saa 12.50 jioni ya  jana  ikiwa ni dakika takribani 30  baada ya ajali ya basi la JM kupinduka eneo  la Mazome  wilaya ya Kilolo. 


waliopoteza maisha katika ajali  hiyo ambayo chanzo ni dereva  wa lori la IT lililokuwa  likisafirishwa kwenda nchi  za  kusini mwa Tanzania aliyekuwa akitaka  kulipita gari la mbele mlimani na katika kona kali . 


Hata  hivyo  dereva  wa  lori  hilo IT aliyetambuliwa kwa jina la Gody  amevunjika mguu  wake ambao umetoka  na  dereva  na utingo la fuso wamekufa papo hapo  huku mwanamke  aliyekuwa katika lori IT akisalimika 


No comments: