advert

http://

Friday 23 August 2013

WATUMISHI wawili katika zahanati ya Mwanhala wilayani Nzega, wamekumbwa na kashfa ya kufanya mapenzi na wagonjwa hospitalini.

Kutokana na kashfa hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Bitun Msangi, ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa watumishi hao.
  
Agizo la mkuu huyo limetolewa hivi karibuni, baada ya Diwani wa kata ya Utwigu, Sawaka Shita kuwalalamikia watumishi hao mbele ya Baraza la Madiwani, kwa kukithiri kufanya mapenzi na wagonjwa nyakati za kazi, licha ya kuonywa kwa mara kadhaa.
  
Diwani huyo aliliambia baraza hilo kuwa vitendo hivyo vina hatarisha maisha ya watumishi hao na ya wananchi, hususani waliotembea nao na kutishia kuvunja ndoa za wananchi.
  
Alidai kuwa taarifa hizo za malalamiko, zilishafika katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, tayari kwa utekelezaji, lakini wananchi wa kata hiyo walitaka kuifunga zahanati hiyo, baada ya kukithiri vitendo hivyo vya kufanya mapenzi katika wodi zilizopo.
  
Aliomba baraza liwahamishe na kuwachukulia hatua kali za kinidhamu watumishi hao, ambapo majina yao yamehifadhiwa kwa usalama wao, huku jitihada za kuwachukulia hatua zikifanyika.
  
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Patric Mbozu alisema suala hilo ni la hatari na linapaswa kufuatiliwa kwa umakini ili lipatiwe ufumbuzi na wananchi waendelee kupatiwa huduma za tiba.
  
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Abraham Mdeme alikiri kupokea malalamiko hayo na kuahidi kuwa suala hilo, litafuatiliwa mapema ikiwemo kuwahamisha kwa kufuata taratibu zilizopo.
  
Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Msangi alisema watumishi hao, wamevunja maadili ya afya, hususani kufanya ngono katika wodi za zahanati kwa nyakati za kazi.

Habari leo 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewavua madaraka Maafisa wanne wa Jeshi la Polisi nchini na kumsimamisha kazi mmoja ambaye atafunguliwa mashtaka ya kijeshi kutokana na kukiuka maadili na taratibu za jeshi hilo.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Waziri Nchimbi amesema hatua hiyo ni katika kuendeleza vita ya kuhakikisha kuwa jeshi la polisi linakuwa na nidhamu, linatekeleza wajibu wake wa kutenda haki na kuwalinda raia na mali zao.

Alisema amewachukulia hatua Maafisa hao baada ya kuridhia maoni ya kamati aliyoiunda kufanya uchunguzi wa matukio yaliyolalamikiwa dhidi ya askari polisi katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro na Kigoma kati ya Desemba 2012 na Mei, 2013.

Waziri Nchimbi aliwataja waliovuliwa madaraka kuwa ni Mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoani Arusha Mrakibu wa Polisi Ramadhan Giro, Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro Inspekta Jamal Ramadhan, Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Dumila Inspekta Juma Mpamba na mkuu wa upelelezi wa wilaya ya 
Kasulu ASP Daniel Bendarugaho na kumsimamisha kazi Inspekta Isaack Manoni.

Alifafanua kuwa  Mrakibu wa Polisi Ramadhan Giro alivuliwa madaraka kwa kushindwa kusimamia kikamilifu askari na maafisa walio chini yake ambao walikamatwa wakisafirisha bangi yenye uzito wa kilogramu 540 kwa kutumia gari la polisi.

Alisema askari hao wawili waliokamatwa wakisafirisha bangi, walikuwa wakifanya kazi kwenye kituo cha Ngarananyuki na baada ya kukiri kosa walifukuzwa kazi mwezi Mei mwaka huu.

Alisema kwa upande wa Inspekta Jamal Ramadhan amevuliwa madaraka yake kwa kutochukua hatua stahiki baada ya kupata taarifa za mfanyabiashara wa Mvomero Samson Mwita kubambikiwa fuvu la kichwa cha binadamu na askari polisi watatu wakishirikiana na matapeli wawili.

“Katika tukio hilo Inspekta Isaack Manoni amesimamishwa kazi na atashtakiwa kijeshi kutokana na tuhuma za kumtorosha mtuhumiwa, Cpl. Edward aliyekuwa dereva wa gari la Polisi lililokamatwa na bangi kitendo ambacho kimelifedhehesha jeshi la polisi” alisema Waziri Nchimbi.

Alibainisha kuwa Inspekta Juma Mpamba amevuliwa madaraka hayo kwa kuonesha udhaifu katika utendaji wake wa kazi kwa kutosimamia kikamilifu askari walio chini yake kitendo kilichosababisha askari kujipangia kazi nje ya utaratibu na kumbambikiza mfanyabiasha huyo kesi kwa lengo la kujinufaisha kinyume na maadili ya kazi. Aliongeza kuwa askari waliohusika na tukio hilo wamefukuzwa kazi na kushtakiwa.

Waziri Nchimbi alisema ASP Daniel Bendarugaho amevuliwa madaraka kwa kutokuwa makini katika kufanya na kusimamia upelelezi wa kesi ya mauaji ya marehemu Gasper Mussa Sigwavumba aliyeuawa baada ya kupigwa na askari polisi wawili Desemba mwaka jana.

Alisema upelelezi mbovu uliofanywa chini ya usimamizi wa Mkuu huyo wa upelelezi ulisababisha kesi hiyo kuondolewa mahakamani. Aliongeza kuwa upelelezi wa kesi hiyo utaanza upya ili haki itendeke.

Imeandikwa na Lydia Churi.

Ndege ndogo ya shirika la Tanzanair iliyokuwa ikitokea mjini Bukoba mkoani Kagera kwenda Dar ss Salaam imelazimika kutua kwa dharura katika ziwa Manyara baada ya injini yake moja kuzimika ghafla ikiwa angani. 

Ndege hiyo ilikuwa na abiria sita na rubani mmoja ambapo wote wamejeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Seliani mjini Arusha kwa matibabu. 

Chanzo: ITV

SIKU chache baada ya kukamatwa kwa askari feki wa usalama barabarani, Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imewakamata watuhumiwa saba wa ujambazi, wakiwa na sare za Polisi, huku mwingine akijifanya ofisa Usalama wa Taifa.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaa, Suleiman Kova alisema watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na sare za Polisi jozi mbili.

Watuhumiwa hao ni Khamis Mkalikwa (40), Magila Werema (31), Nurdin Bakari (46), Materu Marko (32), Louis Magoda (34), Amos Enock (23) na Amiri Mohammed (45), wote wakazi wa jijini Dar es Salaam.
  
Sare hizo, kwa mujibu wa Kamanda Kova, ni zenye cheo cha Sajenti wa Kituo, huku jozi moja ikiwa na jina linalosomeka SSGT A.M Mduvike.
  
Watuhumiwa hao walikamatwa jana katika eneo la Kiluvya, baada ya askari kuweka mtego, ambao ulifanikiwa kuwanasa. 

Alisema watu hao walikuwa wakitumia silaha, sare za jeshi la Polisi na redio ya mawasiliano katika uhalifu wao na hivyo kuwafanya baadhi ya watu kutupia lawama Jeshi la Polisi kwa kujihusisha na uhalifu.
  
Alisema watuhumiwa hao, wanahusishwa na uhalifu katika maeneo ya Boko, Tegeta, Mbweni, Bahari Beach, na maeneo mengine ya jiji. Alisema watu hao ni hatari zaidi.
  
Watuhumiwa hao walikuwa wakitumia gari aina ya Cresta GX, 100 yenye namba T 546 BWR na baada ya kuona wamezingirwa na askari maeneo hayo, walifyatua risasi moja hewani, lakini askari walipambana nao na kufanikiwa kuwakamata.
  
“Mbali na vitu hivyo pia wamekamatwa na bastola moja aina ya Brown yenye namba B.3901, ambayo ilikuwa na risasi nne na ganda moja, tunawashikilia kwa upelelezi na baada ya kukamilika watafikishwa mahakamani,” alisema Kova.
  
Katika hatua nyingine, Kamanda Kova alisema wanamshikilia mtuhumiwa Alquine Masubo (42) maarufu kama Claud, kwa kosa la kujifanya ofisa wa Usalama wa Taifa.
  
Claud ambaye ni mkazi wa Yombo Buza, alikamatwa akiwa na vielelezo mbalimbali pamoja na nyaraka za idara hiyo, ambapo baada ya kuhojiwa alikiri kuwa yeye si mfanyakazi wa idara hiyo.
  
Kova alisema mtuhumiwa huyo alipopekuliwa zaidi, alikutwa na bastola aina ya Browing yenye namba A. 956188-CZ83 ikiwa na risasi 12 ndani ya kasha lake.
  
“Alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na bastola nyingine aina ya Maknov yenye namba BA4799 ikiwa na risasi 19 na kitabu cha mmiliki chenye namba CAR 00071678, ikiwa na jina la P.1827 LT COL Mohammed Ambari, jambo ambalo haliwezekani kwa mtu mmoja kumiliki silaha mbili,” alisema Kova.
  
Mtuhumiwa huyo pia alikutwa na kitambulisho cha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) chenye namba 7001- E. 1075 na kompyuta mpakato aina ya Toshiba.

“Huyu ni tapeli wa siku nyingi na taarifa zake tulikuwa nazo, anatumia kivuli cha idara ya usalama wa taifa kufanya utapeli, lakini sasa ndiyo mwisho wake na wananchi wamjue” alisema.

Habari leo 
Mwanaume  aliyetambulika kwa jina moja la Juma, mkazi wa Tegeta A, Dar amejikuta akikamuliwa faini ya Sh. laki tano kufuatia kufumwa ugoni na mke wa mtu.

 Katika tukio hilo lililojiri Kimara-King’ong’o, Dar, Jumapili iliyopita, Juma alifumaniwa na mke wa mwanaume aitwaye Swai aliyetajwa kwa jina moja la Cesilia, mkazi wa maeneo hayo. 

Ilidaiwa kuwa Cesilia alimwachia mumewe mtoto na kumuaga kuwa anakwenda harusini ambapo mumewe alimkubalia bila kujua kumbe anakwenda kuzini.

Ilisemekana kuwa muda mfupi baadaye, kuna vijana walimfuata Swai na kummwagia ‘upupu’ kuwa mkewe alikuwa akisaliti ndoa yao.
  
Ilifahamika kuwa vijana hao walimchukua Swai na kumpeleka hadi kwenye nyumba ambayo wenyewe hawajahamia iliyopo karibu na biashara yao ya duka ambapo baada ya mwenye mali kuingia, alimkuta Juma akiwa amevaa ‘singlendi’ na bukta ambapo alizidi kuangaza macho huku na kule ili amuone mkewe.
 
Ilidaiwa kuwa alipomaliza kukagua kila ‘engo’ ndani ya nyumba hiyo aliingia chooni ndipo akamkuta mkewe akiwa amejificha chini ya ‘sinki’ la choo.
  
Iliendelea kusemekana kuwa baada ya kumuona mkewe, Swai alimnyanyua na kumuuliza kulikoni lakini hakuweza kumjibu.

Ilidaiwa kuwa Swai aliwaacha wawili hao ndani na kuwafungia ambapo alitoa taarifa kwa mjumbe wa eneo hilo, Zakaria ambaye alifika eneo la tukio mara moja huku akifuatiwa na Mtendaji wa Serikali za Mitaa, Amina Rashid.

Ilielezwa kuwa viongozi hao walipofika walikuta umati mkubwa umejaa uliotaka kujua hatima ya tukio hilo hivyo ilibidi watoe taarifa polisi ambao walifika mara moja na kuwachukua watuhumiwa huku wakisindikizwa na kadamnasi hadi Kituo cha Polisi cha Kimara, Dar.
 
Habari za kipolisi zilieleza kuwa wakiwa kituoni hapo, Swai alimwekea dhamana mkewe huku Juma akibaki ‘lokapu’ hadi alipokwenda kuchukuliwa na mwenyekiti na mjumbe wa mtaa kwani kesi hiyo ilirudishwa kwenye ngazi ya kijiji ili wazungumze na kuyamaliza. 

Viongozi wote walikiri   kuwa walizungumza suala hilo wakiwa na mwenye mke ambapo uamuzi ulifikiwa kuwa Juma amlipe Swai Sh. laki tano kama faini au adhabu kwa kosa alilotenda.

Ilielezwa kuwa Juma hakuwa na kiasi hicho cha fedha hivyo aliwekewa dhamana na ndugu yake na kuahidi kulipa mwezi wa kumi, mwaka huu.
 
Kwa upande wake, Swai alisema kuwa ameamua kumrudisha mkewe kijijini kwao kwa miezi kadhaa au mwaka mmoja huko Rombo, Moshi mkoani Kilimanjaro kama sehemu ya adhabu yake.

Kabla ya kufikiwa kwa uamuzi huo, awali Juma alifunguliwa jalada la kesi katika Kituo cha Polisi cha Kimara-Temboni namba KM/RB/2931/13 TAARIFA alikolala kwa siku moja.

Source: Global publisher. 

Msanii Tundaman amejikuta akiambulia aibu ya mwaka baada ya kujitosa nusu uchi mtaani akiwakwepa askari polisi ambao walivamia kwake leo asubuhi kwa lengo la kumkamata.... 

Chanzo cha Tunda man kusakwa na polisi ni deni la sh. laki nane ambazo alikopa mwanzoni mwa mwaka huu kwa mwanadada mmoja ( jina kapuni).... 

Taarifa zinadai kwamba, baada ya kupewa hela hiyo, Tunda man aligeuka kisima cha matusi ya nguoni kwa mrembo huyo. Kila akipigiwa simu alikuwa hapokei, na akipokea ni matusi ya nguoni..... 

Baada ya hali hiyo, mwana dada huyo aliamua kulifikisha swala lake polisi ambapo Tundaman alikamatwa. Akiwa mikononi mwa polisi, msanii huyo aliomba apewe nafasi ya kulilipa deni lake kwa awamu tatu kuanzia tarehe 12/8/2013 

Baada tarehe hiyo, Tundaman hakuweza kulipa kiasi chochote na wala hakutoa ushirikiano wowote, hali iliyomfanya mwanadada huyo arudi kuripoti polisi.... 

Polisi walianza jitihada za kumsaka ambapo leo majira ya saa nne asubuhi walivamia kwake ( Tabata Savana ) kwa lengo la kumkamata..... 

Bahati nzuri au mbaya, Tundaman alifanikiwa kuwatoroka polisi akiwa na bukta tu ( kwa mujibu wa mashuhuda) na kutokomea kusikojulikana...

Ifuatayo  ni  HATI  YA  MAKUBALIANO  yao  ambayo  mpekuzi  wetu  amefanikiwa  kuipata....

source:mpekuzihuru.